Friday, 10 June 2022

MAROBOTI KUCHEZESHA KOMBE LA DUNIA 2022


Shirikisho la Soka Kimataifa (FIFA) lipo kwenye mkakati wa kutambulisha maroboti watakaokuwa waamuzi wa pembeni katika michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika Qatar, Novemba mwaka huu 2022.

Kwa mujibu wa taarifa, FIFA ipo tayari kuanzisha mfumo huo wa maroboti kuchezesha mechi za michuano hiyo badala ya marefa wa pembeni endapo viongozi wengine wataridhishwa kabla ya kuuzindua.

Endapo FIFA itapitisha mfumo huo, itakuwa mara ya kwanza michuano ya Kombe la Dunia kuchezwa na maroboti katika historia ya soka.
Share:

RAIS SAMIA: RUZUKU YA MAFUTA SHILINGI BILIONI 100 SASA KUTOLEWA KILA MWEZI MPAKA KIELEWEKE

 

Rais Samia Suluhu Hassan
***

Mwandishi Wetu, Bukoba

Akiwa ziarani Bukoba, mkoa Kagera, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa serikali yake sasa itatoa ruzuku ya mafuta Shilingi bilioni 100 kila mwezi hadi kieleweke.

Rais Samia ameagiza ruzuku ya Shilingi bilioni 100 itolewe kwenye bajeti ya matumizi ya kawaida ya serikali (recurrent expenditure) kila mwezi kuanzia Juni mwaka huu hadi hapo bei za mafuta katika soko la dunia zitulie.

Maamuzi haya magumu na ya kishujaa ya serikali kujibana kwenye matumizi yake ili ipatikane ruzuku hiyo tayari yamesababisha bei za mafuta nchini ziteremke kuanzia Juni 1.

Ikumbukwe kuwa matumizi ya maendeleo ya bajeti ya serikali (recurrent expenditure) hayataguswa kwenye ubananaji huo wa matumizi, hivyo kasi ya miradi ya maendeleo itaendelea vile vile.

"Kama mlivyosikia, nilisema natoa ruzuku ya Shilingi bilioni 100 kufidia kwenye mafuta ili bei zishuke, na mwezi huu (Juni) bei zimeanza kushuka polepole," Rais Samia aliwaambia wananchi kwenye ziara yake ya Bukoba jana.

"Tutaendelea kutoa hiyo ruzuku mpaka duniani kukae sawa. Tutaendelea kukata Shilingi bilioni 100 kila mwezi kwenye matumizi ya serikali tuweke ruzuku mpaka bei zikae sawa."

Rais Samia amesema kuwa lengo la uamuzi huo ni kupunguza makali kwa wananchi yanayotokana na upandaji wa bei za mafuta kwenye soko la dunia. 

Aliongeza kuwa kutokana na ruzuku hiyo ya Shilingi bilioni 100 kila mwezi, bei za mafuta nchini zitaendelea kushuka hadi zifikie hali ya zamani ya utulivu.

Uamuzi wa Rais Samia kuweka ruzuku kwenye mafuta umepokelewa kwa shangwe na watu kila kona ya nchi.

Jijini Dar es Salaam, madereva teksi, waendesha pikipiki na bodaboda wamempongeza Rais Samia kwa kuwajali wanyonge kwa kuweka ruzuku kwenye mafuta.

Umoja wa Wamiliki na Waendesha Pikipiki na Bajaji Wilaya 
ya Tanga Mjini (UWAPIBATA) unampongeza Rais Samia kwa hatua madhubuti anazochukua 
kuhakikisha kuwa ongezeko la bei ya mafuta kwenye soko 
la dunia hazileti athari kubwa katika maisha ya wananchi na 
uchumi wa Tanzania kwa ujumla.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ruzuku ya Shilingi bilioni 100 
ya Rais Samia imesaidia kupunguza beiya mafuta, ambapo kwa bandari ya Tanga, petroli imeshuka kwa shilingi 152 kwa lita na dizeli imeshuka kwa shilingi 476 kwa lita.

Nao waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda mkoani Kagera nao wamempongeza Rais Samia kwa kupunguza gharama za mafuta.

Pongezi za bodaboda hao zimewasilishwa na Umoja wa Bodaboda wilayani Bukoba (UBOBU) ikiwa ni siku moja kabla ya Rais Samia kufika mkoani Kagera kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo.

Mwenyekiti wa UBOBU, Mahamud Sued amesema ushushaji wa bei ya mafuta utalisaidia kundi kubwa la bodaboda kuweza kumudu gharama za maisha na kuepuka kujiingiza kwenye vitendo viovu.

"Ili kutambua ukubwa wa kundi hili kwa upande wa Manispaa ya Bukoba pekee kuna bodaboda 8,600 ndio maana tunaomba aendelee kutupunguzia gharama.

Ruzuku imetolewa kwa wakati muafaka na kutupa nahueni sisi ambao riziki zetu zinategemea sana bei ya mafuta."

Share:

MSAMAHA WA MATIBABU HUTOLEWA KWA WATU WASIO NA UWEZO – DKT. MOLLEL



Na WAF – Bungeni, Dodoma.

Licha ya matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza kuwa na gharama kubwa na yana hitaji tiba wakati wote, Serikali imekuwa ikitoa msamaha wa matibabu kwa wagonjwa wanaougua magonjwa yasiyoambukiza ambao wamethibitika kuwa hawana uwezo wa kugharamia matibabu yao kwa mujibu wa Sera ya Afya.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Chaani, Mheshimiwa Juma Usonge Hamad aliyehoji Serikali ina mpango gani wa kutoa matibabu bure kwa maradhi yasiyoambukiza kama Kisukari, Presha na Shinikizo la Damu.

Hata hivyo Dkt Mollel amesema kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote ambao utawezesha wananchi wote kupata huduma za afya katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini.

Akijibu Swali la nyongeza lilioulizwa na Mheshimiwa Usonge aliyehoji usumbufu wanaopata wazee pindi wanapoenda hospitalini kupata huduma za matibabu, Dkt. Mollel ameendelea kuwasisitiza wataalam kufuata maagizo yanayotolewa na viongozi ikiwemo kuhakikisha Wazee wanapata matibabu bure katika vituo vya kutolea huduma za afya.

“Nitumie fursa hii kutoa agizo kwa Waganga wote wa Mikoa na Wilaya, suala la matibabu kwa wazee ni bure na wanatakiwa kuwa na dirisha lao la kupata huduma, hatutegemei kusikia tena malalamiko ya wazee wanapitia mlolongo mrefu wa kupata huduma za matibabu” amesisitiza Dkt. Mollel.
Share:

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 10,2022

Magazetini leo Ijumaa June 10 2022
Share:

MTU HUYU ATAKUSAIDIA KUPATA KAZI UIPENDAYO

Share:

Thursday, 9 June 2022

RAIS SAMIA ATEMBELEA NA KUZINDUA KIWANDA CHA SUKARI MKOANI KAGERA

Share:

KIJANA MBARONI TUHUMA ZA KUMBAKA NA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA MITANOKISA NG'OMBE

Mtuhumiwa aliahidiwa akikamilisha unyama huo atapewa Ng’ombe watatu kama malipo
***
KIJANA mmoja anayefahamika kwa jina la Juma Jackson (30) mkazi wa Kijiji cha Kagunga wilayani Tanganyika Mkoa wa Katavi anashikiliwa na Jeshi la Polisi akituhumiwa kumbaka na kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame amesema mtuhumiwa alimbaka mtoto huyo akiwa anatoka nyumbani kwao kuelekea mji wa jirani.

“Alimvutia vichakani kisha kumvua nguo zake na kuanza kumbaka na kumlawiti huku akimkaba shingo na kumuamru asipige kelele,” amesema Makame.

Kwa mujibu wa ACP Makame, uchunguzi wa awali umebaini kuwa tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina, aliahidiwa kulipwa ng’ombe watatu baada ya kutekeleza kitendo hicho na mtu (jina limehifadhiwa).


“Walikubaliana baada ya kufanya unyama huo aende akamuogeshe shambani kwake ili iwe kama zindiko kwa ajili ya shamba,” amefafanua Makame.

“Tulimkamata baada ya kupata taarifa kutoka kwa wazazi wa mtoto, alifanya ukatili huo Mei 13, 2022 saa 12:00 jioni, anaendelea kuhojiwa tukikamilisha upelelezi tutamfikisha mahakamani,” amesema Makame
Share:

MKE AMVIZIA MMEWE AMESINZIA KISHA KUMUUA KWA KUMKABA SHINGONI




Mwanamke mmoja aitwaye Maria Matheo anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Tabora kwa tuhuma za kumvizia mumewe GABRIEL NGUWA (80) akiwa amelala na kumkaba shingoni hadi kifo.

Chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa muda mrefu baina ya wanandoa hao hususani nyakati za jioni mwanamke anapokuwa amelewa na kuanza kumtuhumu mumewe kuwa hana msaada katika maisha yao.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea katika kitongoji cha Bugweda kijiji cha Budushi tarafa ya Puge wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Share:

FAMILIA YAGOMA KUONDOA KABURI KATIKATI YA BARABARA BARIADI..MKUU WA MKOA DAVID KAFULILA AINGILIA KATI




Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila (aliyeshika kiuno) akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange (mwenye kofia) akimwelezea namna changamoto ya kaburi kuwa katikati ya barabara kijiji cha Nkindwabiye.

Na Constantine Mathias, Bariadi.

Familia ya Saguda Madako katika kijiji cha Nkindwabiye Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, imegoma kuhamisha kaburi linalodaiwa kuzikwa mama yao mzazi ambalo lipo katikati ya Barabara katika kijiji hicho kwa madai hadi walipwe kiasi cha Shilingi Milioni 30 na serikali.


Kaburi hilo limejengwa katikati ya Barabara kuu ya Nkololo-Byuna- Nkindwabiye–Halawa, ambapo familia hiyo imedai mama yao mzazi alizikwa eneo hilo tangu mwaka 1974, na kujengelewa mwaka 2006.


Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa huo David Kafulila wakati akikagua ujenzi wa Barabara hiyo, Meneja Tarura Wilaya, Mhandisi Mathias Mgolozi amemweleza Mkuu huyo wa Mkoa kuwa licha ya kukaa na familia hiyo mara kwa mara kwa ajili ya kuhamisha kaburi hilo lakini imeshindikana.


Mgolozi amesema mara ya kwanza familia hiyo ilitaka Milioni 30 ili kaburi hilo lihamishe, baadaye wakataka Milioni 20, na mara ya mwisho walipunguza na sasa wanahitaji Milioni 1.5.


“Baada ya madai hayo, tulimweleza kwa mujibu wa sheria kuhamisha kaburi familia inapewa kiasi cha Sh. 500,000 na serikali itasaidia kuhamisha kaburi hilo, lakini mpaka sasa familia imegoma,” amesema Mhandisi Mgolozi.


Baada ya hali hiyo Mkuu wa Mkoa, aliagiza kuhamishwa kwa kaburi hilo bila ya kusikiliza uamuzi wa familia kama inataka au hapana na familia ipewe kiasi hicho cha pesa kama sheria inavyotaka.


“Kama sheria inasema hivyo basi naagiza kaburi hili liondolewa mara moja, endapo ujenzi wa Barabara hii utaaanza kaburi liondolewa familia ikubali isikubali kaburi liondolewe na ujenzi wa barabara ufanyike,” amesema Kafulila.
Share:

HUAWEI YATHIBITISHA UMAHIRI WA VITUO VYAKE VYA DATA



Johannesburg - Huawei yatoa ufafanuzi wa Kituo cha Data cha Kizazi Kinachofuata, na kuzindua mfumo wake mpya wa usambazaji wa nguvu ambao ni PowerPOD 3.0. Utoaji mpya, sio tu unathibitisha dhamira ya Huawei ya kujenga vituo vya data visvyo na kaboni, vituo mahiri vya data, pia inasisitiza ukweli kwamba kizazi kijacho cha vituo vya data kitakuwa endelevu, kilichorahisishwa, chenye uendeshwaji uhuru na cha kutegemewa.

Kwa maendeleo endelevu ya uwanda kama vile 5G, ngamizi na mashine nyingine, na Data Kubwa, vituo vya data vitakua kwa ukubwa na umuhimu wa kipekee. Lakini wakati huo huo, kuna shinikizo linaloongezeka kwa vituo vya data kutumia umeme mdogo na kufanya kazi kwa njia endelevu zaidi, haswa kwani uchumi barani Afrika na maeneo mengine unatazamia kupunguza matumizi ya kaboni. Kimsingi, watalazimika kufanya hivyo bila kuathiri utendaji kazi.

PowerPOD 3.0 huwezesha vituo vya data kufanya mambo haya yote. Inapunguza alama ya vituo vya data kwa 40%, kupunguza matumizi yao ya nishati kwa 70%, kufupisha muda wa utoaji kutoka miezi 2 hadi wiki 2, na kupunguza kiwango cha makosa ya kiwango cha makubaliano ya kiwango cha huduma 38%.

"Huku Huawei, tuko tayari kufanya ili kuchangia maendeleo ya kijani barani Afrika," anasema Jason Xia Hesheng, Rais wa Huawei Kusini mwa Afrika. "Tuna utamaduni wa kujivunia wa kuhakikisha kuwa teknolojia zetu zote ni endelevu huku tukisukuma mipaka ya uvumbuzi. Itawaruhusu wateja kufuata baadhi ya teknolojia zinazoleta mabadiliko kama vile 5G na mashine zingine huku wakilinda sayari."

Afrika itanufaika sana na mfumo huo wa PowerPOD 3.0. Nishati hasa inatoa changamoto kubwa barani Afrika. Vituo vya data hutumia kati ya 2% -3% ya nguvu zote za ulimwengu kila mwaka. Hii inaongeza matatizo ya ziada kwenye gridi za nchi za Afrika. Zaidi ya hayo, wastani wa kila mwaka wa Ufanisi wa Utumiaji wa Nishati wa vituo vya data barani Afrika ni 1.8, kumaanisha kuwa havifanyi kazi vizuri iwezekanavyo. Kitu kama PowerPOD 3.0 kinaweza kusaidia sana kuleta alama hiyo karibu na bora ya 1.0.

Kwa kuongezea, uwezo wa mfumo wa kupunguza gharama za matengenzo ya uendeshaji unaweza pia kuwa muhimu, ikizingatiwa kwamba ujenzi wa awali wa kituo cha data unachukua theluthi moja tu ya gharama zake, na theluthi mbili nyingine kutoka kwenye matengenzo ya uendeshaji.

Huku Afrika ikitarajiwa kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 600 wa mtandao na watumiaji wa mwisho wenye akili milioni 360 ifikapo 2025, itakuwa muhimu sio tu kutumia mifumo kama PowerPOD 3.0 kufanya vituo vyake vya data vilivyopo kuwa na ufanisi zaidi, lakini pia kama njia. ya kukumbatia kizazi kijacho cha vituo vya data, vilivyo na sifa ya Uendelevu, Urahisishaji, Uendeshaji wa uendeshaji rahisi na Kutegemewa.

Huku Afrika inavyotazamia kusawazisha ukuaji wa idadi ya watu, ukuaji wa miji, na hamu ya kusonga mbele kwenye mipango mahiri ya jiji na kujitolea kupunguza hewa chafu, aina hizi za vituo vya data vya kizazi kijacho vitakuwa muhimu. Kama "moyo" wa kituo cha data, mfumo wa usambazaji wa nishati unapaswa kuunganisha na kuvumbua vifaa vyote kwenye mnyororo wa usambazaji wa nishati.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 9,2022


Magazetini leo Alhamis June 9 2022













Share:

Wednesday, 8 June 2022

KAMPUNI YA JAMBO FOOD PRODUCTS YASHIRIKI TAMASHA LA UTAMADUNI SHINYANGA

Gari la Matangazo la Kampuni ya Jambo Food Products likiwa kwenye kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma cha Butulwa -Old Shinyanga katika Tamasha la Kwanza la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kampuni ya Jambo Food Products imeshirika Tamasha la Kwanza la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga lililokwenda sanjari na uzinduzi wa Kijiji cha utamaduni wa kabila la Wasukuma na Filamu ya The Royal Tour kwa Mkoa wa Shinyanga.

Tamasha hilo lilizinduliwa Juni 7,2022 na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na kufungwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema Juni 8,2022 katika kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma cha Butulwa kata ya Old – Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kulia) akimkabidhi Mwakilishi wa Kampuni ya Jambo Food Products, Juma Isa Ramadhan cheti cha Shukrani kutambua ushiriki na mchango wa Kampuni ya Jambo Food Products kwenye Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga lililofanyika Juni 6 - 7,2022 katika kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma cha Butulwa - Old Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Gari la Matangazo la Kampuni ya Jambo Food Products likiwa kwenye kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma cha Butulwa -Old Shinyanga katika Tamasha la Kwanza la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga
Banda lenye bidhaa za Kampuni ya Jambo Food Products likiwa kwenye kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma cha Butulwa -Old Shinyanga katika Tamasha la Kwanza la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga
Banda lenye bidhaa za Kampuni ya Jambo Food Products likiwa kwenye kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma cha Butulwa -Old Shinyanga katika Tamasha la Kwanza la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

HII NDIYO MIJI 10 YENYE GHARAMA KUBWA KUISHI DUNIANI


Mji wa Seoul, Korea Kusini.
**

Bara la Asia ndiyo bara la gharama zaidi kuishi kwa mujibu wa utafiti wa 'ECA International' ambapo miji mitano kutoka Asia ipo katika orodha ya miji 10 yenye gharama kubwa ya kuishi duniani.

Utafiti huo umejikita katika kuangalia wastani wa bei za bidhaa za nyumbani, usafiri wa umma na thamani ya sarafu.

1. Hong Kong
2. New York
3. Geneva
4. London
5. Tokyo
6. Tel Aviv
7. Zurich
8. Shanghai
9. Guangzhou
10. Seoul
Share:

TAASISI ZOTE ZINAZOTOA HUDUMA TIC KUTUMIA MFUMO WA DIRISHA MOJA KWA WAWEKEZAJI


Picha ya pamoja ya washiriki na wakuu wa taasisi zinazounda mfumo wa huduma za mahala pamoja (TIC) walipokutana Morogoro kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa Mradi wa Dirisha/Mfumo wa pamoja wa kuwahudumia wawekezaji.
Kamishina Jenerali wa uhamiaji nchini Dkt. Anna Makakala, akizungumza na waandishi wa habari Morogoro baada ya kikao cha pamoja cha wakuu wa Taasisi 12 zinazihusika na utoaji vibali mbalimbali kwa wawekezaji nchini
Dkt. Yusuph Ngenya Mkurugenzi Mkuu Shirika la Viwango Tanzania (TBS) akizungumza na waandishi wa habari Morogoro baada ya kikao cha pamoja cha wakuu wa Taasisi 12 zinazohusika na utoaji vibali mbalimbali kwa wawekezaji nchini
Mwakilishi wa kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw. M. Bunini ameongoza kikao cha dharura cha wakuu wa taasisi zinazounda mfumo wa mahala pamoja (NIFC) kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa Mradi wa Dirisha/Mfumo wa pamoja wa kuwahudumia wawekezaji kilichofanyika Morogoro tarehe 07 June 2022.


"Serikali katika kuhakikisha inaboresha huduma ya uwekezaji hasa kwa kutumia mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) imeandaa mfumo wa pamoja ambao utawezesha taasisi zinazotoa huduma kwa wawekezaji kusomana (Interface)", amesema Bw. Bunini.


Kikao hiki kimepitia taarifa za mfumo ulipofikia, kuwaonyesha wakuu wa taasisi mfumo unavyofanya kazi, kujadili usalama wa mfumo ikiwemo kupitia hati za makubaliano za kubadilishana taarifa ( Data sharing agreement).

Utekelezaji wa Mradi huu umefikia asilimia tisini.

Meneja mradi wa mfumo wa kidijitali wa kuwahufumia wawekezaji Bw. Robert Mtendamema amesema "majadiliano ya leo yamelenga kukubaliana kuanza matumizi ya mfumo huo hivi karibuni".


Taasisi ambazo zitaanza kutumia mfumo huo kwa awamu ya kwanza ya mradi huo ni; BRELA, TRA, NIDA, UHAMIAJI, ARDHI, IDARA YA KAZI na kamishina wa kazi.


Dirisha/Mfumo huu utakapozinduliwa itasaidia, kutoa vibali kwa wakati, Itasaidia kuondoa urasimu, kutoa huduma za haraka kwa wawekezaji na utatunza taarifa za wawekezaji.


Kituo cha uwekezaji Tanzania kinafanya kazi pamoja na taasisi kumi na mbili za Serikali zinazotoa huduma mahala pamoja (NIFC ) taasisi hizo ni BRELA, NEMC, NIDA, TRA, UHAMIAJI, ARDHI, KAMISHINA WA KAZI, TANESCO, OSHA, TBS na TMDA.
Share:

Video : BURUDANI, NGOMA ZOTE ZA KISUKUMA ZILIZOCHEZWA KWENYE TAMASHA LA UTAMADUNI

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger