Monday, 21 March 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 21,2022

Magazetini leo Jumatatu March 21 2022






Share:

Sunday, 20 March 2022

ASKOFU MACHIMU APONGEZA NAMNA RAIS SAMIA ANAVYOSIMAMIA NA KUHIMIZA UADILIFU KWA VIONGOZI

Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Askofu wa Kanisa la EAGT Ushirika Makimbilio Healing Center mjini Shinyanga, Raphael Machimu  amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusimamia uadilifu wa viongozi walioko chini yake.

Askofu Machimu amesema hayo leo Jumapili Machi 20,2022 wakati ibada iliyofanyika katika Kanisa la Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT).

Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja ambacho Rais Samia amekuwa madarakani amekuwa akihimiza uadilifu kwa viongozi walioko chini yake hali inayosababisha nchi kuendelea kupiga hatua kimaendeleo.

Akihimiza waumini kuendelea kusali na kuliombea Taifa la Tanzania na viongozi wake Askofu Machimu amesema ni wajibu wa waumini wa kanisa hilo kuedelea kusali na kuomba katika familia zao wakiliombea Taifa na viongozi wake maana pasipo amani na utulivu waumini hawawezi kupata nafasi ya kufanya shughuli zao.

Pia Machimu, amewashukuru waumini wa kanisa hilo kwa kudumisha umoja na mshikamano kwa wachungaji na viongozi hilo hali inayowapa moyo wa kuendelea kuhubiri na kulitangaza neno la Mungu.

Kwa upnde wao badhi ya waumini walio walio hudhuria ibada hiyo waliahidi kuyezingai maagizo naUshauri ulio tolewa na Asofu kwa kuwa waminifu katika familia najamii ikiwemo kuendelea kuomba na kusali wakiliombea Taifa la Tanzania na viongozi wake.
Share:

MGONGOLWA : RAIS SAMIA AMEUPIGA MWINGI TUMUUNGE MKONO KWA NGUVU ZOTE

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Mjini mkoani Iringa, Joseph Mgongolwa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza mwaka mmoja madarakani huku Watanzania wakitembea kifua mbele kwa mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika sekta mbalimbali.

Mgongolwa ameyasema hayo leo Machi 20,2022 wakati akizungumzia mafanikio ya uongozi wa mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani na kutoa wito kwa wanachama na Watanzania wote kuendelea kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita.

"Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameupiga mwingi sana,kila sekta ina jambo la kujivunia kutokana na uongozi wake mahiri, sisi makada na wanachama tunampongeza sana kwa kazi nzuri. Tunajisikia fahari kuona ndani ya mwaka mmoja wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani amefanya mambo mengi mno",amesema.

Pia amesema, kuna mambo mengi ya maendeleo,kiuchumi,kijamii na kisiasa yamefanyika ndani ya mwaka mmoja ambayo Watanzania wameyasikia na kuyaona ikiwemo miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

"Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameongeza usimamizi wa sera za soko huria, sera za kiuchumi na kifedha zenye mwelekeo wa kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.

"Ukitazama au kufanya tathimini ya haraka utagundua kuwa tangu Machi 2021 hadi leo Machi 2022, Tanzania imeongoza kwa kuvutia kiwango kikubwa zaidi cha uwekezaji kutoka nje kwa Ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kiwango cha uwekezaji kutoka nje kimeonekana kustawi kwa kasi. Hii ni hatua njema sana na inafaa kuungwa mkono kwa hali na mali ili kuhakikisha Tanzania inasonga mbele kiuchumi,"amesema.

Pia amesema taifa la Tanzania lina bahati kubwa ya kumpata kiongozi mwanamke mwenye ujasiri, hodari na hofu ya Mungu katika kuwaongoza Watanzania na kuwatumikia.

"Mheshimiwa Rais Samia, ni kati ya wanawake ambao Mungu amewajalia karama ya kipekee katika uongozi, ni kiongozi ambaye ana uzoefu mkubwa, mwenye kuyajua mahitaji ya wananchi na Taifa kwa ujumla. Rekodi hizi zinamuwezesha kupanga na kuelekeza nguvu katika mipango mbalimbali ya miradi ya maendeleo ili iweze kuwanufaisha Watanzania wote,"amesema Mgongolwa.

Amefafanua kuwa, mwaka mmoja wa Rais Samia akiwa Ikulu ameonyesha uwezo mkubwa na karama ya uongozi uliojaa ukomavu mkubwa wa kisiasa na maono makubwa,hekima na busara.

"Pia Mheshimiwa Rais Samia ana upendo na wananchi wake,ni kiongozi shupavu aliyeshiba dini na hofu ya Mungu, anachukia dhuluma na anataka kuona haki inasimama, hayo yote ni matunda mema ya kupata kiongozi mwenye uzoefu katika nafasi mbalimbali za utumishi.

"Chini ya uongozi wake imara na shupavu,kwa siku 365, Mheshimiwa Rais Samia amezidi kutufanya Watanzania wamoja bila kujali dini,ukabila, kanda, siasa na jinsia,"amesema Mgongolwa.

Amesema, Mheshimiwa Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kupitia serikali yake kuwajumuisha na kuyashirikisha makundi mbalimbali kutoka katika jamii ili yaweze kumsaidia kusimamia na kufanikisha mipango mbalimbali ya maendeleo nchini.

"Kuanzia vijana, wazee,wanawake wakiwemo viongozi wa dini, wanasiasa, machifu, wafanyakazi na wakulima, wafanyabiashara na machinga, wanamichezo,wasanii na wengine wengi wamekuwa sehemu ya kumsaidia Mheshimiwa Rais Samia kufanikisha mipango mbalimbali ya kuleta maendeleo katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Amesema, mbali na kuimarisha uhusiano wa Kimataifa baina ya Tanzania na nchi za jirani, kikanda na jumuiya ya Kimataifa kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo diplomasia ya uchumi, Mheshimiwa Rais amefanikiwa kutafuta fedha ambazo zinatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya, maji, elimu, miundombinu na nyinginezo.

"Kwa msingi huo, nichukue nafasi hii kuwaomba makanda na wanachama wa CCM wakiwemo Watanzania wote kwa ujumla kujitokeza kila kona kuyaeleza mafanikio haya ili kutoa hamasa kwa jamii kushiriki zaidi katika shughuli za maendeleo. Ninaamini kupitia uongozi huu mahiri wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ifikapo Machi 2023, Taifa la Tanzania litakuwa na mafanikio makubwa mno,"amesema Mgongolwa.
Share:

CHANGAMOTO YA UPOTEVU WA MAZAO YA WAKULIMA WAKATI WA MAVUNO YAPATIWA UFUMBUZI


Mkurugenzi wa kampuni ya Imara Teknolojia ya jijini Arusha, Alfred Chengula akielezea mashine ambazo wameweza kuzibuni ikiwemo ya kupukuchua na kupura mazao ya aina Tisa .

Na Rose Jackson,Arusha.

Upotevu wa mazao ya wakulima wakati wa mavuno unaowakabili wakulima wengi sasa umepata ufumbuzi baada ya baadhi ya watafiti kugundua mashine yenye uwezo kudhibiti tatizo hilo.

Akielezea mafanikio hayo jijini Arusha kwa waandishi wa habari waliotembelea kampuni ya Imara Teknolojia ya jijini Arusha kwa lengo la kujifunza habari kwa vitendo ,mara baada ya kupatiwa mafunzo na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Mtafiti na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Alfred Chengula amesema mashine hiyo ina uwezo wa kuwasaidia wakulima kupukuchua mazao ya aina mbalimbali yakiwemo mahindi.

Amesema wameweza kubuni mashine mbili tofauti ambapo mojawapo inapukuchua na kupura mazao tisa tofauti Kama mahindi, Alizeti, maharage mbaazi,choroko na mengineo , ambapo walibuni ili iwasaidie wakulima wadogo na wajasirimali.

Mashine hii inatumia boda boda na ina uwezo wa kupukuchua mahindi gunia mia mbili kwa siku moja tofauti na awali ambapo wakulima walikuwa wanatumia muda mrefu kupiga piga mahindi.

Ametaja mashine ya aina ya pili ambayo wameweza kubuni ni ya kuchakata na kubaraza nafaka mbalimbali kwa ajili ya chakula cha mifugo.

Amedai kuwa mashine hii ina uwezo wa kusaga magunzi ,kukata majani kama mabua na ina uwezo wa kubaraza mahindi na mashudu kwa ajili ya kulishia mifugo.

"Mashine hizi tunazitengeneza wenyewe na lengo letu ni kuwasaidia Wakulima na Wafugaji waweze kufikia malengo yao kwa muda mdupi zaidi kwa kuboresha maisha yao",aliongeza.

Chengula amesema kuwa pamoja na kupata mafanikio hayo ya kubuni mashine hizo lakini bado wanakabiliwa na changamoto ya kuboresha miundo mbinu yao ya kazi hivyo anaamini mara baada ya COSTECH kutembelea kampuni hiyo itamwezesha kutatua changamoto hiyo illi kuweza kufikia ndoto za utengenezaji wa mashine ambazo wameshazifanyia tafiti.

Baadhi ya wakulima waliofikiwa na teknolojia hizo ameeleza kuwa mashine hiyo imemsaidia kupukuchua mahindi kwa muda mchache iikiwa ni pamoja na kueleza changamoto zake ikiwemo ya uwezo mdogo wa kumudu gharama .

Licha ya watafiti kufikia mafanikio hayo na faida zilizoanza kupatikana ,ili lengo liweze kutimia ushirikishaji wa wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari Tume ya Taifa ya sayansi na Teknolojia COSTECH na pia taasisi za fedha unahitajika .
Share:

ESRF YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA



Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) , Dkt. Tausi Kida akizungumza wakati wa ufunguzi wa mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dkt. Hamisi Mkanachi ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akizungumza kwenye mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.
Mtafiti Mshiriki Mwandamizi wa ESRF, Prof. Samuel Wangwe akizungumza kwenye mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.
Mkurugenzi wa masuala ya Kisekta wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Emmanuel Manase akizungumza kwenye mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara (Uwekezaji), Bw. Ally S. Gugu akizungumza kwenye mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.
Balozi Modest Mero akizungumza kwenye mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) akizungumza kwenye mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.
Mjumbe akichangia hoja kwenye mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia 
Washiriki wa mjadala wa kisera katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia wakiwa wamesimama kwa dakika moja kumkumbuka Rais wa awamu ya tano, hayati Dkt. John Magufuli ambaye ametimiza mwaka mmoja tangu kufariki kwake.

Na Mwandishi Wetu.

Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imempongeza Rais wa Awamu ya Sita wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo ameifanya katika kipindi cha mwaka mmoja tangu aingie madarakani.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt. Tausi Kida katika mjadala wa kisera ambao umefanyika katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia ulioandaliwa na ESRF.

Dkt. Kida alisema kwamba kumekuwa na mafanikio makubwa katika maeneo mbalimbali jambo ambalo litaisaidia Tanzania kupiga hatua kubwa katika maendeleo kwa nchi na mwananchi mmoja mmoja.

“Malengo makuu ni kuangalia mafanikio ya kisera ambayo yamepatikana katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Ramia, pia kupata nafasi ya kujadili safari letu ya mafanikio kama mnavyojua mafanikio ya nchi yanahusisha wadau mbalimbali,

“Ukiangalia kwenye kipindi cha mwaka mmoja Rais amefanya mambo makubwa, ukiangalia hata hali ya kiuchumi kila kitu kinaenda vizuri. Kwakweli anastahili pongezi nyingi sana.” alisema Dkt. Kida.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dkt. Hamisi Mkanachi ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, alielezea namna Rais Samia alivyoleta mabadiliko makubwa ya maendeleo katika wilaya ambayo anaiongoza.

Alisema kumekuwa na miradi mingi ambayo inatekelezwa tangu Rais Samia aingie madarakani, hivyo amewataka wananchi kutumia fursa katika miradi hiyo ili kujitengenezea kipato.

“Mhe. Rais ana utu, anajali haki za watu. Nimekuwa Mkuu wa Wilaya kwa miezi 6 au 7 kwahiyo haya ni yale ambayo mimi nimeyaona. Kwenye utoaji wa huduma hakuna wa kumlinganisha, mfano kwenye bajeti ya barabara za TARURA wilayani kwetu bajeti imepanda kutoka Tsh. 2 bilioni hadi Tsh. 4 bilioni.” alisema Dkt. Mkanachi.

Pia alizungumzia namna uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita unavyofanikisha Mpango wa Maendeleo ya Uchumi (LED) katika sekta ya elimu, miradi ya kimkakati na afya ambayo kwa pamoja itasaidia kukukuza uchumi wa nchi na maendeleo kwa wananchi.

Awali akitoa taarifa kuhusu mafanikio ya Rais Samia, Mtafiti Mshiriki Mwandamizi wa ESRF, Prof. Samuel Wangwe alisema licha ya kwa madarakani kwa muda mfupi lakini mafanikio ni mengi.

“Ukuaji wa uchumi katika sekta mbalimbali za uchumi hususani baada ya janga la ugonjwa wa Korona. Lakini pia ameondoa vikwazo vya kibiashara, uhusiano na wawekezaji umeimarishwa. Hata anapofanya safari zote anakuwa na wafanyabiashara, alisema Prof. Wangwe.

Kwa upande wa Balozi Modest Mero ambaye aliwasilisha mada namna Rais Samia alivyoboresha uhusiano wa kimataifa na diplomasia ya uchumi alisema kuwa kazi kubwa imefanywa na Rais na baada ya kipindi kifupi Watanzania wataona mabadiliko makubwa ambayo yametokana na ziara za Rais alizofanya hivyi karibuni kwenye mataifa makubwa duniani.
Share:

Breaking : SPIKA WA BUNGE LA UGANDA AFARIKI DUNIA


Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza kifo cha Spika wa Bunge la Uganda, Jacob Oulanyah leo Jumapili “Alikuwa Kada mzuri nimechelewa kutoa taarifa ili Watoto wake wajulishwe kwanza”.

Kilichosababisha kifo cha Oulanyah hakijabainishwa lakini alikuwa amelazwa Hospitali nchini Marekani kwa zaidi ya mwezi mmoja na ilizua mjadala kwa Waganda ambao walidai iligharimu pesa nyingi sana za walipa kodi kumtibu.

Oulanyah alichukua kiti cha Spika wa Bunge la Uganda mnamo Mei 2021 na kabla ya hapo alikuwa Naibu Spika kuanzia 2011.

Kusafirishwa kwake hadi Marekani kwa matibabu kulizua mjadala miongoni mwa Waganda, ambao walidai kuwa iligharimu pesa nyingi sana za walipa kodi.


Bw. Oulanyah alichukua hatamu ya uongozi wa bunge la Uganda mnamo Mei 2021. Alikuwa naibu spika kuanzia 2011.

Alikuwa na sifa ya kuanzisha vikao vya bunge kwa wakati, na kila mara alitoa wito kwa wabunge kuimarisha ubora wa mijadala, kwa kujadili mambo waliyo na ufahamu wa kina.

Alikuwa mwanasheria na mwanasiasa wa muda mrefui. Aliwahi kuwa mbunge wa Eneo Bunge la Kaunti ya Omoro, kaskazini mwa nchi.

Bw. Oulanyah alikuwa miongoni mwa wanasiasa kutoka eneo hilo walioshiriki katika mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Uganda na waasi wa Lord's Resistance Army walioongozwa na Joseph Kony miaka ya 2000.

Share:

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUELIMISHA WAUMINI UMUHIMU WA SENSA YA WATU NA MAKAZI

Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita Mhasham Flavian Kassala akikata utepe wa ufunguzi wa Kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima. Wa pili kulia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ambaye alikuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita Mhasham Flavian Kassala akifungua rasmi lango Kuu la Kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita katika hafla ya Kutabaruku kanisa hilo iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimpatia zawadi Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita Mhasham Flavian Kassala wakati wa hafla ya kutabaruku Kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita mwishoni mwa wiki.

Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita Mhasham Flavian Kassala akipaka moja ya nguzo 12 za Kanisa mafuta ya krisma ndani ya kanisa mbele ya waumini wakati wa hafla ya kutabaruku Knisa jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita mwishoni mwa wiki.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikabidhi cheti kwa baadhi waumini wakati wa hafla ya kutabaruku Kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita mwishoni mwa wiki.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waumini waliochangia Samani za Kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita kwenye hafla maalum ya Kutabaruku kanisa hilo mwishoni mwa wiki ambapo alimuwakilisha Waziri Mkuu.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwahutubia waumini waliohudhuria hafla ya Kutabaruku Kanisa la Bikira Maria wa Fatima Geita iliyofanyika mwishoni mwa wiki ambapo alimuwakilisha Waziri Mkuu.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katikakati ya Mapadre wakati wa kuendesha harambee ya kuchangia Samani za Kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita katika hafla maalum ya Kutabaruku kanisa hilo mwishoni mwa wiki ambapo alimuwakilisha Waziri Mkuu.

******************

Serikali imewataka viongozi wa dini nchini kuwaelimisha waumini wake umuhimu wa kuhesabiwa katka sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Aidha, imewataka viongozi wa dini kuendelea kusaidia katika suala zima la malezi ya kiroho ili kujenga jamii yenye kumcha mungu, uadilifu na ubinadamu.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa Kutabaruku Kanisa la Bikira Maria wa Fatima Geita mwishoni mwa wiki, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema, Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi ambazo bila ya kuwa na takwimu sahihi haitaweza kupanga mipango thabiti ya matumizi endelevu ya rasilimali hizo.

‘’Viongozi wa Dini mnao waumini wengi tumieni fursa hiyo kuwaelimisha waumini wenu umuhimu wa kuhesabiwa’’ ilieleza hotuba ya Waziri Mkuu.

Alisema, zoezi la sensa ya watu na makazi ni muhimu kwa kuwa linaipatia nchi takwimu za msingi zinazotumika kutunga sera, kupanga mipango na program za maendeleo pamoja na kufuatilia utekelezaji wake.

Kupitia hotuba hiyo, Dkt Mabula alieleza kuwa, takwimu rasmi zitawezesha serikali na wadau wenghine kufuatilia na kutathmini malengo yaliyofikiwa katika kutekeleza mipango ya maendeleo iliyokusudiwa sambamba na chanagmoto mbalimbali zitakazojitokeza katika sekta zote na hatimaye kuweka malengo na mikakati ya kukuza uchumi pamoja na kupunguza umasikini miongoni mwa watanzania.

Aidha, ilieleza kuwa, hivi karibuni kumekuwa matukio yanayohusisha mauaji ya raia kwa raia , moto kwenye masoko na baadhi ya raia kujinyonga ambapo alisema tayari serikali imeanza kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kulitaka jeshi la polisi kuweka mikakati ya kuhakikisha jamii inatoa taarifa sahihi zitakazosaidia kukabiliana na vitendo vya kihalifu.

‘’Niwaombe viongozi wetu wa taasisi za dini kuendelea kusaidia katika suala zima la malezi ya kiroho ili kujenga jamii yenye kumcha mungu , uadiliufu na ubinadamu’’ ilieleza hotuba ya Waziri Mkuu.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki Geita Mhashamu Baba Askofu Flavian Kasala ambaye ni Padre wa kwanza wa Parokia hiyo ya Bikira Maria wa Fatima tangu kuanzishwa kwake alisema, viongozi wa dni wataendelea kuiunga mkono serikali katika suala zima la sensa ya watu na Makazi kwa kuwa suala hilo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

‘’Sisi tutaendelea kuinga mkono serikali na uwepo tofauti ndogo ndogo ndizo zimewapeleka baadhi ya watu kwenye matatizo makubwa na tusiruhusu jambo hilo linaloweza kututofautisha kwenye imani zetu za kidini’’ alisema Askofu Flavian Kasala

Hafla ya kubariki Kanisa la Bikira Maria wa Fatima Jimbo la Geita ambalo ujenzi wake ulianza Januari 03, 2020 na kukamilika Machi 18, 2022 na kugharimu takriban Bilioni 1.9 iligawanyika sehemu ya kutabaruku Kanisa kwa kunyunyizia maji ya Baraka nje na ndani ya kanisa, kupaka mafuta ya krisma altare mpya pamoja na nguzo 12 na kuendelea na ibada ya misa takatifu iliyoanza saa tatu asubuhi hadi saa kumi jioni.

Aidha, kupitia hafla hiyo Dkt Angeline Mabula aliongoza harambee kwa ajili ya kuchangia ukamilishaji Samani za Kanisa ambapo kiasi cha shilingi 88,725,000/- kilipatikana kwa fedha taslim na ahadi kutoka kwa watu mbalimbali.

‘’Uwepo wa jengo hili jipya, kubwa na zuri la Kanisa la Bikira Maria wa Fatima ni ushuhuda wa kukua kwa imani ya kanisa kwa waumini wake ambapo sasa ni miaka 65 imepita tangu injili ilipoingia ukanda huu wa Altare ya kwanza ya Jimbo la Geita ilikuwa katika uwanja lililopojengwa jengo hili jipya’’ alisema Askofu Kasala
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger