Saturday, 25 June 2022

WAZIRI NDAKI AGAWA INJINI ZA BOTI KWA AJILI YA WAVUVI


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki,akizungumza kabla ya kukabidhi Injini tatu za Boti zenye uwezo wa nguvu ya farasi 15 kwa wabunge wa majimbo ya Pangani, Mtwara Mjini na Iringa Vijijini ili ziweze kwenda kuwasaidia wavuvi katika shughuli zao za uvuvi ikiwa ni pamoja na ulinzi wa rasilimali za uvuvi, ambapo pia alisisitiza watumiaji wa injini hizo wazitumie kwa matumizi yaliyokusudiwa na si vinginevyo. Hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.


Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi), Dkt. Nazael Madala akitoa maelezo kuhusu malengo ya sekta katika kuwawezesha wavuvi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mifugo na Uvuvi kuzungumza na kukabidhi injini tatu za boti zenye uwezo wa nguvu ya farasi 15. Hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.


Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso,akiipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) kwa kuipatia Jimbo lake la Pangani Injini moja ya Boti yenye uwezo wa nguvu ya farasi 15 kwa kuwa itakwenda kuwasaidia wavuvi katika shughuli zao za uvuvi lakini pia katika kulinda rasilimali za uvuvi. Hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani kutoka Sekta ya Uvuvi, Prof. Mohammed Sheikh akielezea uwezo wa Injini tatu za Boti ambazo zina uwezo wa nguvu ya farasi 15 wakati wa hafla ya kukabidhi injini hizo. Lakini pia alisema kuwa mpaka sasa Wizara imeshanunua jumla ya injini za boti 26,hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.


Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Hassan Mtenga (Mb) akiishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) kwa kulipatia Jimbo lake la Mtwara Mjini Injini moja ya Boti yenye uwezo wa nguvu ya farasi 15 wakati wa hafla ya kukabidhi injini hizo, ambapo amesema hayo yote yamewezekana kutokana na kuwepo kwa uongozi sikivu na wenye mshikamano. Hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.


Mbunge wa Kalenga, Mhe. Jackson Kiswaga (Mb) akiipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) kwa kuipatia Jimbo lake la Pangani Injini moja ya Boti yenye uwezo wa nguvu ya farasi 15 wakati wa hafla ya kukabidhi kwa kuwa itakwenda kuwasaidia wavuvi katika shughuli zao za uvuvi lakini pia katika kulinda rasilimali za uvuvi. Hafla iliyofanyika Jijini Dodoma.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (kulia) akimkabidhi injini ya boti Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (kushoto) aliyeipokea kwa niaba ya wananchi wa Pangani wakati wa hafla ya kukabidhi injini hizo iliyofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara zilizopo kwenye jengo la Benki ya NBC Jijini Dodoma.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (kulia) akimkabidhi injini ya boti Mbunge wa Kalenga, Mhe. Jackson Kiswaga (kushoto) aliyeipokea kwa niaba ya wananchi wa Pangani wakati wa hafla ya kukabidhi injini hizo iliyofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara zilizopo kwenye jengo la Benki ya NBC Jijini Dodoma.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (kulia) akimkabidhi injini ya boti Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Hassan Mtenga (kushoto) aliyeipokea kwa niaba ya wananchi wa Pangani wakati wa hafla ya kukabidhi injini hizo iliyofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara zilizopo kwenye jengo la Benki ya NBC Jijini Dodoma.


Picha ya pamoja ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (wa nne kutoka kushoto), Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (wa tatu kutoka kulia) Waheshimiwa Wabunge wa Majimbo ya Mtwara Mjini na Kalenga na Watendaji wa Sekta ya Uvuvi mara baada ya kukabishi injini tatu za boti zenye uwezo wa nguvu ya farasi 15. Hafla hii imefanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara zilizopo kwenye jengo la Benki ya NBC Jijini Dodoma.

..........................................

Na Alex Sonna-DODOMA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amekabidhi injini za boti kwa ajili ya wavuvi katika Halmashauri za Wilaya za Pangani, Mtwara Mjini na Iringa.

Akizungumza kabla ya kukabidhi injini hizo leo Waziri Ndaki alisema kuwa Wizara imeendelea na utaratibu wake wa kuwawezesha wavuvi kwa kuwapatia vifaa vinakavyowasaidia kuongeza uwezo wa kuvua mazao ya uvuvi kwa wingi ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya uvuvi hapa nchini.

“Injini za Boti tunazozikabidhi leo zina uwezo wa nguvu ya farasi 15 na tunazitoa kwenye Halmashauri za Wilaya za Pangani, Mtwara Mjini na Iringa ambapo kila Halmashauri itapata injini moja kwa ajili ya kuwawezesha wavuvi kuongeza uwezo wao wa kuvua lakini pia kulinda rasilimali za uvuvi,” alisema

Waziri Ndaki amewasihi wavuvi kuhakikisha wanavitunza vifaa wanavyopatiwa na Wizara pamoja na Wadau wengine wa uvuvi na kuhakikisha wanavitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na ulinzi wa rasilimali za uvuvi.

Aidha, Waziri Ndaki amesema kuwa Serikali kupitia Wizara imejipanga kununua injini nyingine 250 za boti katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 na kama kutakuwa na uwezakano zinaweza kuongezeka injini 70 zaidi ambapo kutakuwa na jumla ya injini 320.

Lengo ni kuhakikisha uzalishaji wa mazao ya uvuvi unaongezeka na mchango wake katika kukuza kipato cha mvuvi na taifa kwa ujumla kinaongezeka. Kwa kufanya hivyo lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan litakuwa limetimia kwa kuhakikisha kipato cha wavuvi kinaongezeka na mchango wa uvuvi kwenye pato la taifa unaongezeka.

Vilevile Waziri Ndaki amesema kuwa injini hizo zitakazo nunuliwa zitatolewa kwenye vyama vya ushiriki vya wavuvi na hata kwa mvuvi mmoja mmoja mwenye uwezo kwa kuwa zitakuwa zikikopeshwa kwa riba ndogo sana ambayo haitawaumiza wavuvi.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Nazael Madala amesema kuwa Wizara imekuwa na utaratibu wa kuwawezesha wavuvi kwa kuwapatia vifaa mbalimbali vinavyowasaidia kuweza kuongeza uwezo wao wa kuvua mazao hayo kwa wingi zaidi.

Naye Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Pangani ameishukuru Wizara kwa kuwapatia injini hiyo na kwamba itakwenda kuwa msaada mkubwa kwa wavuvi katika shughuli zao za uvuvi ikiwa ni pamoja na ulinzi wa rasilimaliza uvuvi. Lakini pia ameishukuru wizara kwa kuamua kujenga soko la samaki Pangani na kwamba wanapangani wataendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara.

Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Hassan Mtenga licha ya kuishukuru Wizara kwa kuwakabidhi injini ya boti, ameiomba Wizara kuendelea kuwawezesha wavuvi kwenye vifaa vingine vya uvuvi ikiwemo majokofu ya kuhifadhia mazao ya uvuvi.

Share:

MacWish COLLEGE OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES YATANGAZA NAFASI ZA MASOMO... HOSTEL FREE!!

Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi 'MacWish COLLEGE OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES' kilichopo Nyasishi Jijini Mwanza kinatangaza nafasi za masomo.


Kozi zinazotolewa

1. Diploma in Clinical Medicine

ADA= Tsh. 1,600,000/=

2. Diploma in Pharmaceutical Sciences
ADA Tsh. 1,400,000/=


HOSTEL FREE


Wasiliana nasi +255 767 302 894
Email : info@macwish.ac.tz
Website : www.macwish.ac.tz


Share:

Friday, 24 June 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNI 25,2022


Magazetini leo Jumamosi June 25 2022












Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 24,2022

Magazetini leo Ijumaa June 24 2022
















Share:

SOLA YAANZA KUKARABATI



Fundi Kiongozi anayekarabati kiwanda cha kuchambua pamba Sola kilichopo Wilayani Maswa Athuman Shabani (mwenye kofia) akiwaonyesha Viongozi wa chama kikuu cha ushirika Mkoa wa Simiyu (SIMCU) wakiongozwa na Mwenyekiti wao ( Mwenye tisherti ya bluu) baadhi ya shughuli zinazofanyika kwenye ukarabati wa kiwanda hicho baada ya kutembelea.

Na Derick Milton, Simiyu.

CHAMA kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu (SIMCU), kimeanza kukarabati kiwanda cha kuchambua Pamba Sola kilichopo katika Wilaya ya Maswa, ambacho kimekaa zaidi ya miaka saba bila ya kufanya kazi.

Kiwanda hicho ambacho kilikuwa kinamilikiwa na Chama kikuu cha Ushirika Shinyanga (SHIRECU) kabla ya kufanyika kwa mgawanyiko wa mali baada ya kuundwa kwa SIMCU, hakikufanya kazi kwa muda huo baada ya umiliki wa awali kushindwa kukiendesha.

Kiwanda cha Sola ni kati ya viwanda vitatu ambavyo SIMCU imevipata kama mgao baada ya kuundwa kwake kutoka vyama vikuu vya SHIRECU na NYANZA, ambapo viwanda hivyo ni pamoja na NASSA GINNERY pamoja na RUGURU GINNERY.

Wakiwa na waandishi wa habari viongozi wa SIMCU wametembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kujionea shughuli za ukarabati zinavyoendelea, ambapo wameridhishwa na kazi ya mhandisi aliyepewa kazi ya kukarabati.

Akitoa maelezo mbale ya viongozi hao, fundi kiongozi Athuman Shabani amesema kuwa tangu wameaza zoezi la ukarabati wamefikia asilimia 20 ambapo ndani ya siku 20 zijazo zoezi zima litakuwa limekamilika.

Amesema kuwa zoezi ambalo wameanza nalo ni kufungua mashine za kuchatakata pamba na sehemu za kupitisha umeme, ambapo asilimia kubwa ya vipuli vya mashine hizo bado imara.

“ Kuna vifaa vichache sana ambavyo tumekuta vimeharibika, lakini kwa kiwango kikubwa mashine bado nzima na zinafanya kazi, kwa kasi ambayo tumeanza nayo ndani ya siku 20 kiwanda kitaanza kufanya kazi,” amesema Shabani.

Mwenyekiti Kamati ya Uchumi SIMCU Simioni Magoma, amesema kuwa katika mikakati ya Chama chao, wamepanga kuhakikisha kiwanda hicho kinaanza kufanya kazi haraka iwezekanavyo hasa kuanza kuchakata pamba katika msimu wa mwaka huu.

Amesema kuwa zoezi la ukarabati linahusisha mashine za kuchambua pamba ikiwemo ukarabati wa maghala matatu ya kuanzia kwa ajili ya kutunza pamba, huku mkakati mkubwa ikiwa ni kukarabati kiwanda kizima.

“ Tunashukuru sana serikali ambayo imeendelea kutuunga mkono katika zoezi hili la kuanza kufufua viwanda vyetu, tumeanza na hii sola lakini tunao mpango wa kuanza kufufua viwanda vingine ambavyo SIMCU tunamiliki,” amesema Magoma.

Kwa upande wake Meneja wa SIMCU Shigela Magembe amesema kuwa Mhandisi Malando Zamu ndiye amepewa kazi ya ukarabati wa kiwanda hicho, kazi ambayo itatumia muda wa mwezi mmoja hadi kukamilika kwake.

Magembe ameeeleza kuwa SIMCU ilipata mkopo kutoka benki ya Kilimo (TADB) kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 ambazo zinatumika kwa ajili ya ukarabati huo pamoja na kuanza ununuzi wa pamba katika msimu huu.

“ Katika mkopo ambao tumepewa na TADB fedha zake ndizo zimeanza kukarabati kiwanda hiki, lakini pia kati ya fedha hizo zitatumika kuanza kununua  pamba msimu huu mara baaada ya ukarabati kukamilika,” amesema Magembe.

Mwenyekiti wa SIMCU Lazaro Walwa amesema kuwa hadi kufikia Julai 14, 2022 kiwanda hicho kitakuwa kimeanza kufanya kazi ya kuchambua pamba na kuuza marobota kwani ukarabati unaoendelea utakuwa umemalizika.

Amesema kuwa mara baada ya kiwanda hicho kukamilika ukarabati wake, zaidi ya watu 300 wataajiliwa wakiwemo vibarua na kitawezesha kuinua uchumi wa wakulima wa pamba ambao watalipwa malipo ya pili mara baada ya chama hicho kuuza marobota ya pamba.

“ Iwe mvua, liwe jua, mwezi Julai, 2022 lazima kiwanda kianze kufanya kazi, fedha zipo na kazi inaendelea kwa kasi, wananchi na wakulima wajiandae viwanda vyetu vinarudi kama zamani,” amesema Walwa.

Mafundi wakiendelea na Shughuli za ukarabati wa mashine katika kiwanda cha kuchambua pamba Sola kilichopo katika Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu, kiwanda hicho ambacho kilikuwa kinamilikiwa na SHIRECU sasa kinamilikiwa na Chama kikuu cha Ushirika mkoa wa Simiyu (SIMCU).

Share:

Thursday, 23 June 2022

KIGAHE : SERIKALI INATHAMINI MCHANGO WA SEKTA BINAFSI KATIKA KUWEKEZA

Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Mb.) akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya miaka 30 ya ushirikiano kati ya Kampuni ya 'Superdoll' na kampuni kubwa inayoongoza duniani kwa utengenezaji wa matairi 'Michellin' iliyofanyika leo Juni 23,2022 katika Ofisi za Kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Mb.) akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya miaka 30 ya ushirikiano kati ya Kampuni ya 'Superdoll' na kampuni kubwa inayoongoza duniani kwa utengenezaji wa matairi 'Michellin' iliyofanyika leo Juni 23,2022 katika Ofisi za Kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kampuni ya 'Superdoll' Bw.Seif Ali Seif akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya miaka 30 ya ushirikiano kati ya Kampuni ya 'Superdoll' na kampuni kubwa inayoongoza duniani kwa utengenezaji wa matairi 'Michellin' iliyofanyika leo Juni 23,2022 katika Ofisi za Kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam.Bw.Gaganjot Singh ambaye ni rais wa Michellin akizunggumza katika hafla ya maadhimisho ya miaka 30 ya ushirikiano kati ya Kampuni ya 'Superdoll' na kampuni kubwa inayoongoza duniani kwa utengenezaji wa matairi 'Michellin' iliyofanyika leo Juni 23,2022 katika Ofisi za Kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Mb.) akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya 'Superdoll' Bw.Seif Ali Seif katika hafla ya maadhimisho ya miaka 30 ya ushirikiano kati ya Kampuni ya 'Superdoll' na kampuni kubwa inayoongoza duniani kwa utengenezaji wa matairi 'Michellin' iliyofanyika leo Juni 23,2022 katika Ofisi za Kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam.

*****************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Mb.) amesema Serikali inathamini mchango wa sekta binafsi katika kuwekeza na itaendelea kushirikiana nayo ili wananchi waweze kupata huduma iliyobora ili kukuza uchumi wa nchi.

Kigahe ameyasema hayo Juni 23, 2022 wakati hafla ya maadhimisho ya miaka 30 ya ushirikiano kati ya Kampuni ya 'Superdoll' na kampuni kubwa inayoongoza duniani kwa utengenezaji wa matairi 'Michellin' yenye Makao Makuu yake nchini Ufaransa yaliyofanyika katika ofisi za Kampuni hiyo,Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa ushirikiano kati ya Superdoll na Michellin ambapo kwa hivi sasa katika miaka 30 ya uwekezaji wameweza kuja na teknolojia mpya ya matumizi ya mataili ya tubulesi ambayo yameleta mageuzi makubwa katika sekta ya usafirishaji hapa nchini.

"Ni asilimia 98 ya Tanzania inatumia tubules tofuti na nchi nzingine, nawapongeza mlipofikia hii ni hatua kubwa, "Serikali ipo na itaendelea kushirikiana na sekta binafsi ili wananchi waweze kupata huduma iliyobora na yenye uhitaji mkubwa". Amesema Mhe.Kigae.

Aidha amewataka wananchi kutumia mataili yenye ubora ili kulinda usalama wa watu na siyo kuangalia mataili yenye gharama nafuu huku yakiwa hayana ubora unaotakiwa hivyo kusababisha ajali barabarani.

Naye, Mwenyekiti wa Kampuni ya 'Superdoll' Bw.Seif Ali Seif amebainisha kwamba ushirikiano huu wa miaka 30 kati ya 'Superdoll' na 'Michellin' umeiwezesha Tanzania kutumia matairi bora ya kisasa ambayo ni salama zaidi kwa vyombo vya usafiri.

Hafla ya Maadhimisho hayo imehudhuriwa na rais wa Michellin wakiwemo viongozi wengine wazito wa Kampuni hiyo, balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui , wateja wa kampuni ya 'Superdoll' na watu wengine mashuhuri hapa nchini.
Share:

SHIGONGO ATANGAZA KUYAPELEKA MAHAKAMANI MAKAMPUNI YA SIMU TANZANIA KUHUSU BANDO NA DATA


Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo amesema anajiandaa kuyapeleka mahakamani makampuni ya simu nchini juu ya matumizi ya mabando ya data.


Kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter, Shigongo ameandika: “Wakili wangu anajiandaa kuzipeleka kampuni za simu mahakamani, juu ya matumizi ya mabando na data; ukombozi umewadia.”


Kwa muda mrefu, watumiaji wa mitandao ya simu hususan wanaotumia simu janja, wamekuwa wakilalamikia kupandishwa bei kiholela kwa mabando ya huduma za intaneti kunakofanywa na makampuni ya simu bila kuwashirikisha watumiaji.



Malalamiko mengine ni kuhusu kuisha haraka kwa mabando hayo ambapo watumiaji wamekuwa wakilalamika kuwa wakati mwingine, mteja anaweza kununua bando la kiasi fulani cha fedha lakini likaisha ndani ya muda mfupi tofauti na matumizi ya kawaida.



Suala hilo limewahi kumuibua Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ambaye kauli yake ya mwisho wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari, alieleza kwamba kama kuna mtu mwenye ushahidi wa kuibiwa bando na mtandao wa simu, basi atoe taarifa kwa Mamlaka ya Mawasiliano TCRA kwa ajili ya hatua za kisheria.



Pia, kupitia akaunti yake ya Twitter, Nape amewahi kuandika: “Kumekuwa na manung’uniko ya watumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu nchini. Baada ya kutafakari kwa kina, nimewataka Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kuandaa taarifa ya kina ya hali halisi na hatua wanazochukua katika usimamizi wa mawasiliano ya simu nchini, na kuwaeleza watumiaji.



Kabla ya Nape kuteuliwa kuwa waziri wa wizara hiyo, mtangulizi wake ambaye alikuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amewahi kuliagiza Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA – CCC) kushughulikia malalamiko ya wananchi na changamoto wanazozipata wakati wanatumia huduma na bidhaa za mawasiliano nchini, ikiwemo bei za mabando.



Hatua ya Shigongo kulipeleka suala hilo mahakamani kama alivyoeleza, huenda likazifanya kampuni za simu kuwajibishwa na kudhibitiwa katika suala la upandishaji holela wa bei za mabando na kupunjwa kwa wateja, jambo litakaloleta unafuu mkubwa kwa mamilioni ya watumiaji wa simu za mkononi nchini.
Share:

MIMBA ZANGU NNE ZILITOKA KWA MIKOSI, ILA SASA NINA WATOTO WAWILI

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger