Saturday, 29 January 2022

MKAKATI WA KITAIFA WA ELIMU JUMUISHI WA MIAKA MITANO WAZINDULIWA JIJINI DODOMA


Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akizungumza wakati akizindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Kamishina wa Elimu Tanzania Dkt.Lyabwene Mtahabwa,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Elimu Maalum na Jumuishi kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknlojia Dkt.Magreth Matonya,akielezea lengo la mkakati huo wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Kimataifa Dkt.Daniel Baheta,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Wanafunzi walioshiriki uzinduzi wakifatilia Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Wadau mbalimba wakifatilia Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Elimu Maalum na Jumuishi kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknlojia Dkt.Magreth Matonya kabla ya kuzindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akizindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akiwa na wadau pamoja na wanafunzi wakionyesha vitabu vya muongozo mara baada ya kuzindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akiwa katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kuzindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi mara baada ya kuzindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.

............................................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imezindua mpango mkakati wa kitaifa wa elimu jumuishi wa miaka mitanto (5) unaolenga kutoa fulsa sawa ya elimu kwa makundi yote bila kujali kikwazo cha aina yotote au mazingira.

Akizindua mpango huo leo Januari 28,2022 jijini Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Eliamini Sedoyeka amesema mpango huo ni wa tatu na umelenga kwenda kuboresha utoaji wa elimu katika ngazi zote bila kujali kikwazo cha aina yoyote katika fulsa ya upataji wa elimu kwa watoto.

"Kama Serikali tulikuwa na mipango mbalimbali na huu tunaozindua ni wa tatu ambao unakwenda kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu kwa usawa bila kujali hali ya mtoto toka ngazi ya awali, msingi, sekondari, ualimu, vyuo vya ufundi, maendeleo ya wananchi, elimu ya nje ya mfumo, na elimu ya juu” amesema. Prof. Sedoyeka.

Amesema mkakati huo unalenga kuwa na mfumo wa elimu unaotoa fulsa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kupata elimu bila vikwazo kimtazamo, mazingira, kiuchumi na kitaasisi katika ngazi zote.

“Mkakati huu unatoa fulsa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kusoma masomo ya ufundi tangu wakiwa darasa la awali lengo kuwajengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi kwa kuwa na uchuzi” amesema.

Ameongeza kuwa “mkakati huu pia utatekelezwa katika ngazi za vyuo vya ufundi, vyuo vya maendeleo ya wananchi ambako wananchi watapata umahiri katika fani mbalimbali zikiwamo za ujasiliamali na TEHAMA kuwaimarisha kiuchumi” Amesema.

Amesema mkakati huo umechapishwa kwa kuzingatia ujumuishi kwa kuwa na nakala za maandishi ya kawaida, maandishi yaliyokuzwa na maandishi Braille kwa ajili ya watu wenye uoni hafifu na wasioona.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu Maalumu Dkt Magreth Matonya amesema mpango mkakati huo umeboreshwa na wanaamini utaendana na mahitaji ya sasa na ili kuhakikisha unafanya vyema mpango huo utakuwa ukifanyiwa tathmini kila baada ya miezi sita ili kuona utendaji kazi wake na matokeo.

“Mkakati huu utatupa dira ya wapi tuelekee katika utekelezaji wa elimu jumuishi, utasaidia upatikanaji wa taarifa za upatikanaji wa taarifa za utelelezaji wa elimu jumuishi ili kurahisisha ufanyikaji wa tathmini” amesema Dkt. Magreth.

Amesema mkakati huo umelenga kurekebisha sera ya elimu iendane na elimu jumuishi, kuimarisha upatikanaji wa elimu bora na kwa usawa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika ngazi zote, kuongeza uandikishwaji na ushiriki wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika ngazi zote za elimu.

Nae Kamishna wa elimu hapa nchini Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema kuzinduliwa kwa mkakati huo ni lengo la kumfanya kila mtoto wa kitanzania anapata elimu bora na kwa usawa kwa maendeleo ya taifa na jamii kwa ujumla.
Share:

MANISPAA YA KAHAMA YAONGOZA UKUSANYAJI MAPATO


Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga imeongoza kwa kukusanya mapato kwa 67%, ikifuatiwa na Musoma 65%, na Ilemela 55%.

Katika kundi hili Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imekuwa ya mwisho ambapo imekusanya 37% ikifuatiwa na Kigoma 38% na Ubungo 40% ya lengo la mwaka.

 Hayo yamesemwa na Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa  wakati akitoa taarifa ya mapato na matumizi ya Halmashauri kwa nusu mwaka wa fedha 2021/2022.

Share:

TUZO ZA WASANII ZAREJEA, WASANII WAKABIDHIWA MIRABAHA

Waziri wa Utamaduni. sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza uzinduzi wa tuzo za muziki pamoja na ugawaji wa mirabaha kwa wasanii uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Utamaduni. sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akipiga ngoma kuashiria Uzinduzi Rasmi wa Tuzo za Muziki Tanzania kwenye Hafla iliyofanyika usiku wa Januari 28, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Wadau wa Muziki nchini wakiwa wamefurika kwaajili ya kufuatilia uzinduzi wa tuzo za muziki pamoja na ugawaji wa mirabaha kwa wasanii uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamduni,Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi (wa kwanza kushoto) akifuatilia uzinduzi wa tuzo za muziki pamoja na ugawaji wa mirabaha kwa wasanii uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Utamaduni. sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa (katikati) akiwa na Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul (wa kwanza kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Mhe.Said Yakubu wakifuatilia buruduni katika uzinduzi wa tuzo za muziki pamoja na ugawaji wa mirabaha kwa wasanii uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mheshimiwa Niki wa Pili akifuatilia uzinduzi wa tuzo za muziki pamoja na ugawaji wa mirabaha kwa wasanii uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Wadau wa Muziki Diwani wa Kilungure Mkubwa Fella (Katikati) akiwa pamoja na Mbunge wa Morogoro Kusini Mheshimiwa Hamisi Taletale maarufu Babu Tale wakifuatilia uzinduzi wa tuzo za muziki pamoja na ugawaji wa mirabaha kwa wasanii uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Wasanii wa ngoma kutoka wilayani Bagamoyo wakitoa burudani katika katika uzinduzi wa tuzo za muziki pamoja na ugawaji wa mirabaha kwa wasanii uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)


****************************


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM


Waziri wa Utamaduni. sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewaongoza wadau wa sanaa wa musiki nchini katika uzinduzi wa tuzo za muziki pamoja na ugawaji wa mirabaha kwa wasanii uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Mchengerwa amesema katika uongozi wake hatotarajia kuona kuna watu wapo kwaajili ya kudhoofisha tasnia ya muziki nchini kwa kuwakandamiza wasanii.


Amesema kuna umuhimu nasi tukaandaa tuzo kubwa za barani Afrika kama MTV na AFRIMA hivyo amewataka watendaji wa Wizara hiyo kuhakikisha wanaandaa mazingira mazuri kwa kujifunza kwa nchi zingiine ambazo huandaa tuzo hizo.


"Sanaa ya muziki inanafasi muhimu sana,muziki uppo katika asili ya mwanadamu pia taifa linaweza kueleza hisia zake kwa kutumia muziki". Amesema Waziri Mchengerwa.


Katika zoezi la ugawaji wa mirabaha kwa wasanii, kwaya zimeonekana kupigwa na kusikilizwa zaidi katika vituo vya radio na luninga nchini nahivyo kuwafanya waimbaji wa nyimbo za injiri kuibuka na kitita zaidi katika mgao wa mrahaba wa kwanza ulianza kutolewa na Serikali kupitia Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA).


Kwaya Kuu ya Mtakatifu Cecilia Arusha imeibuka na mkwanja mzito wa Sh milioni 8.739 ikifuatiwa na Ali Saleh Kiba maarufu King Kiba aliyepokea Sh milioni 7.588 kutokana na mauzo ya nyimbo zake mbalimbali.


Wengine waliopokea mgao mbele ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa ni Rose Mhando Sh. milioni 5.79.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 29,2022










Share:

Friday, 28 January 2022

TUMIA MAJIKO HAYA BORA NA IMARA YANAYOTUMIA MKAA MCHACHE KABISA...PIGA 0745613461

 
Share:

TANZANIA NDIYO NCHI YENYE HIFADHI KUBWA KULIKO ZOTE BARANI AFRIKA


Makundi makubwa ya Tembo yakiwa katika hifadhi ya Taifa ya Nyerere
Twiga ndani ya hifadhi ya Nyerere
Kaimu Mhifadhi Mkuu,Dokta Emilian Kihwele akizungumzia hifadhi ya Mwalimu Nyerere
Mshauri wa Uhifadhi wa Wanyamapori,Maliasili na Mazingira wa shirika la Frankfurt Zoological society Dokta Asantaeli Melita akionyesha kitabu cha sensa  iliyoonyesha kuwepo kwa idadi kubwa ya tembo,sensa hiyo ilifanyika mwaka 2018

****
Na Pamela Mollel,Hifadhi ya Nyerere

Tanzania kwa sasa ndio nchi yenye hifadhi kubwa kupita zote Barani Afrika kwa mujibu wa wataalamu wa sekta za uhifadhi.

Hifadhi mpya ya Nyerere yenye eneo la kilometa za mraba 30,893 imethibitishwa rasmi kuwa ndio kubwa Zaidi katika ukanda wa Afrika mashariki na Kati.

Kaimu mhifadhi mkuu, Dokta Emilian Kihwele anaeleza kuwa kijiografia, Nyerere imo ndani ya mikoa mine, ikiwemo ya Pwani, Lindi, Ruvuma na Morogoro. 

Nyerere pia inashikilia nafasi ya pili kwa ukubwa Barani Afrika baada ya ile ya Namib Naukluft, ya nchini Namibia yenye eneo la kilometa za mraba 49,000.

Kwa mujibu wa Mshauri wa uhifadhi wa Wanyamapori, Maliasili na Mazingira wa shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS), Dokta Asantaeli Melita, Hifadhi ya Nyerere pia ndio eneo lenye idadi kubwa Zaidi ya Tembo nchini.

“Tulifanya sensa ya kuhesabu wanyamapori katika eneo zima la Nyerere na Selous mwaka 2018 na tukagundua kuwa sehemu hii ina tembo takriban 30,000,” alisema Dokta Melita.

Hapa nchini pia Hifadhi ya Nyerere inaongoza kwa Ukubwa baada ya kuipiku ile ya Ruaha ambayo kwa sasa ni ya pili kwa ukubwa nchini.

Hifadhi ya Ruaha pia ndio ya pili kwa ukubwa katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati, ikiwa na eneo la kilometa za mraba 20,226.

Hifadhi zote mbili zinazoongoza kwa ukubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki zinapatika upande wa kusini mwa Tanzania ambako kwa bahati nzuri ndiko Tanzania inakotekeleza mradi maalum wa kuendeleza utalii na uhifadhi endelevu kwenye mzunguko wa kusini, yaani REGROW unaofadhiliwa na benki ya dunia.

Mwaka uliopita Hifadhi ya Nyerere ilizalisha 3.1 billioni za kitanzania. Kwa mujibu wa mhifadhi mkuu, wa Nyerere, hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu, hifadhi hiyo itakuwa imezalisha Zaidi ya Bilioni 3.6.

Tanzania ina hifadhi za taifa 22 na kati ya hizo, hifadhi ya Serengeti, iliyo ya tatu kwa ukubwa nchini ndio maarufu Zaidi.
Share:

HELVETAS TANZANIA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI UPANDAJI MITI


AFISA Mazingira Mkoa wa Simiyu Juma Kazula (mwenye tisheti ya kijani) akitoa elimu ya namna ya kuondoa kiriba kabla ya kupanda mti mbele ya wanafunzi wa sekondari Lubiga iliyopo wilayani Meatu mkoani humo, katikati ni Afisa Mazingira wilaya ya Meatu Thomas Shishwa.

***

Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.

Shirika lisilokuwa na Kiserikali la Helvetas Tanzania lenye makao makuu jijini Dodoma linatarajia kupanda miti zaidi ya elfu 16 mkoani Simiyu ili kuendelea kulinda Uoto wa Asili pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Shirika hilo ambalo pia linatekeleza miradi ya elimu, kilimo, vijana na utunzaji wa mazingira na kwamba miradi hiyi inatekelezwa katika mikoa ya Dodoma, Rukwa, Katavi, Mbeya, Singida na Simiyu.

Aidha, Katika mikoa ya Simiyu na Singida ili kuwezesha akina mama kuweka akiba na kukopeshana ili kumudu hali ya uchumi na kujikwamua kimaisha pamoja shughuli za kilimo hai na utuzajia ili kurejesha uoto wa asili ikiwemo kupanda miti.

Afisa Mtathimini na Ufuatiliaji kutoka shirika hilo Loveness Msemwa anaeleza kuwa wanatekeleza miradi ya kuwezesha akina kuweka na kukopeshana, kilimo hai pamoja na utunzaji wa mazingira katika mikoa miwili nchini.

Anasema kupitia mradi wa kilimo hai unaotekelezwa mkoani Simiyu wanashirikiana na kampuni ya Alliance Ginnery na GIZ kutekeleza mradi wa kilimo hai ndani yake wakipanda miti ili kurejesha uoto wa asili kwa ajili ya kutekeleza shughuli za kilimo hai kisichotumia mbolea wala kemikali za viwandani.

‘’Kilimo hai kinahitaji uoto wa asili, mazao yanayozalishwa hayahitaji mbolea za viwandani wala kemikali, hivyo sisi tunatunza mazingira kwa kupanda miti, wenzetu Alliance ginnery wanafundisha wakulima kilimo hai’’ anaeleza Loveness.

Anafafanua kuwa katika mkoa wa Simiyu, mradi huo unatekelezwa wilaya ya Meatu kwenye kata za Kisesa na Lubiga na wanatarajia kupanda miti 16,715 kwenye taasisi za umma na kila mwananchi atagawiwa miti mitano mitano bure.

‘’Lengo ni kuboresha mazingira katika taasisi za umma, kurejesha uoto wa asili na kufanya utunzaji wa mazingira endelevu…tumejikita kwenye taasisi za umma kwa sababu zina rasilimali watu wa kutunza miti hiyo’’ anasema Loveness.

Anafafanua kuwa kupitia kugawa miti mitano kila kaya, jumla ya kaya 2343 zatapanda miti na wataendelea kufuatilia ukuaji wa miti hiyo kwa sababu mradi huo unatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu.

Anasema kuwa wameshakutana na wananchi kupitia mikutano ya vijiji ili kuunda kamati za mazingira za vijiji na kwamba wajumbe wa kamati hizo wamekuwa mabalozi wazuri wa upandaji miti.

Anafafanua kuwa kamati hizo zimewasaidia kuzifikia taasisi za umma ikiwemo shule, zahanati, misikiti na makanisa na kwamba hadi sasa kila mwananchi anashiriki kupanda miti nyumbani kwake na kwenye taasisi.

Ofisa Mazingira wilaya ya Meatu Thomas Shishwa anawashukuru wadau wa maendeleo wanaojitokeza kupanda miti wilayani humo huku akiwataka wananchi kuunga mkono juhudi hizo kwa kupanda miti katika maeneo yao.

Anasema lengo la Halmashuri ni kupanda miche milioni 1.5, kupitia kwenye taasisi za umma ikiwemo shule za msingi na sekondari, zahanati, vituo vya afya pamoja na nyumba za ibaada lakini pia kila mwananchi atahakikisha anapanda miti mitano.

Hivi karibuni, Afisa Mazingira Mkoa wa Simiyu Juma Kazula alishiriki uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti iliyofanyika katika kata za Lubiga na Kisesa wilayani Meatu mkoani humo, na kuwataka wadau wa mazingira kujitokeza kuunga mkono juhudi za serikali kwenye upandaji miti.

Kupitia Mradi wa utunzaji mazingira unaotekelezwa na Helvetas Tanzania, Kazula anawataka wadau na wananchi kupandaji miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanasababisha madhara makubwa kwa binadamu, wanyama na mimea.

Anayataja madhara hayo kuwa ni ukosefu wa mvua ambao husababisha ukosefu wa malisho, ukame, kukauka kwa vyanzo vya maji, kuongeza kwa joto, mmonyoko wa udongo na kuongezeka kwa hewa ukaa.

Kazula anataka jamii kutunza miti iliyopo pamoja na kuongeza kasi ya upandaji ili kuongeza uoto wa asili ambao unachangia kuleta mvua, kulinda vyanzo vya maji pamoja na kupunguza hewa ya kabondayoksaidi. 

Kazula anawashukuru wadau hao wa maendeleo kwa juhudi za kushirikiana na serikali kupanda miti ili kurudisha hifadhi ya mazingira ambayo ilikuwa imeanza kupotea kutokana na ongezeko la ukataji miti ovyo.

‘’Tunawashukuru Helvetas Tanzania kwa kushiriki kupanda miti wilaya ya Meatu ambao watatusaidia kufikia malengo ya upandaji miti…mpango wetu kila Halmashauri ni kupanda miti milioni 1.5 na kufanya mkoa mzima kuwa na jumla ya miti milioni 9 kwa mwaka mzima’’ Anasema Kazula.

Anasema wanaendelea kushirikiana na Wakala wa Misitu (TFS) pamoja na wazalishaji wengine wa miti ikiwemo kampuni ya Alliance ginnery ili kuifanya Simiyu kuwa ya kijani, huku akimtaka kila mwananchi kupanda miti mitano mitano katika eneo analoishi.

Anaongeza kuwa kupitia Helvetas Tanzania wamejikita zaidi kupanda miti kwenye taasisi za umma ikiwemo shule za msingi na sekondari, makanisani, misikitini pamoja na zahanati ili miti hiyo iweze kusimamiwa ipasavyo.

Oscar Kanuda mkazi wa Lubiga anawataka wananchi wenzake kushiriki kikamilifu upandaji miti katika maeneo yao ili waweze kurejesha uoto na asili hali ambayo tapungua majanga ya asili ikiwemo ukosefu wa mvua na ukame.

‘’Tunaishukuru serikali na wadau kwa kutuletea miti mpaka majumbani kwetu, niwaombe wananchi wenzangu tupande miti ili iweze kutusaidia baadae…miti inaleta mvua, inazuia upepo na pia inatunza vyanzo vya maji’’ anasema Kanuda.

Dotto Saimon Mwanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Lubiga aliwashukuru wadau wa mazingira kwa kuwaletea miti shuleni kwao ambapo alisema ikikua itazuia upepo, itatunza mazingira na vyanzo vya maji pia wataweza kupata kuni.

Naye Kabula Salehe mwanafunzi wa darasa la saba Lubiga shule ya msingi aliwataka wafunzi wenzake kuendelea kuitunza miti hiyo itakayowasaidia wanafunzi kupata hewa safi na kivuli wawapo shuleni.

Leticia Erasto mwanafunzi wa shule ya sekondari Lubiga anasema ameshiriki zoezi la upandaji miti shuleni hapo, huku akiwataka walimu kuwagawia wanafunzi kila mmoja miche ya miti ili aweze kuisimamia kuliko kuipanda kiholela.

‘’Tunawashukuru wadau walioleta miti shuleni, lakini niwashauri walimu wetu kila mwanafunzi agawiwe miti angalau miwili apande na kuisimamia hadi ikue ili tuweze kufika lengo la serikali pamoja na wadau la kupanda miti’’ anasema Mwanafunzi huyo.

Leticia anaiomba serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya faida za upandaji miti ambapo baadhi ya maeneo yameathiriwa na ukosefu wa mvua, ukame na kuongezeka kwa joto ili jamii iweze kubadilika na kupanda miti ya kutosha.

Costantine Phabian, Afisa Kilimo kutoka Kampuni ya Alliance Ginnery anasema kampuni yao inajikita na kilimo hai ambacho hakitumii kemikali za viwandani na kinasaidia utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji.

Anasema wanashirikiana na Helvetas kwenye mradi wa kilimo hai na ndani yake wanapanda miti katika kata za Kisesa na Lubiga ambapo Alliance wanahudumia wakulima kwenye vikundi vya kilimo hai wakiwa na lengo moja na kutunza mazingira.

‘’sisi sote ni wadau wa mazingira, lengo la kilimo hai ni kuhifadhi mazingira na kutunza uoto wa asili, kurutubisha ardhi na kulinda vyanzo vya maji pamoja na viumbe wengine…tunafundisha wakulima kuhifadhi ardhi na kutokata mito ovyo’’ anasema Phabian.

Uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Masuala ya Jamii (ESRF) mwaka 2003 umebainisha kuwa mambo makuu yanayosababisha umaskini ni uchumi duni, uharibifu wa mazingira na kukosekana kwa utawala bora.

Sera ya Mazingira ya mwaka 1997 imeainisha matatizo makuu sita ya mazingira yanayoikabili nchi yetu, ambayo ni Uharibifu wa ardhi, Kutopatikana kwa maji safi kwa wakazi wa mjini na vijijini, Uchafuzi wa mazingira, Upotevu wa makazi ya viumbe pori na bioanuai, Uharibifu wa makazi ya viumbe wa majini na Uharibifu wa misitu.

Kutokana na Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998, Sera ya Taifa ya Hifadhi za Mazingira ya mwaka 2004 na Programu mbalimbali za kuhamasisha upandaji miti kila mwaka, ni dhahiri kuwa Serikali inahimiza wananchi na taasisi zishiriki kikamilifu katika suala la kupanda miti. 

Upandaji miti unaweza kufanywa na taasisi za serikali, makampuni ya wawekezaji, vikundi vya jamii, shule na hata watu binafsi na Watanzania wengi sasa hivi wanaelewa kuwa uchumi wa nchi na maisha yanategemea sana mazingira bora. 

Miti inaweza ikapandwa peke yake ikawa msitu, mti mmoja mmoja katika shamba, kuzunguka shamba, katika maeneo ya makazi, kando kando ya barabara na penginepo kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu.

Mzee Oscar Kanuda (kushoto) akiwa na wanakiji wenzake wakishiriki zoezi la upandaji miti lililofanyika hivi karibuni shule ya msingi Lubiga, zoezi hilo liliratibiwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Helvetas Tanzania.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Lubiga iliyopo wilaya ya Meatu mkoa Simiyu wakishiriki zoezi la upandaji miti lililokuwa likiendeshwa na shirika la Helvetas Tanzania hivi karibuni.
Wanafunzi wa shule ya msingi Lubiga iliyopo wilaya ya Meatu mkoa Simiyu wakishiriki zoezi la upandaji miti lililokuwa likiendeshwa na shirika la Helvetas Tanzania hivi karibuni.
AFISA Mazingira wilaya ya Meatu Thomas Shishwa (aliyechumaa) akikata kiriba kwa ajili ya kupanda miti shule ya msingi Lubiga iliyoko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.
Share:

KITUO CHA ELIMU, USHAURI-TAASISI YA USTAWI WA JAMII CHAPIGA KAMBI SOKO LA KARUME


Banda la kituo cha elimu ushauri na msaada wa kisaikolojia cha Taasisi ya Ustawi wa Jamii lililopo katika uwanja wa ukumbi wa Jiji ilala ambapo huduma ya ushauri na elimu inatolewa bure kwa wafanyabiashara wahanga wa moto uliotokea soko la mchikichini karume Ilala Jijini Dar es Salaam.

Kutoka Kushoto mwenyekiti wa wafanyabiashara walemavu soko la mchikichini Mzee Juma Hamis akisikilizwa kwa umakani mkubwa na maafisa ustawi wa jamii Rukia Mwinyi kutoka kituo cha elimu, ushauri, na msaada wa kisaikolojia (Taasisi ya Ustawi wa Jamii) pamoja na Bi. Lilian Chilo afisa Ustawi wa jamii kutoka Ofisi ya Jiji la Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanya biashara waliofika kwenye uwanja wa ukumbi wa jiji Ilala soko la mchikichini kupata huduma ya ushauri na elimu kutoka kwa maafisa Ustawi wa jamii wa kituo cha elimu na ushari cha Taasisi ya Ustawi wa Jamii na Jiji la Dar es salaam.

Msaikolojia kutoka kituo cha elimu na ushauri Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Zainab Rashid akitoa huduma kwa mfanya baishara mlemavu Bw. Jamal Nassoro Lemu wa soko la mchikichini Ilala ambapo huduma ya elimu na ushauri inatolewa kwa wafanyabiashara wahanga wa moto sokoni hapo hasa wale wenye mahitaji maalum.

Mratibu wa kituo cha elimu, ushauri na msaada wa kisaikolojia Bi Rufina Khumbe akimhudumia mfanyabiashara wa bajaj eneo la soko la mchikichini Bi Ashura Sadiki katika uwanja wa ukumbi wa jiji ilala Dar es Salaam.

Maria Mayanzini afisa ustawi wa Jamii wa kituo cha elimu na ushauri na msaada wa kisaikolojia – Taasisi ya Ustawi wa Jamii akimsikiliza kwa makini mmoja wa wafanya biashara waliofika kupata huduma katika banda la kituo cha elimu na ushauri cha Taasisi ya Ustawi wa Jamii.

****************

Timu ya wataalam wa ustawi wa jamii na saikolojia kutoka kituo cha elimu, ushauri na msaada wa kisaikolojia kilicho chini ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii imepiga kambi viwanja vya ukumbi wa jiji, Dar es Salaam kutoa huduma ya elimu, ushauri na msaada wa kisaikolojia.

Huduma hiyo inatolewa bure kwa wafanyabiashara wa soko la mchikichini maarufu Karume, hususani; walio katika kundi maalum, ambao ni wahanga wa janga la moto lilitokea Januari 16, mwaka huu.

Mratibu wa kituo hicho cha elimu na ushauri Bi. Rufina Khumbe amesema Taasisi ya Ustawi wa Jamii iliona ni vyema kwenda kutoa huduma hiyo kwa waathirika wa janga hilo ambao wanauhitaji mkubwa kwa wakati huu.

“Taasisi imekuwa ikitoa huduma kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha tunastawisha jamii yetu, kwa kutatua changamoto mbalimbali pia kama Taasisi mama chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum tumeguswa, na ni jukumu la kituo chetu cha ushauri kuja kutoa huduma ya elimu hii na ushauri ili wafanyabiashara hawa hasa wenye uhitaji waweze kulipokea hilo na kulikubali kama changamoto” alisema Bi Khumbe.

Bi. Rufina ameongeza kuwa kutokana na janga hilo la moto wengi wao wamekata tamaa ya maisha, kwasababu mali zilizokuwa zinawaingizia kipato na mitaji vimeteketea na moto huku wengine walichukua mikopo ili kukuza na kuanzisha biashara.

"Mali zimeteketea na hawajui wanalipaje hiyo mikopo. Ndio maana Taasisi ikaona ni vyema kuongea na wafanyabiashara hawa ili kuwapa tumaini tena la maisha yao," amesema Bi. Rufina.

Kwa upande wake msaikolojia kutoka Kituo hicho Dkt.Zainabu Rashidi amesema “tunatoa elimu juu ya kujikinga na majanga mbalimbali ikiwa ni pamoja na moto, mafuriko na pia tunatoa elimu ya namna ya kuyakubali na kuishi na majanga na matatizo baada ya kutokea”.

Aidha Dkt. Zainabu amesema watu wengi wanajua wakifika katika banda la Taasisi ya Ustawi wa Jamii (kituo cha elimu shauri na msaada wa kisaikolojia) watapata msaada wa fedha kwa ajili ya mitaji yao ya biashara.

“Jamii yetu haina uelewa juu ya umuhimu wa huduma ya ushauri na msaada wa kisaikolojia kama tiba ya namna ya kupata suluhu ya matatizo yao kwa kuzungumza na wataalam. Jamii haiamini katika ushauri pekee hivyo tuko hapa ili kuondoa hiyo dhana” amesema Bi. Zainabu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye ulemavu soko la Mchikichini (karume), mzee Juma Hamisi amesema anashukuru Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa elimu,ushauri, na msaada wa kisaikolojia.

“Tumepokelewa vizuri tumepata msaada wa ushauri wa kisaikolojia na elimu na tumewasikia, elimu hii inatupa ujasiri na tumejua kuwa janga hili lililotupata sio letu tu bali ni letu sote” amesema mzee Juma na kuongeza:

“Naishukuru serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu kwa kusikia sauti yetu na kuja kutupa msaada wa kisaikolojia na ushauri”.

Zaharan Sulemani mfanyabiashara wa leso, soksi na madaftari katika soko hilo ametoa shukrani kwa Taasisi na kusema kuwa elimu hiyo imewapa ujasiri wa kuanza upya.

“Tunashukuru Taasisi ya Ustawi wa Jamii kwa kuja kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisaikolojia kwa wahanga wa janga la moto pia namshukuru mama Samia Suluhu Hassan kwa kutuweka sisi wamachinga kwenye kundi maalumu chini ya Wizara hii ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwani tunaaini tutapata usaidizi na usimamizi wa karibu zaidi utakaotufaidisha katika biashara tunazofanya”.

Pia Jumanne Kongogo mwenyekiti wa jumuia ya wafanyaniashara sokoni hapo ametoa wito kwa wafanyabiashara wa soko la karume kwenda kupata huduma hiyo ya elimu na ushauri kwenye banda la Taasisi ya Ustawi wa Jamii.

Ameiomba serikali iangalie jinsi itakavyo jenga soko ambalo miundombinu yake itakidhi kwa wafanyabiashara wenye uhitaji maalumu .

Naye mratibu wa huduma za ustawi wa Jamii kutoka Mkoa, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Jiji la Dar es Salaam Bi. Lilian Chilo ametoa wito kwa wafanyabiashara wa soko la mchikichini kujitokeza kupata huduma inayoendelea kutolewa katika uwanja wa ukumbi wa jiji Ilala kwa siku kumi na nne (14) ambapo huduma hiyo ilianzia katika viwanja vya mnazi mmoja.

Taasisi ya Ustawi wa Jamii chini ya Wizara mpya ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaunga mkono jitihada za Mh. Rais kutambua wamachinga kama kundi maalum, pamoja na makundi mengine katika jamii yetu.

Zaidi kwa kutoa kipaumbele na umuhimu wa pekee kwa makundi haya kupata huduma za Ustawi wa Jamii ili kuinua na kuboresha hali zao maisha na hasa pindi kunapotokea majanga mbali mbali kama hili la moto katika soko la mchikichini karume.

Taasisi ya Ustawi wa Jamii itaendelea kutoa ushauri wa kitaaluma na ushauri nasaha na msaada wa kisaikolojia kwa jamii ya watanzania na makundi maalum kama sehemu ya jukumu lake la kutoa ‘’Ushauri Weledi” katika fani bobezi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger