Sunday, 13 March 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 14,2022

















Share:

UMBALI,FOLENI YA MAJI KISIMANI YAWACHELEWESHA WANANCHI KUFANYA SHUGHULI ZA KILIMO


Mradi wa maji kata ya Bugoji
Meneja RUWASA wilaya ya Musoma Edward Silonga akigusa mashine

Na Dinna Maningo,Musoma
WANANCHI wa kijiji cha Kaburabura kata ya Bugoji wilaya ya Musoma mkoani Mara wanalazimika kutembea umbali zaidi ya km15 kufuata maji kwenye visima vya asili vilivyopo wilaya ya Bunda na wanapofika hukuta foleni ndefu na kujikuta wakichelewa kurudi nyumbani kufanya shughuli zao za kilimo.

Hali hiyo inaelezwa kuwa inawakwamisha kufanya kazi za nyumbani na kilimo kwa wakati kwakuwa kijiji chao hakina huduma ya maji safi na salama,wanatumia maji ya madimbwi waliyoyachimba wenyewe ambayo wakati wa kiangazi hukauka.


Wakizungumza na waandishi wa habari kijijini hapo waliotembelea miradi ya maji inayojengwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira (RUWASA) katika wilaya hiyo,wananchi walieleza changamoto ya maji na kusema kuwa mradi wa maji ukikamilika utawaokolea muda wa kufanya shughuli za kilimo.


Mkazi wa kijiji hicho cha Kaburabura Mariamu Bumbasi alisema kuwa wanatembea umbali mrefu zaidi ya km 15 kwenda kuchota maji kijiji cha Kangetutya kilichopo wilaya ya Bunda na wanapofika huko hukuta watu wengi na hivyo kuchelewa kurudi nyumbani.


"Wakati wa kiangazi tunateseka sana unaamka saa tisa kwenda kutafuta maji unatembea masaa mawili ukifika huko unakuta watu wengi foleni ni ndefu mnapanga ndoo zenu kusubiri hadi ifike saa mbili za asubuhi mwenye kisima ndiyo aje afungue kisima mchote" alisema 


Mariamu alisema kuwa pamoja na umbali mrefu wanapofika kisimani wanachota maji kwa saa chache nakisha kufungwa na kufunguliwa tena saa kumi jioni jambo ambalo linawafanya wawahi maji na kuacha kufanya kazi za shamba.


"Kuna ratiba za kuchota maji saa mbili asubuhi hadi saa tano ikifika huo muda kisima kinafungwa kuchota ni saa kumi jioni yaani hata ukiwahi kisimani mtapanga foleni kusubiri huo muda ufike ndiyo mchote maji, sisi tusio na baiskeri tunatembea kwa miguu unawahi asubuhi na ndoo yako moja unakwenda kuchota maji ukienda saa 12 asubuhi kurudi ni saa nne.


"Ikifika mida ya saa nane mchana mnaanza safari kwenda kisimani mkifika mnapanga foleni saa kumi kisima kinafunguliwa wewe una ndoo moja ya maji unakaa kusubiri foleni wenzako wa karibu na kisima wana ndoo hata sita na wa baiskeri wana madumu mengi wachote wamalize ifike zamu yako uchote ndoo yako moja uondoke unachelewa kufika nyumbani kutokana na umbali na na wingi wa watu kisimani yaani akina mama tunateseka sana", alisema Mariamu


Sara Ramadhani alisema kuwa maji ya dimbwi wanayotumia si safi na salama ni machafu hali inayosababisha baadhi ya watu kupata maradhi ya tumbo na kichocho.

"Maji tunayochota kwenye madimbwi ni machafu kiasi kwamba hata uso unashindwa kunawa,hayo hayo ndiyo tunachota,ng'ombe wanakunywa humohumo mbwa,watu wanaugua matumbo,huwa tunafata maji kule Kangetutya tunalipa 2,000 kwa mwezi hiki kijiji kina changamoto kubwa ya maji hata mifugo iliwahi kufa kwa kukosa maji", alisema Sara.


Sikujua Mjora alisema kuwa kutokana na shida ya maji hufua nguo moja yakutokea nakwamba ukosefu wa maji unasababisha wasiweze kupariria kwa wakati mashamba yao ya mihogo.


"Maji ni ya shida unayochota hayatoshi ukitaka kutoka unafua nguo moja uvae utoke,pia muda ambao ungewahi shambani unawahi kwenda kupanga foleni kusubiri maji,tukipata huu mradi wa maji utatusaidia maana tutafanya kazi zote kwa wakati unaenda shambani ukitoka una raha unajua maji yapo karibu utachota, tunashindwa kwenda kupariria mihogo kisa kwenda kutafuta maji,sisi ni wakulima pia wa mahindi,viazi vitamu,mpunga na mtama", alisema Sikujua.


Diwani wa kata ya Bugoji Ibrahimundi Buruya aliishukuru serikali kuipatia kata hiyo mradi wa maji safi na salama ambao utasaidia kupunguza changamoto nakwamba tatizo la ukosefu wa maji uliwatesa kisiasa pindi walipokuwa wakijinadi kutafuta kura.

"Kijiji cha Kaburabura wameteseka sana wengine walifata maji kijiji cha Guta kilichopo Bunda umbali wa km 28, mradi wa pesa za uviko utasaidia ambapo tayali vituo 20 vimewekwa ili watu wapate maji na tuna matenki mawili maji yatasambazwa vijiji vyote kwakweli tunamshukuru sana Rais wetu mama Samia kaokoa watu wa vijijini", alisema.


Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) Edward Silonga alisema kuwa katika mwaka wa fedha  Serikali imetoa fedha Bilioni 2.199 kutekeleza miradi saba ambapo kata ya Bugoji ina matenki mawili yenye ujazo wa lita 200,000 kila mmoja itakayotoa huduma ya maji katika vijiji vya kata hiyo na kwamba miradi yote itakamilika ifikapo Juni,2022.
Share:

WANANCHI BUTIAMA WAHAMASISHWA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA MAJI

Mradi wa maji kijiji cha Biatuka
Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) wilaya ya Butiama Mhandisi Mafuru Dominico

Na Dinna Maningo, Butiama

SERIKALI imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maji lakini baadhi ya wananchi wilaya ya Butiama mkoani Mara wamelalamikiwa kuharibu Miundombinu ya maji jambo linalorudisha nyumba mendeleo ya jamii.

 Hayo yalielezwa na Meneja Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA),Mhandisi Mafuru Dominico wakati waandishi wa habari walipotembelea mradi wa maji kijiji cha Biatuka kata ya Buhemba.

Dominico alisema kuwa baadhi ya vijiji vilivyojengewa mradi wa maji,wananchi wamekata mabomba ukiwemo mradi wa maji wa Bukabwa,Kamgendi na Kitaramanka.


 "Uharibifu unapofanyika kwenye miundombinu ya maji unasababisha kuongezeka kwa gharama za matengenezo fedha ambazo zingetumika kujenga miradi mingine,ukiharibu miundombinu ni lazima utatumia fedha zingine kutengeneza mradi, fedha ambazo zingefanya kazi nyingine hii hali inarudisha nyuma maendeleo maana ukikata bomba maji yatavuja na kupotea bure itabidi utumie fedha nyingine kufanya matengenezo", alisema Dominico.

 Alisema changamoto nyingine ni baadhi ya wananchi kufanya shughuli za kilimo kwenye maeneo ya vyanzo vya maji na kuchunga mifugo jambo linaloathiri vyanzo vya maji nakusababisha kupungua kwa maji kwenye vyanzo vya maji.

 Akizungumzia fehda za mradi Mhandisi huyo alisema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2021|2022 serikali imetoa fedha kutekeleza miradi saba ya maji katika wilaya hiyo kiasi cha sh Bilioni 2;4,vijiji vilivyopewa miradi ni kijiji cha Biatika kata ya Buhemba,Nyasirori kata ya Masaba,mradi wa Uviko-19 kijiji cha Nyamikoma kata ya Kyenyari,kijiji cha Mwibagi kata ya Kyenyari,Buswahili kata ya Buswahili,Kyankoma kata ya Nyamimange na mradi wa uboreshaji wa visima vya pambu ya mikono kwa kufunga sora za umeme katika vijiji vinne ambavyo ni kijiji cha Mmazami,Kyatungwe,Masurura na Nyambili.

Dominico alisema kuwa mradi wa Biatika umetengewa fedha Milioni 663,hatua za ujenzi zinaendelea na tenki la maji lenye ujazo wa lita 135,000 limekamilika kazi iliyopo ni uchimbaji wa mitaro,ulazaji wa mabomba na kuna vituo 25 vilivyojengwa kutoa maji.

Share:

KIWANDA CHA KUTEGENEZA MAGODORO NA MABATI CHA GSM CHATEKETEKEA KWA MOTO


Kiwanda hicho kikiteketea.

KIWANDA cha kutengeneza magodoro na mabati cha GSM kilichopo Mikocheni Jijini Dar, leo kimeteketea kwa moto na kuzua taharuki eneo hilo.

Akizungumza na mwandishi wetu, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kinondoni wa Jeshi hilo, Christina Sunga amesema walipokea taarifa ya moto huo saa kumi na mbili asubuhi ambapo wao kwa kushirikiana na vikosi vingine vya uzimaji moto waliwahi eneo la tukio na kufanikiwa kuudhibiti ingawa baadhi ya mali zilikuwa zimeshateketea.

Kamanda Christina amesema moto huo endapo usingedhibitiwa mapema kulikuwa huenda ungesambaa eneo kubwa na kuhatarisha usalama wa maeneo yote yaliyozunguuka kiwanda hicho.

Kwa upande wake Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Murilo Jumanne Murilo naye alifika eneo la tukio na kumkuta Kamanda wake wa Mkoa wa Kipolisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni , RPC Ramadhani Kingai alikuwa ameshafika akiimarisha usalama na vijana wake.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto mkoa wa Kinondoni, Christina Sunga akiwaeleza jambo wanahabari waliokuwa eneo la tukio.

Kamanda Murilo alivishukuriu vikosi vyote vilivyokuwa vikishirikiana kupambana na moto huo ambao mpaka kufikia mida ya saa tano asubuhi ulikuwa ukiendelea kufuka baadhi ya maeneo ya kiwanda hicho.

Kama Murilo amesema katika janga hilo pamoja na kuteketea kwa mali za kiwanda hicho hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kujeruhiwa. 
Share:

TBS YATOA ELIMU YA UBORA WA BIDHAA KWA WANANCHI WA WILAYA YA KASULU,MLELE NA NKASI

Afisa Masoko (TBS) Bw. Mussa Luhombero akitoa elimu kuhusu majukumu ya TBS, umuhimu wa kusoma maelezo yapatikanayo kwenye kifungashio, umuhimu wa kuangalia mwisho wa muda wa matumizi katika bidhaa na namna ya kutambua alama ya ubora ya TBS kwa bidhaa zilizothibitisha kwa wanafunzi wa shule za Sekondari za Nkasi na Nkomolo wakati wa kampeni ya uelimishaji umma wilayani Nkasi - Rukwa. 

Afisa Udhibiti Ubora (TBS), Bw. Emmanuel Mushi akitoa elimu ya jinsi ya kutambua bidhaa zilizothibitishwa,umuhimu wa kusoma taarifa za mzalishaji na muda wa mwisho wa matumizi ya bidhaa husika kwa wananchi na wafanyabiara wa soko la Sofia wilayani Kasulu-Kigoma wakati wa kampeni ya elimu kwa umma.

*************************

Wananchi 23,745 kati yao 18,645 wakiwa ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika wilaya za Kasulu, Mlele na Nkasi wamepatiwa elimu kuhusu umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) sambamba na kuwahamasisha wafanyabiashara kusajili maduka ya chakula na vipodozi.

Wananchi hao walipatiwa elimu hiyo kupitia kampeni ya kutoa elimu kwa umma iliyoendeshwa na shirika kwenye wilaya hizo ambayo imelizika mwishoni mwa wiki. Kampeni hiyo ya elimu kwa umma ilifanyika katika maeneo mbalimbali kwenye ya shule za msingi na sekondari, masoko, stendi, minadani na maeneo mengine ya wazi ambapo wananchi walijitokeza kwa wingi kupata elimu na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo ubora wa bidhaa.

Afisa Masoko wa TBS, Bw Mussa Luhombero aliwakumbusha wananchi kuwa vita ya bidhaa hafifu sio ya TBS pekee, bali ni ya Taifa kwa ujumla.

“Kampeni hii imeweza kuwafikia wananchi 23,645 kati yao wanafunzi wa shule za msingi na sekondari 18,764 na wananchi 5100,” Alisema Luhombero

Luhombero aliwafafanulia wanafunzi pamoja na walimu umuhimu wa viwango katika maisha yao ya kila siku vilevile kuwafahamisha fursa ya huduma bure kwa wajasiriamali wadogo na aliwaasa kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha ubora katika jamii wanazoishi.

Vilevile aliwasisitiza wananchi kuendelea kutoa taarifa pindi wanapokutana na bidhaa zilizokwisha muda wake au wanapotilia shaka bidhaa yoyote katika soko au zilizopigwa marufuku kama vile nguo za ndani za mitumba, mafuta ya breki dot 3 na baadhi ya vipodozi.

Alitoa mwito kwa wafanyabiashara kufuatilia taratibu sahihi za usajili wa bidhaa au majengo kupitia mawasiliano waliyopewa pamoja na kutembelea ofisi ya TBS iliyopo karibu au kupiga katika kituo cha huduma kwa wateja.
Share:

WAZIRI MCHENGERWA AMTUNUKU ZAWADI YA MFANO WA MELI MAHER ZAIN


*********************

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amemkabidhi zawadi ya mfano wa meli mwanamuziki maarufu Duniani mwenye asili ya Lebanoni Maher Zain kutoka nchini Sweden anayejulikana kwa Nyimbo za Kaswida, kama sehemu ya kuhamasisha utalii hapa nchini.

Waziri Mchengerwa amemkabidhi zawadi hiyo katika tamasha la siku moja lililofanyika usiku wa Machi 12 jijini Dar es Salaam, maalum kwa ajili ya kuwezesha ununuzi wa vyombo vya usafiri na kukuza kipato kwa walemavu wasio ona wanaolelewa katika kituo cha Vimdat kilichoko Kisemvule jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mamia ya mashabiki wake waliofurika kuburidika na nyimbo zake kabla ya kuhitimisha tamasha hilo, mwanamuziki huyo maarufu wa Qaswida duniani aliyevalia tisheti yenye maneno (Tanzania Unforgettable) amesema uwepo wake Tanzania ni jambo asiloweza kulisahau Maishani mwake kutokana na uzuri wa Tanzania na ukarimu wa watu wake.

“Naishukuru Serikali ya Tanzania na ninakupongeza Mheshimiwa Waziri kukuona hapa na wewe umekuja kuburudika na nyimbo zangu kweli Tanzania siyo ya kusahulika” alisme Maher

Akizungumza kwa niaba ya waandaji wa tamasha hilo Mwenyekiti msaidizi Yousra Alnahd amesema tamasha hilo lililopewa jina la Maher Zain in Tanzania pamoja na mapato ya tamasha hilo kulenga ununuzi wa vyombo vya usafiri kwa ajili ya kituo hicho, pia waandaji walilenga kuitangaza utalii kama sehemu ya kumuunga mkono Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu katika kuitangaza Tanzania na vivutio vyake.
Share:

Saturday, 12 March 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MACHI 13,2022




Magazetini leo Jumapili March 13 2022








Share:

KADIO AAGIZA UONGOZI WA MFUKO WA FARAJA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI KUZINGATIA KATIBA NA MWONGOZO WA MFUKO HUO


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Christopher Kadio ambaye pia ni Mlezi wa Mfuko wa Faraja akizindua Mfuko wa Faraja wa Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi leo, katika ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Christopher Kadio pamoja na Mwenyekiti wa Mfuko wa Faraja,Emmanuel Kayuni ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wakionesha nakala ya Katiba ya Mfuko wa Faraja wa Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Watumishi ambao pia ni Wanachama wa Mfuko huo leo.
Katibu Mkuu, Christopher Kadio akikabidhi nakala ya Katiba ya Mfuko wa Faraja kwa baadhi ya Watendaji na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Fungu 51 ambao pia ni wanachama wa Mfuko wa Faraja leo katika ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio akizungumza kwenye Uzinduzi wa Mfuko wa Faraja wa Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Muda wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

……………………….

Na Mwandishi wa MoHA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio ambaye pia ni Mlezi wa Mfuko wa Faraja ameagiza uongozi wa mfuko wa faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuzingatia katiba na mwongozo wa mfuko huo kwenye ukusanyaji wa mapato, matumizi ya fedha za mfuko huo na huduma kwa wanachama wake.

Akizungumza na uongozi wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi amewaelekeza kuingiza mchango wa mwajiri kwenye bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2022/23 ili kuhudumua wanachama wa mfuko huo. Pia amewaagiza kufanya uchaguzi wa Uongozi wa kudumu wa mfuko ndani ya mwaka huu wa fedha.

“Mimi kama Mlezi wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi nawasisitiza kuzingatia katiba na mwongozo wa Mfuko hii pamoja na kuingiza mchango wa nwajiri kwenye bajeti ya Wizara” amesema

Christopher Kadio alisema hayo leo kwenye uzinduzi wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi uliofanyika katika ukumbu wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto, jijini Dodoma.

Aidha amewashauri watendaji na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kujiunga na Mfuko huo kwani faida zake ni nyingi na utawawezesha wafanyakazi kiuchumi na kuongeza tija kwenye majukumu yao.

Katibu Mkuu Christopher Kadio amesema kwamba Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni kama sehemu ya bima ya dharura na kwamba utasaidia kupunguza msongo wa mawazo wa changamoto za masuala ya dharura ya kijamii kama kuuguliwa na kufiwa.

“Licha ya kwamba kujiunga na Mfuko ni hairi ya mtu,lakini kwa faida nilizozieleza ni ushauri wangu kuwa watu wote wajiunge kwa kuzingatia faida nilizozieleza, Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu” alisema.
Share:

WAGENI KUTOKA NCHI MBALIMBALI WAENDELEA KUMIMINIKA KWENYE MABANDA YA TANZANIA MAONESHO UA KILIMO NA MAZINGIRA NCHINI QATAR


Johnson Elibarick Kaaya ni mtaalam wa kilimo kutoka Taasisi ya Bodi ya Korosho Tanzania, Bodi ya korosho ni taasisi ya umma iliyoanzishwa chini ya sheria 18 ya mwaka 2009 na kanuni zake za mwaka 2010 yenye jukumu ya kusimamia tasnia zima ya maendeleo ya zao la korosho nchini Tanzania.Diana Fatukubonye ni Export Manager kutoka Bodi ya Kahawa (TCB).Bodi ya kahawa ni Shirika la umma lenye mamlaka ya kusimamia tansia ya kahawa nchini Tanzania.Uzalishaji wa kahawa kwa sasahivi ni tani 75,000 ya kahawa safi na tuko kwenye mkakati wa kuongeza uzalishaji kufika tani 300,000 mwaka 2025 

NEMC pamoja na washiriki wengine kutoka Taasisi mbalimbali walioshiriki maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar. Natural Shine Trader wanajishughulisha na vipodozi asili, wanatengeneza sabuni za aina mbalimbali, mafuta ya nywele na massage pamoja na kuchakata mwani na kutoa bidhaa mbalimbali hivyo ameshiriki katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar kwa ajili ya kijitangaza, kutafuta masoko na kujifunza kutoka mataifa yaliyoendelea. TAHA ( Mazao ya mbogamboga, Matunda, Maua na Viungo) wameshiriki katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar kwa ajili ya kuwatafutia wakulima masoko pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania kwenye Sekta ya Kilimo.. Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ( CPB) wameshiriki maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar kwa ajili ya kutimiza majukumu yao ya GAPEX ( General Agricultural Produce Export) ambalo ndo jukumu kuu la Bodi katika kutangaza nafaka na mazao mchanganyiko kwenye masoko ya nje. Hapo juu ni Bodi ya Chai wameshiriki maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar kwa ajili ya kutangaza chai ya Tanzania na kutafuta masoko Kituo cha Uwekezaji Tanzania wapo wanatangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini Kwetu, wananadi miradi inayotafuta wabia na wanavutia wawekezaji kuja nchini kuwekeza. 

Wizara ya Mambo ya Nje kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar ndio waratibu wa ushiriki wa Tanzania katika maonesho ya tisa ya Kilimo na ya tatu ya Mazingira jijini Doha nchini Qatar. Diana Fatukubonye ni Export Manager kutoka Bodi ya Kahawa (TCB).Bodi ya kahawa ni Shirika la umma lenye mamlaka ya kusimamia tansia ya kahawa nchini Tanzania.Uzalishaji wa kahawa kwa sasahivi ni tani 75,000 ya kahawa safi na tuko kwenye mkakati wa kuongeza uzalishaji kufika tani 300,000 mwaka 2025.
Share:

TRA YAHIMIZA WAUZAJI WA VINYWAJI KUHAKIKI VINYWAJI KWA KUTUMIA APP "HAKIKI STEMPU"


Balozi wa kodi TRA Bw. Edward kumwembe akifanya zoezi la hakiki stamp. Balozi wa kodi TRA Bw. Edward kumwembe akitoa elimu ya hakiki stempu Mkoani manyara.Afisa wa TRA Bw. Chama Siriwa akitoa elimu ya kodi 

***************** 

Wafanyabiashara wa Vinywaji pamoja na watumiaji wametakiwa kuwa na utaratibu wa kuhakiki Vinywaji kwa kutumia app maalumu ya Hakiki stempu ili kutambuwa bidhaa feki sokoni ambayo zinaweza kuleta athari kwa mlaji. 

Akizungumza mjini Babati Mkoani Manyara Balozi wa Kodi Edward Kumwembe amesema application ya Hakiki stempu inauwezo wa kutambua uhalali wa bidhaa za Vinywaji ambazo zipo sokoni ambapo mtumiaji atapaswa kuwa na Application hiyo katika simu janja na kufanya uhakiki kwa kutumia simu yake kama iwapo bidhaa hiyo inafaa kwa matumizi ya binadamu. 

Kumwembe amesema "kuna app maalumu ambayo inapatikana katika hizi simu za smartphone ambazo Zina application au maarufu watu wanaita App ambayo inahakiki ubora wa Vinywaji vyako, ambayo inahakiki kwa njia mbili wewe ukiwa ni mnunuaji kutoka sehemu nyingine unaweza inahakiki Vinywaji vyako lakini vilevilie wewe unapomuuzia mtu mwingine mteja naye anaweza kuhakiki kwasababu wakati mwingine unaweza kununua kitu ambacho hakina ubora lakini siyo kosa lako" . 

Aidha Kumwembe amesema lengo la kuhakiki ubora wa bidhaa za Vinywaji ni kwa sababu kuna aina nyingi za Vinywaji hivyo siyo rahisi kufahamu ubora wa Vinywaji hivyo. 

Amesema kwa kutumia mfumo huo wa app utaweza kupata taarifa sahihi kuhusu ilipotoka bidhaa,ilipotengenezwa,na lini itaisha muda wake wa matumizi hivyo kumfanya mlaji wa bidhaa husika kuwa salama. 

Kwa Upande wake muuzaji wa Vinywaji mbalimbali kutoka Mjini Babati Bw.Naingwa ameishukuru mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya kutumia application hiyo inayoweza kuhakiki ubora na uhalali wa Vinywaji na kwamba itawasaidia kuepuka kununua bidhaa feki. 

"Application hii inafaida nyingi kwa sisi wafanyabiashara hasa pale tunapo kwenda kununua Vinywaji kwani itatusaidia kutambuwa Vinywaji feki pamoja na kufahamu ubora wa Vinywaji hivyo ili kumlinda mteja"alisema. 

Hata hivyo maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka Makao Makuu wapo Mkoani Manyara kwa siku kumi katika kampeni ya walioiita Mlango kwa mlango (Door to door) inayolenga kutoa elimu kwa Wananchi na wafanyabiashara juu ya matumizi sahihi ya EFD machine,matumizi ya Hakiki stempu inayolenga kutambuwa Vinywaji feki sokoni na msisitizo wa kutoa na kudai risiti baada ya kuuza au kununua bidhaa.
Share:

Friday, 11 March 2022

WADAU WA ELIMU WATAKIWA KURIPOTI MATUKIO YA UKATILI




Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala limewaomba wadau mbalimbali wa elimu kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia yanayowakumba wanafunzi wakati wakiwa mashuleni au majumbani kwao.

Wito huo umetolewa na Kamanda wa polisi  Mkoa wa Ilala ACP DEBORA MAGILIGIMBA  leo tarehe 10/03/2022 Katika kikao cha  wakuu wa shule za msingi na sekondari, na wadau wa elimu wa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam katika ukumbi wa Anatogro - Dar es salaam ambapo amewaomba kutenga muda wa kuzungumza na watoto ili kubaini ukatili wanaofanyiwa na wakaripoti katika sehemu husika ikiwemo madawati ya jinsia na watoto ambayo yapo katika wilaya zote za kipolisi mkoa wa Ilala. 

 "Chukueni muda wa kuongea na hawa watoto na muripoti matukio hayo katika sehemu husika ili kubaini aina ya ukatili wanaofanyiwa na kupata suluhisho ya matatizo hayo.

Ukatili huu unapelekea kumuathiri mtoto kisaikolojia na pia kupelekea kuathiri maendelea ya mtoto shuleni",amesema

Kikao hicho kiliandaliwa na chama cha walimu Tanzania halmashauri ya jiji la ilala na kuhudhuriwa na waratibu kata elimu sambamba na wakuu wa shule za sekondari na walimu wakuu wa shule za msingi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger