Monday, 9 August 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 9,2021



























Share:

UKWELI KUHUSU CHANJO YA CORONA NA NGUVU ZA KIUME....POMBE


Mkurugenzi wa Kuratibu Utafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk. Paul Kazyoba.
**
WATAALAMU wa afya nchini wamebainisha hakuna uhusiano kati ya chanjo na kuongeza nguvu za kiume.

Mkurugenzi wa Kuratibu Utafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk. Paul Kazyoba, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam juzi alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu chanjo ya UVIKO-19.

Alisema hakuna utafiti uliofanywa kuhusu uhusiano wa chanjo ya Johnson & Johnson inayotolewa nchini na kuongeza au kupunguza nguvu za kiume.

“Licha ya kuwa hakuna utafiti uliofanywa kwetu sisi wanaume tuliochanja, mimi binafsi sikuona mabadiliko yoyote kuhusu nguvu za kiume kama ni hasi au chanya, kwa maana hiyo ninaweza kusema chanjo hii haina uhusiano na suala hili,” alisema Dk. Kazyoba.

POMBE MARUFUKU

Kuhusu unywaji wa pombe, Dk. Kazyoba, alisema inashauriwa kuwa anayetaka kuchanja, anapaswa kutokunywa pombe siku tatu kabla na baada ya kuchanja.

“Ni ngumu ‘kum-control’ (kumdhibiti) mtu mmoja mmoja asinywe pombe lakini ni muhimu wakazingatia hili hasa ikizingatiwa kuwa chanjo haifanyi kazi kwenye mwili wa binadamu mara tu baada ya kuchanja,” alisema.

Dk. Kazyoba alisema mgonjwa anayekiuka masharti na kunywa pombe kabla na baada ya kuchomwa chanjo, yupo katika hatari ya kupata madhara kwenye ini.

Alisema kuwa madhara yatajitokeza kwenye ini kwa sababu lina kazi ya kuchuja sumu katika mwili, hivyo litalazimika kuanza kupambana na sumu ya pombe wakati huo huo kupokea chanjo inayoingia mwilini.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani na Mbobezi wa Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Tatizo Sanga, alisema chanjo huanza kufanya kazi kwenye mwili wa mtu kuanzia siku saba hadi 15.

Alisema baada ya mtu kuchoma chanjo, mwili huanza kujipanga kutengeneza utaratibu wa kuipokea kabla ya kuanza kufanya kazi ndani ya wiki mbili.

MAGONJWA SUGU

Kuhusu watu wenye magonjwa sugu kupata chanjo, Dk. Sanga alisema ni muhimu kundi hilo kupewa chanjo ili kuwaepusha na mashambulizi ya UVIKO-19 yanayoweza kuwaweka katika hatari tofauti na wasio na magonjwa hayo.

“Watu wenye matatizo ya moyo ni muhimu kupata chanjo ili waepuke changamoto ya upumuaji inayoongeza shambulizi kwenye mwili na kuleta uwezekano wa mgonjwa kupoteza maisha,” alifafanua Dk. Sanga.

Chanzo - NIPASHE
Share:

Sunday, 8 August 2021

ZITTO KABWE : CHANJO YA CORONA NI SALAMA



Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe licha ya kuipongeza Serikali kwa hatua ya kuruhusu chanjo ya corona kuingizwa nchini, lakini amesema kunatakiwa kuwapo na mkakati maalumu wa kuhamasisha wananchi dhidi ya corona ambao utaongozwa na watu wanaoaminika kwenye jamii tofauti na ilivyo sasa.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Agosti 8, 2021 wakati akifungua kikao cha dharura cha kamati kuu ya chama hicho mjini Unguja chenye ajenda moja ya kujadili hali ya kisiasa nchini.

“Napongeza maamuzi sahihi ya Serikali ya kuruhusu chanjo ziingizwe nchini ili kuwapa kinga Watanzania na kuulinda mfumo wetu wa afya dhidi ya wagonjwa wengi ambao bila kinga hautaweza kuhimili. Hata hivyo, bado kuna kazi kubwa zaidi ya kufanya kwenye uhamasishaji wa watu kujitokeza kupata chanjo. Nitoe rai kwa kila mmoja wenu, nikianza na wanachama wa ACT Wazalendo kufuata taratibu na kupata chanjo mapema iwezekanavyo”


“Napenda kuwahakikishia kuwa nimejiridhisha chanjo zilizoruhusiwa kuingia nchini ni salama na mimi pia nimekwisha chanjwa na niko salama salimini. Nipende kuwaasa kuwa kuchanjwa ni suala la hiari lakini tunapoangalia usalama wa wapendwa wetu, jamii yetu na watanzania wenzetu basi hatuna budi kuhakikisha tunafanya maamuzi sahihi”

“Niweke bayana kuwa ni lazima kuwepo na mkakati maalum wa uhamasishaji dhidi ya Korona ambao utaongozwa na watu wanaoaminika kwenye jamii, na sio watu wale wale ambao walituambia kuwa Tanzania imeishinda Korona, ama watu wale wale ambao walituaminisha kunywa malimau na tangawizi ni kutibu Corona.”

“Hatuwezi kuwa na utekelezaji bora wa sera mpya za kupambana na Korona iwapo tutaendelea kuwa na sura zile zile zilizotuaminisha kutumia njia zisizoshauriwa Kisayansi”

“Vile vile niendelee kusisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote ikiwemo kuepuka mikusanyiko, kuvaa barakoa na kunawa kwa maji tiririka na sabuni kila wakati pamoja na kutumia vitakasa mikono ili kujikinga na maambukizi na pia kuzuia kusambaa kwa maambukizi”

“Kwa upande wa Serikali zote mbili, ya Muungano na ya Zanzibar, hatua madhubuti zichukuliwe kuongeza elimu kwa wananchi kwani kwa mwaka mzima walikuwa wanaambiwa hakuna Korona, hivyo kuwaambia kuwa sasa ipo sio jambo rahisi kueleweka. Jitihada zifanyike kwenye kutoa elimu sahihi kwa Umma” amesema Zitto Kabwe
Share:

SAUDIA YAFUNGUA MIPAKA KWA MAHUJAJI WALIOCHANJWA CHANJO YA CORONA



SAUDIA ARABIA itaanza kuwapokea wageni waliopata chanjo ya Covid-19 katika mji mtukufu wa Kiislamu wa Makka ikiwa kama sehemu ya ibada ya umrah, ni takriban miezi 18 tangu kuifunga mipaka yake baada ya kuzuka janga la virusi vya corona.

Shirika la habari la Saudia limesema Wizara ya Hijja na Umrah imetangaza kuanzia kesho Jumatatu watapokea maombi ya raia na wakazi wake wanaotaka kushiriki ibada ya Umrah.

Lakini pia baadaye watapokea maombi kutoka mataifa mbalimbali ya nje, ruhusa hiyo hata hivyo imetolewa kwa masharti kwamba mahujaji wote wa kigeni lazima wawe wamepata chanjo inayotambuliwa na Saudi Arabia na wakubali kukaa karantini.

Ibada ya Umrah ambayo kwa kawaida inafanyika katika kipindi chochote cha mwaka, ilifunguliwa tena Oktoba kwa mahujaji wa ndani, baada ya kufungwa kabisa kutokana na mlipuko wa janga la virusi vya corona.
Share:

ASKOFU GWAJIMA : SIJALISHWA SUMU NA HAITATOKEA

Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima mbaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe jijini Dar es salaam amekanusha madai kuwa amelishwa sumu kutokana na msimamo wake kuhusu chanjo ya UVIKO -19.

Akizungumza leo Jumapili Agosti 8, 2021 wakati wa ibada kanisani kwake kuwa hajalishwa sumu nahakuna wa kumnywesha sumu na hatotokea.

"Wanataka kusingizia watu, labda kusingizia kwamba serikali imeninywesha sumu. Niwahakikishie kwamba hakuna serikali imemnywesha sumu Gwajima kwa kuwa serikali ndiyo inasema chanjo ni hiari. Suala la afya ya mtu linapaswa kulindwa na mtu mwenyewe. Labda nitoe changamoto kwa wanaojiita watalaam waje walete andiko linaloonyesha kemikali zilizopo kwenye chanjo", amesema Gwajima.
Share:

MWILI WA ELIAS KWANDIKWA WAWASILI NYUMBANI KWAKE BUTIBU USHETU SHINYANGA


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akiongoza mamia ya waombolezaji waliofika katika msiba wa aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, John Elias Kwandikwa kijijini kwake Butibu Kata ya Kinamapula Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga.
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Ulinzi John Elias Kwandikwa uikisindikizwa na Makamanda wa JWTZ kutoka kwenye nyumba yake kuelekea eneo maalum kwa ajili ya kutoa nafasi kwa wana Ushetu kuaga mwili huo kijijini kwake Butibu Kata ya Kinamapula Halmashauri ya Ushetu Shinyanga.
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Ulinzi John Elias Kwandikwa uikisindikizwa na Makamanda wa JWTZ kutoka kwenye gari maalum la kijeshi ili kupelekwa nyumbani kwake kabla ya kuendelea na taratibu za kuaga mwili huo kijijini kwake Butibu Kata ya Kinamapula Halmashauri ya Ushetu Shinyanga.
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Ulinzi John Elias Kwandikwa ukiwa umewasili kijijini kwake Butibu Kata ya Kinamapula Halmashauri ya Ushetu Shinyanga kwa ajili ya wananchi wa wake kuanza kujiweka tayari kuanza taratibu za kuaga na baadaye kesho kuwekwa katika nyumba yake ya milele.
Makamanda wa Jeshi la JWTZ wakitoa heshima kwa viongozi mbalimbali waliofika nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi Marehemu John Elias Kwandikwa kwa ajili ya kuanza taratibu za kuaga na baadaye kesho kupumzisha mwili huo katika Nyumba yake ya milele kijijini kwake Butibu Kata ya Kinamapula Halmashauri ya Ushetu Shinyanga.(Picha zote na Anthony Ishengoma).
Share:

SITA WAKAMATWA SAKATA LA MAAFISA ARDHI KUPIGWA, MALI KUCHOMWA MOTO MOROGORO



Na Farida Saidy Morogoro

Maofisa kutoka idara ya ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero wamenusurika kifo baada ya baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Melela kata ya Chita halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kushambulia gari la mkurugenzi wa hamalshauri hiyo walilokuwa wakitumia na kulichoma moto pamoja na pikipiki.

Inadaiwa wananchi hao walichukua uamuzi huo baada maofisa hao kufika kwenye shamba la mwekezaji ambaye anadaiwa kwa muda mrefu hajaliendeleza shamba hilo, inadaiwa wananchi walivamia shamba hilo na kuanza kuishi zaidi ya miaka 20 sasa.

Maofisa hao walipofika walitaka kufanya upimaji ndipo wakavamiwa na gari kuwashambulia na kuchomwa moto.

Kufuatia tukio hilo, watu sita wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kuchoma moto mali mbalimbali za serikali ikiwemo gari aina ya Land Cruiser ,pikipiki tatu,kifaa cha kupimia mipaka ya mashamba na kompyuta mpakato 3.

Akizungumza na waandishia wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Fortunatus Musilim amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Melela kata ya Chita Wilaya ya Kilombero,ambapo watuhumiwa walitenda kosa hilo baada ya maofisa wa Ardhi kufika katika shamba linalomilikiwa na marehemu Daud Balali ambaye alikuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Aidha Musilim ameongeza kuwa katika tukio hilo dereva aliyefahamika kwa jina la Damas Sanga (51 ) alijeruhiwa baada ya wananchi hao kumkukuta kwenye gari na kuanza kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kwa upande wake Kamishina msaidizi wa Ardhi mkoa wa Morogoro Frank Minzikuntwe amesema vurugu hizo zimetokea baada ya maamuzi ya serikali ya kulipima shamba hilo ili liweze kupangwa upya matumizi yake baada ya kutelekezwa kwa muda mrefu huku wananchi wanalolizunguuka wakikosa maeeneo ya kulima.



Share:

RAIS SAMIA AWASILI DODOMA AKITOKEA DAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kusaili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo tarehe 08 Agosti,2021 akitokea Jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo tarehe 08 Agosti,2021 wakati akitokea Jijini Dar es Salaam alikofanya Shughuli mbalimbali za Kitaifa .

Share:

Nafasi Mpya za Kazi Serikalini,NGOs na Makampuni Binafsi

Kama unatafuta kazi kwa muda mrefu bila mafanikio, basi hii ni nafasi yako!! Hapa kuna  Nafasi za kazi zaidi ya 300 zilizotangazwa wiki hii .
 
Chagua unayoitaka hapo chini

_________

 1.Nafasi za Kazi 100 NGOs mbalimbali Tanzania  <<Bofya Hapa>>

2.Nafasi za Kazi  70, Sekta Binafsi( Makampuni binafsi) <<Bofya Hapa>>

3.Nafasi za Kazi serikalini  <<Bofya Hapa>>

____________

BOFYA HAPA KWA NAFASI ZAIDI ZA KAZI



Share:

Naibu Waziri Mabula Ahimiza Uwajibikaji Sekta Ya Ardhi


 Na Munir Shemweta, MUSOMA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka watendaji wa sekta ardhi katika halmashauri na Manispaa za mkoa wa Mara kuwajibika kwa kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanatoa hati kwa wamiliki wa ardhi pamoja na kuhamasisha ukusanyaji kodi ya pango la ardhi .

Akizungumza na watumishi wa sekta ya ardhi mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara, Dkt Mabula alisema ufanyaji kazi kwa kujituma kwa watumishi wa sekta hiyo itaiwezesha wizara ya ardhi kuongeza kasi ya utoaji hati na wakati huo kukusanya mapato yatokanayo na kodi ya ardhi.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi, kwa sasa katika mkoa huo Mara kasi ya utoaji hati za ardhi pamoja na makusanyo yatokanayo na kodi ya ardhi hairidhishi na juhudi kubwa zinahitajika katika kutoa hati na kuhamasisha wamiliki kulipa kodi ili serikali iweze kupata fedha za kuendesha shughuli zake mbalimbali.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mara Bi. Hapiness Mtutwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 uliweza kukusanya shilingi bilioni 1.065 sawa na asilimia 23 katika malengo ya bilioni 4 huku mwaka wa fedha 2020/2021 ukikusanya bilioni 1.7 sawa na asilimia 47.5 kati ya malengo bilioni 3.7.

‘’Maelekezo yangu mkafanye kazi kwa bidii  katika wilaya zenu na nikikuta mtendaji wa sekta ya ardhi hafanyi haya ninayoelekeza basi  ujue wewe hutufai’  alisema Dkt Mabula

Mkurugenzi Msaidizi idara ya Maendeleo ya makazi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Imaculata Senje aliwataka watendaji wa sekta ya ardhi hasa wale wa Mipango Miji kuwa wabunifu kwa kuwaelimisha wananchi umuhimu wa maeneo yao kupimwa.

‘’Kuna miji midogo inakuwa kwa kasi katika maeneo yenu na inawezekana kama Afisa Mipango Miji ukasema huna kazi lakini unaweza kuanza kwa ktuoa elimu kwa mtu mmoja mmoja ukieleza umuhimu wa eneo lake kupangwa na kupima na kumilikishwa’’ alisema Bi. Senje.

Naye Afisa Kodi Kutoka Wizara ya Ardhi Rehema Kilonzo aliwaeleza watendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Mara kuhakikisha wanayajua na kufuatilia kwa karibu madeni ya wadaiwa wote sugu wa kodi ya pango la ardhi na kubainisha kuwa, pamoja na Wizara kuelewa changamoto zilizopo kwenye mfumo lakini bado watendaji hao wana nafasi ya kujua madeni halisi ya wadaiwa na hivyo kuwafanya kuwa katika sehemu salama kwenye utendaji wao.


Share:

Sebene Mpya : MAGENHIRO - JAMBO

 

Msanii Magenhiro anakualika kusikiliza Wimbo wake mpya kuhusu Jambo.. Burudika hapa chini na Sebene hii kali kutoka kwa  Director Manyero
DOWNLOAD AUDIO <HAPA<
Share:

TTS Cash Analyst at Citi Bank

TTS Cash Analyst    The position has primary responsibility for supporting the  TTS Head TZ and the Cash  Product team TZ  in developing and managing, end-to-end, the cash management products. Specifically role involves assisting in preparation, and distribution of daily, weekly and monthly financial reports – revenue as well as balance sheet movement reports, assistance […]

This post TTS Cash Analyst at Citi Bank has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

TTS Trade Analyst at Citi Bank

TTS Trade Analyst    The principal purpose of this position is to provide assistance to TTS trade product team and the TTS head n preparation of reports, providing analysis on Balance sheet, revenue, customer metrics, coordination with Banking, operations, Markets and other functional partners  . Additionally, the role involves the preparation, analysis and distribution of […]

This post TTS Trade Analyst at Citi Bank has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Project Officer- MEEL at CARE

Project Officer- MEEL   CARE Tanzania-DMDP positions: CARE is a leading humanitarian organization dedicated to fighting poverty and social injustice with a special emphasis on women and girls. CARE Tanzania is part of CARE International, whose vision is to seek a world of hope, tolerance, and social justice, where poverty has been overcome and people […]

This post Project Officer- MEEL at CARE has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

WATU 105,745 TAYARI WAMEPATA CHANJO YA CORONA TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata chanjo ya UVIKO-19 Julai 28,2021 ikiwa ni sehemu ya uzinduzi ili ianze kutumiwa na Watanzania katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona wimbi la Tatu.

Na Veronica Mrema

Watu 164,500 wamejiandikisha kupata chanjo ya CORONA na kati yao 105,745 tayari wamepata chanjo hiyo, kulingana na tathmini iliyotolewa leo Jumapili Agosti 8,2021 na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Tathmini hiyo inaeleza idadi hiyo ya watu ni ndani ya siku 11, ikihesabiwa tangu Julai 28, mwaka huu hadi kufikia Agosti 7, mwaka huu ilipozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Ikulu ndogo ya Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Abel Makubi amesema idadi hiyo ya watu ni katika makundi ya walengwa waliotajwa katika kipaumbele.

" Serikali inachukua hii nafasi kuwapongeza sana wananchi na viongozi walengwa kwa mwitikio mkubwa wa kuchanja," amesema.

CHANZO - MATUKIO NA MAISHA BLOG

Share:

MUHOJA AZINDUA MAKAMBI ,AWATAKA WAUMINI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UVIKO - 19

Meneja wa makambi Usharika wa Ndembezi unao jumuisha makanisa manne ya Ngokolo, Ibadakuli, Bugweto na Ndembezi Deusi Muhoja akizindua makambi hayo yatakayodumu kwa muda wa siku 7.

******
Meneja wa makambi Usharika wa Ndembezi unao jumuisha makanisa manne ya Ngokolo, Ibadakuli, Bugweto na Ndembezi Deusi Muhoja amezindua makambi hayo yatakayo dumu kwa muda wa siku 7.

Akizindua makambi hayo,Muhoja amewaasa waumini wa kanisa la Waadventista Wasabato na waumini wa Madhehebu mengine
kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO 19 kwa kufuata maelekezo na ushauri una tolewa na wataalamu wa Idara ya afya mkoani humo

Muhoja ambaye pia ni Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ametoa wito huo Agosti 7, 2021 katika hafla fupi ya uzinduzi wa makambi ya waumini wa Kanisa la waadventista Wasabato yatakayodumu kwa muda wa siku 7 yakihudhuria na viongozi pamoja na waumini wa kanisa la wasabato kutoka katika makanisa manne yanayounda usharika huo.

Amesema ni wajibu wa waumini kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UVIKO 19 pamoja na kuendelea kumuomba
Mungu ili aweze kusaidia kuliepusha taifa na janga hilo.

Muhoja ametoa wito kwa madhehebu ya dini mengine hapa nchini kushirikiana na serikali katika katika jitihada za kupambana na janga hilo kwa kuchukua tahadhari na kumuomba Mungu.

Muhoja amewataka waumini wakanisa hilo kuhakikisha wanavaa barakoa pamoja na kuhakikisha wananawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni kabla ya kuingia katika maeneo ya kanisa hilo.

Kwa upande wao baadhi ya waumini wa kanisa la Waadventista Wasabato Ndembezi wameahidi kuzingatia maelekezo na utaratibu unaotolewa na viongozi wa kanisa katika kuhakikisha waumini pamoja na wananchi wanashiriki makambi kwa kuchukua taadhari dhidi ya ugonjwa wa UVIKO -19
Meneja wa makambi Usharika wa Ndembezi unao jumuisha makanisa manne ya Ngokolo, Ibadakuli, Bugweto na Ndembezi Deusi Muhoja akizindua makambi hayo yatakayo dumu kwa muda wa siku 7.
Share:

Project Team Leader at CARE

Project Team Leader    CARE Tanzania-DMDP positions: CARE is a leading humanitarian organization dedicated to fighting poverty and social injustice with a special emphasis on women and girls. CARE Tanzania is part of CARE International, whose vision is to seek a world of hope, tolerance, and social justice, where poverty has been overcome and people […]

This post Project Team Leader at CARE has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger