Wednesday, 2 March 2022

BODI MPYA YA OSHA YAZINDULIWA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Usimamizi ya OSHA (hawapo pichani) wakati wa hafla za uzinduzi wa bodi hiyo iliyofanyika Jijini Arusha. (Kulia kwake) ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Jamal Katundu.Kushoto kwa Waziri ni Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Adelhelm Meru na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda. Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Jamal Katundu, akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Usimamizi wa OSHA wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Arusha. Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya OSHA Dkt. Adelhelm Meru (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Bodi wakati wa tukio la uzinduzi wa bodi hiyo jijini Arusha iliyozinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako. Wajumbe wa Bodi ya Usimamizi ya OSHA wakiwa katika kikao kifupi pamoja na wawekezaji wa kampuni ya kuzalisha mbegu za mboga mboga na matunda ya Enza Zaden Africa Ltd wakati wa ziara ya wajumbe hao wakiambatana na viongozi wa Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kutembelea kampuni hiyo kwa lengo la kuangalia jinsi kampuni hiyo inavyoendesha shughuli zake kwa kuzingatia taratibu za usalama na afya mahali pa kazi. Baadhi ya wajumbe wa bodi ya Usimamizi ya OSHA wakiwa katika kikao cha uzinduzi wa bodi hiyo ambayo ilizunduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako jijini Arusha.

**********************

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, amezindua Bodi ya Usimamizi ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) na kuwataka wajumbe wapya wa Bodi hiyo kutumia uzoefu wao kuisaidia Taasisi hiyo kutimiza malengo yake.

Waziri huyo mwenye dhamana ya Masuala ya Kazi na Ajira nchini amesema malengo ya serikali ya awamu ya sita ni kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati wa juu kutoka katika uchumi wa kati wa chini wa sasa ambapo alisema ili kufanikisha azma hiyo ni lazima kuhakikisha kwamba maeneo ya kazi yanakuwa salama na rasilimali watu yenye afya njema.

“Nadhani sote tunaona jinsi Rais wetu anavyofanya jitihada mbali mbali zinazolenga kuvutia uwekezaji mkubwa ndani ya nchi yetu ili kukuza uchumi ambapo kupitia uwekezaji huo ajira nyingi zitazalishwa na ili kuwepo na uzalishaji endelevu tunahitaji watu wenye afya njema pamoja na mazingira salama ya kufanyia kazi na hapo ndipo mchango wenu unapohitajika,” alisema Prof. Ndalichako.

Aidha, aliwaeleza wajumbe hao wa Bodi mpya baadhi ya majukumu yao ya msingi ikiwemo kushauri kuhusu uhuishaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo mbali mbali endapo inakuwa imepitwa na wakati sambamba na kufuatilia mwenendo mzima wa utendaji wa Taasisi husika kwa kipindi chote cha miaka mitatu ambacho Bodi hiyo itahudumu.

Waziri Ndalichako ameitaka Bodi hiyo mpya kuisimamia Taasisi ya OSHA ipasavyo ili iweze kupata mafanikio zaidi ya ambayo yamepatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, Taasisi ya OSHA imepata mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2016/2017-2021/2022) ikiwemo kuongeza idadi ya maeneo ya kazi yaliyosajiliwa na OSHA kutoka 4,003 hadi 23, 239 pamoja na idadi ya kaguzi za Usalama na Afya mahali pa kazi kutoka 96,000 hadi 784,000.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye aliambatana na Waziri Ndalichako katika uzinduzi huo, Prof. Jamal Katundu, amewapongeza wajumbe kwa kuaminiwa na kuteuliwa na kuwaomba kufanya kazi kwa umahiri katika kuisimamia Taasisi ya OSHA.

 

“Ninapohitimisha salumu zangu kwenu naomba niwaachie changamoto moja ambayo ni kufikiria kuacha alama katika Taasisi ya OSHA pindi muda wenu utakapokwisha,” amesema Prof. Katundu.

 

Mtendaji Mkuu wa OSHA ambaye kwa mujibu wa muundo wa Bodi hiyo ndiye Katibu wa chombo hicho, amesema Bodi hizo zimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Taasisi anayoiongoza na hivyo kupitia Bodi hiyo iliyozinduliwa, Taasisi yake itaendelea kukua na kupata mafanikio zaidi.

 

Akitoa shukrani kwa niaba ya wajumbe wenzake, Mwenyekiti wa Bodi ambaye ameteuliwa kwa kipindi cha pili kuiongoza Bodi hiyo, Dkt. Adelhelm Meru, amesem yeye pamoja na wajumbe wenzake wana ari kubwa ya kufanya kazi hivyo watajituma katika kutekeleza majukumu yao pamoja na kuzingatia weledi.

 

Aidha, baada ya tukio hilo la uzinduzi wajumbe wametembelea moja ya mashamba ya mbegu za mboga mboga na matunda ambayo ni miongoni mwa maeneo ya kazi yanayosimamiwa na OSHA ambapo mwakilishi wa Kampuni hiyo ya Enza Zaden Africa Ltd iliyotembelewa, Bw. Gerald Matowo, ameeleza kufurushwa kwao na ziara hiyo ya viongozi wa Wizara, Bodi pamoja na watendaji wa OSHA.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MACHI 2,2022















Share:

News Alert : HAYA HAPA MAJINA 1143 WALIOITWA KWENYE USAILI WA ANWANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI MANISPAA YA SHINYANGA

Hii hapa orodha ya majina ya waombaji wa nafasi ya kazi ya Ukusanyaji wa taarifa za anwani za makazi na Postikodi Manispaa ya Shinyanga waliokidhi vigezo kufika kwenye usaili siku ya Alhamisi na Ijumaa tarehe 03.03.2022 na 04.03.2022 katika ofisi ya Kata ya Ndembezi, Ngokolo na kata ya Mjini

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA ANWANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI

TANGAZO LA USAILI ANWANI ZA MAKAZI.pdf



Share:

Tuesday, 1 March 2022

WIZARA YA NISHATI NA DP WORLD YA DUBAI ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (kulia) na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya DP World ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bandari, Bohari na Eneo Huru la Kibiashara – Dubai, Sultan Ahmed Bin Sulayem (kushoto) wakiwa katika zoezi la kutia saini hati za makubaliano ya ushirikiano kuendeleza miundombinu ya kupokea na kuhifadhia mafuta na gesi itakayojengwa nchini Tanzania.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (kulia) na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya DP World ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bandari, Bohari na Eneo Huru la Kibiashara – Dubai, Sultan Ahmed Bin Sulayem (kushoto) wakipongezana mara baada ya kutia saini hati za makubaliano ya ushirikiano kuendeleza miundombinu ya kupokea na kuhifadhia mafuta na gesi itakayojengwa nchini Tanzania.

**********************

Wizara ya Nishati na kampuni ya DP World ya Dubai zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kuendeleza miundombinu ya kupokea na kuhifadhia mafuta na gesi itakayojengwa nchini Tanzania.

Utiaji saini huo umefanywa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya DP World ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bandari, Bohari na Eneo Huru la Kibiashara – Dubai, Sultan Ahmed Bin Sulayem.

Mradi uliolengwa katika Hati ya Makubaliano husika ni kuendeleza miundombinu ya kitaifa iliyo bora na ya kisasa ya kupokea na kuhifadhi mafuta na gesi ambayo itatumika katika kuboresha sekta ya mafuta na gesi nchini na katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki.

Tukio hili lilifanyika tarehe 27 Februari, 2022 katika Kikao cha Kibiashara kilichofanyika huko Dubai – Umoja wa Falme za Kiarabu.
Share:

NAIBU WAZIRI KHAMIS ASHIRIKI MKUTANO WA UNEA 5 NAIROBI


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akizungumza aliposhiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEA 5) unaofanyika jijini Nairobi nchini Kenya.


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis (kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Simbachawene wakishiriki ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEA 5) unaofanyika jijini Nairobi nchini Kenya.


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis (kulia) akishiriki ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEA 5) unaofanyika jijini Nairobi nchini Kenya.

**********************

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ameshiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEA 5) unaofanyika jijini Nairobi nchini Kenya.


Katika sherehe za ufunguzi wa mkutano huo Mhe. Khamis aliwasilisha ujumbe maalumu wa Tanzania kuhusu mazingira ambapo alieleza jitahada za Tanzania ilizozichukua katika kukabilina na uharibifu wa mazingira.


Alizitaja jitihada hizo kuwa ni pamoja na kupambana na uharibifu wa mazingira unaotokana na mifuko ya plastiki akisema kuwa ili kukabiliana na changamoto hiyo Tanzania imechukua hatua za kupiga marufuku uzalishaji, uingizaji na matumizi ya mifuko hiyo.


Pia, Naibu waziri huyo aliongeza kwa kusema kuwa mwaka 2019 Tanzania ilitunga Kanuni kwa ajili ya utekelezaji wa katazo la mifuko ya plastiki huku akieleza kuwa ili kufanikiwa unahitajika ushirikiano madhubuti wa kimataifa ikiwemo kuwa na sera ya pamoja na hatua madhubuti za pamoja za kuhakikisha dunia inakuwa salama.


Alisema katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, Tanzania imeendelea kutekeleza wajibu wake kama ilivyojieleza katika Mchango wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (NDC) pamoja na Mkakati wa Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi (NCCRS) wa mwaka 2021-2026.


Naibu Waziri Khamis alisema kuwa mbali ya jitihada hizo pia, Tanzania imeendelea kuimarisha uwezo wa nchi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.


Inaelezwa kuwa takriban mataifa 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa (UN) ambayo yamepitisha maazimio yanayolenga kubuni makubaliano mwafaka ya kutokomeza taka za plastiki kwa kupunguza matumizi yake kutoka vyanzo vyake hadi baharini.

Aidha, wajumbe wa mkutano huo wanatarajia kufikia maamuzi ya pamoja katika hatua za mwanzo za kukabiliana na uchafuzi wa mazingira unaotokana na mifuko ya plastiki ambayo itajwa kama chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira.


Kwa mujibu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), zaidi ya chupa za plastiki milioni moja hununuliwa kila dakika kote ulimwenguni kwa matumizi ya maji ya kunywa huku mifuko ya plastiki zaidi ya trilioni 5 hutumiwa kila mwaka duniani.


Mkutano wa UNEA 5 uliofunguliwa Februari 28 unatarajiwa kuhitimishwa Machi 2, 2022 huku ukijumisha wajumbe mbalimbali wakiwemo mawaziri na wadau mbalimbali wa mazingira duniani.

Share:

NAIBU WAZIRI SAGINI ATEMBELEA VITUO VYA POLISI NA MAKAZI YA ASKARI YALIYOLALAMIKIWA BUNGENI, ZANZIBAR.


NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Mwantumu Mdau Haji pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadidi alipotembelea Kituo cha Polisi cha Makunduchi, ikiwa sehemu ya ziara yake Zanzibar.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini akizungumza na Maafisa wa Polisi na wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, kwenye kikao cha pamoja kilichofanyika leo katika ukumbi wa Chuo cha Polisi Zanzibar baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili visiwani humo.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini akikagua ujenzi wa Vituo vya Polisi vipya vya Kizimkazi Dimabani, Daraja C pamoja na Kituo cha Polisi Mkokotoni, Daraja A Kaskazini Unguja leo, ikiwa sehemu ya ziara yake visiwani Zanzibar.

.................................................................

Na Mwandishi wetu, MoHA.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini ametembelea Ofisi za Makamanda wa Polisi wa Mkoa na Wilaya, Vituo vya Polisi na Makazi ya askari wa Jeshi la Polisi Zanzibar, vilivyolalamikiwa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Zanzibar, katika Bunge lililopita. Naibu Waziri Sagini ametembelea maeneo hayo, ili kufahamu changamoto, mapungufu waliyonayo pamoja na kupata suluhisho ya changamoto hizo.

Vituo vya Polisi pamoja na Makazi ya Askari wa polisi Zanzibar yaliyolalamikiwa na kutembelewa na Naibu Waziri Sagini ni Kituo cha Polisi Uzi, Kituo cha Polisi Bet-Ras, Kituo cha Kidongo-Chekundu, Kituo cha Polisi Mwanakwerekwe, Kituo cha Polisi Chukwani, Kituo cha Polisi Mwembemadafu pamoja na Kituo cha Polisi na Makazi ya Polisi Makunduchi Zanzibar.

“Katika Bunge lililopita, lilikuwa na maswali mengi sana ya Wabunge wanaowakilisha Ubunge kutoka Zanzibar yalioashiria kwamba pana mambo yanahitaji kufuatiliwa na Wizara yetu hususan kwenye vituo vya polisi, makazi ya askari, ofisi za makamanda wa Polisi” Sagini alisema .

Naibu Waziri Sagini alisema hayo leo, Februari 28, 2022 wakati akizungumza na Maofisa wa Polisi pamoja na wa Idara ya Uhamiaji katika ukumbi wa Chuo cha Polisi Zanzibar, baada ya ziara yake ya siku mbili. Hata hivyo Naibu Waziri Sagini amesema kuwa baada ya kupitia Vituo hivyo vya Polisi pamoja na makazi ya askari Wizara ya Mambo ya Ndani itajipanga pamoja na Jeshi la Polisi kuzifanyia kazi hatua kwa hatua changamoto hizo na kuboresha miundombinu hiyo.

“Vituo vyote vilivyolalamikiwa vitafanyiwa kazi, vituo vyote vilivyokuwa vimefungwa tayari vimerejeshwa kwenye kutoa huduma” alisema.

Naibu Waziri Sagini pia amelipongeza Jeshi la Polisi kwa ujenzi wa Vituo vipya vya Polisi vilivyojengwa Unguja Zanzibar.

Aidha akizungumza na Maofisa wa Polisi pamoja na wa Idara ya Uhamiaji, Naibu Waziri amewataka Viongozi wa Polisi Kamsheni ya Zanzibar wasione ‘muhali’ huruma kuwawajibisha na kuwaadhibu askari wanaokiuka maadili ya kazi wa cheo chochote. Amesema Jeshi la Polisi lina wimbo wa maadili mzuri sana na ametaka kila askari kuyazingatia maneno ya wimbo huo katika utendaji wake wa kazi.

“ Nimekuja kuwakumbusha juu ya wajibu wenu. Polisi ndio chombo cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinachosimamia utekelezaji wa Sheria kwahiyo, Wizara inataka kuwakumbusha wajibu wenu kwa kuzingatia miiko ya maadili na Sheria inayosimamia Jeshi la Polisi”

Pia amelitaka Jeshi la Polisi Zanizbar kuendelea kufanya doria na kuimarisha utendaji kazi wao kwenye maeneo hatarishi ili watalii wazidi kuingia Zanzibar na kupelekea kukuza uchumi.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEBRUARI 01,2022


Tanzania, Kenya, Uganda zatarajia mvua kubwa
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger