Saturday, 5 February 2022

KATIBU UVCCM TAIFA AWATAKA VIJANA KUACHA MAJUNGU,ASEMA RAIS SAMIA ATAONGOZA HADI 2030

Katibu UVCCM Taifa,Kenani Kihongosi na viongozi wengine na vijana wa UVCCM wakitembelea miradi Tarime

****
Na Dinna Maningo, Tarime

KATIBU wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Kenani Kihongosi amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu ataongoza hadi 2030 kwa kuwa ndiyo utaratibu wa chama Rais kuongoza katika kipindi cha miaka kumi na kwamba asiyetaka aende zake.

Kihongosi aliyasema hayo jana kwenye kikao cha UVCCM kilichofanyika Kitaifa katika Hoteli ya CMG mjini Tarime,wakati wa kuadhimisha miaka 45 ya kuzaliwa CCM na kukumbushana mambo ya chama kilichohudhuriwa na wanachama wa Umoja huo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.


Washiriki wengine ni baadhi ya viongozi wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tarime Daud Ngicho,Mbunge wa jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki, Mwita Waitara Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini, Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Tarime Daniel Komote na Simon Samwel wa halmashauri ya wilaya ya Tarime.

Katibu huyo wa UVCCM Taifa alisema kuwa Chama cha CCM siyo chama cha mtu kusema anavyotaka kwani kina taratibu zake,kanuni,miongozo na katiba na kwamba kwa yeyote atakayemuongea vibaya Rais Samia UVCCM wataruka nae.


"Wapo watu wanamuongea Rais wanavyotaka,sisi vijana hatutakubali mtu ndani ya chama anakichafua chama na Rais, asiyemtaka aende zake huko,kama mtu akija vibaya tutaruka nae,wajibu wetu ni kumlinda Rais wetu na chama chetu,2025 tunachukua tunaweka waaa" alisema Kihongosi.


Katibu huyo aliwataka vijana wa UVCCM kuacha chuki,uongo,umbea na kujipendekeza kwa madai kuwa inashusha heshima na kwamba malumbano kisa cheo siyo vizuri na badala yake washirikiane.


"Watu wanajipendekeza hadi inakera,tuache majungu,watu wanatengeneza maneno ya uongo, umbea,wengine wanapiga simu kwa viongozi wanaongea mambo ya ovyo ovyo mambo ya uongo ambayo hayapo ilmradi kumshusha mtu,jambo la kijana mwenzetu ni letu sote,tuache tabia za umbea,uchonganishi na kujipendekeza" alisema.


Kiongozi huyo alisema UVCCM wakishirikiana watafika mbali huku akiwasisitiza vijana kutovunja undugu kisa madaraka kwani mbali na uongozi wao ni familia moja wana wajibu wa kushirikiana kwakuwa Rais Samia ameonesha imani kubwa hivyo wasimuangushe.


Akizungumzia uchaguzi ndani ya chama hicho aliwaomba vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na siyo kubeba mikoba ya viongozi huku akikemea tabia ya baadhi ya wanachama wanapoona vijana wakionesha nia ya kugombea wanawaridisha nyuma.


"Tuache vijana wajitokeze kugombea hii tabia ya kuona kijana anaonesha nia unamrudisha nyuma hili jambo sitalikubali,nawapongeza vijana wa Tarime mnajituma jambo langu moja, Tarime chapeni kazi,niwapongeze viongozi wote wa chama mkoa na wilaya mmetupokea vizuri na mmefanya kazi nzuri,nimpongeze Dc Rorya ni kijana nilikuwa Rorya tumeona kazi zake nzuri" alisema.


Naibu Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Zanzibar,Mussa Haji alisema kuwa wamefurahi Baraza la la UVCCM Taifa kufanyika wilayani Tarime nakuwapongeza kwa ukaribu wao na akaomba wakati ujao Baraza hilo lifanyike Zanzibar.


Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mara Jacob Mangaraya aliwataka waliovuka umri wa ujana wa miaka 35 kuwaachia wengine nafasi kwa madai kuwa baadhi ya watu ung'ang'ania nafasi hiyo licha ya kuvuka umri "Tunalipongeza Baraza la kuu la UVCCM kwa upendo wenu wa kuja Mara wilaya ya Tarime kuzungumza na vijana,niwaombe viongozi tuliovuka umri wa vijana tuachie wengine nafasi" alisema.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tarime Daud Ngicho aliwahimiza vijana kuzingatia maadili na heshima na pale wanapoonywa au kukosolewa kutofanya jambo ambalo ni kinyume wawe tayari kusikiliza na kuwa tayari kutii.


Aliongeza kuwa Tarime haina ukabila kwani wapo viongozi ndani ya chama ndani ya wilaya hiyo si Wakurya akitolea mfano kwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya Godfrey Francis ambaye ni mkazi wa Tarime na mwenyeji kutoka wilaya ya Rorya pamoja na Katibu Hamasa wilaya hiyo Remmy Mkapa anayetoka mkoa wa Singida.


Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini Mwita Waitara alipongeza UVCCM kuadhimisha miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM Kitaifa katika wilaya ya Tarime na kusema kuwa shughuli nyingi alijifunza wakati alipokuwa UVCCM.


Mbunge wa jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki yeye aliisifia wilaya hiyo na kuwakaribisha tena vijana kwa kuwa Tarime hakuna njaa vyakula ni vingi na ardhi ya Tarime ina rutuba nzuri inayostawisha mazao.


Mkuu wa wilaya ya Rorya Juma Chikoka alisema"Mimi niliposikia vijana wanakusanyika Tarime nilisema lazima nifike kwa namna yoyote ile nimelelewa na kukuzwa UVCCM nipo Rorya kimwili lakini kiroho nipo pamoja na nanyi,hakuna kitu kikubwa kama kuweka alama kwa watu unaoishi nao lazima ujiulize ni kitu gani umekifanya kwa wenzako",alisema Chikoka.


Umoja wa vijana wa CCM umeadhimisha Kitaifa miaka 45 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi katika wilaya ya Tarime mkoa wa Mara ambapo viongozi wa chama hicho Kitaifa wameshiriki wakiwemo wajumbe wa baraza kuu la UVCCM Taifa,Wenyeviti wa UVCCM mikoa mbalimbali.


Wenyeviti wa UVCCM waliofika Tarime katika maadhimisho hayo ni kutoka Tanzania Bara na Zanzibar katika mkoa wa,Songwe,Mbeya,Dodoma,Geita,Tanga,Dar es salaam,Njombe,Tabora,Mara,Kilimanjaro,Pwani,Simiyu,Lindi,Shinyanga,Mwanza,Kigoma, Unguja kusini,Unguja kaskazini,na Unguja mjini magharibi.


Wajumbe wa baraza kuu UVCCM wameshiriki kutoka mkoa wa Kagera, Pemba kusini,Kigoma,Dodoma,Singida,Mwanza, Pemba kaskazini,Unguja mjini Magharibi,Njombe, Unguja kusini,Unguja kaskazini,Geita,Rukwa na Mbeya.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEBRUARI 5,2022




Magazetini leo Jumamosi February 5 2022

















Share:

Friday, 4 February 2022

HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA NA KASI YA MIKOPO KWA WAJASIRIAMALI KUCHOCHEA UCHUMI


Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru akiongea na wajasiriamali wakati wa makabidhiano ya mikopo ambayo imetajwa kuwanufaisha kiuchumi.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri akisisitiza jambo kwenye hafla ya makabidhiano ya mikopo kwa wajasiriamali ili kuchochea kasi ya uchumi.
Baadhi ya wajasiriamali wanufaika wa mikopo iliyotolewa na Jiji la Dodoma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Wajasiriamali wakiwa wamebeba picha yenye mfano wa hundi ikiwa ni sehemu ya fedha walizokopeshwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Na Dotto Kwilasa-Malunde 1 Blog-DODOMA.

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imekabidhi vifaa mbalimbali kwa vikundi vya ujasiriamali mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake katika kuwatumikia wananchi ipasavyo kwa kuwasaidia kuzitambua fursa zao ili kuchochea kasi ya ukuaji uchumi nchini.


Mikopo hiyo ni pamoja na Lori aina ya fuso (Tan.7) kwa ajili ya kubebea mchanga na matofali,Pikipiki,na Bajaji ikiwa ni asilimia kumi ya mapato ya ndani ambayo yanatakiwa kurejeshwa kama mkopo kwa Vijana, Wanawake, na Watu Wenye Ulemavu.


Akiongea wakati wa makabidhiano ya mikopo hiyo leo Februari 3, 2022, mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri amesema kuwa mikopo hiyo ni kwa ajili ya shughuli za viwanda,Guta 1,Lori moja la kubebea tofari na mchanga,fuso tani saba na mikopo kwa ajili ya biashasha ndogondogo, mikopo ya kilimo,mikopo ya mifugo na mikopo kwa ajili ya mama lishe na baba lishe.


Shekimweri amesema kuwa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha halmashauri ya Jiji la Dodoma imeweza kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 8.87 kwa vikundi 78 vilivyokabidhiwa hundi leo.


Amesema juhudi hizi Kwa pamoja zinafaa zitumike katika kuwaletea maendeleo ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja,jamii inayomzunguka pamoja na taifa kwa ujumla kwa kutimiza nia ya serikali ya kukuza uchumi wa mtu na uchumi wa vitu.


Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru ameeleza kuwa hatua hiyo Itaibua fursa za uchumi kwa Vijana Mkoani hapa huku akiitaja hatua hiyo kuwa itasaidia katika mwelekeo wa kukuza sekta ya viwanda Mkoani Dodoma kama njia mojawapo ya kuchochea uchumi.


Amefafanua kuwa katika kutekeleza sera ya kutoa asilimia kumi katika makundi ya vijana,akina mama na makundi maalumu halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kipindi cha mwaka wa fedha imetoa jumla ya mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 8.87.


Mafuru pia ameeleza kuwa hadi sasa taarifa inaonesha kwamba shilingi 3,981,070,933.62 tu ndizo zimerejeshwa ambapo ni sawa na asilimia 44.9 ya kiasi cha mkopo kilichotolewa .


Kadhalika Mkurugenzi huyo wa Jiji la Dodoma amesema; "Katika mikopo iliyotolewa leo kwa upande wa vikundi 46 vya wanawake wamepata sh.395,000,000 ,vikundi 23 vya vijana wamepata sh.364,000,000 na vikundi 19 vya watu wenye ulemavu wamepata sh.58,400,000 na kufanya jumla ya vikundi 78 kupata jumla ya fedha sh.817,400,000,"amefafanua Mafuru.


Kutokana na umuhimu wa tukio hilo,Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde ametumia nafasi hiyo kuvitaka vikundi vyote vilivyonufaika na mikopo hiyo kuitumia kwa lengo lililokusudiwa.


Mavunde ameimwagia sifa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kutekelezwa kwa kiwango kikubwa takwa hilo la kisera la kutoa asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa makundi hayo.


Naye Mwenyekiti wa kikundi cha Ilumbo Group ambacho kimenufaika na utaratibu huo Monica Masado amesema mikopo hiyo inawaoa chachu ya kujituma zaidi na kuondokana na utegemezi na kuweza kuinua maisha yao.


Akiongea kwa niaba ya wanufaika wa mikopo hiyo Masado ametumia nafasi hiyo kuwataka wakopaji wanaokopa mikopo hiyo kuwa waaminifu na kuhakikisha wanakopa na kurejesha kwa wakati.


"Lazima tuelewe tumekopa kujikwamua kiuchumi, wajasiriamali wenzangu lazima tuhakikishe tunafanya kazi na kufanya shughuli za maendeleo ,tusitumie fedha na vifaa hivi kwa makusidio tofauti kwani kwa kufanya hivyo tutawakwamisha wengine,"amesisitiza mjasiriamali huyo.


Share:

NIVISHE NISOME, MTAKA WASHIRIKIANA KUCHOCHEA ELIMU DODOMA

 

Na Dotto Kwilasa Malunde 1 Blog-DODOMA.

TAASISI ya 'Nivishe Nisome' inayojihusisha na masuala ya elimu nchini, imetoa msaada wa sare za shule kwa wanafunzi 241 katika shule ya Msingi Mbabala,Kata ya Mbabala,mkoani hapa huku wakitarajia kutoa sare za shule 5000 katika shule zote za Mkoa wa Dodoma ili kuchochea elimu.

Hayo yamejiri leo Mkoani hapa wakati wa ziara ya Taasisi hiyo katika shule ya Msingi Mbabala ikiongozana na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuhamasisha elimu kwa watoto na kuwapa moyo wa kuendelea kutamani kusoma na kujifunza zaidi.


Akizungumzia ujio wa ziara yao, Mkurugenzi wa Nivishe Nisome,Godfrey Kilimwomeshi,amesema wao kama taasisi ya vijana wanaojihusisha na uchechemzi wa elimu nchini, wanatamani kuona kila kijana anasoma katika mazingira mazuri na kuhakikisha  wanatumia jitihada zao zote kuwapatia sare  wanafunzi wasiojiweza.

Amesema ,maono ya Taasisi hiyo ni kuwajali wanafunzi wasiojiweza hususani wale wa  pembezoni jambo litakalowafanya wasahau shida zao japo kwa muda na kujiona bora kama wenzao na kwamba hali hiyo itasaidia kuboresha na kuinua kiwango cha elimu yao.

"Tunatambua haki ya kila mtoto ni elimu,tunaamini hapa kwenye elimu ndio wanatoka viongozi mbalimbali na ndio maana "Nivishe Nisome'" tumekuwa na maono ya kuwajali wanafunzi  kadiri tunavyojaaliwa ,"ameeleza Mkurugenzi huyo na kuongeza;

"Tunaamini mtoto akiwa katika mzingira mazuri basi na uelewa wake unakuwa mkubwa tofauti na akiwa kwenye mazingira",amesisitiza.

Kutokana na hayo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka ameishukuru Taasisi hiyo kwa mchango wake katika elimu huku akiwataka wazazi na walezi wa watoto hao waliopewa sare za shule kuwahimiza masomo watoto wao ili wasome kwa bidii .

Pia ametoa angalizo kwa walimu wa shule hiyo kuwahimiza  wazazi wote wenye watoto wa  madarasa ya mitihani ya Taifa kuwapa muda wa kujisomea na kuwapunguzia kazi za kufanya nyumbani ili watoto wasome na wawe na nia na mahangaiko moyoni hali itakayo ongeza ufaulu.

"Kupitia msaada huu wa sare za shule,sisi kama Wazazi tunapaswa tusimame kwenye nafasi yetu na si kujibweteka,wenzetu hawa wa Nivishe nisome wamekuja kwangu wakasema sisi hatuna uwezo wa kujenga shule lakini tunataka kutoa sare kwa shule 5000 hii inahamasisha wanafunzi kwenda shule,na kusoma Kwa bidii",amesema Mtaka.

Mtaka ambaye ameambatana na Taasisi hiyo shuleni hapo ameonesha pia kukerwa na tabia ya baadhi ya watoto ambao wapo kwenye rika la kuwepo shuleni lakini wanaishia kuzurura ovyo mitaani kwa madai ya kutafuta vibarua  masokoni na minadani wakati wa masomo na kusema hataki kuona mtoto yoyote mwenye umri huo  akiwa mtaani.

"Malezi ya watoto ni ya jamii nzima,ukiona mtoto  wa mwezio hayupo darasani wakati wa masomo hakikisha unamrudisha darasani,hayo ndiyo malezi mema,na sio kumtumikisha mtoto wa mwenzako muda wa masomo,ni dhambi kubwa,"amesema Mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma huku akiongeza kuwa;

Watoto wote ni mali ya serikali ndio maana kila wakati huwa nasisitiza sitaki kuona mwanafunzi anazurura mtaani wala mnadani,kila mzazi mwenye mtoto aliyefikia umri wa kuanza darasa la kwanza apelekwe shule na mzazi asipompeleka mtoto shule akamatwe akafanye kazi za usafi shuleni,"amesema. 

Katika hatua nyingine,Mtaka amewataka Afisa Elimu Sekondari na Afisa Elimu Msingi wa jiji la Dodoma kutoa maagizo kwa Wakuu wa shule zote kuwa wakati wa kufunga shule wazazi wa wanafunzi wawe wanapewa taarifa mapema ili wawepo shuleni kwa ajili ya kubadilishana changamoto za watoto wao  na kuona namna ya kusaidia na walimu kuzitatua.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Nathaniel Mwijumbe ameahidi kuyafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa na kushukuru kwa msaada huo na kusema  utawasaidia wanafunzi kuwa na moyo wa  kujifunza na wenzao.

Amesema baadhi ya wanafunzi hushindwa kuwa na ufaulu mzuri kwenye masomo Kutokana na upweke unaotokana na umasikini hivyo kupitia msaada huo wa sare za shule wengi wao watajiona hawako peke yao kwani nyuma yao kuna watu wanaowajali na kuwalinda.

"Sisi kama viongozi tupo na wewe katika juhudi zako za kupeleka mbele elimu,tutahakikisha watoto wanasoma vizuri kwa kufanya jitihada ikiwa ni pamoja na kuwapatia wanafunzi  chakula shuleni,hii itaongeza ufaulu mara dufu na hapo tutakuwa tumetimiza ndoto yako ya kuondoa ziro katika Mkoa wa Dodoma,"amesisitiza Mwl.Mwijumbe. 

Share:

AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUIBA BIBLIA..MWENYEWE AJITETEA ALITAKA TU KUMJUA MUNGU



Mwanaume ambaye amekamatwa na kushtakiwa kwa kuiba biblia mbili kwenye duka kubwa jijini Nairobi anasema alichokuwa akitaka ni kumjua Mungu tu.

Augustine Wanyonyi, 35, aliambia mahakama kwamba aliiba Biblia hizo ili asome na kumjua Mungu zaidi.Alipoulizwa kwa nini aliiba nakala mbili badala ya moja, alisema Biblia ya pili alikusudia kwa ajili ya mkewe.

Wanyonyi alifika mbele ya Hakimu Mkuu wa mahakama ya Milimani katika Jiji la Nairobi Susan Shitubi ambapo alikiri kutenda kosa hilo.

Niliiba biblia ili nisome, nielewe na kuhubiri neno la Mungu badala ya kujiua kutokana na matatizo yanayonikabili,” Wanyonyi aliambia mahakama. Alishtakiwa mnamo Jumanne tarehe 1 Februari na kurudi mahakamani kuhukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kosa hilo.

Wanyonyi alikamatwa Jumapili baada ya kupatikana na nakala mbili za biblia zenye thamani ya Shilingi 2,100 za Kenya.

Kulingana na ripoti ya polisi iliyosomwa na wakili wa Serikali Alice Mathangani, mshtakiwa alikwenda kwenye duka hilo mwendo wa saa tisa mchana katika tarehe iliyotajwa, na kuiba biblia hizo mbili na kuzificha ndani ya suruali yake.

“Alinaswa na kanda ya CCTV ya duka kuu na baadaye kukamatwa na wahudumu wa CCTV baada ya kushindwa kulipia bidhaa sawa na hiyo alipofika kwa kaunta,” mwendesha mashtaka alisema.


Mwendesha mashtaka pia aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa alikuwa na rekodi ya awali ya wizi wa dukani ambapo alishtakiwa Desemba 2021 lakini akaachiliwa na mahakama nyingine baada ya kuomba msamaha.

Hakimu aliamuru ripoti ya kabla ya hukumu iwasilishwe mahakamani ndani ya siku saba. Atafikishwa mahakamani kuhukumiwa mnamo Februari 16.
Share:

Thursday, 3 February 2022

MWANAFUNZI ATEMBEZEWA KICHAPO KISA AMEKULA CHAPATI ZA MWALIMU MKUU



Mwanafunzi wa Shule ya Gremon Education Center eneo la Bamburi, kaunti ya Mombasa nchini Kenya anauguza majeraha mabaya katika Hospitali ya Rufaa ya Coast General baada ya kudaiwa kupokezwa kichapo cha mbwa koko na mwalimu mkuu kwa kula chapati zake.

Mama yake mwanafunzi huyo, Agnes Ngure alisema kuwa mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 15, anapokea matibabu ya figo hospitalini humo baada ya kujeuriwa vibaya na mwalimu mkuu wa shule hiyo Nancy Geshew na wanafunzi wenzake.

Kulingana na mama huyo, mwanawe aliadhibiwa na mwalimu mkuu kwanza kabla ya kumkabidhi kwa wanafunzi wenzake na kuwaelekeza wamwadhibu.

"Walioshuhudia tukio hilo wanadai kuwa mwalimu huyo alimvamia mwanangu kabla ya kumkabidhi kwa wanafunzi wenzake ambao walimpiga kwa njia ambayo imetajwa kuwa haki ya kundi," alisema.

 Mwanafunzi huyo anashtumiwa kula chapati mbili ambazo zilikuwa zimetengewa mwalimu mkuu wa shule hiyo, K24 yaripoti. 

Ngure pia aliongeza kuwa mwanawe alitengwa katika bweni la shule hilo bila kupewa matibabu na wazazi wake walijuzwa tu baada ya hali yake kuanza kudorora.

 "Aliwekwa ndani ya bweni tangu Januari 23 na nilijulishwa hali yake jana (Januari 31) nilipoambiwa niende kumchukua mwanangu ambaye walidai alipata majeraha baada ya kutumia maji ya moto kuoga. Muda wote huo walikuwa wamemweka kitandani huku wakitumia chumvi, maji moto kuponya majeraha yake,” Ngure alisema.


Kisa hicho kiliripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Kazadani huku Kamanda wa Polisi wa kaunti ndogo ya Nyali, Ibrahim Dafar akithibitisha kwamba mwalimu mkuu huyo amekamatwa. Dafar alisema wanasubiri ripoti ya p3 kabla ya mwalimu huyo kufikishwa kortini Jumatano, Januari 2.

Kamanda huyo wa polisi pia alifichua kuwa mwanafunzi wa Kidato cha Nne ambaye aliongoza kundi lililompiga mwenzao anasakwa baada ya kuingia mafichoni.
Share:

JAMAA AJIUA KWA SUMU YA PANYA KISA MKE WAKE KAGOMA KURUDI

Mfano wa chupa zenye sumu
**

Kijana aliyejulikana kwa jina la Ginasa Petro (30)  mkazi wa kijiji cha Kayenze, kata ya Kafita wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita  amejiua kwa kunywa sumu ya Panya baada ya mke wake Sarah Jeremia kukataa kurudi kuishi naye baada ya hapo awali kuondoka kutokana na mgogoro wa kimapenzi.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba wivu mkubwa ndiyo uliopelekea mwanaume kuchukua maamuzi hayo 

Ameshauri wanandoa  kuwa wanapaswa kuwaona viongozi wao wa dini ili kusuluhisha changamoto zao na si kujitoa uhai.

Share:

MCHENGERWA AIPONGEZA DSTV KWA KUTANGAZA MAUDHUI YA KITANZANIA


*************************

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa Kongole kwa Kampuni ya Multichoice Tanzania (DSTV) kwa kurusha maudhui ya kitanzania hususan Muziki na Filamu ambayo yameleta manufaa kwa wasanii.

Mhe. Mchengerwa ametoa pongezi hizo leo Februari 3, 2022 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Jacqueline Woiso katika ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma.

"Nitakutana na wasanii wote wakiwemo waigizaji na wanamuziki na kufanya nao mazungumzo, hii itatuwezesha kujua changamoto zao na mahitaji yao katika kufanya kazi zao za sanaa na hili ningeomba ushirikiano kutoka kwenu Multichoice Tanzania ili kuweza kufanikisha,"amesema Mhe. Mchengerwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi huyo, ameahidi ushirikiano wa karibu na Wizara katika kuhakikisha sanaa inakuwa na wasanii wanapata kipato kutokana na kazi zao.
Share:

KICHWA CHA MLINZI WA SHULE ALIYEUAWA CHAPATIKANA KWA MLINZI MWENZAKE



JESHI la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Raymond Mollel ammbaya amekamatwa kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa mlinzi wa shule ya Winnings Spirit iliyopo eneo la Terati jijini Arusha, Issa Dinaiah (57) aliyekutwa ameuawa kwa kuchinjwa huku kichwa chake kikiwa hakipo.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Joshua Mwafrango amekiri kukamatwa kwa kumtuhumiwa huyo ambaye mpaka sasa anaendelea kuhojiwa.

“Tumemkamata kijana mmoja anayeitwa Raymond Mollel kwa tuhuma za mauaji hayo. Huyu mtuhumiwa ni mlinzi mwenzake. Raymond na marehemu walikuwa walinzi wa Meya wa Arusha, Maxmillian Iranghe.

“Baada ya kumkamata tulimhoji, amekiri kutekeleza mauaji hayo na kuonesha alipokificha kichwa cha mwenzake. Pia, kichwa cha marehemu kimepatikana. Hakuna kitu kilichovunjwa wala kuibiwa eneo la tukio, bali ni hayo mauaji yaliyofanyika.

Mwili wa mlinzi huyo ulikutwa jana Jumatano Februari 2, 2022 asubuhi na wafanyakazi wa shule hiyo inayomilikiwa na Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranghe.
Share:

WIZI ULINIRUDISHA HATUA NYUMA, MADUKA YANGU YALIIBIWA KILA UCHAO


 
Nilikuwa mfanyabiashara aliyetia fora katika swala zima la biashara. Nilikua na maduka ya kuuza bidha za kielectroniki kama vile radio, simu, vipatakilishi na bidhaa zingine za kielektroniki.
 Biashara yangu ilikua imenoga kwani mjini mahali ambapo niliuzia bidhaa zangu, wateja walikuja kwenye maduka yangu pekee. Jambo hili lilifanya biashara zingine kando yangu kufungwa kila mara.

 Wafanyibiashara wengine walianza kunionea gere kwani walishusha bei ya bidhaa zao ile kuwavutia wateja lakini hilo halikufua dafu kivyovyote. Ama kwa hakika biashara ndiyo ilikuwa kipaji changu cha maishani. Nilikuwa nimesomea mambo ya biashara chuoni hii pia ilinipiga jeki katika shughuli zangu za kila siku za biashara. Hali ilikua shwari hadi wakati ambapo maduka yangu yalianza kuvunjwa na kuibiwa kila mara.

 Maduka yangu yalikua yakivunjwa kila baada ya wiki mbili na kuibiwa kila mara. Nilijaribu kuajiri walinzi lakini wengi wao ndiyo waligeuka kua wenye mikono mirefu katika maduka yangu ya kuuzia bidhaa za kielektroniki. Hii ilikuwa ni fursa nzuri ya wafanyibiashara wenye biashara kama yangu kutia fora kwani wizi ule ulinirudisha hatua nyingi nyuma. 

Kila wakati ilikuwa ni kurudisha bidhaa zilizoibiwa kwani biashara haikuwa kamili bila ya bidhaa zingine wakati wowote. Nilitembea kila sehemu ya nchi nikitafuta suluhisho la kudumu la hali ile lakini ilikua ni vigumu kupata suluhisho la kudumu.

 Siku moja niliamkia kwenye maduka yangu nikapigwa na butwaa punde tu nilipowasili. Maduka yote yalikuwa wazi. 

Bidhaa zote zilikua zimeibiwa. Nilipoangalia kwenye kamera za CCTV hakuna chochote nilichoona kwa kuwa ilikua imepakwa mafuta kwa hivyo haingeonyesha lolote wakati wa tendo la wizi. Sikupoteza imani na biashara ile kwani nilitafuta mikopo kwenye benki na nikafungua biashara zile upya. 

Wakati huu niliajiri walinzi wengi ili kuepukana na wizi wa kila mara kwenye biashara zile. Biashara zile zilikaa kwa muda wa mwaka moja bila ya wizi wowote kufanyika hali ambayo ilileta mapato mengi zaidi. Nililipa mikopo yangu niliyokua nayo na hapo nikajipiga kifua kwamba wizi ulikua umetokomea na tukauzika katika kaburi la sahau. 

Huu ulikua tu ni mwanzo wa mahangaiko. Maduka yale yalivunjwa mara nyingine ambapo mara hii yaliteketezwa moto pia ili kufanya nisiweze kufungua biashara kwa mara nyingine iwapo nilikua na wazo kama hilo. Sikuwa na lolote la kufanya ila kusalimu amri na kukaa nyumbani mzongo wa mawazo ukinikumba. Hali hii ilipelekea vidonda vya tumbo kunikosesha usingizi kwani nilikuwa mwadhiriwa. 

Marafiki wote walinitoroka kwani kila waliponiona walidhani ilikuwa firsa yangu ya kuwaomba mikopo. Kampuni ya bima niliyokuwa nimejisajili nayo pia ilidinda wakati ule kunipa fidia ili nifufue biashara yangu kwa mpigo. 

Nilipoteza tumaini kabisa wakati ule. Mke alinikimbia pamoja na watoto kwani singeweza kukimu mahitaji ya familia. Nilitembelea waganga mashuhuri kwa ushauri lakini kila mara pesa zangu ndizo zilikua zikiisha. Wahubiri wa makanisani pia walijifanya kua na uwezo wa kutatua shida yangu lakini yote yaliambulia patupu kwani nilipanda mbegu kila mara jumapili kuwatajirisha tu.

 Kila mtu kwenye mtaa nilipokua nikiishi alinifahamu kwani nyumba nilikua nimefungiwa kwa ukosefu wa kodi. Nilikua nimechakaa ajabu. Hakuna pahili popote ningekopa mkopo ili nianzishe biashara upya kwa kua tayari mikopo niliyokua nayo nilikua nimefika ukiongo wa kuongezea mikopo mingine kwa wakati ule. 

Nilipokuwa nikisoma mitandaoni kuhusu kazi nyingine ambazo ningefanya, nilipatana na wavuti www.kiwangadoctors.com palikua na nakala ambazo watu wengi walikuwa wamepitia shida kama yangu kwenye biashara zao lakini madaktari wa Kiwanga walikua wamewasaidia kusuluhisha.

 Nilifuata maagizo ya jinsi ningewafikia. Siku iliyofuatia niliwasili katika ofisi zao mjini Nakuru tayari kuzika suala zima la wizi kwenye kaburi la sahau. Nilihudumiwa na kurejea nyumbani.

 Baada ya siku tatu, kampuni ya bima ilinipigia simu ya kwamba ingegaramia maduka yangu yote yaliyoibiwa na kuteketezwa moto. Baadaye nilifungua biashara zangu kwa mpigo na tangu siku ile hakuna siku hata moja maduka yangu yamevunjwa kwa kua hali ilikua shwari. 

Mtu yeyote anayekumbwa na mambo ya wizi katika biashara kama nilivosumbuka anaweza watembelea madaktari wa Kiwanga kwa usaidizi. Wanasuluhisha matatizo ya mapenzi, uchawai na mengineyo. Waweza kumpata Dkt. Kiwanga kupitia wavuti www.kiwangadoctors.com barua pepe kiwangadoctors@gmail.com au piga simu kwa nambari +254769404965.
Share:

MSHINDI WA BIKO TABATA SEGEREA AVUNA MILIONI 10 ZAKE


Meneja Masoko wa mchezo wa kubahatisha wa Biko Mshiko Nje Nje, Goodhope Heaven kushoto akishiriki tukio la kumkabidhi mshindi wa sh Milioni 10 Karimu Malisawa Mwema katikati. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Tawi la benki ya CRDB lililopo Palm Beach, jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Balozi wa Biko Kajala Masanja wa pili kutoka kushoto, Meneja wa CRDB Palm Beach, Pendo Kitula wa pili kutoka kulia akiwa na Catherine Momburi Meneja huduma kwa wateja wa Tawi hilo. Picha na Mpiga picha wetu.
Balozi wa Biko, Kajala Masanja kushoto akishirikiana na Pendo Kitula, Meneja wa CRDB, Tawi la Palm Beach jijini Dar es Salaam, kumkabidhi mshindi wa Biko sh Milioni 10, Karimu Malisawa Mwema katikati alizoshinda katika droo kubwa ya Buku nibukue iliyochezeshwa Jumapili iliyopita.
Mshindi wa Biko sh Milioni 10, Karimu Malisawa Mwema wa Tabata Segerea, akionyesha pozi matata lenye shangwe baada ya kukabidhiwa fedha zake alizoshinda katika droo kubwa iliyofanyika Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam. Picha na Mpiga picha wetu.

***
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKAZI wa Tabata Segerea, jijini Dar es Salaam, Karimu Malisawa Mwema, amefanikiwa kukabidhiwa fedha zake jumla ya sh milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye droo kubwa ya Biko Buku Nibukue iliyofanyika Jumapili, akipkea fedha zake katika Tawi la CRDB Premier lililopo Palm Beach jijini Dar es salaam.


Makabidhiano hayo yameendeshwa na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kwa kushirikiana na Balozi wake Kajala Masanja, huku upande wa CRDB, ukiwakilishwa na Meneja wa Tawi hilo, Pendo Kitula na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa tawi hilo, Catherine Momburi, ambapo mshindi huyo wa Biko alisema fedha zake atazitumia kusomesha watoto wake pamoja na kujikita kwenye kilimo mkoani Morogoro.

Biko ni mchezo unaochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi unachezwa kwa kufanya miamala kuanzia sh 1000 na kuendelea, ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu namba 2456, bila kusahah wanaocheza kwa mtandao www.biko.co.tz.

Mbali na wanaocheza kwa kupitia www.biko.co.tz, pia wanaotumia simu za kawaida nao wataendelea kucheza kama zamani kwa kutumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 na wote kujishindia kuanzia sh 2500 hadi milioni tano papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili.


Share:

WAYA WA UMEME WAUA WATU 26 SOKONI

Picha ya DRC iliyopachikwa kwenye Mitandao.

**

Takriban watu 26 wamefariki baada ya waya wa Umeme kukatika na na kuanguka sokoni katika wilaya ya Matadi-Kibala iliyopo viungani mwa mji mkuu Kinshasa, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kwamba watu kadhaa walifariki mara moja, polisi imesema.

Waya uliokuwa na kiwango cha juu cha umeme ulikatika ghafla na kuangukia ndani ya nyumba na watu waliokuwa wakinunua bidhaa karibu na mji mkuu Kinshasa Jumatano.

Picha ambazo zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii ambazo hazijathibitishwa zinaonyesha hali baada ya tukio hilo, huku miili kadhaa ikionekana.

Taarifa, iliyotolewa na kampuni ya taifa ya umeme ya DRC imesema kuwa inaamini radi ilipiga sehemu ya waya huo, na kusababisha uanguke ardhini. Kampuni hiyo imetuma salamu za rambirambi kwa familia za waathiriwa wa mkasa huo.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI FEBRUARI 3,2022














Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger