Saturday, 31 July 2021

KATIBU MKUU WA UVCCM KENANI KIHONGOSI AWAAGIZA WENYEVITI NA MAKATIBU WA CCM KUANZISHA KLABU ZA MAZOEZI

 


Na Dotto Kwilasa, DODOMA.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kenani Kihongosi amewaagiza Wenyeviti na makatibu wa Chama hicho kwa ngazi ya mikoa  kuanzisha utaratibu wa Club  za mazoezi kwa kila Mkoa ili kuwahamasisha vijana kufanya mazoezi ili kuimarisha afya.

Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Vijana Joging Club uliofanyika kwa lengo la  kuwapa fursa vijana kuwa na utayari wa kufanya mazoezi mara kwa mara kuepukana na maradhi hasa ya Corona.

Akiongea kwenye uzinduzi huo Kihongosi amesema Jumuiya hiyo imezindua program hiyo ambayo itawahusu vijana kwa nchi nzima na sio Dodoma peke yake huku ikiongozwa na kauli mbiu ya"amani yetu,maisha yetu".

"Fanyeni mazoezi mjikinge na magonjwa,hasa katika kipindi hiki ambapo dunia inapambana na corona,"amesema.

Mbali na hayo Katibu huyo pia ametumia nafasi hiyo kuwashawishi watanzania hususani vijana,kuona umuhimu wa kuungana na Serikali Katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona  kwa kukubali kupokea chanjo ya ugonjwa huo ambayo tayari imeshaingia nchini.

"Sisi kama vijana tunampongeza Mama yetu Samia kuleta suala la chanjo kwenye nchi yetu kwani linatuhakikishia usalama wa afya zetu hivyo ni wajibu wetu kujitokeza na kuepuka kusikil8za watu wanaopotosha,"amesisitiza.

Kupitia uzinduzi huo Katibu huyo wa jumuiya ya Vijana wa CCM amefikisha ujumbe pia kwa watanzania kuepukana na maneno ya kuyumbishwa kwani yanaweza kuvuruga amani ya nchi .

"Nchi yetu itajengwa na sisi watanzania,kumbukeni amani yetu ndiyo  maisha yetu,amani ikitoweka ni sisi tunaotaabika,"amesema.

Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewahakikishia kuwapa ushirikiano  vijana kwenye masuala ya michezo.

"Michezo ni ajira,ni matumaini yangu jumuiya hii ya UVCCM itaendelea kuwaandaa vijana ,nami naahidi kushirikiana na Katibu wa UVCCM kuunga mkono juhudi za Rais wetu Samia Suluhu Hassan  tukiwa  bega kwa bega kuhakikisha vijana wetu wanakuwa mstari wa mbele Katika kutetea na kulinda afya zao,"amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Bill Chidabwa ameeleza kuwa michezo ni fursa  kwa  vijana kwani huwakutanisha, kuwaunganisha na kuwapa ajira.

Share:

MAWAZIRI WA MAWASILIANO NA HABARI WAZINDUA MFUMO ULIOBORESHWA WA LESENI TCRA

Share:

Naibu Waziri Kundo Amtumbua Meneja Wa TTCL Kagera, Shirika La Posta Kagera Kuchunguzwa


Na Faraja Mpina, BUKOBA
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew ametengua uteuzi wa Meneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wa Mkoa wa Kagera Bi. Irene Shayo kuanzia tarehe 30/07/2021 kwa kile kilichobainika kuwa taratibu za uteuzi wake zilikiukwa na utumishi wake umekuwa wa kusuasua, amekuwa akikwepa ziara za viongozi katika eneo lake pamoja na kupika taarifa za mapato na matumizi

Mhandisi Kundo ameyazungumza hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Kagera ambapo alitembelea ofisi za TTCL na Shirika la Posta Tanzania (TPC) na kuona kuwa Meneja wa TTCL katika Mkoa wa Kagera hatoshi kuwa katika nafasi hiyo ukizingatia Kagera ni mkoa wa kimkakati kwasababu unapakana na nchi takribani nne hivyo  Meneja wake anatakiwa kuwa na uwajibikaji wenye ufanisi mkubwa

“Ninaagiza Meneja wa Mkoa wa Kagera aondoshwe mara moja katika Mkoa wa Kagera na kuanzia leo asitambulike kama Meneja wa Mkoa wa Kagera, taratibu zifuatwe na apangiwe kazi zingine kulingana na wasifu wake kitaaluma ili aweze kufanya kazi vizuri kwasababu majukumu ya sasa hana uwezo nayo”, alizungumza Mhandisi Kundo

Ameongeza kuwa wao kama Wizara kupitia kwa Waziri mwenye dhamana Dkt. Faustine Ndugulile wana kasi ya kutaka kuona matokeo ya kile ambacho Serikali imedhamiria kukifanya kwa watanzania katika Sekta ya Mawasiliano

Amesisitiza kuwa ili kufanikisha hilo ni wajibu wao kufanya maamuzi ya kuhakikisha taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo zinaimarisha mifumo ya utendaji kazi katika ngazi za mikoa na utoaji wa huduma bora zinazokidhi mahitaji ya watanzania

Katika hatua nyingine Mhandisi Kundo alitembelea na kukagua ukarabati wa Ofisi za Shirika la Posta Bukoba zilizogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 78,801,000 na kutorudhishwa na kiasi cha fedha kilichotumika kwasababu hakiendani na hali halisi ya ukarabati uliofanywa na kuagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini gharama halisi zilizotumika katika ukarabati huo

BONYEZA HAPA KUJUA VITUO VITAKAVYOTOA CHANJO YA CORONA TANZANIA

“Nimetoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Moses Machali  aunde kamati itakayohusisha wataalam wa Ujenzi, TAKUKURU na Ofisi ya Usalama wa Taifa (W) ili wakafanye tathmini na kujiridhisha kile ambacho kimefanyika na iwapo ikibainika kuna watu ambao wamefanya ubadhirifu wa fedha za umma watachukuliwa hatua za kisheria

Sambamba na hilo ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL na PostaMasta Mkuu wa Shirika la Posta kuhakikisha mameneja wao wa Mikoa ambao hawana vigezo na uwezo wa kuongoza Mikoa hasa ile ya  kimkakati wanaondolewa na kuwekwa watu wenye uwezo na vigezo vya kuongoza katika Mikoa hiyo

Mhandisi Kundo yupo katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Kagera kwa ajili ya kukagua miundombinu ya mawasiliano na upatikanaji wa huduma za mawasiliano ambapo ametembelea katika wilaya ya Muleba, Bukoba na Misenyi na amepanga kuendelea katika Wilaya za Kyerwa, Karagwe na Ngara. Ziara yake katika Mkoa huo ilianza tarehe 29 Julai hadi tarehe 2 Agosti 2021

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari




Share:

Mhandisi Masauni Aridhishwa Na Utendaji Wa Shirika La Bima La Taifa

 Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amelipongeza Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa kuongeza ufani na kuboresha utendaji kazi wa Shirika hilo na kufanikiwa kuongeza kiwango cha uwekezaji kutoka sh. bilioni 85 mwaka 2018/2019 hadi kufikia shilingi bilioni 245 Mwaka 2020/2021.

Mhandisi Masauni ametoa pongezi hizo alipotembelea Makao Makuu ya Shirika la Bima la Taifa Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Shirika hilo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Taasisi zote zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango, baada ya kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo.

“Moja ya eneo lililonivutia ni namna Shirika hili lilivyoboresha huduma zake na  mapato kwa kutumia mifumo ya TEHAMA, kutoka asilimia 10 za miaka ya nyuma hadi kufikia asilimia 95 katika kipindi cha miaka miwili tu iliyopita” Alisema Mhe. Masauni

Ameuagiza uongozi wa Shirika hilo kuongeza ubunifu na bidii zaidi na kuhakikisha kuwa linakuwa Shirika bora zaidi la Bima hapa nchini, Ukanda wa Afrika Mashariki na nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Aidha, alitoa wito kwa wananchi kutumia huduma za Bima zinazotolewa na Shirka hilo la Umma na kuahidi kuwa Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kuliunga mkono na kulisaidia liweze kutimiza malengo yake ya kuwahudumia wananchi kikamilifu.

Akitoa taarifa ya utendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Dkt. Elirehema Doriye alisema katika kipindi kifupi cha miaka miwili iliyopita ambacho NIC imefanya mageuzi na mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa Shirika, Shirika limewekeza kiasi hicho cha shilingi bilioni 245 sawa na ufanisi wa silimia 136.05.

“Katika kipindi hicho pia Shirika limelipa madai mbalimbali ya Bima ya Maisha yaliyohakikiwa kwa wateja wetu, kiasi cha shilingi bilioni 15.8 kati ya shilingi bilioni 22.53 ambazo shirika  linadaiwa, hatua iliyosababisha kurejea kwa imani ya wateja na kuvutia wateja wapya kujiunga na huduma zinazotolewa na Shirika, na tunatarajia kulipa madeni yote kabla ya mwaka 2021 kuisha” Alisema Dkt. Doriye

Dkt. Doriye alimweleza Mhe. Masauni kwamba Shirika lake pia linazidai Taasisi na Mashirika mbalimbali ya Umma ambazo hazijalipia Bima za Maisha za mali zao kiasi cha shilingi bilioni 34.42 na kwamba fedha hizo zikipatikana zitaongeza mtaji wa Shirika na uwezo wa kuwahudumia wateja wao.

Aidha, alisema kuwa NIC inaandaa bidhaa mpya ikiwemo kuanzisha Bima ya Mifugo na kubuni bidhaa nyingi zaidi za Kilimo ili kuchangia juhudi za Serikali za kuinua sekta za ufugaji, kilimo na viwanda.
Mwish



Share:

Serikali Ya Zanzibar Yaapa Kuulinda Muungano

 Na mwandishi wetu, Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuulinda Muungano kwa kuwa ndio tunu kubwa ambayo imeachwa na waasisi wa Muungano huo na kwamba Serikali haitotumia nguvu kwa baadhi ya wananchi wenye maoni taofauti bali itawaelimisha.

Ahadi hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla wakati alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulioongozwa na Waziri wa Wizara hiyo Balozi Liberata Mulamula (Mb) na kuongeza kuwa Zanzibar inatambua umuhimu wa Muungano uliopo pamoja na manufaa yake huku akitolea mfano kwa baadhi ya Wazanzibar wanaoishi Bara ambao ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameongeza kuwa kwa sasa Serikali imeweka kipaumbele katika masuala ya kuimarisha uchumi na kuwaletea Wazanzibar maendeleo kutokana na umoja, amani na mshikamano uliopo tangu uwepo wa muafaka wa Serikali ya Kitaifa na kuwataka wafanyabiashara na wawekezaji kujitokeza kuwekeza visiwani humo katika sekta mbalimbali ikiwemo eneo la Uchumi wa Buluu.

BONYEZA HAPA KUJUA VITUO VITAKAVYOTOA CHANJO YA CORONA TANZANIA


Akizungumza wakati wa kujitambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano uliopo katika utendaji kazi na kwamba kwa sasa Wizara inaendelea na maandalizi ili kuwawezesha Viongozi wakuu wa pande zote mbili kushiriki kikamilifu katika mikutano ya Kimataifa.

Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukiongozwa na Balozi Liberata Mulamula ambaye ameambatana na Naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine pamoja na Naibu Katibu Mkuu Balozi Fatma Mohammed Rajab na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara hiyo uko visiwani Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha kwa viongozi wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Share:

Usajili Wa Wakulima Washika Kasi

 Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na TAMISEMI, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Serikali za Mitaa zinaendelea na usajili wa wakulima kwenye mfumo wa M-Kilimo ili waweze kutambuliwa, kutoa huduma kwa njia ya simu na pia Serikali kutoa huduma zingine kwa urahisi.

Mpaka sasa hivi zaidi ya nusu ya mikoa yote Tanzania Bara, Mikoa 14 imeweza kusajili na kufikia asilimia 50 au zaidi kwenye mfumo huo wa M-Kilimo.

Akizungumzia hali ya usajili wa wakulima mpaka hivi sasa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Prof. Siza Tumbo amesema kuwa Mikoa 12 bado ipo chini ya asilimia 50 kwenye usajili wa wakulima.

Prof. Tumbo ameeleza kuwa Mikoa minne (4) ambayo ni Njombe, Arusha, Simiyu na Singida imeweza kufikia lengo la asilimia 100 na zaidi. Wizara ya Kilimo inaipongeza sana mikoa hii kwa kufikia hatua hiyo.

Amesema kuwa Mikoa ya Shinyanga, Kagera na Dar-es-Salaam bado wapo chini ya asilimia 30, hivyo kuwasihi kuongeza kasi ili kufikia malengo ya Serikali.

Pia, Wizara ya Kilimo inatoa shukrani za dhati kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Watendaji Wakuu na Wakati kayika ngazi ya Mikoa na Wilaya/Halmashauri na Maafisa Kilimo na Wagani wote kwa kazi kubwa ya kuwezesha, kuhamasisha na kusajili wakulima kwenye mfumo wa M-Kilimo.

BONYEZA HAPA KUJUA VITUO VITAKAVYOTOA CHANJO YA CORONA TANZANIA



Share:

Je, Unasumbuliwa na Tatizo la Kisukari na Nguvu za Kiume?...SUPER NHESHA ni Tiba Sahihi. Bofya Hapa Kujua Zaidi


SUPER – NHESHA
Ni dawa ya kutibu tatizo la sukari au jina la kitaalamu (Diabetes Mellitus) ni kundi la magonjwa yanayohusiana na ufanyaji kazi wa mwili ambapo Mtu anakuwa na kiwango kikubwa cha sukari aina ya Glucose katika mwili kutokana na mwili wake kukosa uwezo wa kutengeneza Insulin ya kutosha au seli za mwili wake kutumia insulin iliyopo au pengine mwili kuwa na matatizo yote kwa pamoja na kupelekea mgonjwa wa sukari kupata haja ndogo mara kwa mara (Polyuria) uhisi kiu kila wakati (Polydipsia) Na (Polyphagia).


AINA YA KISUKARI
Kuna aina chache tofauti za ugonjwa wa kisukari (1) ni ugonjwa wa Auto hii aina mgonjwa wa Auto hushambulia mfumo wa kinga na kuharibu seli katika kongosho ambako insulin huzalishwa asilimia 10% ya watu wenye ungonjwa wa kisukari wanayo aina hii (Auto).


AINA YA PILI
Hii hutokea wakati mwili wako unakuwa sugu kwa insulin na sukari hujenga katika damu yako hii husababishwa na kuwa na sukari nyingi kwenye damu yako kuliko kawaida.


CHANZO CHA UGONJWA SUKARI
Viko vyanzo vingi mbalimbali vya sukari
1.     Shinikizo la damu (B.P)
2.     Viwango vya juu vya triglyceride (mafuta)
3.     Lishe yenye mafuta mengi na wanga
4.     Utumiaji mkubwa wa pombe kupita kiasi
5.     Ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi
6.     Mtindo wa maisha usiofaa kiafya
7.     Uzito na unene uliozidi
8.     Kutofanya mazoezi
9.     Umri
10.     Kurith


UNAJUAJE KUWA UNADALILI ZA KISUKARI
1.     Kusikia njaa mara kwa mara
2.     Kusikia kiu mara kwa mara
3.     Kupungua uzito
4.     Maono machafu
5.     Uchovu mara kwa mara
6.     Ukipata kidonda hakiponi
7.     Kushuka kwa kinga mwili


DALILI ZA KISUKARI KWA MWANAUME
Mbali na dalili za jumla za ugonjwa wa sukari wanaume wenye tatizo hilo wanakuwa na upungufu wa nguvu za kiume na kushindwa kufanya tendo la ndoa uume hushindwa kusimama misuri hulegea na kusinyaa, maumivu ya mgongo, kiuno, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kupata choo  kama cha mbuzi


DALILI ZA WANAWAKE
Wanawake wenye ugonjwa wa sukari wanaweza pia kuwa na dalili kama vile maambukizi kwa njia ya mkojo (U.T.I) maambukizi  ya gonzi kukakamaa


TIBA YA MAGONJWA YA SUKARI
Ugonjwa wa sukari unatibika bila kujali ni mda gani umepata hilo tatizo wengi wamekata tama na kuwa wabishi amini tatizo hili linatibika vizuri sana wengi wemepona.


Tumia dawa ya SUPER-NHESHAambayo ni dawa ya miti shamba yaani (asilia) ambayo humfanya mtu kupona na kuimalika kabisa.


Tutakuelekeza pia mfumo wa mtindo wa maisha utakao takiwa kutumia ili kutoluhusu tatizo hilo kurudi tena.


BABU MADUHU ANAPATIKANA MAGOMENI MOROCCO/KANISANI NJIA PANDA YA KWENDA SINZA  SIMU: 0652 102 152/0788 330 105/ 0755 684 297 NYOTE MNAKARIBISHWA PIA TUNATUMA MIKOANI WHATAPPS NO 0652 102 152 



Share:

HESLB Yampongeza Rais Samia Ongezeko La Bajeti Ya Mikopo

Na Mwandishi Wetu,
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua ya Serikali kuongeza bajeti ya Mikopo ya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2021/2022 yenye kiasi cha TZS 570 Bilioni iliyoweka historia katika taasisi hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi tarehe 31 Julai, mwaka huu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema ongezeko la bajeti hiyo ni kielelezo cha dhamira ya dhati ya Serikali ya kusaidia Watanzania wahitaji.

Badru alisema katika bajeti hiyo yenye uwezo wa kusomesha wanafunzi 160,000, imewalenga wanafunzi wahitaji wanaotokea katika kaya zisizojiweza na hivyo kuwataka kuhakikisha kuwa wanakamilisha taratibu za maombi kama zilivyoanishwa katika mwongozo wa uombaji mikopo wa mwaka 2021/2022.

Kwa mwaka jana bajeti yetu ilisomesha wanafunzi 55,000 wa mwaka wa kwanza na kwa mwaka huu tunaratajia kusomesha wanafunzi 62,000 hii ni idadi kubwa kwa mwaka huu, tunawaomba wanafunzi wahitaji kuhakikisha wanaomba kwa usahihi” alisema Badru.

Akizungumzia kuhusu hali ya urejeshaji Mikopo, Badru alisema kwa sasa kumekuwa na mwitikio mkubwa kwa wanafunzi wanufaika kurejesha mikopo yao kwa hiari, hatua iliyotokana na Serikali kufuta tozo na adhabu mbalimbali zilizokuwepo awali.

Kuanzia Mwezi Julai mwaka huu, kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanufaika kurejesha mikopo yao, na hapa katika maonesho tumeshuhudia wanufaika wengi wakifika katika Banda kwa ajili ya kupata taarifa za madeni ya mikopo” alisema Badru.

Aidha Badru alisema HESLB itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo waajiri ili kuhakikisha kuwa madeni ya mikopo kutoka kwa wanafunzi wanufaika inarejesha ili kuiwezesha Serikali kuwa na Mfuko endelevu.

BONYEZA HAPA KUJUA VITUO VITAKAVYOTOA CHANJO YA CORONA TANZANIA



Share:

MWANZA FRIENDS WAKUTANA SHINYANGA MJINI KUZINDUA KATIBA ,KUSAKA FURSA ZA UWEKEZAJI


Mwenyekiti wa Mwanza Friends Association, Patrick Joseph akionesha Katiba na Nyaraka mbalimbali za Kikundi cha Mwanza Friends Association.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wanachama wa Kikundi cha Wafanyabiashara na Watumishi wa Umma  Marafiki kutoka Mwanza maarufu ‘Mwanza Friends Association’ wanaofanya shughuli zao kwenye mikoa mbalimbali nchini Tanzania wamekutana Mjini Shinyanga kwa ajili ya kikao na kuzindua rasmi Katiba yao pamoja na kutafuta fursa za uwekezaji katika Mkoa wa Shinyanga.

Wanachama hao wa Mwanza Friends Association wamefanya kikao chao kilichoambatana na ziara ‘Tour’ mkoani Shinyanga leo Jumamosi Julai 31 katika Hoteli ya Liga Mjini Shinyanga.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Mwanza Friends Association, Patrick Joseph amesema walianzisha kikundi hicho mwaka 2014 kwa lengo ya kusaidiana katika shida na raha.

“Kikundi cha Marafiki kutoka Mwanza 'Mwanza Friends Association' chenye Makao yake Makuu Jijini Mwanza kinaundwa na Wafanyabiashara na Watumishi wa Umma wanaotoka Mkoa wa Mwanza lakini sasa wanaishi kwenye mikoa mingine nchini”,amesema Joseph.

“Sisi tunajihusisha na masuala ya kusaidiana kijamii katika shida na raha. Hivi sasa tuna wanachama 35 na tuna miradi ukiwemo mradi wa VIP Bar iliyopo Maduka Tisa Ilemela Jijini Mwanza”,ameeleza.

Amesema wanachama wa Mwanza Friends Association kutoka mikoa mbalimbali nchini wameamua kufanya kikao chao Mjini Shinyanga na kuzindua rasmi Katiba yao ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kutafuta fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga.

Joseph ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wanaotaka kujiunga na Mwanza Friends Association na kuwaomba wawasiliane na Mwenyekiti wa Mwanza Friends Association kwa simu namba 0755 863 330 (Patrick Joseph) au Katibu Omary Haji (0653261226).

ANGALIA PICHA HAPA
Mwenyekiti wa Mwanza Friends Association, Patrick Joseph akionesha Katiba ya Kikundi cha Mwanza Friends Association wakati wa kikao cha Wanachama wa kikundi hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Mjini Shinyanga leo Jumamosi Julai 31,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Mwanza Friends Association, Patrick Joseph akizungumza wakati akifungua kikao cha Wanachama wa kikundi hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Mjini Shinyanga leo Jumamosi Julai 31,2021. Kulia ni Mweka Hazina, Respicius Rwegoshora, kushoto ni Katibu, Omary Haji.
Mwenyekiti wa Mwanza Friends Association, Patrick Joseph akizungumza wakati akifungua kikao cha Wanachama wa kikundi hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Mjini Shinyanga leo Jumamosi Julai 31,2021.
Mwenyekiti wa Mwanza Friends Association, Patrick Joseph akizungumza wakati akifungua kikao cha Wanachama wa kikundi hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Mjini Shinyanga leo Jumamosi Julai 31,2021.
Mwenyekiti wa Mwanza Friends Association, Patrick Joseph akiwakaribisha wanaotaka kujiunga na Mwanza Friends Association na kuwaomba wawasiliane na Mwenyekiti wa Mwanza Friends Association kwa simu namba 0755 863 330 (Patrick Joseph) au Katibu Omary Haji (0653261226).
Katibu wa Mwanza Friends Association Omary Haji akizungumza kwenye kikao cha Wanachama wa kikundi hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Mjini Shinyanga leo Jumamosi Julai 31,2021.
Mweka Hazina wa Mwanza Friends Association, Respicius Rwegoshora akizungumza kwenye kikao cha Wanachama wa kikundi hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Mjini Shinyanga leo Jumamosi Julai 31,2021.
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakiwa kwenye kikao
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakiwa kwenye kikao
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakiwa kwenye kikao
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakiwa kwenye kikao
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakiwa kwenye kikao
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakiwa kwenye kikao
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakiwa kwenye kikao
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakiwa kwenye kikao

Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakila chakula cha pamoja Liga Hotel Mjini Shinyanga.
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakila chakula cha pamoja Liga Hotel Mjini Shinyanga.
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakila chakula cha pamoja Liga Hotel Mjini Shinyanga.
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakila chakula cha pamoja Liga Hotel Mjini Shinyanga.
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakila chakula cha pamoja Liga Hotel Mjini Shinyanga.
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakila chakula cha pamoja Liga Hotel Mjini Shinyanga.
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakila chakula cha pamoja Liga Hotel Mjini Shinyanga.
Mweka Hazina wa Mwanza Friends Association, Respicius Rwegoshora akipata chakula
Katibu wa Mwanza Friends Association Omary Haji akipata chakula
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakila chakula cha pamoja Liga Hotel Mjini Shinyanga.
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakila chakula cha pamoja Liga Hotel Mjini Shinyanga.
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakila chakula cha pamoja Liga Hotel Mjini Shinyanga.
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakipiga picha ya kumbukumbu Liga Hotel Mjini Shinyanga.
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakipiga picha ya kumbukumbu Liga Hotel Mjini Shinyanga.
Wanachama wa kikundi cha Mwanza Friends Association wakipiga picha ya kumbukumbu Liga Hotel Mjini Shinyanga leo Jumamosi Julai 31,2021.


Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA ATOA NENO FEDHA ZINAZOKUJA NCHINI KWA AJILI YA NGOs

 

MBUNGE wa Viti Maalumu CCM (NGOs Tanzania Bara) Neema Lugangira akizungumza  wakati wa  Uzinduzi wa Wiki ya Azaki imefanyika Jijini Dar es Salaam Julai 29 Julai 2021

MBUNGE wa Viti Maalumu CCM (NGOs Tanzania Bara) Neema Lugangira amesema wakati umefika kuhakikisha fedha za ufadhili ambazo zinatoka nje ya nchi zinazokuja nchini ziweze kufanyiwa kazi na kutelezwa na NGOs na CSOs kutoka ndani ya nchi.

Aliyasema hayo Siku ya Uzinduzi wa Wiki ya Azaki imefanyika Jijini Dar es Salaam Julai 29 Julai 2021 ambapo alisema takwimu zinaonyesha kwamba zile fedha ambazo zinazoingia kwa ajili ya Sekta ya Azaki ni asilimia 1 pekee yake ndio zinaekwenda kwa CSOs, NGOs ambazo zimeanzishwa na Watanzania.

Mbunge Lugangira alisema kwa sababu takwimu zinaonyesha asilimia 99 ya fedha zinazotoka nje zinapita kupitia mashirika ambazo sio ya kiserikali lakini ni ya Kimataifa 
 
Alisema  ili miradi iwe endelevu lazima NGOs/CSOs za ndani ziweze kushiriki katika utekelezaji wa miradi hiyo na ndio maana mara nyingi wanaona kuna miradi fulani ukishaasha ufadhili na mfadhili akishaondoka mradi unakuwa hauendelei.

Alisema pia mara nyingi Sekta ya Azaki wanahesabiwa kama sehemu ya Sekta Binafsi lakini Sekta Binafsi ni tofauti zaidi kwa sababu wale ni wafanyabiashara zaidi na wanapokwenda kuongea mwakilisha Sekta Binafasi hawezi kuwakilisha Sekta ya Azaki.

“Nimejaribu kutoa changamoto kama wadau mnatambulika kama sekta inayosimama inachangia kwenye maendeleo ili kufanya hivyo lazima waonyeshe mchango wao dhahiri ni upi ili waweze kutambulika”Alisema

Hivyo alisema ni matarajio yake itapoandaliwa wiki ya Azaki mwezi Octoba mwaka huu basi watapata majawabu kwenye eneo hilo na watafanya mikakati madhubiti ya kutoka asilimia 1 na iongezeke



Share:

TVMC YATOA ELIMU UKATILI WA KIJINSIA, LISHE MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA


Mratibu wa Miradi wa Shirika lisilo Kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la Mjini Shinyanga, Mary Mahanya (kulia) akizungumza katika banda la TVMC kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Julai 31,2021.

Shirika la TVMC limeshiriki Maonesho hayo  kwa kuelimisha wananchi kuhusu kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto, kutoa elimu ya masuala ya Lishe zikiwemo njia sahihi za kunyonyesha mtoto na kutoa msaada wa Kisheria  ili kusaidia kutatua migogoro mbalimbali kama vile ya ardhi na ndoa.

Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayoongozwa na kauli mbiu “Uwekezaji wa Madini na Viwanda Shinyanga kwa Uchumi Endelevu” yameanza tarehe 23 Julai, yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 1 Agosti, 2021.

Mratibu wa Miradi wa Shirika lisilo Kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la Mjini Shinyanga, Mary Mahanya (kulia) akielezea huduma zinazotolewa na TVMC kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
 Afisa Utawala wa Shirika lisilo Kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la Mjini Shinyanga, Chiku Hamis akionesha kipeperushi kinachoelezea masuala ya Lishe kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
 Afisa Utawala wa Shirika lisilo Kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la Mjini Shinyanga, Chiku Hamis akionesha kipeperushi kinachoelezea masuala ya Lishe kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger