Thursday, 18 August 2022

SIDO , NELICO & PACT WATOA MAFUNZO YA VITENDO KWA WAJASIRIAMALI MANISPAA YA SHINYANGA

Afisa Uendelezaji Biashara SIDO Mkoa wa Shinyanga, Joseph Taban (wa pili kulia) na Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Hopeness Eliya wakionesha sabuni zilizotengenezwa na wajasiriamali waliopatiwa mafunzo ya vitendo kwa muda wa siku 8. Aliyevaa suti nyeusi ni mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo hayo, Simeo Makoba ambaye ni Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Redio Faraja Fm. Kulia ni Afisa Uchumi kutoka shirika la NELICO, Fortunatus Richard akifuatiwa na Afisa Uhusiano Radio Faraja, Getrude Thomas. Wa kwanza kushoto ni mmoja wa wajasiriamali hao Suzana Nuhu.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na New Light Children Center Organization (NELICO) na Shirika la PACT Tanzania wametoa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waweze kujiajiri na kuajiri wengine huku wakiinua uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.

Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku 8 katika ukumbi wa SIDO Mkoa wa Shinyanga yamefungwa leo Alhamisi Agosti 18,2022 na Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyohusisha wanawake 39 na mwanaume mmoja, Makoba ameishukuru SIDO, NELICO na PACT kwa kutoa mafunzo ya vitendo bure kwa wajasiriamali hao ambayo yatawasaidia kujiinua kiuchumi.

“Mmepata mafunzo haya nendeni mkatumie ujuzi mliopata kuanzisha viwanda vidogo ili mjiajiri na kuajiri wengine. Nimeo ana bidhaa mlizotengeneza ni za viwango vya hali ya juu. Kazalisheni bidhaa kwa viwango na ubunifu ili mpate masoko mazuri. Ubora wa bidhaa ndiyo utakuweka sokoni”,amesema Makoba.

Makoba ametumia fursa hiyo kuwataka wajasiriamali kupitia vikundi kuchangamkia mikopo inayotolewa na serikali kwenye Halmashauri za wilaya.

Aidha ameeleza kuwa hivi karibuni Radio Faraja FM Stereo itaanzisha Kipindi maalumu kwa ajili ya wajasiriamali ambapo wajasiriamali wadogo watapewa nafasi ‘Air time’ ya kuelezea shughuli zao.

Kwa upande wake, Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Hopeness Eliya amesema kazi kubwa inayofanywa na SIDO ni kutoa elimu na ujuzi kwa wajasiriamali kwa ajili ya kwenda kutengeneza bidhaa ‘Vitu halisi’ ili wajipatie kipato na kuongeza pato la taifa.

“SIDO ni walezi wa wajasiriamali, njooni SIDO mpate elimu na ujuzi wa kutengeneza bidhaa. Wajasiriamali hawa tumewapa ujuzi ‘mbegu’ nendeni mkakue”,amesema Eliya.

Naye Afisa Uchumi kutoka shirika la NELICO, Fortunatus Richard amewataka washiriki wa mafunzo hayo kwenda kuwa mabalozi wazuri wa NELICO,SIDO na PACT Tanzania huku akiwasihi kutokuwa wachoyo wa ujuzi waliopata kwa watu wengine katika jamii.

“Katumieni ujuzi mliopata kujiinua kiuchumi, msiwe wachoyo wa ujuzi. Usimnyime mtu ujuzi, hata ukimfundisha hawezi kukuzidi ujuzi”,amesema.

Akisoma risala kwa niaba ya washiriki wa mafunzo,Ramadhan Hamis amesema mafunzo hayo yamewaongezea ari na hamasa ya kujiajiri ili kujipatia kipato na kwamba yatawasaidia kuzalisha bidhaa kwa tija na kuingia kwenye soko la ushindani licha ya kwamba changamoto kubwa ni mtaji na vifaa vya kufanyia kazi.
Muonekano wa sabuni za maji, kufulia na kuogea, batiki na vifungashio vilivyotengenezwa  na wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga waliopatiwa mafunzo ya vitendo yaliyotolewa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania. Picha na Kadama Malunde
Muonekano wa sabuni za kuogea ziliotengenezwa  na wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga waliopatiwa mafunzo ya vitendo yaliyotolewa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Afisa Uendelezaji Biashara SIDO Mkoa wa Shinyanga, Joseph Taban akionesha batiki zilizotengenezwa na wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga waliopatiwa mafunzo ya vitendo yaliyotolewa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania. Kushoto ni Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba akifuatiwa na Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Hopeness Eliya.
Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba ( wa pili kushoto) akiangalia vifungashio vilivyotengenezwa na wajasiriamali waliopewa mafunzo ya vitendo na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Afisa Uendelezaji Biashara SIDO Mkoa wa Shinyanga, Joseph Taban (wa pili kulia) akionesha sabuni za kuogea zilizotengenezwa na wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga waliopatiwa mafunzo ya vitendo yaliyotolewa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba akizungumza wakati akifunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba akizungumza wakati akifunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba akizungumza wakati akifunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Wajasiriamali wakimsikiliza Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba.
Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Hopeness Eliya  akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Hopeness Eliya  akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga, Hopeness Eliya  akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
  Afisa Uchumi kutoka shirika la NELICO, Fortunatus Richard akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
  Afisa Uchumi kutoka shirika la NELICO, Fortunatus Richard akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
  Afisa Uchumi kutoka shirika la NELICO, Fortunatus Richard akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Afisa Uendelezaji Biashara SIDO Mkoa wa Shinyanga, Joseph Taban akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Ramadhan Hamis akisoma risala wakati wa kufunga mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kwa wajasiriamali kutoka kata za Ngokolo,Chamaguha, Ndala na Kambarage Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na SIDO, NELICO na PACT Tanzania.
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) wakiwa ukumbini.

Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) wakiwa ukumbini.
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kutoka kata ya Ngokolo wakipiga picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba, viongozi wa SIDO na NELICO
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kutoka kata ya Kambarage wakipiga picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba, viongozi wa SIDO na NELICO
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kutoka kata ya Chamaguha wakipiga picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba, viongozi wa SIDO na NELICO
Washiriki wa mafunzo ya vitendo (utengenezaji wa sabuni, batiki na vifungashio) kutoka kata ya Ndala wakipiga picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi Meneja wa Vipindi na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Matangazo Radio Faraja Fm Stereo, Simeo Makoba, viongozi wa SIDO na NELICO.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

JAPAN YAWATAKA VIJANA WAKE KUONGEZA KASI YA KUNYWA POMBE


Vijana wa Japani hawanywi pombe ya kutosha - jambo ambalo mamlaka zinatarajia kubadilisha kupitia kampeni mpya.


Vijana wa kizazi kipya hunywa kiasi kidogo cha pombe kuliko wazazi wao - hatua ambayo imeathiri ushuru kutoka kwa vinywaji kama sake (mvinyo unaotokana na mchele).


Kwa hivyo shirika la kitaifa linalosimamia ushuru limeingilia kati na shindano la kitaifa ili kubadilisha mawazo ya wengi .


"Sake Viva!" kampeni inatarajia kuja na mpango wa kufanya unywaji wa pombe kuvutia vijana zaidi - na kukuza sekta hiyo .


Shindano hilo linawataka vijana wenye umri wa miaka 20 hadi 39 kushiriki mawazo yao ya biashara ili kuanzisha mahitaji miongoni mwa wenzao - iwe ni kwa ajili ya Kijapani, shochu, whisky, bia au divai.


Kundi linaloendesha shindano la mamlaka ya ushuru linasema tabia mpya - ambazo ziliundwa wakati wa janga la Covid - na idadi ya watu wenye umri wa juu imesababisha kupungua kwa uuzaji wa pombe.


Inataka washindani kuja na matangazo, chapa, na hata mipango ya kisasa inayohusisha akili bandia.


Vyombo vya habari vya Japan vinasema majibu yamechanganyika, na ukosoaji fulani kuhusu jitihada ya kukuza ‘tabia mbaya’ ya unywaji pombe. Lakini wengine wamechapisha mawazo ya ajabu mtandaoni - kama vile waigizaji maarufu "wanaoigiza" kama wahudumu wa uhalisia katika vilabu vya kidijitali.


Washiriki wana hadi mwisho wa Septemba kuweka maoni yao. Mipango bora itatayarishwa kwa usaidizi kutoka kwa wataalam kabla ya mapendekezo ya mwisho kuwasilishwa mnamo Novemba.


Tovuti ya kampeni hiyo inasema soko la pombe la Japan linapungua na idadi kubwa ya watu nchini humo - pamoja na kupungua kwa viwango vya kuzaliwa - ni sababu kuu .


Takwimu za hivi majuzi kutoka kwa wakala wa ushuru zinaonyesha kuwa watu walikuwa wakinywa kiasi kidogo cha pombe mnamo 2020 kuliko 1995, na idadi hiyo ilishuka kutoka lita 100 (galoni 22) kwa wiki hadi lita 75 (galoni 16).


Mapato ya ushuru kutoka kwa ushuru wa pombe pia yamepungua kwa miaka ya hivi karibuni. Kulingana na gazeti la The Japan Times, iliunda 5% ya mapato yote mnamo 1980, lakini mnamo 2020 mapato yalifika 1.7%.


Benki ya Dunia inakadiria kuwa karibu theluthi moja (29%) ya wakazi wa Japani wana umri wa miaka 65 na zaidi - idadi kubwa zaidi duniani.


Wasiwasi juu ya mustakabali pombe ya ‘sake’ sio shida pekee ambayo inayotishia uchumi wa Japani - kuna wasiwasi juu ya usambazaji wa wafanyikazi wachanga kwa aina fulani za kazi, na utunzaji wa wazee katika siku zijazo.

Via >> BBC SWAHILI


Share:

DOWNLOAD/ INSTALL UPYA APP YA MALUNDE 1 BLOG..Tumeboresha zaidi

Share:

SHAKA:RAIS SAMIA ANAIFUNGUA NCHI KUPITIA UJENZI WA BARABARA NCHINI


Shaka akicheza Ngoma yenye asili ya Wanyamwezi katika Kijiji cha Ushokola, Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na Wananchi wa Ushokola katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akisoma baadhi ya Nyaraka zilizowasilishwa kwake na mmoja wa Wananchi kwenye mkutano wa Ushokola katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akimvisha kanga ya Nyamitwe Maganga mkazi wa Ushokola katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).
Shaka akisikiliza kero kutoka kwa Nyandwi Dubo (aliyeshika vipazasauti) huku wananchi wakifuatilia mkutano katika Kijiji cha Ushokola katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Tabora.

***

*Ataja mabilioni ya fedha yaliyotengwa kufanikisha mpango huo

*Ataka wananchi wote kumpongeza na kumuunga mkono kila hatua


Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka amesema Rais Samia Suluhu Hassan amesimama kidete kuhakikisha anaifungua nchi kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Shaka amesema hayo jana alipokuwa akizungumza na wananchi Ushokola wilayani Kaliua mkoani Tabora ambapo alifika kwa ajili ya kukagua ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 2.7 inayojengwa kwa kiwango cha lami.

“Nataka kuchukua nafasi hii kumpongeza kwa dhati kabisa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo watanzania , mmenituma nije nikague barabara hii inayojengwa hapa Kaliua.Kwenye Wilaya hii Rais Samia ndani ya kipindi kifupi sana cha uongozi wake anakwenda kujenga barabara kilometa 10.

“Jambo ambalo halijawahi kutokea tangu nchi imepata uhuru na kwa mara ya kwanza kabisa ndani ya Wilaya hii Rais Samia ndio anajenga barabara za lami. Anawajengea barabara lakini wakati huo huo anawawekea na taa inamaana Kaliua inakwenda kuwa ya kileo,”amesema Shaka.

Ameongeza kuwa “Kwa hiyo wote kwa pamoja tumpongeze Rais Samia , tumekuwa mashuhuda namna Rais Samia amesimama kidete kufungua uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini uchumi wa kikanda na uchumi wa kimaeneo.

“Kukamilika kwa barabara hizi kilometa 10 ni hatua mpya ya kufungua uchumi wa wana Kaliua.Mtasafirisha mazao lakini mtarahisisha maisha yenu ya kila siku kwa kuhakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa urahisi zaidi.

“Kazi hii sio kazi ndogo kumpata Rais mwenye maarifa , mwenye mawazo lakini kupata Rais ambaye anafikiria wananchi wake wanahitajia nini na kwa wakati gani,”amesema Shaka.

Amefafanua ni jambo la kumshukuru Mungu, tunaye Rais anayejua wananchi wake wanataka nini , lakini tunaye Rais ambaye kwa wakati huu anajua wana Tabora wanahitaji nini.

“Tunaye Rais anayejua wana Kaliua wanataka nini , hasa kuliona hilo kwa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan nadhani wote mmesikia amesaini mikataba 10 kwa niaba ya mikataba 968 ambayo inakwenda kujenga barabara za kisasa kabisa.

“Anakwenda kufungua miundombinu ya barabara nchi nzima, mikataba hiyo fedha ni nyingi mno zinazokwenda kutumika zaidi ya Sh.bilioni 248 kwa ajili ya kujenga miundombinu ya barabara ndani ya nchi yetu.Niwaombe wananchi itakapokamilika barabara hizo tutunze ili ziishi kwa muda mrefu,”amesema.

Amewaomba wananchi wote kuendelea kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kwa nia njema aliyokuwa nayo akitoa mfano kwamba Kaliua wameanza kuona maajabu.“Kaliua mlitegemea kuyaona haya nani kama Rais Samia, kwa hiyo maendeleo haya naomba myathamini sana.
Share:

DEREVA WA DALADALA MBARONI TUHUMA ZA KUUA KONDAKTA 'MPENZI WAKE'

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Maarifa Matala mwenye umri wa miaka 45, ambaye ni dereva wa daladala na mkazi wa Kimara kwa tuhuma za mauaji ya mtu aliyedaiwa kuwa mpenzi wake ambaye alikuwa ni kondakta.


Akizungumza Agosti 17, 2022, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kutoroka na kukimbilia mkoani Lindi akidaiwa kumuua mpenzi wake aliyetambulika kwa jina la Sharifa ambaye alikuwa ni kondakta.


Aidha Muliro ameeleza kuwa katika hatua nyingine wamemkamata Gama Swai, anayetuhumiwa kwa kuuza spea za magari zinazodhaniwa kuwa vifaa vilivyoibwa kwenye magari ya wananchi.

Via >EATV
Share:

RADI YAUA WATU WATATU WA FAMILIA MOJA

Watu watatu wa familia moja, wakazi wa kitongoji cha Idoselo, Kijiji cha Kasesa Kata ya Kaseme mkoani Geita wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi iliyoambatana na mvua kali iliyonyesha Agosti 16, 2022, majira ya saa 5:00 asubuhi.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 18,2022

Share:

Wednesday, 17 August 2022

TAWI LA CHUO KIKUU CHA MISRI KUANZISHWA TANZANIA

 

Picha ya pamoja kati ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Balozi wa Misri nchini Tanzania  Mohamed Gaber Abulwafa.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.


Na Dotto Kwilasa, DODOMA


CHUO Kikuu cha Misri kimeeleza kusudio la kuanzisha tawi lake nchini Tanzania kwa ajili ya kuanza kutoa elimu katika fani mbalimbali.


Kutokana na hayo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amemuelekeza Mkurugenzi anayeshughulikia Vyuo Vikuu katika Wizara hiyo Dkt.Kenedy Hosea kuhakikisha anaanza mazungumzo na vyuo vikuu nchini ili kuona ni chuo gani kipo tayari kuanza ushirikiano huo ili utekelezaji uanze mara moja .


Waziri Mkenda ameeleza hayo leo 16, Agosti 2022 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mohamed Gaber Abulwafa katika ukumbi wa mikutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jijini Dodoma.


Amemweleza Balozi huyo kuwa serikali ya Tanzania imetoa fursa ya wawekezaji kuja nchini kwa kufuata taratibu za kisheria na kuwekeza haraka iwezekanavyo.


Amesema  wakati taratibu zingine zinaendelea za uwekezaji huo, Chuo kikuu hicho kinaweza kuunda ushirika na Chuo Kikuu chochote kilichopo nchini ili kuanza kutoa elimu kusudiwa kwa haraka.


Kwa upande wake Balozi wa Misri nchini Tanzania  Mohamed Gaber Abulwafa amemuhakikishia Waziri Mkenda kuwa nchi yake itaendeleza ushirikiano na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu.


Katika mazungumzo hayo wamejadiliana pia namna ya kuanza utekelezaji wa haraka wa (MOU) zilizosainiwa wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoifanya nchini Misri.


Pia Balozi Abulwafa amewasilisha mualiko wa Waziri wa Nishati wa Misri kumualika katika mkutano utakaokuwa unajadili masuala ya Atomiki pamoja na mwaliko wa Waziri wa elimu wa Misri ili kujadili kwa kina umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika sekta ya elimu.



Share:

WAZIRI MBARAWA ATEMBELEA MRADI WA BRT II, AFURAHISHWA NA KASI YA UJENZI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akimuelekeza jambo Msimamizi wa Mradi wa BRT II, Mhandisi Bw.Frank Mbilinyi mara baada ya kutembelea mradi wa BRT II leo Agosti 17,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akiwa pamoja na wahandisi wa ujenzi akitembelea mradi wa BRT II leo Agosti 17,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mradi wa BRT II leo Agosti 17,2022 Jijini Dar es Salaam.Msimamizi wa Mradi wa BRT II, Mhandisi Bw.Frank Mbilinyi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa kutembelea mradi wa BRT II leo Agosti 17,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia nyeusi) akizungumza na wanaohusika na ujenzi wa mradi wa BRT II Mbagara mara baada ya kutembelea mradi wa huo leo Agosti 17,2022 Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa daraja bandari kwaajili ya kutumika mradi wa BRT II

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi BRT II umefikia asilimia 66.6 na unategemewa ujenzi huo kukamilika ifikapo Mwezi Februari, 2023.

Ameyasema hayo leo Agosti 17,2023 mara baada ya kutembelea ujenzi wa mradi huo ambapo amesema hali inaenda vizuri kwa ujumla na kuna mategemeo kumalika kwa muda ambao umewekwa ili mradi huo uweze kufanya kazi.

"Miundombinu muhimu ambayo inatakiwa kusimamiwa kwa makini ni miundombinu ya madaraja hivyo katika daraja lililopo bandarini tumekubaliana kufikia mwezi Desemba 2022 liwe limekamilika na madaraja mengine kufikia Mwezi Januari, 2023 yawe yamekamilika". Amesema Waziri Mbarawa.

Aidha Waziri Mbarawa amewataka wahandisi wanaosimamia ujenzi wa mradi huo kuhakikisha wanaendelea kujenga barabara hiyo na kusimamia kwa viwango walivyokubaliana kwenye mkataba na mpaka sasa kazi ni nzuri na wao waendelee kusimamia.

Pamoja na hayo amewataka wale ambao wapo karibu na mradi waendelee kutoa ushirikiano kwa mkandarasi ili mradi huo umalizike mapema iwezekanavyo ili tuweze kuona matokeo yake kwa muda mfupi.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi wa BRT II, Mhandisi Bw.Frank Mbilinyi amesema kuwa wanatarajia daraja lililopo bandarini kumalizika na magari kuanza kupita kufikia Mwezi Oktoba mwishoni wakati madaraja mengine yameshakamilika kwa upande mmoja na magari yameruhusiwa kupita.

"Madaraja kama pale Chang'ombe, upande mmoja umeshafunguliwa na upande mwingine unaendelea kujengwa na ile fly over ya pale Mandela na Kilwa Road imeshamalizika upande mmoja na magari yanapita na upande mwingine unaendelea kujengwa, ni matazmio yetu makubwa hata hili la bandarini linaweza kukamilika kwa kipindi kizuri". Amesema Mhandisi Mbilinyi.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger