Saturday, 23 July 2022

BINGWA WA MAJI ACHAKAZWA SHINYANGA


Anasifika kwa kumwagia maji marafiki zake pale wanapoadhimisha siku zao za kuzaliwa ‘ Birthday’..Kama una birthday usiombe ukutane naye... Si mwingine ni Mwandishi wa habari maarufu Josephine Charles ambaye hivi karibuni amezindua Kola Online Tv na Kola Liquid Soap…Josephine aliyebatizwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha maji , Humlazimu kutumia mbinu zote ili kuhakikisha anatimiza lengo lake la kumwagia maji ndugu na marafiki.. Na hufurahia sana kwa kitendo hicho!!

Sasa leo Jumamosi Julai 23,2022 akiwa anatimiza miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwake..Mrembo huyo anayejulikana kwa jina la Josephine Charles mkazi wa Shinyanga amejikuta katika wakati mgumu baada ya kunaswa na wadau kisha kupigwa maji na matope ya kutosha kama anavyoonekana kwenye picha!!

La haula!! Josephine Charles yule Bingwa wa maji, mbabe wa maji ya Birthday hana ujanja leo, ama kweli malipo ni hapa hapa duniani.

Happy Birthday Josephine Charles!!
Josephine Charles alivyoanza kumwagiwa maji na marafiki zake
Josephine Charles akiendelea kuoga maji na matope
Share:

KATIBU MKUU WA WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA AFUNGA MAONESHO YA 17 YA TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael akizungumza wakati akifunga Maonesho ya 17 ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania yaliyokuwa yakiendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa akizungumza katika Maonesho ya 17 ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania yaliyokuwa yakiendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) Prof. Penina Muhando akizungumza katika Maonesho ya 17 ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania yaliyokuwa yakiendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA), Prof. Raphael Chibunda akizungumza katika Maonesho ya 17 ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania yaliyokuwa yakiendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wakuu wa Taasisi za Elimu nchini wakifuatilia hafla ya kufunga Maonesho ya 17 ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania yaliyokuwa yakiendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SERIKALI inaendelea na programu mbalimbali za maboresho ya elimu ya vyuo vikuu nchini, ambapo katika mwaka huu wa fedha zaidi ya mitaala 300 inafanyiwa mapitio na kuhuishwa kwa kuzingatia maoni ya wadau mbalimbali ili kukidhi matarajio yao na mahitaji ya soko.

Ameyasema hayo leo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael wakati akifunga Maonesho ya 17 ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania yaliyokuwa yakiendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Amesema Wizara kupitia TCU itaendelea kutoa mafunzo ya kubadilishana uzoefu kwa wana taaluma wa vyuo vikuu kuhusiana na mbinu bora za ukusanyaji wa maoni ya wadau na vigezo vya uandaaji na uhuishaji wa mitaala itakayozingatia mahitaji ya wadau na soko la ajira.

“Wizara imesaini dola za kimarekani milioni 625 kwa ajili ya kujenga Vyuo Vikuu Vishiriki katika Mikoa ambayo isiyokuwa na vyuo vikuu, na Tanzania Bara na Zanzibar kote watapata vyuo vikuu vishiriki ambavyo baadae vitatanuka na kuwa vyuo vikuu,” Amesema

Aidha amesema Serikali imekuwa ikijivunia mafanikio makubwa katika sekta ya elimu kwa upande wa elimu ya juu imeimarisha mifumo ya udhibiti ubora wa elimu inayotolewa na elimu ya vyuo vikuu nchini ili kukidhi viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa.

Pamoja na hayo amesema Serikali kwa kushirikiana na TCU inawajibu wa kuendeleza maonesho hayo kila mwaka hivyo taasisi za vyuo vikuu viongeze muunganiko na vyuo vya nje ili kuwekeza kwenye elimu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) Prof. Penina Muhando amesema maonesho hayo yana lengo ya kujenga na kuimarisha mahusiano baina ya taasisi zetu za elimu ya juu .

"Maonesho haya yatawezesha wananchi kupata fursa za kuona shughuli mbalimbali zinazotendwa na taasisi za elimu ili kuwasaidia wanaotaka kuendelea na elimu ya juu kufanya maamuzi ya kujiendeleza". Amesema Prof.Muhando.

Naye, Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA), Profesa Raphael Chibunda akizungumza kwa niaba ya washiriki wote alihimiza uwepo wa maonesho hayo kila mwaka kwa sababu yamekuwa yakisaidia bidadi ya wadahili kuongezeka.

Share:

WARUNDI WAUAWA TUKIO LA UJAMBAZI KIGOMA


Kaimu Kamanda wa polisi mkoa Kigoma Mendrad Sindano (kushoto) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (kulia) kuhusu tukio la ujambazji wa kutumia bunduki lililotokea wilayani Kakonko mkoani Kigoma ambapo watu wawili raia wa Burundi waliuawa wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa Kigoma Mendrad Sindano akionesha bunduki iliyokamatwa katika tukio la ujambazi lililotokea wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma ambapo watu wawili wanaodhaniwa kuwa raia wa Burundi waliuawa kuhusika na tukio hilo.
Bunduki aina ya AKA 47 iliyokamatwa kwenye tukio la uporaji kijiji cha Bukirillo wilaya ya Kakonko ambapo majambazi wawili wanaosadikiwa kuwa raia wa Burundi waliuawa wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo. (Picha na Fadhili Abdallah)


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

POLISI mkoani Kigoma imewaua kwa risasi watu wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wakituhumiwa kuhusika na tukio la uporaji kwa kutumia bunduki kwenye soko la kijiji cha Bukirilo wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma lililopo mpakani mwa Tanzania na Burundi.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Menrad Sindano akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini Kigoma amesema kuwa tukio hilo lililotokea juzi majira ya saa mbili usiku kijijini hapo ambapo majambazi waliouawa wanadaiwa kuwa ni raia wa Burundi.

Sindano alisema kuwa katika tukio hilo majambazi hao wakiwa watatu wakitumia budnuki aina ya AKA 47 walipora vitu mbalimbali ikiwemo vitenge, simu na pesa taslimu katika maduka matatu likiwemo dula la dawa, vitenge na kibanda cha M-pesa.

“Baada ya tukio hilo wananchi waliripoti tukio hilo kituo cha polisi Gwanumpu wakiomba msaada baada ya kuwazingira majambazi hao wakiwarushia mawe ndipo askari polisi na jeshi kutoka kikosi cha mpakani cha Bukirilo walifika eneo la tukio na kuanza kurushiana risasi ambapo majambazi wawili walijeruhiwa vibaya na mmoja alifanikiwa kukimbia,”Alisema Kamanda Sindano.

Alisema kuwa baada ya majibizano ya risasi na majambazi hayo kujeruhiwa walifariki njiani wakipelekwa hospitali ya wilaya Kakonko ambapo msako unaendelea kumtafuta jambazi mmoja aliyekimbia.

Katika tukio hilo Kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma alisema kuwa walifanikiwa kukamata bunduki moja aina ya AKA 47 ikiwa na magazine mbili na risasi 15 sambamba na maganda matatu ya risasi, simu tisa walizokuwa wamepora na fedha taslimu shilingi 82,000/

Kamanda Sindano alisema kuwa katik upekuzi huo marehemu hao walikutwa na vitambulisho viwili kwenye nguo zao na kutaja majina kwenye vitambulisho hivyo kuwa ni Harelimana Ananias (30) na Nimpangalitse Jean (36) wakazi wa mkoa Ruyigi nchini Burundi.
Share:

SALEH JEMBE " MANARA AACHANE NA MARAFIKI WANAFIKI WANAOMJAZA UPEPO

Haji Manara Msemaji wa Yanga
Saleh Ally ‘Jembe’

MCHAMBUZI wa soka nchini Saleh Ally ‘Jembe’ amesema Haji Manara anapaswa kujiweka mbali na marafiki wanafiki ambao wanamjaza upepo (Kumdanganya) kwamba hana makosa kutokana na hukumu aliyoipata ya kufungiwa miaka miwili kutojihusisha na soka pamoja na faini ya shilingi milioni 20.

Akifanya mahojiano maalum na mwandishi wa habari wa Global TV, Jembe amenukuliwa akisema:

“Mimi natakuwa tofauti na rafiki zake wengine wote, natakakuwa tofauti na rafiki zake especially rafiki zake wanafiki rafiki ambao badala ya kumuambia kitu sahihi cha kufanya wanazidi kumpoteza zaidi kwa kufuata masuala ya kishabiki kwasababu tunaona kweli Haji amekosea na kama amekosea imefikia hatua Haji amehukumiwa hatuwezi kuwa watu wazuri kama tutakuwa tunafurahia kuhukumiwa kwa Haji badala yake tunatakiwa kuwa watu ambao tunatakiwa kumueleza ukweli.”


Aidha Jembe amemtahadharisha Manara kuhusu kutaka kushindana na Mamlaka ya soka nchini kwani kwa kufanya hivyo hawezi kufanikiwa kwa lolote na hakutakuwa na manufaa au afya kwa maendeleo ya soka nchini.


Jembe amemshauri Manara kujitathmini na kuzingatia maelekezo ya Mamlaka ya soka kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kutengeneza mazingira ya yeye kuja kusamehewa baadaye kwani tayari kuna ushahidi wa watu wengi ambao walishawahi kufungiwa na baada ya kuonesha mwenendo mzuri wakafunguliwa vifungo vyao na mmoja wapo ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Fredrick Mwakalebela.
Share:

AMVIZIA KISHA KUMBAKA NA KUMUUA MKE WA RAFIKI YAKE AKIWA KAZINI


Polisi wanawazuilia wanaume wawili kuhusiana na mauaji ya mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 26 eneo la Mowlem, mtaani Umoja katika Kaunti ya Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), Edwin Onditi Odada (mshukiwa mkuu) na Samuel Juma Otieno walinaswa Jumatano, Julai 20, kuhusiana na kifo cha Pamela Asesa.

 Ripoti ya DCI inasema kuwa Odada ambaye ni rafiki wa karibu wa mume wa mwendazake, alibisha kwa nyumba ya wawili hao na Pamela kumkaribisha huku mumewe ambaye ni mhandisi katika kampuni moja kwenye barabara ya Mombasa jijini Nairobi akiwa kazini.


Mshukiwa mkuu anaripotiwa kumbaka mke wa rafiki yake kabla ya kumuua kwa kumnyonga kutumia nguo ambayo pia aliijaza kwenye mdomo wa mwendazake kabla ya kufunga mlango na kutoroka.


Odada amekiri kutekeleza mauaji hayo mnamo Julai 12,2022 huku Otieno akiwa mshukiwa wa pili kwa kupatikana na simu ya mwendazake. 

Uchunguzi wa polisi unaonyesha kuwa mumewe alirejea nyumbani mwendo wa saa mbili usiku na kupata mlango wa nyumba yake umefungwa huku simu zake zikikosa kupokelewa.

 Alitiisha usaidizi na kuvunja mlango huo ambapo alipigwa na butwaa baada ya kupata mwili wa mkewe ukiwa kitandani na kitambaa mdomoni. 

Washukiwa walikamatwa eneo la Tushauriane mtaani Kayole wakitarajiwa kufikishwa mahakamani. Kabla ya tukio hilo, mwanamke huyo aliwahi kumwambia mumewe kuwa rafiki yake alijaribu kumbaka.

 Mshukiwa alikuwa rafiki wa karibu wa mume wa mhasiriwa kiasi kwamba walikuwa wakiishi pamoja katika nyumba hiyo. Oduor hata hivyo alimtimua mshukiwa baada ya kuarifiwa na mkewe kuwa alijaribu kumbaka kisha baadaye akarejea kutekeleza unyama huo.

Via > Tuko news
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 23,2022


Magazetini leo Jumamosi July 23,2022









Share:

Friday, 22 July 2022

JAMII ZATAKIWA KUTUMIA TAMASHA LA SIKU YA UTAMADUNI WA MTANZANIA KUJIKWAMUA KIUCHUMI


*********************

Jamii za Kitanzania zimetakiwa kulitumia Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania kama chachu ya majadiliano ya kimaendeleo na kuunga mkono jitihada za Serikali zinazolenga kuwahimiza Wananchi kujikwamua katika hali ya umaskini, ujinga na maradhi.

Hayo yamesemwa leo Julai 22,2022 na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Siku ya Utamaduni wa Mtanzania iliyowakilishwa na Jamii ya Wasafwa katika eneo la Kijiji cha Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

“Ni matumaini ya Serikali kuwa jamii mbalimbali zitaendelea kulitumia tamasha hili siyo tu kuonesha mila na desturi zao kwa Watanzania wenzao, bali pia kama chachu ya majadiliano ya kimaendeleo” Mhe. Masanja amesisitiza.

Amevipongeza vikundi vya Mkoa wa Rukwa na Katavi vya makabila ya Waha, Wanyasa, Jamii za Lindi na Wanamakete ambavyo kupitia tamasha hilo vimefanikiwa kuanzisha programu za kujikwamua kiuchumi hasa kilimo, ufugaji na ujasiriamali wa biashara ndogondogo.

Amefafanua kuwa kupitia tamasha hilo wananchi wanapata elimu na ufahamu juu ya desturi zilizopo na zinazofaa kudumishwa.

Pia, ameongeza kuwa kupitia tamasha hilo, Shirika la Makumbusho ya Taifa linapata fursa ya kukusanya na kuhifadhi mikusanyo ya urithi wa utamaduni unaoshikika na usioshikika ambayo ni mojawapo ya kazi zake za msingi.

Aidha, amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi zake itaendelea kuhamasisha jamii kutangaza utalii wa Utamaduni ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuurithisha kutoka kizazi kimoja hadi kingine kama dira ya Makumbusho ya Taifa inavyopambanua.

Kwa upande wake Mwenyeji wa Sherehe za Siku ya Utamaduni wa Mtanzania, Chifu Roketi Mwashinga amewataka Watanzania kuenzi mila na desturi ili kutunza maadili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

“Vijana wa sasa hivi tusizitupe mila tutadumbukia kwenye shimo, hata kama umesoma sana ni lazima kutunza mila na desturi kwa kila kabila” amesema Chifu Mwashinga.

Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania lilianzishwa mwaka 1994 kwa lengo la kutangaza tamaduni za jamii mbalimbali za Kitanzania na mpaka sasa takribani jamii 33 kati ya makabila 120 nchini Tanzania zimeshakutana kwa ajili ya kusherehekea tamaduni zao.
Share:

WAZIRI MHAGAMA ATIMIZA AHADI YA KUWASHA UMEME NAKAWALE... WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI

Share:

UMUHIMU WA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA HABARI NA KUIMARIKA KWA UHURU WA KUJIELEZA TANZANIA


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki ya uhuru wa kujieleza kwa raia yeyote wa Tanzania. Katiba hii inampa kila raia haki ya kutoa na kupokea taarifa zinazohusu ustawi wake. 

Hata hivyo, haki hii ya kikatiba inakwamishwa na uwepo wa sheria zinazokwamisha uhuru wa watu kujieleza, kupata na kutoa taarifa kupitia vyombo na majukwaa mbalimbali ya mawasiliano.

Kwa muda mrefu wanahabari na wadau wa habari wameendesha harakati mbalimbali za kuitaka Serikali kuzifanyia marekebisho sheria hizi.
Mojawapo ya sheria zilizolalamikiwa ni Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya 2016, Sheria ya Uhalifu wa Kimtandao ya mwaka 2015, Sheria ya Kupata Taarifa ya mwaka 2016 na Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta ya mwaka 2010. 

Pamoja na uzuri wake katika kusimamia haki ya kupata taarifa na kujieleza bado Sheria hizi zina vipengele vinavyokandamiza uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata taarifa.

Matumizi ya sheria hizi yamepelekea maamuzi ya kufungiwa kwa magazeti na waandishi wa habari, utozaji wa faini kwa vyombo vya habari, na utoaji wa maonyo kwa vyombo na waandishi wa habari nchini. 

Adhabu hizi sio tu zinadumaza uhuru wa kujieleza na kupata taarifa bali pia zinaathiri weledi katika taaluma ya uandishi wa habari nchini. 

Mfano ni kuzorota kwa uandishi wa habari za kiuchunguzi na kuhoji masuala ya msingi, waandishi wa habari kujidhibiti kuandika habari zinazokosoa watawala na kuongezeka kwa uandishi wa habari wa ukasuku.

Baada ya harakati za muda mrefu za wanahabari na wadau wa habari kudai mabadiliko ya sheria za habari na/au vipengele vyake, hatimaye serikali imesikia na kuanzisha mchakato wa marekebisho ya sheria na sera zinayoongoza tasnia ya habari hapa nchini. 

Mchakato huu unaowashirikisha waandishi na wadau wa habari unalenga kufanya mapitio na hatimaye kuboresha vipengele vinavyokandamiza uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kupata taarifa. 

Hivyo, ni matarajio ya kila mdau wa habari hapa nchini kwamba mchakato huu utapelekea kupatikana kwa sheria nzuri.

Hata hivyo, ni wajibu wa kila mwanahabari na mdau wa habari kushiriki kikamilifu katika mchakato huu ili dhamira ya kupata sheria na sera zitakazolinda na kutetea haki na uhuru wa habari iweze kutimia.
Share:

HIZI HAPA DAWA UNAZOPASWA KUZIEUPUKA, ZINAPUNGUZA NGUVU ZA KIUME

Tafiti mbalimbali zimegundua dawa ambazo zina athari kubwa juu ya nguvu za kiume na hutumiwa mara kwa mara.

Hapa chini ni dawa zinazopaswa kuepukwa na wanaume, ili wasipoteze nguvu zao za kiume.


Maisha ya kitandani ni moja ya mahitaji makubwa ya mwanadamu, lakini wakati mwingine huja na changamoto.


Sababu mbalimbali zinaweza kusababisha vikwazo hivi, lakini baadhi ya sababu zinahusishwa na aina sita ya dawa kama ilivyotangazwa na Shirika la Habari la ANI, ambalo lilitayarisha taarifa maalum juu ya mada hii.

Dawa ya kutuliza maumivu


Watu wengi hawasiti kutumia dawa za kutuliza maumivu hata kwa maumivu wanayohisi ni madogo.


Lakini, je, unajua kwamba dawa zilezile za kutuliza maumivu zinaathiri uanaume wako na kuufanya usiwe na matokeo mazuri kitandani?


Dawa za kutuliza maumivu huzuia kuundwa kwa seli za uzazi na huvuruga homoni nyingi ambazo ni muhimu katika kufanya tendo la ndoa kati ya wanaume na wanawake.

Dawa ya kuzuia wasiwasi (anti-anxiety)


Watu wengi wanaolalamika kuhusu matatizo ya akili na kuwa na wasiwasi hutumia dawa ili kukabiliana na hofu.


Walakini, dawa kama hizo hupunguza hamu ya tendo la ndoa.


Dawa hizi zinaweza kusababisha mtu kupoteza hamu ya kufanya mapenzi.


Wakati mwingine hata husababisha wanaume kupoteza fahamu zao kabisa.


Dawa ya kutibu kuganda kwa damu


Dawa zinazotumika kutibu kolesto, ambayo ni mgando wa damu, pia zina mchango mkubwa katika kupunguza nguvu za kiume.


Wataalamu wa matibabu wanasema kuwa dawa hizi huingilia utendaji wa seli za uzazi.


Utafiti unaonyesha kuwa dawa zinazotumika kutibu kuganda damu wakati mwingine husababisha matatizo kwa wanaume wanapolala kitandani na wake zao.


Dawa za msongo wa mawazo (Sonona)


Dawa hizi, zinazojulikana kama "benzodiazepines," mara nyingi hutumiwa kutibu magonjwa ya wasiwasi, kama vile wakati mtu anaogopa vitu ambavyo havipo na yuko peke yake.


Magonjwa mengine ambayo hutumia dawa hizi ni pamoja na kukosa usingizi na maumivu ya misuli.


Lakini, upande wa madhara ni kwamba huathiri utendaji wa seli za uzazi wa kiume na hisia.

Dawa ya Kuzuia Shinikizo la damu

Wagonjwa wanaotumia dawa za shinikizo la damu wanaweza pia kukumbana na changamoto nyingine ambayo ni kupungua kwa nguvu zao.


Dawa hizi zinaingiliana moja kwa moja na mishipa ya damu na pia hufanya kazi na mfumo wa neva.


Wataalamu wengine wameongeza kuwa yapo hata matatizo ambayo wanawake wenyewe wanakumbana nayo na dawa hizo ambazo zinahusiana na viungo vya uzazi.


Dawa za Kifua Kikuu


Dawa za dukani kama vile dawa za kupuliza katika pua zilizoziba na dawa za kwaida za kupunguza kuziba kwa pua zina athari zake.


zinaweza kusababisha matatizo katika tendo la ndoa kwa wanaume na wanawake.

Ongea na daktari


Zungumza na daktari wako ikiwa unafikiri kuwa dawa ina athari mbaya kwenye utendaji wako wa tendo la ndoa. Usiache kutumia dawa yoyote bila kwanza kuzungumza na mtoa huduma wako.

Chanzo - BBC Swahili


Share:

SIMBA WASAJILI BEKI MPYA



Beki mpya wa Simba Mohamed Ouattara

KLABU ya Simba imekamilisha usajili wa mlinzi wa kati kutoka klabu ya Al Hilal ya nchini Sudan Mohamed Ouattara.

Ouattara amesaini kandarasi ya miaka miwili kuwatumikia wekundu wa msimbazi na anaingia moja kwa moja kuziba pengo la Pascal Wawa aliyemaliza mkataba wake na tayari ameshatimka klabuni hapo.


Ouattara ametambulishwa rasmi kupitia ukurasa wa klabu hiyo wa mtandao wa kijamii wa Instagram.


Beki huyo raia wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 29 amewahi pia kukipiga katika Ligi Kuu nchini Morocco akiwa na moja ya miamba ya soka Barani Afrika Klabu ya Wydad Casablanca.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger