Tuesday, 17 May 2022
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE CHANGARA MAKISATU
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa maonesho haya.
Mbunifu Ashirafu Madai Selemani kutoka chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere aliyegundua mfumo wa kuwezesha magari ya dharura kubadili taa za barabarani 'Traffic Light Control for emergency Vehicle"
Mbunifu Nauriya Abbdallah Kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere aliyegundua mfumo wa kisasa wa ukusanyaji taka.
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere leo kimeshiriki ufunguzi wa maonesho ya Wiki ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) 2022 yanayofanyika Mkoani Dodoma.
Akizungumza wakati akifungua maonesho hayo mgeni rasmi Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman amewataka watu mbalimbali wenye uwezo wa kuonesha bunifu mbalimbali kuendelea kujitokeza ili serikali ione namna itakavyowaunga mkono.
Akizungumza akiwa kwenye banda la Chuo hicho Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila amesema Chuo kimeendelea kuibua bunifu nyingi zaidi ambazo zitasaidia Serikali katika kuchangia Uchumi wa Kati wa Viwanda.
Prof. Mwakalila amesema Zaidi ya bunifu 20 zinashiriki maonesho ya Wiki ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.(MAKISATU).
Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni Ubunifu kwa Maendeleo Endelevu.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
16.05.2022
SHAKA ASEMA UONGOZI WA RAIS SAMIA UNASIMAMIA MISINGI YA HAKI, DEMOKRASIA NA UTAWALA BORA
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza kwenye moja ya mikutano yake ya ndani mjini Babati,mkoani Manyara akiwa kwenye ziara yake ya kujitambulisha mbele ya wanachama wa ccm , kama mlezi mpya wa chama hicho akichukua nafasi ya Waziri mkuu mstaafu Mzee Mizengo Pinda.
Wanachama wa CCM mjini Babati wakimsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza nao kwenye kikao cha ndani
Wanachama wa CCM mjini Babati wakifurahia jambo baada ya kumsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka alipokuwa akizungumza nao kwenye kikao cha ndani. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG
***
*Awahimiza watanzania kuunga mkono jududi za Serikali za kuleta maendeleo
Said Mwishehe,Michuzi TV-Manyara
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka ameendelea kuhimiza wananchi wote kuhakikisha wanashirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo na uongozi wa Rais umekuwa kinara katika kutenda haki, demokrasia na utawala bora.
Aidha amesema tangu Rais Samia ameingia madarakani amekuwa na uthubutu wa kufanya mambo makubwa kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na maendeleo huku akiwataka wananchi na shaka yoyote kwani Rais atawavusha salama na ataendelea kuwatumikia kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo mkubwa.
Akizungumza kwenye mikutano yake aliyofanya mkoani Manyara kwa nyakati tofauti Shaka amesema uongozi wa Rais Samia pamoja na mambo mengine ya kimaendeleo umekwenda kufungua uhuru, haki na demokrasia kwa kila mmoja wetu na lengo ni kuhakikisha wananchi wanashiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa taifa la Tanzania.
“Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara katika kuheshimu misingi yakutenda haki, demokrasia na utawala bora na tangu alipoingia madarakani ameweka mazingira mazuri ya kufanya siasa hapa nchini.
Shaka amesema wananchi hivi sasa ni mashahidi wameshuhudia vyama vya siasa na wanasiasa wakiwa huru kufanya shughuli zao za kisiasa bila kusumbuliwa tofauti na huko nyuma.“Rais Samia ametoa uhuru mkubwa kwa wanasiasa na vyama vya siasa kufanya siasa kiungwana na kuvumiliana” amesema Shaka na kuongeza
“Rais Samia tangu aingie madarakani ameshakutana mara mbili na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe lakini pamoja viongozi wengine wa upinzani.Tunaposema Rais Samia amekuwa kinara wa haki, kinara wa demokrasia na kinara wa utawala bora tunayo mifano.
“Ndio maana husikii wanasiasa wakilalamika lakini hata yale mambo ya kusikia fulani kapotea , haonekani siku hizi hayapo tena.Watu wako huru kufanya shughuli zao na wala hawasumbuli, Rais Samia nia yake ni njema kwa taifa hili hivyo ni wajibu wetu kumuunga mkono na kumpa ushirikiano.”amesema Shaka.
Pamoja na hayo Shaka amewataka wananchi wote ujumla kujiandaa kwa mambo makubwa zaidi ya kufurahisha ndani ya utawala wa Rais Samia na kwa uthubutu ambao amekuwa akiuonesha ni imani yake yajayo yanafurahisha zaidi.
Hata hivyo katika ziara yake kwenye Mkoa huo shaka ameendelea kuwakumbusha wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanaelezea mafanikikio yaliyopatikana kwenye maeneo yao kotokana na fedha wanazopewa na Serikali badala ya kukaa kimya wakati kuna mambo makubwa ya maendeleo yamefanyika.
SERIKALI YAZITAKA TAASISI KUWAJENGEA UWEZO WAKAGUZI WA NDANI
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Bw. Athumani Mwituka alipokuwa akizungumza kwenye warsha ya wakaguzi wa ndani iliyoandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa Ndani nchini (IIA), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uelewa wa Wakaguzi wa ndani duniani.
Baadhi ya washiriki kwenye warsha ya wakaguzi wa ndani iliyoandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa Ndani nchini (IIA), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uelewa wa Wakaguzi wa ndani duniani.
Viongozi wa Meza kuu kwenye warsha ya wakaguzi wa ndani iliyoandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa Ndani nchini (IIA), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uelewa wa Wakaguzi wa ndani duniani, iliyofanyika mkoani Tanga.
Mwandishi Wetu, Tanga
SERIKALI inategemea kuwa na Wakaguzi 300 wa Mifumo kote nchini katika sekta za Umma ifikapo Mwaka 2026 ili kuhakikisha inaweka udhibiti wa mapato kwenye shughuli zinazofanywa na taasisi zake mbalimbali.
Wakati huo huo imezitaka sekta binafsi kuhakikisha zinatambua umuhimu wa wakaguzi wa ndani na kuwajengea uwezo wakaguzi wao ili waweze kufanya ukaguzi wa mifumo kwa ufanishi, huku wakiwa na vyeti vinavyotambulika kimataifa.
Kauli hiyo, imetolewa juzi jijini Tanga na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Bw. Athumani Mwituka alipokuwa akizungumza kwenye warsha ya wakaguzi wa ndani iliyoandaliwa na Taasisi ya Ukaguzi wa Ndani nchini (IIA), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uelewa wa Wakaguzi wa ndani duniani.
Katika warsha hiyo Serikali imeweka wazi mapungufu ambayo hung'amuliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG na nini kifanyike ili kupunguza hoja za mashaka ndani ya taasisi zao, amewataka wakaguzi hao kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na miongozo ya kimataifa, hivyo wana kila sababu ya kuongeza ujuzi wao kwa manufaa ya taasisi na taifa kwa ujumla.
Alisema kwa kuanzia aupande wa Serikali imeanzisha mifumo mingi ya ukusanyaji mapato ambayo inachangia katika udhibiti matumizi mabaya na pia imechangia kurahisisha utendaji kazi wa shughuli zake.
" Upande wetu serikalini tumejipanga ifikapo Juni 2026 tuwe na wakaguzi wa mifumo kwa sekta za umma takribani 300. Tunatoa wito kwa sekta binafsi nao kuhakikisha inawajengea uwezo wakaguzi wao ili waweze kufanya ukaguzi wa mifumo kwa ufanishi, huku wakiwa na vyeti vinavyotambulika.
Serikali itaendelea kuongeza uwezo wa wakaguzi wa ndani ikiwemo kufanya ukaguzi wa miradi na tayari Waziri wa Fedha na Uchumi, ametoa maelekezo ya kuwa kila unapobuniwa mradi ndani ya taasisi zake itengwe fedha kwa ajili ya kufanikisha mkaguzi wa ndani kufanya ukaguzi wake.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya IIA, Bi. Zelia Njeza akizungumza alisema taasisi hiyo ya wakaguzi inaungana na wakaguzi wengine duniani kote kusherekea mwezi huu wa wakaguzi wa ndani, na umejipanga kusherehekea kitofauti zaidi kwa kuhakikisha tunawajengea uwezo wakaguzi wa ndani.
Alisema maadhimisho ya mwaka huu pamoja na kuwajengea uwezo wanachama wao, lakini wamelenga zaidi kujumuika na kusherekea mafanikio ya ukaguzi wao ndani ya taasisi wanazofanyia kazi.
Alisema bado kunachangamoto ya uelewa wa kazi za wakaguzi wa ndani katika jamii na changamoto hii ya uelewa haipo katika jamii ya Watanzania tu bali hata katika nchi zingine.
"...Kwa ujumla ukitofautisha na fani zingine kama udaktari, mtu yeyote ukimuuliza kuhusu daktari atakujibu ni nani...tumekubaliana mwezi huu wa tano uwe ni mwezi maalum kuweza kusherehekea mafanikio yoyote tuliyoyaleta kwa kutumia kazi zetu.
"...Na ni kipindi ambacho tunatumia fursa hii kuweza kuwaelimisha wadau wetu kuhusu umuhimu wa wakaguzi wa ndani na ni kitu gani wategemee kutokana na kazi zetu, kutoa elimu kwa wadau ni muhimu kwani kama hawatajua nini tunakifanya wanaweza wakawa na kigugumizi hata kuitaji huduma zetu," alisema.
SIMBA SC YAKUTANA NA RUNGU KUTOKA CAF KWA KOSA LA KUWASHA MOTO UWANJANI
SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF) limeipiga faini ya dola za Kimarekani 10,000 (zaidi ya shilingi milioni 22.8) Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Ni baada ya kupatikana na hatia kuwasha moto katika uwanja wa Orlando katika mchezo dhidi ya Orlando Pirates.
Kabla ya mchezo huo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho,wachezaji wa Simba walionekana kukusanyika katikati ya uwanja na baadaye moshi kutokea katikati ya kundi hilo.
Taarifa kutoka CAF imesema, maafisa wa mchezo walionesha katika ripoti zao kwamba, wachezaji wa Simba waliwasha moto katikati ya uwanja wakati wakijifanya kuomba kabla ya mechi.
"Ilitubidi kumwaga maji ili kuuzima moto,”wameeleza huku wakibainisha kuwa, malipo hayo yanapaswa kufanyika ndani ya siku 60 kuanzia sasa.