Saturday, 27 August 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AGOSTI 27,2022












Share:

Friday, 26 August 2022

Tanzia : AFISA UHAMIAJI MKOA WA SHINYANGA RASHID AFARIKI DUNIA


Ofisa Uhamiaji wa mkoa wa Shinyanga, Rashid Salum Magetta amefariki dunia leo asubuhi Ijumaa Agosti 26,2022 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza.

Mmoja wa maafisa wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga amesema Afande Rashid Salum Magetta amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Bugando Mkoani Mwanza.

R.I.P Afande Rashid Salum Magetta.
Share:

MGEJA AWAOMBA WATANZANIA KUDUMISHA MILA NA UTAMADUNI


Mwenyekiti wa Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja (katikati) amewaombaWanatanzania kudumisha utamaduni kwa kupenda vyakula vya asili kwani vina faida nyingi katika kujenga afya ya mwili.


Mgeja ametoa ushauri huo ofisini kwake Mjini Kahama alipokuwa akipata chakula cha asili asubuhi alipotembelewa na wajasiriamali na kupeana ushauri wa ukuzaji wa mitaji.

"Wenzetu raia wa China wameshikilia utamaduni wao na kuendeleza mpaka sasa ushauri wangu sio mbaya au dhambi kuiga mazuri kwa mwenzako",amesema Mgeja.

Share:

WANANCHI MBIZI WASHINDWA KUTUMIA MAJI YA BOMBA


Moja ya miundombinu ya maji wilayani Kakonko
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kakonko,Fidelis Ndelego,akizungumza na madiwani
Madiwani wa Kakonko wakisikiliza kwa makini wakati kikao kikiendelea.

***

Na Daniel Limbe,Kakonko

LICHA ya Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa) wilayani Kakonko mkoani kigoma kushika nafasi ya kwanza kitaifa kwa usambazaji wa bora wa maji, baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mbizi kata ya Kakonko wameshindwa kutumia huduma hiyo kutokana na imani potofu.


Hayo yamebainishwa kwenye baraza la madiwani wa halmashauri hiyo na Kaimu Meneja wa Ruwasa,Denis Manji,wakati akijibu swali lililoulizwa na diwani wa kata ya Kakonko,Masumbuko Linze,aliyetaka kujua ni lini wananchi wake satanufaika na huduma ya maji safi.


Pamoja na mambo mengine,Manji amesema Kijiji cha Mbizi kimewekewa vituo vitatu vya kutolea maji lakini wananchi wameshindwa kuvitumia badala yake wameendelea kutumia maji ya chemichemi hali iliyosababisha kushusha bei ya maji kutoka shilingi 50 kwa ndoo moja ya lita 20 hadi kufika shilingi 20.


Amesema kuwa wakala hiyo, imefanikiwa kusambaza maji kwa aslimia 87 kwenye wilaya ya Kakonko huku vijiji vinne pekee ndiyo vikiwa vimesalia kupata huduma hiyo.


Amevitaja vijiji hivyo kuwa ni Kabale,Nyamtukuza, Huruhuru pamoja na Nyakiyobe na kwamba ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu mamlaka hiyo itakuwa imeunganisha mtandao wa maji kwa aslimia 91.


Hata hivyo,Manji amewataka Madiwani hao kuwasisitiza wananchi wao kuvuta maji majumbani pamoja na kulipa gharama za utumiaji kwa lengo la kusaidia huduma hiyo kuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Fedelis Ndelego, ameipongeza Ruwasa wilaya ya Kakonko kwa jitihada kubwa za kusambaza maji vijijini na kwamba waendelee kusambaza hadi kwenye vijiji vilivyosalia ili kuvuka malengo waliojipangia.

Share:

JINSI YA KUGUNDUA KAMA MTOTO WAKO ANA KIPAWA


Suala la kwamba mtoto anaweza kuwa na zawadi ya kipaji ni jambo ambalo wakati mwingine linaweza kupingwa.

Kwa upande mmoja, wanasayansi wa neva pamoja na wanasaikolojia na wengine wanasema kwamba watoto pekee wana mgao wa akili (IQ) ambayo ni zaidi ya inavyopaswa kuwa, kuwa nayo ni zawadi kubwa.


Kwa upande mwingine, wananadharia wa elimu pamoja na wale wanaotoa mafunzo ya michezo, wanasema kuwa Zawadi ya aina hii ni hatua kubwa, na pia wanasema kwamba watoto wana akili katika baadhi ya mambo tofauti.


Mjadala kuhusu mada hii bado unaendelea kwa muda mrefu.

Lakini kuna makubaliano kwamba watoto wanaofanya mtihani wa IQ ili kujua kiwango chao cha akili wana vipawa vya angalau asilimia 97.


Kwa mfano, huko Brazili, Theo Costa Ribeiro ni mtoto mwenye umri wa miaka sita kutoka jiji la Sao Paulo, ambaye ana zawadi ya hekima.


Alianza kuzungumza akiwa na umri wa miezi sita tu, na alipokuwa na umri wa mwaka mmoja na miezi sita tu, alianza kusema kwa sentensi na kuanza kwenda shule.


Ygor Ribeiro, babake Theo, anasema kwamba "aliona neno moja na akatuuliza maana ya neno hilo, kwa maneno mengine, lakini maswali hayo hayakuwa maswali ya kijinga."


Ygor aliambia BBC kwamba familia yake haikumlazimisha Theo kujifunza chochote, wala hawakupuuza maswali yake.


Wakati Theo alipokuwa na umri wa miaka mitatu, alikuwa tayari kusoma, kuandika na kufanya hisabati.


Walimu walikuja na kuwataka wazazi wake wampime IQ, kwa sababu alionyesha akili nyingi kuliko wenzake.


Jaribio hilo lilionyesha kuwa Theo, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka mitano, alikuwa na akili ya mtoto wa miaka 14-15.


Hii haimaanishi kuwa haishi kama mtoto. Anapenda kupata marafiki wapya, anapenda kucheza michezo, michezo ya harakati na anapenda kucheza na watoto wa umri wake.


Utagunduaje kwamba mwanao ana kipawa?


Kwa kuanzia, ingawa ni kiashiria kizuri, kwamba mtoto mwenye akili ya juu haimaanishi kuwa ana kipawa, inajulikana haswa baada ya kukamilika kwa vipimo mbalimbali, haswa IQ ambayo hufanywa kuelewa asili ya ubongo.


Wanasaikolojia wa neva /au wanasaikolojia na wataalamu katika nyanja hii hufanya utafiti huu.


Haya ni mambo ambayo Sekretarieti ya Elimu Maalum ya MEC (2006) inabainisha mambo yanayoweza kuashiria kuwa mtoto wako amejaaliwa:



Udadisi
Misamiati zaidi ya wenzake
Mwanafunzi anayeshika haraka na uwezo wa juu wa kiakili
Kufikiri kwa haraka
Kuwa kiongozi na kujiamini
Kukumbuka mambo haraka
Kuwa mbunifu
Uwezo wa kurekebisha au kubadilisha mawazo yake
Kuchunguza siri
Jitahada za kupata anachotafuta
Mtoto anaandika kwenye kompyuta



Kwa upande mwingine, kuna watoto ambao wana zawadi ya hekima ambayo hawajui kama wanayo.


Wakati fulani hawapendi kwenda shule, wakati mwingine wana matatizo ya kitabia.


"Kuna watu wengi wenye vipawa ambao hawafanyi vizuri shuleni kwa sababu hawana nia ya kujifunza, na kwa sababu hakuna kitu cha kusisimua akili zao, shuleni wamechoka na hawaboreshi kile wanachoweza kufanya," alisema Fabiano de Abreu , daktari katika uwanja wa 'sayansi ya neva'.

Chanzo - BBC Swahili
Share:

MKUU WA POLISI AFUKUZWA KAZI KWA UZEMBE


Pete Arredondo

MKUU wa Polisi, Pete Arredondo aliyetuhumiwa kwa kutochukua hatua stahiki katika tukio la mauaji ya wanafunzi 19 na walimu wawili huko Uvalde, katika Jimbo la Texas, amefukuzwa kazi nchini Marekani.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya bodi ya shule kupiga kura kwa kauli moja ya kumfukuza kazi Arredondo ambaye alikuwa likizo tangu Juni mwaka huu.


Shangwe zilisikika katika ukumbi huku bodi ya wadhamini wa Shule ya Robb Elementary ikiwasilisha hoja ya kumwondoa kwenye wadhifa wake mara moja.

Shambulio la mauaji ya Wanafunzi na Walimu lilitokea Mei 24, mwaka huu katika Shule ya Msingi ya Robb Elementary

Taarifa iliyotolewa na mawakili wa mkuu huyo wa polisi inaeleza kuwa Arredondo alikuwa hamjui mtu yeyote aliyekuwa ndani ya madarasa kisha kufyatua risasi.

Tukio la mauaji ya wanafunzi na walimu limetokea miezi mitatu iliyopita ambapo ilikuwa ni kabla ya wiki mbili muhula mpya wa shule kuanza.


Shambulio hilo limetokea Mei 24, mwaka huu katika Shule ya Msingi ya Robb Elementary na kwamba lilikuwa tukio baya zaidi la ufyatuaji risasi kuwahi kutokea nchini Marekani.

Askari Polisi wakliwa katika eneo la tukio

Wazazi wengi waliokuwa wahanga wa tukio hilo wameonesha kukerwa sana na mwitikio wa polisi nchini humo hivyo kumekuwa na shinikizo la kutaka vyombo vya sheria kuwawajibisha polisi.


Arredondo alikosolewa vikali kutokana na kuchelewa kwa maafisa kwa dakika 77 ili kumkabili kijana huyo mwenye bunduki na ndiye afisa wa kwanza kufukuzwa kazi.


Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao
Share:

Thursday, 25 August 2022

WFP YAKABIDHI VIFAA VYA MAWASILIANO OFISI YA WAZIRI MKUU KUKABILIANA NA MAJANGA

 

Naibu  Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Ummy Nderiananga.

Na Dotto Kwilasa, DODOMA

 NAIBU  Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Ummy Nderiananga amepokea vifaa vya mawasiliano vitakavyotumika katika kukabiliana na maafa mbalimbali hapa nchini ambavyo ni  Ndege zisizo na Rubani (Drones) zenye thamani ya shilingi Milioni 102,741,400 vilivyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la  Mpango wa Chakula Duniani (WFP).

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma Ummy  amesema vifaa hivyo vitawezesha Ofisi ya waziri mkuu  kutekeleza shughuli za uratibu na  udhibiti  wa maafa  mbalimbali hasa katika kuchukua taarifa  katika picha ili kupata  majanga na madhara pindi yanapotokea katika nyanja za sekta na taasisi za serikali.

Ameeleza kwamba vifaa hivyo ni muhimu kwa kuzingatia jukumu kuu la Ofisi ya Waziri Mkuu ambalo ni Uratibu wa shughuli za Serikali  na uratibu wa shughuli za maafa na taasisi zisizo za kiserikali kwa njia ya mtandao.

 “Kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, tunaishukuru WFP  binafsi na shirika la WFP kwa kutupatia vifaa hivi muhimu kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano kwa njia ya mtandao, kufanya operesheni za utafutaji na uokoaji, kupata ramani za hatari zilizopo, uwezekano wa kuathiriwa na janga na uwezo wa jamii husika,”amesema Naibu waziri huyo.

Aidha ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na  Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ambayo yamekuwa yakiiunga mkono Serikali katika miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi na Taifa.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu ) Ummy Nderiananga, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. John Jingu amebainisha kwamba  Ofisi ya Waziri Mkuu iko tayari kushirikiana na  (WFP) kwa kila eneo ambalo watahitaji ushirikiano huku akiahidi vifaa hivyo kutumika kama ilivyokusudiwa.

 “Tunakumbana na maafa mengi na huwa inachukua mda mrefu kwa waokozi au upataji wa taarifa unachelewa hivyo,kwaajili ya hizi drone naamini ufanyaji kazi na upatikanaji wa uhalisia wa tukio utapatikana kwa urahisi”amesema

Aidha  Mkurugenzi Mkazi Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)Sarah Gibson mefafanua kuwa mradi huo  ni endelevu kwa miaka mitano kuanzia Julai 2022 hadi Juni 2027 na kwamba Shirika litafanya kazi zake kulingana na vipaumbele vya serikali na kuwenkeza katika kilimo, elimu na  maafa
Share:

HAYA HAPA MAGZAETI YA LEO IJUMAA AGOSTI 26,2022



























Share:

DC MBONEKO AHAMASISHA WAKUU WA KAYA KUACHA TAARIFA HIZI MUHIMU NYUMBANI KUFANIKISHA SENSA


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko
**

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewasihi wakuu wa kaya kuhakikisha wanaacha taarifa muhimu wanapoondoka nyumbani, ili kufanikisha zoezi la Sensa ya Watu na makazi linaloendelea nchini kote.


Mboneko amezitaja taarifa hizo kuwa ni pamoja na Namba za kitambulisho cha taifa (NIDA), kwa kila mwanafamilia mwenye sifa ya kuwa na kitambulisho hicho, kadi ya Bima ya Afya kwa wenye nazo, pamoja na namba za simu za mkuu wa Kaya.


Amesema namba hizo ni muhimu kuachwa kwa anayebaki nyumbani, ili makarani wa Sensa wazitumie kumpigia mkuu wa Kaya pale wanapohitaji ufafanuzi wa taarifa mbalimbali.


Wakati huohuo Mboneko amewasisitiza Wananchi kuendelea kushirikiana na Makarani wa Sensa, pale wanapofika katika familia zao, ili kufanikisha zoezi hilo, ambalo ni muhimu katika kuiwezesha Serikali kupanga mipango ya Maendeleo.


Zoezi hilo la Sensa ya Watu na makazi ambalo limeanza nchini kote Jumanne Agosti 23 ,2022, limeelezwa kuwa litachukua muda wa siku kumi mpaka kukamilika kwake, ambapo kwa muda wa siku sita kuanzia siku ya kwanza ya Agosti 23 hadi Agosti 28, 2022, Makarani Sensa watajielekeza katika kuchukua taarifa za Wanafamilia pekee, ambapo siku nne zilizosalia kuanzia Agosti 29 hadi 31 mwaka 2022, watarudi tena kwenye kaya walizopita kwa ajili ya kuchukua taarifa za Majengo.


Zoezi hilo ambalo kwa mwaka huu linafanyika Kidigitali, linachukua muda wa siku kumi kutokana na taarifa muhimu zinazohitajika, ambazo hazikuwemo kwenye Madodoso ya Sensa zilizopita.
Share:

KARANI AJIUA AKIGOMBANA NA MKEWE...AACHA UJUMBE NA KISHIKWAMBI





Kamba ya katani

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao, amesema kuwa Karani wa Sensa ambaye alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi Buchenjegele wilayani Igunga, aliyejinyonga mkoani humo aliacha ujumbe ambao ulihusisha mgogoro wa kifamilia baina yake na mke wake.

Karani huyo aliyefahamika kwa jina la Edmund Zakayo, amejinyonga Agosti 22, 2022, majira ya saa 10:00 ndani kwake kwa kujitundika juu ya kenchi ya nyumba kwa kutumia kamba ya katani iliyosokotwa .

Katika eneo la tukio hilo jeshi la polisi lilikuta ujumbe ambao uliandikwa na marehemu ukihusisha mgogoro wa kifamilia baina yake na mke wake, hata hivyo pamoja na barua hiyo marehemu aliacha nyaraka zote ambazo alikabidhiwa kama karani kwa ajili ya zoezi la sensa ikiwemo kishikwambi.

Chanzo - EATV
Share:

KIJANA WA WAZIRI SIMBACHAWENE AHUKUMIWA MAHAKAMANI




Mahakama ya kinondoni imemhukumu Mfanyabiashara, James Simbachawene (24) ambaye ni mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene, kulipa faini ya Sh250, 000 na kufungiwa leseni yake ya udereva kwa miezi sita baada ya kukiri makossa matatu.


Mshtakiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano Agosti 24, 2022 jioni na kusomewa mashtaka yake na wakili wa Serikali, Daisy Makakala, mbele ya Hakimu Mkazi Aron Lyamuya.


Mashitaka hayo ni pamoja na kuendesha gari kwa hatari, kuendesha gari akiwa amelewa na kuendesha gari bila kuwa na bima.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, mshtakiwa amekiri na ndipo hakimu Lyamuya alipoahirisha kesi kwa muda ili kumwandikia hukumu.

Baada ya muda mfupi, ndipo hakimu Lyamuya amemhukumu mfanyabiashara huyo kulipa faini ya Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari kwa hatari, Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na Sh50,000 kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na bima.

Mbali na faini hiyo, leseni ya Simbachawene imefungiwa kwa miezi sita.

Awali, Wakili Makakala alidai kuwa mshtakwia anakabiliwa na kesi ya makosa ya Usalama barabara namba 284/2022.
Share:

Wednesday, 24 August 2022

MTOTO WA MBUNGE MWAMBE AFARIKI KWA KUNYWA MAJI MENGI SWIMMING POOL


Cellie Mwambe kwenye picha akiwa na Baba yake
 **
CELLIE Mwambe (14), ambaye ni mtoto wa Mbunge wa jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe, amefariki dunia jana Agosti 23, 2022, baada ya kujirusha kwenye swimming pool ya nyumbani kwao maeneo ya Ada Estate Kinondoni Dar es Salaam, wakati akicheza na wenzake na kujigonga chini.


Akizungumza hii leo Agosti 24, 2022, kuhusu tukio hilo, mbunge huyo amesema kwamba, mtoto wake huyo baada ya kujirusha alienda upande wenye kina kidogo na kujigonga chini na kwamba alichelewa kutolewa majini ili kupelekwa hospitali.


“Hakukuwa na watu wazima karibu hivyo akanywa maji mpaka walipokuja kumuokoa ikawa ‘late’. Walivyomfikisha hospitalini ikashindikana kumuokoa, alifia hospitali baada ya kuwa amekunywa maji mengi nadhani hata pale alipojigonga alipata jeraha kubwa,” amesema Mbunge Mwambe.


Mwili wa marehemu Cellie unatarajiwa kuzikwa keshokutwa, Ijumaa, Agosti 26, 2022, jimboni Ndanda mkoani Mtwara.
Share:

MWALIMU MKUU AANGUKA NA KUFARIKI AKIELEKEA SHULENI


Hali ya huzuni ilitanda katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Shitoto iliyoko Mumias Mashariki, Kaunti ya Kakamega baada ya mwalimu wao mkuu kuzirai na kufariki alipokuwa akielekea shuleni.


Akizungumza na moja ya vyombo vya habari ,mtoto wake Edgar Akwabi alisema marehemu Lily Mbati ambaye alikuwa na ugonjwa wakisukari alikuwa mzima usiku wa kuamkia jana.


"Nilizungumza na mama kwa simu na kumhimiza anywe dawa zake kama kawaida, na alinijibu kuwa atafanya hivo," Akwabi alisema.


Baadaye alipigiwa simu asubuhi na majirani waliomjulisha kuwa mama yake alianguka akielekea kazini na kufariki.


Naibu wa Mbati, Ruth Musafu kwa upande wake alimkumbuka marehemu bosi wake kama kiongozi wa kutegemewa, aliyejitolea na aliyependa kazi ya ualimu.


"Sote tutamkumbuka sana. Tunaomba neema huku tukimuomboleza mkuu wetu mpendwa," Musafu alisema.


Marehemu Mbati ndiye aliyekuwa mwalimu pekee wa somo ya Sayansi ya Nyumbani katika shule hiyo.


Taasisi hiyo imeitaka Wizara ya Elimu kuliangalia suala hilo wanapojiandaa na mitihani ya kitaifa.


Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia aiti cha hospitali ya St Mary's.


Haya yanajiri baada ya kifo ya naibu ya mwalimu mkuu katika shule ya wasichana ya Migigo, ambapo mtoto wa marehemu mvulana aliuwa mamake katika hali isiyoeleweka.


Hii ikiwa ni kisa cha pili mwezi huu kuhusu vifo vya walimu kwa hali isi
Share:

KAULI YA KWANZA YA MKE WA MAREHEMU AUGUSTINO MREMA


Kufuatia kifo cha aliyekuwa mwanasiasa mkongwe na mwenye wa chama cha TLP Augustino Lyatonga Mrema, mke wake Doreen amefunguka haya.


“Namshukuru Mungu kwa maisha aliyompatia hapa duniani na kipindi ambacho nilipata nafasi ya kuwa naye pamoja.
Nitakumbuka vitu vingi kutoka kwake, siwezi kuvisema kwa sasa, ila yule ni mume wangu, rafiki yangu, mpenzi wangu, alikuwa mshauri na mwalimu wangu, ni vingi ambavyo namkumbuka navyo kwa sasa siko sawa kuongea ila nikikaa vizuri nitaongea na Watanzania,” alisema Doreen.


“Kwa sasa ninachoweza kusema ni kuwashukuru watu wote waliokuwa wakimuombea mume wangu wakati wa ugonjwa, lakini pia niwashukuru wote ambao mnaendelea kuungana nasi katika kipindi hiki kigumu sana kwetu, naomba tuendelee kumuombea apumzike kwa amani,” alisema


Mrema alifariki dunia Jumapili Agosti 21, 2022, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu, ameacha mke na watoto watano.


Mwili wa marehemu Agustino Mrema unatarajiwa kuzikwa kesho Alhamis mkoani Kilimanjaro
Share:

WAOMBAJI 106,295 WAMETUMA MAOMBI YA KUJIUNGA KATIKA VYUO 76 NCHINI


 Katibu Mtendaji Mkuu Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof.Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 24,2022 Jijini Dar es Salaam.

*****

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Jumla ya waombaji 106,295 wametuma maombi ya kujiunga katika Vyuo 76 vilivyoidhinishwa kudahili.

Aidha Jumla ya programu 757 zimeruhusiwa kudahili ikilinganishwa na programu 724 mwaka 2021/2022.

Ameyasema hayo leo Agosti 24,2022 Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji Mkuu Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof.Charles Kihampa wakati akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa habari.

Amesema kwa mwaka huu kuna jumla ya nafasi 172,168 ikilinganishwa na nafasi 164,901 mwaka uliopita. Hii ni ongezeko la nafasi 7,267 sawa na asilimia 4.4 katika programu za shahada ya kwanza.

“Katika mwaka wa kwanza ya udahili, Jumla ya waombaji 75,163 sawa na asilimia 70.71 ya waombaji wote walioomba udahili wameshapata udahili vyuoni”. Amesema Prof.Kihampa.

Aidha amesema mwenendo wa udahili wa awamu ya kwanza kwa kipindi Cha miaka mitano (2018/2019 hadi 2022/2023) unaonesha ongezeko kubwa la waombaji ikiashiria ongezeko la wahitimu wa kidato cha Sita na wale wa Stashahada.

Pamoja na hayo Prof.Kihampa ametoa wito kwa waombaji udahili wa shahada ya kwanza wanakumbushwa kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasikishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.

“Kwa wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa”. Amesema
Share:

MKOA WA KATAVI UMEFANIKIWA KUYAFIKIA MAENEO YOTE TA WATU WALIOTAKIWA KUHESABIWA


Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akiwa anahesabiwa na Karani wa sensa wa eneo Namba 002 Astoni Kajiba katika mtaa wa Ilembo manispaa ya Mpanda nyumbani kwake kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi lililoanza tarehe 23.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akiwa katika Mtaa wa Mpanda Hoteli nyumbani kwa Mzee Alikado Mwima wakati akiwa anatembelea kaya mbambali za wananchi wa Mkoa wa Katavi wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya zoezi la sensa linavyoendelea kufanyika Mkoani Katavi katika siku ya kwanza ya zoezi la sensa ya watu na makazi linaloendelea Mkoani hapa na limefanyika kwa ufanisi mkubwa. picha na Walter Mguluchuma

Na Walter Mguluchuma - Katavi.

Mkoa wa Katavi umefanikiwa kuyafikia maeneo yote ya muhimu kwa wakati ambayo watu walitakiwa kuhesabiwa kuanzia saa sita na dakika moja usiku yakiwepo maeneo ya stendi zote za nyumba za kulala wageni ,baa, Hospitalini, magereza, watoto wa mitaani na kwenye treni ya abiria inayofanya safari ya kutoka Mpanda kwenda Tabora.


Pia kwenye zoezi hilo la Sensa ya watu na Makazi linaloendelea kufanyika mkoani Katavi hadi sasa hakuna changamoto yoyote ambayo imeishajitokeza na wananchi wamehamasika sana na wanatoa ushirikiano mkubwa kwa makarani wa sensa .


Akizungumza na waandishi wa Habari mbele ya wananchi wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko kwenye maeneo mbalimbali aliyokuwa akiyatembelea katika Manispaa ya Mpanda wakati akikagua maendeleo ya zoezi la sensa alisema kuwa maeneo yote ya muhimu yameweza kufikiwa kwenye zoezi la sensa kwa wakati na na bila kuwepo kwa changamoto yoyote ile hadi sasa.


Amebainisha kuwa wananchi wa Mkoa wa Katavi wamehamasika  kwenye zoezi hilo na wako tayari kuhesabiwa ambapo kwenye zoezi hili wananchi wamekuwa wakitoa ushirikiano mkubwa huku hali ya maeneo yote ni salama.

Mrindoko alisema kuwa kwenye zoezi hilo wanahakikisha linafanikiwa kwa asilimia mia moja na watu wote wanafikiwa na kuhesabiwa kama ilivyokusudiwa bila kujali hali ya jiografia ya Mkoa ilivyo.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Haasan Abasi Rugwa amesema kuwa zoezi hili katika Mkoa wa Katavi limeanza kwa ufanisi mkubwa huku ulinzi na usalama ukiwa umeimarika na mpaka sasa hakuna malalamiko yoyote ya kutoka kwa wananchi kutokana kazi kubwa ambayo imefanywa ya zoezi la sensa kwenye Mkoa wa Katavi.

Hivyo amewataka kila wananchi wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha anahesabiwa na ndiyo mkakati ambao Mkoa umejiwekea wa kuhakikisha hakuna mtu hata mmoja ambaye hatahesabiwa kwenye zoezi hili .


Karani wa Senza wa eneo namba 002 huko katika eneo la Ilembo Aston Kajiba amesema kuwa zoezi hilo kwa upande wake limekuwa likienda vizuri kutokana na ushirikiano kutoka kwa wana wananchi kwani kila Kaya ambayo amekuwa akiifikia amekuwa amekuta wakiwa tayari wameandaa nyaraka muhimu zinazo hitajika kwenye zoezi hilo hali ambayo inaonyesha kuwa watu wamekuwa na uwelewa wa umuhimu wa sensa ya watu na makazi
Share:

WAZIRI MKUU MSTAAFU AFARIKI GEREZANI


Lounceny Camara

WAZIRI wa zamani wa Guinea Lounceny Camara alikuwa tayari amelazwa hospitali mara moja kabla ya kufungwa jela mwezi Mei, chanzo cha kifo chake kilitokana na kupatwa na kiharusi Ijumaa na alifariki hospitalini jioni iliyofuata, kaka yake alithibitisha.


Familia ya Lounceny Camara ilikata rufaa mahakamani bila mafanikio ili Camara aruhusiwe kusafiri nje ya nchi kupata matibabu, ameongeza kaka yake alie kuwa anatoa taarifa.

Kanali Mamady Doumbouya, Rais wa Guinea

Lounceny Camara,aliekuwa na umri wa miaka 62, ni kati ya mawaziri wa zamani na maafisa waandamamizi walioshtumiwa ubadhilifu wa pesa za umma na kufungwa jela baada ya jeshi kumuondoa madarakani Rais wa zamani Alpha Conde mwaka uliopita.



Imeandikwa:Leokadia Charles kwa msaada wa mtandao
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger