Thursday, 13 May 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 12,2021


Share:

SIKUKUU YA EID -EL- FITR NI IJUMAA MEI 14


Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi ametangaza kuwa Sikukuu ya Eid El-Fitr ni Ijumaa Mei 14, 2021.

Amesema leo Mei 12, 2021 mwezi haujaonekana hivyo waumini wa dini ya Kiislamu wataendelea kufunga kwa siku ya 30.
Share:

Wednesday, 12 May 2021

Museveni aapishwa kuiongoza Uganda kwa muhula wa sita


Rais Yoweri Museveni amekula kiapo hii leo nchini Uganda kuliongoza taifa hilo kwa muhula wa sita.


Museveni ataiongoza Uganda kwa miaka mengine mitano, ikiwa ni muhula wake wa sita madarakani.

Aliingia madarakani Januari 1986 kwa mapinduzi ya kijeshi, hadi utakapofika uchaguzi mwingine 2026 atakuwa madarakani kwa miaka 40, sawa na miongo minne. Wakati huo akiwa na umri wa miaka 81.

Alishinda uchaguzi wa Januari 14, 2021 kwa kuwabwaga wagombea wengine kumi katika nafasi ya Urais kwa ushindi wa asilimia 58 ya kura zote.


Share:

Usichelewe .....Pakua sasa hivi App Ya Mpekuzi Ikiwa na Maboresho Mapya. Ipo PlayStore

Tumefanya Maboresho Kwenye App Yetu ya Mpekuzi Ili Kukuwezesha Kupata Habari zetu Haraka

Usikubali kupitwa na taarifa muhimu zinazoendelea hapa nchini na Duniani  kwa Ujumla . Tumejipanga vizuri sana kukupatia taarifa sahihi na kwa wakati.

👉1. Tumebadili muonekano na kuufanya kuwa mzuri zaidi
👉2. Kila habari tunayoweka kuanzia sasa utapata notification kwenye simu yako 
👉3. Habari zote kwa sasa zinafika kwa haraka kwenye simu yako kuliko ilivyokuwa hapo awali

KUMBUKA: App yetu ni BURE. Unachotakiwa kukifanya ni kuingia Playstore na kupakua MPEKUZI APP

Kama tayari unayo, basi Ingia Playstore kwa ajili ya kupata UPDATE hii ya Toleo Jipya

Tumekurahisishia, Unaweza pia ...<<KU BOFYA HAPA>> Kupata toleo hili Bure Kabisa


Share:

Zaidi ya wagonjwa Mil. 20 Watibiwa 2020/21- Serikali

 


Na Nteghenjwa Hosseah, Manyara
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, anayeshughulikia Afya, Dkt. Grace Maghembe amesema katika mwaka wa fedha 2020/21 wauguzi waliopo katika vituo vya kutolea huduma wamehudumia wagonjwa wapatao milioni 20 waliofika katika vituo hivyo kupata huduma za kiafya.

Akitoa salamu za Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Manyara. Dkt. Magembe ameyasema, huduma zilizotolewa kwa wingi ni pamoja na huduma za Nje maarufu kama huduma za Mkoba  ambazo zilihusiaha takribani watu milioni 1.2 ambazo zimejikita zaidi katika kumhudumia mama na mtoto.

Dkt. Magembe, amesema wauguzi hao walifanikiwa kuwazalisha kina mama takribani laki moja na kutoa huduma dawa ya usingizi kwa wajawazito 25,000.

Dkt. Magembe, alibainisha mahitaji ya wauguzi wa sasa ni 41,000 lakini waliopo katika vituo vya kutolea huduma ni 19,000 ambapo ni sawa na asilimia 41 ya mahitaji.

Kuhusiana na wauguzi walio ajiriwa katika mwaka wafedha wa 2017/2019  ni 3,625 ambapo watumishi hao waliajiriwa na Serikali pamoja na wadau  wa Taasisi ya Benjamini Mkapa.

"Na katika ya ajira 2,720 za kada ya afya zilizotangazwa Mei 9 mwaka huu na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, jumla ya ajira za wauguzi miongoni mwake ni 954 sawa na asilimia 35 ya ajira zote zilizotangazwa."

Siku ya wauguzi husherehekewa tarehe 12 mwezi Mei ya kila Mwaka, ambayo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Florence Nightngale, mwana takwimu na mwanzilishi wa uuguzi wa kisasa. Maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani kitaifa yamefanyika mkoani Manyara na kubebwa na kauli mbiu “Wauguzi sauti inayoongoza, Dira ya huduma ya afya”


Share:

Shilingi milioni 61 kujenga barabara na makalvati 14 Wilayani Same


 Na Mathew Kwembe, Dodoma
Serikali imetenga shilingi milioni 61 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kutoka Makanya kwenda kwenye Machimbo ya Jasi Wilayani Same kwa kiwango cha changarawe yenye urefu wa kilomita moja pamoja na ujenzi wa makalvati 14 katika mwaka wa fedha 2021/22.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe Zuena Athumani Bushiri, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.David Silinde amesema serikali itatoa kipaumbele cha ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami katika bajeti zijazo ili kuiboresha na kurahisisha usafirishaji wa Jasi.

Amesema kipaumbele cha Serikali ni kuhakikisha barabara hii inapitika muda wote na ndio maana imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya matengenezo ya mara kwa mara.

Naibu Waziri amesema katika mwaka wa fedha 2019/20 Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Same umefanya matengenezo ya barabara ya Makanya hadi kwenye Machimbo ya Jasi maeneo korofi yenye urefu wa kilomita 3.5 kwa gharama ya Shilingi milioni 77.3.

Aidha, katika mwaka wa fedha 2020/21 TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Same   imefanya matengenezo ya barabara hiyo kipande chenye urefu wa kilomita mbili kwa kiwango cha Changarawe kwa gharama ya Shilingi milioni 49.4.

Barabara ya Makanya hadi kwenye machimbo ya Jasi Wilayani same ina urefu wa kilomita 40.9. Kipande cha kilomita 4.5 cha barabara hii kimeinuliwa kwa kujengwa tuta kati ya kilomita 14.5 zinazotakiwa kujengwewa tuta kwa kiwango cha changarawe.

Wakati huo huo Naibu Waziri Mhe.Silinde amesema katika mpango wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2020/21 barabara za kutoka Rubanga, Isurwa, Butundwe, Mkoba, Kukuruma, Kamhanga, Kishinda na Mkorani zimetengewa Shilingi milioni 318.8 kwa ajili ya matengenezo ya kilometa 33 na wakandarasi wanaendelea na utekelezaji wa kazi.

Amesema matengenezo ya barabara hii yanatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2021 na kuwa vijiji vilivyotajwa vinaunganishwa na barabara za Mkoba bridge – Isulwabutundwe – Lubanga yenye urefu kilomita 15  na Geita – Isamilo – Mkolani (Busekeseke) yenye urefu wa kilomita 18 ni barabara muhimu sana wananchi.


Share:

Jaji Imani Aboud Apendekezwa Kugombea Urais Wa Mahakama Ya Afrika


Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kutoka Tanzania Mhe. Jaji Imani Aboud amependekezwa kugombea Urais wa Mahakama hiyo.


Jaji Aboud amesema endapo atashinda katika nafasi hiyo na kuibuka mshindi itakuwa ni heshma kubwa kwa nchi na kwake mwenyewe kushika wadhifa mkubwa katika mahakama ya Afrika kuhusu masula ya haki za binadamu…


Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema Tanzania inayo imani na Jaji Imani Aboud kwa kuwa ana uzoefu mkubwa katika masula ya kimahakama hivyo ushindi wake utakuwa ni sifa kwa Taifa na kwa wanawake kuendelea kushika nyadhifa kubwa sio Serikalini tu, bali kwenye taasisi na mashirika ya kimataifa.


Majaji wengine wanaogombea nafasi hiyo ni kutoka katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Malawi na Cameroon ambapo Hayati Jaji Augustino Ramadhani ndie alikuwa Mtanzania wa mwisho kushika nafasi hiyo ya Urais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.




Share:

Uzinduzi Msimu wa Ununuzi wa Pamba Kitaifa 2021/2022; Wadau Watakiwa Kushirikiana ili Kuongeza tija ya Zao la Pamba


Msimu wa ununuzi wa Pamba kitaifa 2021/2022 umezinduliwa wilayani Busega, mkoani simiyu. Akizindua, msimu wa ununuzi wa pamba, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Tano Mwera kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Mwera amesema ushirikiano wa wadau wa kilimo cha pamba utaongeza tija ya zao hilo.

“Zao la pamba ni miongoni mwa mazao ya kimkakati, hivyo wadau washirikiane ili kuongeza tija”, alisema Mhe. Mwera. Katika kuleta tija ni vyema wakulima kufuata kanuni za kilimo bora ikiwemo upandaji wa pamba kwa nafasi inayotakiwa ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo, aliongeza Mhe. Mwera.

Awali, Mkurugenzi wa bodi ya pamba, Bw. Marko Mtunga amesema uzinduzi wa msimu wa ununuzi wa pamba una manufaa makubwa hivyo Busega imepewa heshima kubwa, na hii imetokana na kazi kubwa ya usimamizi mzuri wa viongozi wa Wilaya katika kilimo cha pamba. “Katika msimu wa 2020/2021, wilaya ya Busega imezalisha takribani kilo milioni 3, lakini msimu wa mwaka 2021/2022 tunategemea uzalishaji zaidi ya kilo milioni 10” aliongeza, Mtunga.  

Aidha, Mhe. Mwera amesema licha ya Wilaya kuwa na uzalishaji mzuri katika zao la pamba, lakini changamoto kubwa inayowakabili wakulima, ikiwemo wadudu. Hali hiyo imewafanya wakulima wengi kushindwa kutambua jinsi ya kukabiliana na wadudu wanaoshambulia zao la pamba, hivyo bodi ya pamba itoa elimu zaidi kwa wakulima ikiwemo elimu ya kupambana na wadudu.

Kauli mbiu ya uzinduzi wa msimu ununuzi wa pamba kitaifa 2021/2022 inasema “Tuboreshe Ubora na Usafi wa Pamba kwa Uhakika wa Soko na Malipo kwa Wakati”. Kauli ambayo imeelezwa kuwa na manufaa makubwa kwa wakulima wa zao la pamba. Wanunuzi wa pamba walioshiriki uzinduzi huo wamesema wapo tayari kununua pamba na kuahidi wakulima watalipwa kwa wakati. Katika uzinduzi huo, Serikali imetoa bei elekezi ya zao la pamba kwa msimu wa 2021/2022, ambapo pamba daraja A itanunuliwa kwa Tzs 1,050 na daraja B itanunuliwa kwa Tzs 525.

Baadhi ya wa wakulima wa pamba Wilayani Busega wanasema Serikali, wakulima na wadau wengine wanapaswa kushirikiana ili kuongeza uzalishaji wa zao la pamba nchini. Kwa upande mwingine wameiomba Serikali kutoa elimu zaidi ya zao hilo ikiwemo kanuni bora za ulimaji wa zao hilo.


Share:

WAKILI MOSHA : WAANDISHI WA HABARI MSICHUKULIE POA USALAMA WENU UKIWA HATARINI


Wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Leopold Mosha
***
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Waandishi wa habari wamekumbushwa umuhimu wa kuzingatia na kuchukua tahadhari za kiusalama wanapotekeleza majukumu yao katika kuihabarisha jamii.

Rai hiyo imetolewa leo Jumatano Mei 12,2021 mkoani Morogoro na Wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Leopold Mosha  wakati wa semina kwa Waandishi wa Habari Mtandaoni (Online Media Journalists, Bloggers and Editors) ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria mbalimbali zinazohusu Tasnia ya Habari ili waweze kuripoti kwa weledi zaidi juu ya Haki za Binadamu iliyoandaliwa na THRDC.

Wakilia Mosha amesema suala la usalama kwa waandishi wa habari ni la kuzingatia wanapotekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola,vyombo vyao vya habari na waandishi wa habari wenzao pindi wanapoona au kuhisi dalili za kuhatarisha usalama wao.

“Waandishi wa habari toeni taarifa pindi mnapoona usalama wenu upo hatarini. Usichukulie poa pindi unapoona usalama wako upo hatarini. Usikubali kitu kipite tu walau fanya jambo kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka mbalimbali ikiwemo vyombo vya dola, taasisi zinazohusu utetezi wa haki za waandishi wa habari na haki za binadamu kwa ujumla ikiwemo THRDC ili upate msaada”,amesema.




Share:

Waziri Mkenda Awataka Wakala Wa Mbegu Za Kilimo Kufufua Mashamba Yake Yote


 Waziri wa Kilimo Prof. Aldof Mkenda ameitaka Menejimenti ya Wakala wa Mbegu (ASA ) pamoja na Bodi mpya inayotarajiwa kupatikana hivi karibuni kufufua mashamba 13 ya kuzalisha mbegu bora na kuweka miundombinu ya umwagiliaji ili kuahakikisha yanazalisha kwa tija ili kuwasaidia Wakulima kupata mbegu bora; Kwa wakati na kwa bei nafuu.

Waziri Mkenda amesema jana Mei 11, 2021 Ofisi za Wizara ya Kilimo, Jijini Dodoma wakati akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi ya (ASA) iliyomaliza muda wake pamoja na Menejimenti ya kuwa uzalishaji wa mbegu bora ni lazima uende sambamba na matumizi ya maji ili kuhakikisha mbegu zinazalishwa kwa bei nafuu.

Prof. Mkenda amesema uzalishaji wa mbegu bora kwa mwaka ujao wa fedha ni kipaumbele cha Wizara hiyo ni katika uzalishaji wa mbegu bora kupitia mashamba hayo ndio maana Wizara imeamua kuanzisha Mfuko Maalum wa Kilimo ambao unataraji kugharamia shughuli mbalimbali za maendeleo ya Sekta ya Kilimo, mbegu ni eneo moja wapo.

Waziri Mkenda amesema ili kuongeza tija Wakala wa Mbegu Bora za Kilimo (ASA) inatakiwa kufunga miundombinu hiyo ya umwagiliaji ili kuongeza tija kwenye upatikanaji wa mbegu bora.

“Tuyafufue mashamba yote 13 ya ASA na yafungiwe miundombinu ya umwagiliaji na kwa sababu Tume ya Maendeleo ya Umwagiliaji ipo chini ya Wizara ya Kilimo; Na tumeelekeza hakuna kuanzisha Mradi mpya wa umwagiliaji mpaka tuwe tumemaliza kujenga miundombinu ya umwagiliaji kwenya mashamba yote ya ASA.” Amesisitiza Waziri Mkenda.

Waziri Mkenda ameongeza kuwa njia pekee ya kuhakikisha maisha ya Watanzania yanakuwa bora ni kuongeza tija kwenye kilimo kwa kuhakikisha mbegu bora zinapatikana kwa bei nafuu ili Wakulima wazitumie kuzalisha kwa tija na kwa kufanya hivyo mazao ya chakula yatapatikana kwa wingi na kwa bei nafuu. Jambo hilo litachangia kupunguza gharama za maisha na kwa ajili hiyo. Wananchi wengi watanunua chakula kwa bei nafuu.

Waziri Mkenda amesema uzalishaji wa tija kwenye mbegu za mafuta utasaidia kupunguza matumizi ya fedha za kigeni kutokana na kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi ambapo Serikali imekuwa ikitumia zaidi ya nusu tilioni kuagiza mafuta kutoka nje.

Pia Prof.Mkenda amesema kuwa ipo haja kwa Serikali kuwa msimamo unaoakisi kauli mbiu ya kilimo ni uti wa mgongo ili Wakulima walime kwa tija na kuondokana na umaskini miongoni mwao.

“Tunaweza kuwa kwenye uchumi wa kati na hata kufikia uchumi wa juu lakini wimbi la umaskini likaendelea kwa Wananchi na tukawa tegemezi wa chakula; Lakini pia hatuwezi kuwa na mageuzi ya viwanda bila kufanya mageuzi ya kilimo hususani katika suala la uzalishaji wa mbegu.” Amesisitiza Waziri Mkenda.

Hata hivyo amesema kuwa ni lazima mashamba yote ya ASA yafufuliwe kwa kuwa utegemezi wa mbegu kutoka nje ya nchi wakati mwingine hausaidii kilimo cha hapa nchini.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya ASA, Dkt. Ashura Kihupi amesema kuwa zipo kero kubwa kwenye Sekta ndogo ya Mbegu ni uwekezaji mdogo uliofanywa pamoja na mtaji mdogo kwa ajili ya kuzalisha mbegu.

Dkt. Kihupi ametoa mfano wa shamba la mbegu la Msimba lililopo Kilosa mkoani Morogoro; Kuwa uzalishaji umekuwa mdogo kwa sababu hakuna miundombinu ya umwagiliaji maji.


Share:

Majaliwa: Watendaji Sekta Ya Maji Fanyeni Kazi Wa Uzalendo

 


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi na watendaji wote wa sekta ya maji nchini kufanya kazi kwa uzalendo, bidii na weledi na kwa kutanguliza maslahi mapana ya nchi.

Amesema lengo ni kuhakikisha kuwa kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji nchini kinaongezeka ili kufikia malengo ya kufikisha maji kwa kiwango cha asilimia 85 Vijijini na asilimia 95 Mijini ifikapo mwaka 2025.

Ametoa kauli hiyo jana (Jumanne, Mei 11, 2021) wakati wa mkutano wa watendaji wa sekta ya maji uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma.

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwataka watendaji wa sekta maji nchini kushirikiana na wanajiosayansi kufanya tafiti za mara kwa mara zitakazotuwezesha kuwa na takwimu za uhakika kuhusu kiwango cha maji, mahali yalipo na ujazo wake.

“Kama nilivyotangulia kueleza kuwa maji ni chachu katika maendeleo ya viwanda nchini. Kwa mantiki hiyo, uwepo wa takwimu sahihi kuhusu upatikanaji wa maji ni muhimu katika kurahisisha na kuvutia uwekezaji wa viwanda kote nchini”

Aidha, Waziri Mkuu ameigiza Wizara ya Maji ishirikiane na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kusimamia vema na kwa uadilifu rasilimali fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji ili miradi iweze kukamilika kwa wakati na uwepo wa thamani ya fedha za walipa kodi.

Akizungumzia kuhusu uboreshwaji wa huduma ya upatikanaji wa majisafi na salama kwa wananchi waishio vijijini na mijini, Waziri Mkuu amesema “kufikia Machi 2021, jumla ya miradi 177 ya maji imeendelea kutekelezwa katika Miji Mikuu ya Mikoa, Miji Mikuu ya Wilaya, Miji midogo na Miradi ya Kitaifa. Tayari, miradi 67 imekamilika kwa gharama ya shilingi bilioni 759.211 na utekelezaji wa miradi 110 upo katika hatua mbalimbali”

Waziri Mkuu pia alikabidhi pikipiki 147 kwa ajili ya mameneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Viijini, malori matatu ya kunyonya majitaka kwa halmashauri za miji ya Kahama, Tanga na Lindi.

Awali akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa hatakuwa na huruma na mtendaji yeyote atakayegundulika anahujumu miradi ya maji, lengo ni kuhakikisha watanzania wanapata huduma ya maji safi na salama wakati wote.

Amesema “Hatuwezi kukubali wakandarasi wasio na uwezo wa kufanya kazi, tutawapa kazi wakandarasi wenye uwezo wa kuwasaidia wananchi kupata huduma ya maji”

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema kuwa ataweka mazingira rafiki kwa RUWASA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ili kuhakikisha miradi yote maji inakamilika.


Share:

Rais Mwinyi Aishukuru Ofisi Ya Rais Utumishi Na Utawala Bora Kwa Ushirikiano Mzuri Na SMZ Katika Masuala Ya TASAF, MKURABITA Na Ajira

 Na. James K. Mwanamyoto-Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuboresha maisha ya kaya maskini, urasimishaji ardhi, biashara na utoaji wa fursa za ajira kwa uwiano uliokubalika kwenye vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na vikao vya mashirikiano vya Mawaziri kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mhe. Rais Mwinyi ameyasema hayo leo Ikulu ya Zanzibar alipokuwa akizungumza na ujumbe kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ulioongozwa na Waziri mwenye dhamana ya Ofisi hiyo, Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Mhe. Rais Mwinyi amesema ni matarajio yake kuona ushirikiano huo ukiendelezwa na kuondoa changamoto za kiutendaji zilizopo ili wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar wanufaike na masuala yote yanayohusu MKURABITA, fursa za ajira na ruzuku inayotolewa na TASAF.

Kuhusiana na fursa za ajira kwa Wazanzibari, Rais Mwinyi amempongeza Mhe. Mchengerwa kwa utashi wake katika kusisitiza uzingatiaji wa makubaliano ya uwiano wa Ajira kwa taasisi za Muungano ambapo katika vikao vya Bunge ilikubalika kuwa Tanzania Bara iwe na asilimia 79% na Tanzania Zanzibar asilimia 21% ya nafasi za Ajira kila zinapotangazwa.

Akizungumzia suala la kujengeana uwezo kwenye mchakato wa ajira, Mhe. Rais amesema ni muhimu Zanzibar ikajifunza kutoka Bara kwa kuwa na kanzidata ya waombaji wa ajira ili fursa za ajira zinapotolewa iwe rahisi kuwapata watu sahihi wanaohitajika.

Akizungumiza melekezo ya Mhe. Rais Mwinyi, Mhe. Mchengerwa amesema, Ofisi yake imejipanga kuhakikisha suala la kubadilishana uzoefu kwa Watumishi wa Umma wa pande zote mbili litafanyiwa kazi.

Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa, atashirikiana na Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Utumishi wa Umma Zanzibar kuhakikisha Watumishi wa Umma wanapata mafunzo ya kuwajengea uwezo kiutendaji ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi.

Tutajipanga vizuri kuhakikisha wataalam wa vyuo vya Utumishi wa Umma Tanzania Bara na Zanzibar wanakutana na kupanga namna bora ya kuwawezesha Watumishi wa Umma kupata mafunzo yenye tija katika utumishi wao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Ladislaus Mwamanga amemueleza Rais Mwinyi kuwa, Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 112.87 kwa upande wa Zanzibar kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu.

Amefafanua kuwa, kiasi hicho kitatumika katika kutekeleza miradi ya kutoa ajira za muda, ikiwa ni pamoja na kuondoa mapungufu yaliyopo katika sekta ya elimu, afya na maji na kuongeza kuwa wazee wataendelea kupata ruzuku kama kawaida kwani hawana uwezo wa kushiriki katika miradi ya kutoa ajira za muda.

Naye Mratibu wa MKURABITA, Dkt. Seraphia Mgembe amesema urasimishaji wa biashara kwa upande wa Zanzibar umefanyika katika maeneo 8 ambapo wameweza kuwafikia wananchi kwa kutoa mafunzo na kusajili biashara zao ambapo watu 2926 wamepata leseni za biashara na utambulisho wa mlipa kodi ambao umewawezesha kuchangia pato la taifa kwa kulipa kodi.

Kwa upande wake Katibu wa Sekretarieti ya Ajira, Bw. Xavier Daudi amesema Ofisi yake iliyoko Zanzibar itahakikisha inatoa elimu kwa wahitimu ili waweze kupata taarifa sahihi zitakazowawezesha kuomba ajira zinazotangazwa.

Ameongeza kuwa, Ofisi yake hivi sasa imeanzisha dirisha litakalowawezesha waombaji wa fursa za ajira kupata taarifa za ajira, kuwasilisha maombi popote walipo na kupata mrejesho wa maombi yao.

Rais Mwinyi amekutana na ujumbe kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora uliolenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa upande wa Zanzibar.




Share:

Roketi zapiga mji wa Tel Aviv - Israel baada ya ghorofa kuharibiwa Gaza


Wanamgambo wa Kipalestina wanasema wamerusha makombora 130 katika mji wa Israeli wa Tel Aviv baada ya shambulio la anga la Israeli kuangusha ghorofa katika eneo la ukanda wa Gaza.

Jumba hilo la ghorofa 13- lilishambuliwa saa moja unusu baada ya wakazi na wenyeji wa eneo hilo kushauriwa waondoke, shirika la habari la Reuters liliripoti.

Jeshi la Israel linasema kuwa linalenga wanamgambo mjini Gaza kujibu shambulio la awali la roketi.

Watu 31 wameuawa baadhi yao katika ghasia mbaya zaidi zilizowahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni.

Jamii ya kimataifa imetoa wito kwa pande zote mbili kukomesha mapigano, yaliyofuatiwa na siku kadhaa za ghasia mjini Jerusalem.

Wanamgambo walikuwa tayari wafyatua mamia ya maroketi kuelekea upande wa Jerusalem na maeneo mengine.

Watu watatu wameuawa katika maeneo ya Israeli huku Wapalestina 28 wakiuawa kwa makomboro ya Israel.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu awali ailisema kundi kubwa la wanamgambo, Hamas, “limevuka mpaka” kwa kurusha maroketi kuelekea Jerusalem kwa mara ya kwanza ndani ya miaka kadhaa.

Hamas, ambayo inadhibiti Gaza, inasema imechukua hatua hiyo kulinda msikiti wa al-Aqsa mjini Jerusalem dhidi ya “ dhalimu na ugaidi” wa Israel baada ya eneo hilo, takatifu kwa Waislamu na Wayahudi, kukumbwa na makabiliano kati ya polisi wa Israeil na Wapalestina siku ya Jumatatu na kusbabisha mamia kujeruhiwa.

 

Credit:BBC



Share:

Branch Manager – Stone Town, Zanzibar at KCB

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Job Summary: The role holder is responsible for overall leadership of the branch to achieve growth, profitability and customer service excellence whilst ensuring implementation of an effective risk management framework through efficient utilization of resources. Job Details: Key Responsibilities Achieve profitability targets through revenue maximisation and prudent cost management. Grow and monitor branch’s liability and […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Training Centre Administrator at Sustainable Agriculture Tanzania

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Training Centre Administrator alias Hotel Manager We are looking for an experienced Training Centre Administrator with experience in Hotel Management. As our Training Centre Administrator, you will oversee the daily operations of our Centre and provide strategic direction. You will plan and supervise the activities of an extensive and diverse workforce to ensure the smooth and […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Construction Supervisor at Sustainable Agriculture Tanzania

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Job Description We are looking for an experienced, driven Construction Supervisor with construction experience. To ensure success, the ideal candidate should be comfortable splitting their hours between the office, on-site visits and engaging the communities. The Construction Supervisor plans and oversees the construction site. They lead crews, ensure safety regulations and health codes are observed, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Technical Operator-Brewing at Serengeti Breweries

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

About us From Arthur Guinness to Johnnie Walker, our business was founded on people of great character, and in 250 years, nothing’s changed. We’re the world’s leading premium alcohol company. Our brands are industry icons. And our success is thanks to the strength of our people, in every role. It’s why we trust them with […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger