Saturday, 10 July 2021

Waziri Jafo Akipa Kiwanda Cha Tanzania Raidar Miezi Mitatu Kubadilisha Mfumo Wa Maji Taka

Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo, ametoa miezi mitatu kwa kiwanda cha Tanzania Raidar Company Limited kubadilisha mfumo wa maji taka. Ameyasema hayo alipotembelea kiwanda hicho kilichopo maeneo ya Kisarawe II Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es salaam.

Mhe. Jafo ametembelea kiwanda cha Raidar kinacho jishughulisha na urejerezaji wa taka za plastiki kuwa bidhaa aina ya mabomba na chupa za plastiki. Akiwa katika ziara hiyo amebaini utiririshwaji wa maji machafu kutoka kiwandani hapo kwenda katika makazi ya watu na kupelekea uchafuzi wa mazingira na malalamiko kutoka kwa wananchi wanaokaa karibu na kiwanda hicho.

“Nimefurahishwa na kiwanda hiki kurejereza taka kwani inasaidia kutoa taka zinazozagaa mtaani, hii ni njia nzuri ya utunzaji wa mazingira, lakini kitendo cha kutiririshaji wa maji machafu kutoka kiwandani na kwenda kwenye makazi ya watu sio suala zuri kiafya na kimazingira. Hivyo natoa miezi mitatu kuhakikisha tatizo hilo linashughulikiwa na sitaki kusikia malalamiko tena” Mhe. Jafo

Vile vile Mhe. Jafo ametembelea kiwanda cha Gueng Cheng Industry Limited kilichopo Kisarawe II Wilaya ya Kigamboni Mkoa wa Dar es Salaam, kiwanda kinachozalisha mafuta machafu yanayotokana na matairi yaliyotumika.  Mhe. Jafo Amesema kuwa kiwanda hiki kinalalamikiwa na wananchi kutokana na moshi mwingi na vumbi linalotokana na uchomaji wa matairi kiwandani hapo.

“Sijaridhika kabisa na utendaji wa kazi katika kiwanda hiki, natoa miezi sita kuhakikisha mitambo inayotumika ibadilishwe ili kuzuia moshi unaokwenda kwenye makazi ya watu ambao unaathari kubwa kiafya kwa wananchi pamoja na mazingira. Pamoja na hayo kiwanda hiki kipo katika makazi ya watu hivyo ni bora kutafuta eneo lingine ili isiwe usumbufu kwa wakazi hao. Pia naiagiza NEMC kufatilia hili na baada ya miezi sita nitarudi kuangalia utekelezaji” Mhe. Jafo

Kwa upande wake meneja wa NEMC Mashariki Kusini Bw. Hamad Taimuri, amesema kuwa amepokea maelekezo ya Mhe. Waziri Jafo na ufuatiliaji wa viwanda vyote viwili utafanyika ili kuhakikisha wanafanya uzalishaji wao bila ya kuathiri mazingira na Afya kwa watu. Ameendelea kusema kuwa ni kweli wamepata malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya uchafuzi wa mazingira kutoka katika viwanda hivyo na watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Naye Mkazi wa Kisarawe II Bw. Said Bomeza, ameiomba Serikali kufuatilia suala hili kwani wananchi wanateseka sana na wawekezaji wasiozingatia sheria. Ameendelea kusema kuwa japo kiwanda kinachotoa moshi wamepewa miezi sita lakini Maisha ya watu yako hatarini hivyo ingekuwa bora baada ya miezi sita kufatilia hilo na kukiwajibisha kiwanda hicho.

Waziri Jafo pia ametembelea kiwanda cha Lake Cement Limited kiwanda cha kuzalisha saruji kilichopo Kimbiji Wilaya ya Kigamoni jijini Dar es Salaam, kujionea namna wanavyofanya uzarishaji wake bila ya kuathiri mazingira na afya kwa watu. Mhe. Jafo amekipongeza kiwanda hicho kwa wanavyotunza mazingira na amewataka wazarishaji wengine wa saruji kuiga mfano wa tekinolojia wanayotumia ambayo haichafui mazingira.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Fatma Nyangasa, amesema kuwa Wilaya ya kigamboni inauwekezaji wa viwanda hivyo kama ofisi ya wilaya kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kigamboni itaendelea kukagua viwanda hivyo ili kuhakikisha kunakuwa na uwekezaji wenye tija kwa maslahi ya Taifa.

Share:

WATU 284 KATI 408 WANAOUGUA CORONA TANZANIA WANATUMIA MITUNGI YA OKSIJENI

Tanzania imeanza kutoa takwimu ya watu walioambukizwa virusi vya corona ambapo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amesema hadi kufikia Julai 8, 2021 jumla watu 408 walibainika kuwa na ugonjwa wa Corona huku 284 wakitumia mitungi ya Hewa ya Oksijeni.

Dk Gwajima ametoa taarifa hiyo leo Jumamosi Julai 10, 2021 wakati akitoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwenye mnada wa Msalato jijini Dodoma.

Rais Samia Suluhu Hassan mara kwa mara amekuwa akiwakumbusha Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na kujilinda dhidi ya wimbi la tatu la janga la corona.

Katika moja ya ziara yake akiwa njiani kutoka Dodoma Rais Samia alielezea kushangaa kuona mamia ya watu bila barakoa.
Share:

SHULE 10 BORA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2021

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa Kidato Cha Sita mwaka 2021 pamoja na matokeo ya mtihani wa ualimu.

                                         πŸ‘‰πŸ‘‰MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA (ACSEE) 2021

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza  na kutaja shule kumi bora zilizofanya vizuri katika mtihani huo.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema shule iliyoshika nafasi ya kwanza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2021 ni Kisimiri ya mkoani Arusha iliyokuwa na watahiniwa 72.

Msonde amesema Kemebos ya Kagera yenye watahiniwa 35 imeshika nafasi ya pili ikifuatiwa na Dareda ya Manyara watahiniwa 101.

Nafasi ya nne imechukuliwa na Tabora Girls yenye watahiniwa 100 ikifuatiwa na Tabora Boys yenye watahiniwa 120.

Nafasi ya sita imeshikwa na Feza Boys ya mkoa wa Dar es Salaam iliyokuwa na watahiniwa 71 ikifuatiwa na Mwandet ya Arusha yenye watahiniwa 53.

Zakia Meghji imeshika nafasi ya nane ikitokea mkoani Geita. Ilikuwa na watahiniwa 31, ikifuatiwa na Kilosa ya Morogoro yenye watahiniwa 91, na Mzumbe watahiniwa 135.
Share:

RAIS MWINYI ATEUA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU MAKATIBU WAKUU

Share:

RAIS MWINYI AWATUMBUA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI, TAASISI NA WATENDAJI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amewasimamisha kazi Wakurugenzi wote wa halmashauri za wilaya za Unguja, baadhi ya Wakurugenzi wa Taasisi na Idara za Serikali, pamoja na Watendaji wengine waliobainika kuhusika na wizi, kutowajibika kazini na ubadhirifu wa mali za Serikali.

Dkt. Mwinyi ametangaza kuwasimamisha kazi Watendaji hao katika mkutano wa majumuisho baada ya kuhitimisha ziara yake katika mikoa mitatu ya Unguja.

Baadhi ya Watendaji waliosimamishwa kazi ni Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ya Mjini, Magharibi A na B, Kaskazini A na B, Kusini, wilaya ya Kati pamoja na Mkurugenzi wa SMIDA.

Akitangaza uamuzi huo, Dkt. Mwinyi amewataka Watendaji wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kubadilika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Amesema kumekuwa na mikataba mingi ya kifisadi inayofanyika katika baadhi ya halmashauri za wilaya, na kutolea mfano halmashauri ya wilaya ya Mjini ambayo imeingia mikataba ya aina hiyo na kampuni za simu pamoja na mikataba katika uwekaji wa mabango.

Share:

HAWA NDIYO WANAFUNZI BORA 10 WALIOFANYA VIZURI KATIKA MASOMO YA SAYANSI MATOKEO KIDATO CHA SITA 2021

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa Kidato Cha Sita  mwaka 2021 pamoja na matokeo ya mtihani wa ualimu.

Bofya Hapa chini Kutazama

πŸ‘‰πŸ‘‰MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA (ACSEE) 2021

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha sita ya mwaka 2021 na kutaja wanafunzi kumi bora waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi.

Akizungumza leo Jumamosi Julai 10, 2021 visiwani Zanzibar wakati akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amemtaja Perucy Astus Mussiba kutoka shule ya Canossa, Dar es Salaam kuwa kinara wa matokeo hayo, katika masomo ya sayansi mchepuo wa PCB.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Donard Rulers Mosile kutoka Shule ya Sekondari Kisimiri (Arusha) kutoka PCB. Cretus Amos Mihayo kutoka Tabora Boys (Tabora) PCB akishika nafasi ya tatu akifuatiwa na Ismail Mtumwa kutoka Kibaha Sekondari(Pwani) PCM aliyeshika nafasi ya nne.

Nafasi ya tano imechukuliwa na Olais Julius Mollel kutoka Kisimiri (Arusha) PCM akifuatiwa na Geofrey Sanga aliyeshika nafasi ya sita kutoka Tabora Boys (Tabora) PCM.

Anord Msanga kutoka Tabora Boys (Tabora) PCM akichukua nafasi ya saba Caroline Mpale amechukua nafasi ya nane kutoka Canossa Sekondari( Dar es Salaam) akichukua mchepuo wa PCM.

Nafasi ya tisa na kumi imechuukuliwa na wanafunzi kutoka Feza Boys (Dar es Salaam) PCM John Bugeraha aliyechukua nafasi ya tisa na Harry Mshana aliyechukuwa nafasi ya kumi.
Share:

Video : BEXY - AVOCADO

Share:

Breaking News : TAZAMA HAPA MATOKEO YA MTIHANI KIDATO CHA SITA 2021, UALIMU 2021

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa Kidato Cha Sita  mwaka 2021 pamoja na matokeo ya mtihani wa ualimu.

Bofya Hapa chini Kutazama

πŸ‘‰πŸ‘‰MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA (ACSEE) 2021

Share:

Mpyaa : PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ILIYOBORESHWA ZAIDI 2021...HABARI BURE MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO

Share:

How to check Form Six Results 2021/2022

Release of 2021 Advanced Certificate of Secondary Education Examination (ACSEE) results Following Two years of studies in secondary school, students must prepare for the final and most important hurdle, The Advance Certificate of Secondary Education Examination (ACSEE). After completing their exams, students need not endure long queues or waste time and resources travelling to school […]

This post How to check Form Six Results 2021/2022 has been posted by Udahiliportal

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

WAZIRI SIMBACHAWENE ARUHUSU KUTUMIKA KWA NYUMBA ZA ASKARI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene ameruhusu askari polisi kuanza kutumia nyumba za kisasa zenye uwezo wa kukaliwa na familia zaidi ya 300 zilizopo eneo la Kunduchi na Mikocheni mkoani Dar es salaam.

Waziri Simbachawene amesema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi huo wa nyumba za kisasa za makazi ya askari.

Amesema kuanza kutumika kwa nyumba hizo kutasaidia kupunguza uhaba wa nyumba za askari, na kutaleta ufanisi kwa askari wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za Kipolisi.

Kwa upande wake mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro amesema zaidi ya miaka mitatu imepita tangu kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa nyumba hizo.

Amesema baadhi ya nyumba hizo kwa sasa zimeanza kuchakaa kutokana na kutokaliwa kwa muda mrefu, pamoja na kukosa matunzo.

Share:

Bancassurance Manager at Alliance Insurance

BANCASSURANCE MANAGER   Alliance Life Assurance Ltd was established in 2010 as the first locally privately owned Life Insurance Company in Tanzania. The company has spread its sphere of influence throughout the region to become one of the leading insurance and financial services companies in East Africa providing life insurance solutions to both corporates and […]

This post Bancassurance Manager at Alliance Insurance has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Chief Operating Officer (COO) at Alliance Insurance

CHIEF OPERATING OFFICER (COO)   The Role: We are looking for an experienced Chief Operating Officer (COO) to join our team! As a COO, you will be responsible for planning, directing, and overseeing the company’s operational policies, rules, initiatives, and goals to help the organisation execute long-term and short-term plans and directives by implementing judgement, […]

This post Chief Operating Officer (COO) at Alliance Insurance has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Data clerk officers at Job Junction

Data clerk  officers Details Employer name :Job Junction Tanzania Minimum Qualification:Diploma/Bachelor Years of Experience :1 years Main Job Task and Responsibilities   Maintains database by entering new and updated customer and account information. Prepares source data for computer entry by compiling and sorting information. Establishes entry priorities. Processes customer and account source documents by reviewing […]

This post Data clerk officers at Job Junction has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Human Resources Manager at RTI

Research Triangle Institute (RTI) has over 30 years’ experience assisting governments, communities, and the private sector in managing their environment and natural resources. We have delivered innovative, breakthrough solutions in key development sectors including: countering wildlife crime, forestry, protected area management, climate change, economic livelihood development, community engagement, and institutional capacity building. Project Description The […]

This post Human Resources Manager at RTI has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

ICT Associate – Dar es Salaam at UN Women

Background   UN Women, grounded in the vision of equality enshrined in the Charter of the United Nations, works for the elimination of discrimination against women and girls; the empowerment of women; and the achievement of equality between women and men as partners and beneficiaries of development, human rights, humanitarian action and peace and security. […]

This post ICT Associate – Dar es Salaam at UN Women has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

WAWEKEZAJI VITALU VYA NARCO WATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA MIKATABA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akizungumza na wawekezaji waliochukua vitalu katika Ranchi ya Mabale wilayani Misenyi Mkoa wa Kagera ambapo amewaagiza kuhakikisha wanayatumia maeneo hayo kwa malengo yaliyokusudiwa kwani wasipofanya hivyo watanyang’anywa na kupatiwa wawekezaji wengine.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Mifugo na Uvuvi na wawekezaji katika Ranchi ya Mabale wilayani Misenyi Mkoa wa Kagera ambapo pia amewaeleza kuwa wizara inamalengo ya kuhakikisha uzalishaji wa mifugo na mazao yake unaongezeka.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akiwa kwenye kitalu namba 2 kinachomilikiwa na mfugaji, Primus Karokola (kulia) wakati alipotembelea kitalu hicho kuangalia mifugo iliyopo kwenye Ranchi ya Mabale wilayani Misenyi Mkoa wa Kagera. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki aliyesimama katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge (wa pili kutoka kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel (wa kwanza kulia), Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Prof. Faustine Kamuzora (wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Prof. Peter Msoffe (wa kwanza kushoto) mara baada ya kumalizika kwa kikao kifupi kilichofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi kutoka wizarani na wawekezaji wa vitalu mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika kwenye moja ya kitalu katika Ranchi ya Mabale wilayani Misenyi Mkoa wa Kagera.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki amewataka wawekezaji kwenye vitalu vya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kufuata taratibu zilizowekwa kulingana na mikataba yao.

Ndaki ameyasema hayo wilayani Misenyi Mkoa wa Kagera wakati alipotembelea Ranchi ya Mabale na kuzungumza na baadhi ya wawekezaji wenye mifugo katika vitalu hivyo.

Waziri Ndaki amesema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wawekezaji kuchukua vitalu na kutovitumia kama ilivyoelekezwa kwenye mikataba kitu ambacho kinasababisha maeneo kuwa mapori na kuvamiwa na watumiaji wengine wa ardhi.

Wizara kupitia NARCO imejipanga kuhakikisha wafugaji wanapata maeneo ya vitalu kwa ajili ya kufugia kitu ambacho kitasaidia kuondokana na tatizo la malisho na kupunguza migogoro ya ardhi kati ya wafugaji na watumiaji wengine.

“Hivyo wizara kwa sasa imejipanga kuhakikisha wawekezaji katika vitalu wanatumia maeneo hayo kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanalipa kodi kwa wakati,” alisema Waziri Ndaki.

Vilevile alisema kuwa wizara kwa sasa inaiona NARCO kama ni sehemu ya kotokea kwani kupitia kampuni hiyo wizara itaweza kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuongeza kipato wa wafugaji.

Akiwa katika Ranchi hiyo Waziri Ndaki amemtaka mwekezaji wa Kampuni ya Chobo Investment kuachia eneo analolimiliki kwa sasa wakati akiendelea kujipanga ili wawekezaji wengine ambao tayari wanayo mifugo waweze kulitumia. Aidha, amemuhakikishia mwekezaji huyo kuwa atapewa eneo kwenye Ranchi nyingine ikiwa atafuata masharti ya mkataba wa NARCO.

Vilevile kutokana na changamoto iliyoibuliwa kuhusu muda mfupi wa ukodishaji vitalu, Waziri Ndaki amewaagiza NARCO kuangalia uwezekano wa kuongeza muda wa mikataba ya muda mfupi ili iwe ni ya miaka mitano badala ya mwaka mmoja wa sasa.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayesimamia sekta ya Mifugo, Prof. Elisante Ole Gabriel amesema wizara imejipanga kuhakisha uzalishaji wa Mifugo na mazao yake unaongezeka na kuhakikisha wawekezaji katika sekta wanasaidiwa ili wasikwame katika uwekezaji wao.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Abdallah Mayomba amesema kuwa uwepo wa Ranchi katika Wilaya hiyo umesaidia sana kupunguza migogoro ya ardhi lakini pia imesaidia kupunguza tatizo la malisho ambalo lilikuwa linawasumbua wafugaji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wawezekaji hao wamemueleza waziri kuwa bado wanahitaji maeneo kwa ajili ya kufugia na kuwa wanaishukuru serikali kupitia NARCO kwa ajili ya kutenga maeneo hayo na kuwashushi gharama ya ukodishaji wa vitalu.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger