Wednesday, 24 August 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 24,2022




Share:

Tuesday, 23 August 2022

KATAMBI ASHIRIKI SENSA...."KUNA HAJA YA KILA MMOJA KUHESABIWA"


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu, akishiriki zoezi la kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi, kwenye Makazi yake Kata ya Old Shinyanga (kushoto) ni Karani Simoni Samweli akichukua taarifa zake.

Katambi akizungumza mara baada ya kumaliza kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi leo Agosti 23, 2022, amesema
Upo umuhimu wa kila mmoja kuhesabiwa ili Taifa lijue linahudumia watu wangapi na kukidhi matakwa ya wananchi kuirahisishia Serikali kutekeleza majukumu yake.
Share:

UWT MISUNGWI YAKABIDHIWA MIZINGA YA NYUKI 50 KWA AJILI YA MRADI WA UFUGAJI NYUKI


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akimkabidhi mizinga ya nyuki Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania ya Wilaya ya Misungwi, Bahati Makala (kulia) kwa ajili ya mradi wa ufugaji nyuki alipofanya ziara leo. Wengine ni Katibu wa CCM Wilaya ya Misungwi, Cholage Mohamed (katikati), Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Misungwi, Benson Mihayo (wa tatu kutoka kulia), Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Rahma Emmanuel (wa tatu kutoka kushoto) na viongozi wengine wa UWT Misungwi.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akikabidhi mizinga ya nyuki kwa wanajumuiya ya UWT Misungwi kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ufugaji nyuki alipofanya ziara katika Ofisi za UWT Misungwi


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akifurahia baada ya kukabidhi mizinga ya nyuki 50 kwa wanajumuiya ya UWT Misungwi kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ufugaji nyuki alipofanya ziara katika Ofisi za UWT Misungwi leo. Wengine ni viongozi wa UWT Misungwi, CCM Misungwi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akizungumza na wanajumuiya ya UWT Misungwi (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa mradi wa ufugaji nyuki alipofanya ziara katika Ofisi za UWT Misungwi


Baadhi ya wanajumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania wa Wilaya ya Misungwi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (hayupo pichani) akizungumza na wanajumuiya ya UWT Misungwi (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa mradi wa ufugaji nyuki alipofanya ziara katika Ofisi za UWT Misungwi


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misungwi , Cholage Mohamed Cholage akitoa neno la shukrani baada ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kulia kwake) kukabidhi mizinga ya nyuki 50 kwa Jumuiya ya Wanawake Tanzania ya Wilaya ya Misungwi katika Ofisi za UWT Misungwi.

………………………………………..

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja amekabidhi mizinga ya nyuki 50 kwa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) ya Wilaya ya Misungwi kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ufugaji nyuki.

Akizungumza leo katika Ofisi za UWT Misungwi Mhe. Masanja amesema mizinga hiyo imegharimu kiasi cha shilingi milioni tano.

“Naahidi kuongeza mizinga mingine endapo itaendelea kuleta faida kwa jumuiya” Mhe. Masanja amesisitiza.

Amefafanua kuwa mradi huo wa ufugaji nyuki utasaidia mapato ya jumuiya kutokana na mazao ya nyuki ambayo ni asali, nta na sumu ya nyuki ambayo soko lake ni la uhakika.

Mhe. Masanja amefafanua kuwa kupitia mapato yanayotokana na miradi ya jumuiya, itaiwezesha kujisimamia yenyewe hasa katika kukidhi mahitaji muhimu ya wanajumuiya.

Aidha, amewapongeza viongozi wa UWT Misungwi kwa kusimamia vizuri miradi ambapo wameweza kuzalisha lita 40 za nyuki zenye thamani ya shilingi laki nne kutokana na mizinga ya nyuki mitano ya awali.

Pia, Mhe. Masanja ameahidi kuipatia jumuiya hiyo pikipiki nyingine kwa ajili ya kuendeleza mradi wa pikipiki.

Naye, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misungwi , Cholage Mohamed Cholage amewataka viongozi wa UWT Misungwi kuwa waaminifu kwenye kusimamia miradi ya jumuiya ili ilete manufaa yalikosudiwa.

Pia, amempongeza na kumshukuru Naibu Waziri Masanja kwa kuwa na moyo wa kuijitolea mizinga 50 kwa jumuiya ya UWT Misungwi.

Naibu Waziri Masanja anaendelea na ziara katika Kanda ya Ziwa ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku
Share:

DOWNLOAD/ INSTALL UPYA APP YA MALUNDE 1 BLOG..Tumeboresha zaidi

Share:

FULL POWER NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya tendo la ndoa kikamilifu ,shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili, homoni, neva, misuli, hisia na mirija ya damu. Upungufu wa nguvu za kiume huashiria kutokuwa sawa kiafya hivyo ni tatizo linalohitaji tiba.

CHANZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Tatizo la nguvu za kiume lina vyanzo vingi ambavyo mara nyingi wengi huvipuuza, hivyo vyanzo huathiri taratibu na vingine huathiri haraka, tunashauri watu kuwa makini sana ili kujiimarisha vizuri. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata tatizo la nguvu za kiume nayo ni pamoja na;


1. Kuwa na halemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P) au ugonjwa wa moyo

2. Kuvuta sigala na unywaji wa pombe

3. Uzito kupita kiasi na unene uliozidi

4. Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi

5. Kisukari

6. Kuwa na mawazo na wasiwasi

7. Matumizi ya madawa mbalimbali

8. Umri hasa wazee

9. Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili

10. Kuwa na tatizo la kibofu

11. Tabia za kujichua kwa muda mrefu

12. Kutopata usingizi kamili

13. Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibia magonjwa kama kansa, vidonda vya tumbo, moyo, kisukari, B.P, na magonjwa mengine


DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Dalili za kuonesha kuwa una tatizo la upungufu wa nguvu za kiume karibia zote zinahusiana na hali itakayo onekana katika tendo la ndoa au mda wa kujamiiana, hizo dalili zake ni kama;


1. Kuwahi kufika kileleni

2. Kukosa hamu ya mapenzi

3. Kushindwa kurudia tendo la ndoa

4. Uume kusimama kwa ulegevu au kushindwa kusimamisha

5. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu; Miguu, uso na tumbo kuvimba na kujaa maji

6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo

7. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa)

8. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji


TIBA SAHIHI YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

FULL POWER

⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa

⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.


ZAT 50
⇨ Inarutubisha maumbile ya uume na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.


Pia tunatibu Magonjwa mengine kama


Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonda vya tumbo, Kisukari, Magonjwa sugu ya zinaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kung’oa


Ndugu mteja Epuka midawa inayouzwa mitaani ambayo sio sahihi kwa matumizi ya binadamu JALI AFYA YAKO OKOA NDOA NA MAISHA YAKO

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27 au 0754568767  utatumiwa sehemu yoyote ulipo
Share:

Monday, 22 August 2022

TBS YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUSAJILI BIDHAA ZA CHAKULA NA VIPODOZI

Kaimu Meneja Usajili wa Bidhaa na Majengo TBS, Bi.Gwantwa Mwakipesile akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti22,2022 katika ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es Salaam Afisa Udhibiti Ubora TBS, Bi.Mbumi Mwampeta akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti22,2022 katika ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es Salaam.

***************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kuwakumbusha wazalishaji,wasambazaji na wauzaji wa bidhaa kuhakikisha wanasajili bidhaa zao za chakula na vipodozi na majengo ili kuweza kumlinda mtumiaji.

TBS imekuwa inafanya usajili wa bidhaa za chakula na vipodozi na majengo yanayofanyiwa usajili ni majengo ambayo yanajihusisha na biashara za bidhaa za chakula na vipodozi.

Akizungumza leo Agosti 22,2022 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Usajili wa Bidhaa na Majengo TBS, Bi.Gwantwa Mwakipesile amesema lengo la kufanya usajili wa bidhaa na majengo ni kujiridhisha kabla ya kuruhusu majengo kutumika kuhifadhi bidhaa za vipodozi na chakula kwamba yanakidhi vigezo vilivyowekwa ambavyo vitafanya bidhaa zinazotunzwa kwenye majengo hayo ziendelee kuwa bora na salama kwaajili ya matumzi.

Amesema usajili wa vyakula unafanyika kabla ya vyakula havijaruhusiwa kuingia nchini na kuuzwa ili kujiridhisha kwamba bidhaa hizo zinakidhi viwango na vigezo mbalimbali vya usalama na ubora vilivyowekwa kabla ya bidhaa hizo hazijaruhusiwa kuuzwa kwaajili ya matumizi ya binadamu.

"Katika usajili wa bidhaa, yapo mahitaji tofautitofauti kulingana na aina ya bidhaa zinazosajiliwa. Suala hili la usajili linafanyika kwa mujibu wa sheria ya viwango ambapo pia zipo kanuni zilizotungwa chini ya sheria hiyo na kanuni moja wapo ipo kanuni ambayo inahusika na mambo ya import regestration na product registration ambayo yenyewe inapatikana kwenye tovuti ya TBS". Amesema Bi.Mwakipesile

Aidha amesema katika usajili mambo makubwa ambayo Shirika linaangalia ni suala zima la vifungashio vinavyotumika kuhifadhi bidhaa hizo za chakula na vipodozi lakini pia wanaangalia usalama na ubora wa viambato na vikolezo vilivyotumika katika kutengeneza bidhaa hizo na vilevile pia wanaangalia taarifa zilizopo kwenye lebo ya bidhaa.

"Taarifa zinazowekwa kwenye lebo ni aina ya mawasiliano kutoka kwa mtengenezaji wa bidhaa kwenda kwa mtumiaji kumpa taarifa kwamba hii bidhaa unayotaka kuitumia au bidhaa niliyoitengeneza ina vitu mbalimbali kama jina na matumizi". Amesema

Nae Afisa Udhibiti Ubora TBS, Bi.Mbumi Mwampeta amesema mara baada ya mfanyabiashara kusajili bidhaa yake ya Vipodozi atapatiwa Cheti na atatakiwa kuhuwisha Cheti hicho kila baada ya miaka Mitano (5) hivyo amewaomba wafanyabiashara wote wa Vipodozi nchini kutembelea tovuti ya TBS kwa kuanza taratibu za usajili maana ni takwa la kisheria.

Share:

Picha : SHAMRA SHAMRA KATAMBI AKIHAMASISHA SENSA NA KUPONGEZA VIONGOZI WA CCM

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu akiwa amebeba picha ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akiwasili katika Ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini leo Jumatatu Agosti 22,2022 kwa ajili kuwapongeza Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Jumuiya zake Ngazi ya Kata waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa chama hicho sambamba za kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika Agosti 23,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog




Share:

MEYA MANISPAA YA SHINYANGA AGEUKA MBOGO....."SISI SIYO MITAMBO YA KUCHAKATA MAKABLASHA"


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 22,2022.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko ameziagiza taasisi mbalimbali katika Manispaa hiyo kuwa wanapeleka taarifa zao (Makablasha) kwa wakati badala ya kusubiri hadi siku ya kikao na kupeleka taarifa mezani akibainisha kuwa Madiwani hawawezi kusoma makablasha na kuelewa taarifa wakati kikao kinaendelea.

Masumbuko ametoa agizo hilo leo Jumatatu Agosti 22,2022 wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

“Nikupongeze Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola kwa kitu kimoja ambacho umekuwa tofauti na taasisi zingine,.... umekuwa wa kwanza kutuletea taarifa yako ambapo Waheshimiwa Madiwani wameipitia vizuri, wakaichakata na wakaielewa na maswali yamepungua. Lakini taasisi zingine tunakutana na taarifa zao mezani, mnategemea sisi tunapata muda gani wa kuelewa mambo haya?, Kablasha la SHUWASA tumelipata mapema sana”,amesema Meya huyo.


“Leteni Makablasha yenu kwa wakati, Sisi siyo mitambo ya kuchakata makablasha wakati kikao kinaendelea…. Sisi siyo mitambo ya kuchakata makablasha kiasi hicho, kwa hiyo tunaomba tuzipokee taarifa hizo mapema, kwa hiyo hili nisisitize hili lisijirudie tena, tulichukue kuwa ni jambo la msingi kwani sisi Madiwani ni wasimamizi wa Halmashauri lazima tuwe na taarifa za kutosha”,amesema Masumbuko.


“Sijaelewa kwanini tunapokea taarifa mezani…huo muda wa kusoma makablasha mezani haupo kwa hiyo tutapitishana tu tutapishana tu, sisi Halmashauri hatutaki kuendesha vikao kwa namna hiyo, tubadilike kama tunataka kuipeleka hivyo basi tuipeleke Kidijitali, sasa tutachakata vipi taarifa yako umetuletea mezani?, mwingine taarifa yake ina kurasa nane, nyingine 10",ameongeza.

Soma Pia :
Share:

ODINGA ATUA MAHAKAMA KUU KUPINGA URAIS WA RUTO

Mahakama Kuu ya nchini Kenya
Raila Odinga
**

RAILA Odinga aliyekuwa mgombea katika nafasi ya Urais Kenya ameahidi leo saa nane kupeleka mapingamizi ya kushinda kwa mpinzani wake Rais Mteule wa Kenya William Ruto katika kura zilizopigwa Agosti 19, 2022.


Odinga, mgombea mwenza wake Martha Karua, na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka jana walisalia na msimamo wakisisitiza kwamba adhma yao katika Mahakama ya upeo itaonyesha ulimwengu jinsi ushindi wao “uliibiwa”.

Wakenya wanasubiri kuona maamuzi yatakayo tolewa na mahakama kuu kama yatafanana na maamuzi ya uchaguzi uliopita, katika hali hiyo Mahakama inatarajia kuweka historia nyingine ya kutoa maamuzi.



Hadi sasa Tume huru ya Uchaguzi nchini Kenya imemtangaza William Samoei Ruto kama Rais Mteule wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Kenya
Share:

SATURA : TUNAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA KIJAMII MANISPAA YA SHINYANGA ILI KULINDA HADHI YA MAKAO MAKUU YA MKOA


Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 22,2022.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura amesema Maboresho ya huduma za kijamii yanayoendelea katika Manispaa ya Shinyanga ni sehemu ya mikakati ya kuendelea kulinda hadhi ya Makao Makuu ya Mkoa wa Shinyanga.

Satura amesema hayo leo Jumatatu Agosti 22,2022 wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

“Jukumu la msingi tulilo nalo ni kuwaletea wananchi maendeleo, kubwa zaidi ni uboreshaji wa huduma za kijamii na mahitaji mengine ya kijamii sambamba na kukuza uchumi na katika hili la kukuza uchumi kuna kilimo, mifugo na biashara”,amesema Satura.

“Fursa kuu tuliyonayo sisi Manispaa ya Shinyanga ni kuwa makao Makuu ya Mkoa wa Shinyanga. Sisi hatuna madini lakini pia changamoto ya Kijiographia, hali hii imesababisha tuwe na mzunguko duni wa kibiashara. Tunaendelea kuboresha muonekano wa mji wetu kwani hii ndiyo fursa iliyopo kwenye Manispaa ya Shinyanga ili kuendelea kulinda hadhi ya Makao Makuu ya Mkoa”, ameeleza.

Ameongeza kuwa Maboresho ya huduma za kijamii yanayoendelea katika Manispaa ya Shinyanga ni endelevu ili kusitiri manispaa ya Shinyanga.

“Tuna haja ya kuifanya Manispaa yetu ili iendelee kuwa na hadhi ya Makao Makuu ya Mkoa wa Shinyanga. Jitihada tunazoendelea nazo katika kuboresha huduma za kijamii ni kubakiza hadhi ya Makao Makuu ya Mkoa na tuna nafasi ya kuwa Soko ili kuwa na fursa ya kibiashara”,amesema.

“Tuna mpango wa kuanzisha taasisi za elimu ya Juu… Chuo chetu cha Ushirika Tawi la Kizumbi Shinyanga kimetengewa  Dola Milioni 5 ambazo zitaletwa na Serikali kuboresha miundo mbinu ili chuo kiwe na hadhi ya Chuo Kikuu. Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto pia nacho tunaangalia namna ya kukipandisha hadhi kiwe Chuo Kikuu”,ameongeza Satura.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 22,2022. Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura, kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 22,2022.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 22,2022.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 22,2022.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura akizungumza kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 22,2022. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akifuatiwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi (katikati) na Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune (kushoto) wakiandika dondoo muhimu wakati wa kikao cha baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura (kulia), Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (kushoto) akifuatiwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Jomaary Satura wakiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga.
Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kikiendelea
Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kikiendelea
Watumishi wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Watumishi wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga
Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kikiendelea.


Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger