Monday, 7 November 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 8,2022
















Share:

MKURUGENZI MAIPAC : WAANDISHI WA HABARI ANDIKENI HABARI ZA KUISAIDIA JAMII







Mussa Juma Mkurugenzi Maipac na Mjumbe wa Bodi Misa- tan akitoa nasaha Kwa wahitimu na wageni katika chuo cha uandishi wa habari Fanikiwa Arusha yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika chuoni apo kilichopo mbauda ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha

Mjumbe wa Bodi Fanikiwa Journalism School Arusha Elson Makaye kushoto akimkabidhi cheti Cha shukrani mgeni rasmi katika mahafali ya 16 ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika chuo hicho kilichopo Ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha mkoani Arusha

Na Woinde Shizza ,Arusha
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuandika habari zenye manufaa Kwa jamii Kwa kuandika habari bunifu zinazolenga kuwakwamua wananchi kuondokana janga la umaskini.


Sekta ya habari na utangazaji ikitumika ipasavyo hususani vyombo vya habari mtandaoni kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia vinaharakisha zoezi la kuipasha jamii habari kwa wepesi na haraka zaidi hivyo kuwa chachu ya mabadiliko.


Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya wanahabari inayosaidia jamii za pembezoni nchini MAIPAC, Musa Juma alisema hayo wakati akihutubia wahitimu na wazazi katika mahafali ya 16 ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Fanikiwa Arusha yaliyofanyika hivi karibuni.


Alisema kuwa ulimwengu wa sasa umekua, haswa katika eneo la sayansi na teknolojia hivyo wana habari wanapaswa kukimbia na ukuaji huo wa teknolojia kwa kuandika habari bora na bunifu pia kuanzisha vyombo vya habari vya mitandaoni ambavyo vitawasaidia wao kujiajiri.


Hata hivyo ameeleza kuwa waandishi wengi wanaweza kufungua "Blog, radio mtandao na Tv za Mitandaoni ambazo wanaweza kupeleka maudhui mbali mbali ya kihabari na kupitia vyombo hvyo watapatikana wawekezaji mbalimbali ambao wataweka matangazo ya biashara zao ili zionekane na watazamaji au pengine wasomaji.


Musa Juma ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi MISA - TAN na Mkuu wa magazeti ya mwananchii Mkoani Arusha amewataka wahitimu hao wa ngazi ya Stashahada kuzingatia maadili wawapo kazini lakini pia kuwa wabunifu katika kuandika habari za mazingira, kilimo, uchumi, na mabadiliko ya TABIA NCHI ili kusaidia kuwaweka katika mazingira mazuri zaidi ya kihabari.


Naye mkuu wa chuo hicho Bwana Andrea Ngobole, amewataka wazazi wa wahitimu kuwaendeleza zaidi vijana hao katika chuo kikuu ili waendelee kupata elimu zaidi juu ya tasnia ya habari na sekta nyinginezo
Share:

Live : MATUKIO YANAYOENDELEA MKUTANO WA BUNGE LA AFRIKA ....MAJADILIANO KUHUSU MAKUBALIANO YA ENEO HURU LA BIASHARA BARANI AFRIKA


Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Sita la Afrika (Pan African Parliament - PAP) unaendelea leo Jumatatu Novemba 7,2022 katika ukumbi wa Makao Makuu ya Bunge la Afrika, Midrand Afrika Kusini. 
Kinachoendelea sasa Kuwasilisha na kujadili Ripoti kuhusu Makubaliano ya eneo huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) 

Share:

Sunday, 6 November 2022

WAZIRI NAPE NNAUYE AONGOZA TAMASHA LA KUMUOMBEA RAIS SAMIA JIJINI MWANZA


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye akipokelewa na Bw. Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion iliyoandaa tamasha la kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan wakati alipomwakilisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Jumapili Novemba 6,2022 ambapo waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili wametumbuiza huku maaskofu na wachungaji mbalimbali wakifanya maombi kumuombea Rais na taifa kwa ujumla. (NA JOHN BUKUKU-MWANZA)
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye akiteta jambo mara baada ya kupokelewa na Bw. Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion alipowasili kwenye tamasha la kumuombea Rais kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye akisalimiana na viongozi mbalimbali wa dini wakati alipowasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza ili kushiriki katika tamasha hilo kama mgeni rasmi.


Mwimbaji wa nyimbo za Injili Ambwene Mwasongwe akitumbuiza Katika Tamasha la kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo Mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amewakilishwa na Waziri wa Habarii, Mwasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye.


Wananci mbalimbali wakiwa katika tamasha hilo.


Mwimbaji Akilimali Tumaini kutoka nchini Kenya akitumbuiza katika tamasha hilo.


Bw. Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion akimpongeza Mwimbaji Akilimali Tumaini kutoka nchini Kenya mara baada ya kutumbuiza katika tamasha hilo


Mwimbaji Joshua Ngoma kutoka nchini Rwanda akitumbuiza katika tamasha la Kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan ililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Jumapili Novemba 6,2022.


Waimbaji wa kwaya ya Zablon Singers wakitumbuiza Katika Tamasha la kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan linalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo Mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewakilishwa na Waziri wa Habarii, Mwasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye


Waimbaji wa kwaya ya Zablon Singers wakitumbuiza Katika Tamasha la kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan linalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo Mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewakiliswa na Waziri wa Habarii, Mwasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye


Mwambaji nguli wa muziki wa Injili nchini Tanzania Eose Muhando akifanya yake katika tamasha hilo.


Bw. Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion akicheza pamoja na MC Mwakipesile na na baadhi ya waimbaji katika tamasha hilo.


Mwambaji nguli wa muziki wa Injili nchini Tanzania Eose Muhando akifanya yake katika tamasha hilo.


Baadhi ya viongozi wa dini wakijiandaa kufanya maombi kwa ajili ya Rais Samia Suluhu Hassan katika tamasha hilo.


Waziri wa Habarii, Mwasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye akishiriki katika tukio la Maaskofu kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan wakati mmoja wa maaskofu hao kutoka makanisa ya Mwanza Askofu Charles Sekelwa akifanya maombi wakati wa Tamasha la kumuombea lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


Waziri wa Habarii, Mwasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye akishiriki katika tukio la Maaskofu kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan wakati mmoja wa maaskofu hao kutoka makanisa ya Mwanza Askofu Charles Sekelwa akifanya maombi wakati wa Tamasha la kumuombea lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Waziri wa Habarii, Mwasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye akizungumza na kutoa salamu zake mara baada ya kufanyika kwa maombi ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Share:

WAZIRI UMMY -TANZANIA BADO INA UHABA WA MADAKTARI BINGWA

 



WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa uzinduzi wa  mpango wa kutoa huduma za upasuaji wa kibingwa bila malipo kwa wakazi wa Jiji la Tanga uliofanyika kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo ambao umewezeshwa na Taasisi ya Watumishi Health Check, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Tanga mjini ambapo kwa pamoja wamewaleta wataalamu hao wa upasuaji kutoka nchini Uingereza.

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa uzinduzi wa  mpango wa kutoa huduma za upasuaji wa kibingwa bila malipo kwa wakazi wa Jiji la Tanga uliofanyika kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo ambao umewezeshwa na Taasisi ya Watumishi Health Check, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Tanga mjini ambap kwa pamoja wamewaleta wataalamu hao wa upasuaji kutoka nchini Uingereza.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Seif Kallage akizungumza wakati wa halfa hiyo

MKUU wa wilaya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mkurugenzi wa Watumishi Afa Check Dkt Siraji Mtulia akizungumza wakati wa uzinduzi huo
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo akizungumza 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Jonathan Budemu akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Sehemu ya madaktari bingwa wakiwa kwenye uzinduzi


Na Oscar Assenga,TANGA.

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amesema Tanzania bado ina uhaba mkubwa wa Madaktari Bingwa hivyo uwepo wa mpango wa kambi ya upasuaji wa huduma za kibingwa unahitajika sio kwa mkoa wa Tanga bali ni mikoa yote nchini.

Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) aliyasema hayo wakati akizindua mpango wa kutoa huduma za upasuaji wa kibingwa bila malipo kwa wakazi wa Jiji la Tanga uliofanyika kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo.

Alisema hivyo uwepo wa mpango huo utawasaidia wana Tanga na watanzania kwa ujumla kupata matibabu, dawa, vifaa tiba bila gharamu yoyote.

Mpango huo ambao utasaidia kufanya upasuaji utafanywa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Peleks Humanitarian Organizationya nchini Uingereza ambapo jumla ya wagonjwa 380 watafaidika kati yao wagonjwa zaidi ya 700 waliofanyiwa uchunguzi.

Kambi hiyo ya matibabu Bingwa ya upasuaji imewezeshwa na Taasisi ya Watumishi Health Check, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Tanga mjini ambap kwa pamoja wamewaleta wataalamu hao wa upasuaji kutoka nchini Uingereza.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Watumishi Afa Check Dkt Siraji Mtulia alisema kuwa upasuaji huo utafanyika kuanzia Novemba 5 hadi 11 mwaka huu na utagharimu milioni 876.

Naye kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Seif Kallage alisema uwepo wa kambi hiyo ni jitihada za Waziri Ummy kwa sababu ni jukumu ambalo amepewa na Rais Samia Suluhu kuhakikisha afya za watanzania vinaimarika na kuboresha huduma.

Alisema hata ukiangalia ile kampeni ya Mama Samia yeye ndio anaiendeleza amenza na Tanga kwa kushirikiana na Peleck anataendelea na mikoa mengine nchini.

Hata hivyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Jonathan Budemu alisema kwamba kambi hiyo itaweza kuwasaidia wananchi na katika watu 700 walionwa na madaktari walikuwa hawana uharaka ule na muendelezo wa kambi hii utawasaidia kuweza kuwaonaa.

Alisema katika kambi hiyo watakuwa na changamoto ya vitanda hivyo Mstahiki Meya wale ambao watakosa maeneo ya kuwaweka wanaomba kuwaweka kwenye vituo vyengine baada ya upasuaji kama Ngamiani na Makorora na vya jirani ili wote waweze kupata huduma kwa wakati.

“Lakini pia wasikose huduma kwa sababu ya kukosa sehemu ya kulala kwa sababu vitanda ni vichache ukilinganisha na wagonjwa wenyewe hivyo wakishafanyiwa wakikosa nafasi hapo watapelekwa kwenye maeneo mengine”Alisema Dkt Budemu.

Katika uzinduzi wa matibabu ya upasuaji wa Kibingwa pia imehudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Seif Kallaghe,Mstahki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Jonathan Budemu na viongozi wa CCM.

Mwisho.




















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger