Friday, 11 February 2022
Thursday, 10 February 2022
WAENDESHA BODABODA, BAJAJI NA WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUJIUNGA NA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII 'NSSF'
Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa wajasiriamali katika Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umewashauri Waendesha bodaboda,bajaji na Wajasiriamali wajiunge na kujiwekea akiba kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii wa NSSF kwa ajili ya kujiwekea akiba ya baadae, kutimiza malengo yao na kuweza kupata Pensheni ya uzeeni.
Rai hiyo imetolewa Februari 9,2022 na Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance wakati akitoa elimu kwa waendesha bodaboda, bajaji na wafanyabiashara wa Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuwaeleza namna ya kufanya biashara kwenye mfumo rasmi pamoja na fursa zinazotolewa na taasisi mbalimbali ikiwemo NSSF.
Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance alisema NSSF imefungua milango kwa ajili ya Wajasiriamali, wakulima,wavuvi na watu wote waliojiajiri wenyewe hivyo kuwaomba wajiunge na NSSF ili kupata huduma mbalimbali ikiwemo mikopo na kujiwekea akiba ya baadae.
"Mjasiriamali, mkulima,mvuvi na wote waliojiajiri wenyewe NSSF imewafikia, njoo ujiunge na ujiwekee akiba kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii wa NSSF kwa ajili ya kujiwekea akiba ya baadae, kutimiza malengo yako na pia kuweza kupata pension ya uzeeni",alisema Janeth.
"Pia kwa wajasiriamali wenye viwanda vidogo na vya kati kuna fursa ya mikopo ambayo mikopo hii inalenga kuchochea kukua na kuongezeka kwa viwanda vya ndani. Mikopo hii itawasaidia kukuza mtaji ,kununua malighafi na kununua mashine na vitu vitakavyotumika katika uzalishaji kwenye viwanda husika",alieleza.
Alifafanua kuwa Mikopo hii inatolewa kwa ushirikiano kati ya NSSF,SIDO,VETA, NEEC na AZANIA Bank.,Mwanachama anaweza kunufaika na mkopo huo kuanzia shilingi 8,000,000/= mpaka shilingi 500,000,000/= kulingana na uhitaji nawa uwezo wake wa kurudisha mkopo, Marejesho ya mkopo huu ni kuanzia mwaka 1 mpaka 7 kulingana na kiwango huku riba yake ikiwa 13%.
"Ikumbukwe kuwa kujiunga na NSSF ni bure ambapo Kima cha chini cha kujichangia kwa mwezi ni shilingi 20,000/= au zaidi kulingana na kipato. Mwanachama anaweza kuweka mara moja kwa mkupuo au kuweka kidogokidogo kila siku au kila wiki ili kufikia au kuzidi kiwango hicho kulingana na malengo au kipato cha mwanachama",alieleza Janeth.
"Kutolewa kwa mikopo yote hii hakuta angalia kiasi mwanachama alicho jihifadhia kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF. Mwanachama anaweza kujichangia pindi atakapopata control namba yake(kumbukumbu namba) kwa watoa huduma wote wa fedha kama Mpesa, Tigo pesa, Airtel Money, Halo pesa pia kwa Mawakala wote wa huduma za Benk",aliongeza.
Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa wajasiriamali katika Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga Jumatano Februari 9,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Uandikishaji Mwandamizi NSSF Mkoa wa Shinyanga, Rose Robert akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa wajasiriamali katika Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga.
Afisa Uandikishaji Mwandamizi NSSF Mkoa wa Shinyanga, Rose Robert akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa wajasiriamali katika Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga.
Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga.
Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga.
Afisa Uandikishaji Mwandamizi NSSF Mkoa wa Shinyanga, Rose Robert akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga.
Afisa Uandikishaji Mwandamizi NSSF Mkoa wa Shinyanga, Rose Robert akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga.
Waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga wakifuatilia elimu iliyokuwa inatolewa
Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance (katikati) akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Breaking News : SERIKALI YAYAFUNGULIA MAGAZETI YA MWANAHALISI, MAWIO, MSETO NA TANZANIA DAIMA
"Agizo la Rais ni Sheria, Leo hii natoa Leseni kwa Magazeti manne ambayo ni Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima.
Mama kasema Kazi Iendelee tuanze ukurasa mpya" - Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza na wahariri wa vyombo vya Habari leo Alhamisi Februari 10,2022
WAZIRI GWAJIMA AZINDUA KITUO CHA WATOTO KATIKA SOKO LA MIRONGO MWANZA
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (wa tano kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto kilichopo katika soko la wafanyabiashara wadogo Mirongo jijini Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amezindua rasmi Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo kilichopo katika soko la wajasiriamali Mirongo jijini Mwanza na kutoa rai kwa uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kukisimamia vyema Kituo hicho.
Uzinduzi huo ulifanyika Februari 09, 2021 ambapo ujenzi wa Kituo hicho ulienda sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya Soko la Mirongo ambayo ni pamoja na vyoo, mitaro na mabanda mawili ya kufanyia biashara na ujenzi wa visimba ambao unaendelea hivyo kuondoa adha kwa wajasiriamali katika soko hilo ambalo ni maarufu kwa bidhaa za mbogamboga na matunda.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Gwajima alisema Serikali inaandaa mfumo utakaosaidia malezi na makuzi kwa ajili ya watoto hatua itakayosaidia kuwakinga na vitendo vya ukatili wa kijinsia na hivyo kupingeza hatua ya ujenzi wa kituo hicho katika soko la Mirongo kwani kitasaidia jitihada za malezi bora kwa watoto.
Naye Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi alisema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Kituo hicho, Serikali itasaidia upatikanaji wa waalimu walezi watakaokuwa na jukumu la uangalizi wa watoto watakaokuwa kituoni hapo pindi wazazi wao watakapikuwa kwenye shughuli za biashara.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema utafiti uliofanywa na shirika hilo ulibaini kuwa asilimia zaidi ya 60 ya wafanyabiashara wadogo masokoni ni wanawake na wanakumbana na changamoto za malezi ya watoto wanapokuwa kwenye biashara na hivyo kuja na wazo la ujenzi wa Kituo hicho ili kusaidia kukabiliana na changamoto hiyo.
Maboresho hayo yaligharimu shilingi milioni 88 ambapo shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo I4IF, UKAid, IrishAid limetoa shilingi milioni 60 huku Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikitoa shilingi Milioni 20.
Miundombinu bora katika soko la Mirongo itasaidia wajasiriamali kufanya biashara zao katika mazingira salama na kukuza biashara zao huku Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto kikisaidia kuimarisha usalama wa watoto pindi wazazi wao wanapokuwa kwenye biashara huku pia akina mama wanaonyonyesha wakiwa na eneo maalum la kunyonyeshea.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo jijini Mwanza.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (katika) akimpongeza Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kulia) kwa kusaidia ujenzi wa Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo ambapo shirika lake kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo limetoa shilingi milioni 68 na Halmashauri ya Jiji la Mwanza Milioni 20 na kusaidia uboreshaji wa miundombinu katika soko la wajasiriamali Mirongo pamoja na ujenzi wa Kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi (katikati) akizungumza kwenye uzinduzi wa Kituo hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (hayuko pichani).
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto KIVULINI, Yassin Ally akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo hicho ambapo alisema kitasaidia pia wanawake wajasiriamali katika soko la Mirongo kupata eneo maalum kwa ajili ya kunyonyeshea.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (wa kwanza kushoto) pamoja na viongozi mbalimbali jijini Mwanza akizindua rasmi Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo jijini Mwanza.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (katikati) akimsaidia kubembea mmoja kati ya watoto walio katika Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo kilichojengwa katika soko la wajasiriamali Mirongo jijini Mwanza. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya Nyamagana Amina Makilagi na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI Yassin Ally.
Baadhi ya akina mama wajasiriamali katika soko la Mirongo jijini Mwanza wakiwa na watoto wao katika Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo wakati wa uzinduzi rasmi wa Kituo hicho.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (katikati) akiwasili katika viunga vya soko la Mirongo kwa ajili ya uzinduzi wa Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya Nyamagana Amina Makilagi na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI Yassin Ally.
Wanawake wajasiriamali katika soko la Mirongo wakimkaribisha Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (hayuko pichani).
Wanachi waliojitokeza kwa ajili ya uzinduzi wa Kituo hicho.
Wakazi wa jiji la Mwanza wakishuhudia uzinduzi wa Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima pia alikutana na Kamati za MTAKUWWA ngazi za Mitaa katika jiji la Mwanza na kuwahimiza wajumbe Kamati hizo kuwajibika ipasavyo ili kuzuia vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kutokea katika Mitaa yao.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wajumbe wa Kamati za MTAKUWWA ngazi za Mitaa katika jiji la Mwanza.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (hayuko pichani) pia alikutana na wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA ngazi ya Mkoa Mwanza (pichani) kwa ajili ya kupeana mikakati mbalimbali ya kupambana na Ukatili wa Kijinsia ambapo aliipongeza Kamati hiyo kwa kufanya jitihada kubwa kupamabana na Ukatili wa Kijinsia.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima alikutana pia na viongozi wa Machinga Mkoa Mwanza na kuagiza viongozi wa Serikali mkoani Mwanza kukutana na makundi yote mawili (Shirikisho la Machinga Tanzania na Muungano wa Machinga Mkoa Mwanza) kuja na mikakati ya kupata shirikisho moja la linakalowaunganisha machinga wote.
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Ngusa Samike akizungumza kwenye kikao baina ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (hayuko pichani) na wajumbe wa Kati ya MTAKUWWA ngazi ya Mkoa Mwanza.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima pia alitembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi (CDTTI) na kuwahimiza wanafunzi wa Chuo hicho kuwa wabunifu na kutumia vyema taaluma wanayoipata kujiajiri na kuajiriwa ili kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na uongozi na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi (CDTTI).
Tazama Video hapa chini
Wednesday, 9 February 2022
RAIS SAMIA AELEZA ANAVYOISIKIA SAUTI YA MAGUFULI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto, wakiondoa kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Barabara ya mzunguko wa nje katika mji wa Dodoma itakayotoka Ihumwa-Matumbulu-Nala-Veyula-Ihumwa Kilometa 112.3 Hafla hiyo imefanyika kwenye Sherehe zilizofanyika leo tarehe 09 Februari, 2022 katika eneo la Veyula Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi katika Sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Ujenzi wa Barabara ya mzunguko wa nje katika mji wa Dodoma itakayotoka Ihumwa-Matumbulu-Nala-Veyula-Ihumwa Kilometa 112.3 katika Sherehe zilizofanyika katika eneo la Veyula Jijini Dodoma.
Na Dotto Kwilasa-Malunde 1 Blog-DODOMA.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma yenye urefu wa Kilomita 112.3 huku akieleza namna anavyoisikia sauti ya mtangulizi wake hayati Dkt.John Magufuli akimtaka kuendeleza miradi mingine yote aliyoiacha .
Rais Samia amesema atahakikisha anaiendeleza miradi yote iliyoachwa na Dk. John Pombe Magufuli na kuwataka wananchi kuitunza.
Kauli hiyo ameitoa leo Februari 9,2022 wakati akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa arabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma( km 112.3).
Rais Samia amesema siku ya leo toka asubuhi anasikia sauti ya mtangulizi wake ikimueleza kuhusu miradi aiyoiacha ikiwemo ya kuhamia Dodoma na mingine ikiwemo huu wa barabara ya mzunguko wa nje Dodoma.
"Ndugu zangu siku kama ya leo mimi mwenzenu toka asubuhi nasikia sauti ya mtangulizi wangu Dkt John Pombe Magufuli ananiambia kuhusu miradi hii ,,kuhusu Dodoma kuwa makao makuu, kuhusu mambo mengi.
Na leo hii tupo hapa kuweka jiwe la msingi la mradi huu lakini kà zi hii waswahili wanasema ukiona vinaelea vimeundwa na kwa bahati nzuri muundaji wa suala hili aliyetekeleza maono ya taifa kuhamia Dodoma akataka kuipanga Dodoma ,kwa bahati mbaya hatunaye,Mungu amemchukua,
Lakini ameniachia urithi mzito nami niahidi mawazo yote aliyoyaanzisha nita kwenda kuyatekeleza kikamilifu,leo hii ni moja kati ya mawazo aliyoyaanzisha niahidi pamoja na kuungwa mkono na African Bank tunaenda kukamilisha mradi huu kama alivyotaka Magufuli,"alisisitiza Rais Samia.
Katika hatua nyingine Rais huyo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema Serikali inatumia fedha nyingi katika ujenzi wa barabara ambapo gharama ya ujenzi wa kilomita 1 ni shilingi bilioni 1.2 hadi 1.5 hivyo amewaomba watanzania kuzitunza.
Amesema ujenzi wa barabara hiyo unaenda kufungua masoko hivyo ametaka ujenzi huo ukamilike kwa wakati kwani utatoa fursa mbalimbali hivyo watanzania kujiongezea kipato.
"Ndugu zangu Benki kudhamini miradi 11 hii inadhihirisha kweli hii ni Benki kwa ajili ya Waafrika,"amesema.
Amesema kilomita moja ni shilingi bilioni 1.2 hadi 5 hivyo amesema Serikali inatumia fedha nyingi hivyo kutumia nafasi hiyo kuwaomba watanzania Kutunza Miundombinu na kuacha mambo ya hovyo yanayofanywa katika uharibifu huo.
Kadhalika Rais Samia amesema Serikali inajenga barabara 23 kwa fedha za ndani huku 13 kazi ikiwa inaendelea.
"Tunashukuru sana Serikali ya awamu ya tano kuleta vuguvugu hili pamoja na kuungwa mkono na Benk ya Maendeleo na hawapo katika barabara wapo pia katika maji na umeme tumewaomba kutusaidia katika uwekezaji wa watu,"amesema
Akiwasilisha taarifa ya Mradi huo,Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila amesema lengo la kujenga barabara hiyo ni kupunguza msongamano katika Jiji la Dodoma.
Amesema jumla ya gharama ya Mradi huo ni shilingi bilioni 249 ambazo ni Kwa ajili ya fidia na ujenzi ambapo amedai kuna miradi midogo midogo kama ujenzi wa vituo vya afya,ununuzi wa ambulance wakati wa utekelezaji wa mradi huo.
Mtendaji huyo wa TANROADS ameeleza kuwa lengo ni kupunguza msongomana mkubwa wa magari katika Mkoa wa Dodoma ambao ungesababishwa na muingiliano wa magari yanayosafiri kupitia mjini.
Ameeleza kuwa barabara hiyo ina umbali wa Kil 20 kutoka katikati ya Jiji la dodoma ikiwa imegawanywa kwa wakandarasi wawili ambao ni M/sAVIC INTL Project na China Civil Engineering Construction Cooperation zote kutoka Jamhuri ya watu wa China.
Alifafanua kuwa awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa Kilomita 52.3 kupitia Nala,Veyula,Mtumba na Ihumwa wakati awamu ya pili itahusisha Kilomita 60 kupitia Ihumwa, Matumbulu na Nala.
Kwa upande wake,Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AFDB) Dk.Akinwumi Adesina amesema wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ambapo amedai wanaamini Tanzania ni sehemu sahihi ya uwekezaji.
Amesema Benki hiyo imewekeza kwa kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali yenye thamani ya Dola za kimarekani bilioni 2.5.
"Miaka kadhaa iliyopita nilikaa na kuzungumza na rafiki yangu,mtu wa watu hayati Dk.Magufuli kuhusu kutekeleza mradi huu ,Kwa bahati mbaya hayupo tena lakini Kutokana na ushirikiano wake kwetu tunaahidi kuendelea kishirikina na watanzania kwa miradi mingi zaidi,"amesema.
Naye,Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali iliona kuna umuhimu wa Kujenga barabara hiyo kutokana na ongezeko la watu pamoja na Dodoma kuwa Makao Makuu hivyo magari yanayoingia na kutoka kuwa mengi.
"Tunatoa shukrani kwa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kutekeleza mradi huu,imetoa fedha nyingi katika miradi ikiwa ni pamoja na kulipa madeni ya wakandarasi,
Bila kuwa na Mahusiano mazuri hili lisingetokea niipongeze Wizara kwa mradi huu mkubwa ni ubunifu mkubwa na utafungua fursa nyingi hivyo ,"amefafanua.