Monday, 17 May 2021

KANISA LA KKKT LASHAURIWA KUPIMA MAENEO YAKE KUEPUKA MIGOGORO YA ARDHI



Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mshariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Joseph Makala akizungumza wakati akifungua mkutano wa halmashauri kuu ya dayosisi hiyo leo

Na Frank Mshana, Shinyanga
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) limeshauriwa kupima maeneo yote yanayomilikiwa na Kanisa hilo na kupata hati za umiliki kwa lengo la kuepuka migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara baina ya Kanisa na baadhi ya watu wasio na hofu ya Mungu wanaotaka kupora maeneo ya Kanisa yaliyokaa muda mrefu bila kupimwa na kutambuliwa rasmi kuwa ni mali za kanisa.

Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria katika mkutano wa Halmashauri kuu ya Dayosisi hiyo uliofanyika Mei 14 na 15, mwaka huu katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mwadui inayomilikiwa na KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria.

Akizungumzia umuhimu wa Kanisa kupima maeneo na kutambua mipaka halisi ya maeneo Kamishna wa ardhi mkoa wa Shinyanga, Ezekieli Kitilya amesema yuko tayari kushiriki bega kwa bega kuhakikisha maeneo ya Kanisa yanapimwa na kupewa hati miliki lengo likiwa ni kuepuka migogoro ya ardhi inayosababisha maeneo mengi ya Makanisa kuporwa na watu wachache wasio na hofu ya Mungu.

Akizungumzia baadhi ya mifano ya maeneo ya Kanisa ambayo yamepata changamoto kama hiyo Mkuu wa Jimbo la Magharibi Kahama Mchungaji, Dkt. Daniel Mono amelitaja eneo la Bushushu ambalo linajengwa makao makuu ya Dayosisi kuwa ni mfano wa maeneo ya Kanisa la KKT yaliyokumbwa na changamoto ya kuvamiwa na kusababisha mgogoro uliowahi kufika Mahakamani huku akiunga mkono ushauri wa wajumbe wengine wa Halmashauri kuu juu ya upimaji wa maeneo yanayomiulikiwa na Kanisa.

Kwa upande wake, Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mshariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Joseph Makala ameunga mkono hoja hiyo na kuagiza mchakato wa kupima maeneo ya Kanisa uanze mara moja huku akiwataka waumini wa Kanisa la KKT katika Mikoa inayounda Dayosisi hiyo ambayo ni Shinyanga na Simiyu kutumia fursa ya uwepo wa Ofisi ya Kamishna wa ardhi Mkoani Shinyanga kupima maeneo yao ya makazi, biashara pamoja na mashamba ambapo Kamishna wa Ardhi, Ezekiel Kitilya ameahidi kutoa ushirikiano.

Mwisho viongozi pamoja na wajumbe wa Halmashauri kuu ya dayosisi wakaweka patano muda usiozidi mwaka mmoja kazi ya kuainisha, kupima na kuyatambua maeneo yote yanayomilikiwa na Kanisa iwe imefanyika.

Pamoja na agenda nyingine, mkutano ulikuwa na agenda ya Mkutano Mkuu wa tano wa Dayosisi ambao umepangwa kufanyika Juni 25 na 26, mwaka huu katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwadui.



MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
Askofu wa KKKT Dayosisi Kusini Mshariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Joseph Makala akifungua mkutano huo
Mkuu wa Jimbo la Magharibi Kahama Mchungaji, Dkt. Daniel Mono akielezea mambo mbalimbali kwenye mkutano huo
Kamishna wa ardhi mkoa wa Shinyanga, Ezekieli Kitilya akielezea utayari wa ofisi yake katika kulisaidia kanisa hilo kupima maeneo yake ya ardhi inayoyamiliki
Mkutano ukiendelea
Baadhi ya wajumbe wakichangia hoja mbalimbali

Picha ya pamoja Wajumbe wa Halmashauri Kuu, Wenyevuti wa Kamati mbalimbali, Wakuu wa Majimbo, Viongozi mbalimbali,Askofu Msaidizi Mch. Yohana Ernest Nzelu na Askofu Emmanuel Joseph Makala baada ya kumalizika Mkutano
Share:

Sunday, 16 May 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 17,2021















Share:

SIMBA VS YANGA KUPIGWA JULAI 3, VIPORO VIWILI VYA SIMBA KULIWA MWANZA


BODI ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) imefanya maboresho ya ratiba ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) michezo ya viporo ambayo inazihusisha timu za Namungo FC na Simba ambao bado wana mechi nyingi mkononi.

Miongoni mwa maboresho hayo, TPLB imeupangia tarehe mpya mchezo wa watani wa Jadi, Simba na Yanga ulioshindwa kufanyika Mei 8, mwaka huu ambapo sasa utachezwa Julai 3, mwaka huu.

Tazama ratiba hiyo hapa chini 




Share:

KITABU CHA MBIO ZA MWENGE CHAZINDULIWA


Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja wakionyesha kitabu maalum chenye ratiba ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2021 ambazo zitazinduliwa Mkoa wa kusini Unguja Mwehe tarehe 17 Mei 2021 na kilele cha mbio hizo kufanyika mkoani Geita tarehe 14 Oktoba 2021,kauli mbiu kwa mwaka huu ni “Tehama ni msingi wa Taifa Endelevu ,itumie kwa usahihi na Uwajibikaji”
Kaimu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Lela Muhamed Mussa akisoma taarifa maalum kwa vyombo vya habari juu ya suala zima la Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Mwehe Makunduchui Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 17 Mei 2021 ambapo kauli mbiu ni “Tehama ni msingi wa Taifa Endelevu, itumie kwa usahihi na Uwajibikaji” hafla iliyofanyika Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya kale Kikwajuni Zanzibar.
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Maswala ya Ulemavu Vijana, Sera na Uratibu wa Shughuli za Bunge Jenista Mhagama akitoa historia ya mwenge wa uhuru na kutolea ufafanuzi faida zinazopatikana katika mbio za Mwenge huko Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya kale Kikwajuni Zanzibar.
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Maswala ya Ulemavu, Vijana, Sera na Uratibu wa Shughuli za Bunge Jenista Mhagama (kulia) akimkabidhi Kaimu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Lela Muhamed Mussa vitabu maalum vya mbio za Mwenge wa uhuru 2021 aweze kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa vitabu hivyo vitakavyomfikia kila mtu kupitia Ofisi za Wilaya hafla iliyofanyika Ukumbi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya kale Kikwajuni Zanzibar.
Share:

APP YA MFUMO WA ANWANI NA POSTIKODI YATAMBULISHWA KWA MA - DED NA MA -RAS



Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akionesha Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi wakati Wizara hiyo ikitambulisha programu tumizi ya simu za mkononi (Mobile Application) ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi kwa Wakurugenzi wa halmashauri na Makatibu Tawala wa mikoa katika Mkutano wa 11 wa TOA uliofanyika jijini, Dodoma .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Mweli Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi wakati Wizara hiyo ikitambulisha programu tumizi ya simu za mkononi (Mobile Application) ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi kwa Wakurugenzi wa halmashauri na Makatibu Tawala wa mikoa katika Mkutano wa 11 wa TOA uliofanyika jijini, Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Mweli akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi wakati Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ikitambulisha programu tumizi ya simu za mkononi (Mobile Application) ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi kwa Wakurugenzi wa halmashauri na Makatibu Tawala wa mikoa katika Mkutano wa 11 wa TOA uliofanyika jijini, Dodoma.

********************

Na Faraja Mpina, WMTH, Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula na timu yake ya wataalamu wametoa wasilisho la programu tumizi ya simu za mkononi (Mobile App) ya Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi pamoja na hatua iliyofikiwa ya usimikaji wa Mfumo huo nchini kwa Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Mkutano wa 11 wa Maboresho ya Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa (TOA).

Akizungumza katika mkutano huo jijini Dodoma, Dkt. Chaula amesema kuwa Wizara hiyo inatekeleza ujenzi na usimikaji wa Mfumo huo kupitia Halmashauri zote nchini ambapo kwa mwaka wa fedha 2020/21 halmashauri 13 ziliingizwa kwenye mpango wa kusimikwa mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi.

Ameongeza kuwa mpango wa Wizara hiyo ni nyumba zote nchini ziwe na Anwani za Makazi ifikapo June 2022 na kuzipongeza halmashauri za mji wa Bukoba na Jiji la Mwanza kwa kuwa vinara wa utekelezaji wa Mfumo huo

Ili kuongeza ufanisi wa matumizi ya Mfumo huu Wizara imetengeneza programu tumizi ya simu ya mkononi (mobile application) ambayo itawezesha kutambua na kuonesha nyumba ilipo au popote mwananchi anapotaka kwenda na pia utarahisisha shughuli za biashara, alizungumza Dkt. Chaula

Akizungumzia mwongozo wa utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi, Dkt. Chaula amesema kuwa mwongozo huo umefanyiwa maboresho na utagawanywa kwa wadau kwa sababu utekelezaji wake unahusisha Wizara zaidi ya moja ikiwemo TAMISEMI na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,ambapo Ofisi ya Waziri Mkuu inaratibu kama Serikali na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ikiwa kama sekretarieti.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano wa Wizara hiyo ameizungumzia programu tumizi ya Mfumo huo kuwa na manufaa mengi kiuchumi na kijamii hasa katika dhana nzima ya uchumi wa kidijitali ambapo mfumo huo utarahisisha shughuli za kiuchumi kuweza kufanyika kidijitali.

Ameongeza kuwa chimbuko la mfumo huo ni Sera ya Taifa ya Posta inayoelekeza kuwa na Anwani ya Makazi ili kuweza kufikishiwa huduma mahali mwananchi alipo na kuongeza manufaa ya kijamii, kiuchumi na pia kimataifa ambapo nchi ya Tanzania ni mwanachama wa Umoja wa Posta Afrika.

Naye Mhandisi Jampyon Mbugi wa Wizara hiyo amezungumza na wajumbe wa Mkutano huo na kuwaomba kila mmoja kutimiza wajibu wake na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kurahisisha zoezi zima la usimikaji wa majina ya barabara, mitaa na namba za nyumba pamoja na ukusanyaji wa taarifa za makazi.

Aidha, wataalamu wa programu tumizi ya mfumo huo waliitambulisha program hiyo kwa wajumbe wa kikao hicho na kuonesha namna ya kuingia katika program hiyo na jinsi ya kuitumia ambapo inaonesha njia na barabara ya kupita mpaka kufika mahali ambapo mtumiaji anataka kufika

Share:

HUAWEI YATOA WITO WA USHIRIKIANO KATI YA SEKTA ZA UMMA, BINAFSI

Share:

TBS YATOA ELIMU YA VIWANGO KWA WANAFUNZI 15,526 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI NA WANANCHI 12,250


Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari 15,526 na wananchi 12,250 wanaoendesha shughuli zao kwenye maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu,  kama stendi, kwenye masoko, minada,magulio katika maeneo mbalimbali ya Wilaya za Kilosa, mkoani Morogoro, Bagamoyo mkoani Pwani  na Mkinga,  Tanga wamepewa elimu kuhusiana na umuhimu wa kutumia bidhaa zilizothibitishwa ubora na kusajiliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) .

Kampeni hiyo ya elimu kwa umma ilianza kutolewa maeneo mbalimbali ya wilaya za Kilosa, Bagamoyo na Mkinga na maofisa wa TBS  kuanzia Mei 4 hadi mwishoni mwa wiki hii.

Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Uhusiano wa TBS, Neema Mtemvu, alisema kitu kikubwa ambacho wamekifanya ni kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari juu ya umuhimu wa kutumia bidhaa zilizothibitishwa na kusajiliwa na TBS,majukumu ya shirika ikiwa ni pamoja na kuwapa namba ya mawasiliano kwa ajili ya kupiga bure kuwasiliana na shirika hilo pindi ikitokea wakapata matatizo  au changamoto kwenye bidhaa.

Alisema wamefikisha elimu hiyo kwa wanafunzi kwa kutambua kwamba wataenda kuwa mabalozi wazuri kwa wazazi na walezi kuhusiana na umuhimu wa kutumia bidhaa zilizothibitishwa na TBS.

Kwa upande wa maeneo yenye mikusanyiko ya watu, Mtemvu alisema elimu hiyo imetolewa Mkinga katika Stendi  ya Hororo na gulio la Duga, huku kwa upande wa Kilosa  elimu hiyo ikitolewa Uhindini, Sabasaba na Kimamba.

Aidha elimu hiyo ilitolewa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bagamoyo katika stendi ya Bagamoyo na soko la toptop ambako ilihitimishwa katika wilaya hizo tatu.

Kuhusu mwitikio wa wananchi katika maeneo hayo yenye mikusanyiko ya watu, Mtemvu alisema wengi wamefurahishwa na elimu hiyo na wameomba iwe endelevu .

"Wananchi wameshukuru shirika kwa kuona umuhimu wa kuwapatia taarifa hizo kuhusu viwango  kwa sababu wamekuwa wakipata changamoto kubwa, lakini walikuwa hawajui wafanyeje.

Lakini kwa sasa na wenyewe wameahidi kuingia kwenye vita ya bidhaa hafifu kwa sababu wana uwezo wa kuwasiliana na TBS, kwani wanajua tupo," alifafanua Mtemvu.

Alisema miongoni mwa mambo walioelimishwa wananchi hao kupitia kampeni hiyo ni pamoja na majukumu ya TBS,  umuhimu ya kuangalia tarehe ya mwisho ya matumizi ya bidhaa wanazotaka kununua, ambapo taarifa hizo zinapatikana kwenye vifungashio.

Eneo lingine ambalo wananchi hao walielimishwa ni umuhimu wa wao kununua bidhaa zilizothibitishwa na kusajiliwa na TBS. Mtemvu alitaja baadhi ya faida za kununua bidhaa zilizothibitishwa na shirika hilo kuwa ni pamoja na kulinda afya zao na thamani za fedha zao.

Alisema mtu anaponunua bidhaa ambazo zimethibitishwa na TBS anakuwa na uhakika na bidhaa anazozitumia.

Share:

PROF. MKUMBO AWATAKA WANANCHI KUWATUMIA WMA KUTATUA CHANGAMOTO ZA VIPIMO


Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) mkoa wa Pwani kuhusu namna zoezi la kuhakiki mita za maji linavyofanyika mara baada ya kutembelea leo Kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu Mkoa Pwani
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo akiambatana na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu (WMA) Bi.Stella Kahwa mara baada ya kuwasili leo katika kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu mkoani Pwani na kushuhudia kazi zinazofanywa na (WMA).
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo (wa pili kushoto) akishuhudia uhakiki wa matanki ya magari ya mafuta ukifanyika mara baada ya kuwasili leo katika kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu mkoani Pwani na kushuhudia kazi zinazofanywa na (WMA).
Magari ya mafuta yakihakikiwa matanki
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo (katikati) akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wakala wa Vipimo (WMA) mara baada ya kufika leo katika Kituo cha (WMA) Misugusugu mkoani Pwani kushuhudia kazi zinazofanywa na (WMA).

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*******************

NA EMMANUEL MBATILO, PWANI

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo amesema serikali ina mfumo mzuri wa kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma ambazo zimehakikiwa kupitia Wakala wa Vipimo (WMA) ili wananchi waweze kupata huduma iliyosahihi.

Ameyasema hayo leo alipotembelea Kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu Mkoa aa Pwani kuangalia namna shughuli inavyofanyika katika kituo hicho.

Aidha Prof.Mkumbo amewataka wananchi ambao walikuwa na malalamiko ya kubambikiwa bili na mamlaka husika kutumia Kituo hicho kuweza kutatuliwa changamoto zao katika vipimo.

"Kwa wale wananchi ambao wapo karibu na kituo hiki wasisite kutumia kituo hiki lakini kwa nchi nzima ni vizuri wananchi wanapokuwa na wasiwasi watumie vituo vyetu vya wakala ambavyo vipo katika kila Mkoa hapa nchini ili kupata huduma ambazo zimehakikiwa". Amesema Prof.Mkumbo.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) mkoa wa Pwani Bw. Alban Kihula wamenunua mtambo wa kuhakiki mita za umeme ambao unaweza kuhakiki mita 20 kwa mara moja ambapo utaanza hivi karibuni.

"Tumeshakaa na wazalishaji wa mita za umeme hapa nchini na zoezi linaloendelea kwa sasa kuhakiki sampuli za mita kabla hazijakwenda kwa wateja".Amesema Bw.Kihula.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger