Thursday, 3 November 2022

Picha : MKUTANO WA 13 WA BUNGE LA AFRIKA JUU YA HAKI ZA WANAWAKE WAFANYIKA...CHARUMBIRA ASISITIZA WANAWAKE WASHIRIKISHWE KWA VITENDO NGAZI ZA MAAMUZI NA UTAWALA

Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP), Mhe. Chief Fortune Charumbira akitoa ujumbe wa Mshikamano wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake.

Na Kadama Malunde - Midrand Afrika Kusini

Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP) juu ya Haki za Wanawake umefanyika leo Alhamisi Novemba 3,2022 katika ukumbi wa Bunge la Afrika Midrand Afrika Kusini ambapo Rais wa Bunge la Afrika Mhe. Chief Fortune Charumbira akihamasisha nchi za Afrika kuwashirikisha wanawake katika utawala na ngazi za maamuzi.

Akitoa Ujumbe wa Mshikamano wakati wa mkutano huo ulioongozwa na mada isemayo ‘Uwezeshaji na ushirikishwaji wa wanawake katika utawala’, na kuhudhuriwa na wanaharakati wa haki za wanawake kutoka nchi mbalimbali, Mhe. Charumbira amesema ni vyema wanawake wakawezeshwa kwa vitendo badala ya kuwafurahisha tu wanawake kwa kusema wanawezeshwa.

“Bado wanawake hawajawezeshwa kikamilifu, bado kuna ni maneno tu. Ni lazima tuwawezeshe wanawake kwa vitendo. Je ndani ya uwezeshaji huu tunaoimba kila mara kuna nini?. Jinsia kwa uhalisia wake ni nini hasa? Tusiyatamke tu maneno haya (Uwezeshaji wanawake) kuwafurahisha wanawake kwa kusema tunawezesha wanawake, tufanye kwa vitendo mfano kwa kuongeza bajeti kwa masuala yanayohusu wanawake”,amesema Mhe. Charumbira.

“Lazima tuwaingize wanawake katika utawala, huku tukitambua kuwa utawala unaenda sambamba na masuala ya siasa hivyo wanawake waingie katika siasa. Tujiulize je kuna wabunge wangapi kwenye mabunge yetu ya nchi, kuna mawaziri wangapi?”,amesema Chifu Charumbira.

Ameongeza kuwa wanawake wanahofu kubwa na vitendo vya rushwa hivyo endapo watapata nyadhifa za uongozi vitendo vya rushwa vitapungua katika nchi za Afrika.

“Suala la rushwa limeturudisha nyuma sana kimaendeleo. Endapo tutakuwa na wanawake wengi katika maeneo mengi ya utawala na ngazi za maamuzi rushwa itapungua. Tukishirikisha wanawake katika masuala ya utawala tutasonga mbele”,amesema Rais huyo wa Bunge la Afrika.

Akizungumzia kuhusu mimba na ndoa za utotoni, Chief Charumbira amesema mimba na ndoa za utotoni bado ni tatizo kubwa katika jamii hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuchukua hatua ikiwemo kutunga sheria kali ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vinakatisha ndoto za watoto wengi. 

“Watoto wa kike wameathirika sana na mimba na ndoa za utotoni ni wajibu wa kila mmoja wetu kuchukua hatua kudhibiti vitendo hivi”,amesema.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Tatu wa Bunge la Afrika, Mhe. Lucia Doss Passos amesema Wanawake wanatakiwa kushirikishwa katika ngazi za utawala lakini pia wawezeshwe kuwa na biashara, umiliki wa ardhi na kupata usaidizi wa kifedha na kuondoa kabisa ubaguzi wa kijinsia,kidini, kisiasa, na kiutamaduni.

“Wanawake wanachukua nusu ya idadi ya watu duniani lakini nafasi yao katika uchumi, kisiasa na utamaduni haioneshwi. Tunapaswa kuweka sheria ambazo zitaweka usawa wa jinsia ili kuleta usawa katika jamii. Wanawake wanatakiwa kupewa nafasi katika nyadhifa za uongozi na maamuzi”,amesema Mhe. Lucia.

“Wanawake wahusishwe katika maendeleo, wapewe elimu, kulindwa kiafya, kuwa na uwezo wa kifedha.Ili kuwa na jamii inayoheshimika lazima wanawake washirikishwe katika shughuli za maendeleo. Wanawake ndiyo wanaweza kuendeleza maendeleo”,ameongeza.

 ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP), Mhe. Chief Fortune Charumbira akitoa ujumbe wa Mshikamano wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP) juu ya Haki za Wanawake leo Alhamis Novemba 3,2022 katika ukumbi wa Bunge la Afrika, Midrand Afrika Kusini. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP), Mhe. Chief Fortune Charumbira akitoa ujumbe wa Mshikamano wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake leo Alhamis Novemba 3,2022.

Makamu wa Rais wa Tatu wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament - PAP), Mhe. Lucia Doss Passos  akizungumza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge la Afrika juu ya Haki za Wanawake leo Alhamis Novemba 3,2022.

Share:

WATEJA BENKI YA CRDB WAJISHINDIA SAFARI YA QATAR KUSHUHUDIA KOMBE LA DUNIA

Benki ya CRDB leo imehitimisha awamu ya kwanza ya kampeni yake ya “Tisha na TemboCard” kwa kuwakabidhi tiketi za kushuhudia mashindano ya Kombe la Dunia wateja wake wanne walioibuka washindi wa jumla wa kampeni hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kubadhi tiketi hizo iliyofayika kwenye makao makuu ya Benki hiyo yaliyopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Manunuzi wa Benki ya CRDB, Pendason Philemon aliwapongeza washindi hao ambao walipatikana kutokana na kufanya miamala mingi zaidi kupitia kadi zao za TemboCard wakati kampeni hiyo ikiendelea.

“Kwa niaba ya benki niwapongeze kwa kuibuka washindi katika kampeni hii ambayo lengo na madhumuni yake ilikuwa ni kuwajengea watanzania utamaduni wa kutumia kadi zao kufanya malipo mbalimbali” alisema Pendason.

Pendason alisema Benki hiyo inafahamu namna ambavyo Watanzania wanapenda michezo na katika msimu huu wa kuelekea mashindano makubwa ya Kombe la Dunia, imeona ni vyema ikawa sehemu ya kutimiza shauku yao ya kushiriki katika mashindano hayo.

Akielezea kuhusiana na zawadi hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul alisema pamoja na tiketi hizo za kushuhudia mechi za Kombe la Dunia, safari nzima ya washindi hao itagharamiwa kuanzia tiketi za ndege kuelekea Doha Qatar, malazi, pamoja na fedha za matumizi wakifika huko.

Washindi walioibuka kidedea kwenye safari ya kushuhudia Kombe la Dunia mwaka huu wa 2022 ni:, Haji Athumani Msangi, Erick Boniface Kashangaki, Kelvin Jackson Twissa na Rajabu Dossa Mfinanga wote ni wakazi wa jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo Benki ya CRDB pia ilikabidhi zawadi za fedha taslimu kwa washindi wengine watatu wa kampeni hiyo ambao ni, Janeth Nyingi amejishindia shilingi Milioni Moja, Benedict Tilisho na Marsh Bakari wamejishindia shilingi laki tano kila mmoja.

Akitoa shukrani kwa wateja na wadau wote walioshirki katika kampeni hiyo, Meneja Masoko wa Bidhaa na Huduma Benki ya CRDB, Julius Ritte alisema kampeni hiyo ya “Tisha na Tembocard” sasa inakwenda kuingia katika awamu ya pili huku akiwataka wateja kuendelea kutumia kadi zao za TemboCard.
Mkurugenzi wa Manunuzi wa Benki ya CRDB, Pendason Philemon (wa pili kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya safari iliyolipiwa kwenda Doha – Qatar kushuhudia mashindano ya kombe la Dunia mmmoja wa washidi Haji A. Msangi (katikati) katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa jumla katika hitimisho la awamu ya kwanza ya kampeni “Tisha na TemboCard”, iliyofanyika Makuu ya Benki, Palm Beach, jijini Dar es salaam leo Novemba 03, 2022. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati Bonaventure Paul, Mkuu wa Kitengo cha Masoko Joseline Kamhanda, na Mkuu wa Biashara ya Kadi Benki ya CRDB, Farid Seif.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger