Tuesday, 24 May 2022

MWANAMKE AUAWA KWA KUCHOMWA KISU GESTI MJINI KAHAMA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando

Na Marco Mipawa - Kahama

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Zuena au Ashura Salum (25-30) mkazi wa Dar es Salaam, amekutwa chumbani akiwa ameuawa kwa kuchomwa kisu  na mtu anayedhaniwa kuwa ni mwenza wake katika nyumba ya kulala wageni ya Kalunde iliyoko mjini Kahama, usiku wa kuamkia Mei 22, 2022.


Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga George Kyando amethibitisha kutokea kwa  tukio hilo na kwamba, Zuena na mwanaume huyo waliingia chumbani hapo majira ya saa 11:00 alfajiri na kwamba mwanaume alitoka na kutokomea kusikojulikana kabla ya wahudumu wa nyumba hiyo kugundua mauaji hayo.


Kyando amesema, mapema asubuhi siku hiyo wahudumu wa nyumba hiyo waliukuta Mwili wa marehemu chumbani pamoja na simu mbili zenye laini zinaonesha majina hayo.

Amesema jeshi la polisi linaendelea kufuatilia tukio hilo, huku akitoa Rai kwa jamii kujihadhari na watu wasiotambulika vizuri.
Share:

Monday, 23 May 2022

WAZIRI MABULA AFUNGUA MKUTANAO WA MAJADILIANO YA KISEKTA KATI YA WIZARA NA WADAU WA SEKTA YA ARDHI

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akizungumza katika mkutano wa majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara na wadau wa sekta ya ardhi, Nyumba na Makazi uliofanyika leo Mei 23,2022 Jijini Dar es Salaam Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano wa majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara na wadau wa sekta ya ardhi, Nyumba na Makazi uliofanyika leo Mei 23,2022 Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Allan Kijazi akizungumza katika mkutano wa majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara na wadau wa sekta ya ardhi, Nyumba na Makazi uliofanyika leo Mei 23,2022 Jijini Dar es Salaam Kaimu mwenyekiti wa Sekta Binafsi (TPSF) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Bi.Mercy Silla akizungumza katika mkutano wa majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara na wadau wa sekta ya ardhi, Nyumba na Makazi uliofanyika leo Mei 23,2022 Jijini Dar es Salaam Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC),Godwill Wanga akizungumza katika mkutano wa majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara na wadau wa sekta ya ardhi, Nyumba na Makazi uliofanyika leo Mei 23,2022 Jijini Dar es Salaam Wadau mbalimbali wa sekta ya ardhi wakiwa katika mkutano wa majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara na wadau wa sekta ya ardhi, Nyumba na Makazi uliofanyika leo Mei 23,2022 Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WIZARA ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewezesha kutafuta fedha za kugharamia utekelezaji wa miradi ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi ambapo Wizara imetoa kiasi cha Bilioni 50 kwa halmashauri 55 ili kufanikisha mradi huu.

Ameyasema hayo leo Mei 23,2022 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula katika Mkutano wa majadiliano ya Kisekta kati ya Wizara na wadau wa sekta ya ardhi, Nyumba na Makazi.

Amesema utekelezaji huo unafanyika kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na TAMISEMI.

Aidha amesema Wizara imewezesha upatikanaji wa mkopo wa benki ya dunia kiasi cha shilingi Bilioni 340.5 ambao pamoja na kazi zingine uttawezesha kuimarisha miundombinu ya TEHAMA na Usalama wa miliki.

Hata hivyo amesema Wizara imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za utatuzi wa changamoto zinazojitokza ikiwemo, kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za ardhi, kuendelea kuimarisha na kuziwezesha Ofisi za Ardhi zilizopo katika kila mkoa katika kuhakikisha huduma zinapatikana karibu na wananchi.

"Wadau na wamiliki wote wa ardhi mtumie utaratibu wa ukadiliaji na upimaji kodi ya pango la ardhi ki-elekroniki kwa kuwa utaratibu huu ni rafiki, unaokoa muda na ni nafuu". Amesema Waziri Mabula.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Allan Kijazi amesema kupitia mkutano huo watapokea maoni ya sekta binafsi kuhusu maboresha yanayotakiwa kufanyika kwenye sekta ya ardhi na lengo ikiwa ni kuchochea mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi jumuishi na kukuza maendeleo ya jamii na kuhakikisha uendelevu wa mifumo ya kimazingira.

"Sekta binafsi inamchango mkuwa kwenye maboresho ya sekta ya ardhi nchini kwani inatoa mchango mkubwa kwenye ubunifu, upatikanaji wa mitaji na uwekezaji ambao huchangia kwa kiasi kikubwa kwenye shughuli za uzalishaji hasa katika sekta ya viwanda, kilimo, mifugo na shughuli nyingine nyingi za maendeleo". Amesema

Amesema ufanisi wa sekta hizi unategemea kwa kiasi kikubwa kuwa na mifumo ya usimamizi na uendelezaji wa sekta ya ardhi ambayo inaweza kujenga mazingira wezeshi bila kukwamisha mipango ya sekta nyingine.

Nae Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC),Godwill Wanga amesema wameanzisha mkutano huo ili kukutanisha Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali na wadau wa sekta binafsi ili kujadili changamoto, fursa na maboresho kwaajili ya kukuza mchango wa sekta katika maendeleo ya uchumi na jamiii nchini.

Share:

MBUNGE ABINUKA SARAKASI AKIONESHA HISIA ZAKE BUNGENI DODOMA



Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay akiwa amebinuka sarakasi ndani ya ukumbi wa Bunge alipokuwa akichangia mjadala wa kupitia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 jijini Dodoma leo Mei 23,2022.

Flatei alichukua uamuzi huo ikiwa ni njia ya kuonyesha hisia zake kwa kero ya kutokuwa na barabara ya lami katika jimbo lake. Picha na Edwin Mjwahuzi
Chanzo #mwananchi



Share:

WATEJA KUOKOA HADI Tsh 1,000,000 KAMPENI MPYA YA "LGs SOMETHING BETTER"

Dar Es Salaam, , Kampuni mashuhuri kwa uuzaji wa bidhaa zinazotumia umeme ya LG Electronics East Africa imetangaza kuzindua Kampeni ya " LGs Something Better " kote nchini inayolenga kuboresha uzoefu wa ununuzi kwa wateja.

Kampeni hiyo, inatarajia kuendelea hadi tarehe 12 Juni 2022 kwa lengo la kuwapa wateja punguzo la hadi 20% kwa bidhaa zilizochaguliwa pamoja na thamani na manufaa zaidi kwa wateja wanaonunua bidhaa kutoka kwa maduka ya chapa ya LG.

 Kwa punguzo la ofa, wateja wanatarajiwa kuokoa kuanzia shilingi 50,000/= hadi kufikia Tsh 1,000,000/= katika kipindi cha wiki tano zijazo katika bidhaa zote katika kategoria ya Burudani , Vifaa vya Nyumbani na Viyoyozi vya Makazi. Akitoa maoni yake kuhusu kampeni hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa LG Afrika Mashariki, Sa Nyoung Kim alisema, “Kupitia ubunifu na bidhaa zetu za hivi punde, lengo letu ni kuwasaidia wateja wetu kuishi maisha bora na rahisi zaidi. Huu ukiwa ni mwezi wa Eid al-Fitr, tunatoa nafasi kubwa kwa kila mtu kuchagua maisha haya bora sio tu ya leo bali ya kesho pia”.

 "Hii pia ni fursa kwa Watanzania kubadilisha na kuboresha burudani zao za nyumbani au vifaa ambavyo wamekuwa navyo kwa muda mrefu hadi kufikia teknolojia mpya, ya kisasa na vifaa vya ufanisi zaidi". 

Hii si tu katika maduka yenye chapa ya LG bali pia katika maduka makubwa ya washirika kama vile Shoppers na Game Super Market. Wanunuzi wamehakikishiwa kupata punguzo kubwa la hadi Tsh 539,200/=kwenye jokofu za LG Instaview 668(L), na Tsh 225,000/= kwenye jokofu la LG Instaview 544(L).

 Kwenye mashine za kufulia zinazotolewa, punguzo linaanzia Tsh 100,000/= hadi Tsh. 300,000 kwa mashine za kufulia ya 8Kg hadi ya 15Kg / dryer. LG microwaves, Neo Chef 20L, 23LNeoChef na 42L Neo Chef zote zina punguzo la kati ya Tsh 81,600/= na TZsh 122,800/= Kufahamu zaidi kuhusu kampeni hii kabambe tafadhari tembelea mitandao ya kijamii ya LGs East Africa. 
    
Share:

KONGAMANO LA AIESEC LAFANYIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA

Kongamano la kuwajengea uwezo Wanafunzi wa vyuo vikuu kuchangamkia fursa mbalimbali lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC Tanzania na kudhaminiwa na kampuni ya Madini ya Barrick, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali limefanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Katika kongamano hilo wanafunzi walipata nafasi ya kusikiliza mada mbalimbali zilizotolewa na wasomi kutoka kwenye makampuni yanayofanya vizuri ambazo zilijikita kuwajengea uwezo wa kujiamini, kuwa wabunifu sambamba na kusoma kwa bidii ili wasiachwe nyuma katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazojitokeza pia kuweza kuajirika na kuweza kujiajiri.
Meneja Raslimali Watu wa Mgodi wa Bulyanhulu,Lumbu Kambula akiongea katika kongamano hilo.
Mwanafunzi wa UDOM akiuliza swali wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya Wanafunzi wa UDOM wakifuatilia mada wakati wa kongamano hilo.
Wanafunzi wakiwa katika picha na Afisa wa kampuni ya Barrick.
Baadhi ya Wanafunzi wa UDOM wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa IESEC,Barrick na waliotoa mada mbalimbali katika kongamano hilo.
Share:

AUAWA KWA KUPIGWA RISASI AKIVUA SAMAKI ENEO LA MGODI KISHAPU




Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Mei 23,2022

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Hamis Mayunga (27) mkazi wa Kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu ameuawa kwa kupigwa risasi na anayedaiwa kuwa Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Sam Security aitwaye Emmanuel Chacha katika eneo la Mgodi wa Almasi wa El – Hilal wilayani Kishapu.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumatatu Mei 23,2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema tukio hilo limetokea Mei 20,2022 majira ya saa nne usiku katika eneo la mgodi wa El - Hilal.


“Hamis Mayunga (27) mkazi wa kijiji cha Dulisi wilayani Kishapu aliuawa kwa kupigwa risasi na Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Sam Security yenye makao Makuu yake Mjini Shinyanga katika eneo la Mgodi wa El Hilal.


Huyu Hamisi Mayunga akiwa na wenzake wasiopungua 10 walikuwa wanavua samaki katika bwawa lililopo katika mgodi wa El – Hilal ndipo Mlinzi wa Kampuni ya Sam Security aitwaye Emmanuel Chacha akiwa na wenzake wanne waliondoka katika lindo lao walilopangiwa wakaenda katika bwawa hilo (ambalo siyo eneo lao la kazi, hawa hawafanyi doria) wakawazuia kuvua samaki , pakatokea kutoelewana ndipo akamfyatulia risasi kwa kututmia bunduki aina ya Shortgun ikampiga kwenye moyo upande wa kushoto na kusababisha kifo chake papo hapo”,ameeleza Kamanda Kyando.


“Mtuhumiwa wa mauaji Emmanuel Chacha alitoroka baada ya kutekeleza mauaji hayo na kutelekeza bunduki kwenye mlango wa mgodi. Tayari tunawashikilia walinzi wanne huku tukiendelea kumtafuta mtuhumiwa ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake”,ameongeza Kamanda Kyando.


“Natoa wito kwa walinzi wa makampuni binafsi ya ulinzi kuacha kujichukulia sheria mkononi na kuacha kutumia nguvu kupita kiasi…Haiwezekani mtu anavua tu samaki, vipelege umpige risasi…Nimepanga kukutana na Makampuni binafsi ya ulinzi kwani hili sasa ni tukio la pili mwezi huu ambapo hata kule Mwakitolyo Mlinzi wa Kampuni ya Light Ndovu Security Abdul Chacha naye aliua mwananchi aliyekuwa anagombana na mke wake…Yaani mtu agombane tu na mkewe umpige risasi?”,amesema Kamanda Kyando.


Pia ametoa wito kwa wananchi wakiona eneo linalindwa wasiingie kwa nguvu.
Share:

Sunday, 22 May 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 23, 2022


Magazetini leo Jumatatu May 23 2022






















Share:

RAIS SAMIA APOKEA UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA RAIS WA JAMHURI YA ZIMBABWE EMMERSON MNANGAGWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa, Balozi Simbarashe Mumbengengwi mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 22 Mei,2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa, uliowasilishwa kwake na Mjumbe huyo Maalum Balozi Simbarashe Mumbengengwi, Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 22 Mei,2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, Balozi Simbarashe Mumbengengwi mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 22 Mei,2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mjumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa, Balozi Simbarashe Mumbengengwi mara baada ya kuwasilisha Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais Mhe. Emmerson Mnangagwa Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 22 Mei,2022.
Share:

WAZIRI DKT MABULA ASHIRIKI MKUTANO WA MAJIJI KISUMU KENYA


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha na baadhi ya viongozi kutoka nchi mbalimbali walioshirikia Mkutano wa Tisa wa Kimataifa wa Majiji uliomalizika Mei 22, 2022 katika mji wa Kisumu nchini Kenya.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Katibu Mkuu wa Taasisi ya United Cities and Local Government of Africa (UCLG Africa) Jean Pierre Elong Mbassi (Kulia) wakati wa mkutano wa tisa wa kimataifa wa Majiji uliomalizika katika mji wa Kisumu nchini Kenya Mei 22, 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa na Mawaziri wa Eswatini wakati wa Mkutano wa Tisa wa Kimataifa wa Majiji uuliomalizika katika mji wa Kisumu nchini Kenya Mei 22, 2022

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa ameshikilia Tuzo ya Heshima iliyotolewa na Taasisi ya United Cities and Local Government of Africa (UCLG Africa) kwa Rais Mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne Jakaya Kikwete wakati wa mkutano wa tisa wa kimataifa wa Majiji uliofanyika Kisumu nchini Kenya.

*****************************

Kisumu, KENYA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameshiriki mkutano wa tisa wa viongozi wa majiji huko Kusumu nchini Kenya.

Mkutano huo uliomalizika Mei 222, 2022 uliwakutanisha maelfu ya wadau ulijadili maendeleo ya miji Barani Afrika na ulifunguliwa kwenye mji wa Kisumu, Magharibi mwa Kenya.

Mbali na maelfu ya Wadau, Watalaam na Viongozi wa Miji waliokutana kwenye mkutano huo, viongozi kadhaa wa mataifa ya Afrika, pamoja na wale waliostaafu nao walihudhuria mkutano huo.

Aidha, kupitia mkutano huo Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula alikabidhiwa Tuzo ya Heshima (Commitment in Fevour of the African Movement of the Territorial Government) kwa niaba ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete iliyotolewa na Taasisi ya United Cities and Local Government of Africa (UCLG Africa).

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo wa kimataifa maarufu kwa jina la Africities ni kuhusu hali ya miundo mbinu kwenye miji mbalimbali na namna bora ya kuimarisha maisha ya wakazi wa miji hiyo.

Mameya wa miji mbalimbali, Mawaziri wa serikali za mitaa walihudhuria mkutano huo na kutafuta suluhu ya changamoto zinazowasumbua wakazi wa miji yao kama vile mipangilio mibaya ya majengo, mitaa pamoja na changamoto za upatikanaji wa umeme.

Huo ni mkutano wa kwanza kufanyika katika jiji ambalo lina wakazi kati ya Elfu 50 na Laki tano ambapo kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2009 lina watu 409,000.

Kauli mbiu ya mkutano huu ni mchango wa miji inavyoweza kuchangia utekelezwaji wa dira ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 na Umoja wa Afrika mwaka 2063.

Majiji mengine ambao yamewahi kuandaa mkutano huu unaofanyika kila baada ya miaka mitatu tangu1998 jijini Abidjan, umewahi pia kufanyika jijini Johannersburg, Dakar Kule Senegal na Marakesh Nchini Morocco.
Share:

BOSI AFUKUZWA KAZI KWA KUTAZAMA VIDEO ZA NGONO OFISINI

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger