Saturday, 8 May 2021
Picha : BENKI YA CRDB YATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA SHINYANGA
Waziri Bashungwa asitisha Utekelezaji wa Kanuni ya Uhakiki wa kazi za Muziki
Na Anitha Jonas - COSOTA,Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa awatoa hofu Wasanii kuhusu suala la ugawaji wa Mirabaha kwa kuelezea kuwa Serikali imeandaa mifumo ya kidijitali ambayo itarahisisha ukusanyaji wa mirabaha hiyo na kuongeza gawio.
Mhe. Bashungwa ameyasema hayo leo Mei 08, 2021 katika kikao chake na Viongozi wa Vyama na Mashirikisho ya Muziki na Filamu nchini kilicholenga kuzungumzia Kanuni ya 26 ya BASATA inayohusu uhakiki wa kazi za Muziki na Filamu kabla ya kuingia sokoni au kusambazwa.
"COSOTA imekuwa na changamoto ya ukusanyaji wa mirabaha kutokana na uhaba wa watumishi hivyo kwa kupitia mfumo mpya wa kidijitali utakao anzishwa hivi karibuni utarahisisha ukusanyaji wa mirabaha hiyo, Serikali inataka kutoa gawio la pesa nyingi kwa wasanii na siyo fedha kidogo hivyo tunawaomba mvumilie kidogo kuanzia mwaka mpya wa fedha mambo yatakuwa mazuri,"Mhe.Bashungwa.
Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Waziri huyo alitoa maelezo mahususi kwa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) akiwataka kusitisha utekelezaji wa Kanuni ya 26 inayotaka kazi zote za Muziki kukaguliwa nao kabla ya kusambazwa.
Aidha, Mhe.Bashungwa alisisitiza kuwa maelekezo hayo ya kusikitishwa kwa matumizi ya Kanuni hiyo ni kwa upande wa Muziki pekee ila kwa upande wa Filamu itaendelea kutumika kama kawaida.
Pamoja na hayo Mhe.Bashungwa aliendelea kutoa maelekezo ya haraka kwa BASATA kwa kuwataka kuanzisha mchakato wa kurekebisha Kanuni hiyo kwa kuwashirikisha wadau hao wa vyama na mashirikisho ili kuweza kupata Kanuni mpya isiyodumaza tasnia ya Muziki lakini izingatie maadili ya taifa.
Halikadhalika Waziri huyo ameelekeza BASATA kwa kushirikiana na wadau kuandaa mwongozo utakao kuwa kukitoa dira njema ya uendeshaji na ukuzaji wa tasnia ya Muziki.
Naye mmoja wa wasanii hao Soggy Doggy alimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa maamuzi aliyoyafanya na kumpongeza na kuahidi kuendelea kushirikiana na wasanii wa Muziki katika kukuza na kuiendeleza tasnia ya Muziki nchini.
*****MWISHO*****
MECHI YA SIMBA NA YANGA KUPIGWA LEO SAA MOJA USIKU
PASTA ANASWA 'LIVE KITANDANI' AKIPAKUA ASALI YA MKE WA MTU
Waziri Mulamula Akutana Na Mabalozi Wanne, Kupokea Nakala Ya Hati Ya Utambulisho
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kuzungumza na mabalozi wanne wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na kupokea nakala ya hati ya utambulisho ya balozi mteule wa Msumbiji hapa nchini.
Mabalozi waliokutana na Waziri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam ni Balozi wa Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba, Balozi wa Indonesia Mhe. Ratlan Pardede, Balozi wa Sweden Mhe. Anders Sjöberg na Balozi wa Norway Mhe. Elisabeth Jacobsen.
Pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri Mulamula na mabalozi hao wamejadili juu ya kuimarisha na kuongeza ushirikiano baina ya mataifa wanayoyawakilisha hapa nchini na Tanzania.
“Leo nimekutana na mabalozi kadhaa wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, akiwemo Balozi wa Rwanda, Sweden, Norway na pia nimepokea nakala ya hati ya utambulisho ya balozi mteule wa Msumbiji na kuwahakikishia ushirikiano wetu kama wizara, kama nchi katika kuboresha na kukuza mahusiano yetu,” amesema Balozi Mulamula
Nae Balozi wa Rwanda hapa nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba amesema kuwa ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda ni mzuri hivyo wataendelea kuudumisha uhusiano huo kwa maslahi ya pande zote mbili.
“Nchi zetu mbili zimekuwa zikishirikiana vizuri hivyo tumekubaliana kuendelea kudumisha ushirikiano huu kwani Watanzania na Wanyarwanda ndugu na marafiki,” amesema Balozi Karamba
Kwa upande wake Balozi wa Indonesia hapa nchini Mhe. Ratlan Pardede amesema Indonesia na Tanzania zitaendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali ikiwemo uchumi, utalii na kijamii na kuhakikisha kuwa ushirikiano huo unazidi kuimarika.
“Tumejaribu kuwahamasisha wawekezaji kutoka Indonesia kuja kuwekeza hapa Tanzania na hadi sasa kampuni kumi (10) zimewekeza katika sekta za biashara na uwekezaji, madini, uvuvi, ujenzi na viwanda,” amesema Balozi Pardede
Nae Balozi wa Sweden Mhe. Anders Sjöberg amesema kuwa Sweden itaendelea kuimarisha mahusiano na ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji, utunzaji wa mazingira na masuala ya kijamii kama vile usawa wa kijinsia, uhuru wa vyombo vya habari pamoja na haki za binadamu.
“Tumejadiliana kuhusu kuimarisha mahusiano, biashara na uwekezaji, utunzaji wa mazingira pamoja na masuala ya kijamii kama vile usawa wa kijinsia, uhuru wa vyombo vya habari na haki za binadamu,” amesema Balozi Sjöberg.
Kwa upande wake Balozi wa Norway hapa nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen amesema Norway na Tanzania zimekuwa na uhusiano mzuri ambapo kwa sasa Norway inaangalia fursa za uwekezaji na biashara hapa nchini ili kuimarisha mahusiano na kukuza uchumi.
“Norway itaendela kutumia fursa za uwekezaji na biashara zilizopo Tanzania ili kuimarisha mahusiano yetu na kukuza uchumi wa pande zote mbili,” amesema Balozi Jacobsen
Katika tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amepokea nakala ya hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Msumbiji hapa nchini Mhe. Ricardo Ambrosio Sampaio Mtumbuida.
ATCL Yazindua Safari za China
Uzinduzi huo uliofanyika kwenye Jengo Namba 3 la abiria (terminal 3) katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere umeongozwa na Mhandisi. Dkt. Leonard Chamuriho, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi. Ladislaus Matindi.
Kwa mujibu wa ATCL, safari kati ya Dar es Salaam na Guangzhou itatumia saa 11 na zitakuwa safari pekee za moja za moja kwa moja kati ya maeneo hayo mawili.
Tangu mwaka 2015 serikali imewekeza nguvu katika kufufua kampuni hiyo ambapo jitihada hizo ni pamoja na kununua ndege, kukarabati na kujenga viwanja vya ndege na kuongeza rada za kuongozea ndege ili kuziwezesha ndege za shirika hilo kufika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Infinix Yanyakua Tuzo Ya Nidhamu Duniani 2021.
Infinix ZERO 8 ilishinda baraza la washiriki 98 linaloundwa na wataalamu wakujitegemea kutoka ulimwenguni kote, design ya Infinix ZERO 8 iliyotawaliwa na mzunguko wa kioo na chuma, sifa nyengine zilizoifanya Infinix ZERO 8 kuibuka kinara ni display ya nch 6.85 FHD+ camera yenye uwezo wa kunasa matukio kila pembe. Ushindani ulikuwa ni mkubwa takribani nchi 52 ziliweka muhuri wa kukubalia Infinix ZERO 8 ndio simu bora kwenye kipengele cha nidhamu ya mawasiliano baada ya kuyapiga chini makampuni mengine ya simu. http://www.infinixmobility.com/
IF DESIGN huandaliwa kila mwaka na shirika la ubunifu ulimwenguni Hannover-based If international Forum Design GmbH. Tuzo za IF DESIGN ni tuzo zenye kujumuisha bidhaa zote zenye muonekana wa kuvutia, kipekee na imara. IF DESIGN imekuwa ikitoa tuzo hizi kwa kupambanisha bidhaa kwenye taaluma zifuatazo nidhamu, ufungashaji (packaging), ubunifu wa huduma, usanifu na usanifu wa mambo ya ndani pamoja na dhamana ya utaalamu.
Na msemo wake wa THE FUTURE IS NOW, Infinix inakusudia kuwapa nguvu vijana wa leo kujitokeza katika um ana kuonyesha ulimwengu wanachokiamini na kukisimamia.
Bidhaa za Infinix zinapatikana zaidi ya nchi 40 ulimwenguni, zikijumuisha Afrika, Amerika kusini, Mashariki ya kati na Kusini mwa Asia. Infinix kwa mwaka wa 2018-2020 imekuwa kwa kasi ya 160% kiasi cha kushangaza na huku kila leo ikija na mikakati mbalimbali kufikia watu wengi zaidi kupitia matangazo ya mitandaoni na uzalishaji wa simu zenye teknolojia ya hali ya juu.
VIONGOZI WA USHIRIKA IRINGA WAHIMIZWA KUSIMAMIA STAKABADHI YA GHALANI
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi Bw. Ellias Luvanda (kulia) akikabidhi tuzo ya kutambua utendaji mzuri katika uagizaji wa Mbolea kwa pamoja iliyotolewa na Mamlaka ya Mbolea TFRA , akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Iringa (IFCU) Bw. Victor Mwipopo (kushoto) wakati wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama hicho mkoani Iringa
Mrajis wa Vyama vya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akieleza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama hicho mkoani Iringa
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama Kikuu cha Ushirika IFCU Wakifuatilia taarifa wakati mkutano huo ukiendelea
Viongozi wa Vyama vya Ushirika wamepewa wito kusimamia matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani ili kuhakikisha wakulima wanapata masoko ya mazao yao na bei zenye tija kwa kuweka vipaumbele vya mipango ya ujenzi wa maghala kuanzia ngazi ya vijiji.
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa kupitia hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu tawala Msaidizi Uchumi Elias Luvanda wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 20 wa mwaka wa wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Iringa IFCU (1993) Ltd, uliofanyika Ijumaa Mei 07, 2021 Mkoani Iringa.
Katibu Tawala Msaidizi Luvanda amesema Serikali inahamasisha na kuendeleza wakulima kwa kuhakikisha Mfumo wa Stakabadhi ya Ghalani unaimarika.
Hivyo, amewataka Viongozi katika mkutano huo kuweka mipango yenye malengo ya kuongeza maghala ya kuhifadhi mazao ya wakulima ili kukabiliana na changamoto ya uchache wa maghala na kuzingatia matumizi bora ya maghala.
Aidha, amewataka viongozi wa Ushirika kuwa wasimamizi wazuri wa rasilimali za Vyama vya Ushirika, kuwajibika kwa wanachama wao kwa kufuata misingi na taratibu za Ushirika zitakazosaidia kuondokana na matumizi mabaya ya mali iza vyama pamoja na ubadhilifu.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika Dkt. Benson Ndiege akiongea kwa niaba ya wanaushirika amesema Vyama vya Ushirika vitaendelea kutoa ushirikiano na kuvitaka Vyama vya Ushirika kuanzia ngazi ya Vyama vya msingi kutimiza wajibu wao Kiushirika kama vile kuandaa makisio, kufanya mikutano mikuu ya mwaka pamoja na kuhakikisha wanachama wanalipa hisa za chama. Hivyo, kuwezesha Chama kikuu kufanya kazi vizuri na hatimaye mfumo wote wa Ushirika kutimiza wajibu wake.
“Wanachama wa Ushirika ndio wamiliki wa Vyama vya Ushirika hivyo viongozi wa Ushirika mnawajibika kwa wanachama wenu kuhakikisha mnatoa taarifa za utendaji, taarifa za fedha na maendeleo ya Vyama kupitia mikutano pamoja na matakwa mengine ya Sheria ya Vyama vya Ushirka Na.6 ya mwaka 2013,” alisema Mrajis
Aidha amewataka wajumbe wa Mkutano kusoma taarifa zinazotolewa na kuhoji pale inapobidi kuhusu masuala ya uendeshaji wa Chama chao kwani Mkutano Mkuu ndio ngazi ya juu ya maamuzi ya Chama
Hakikisheni mnafuatilia taarifa zitakazoendelea katika Mkutano huu pale mnapoona hamridhiki mna haki ya kuhoji, kupata majibu pamoja na kupitisha makisio na baada ya hapo Mrajis Msaidizi wa Mkoa na Maafisa Ushirika wanaidhinisha kwa mujibu wa Sheria.
Mrajis amewataka Viongozi wa Vyama vya Ushirika kuwa wabunifu kwa kubuni miradi mbalimbali yenye tija na maendeleo kwa Vyama vyao. Akiongeza kuwa ni muhimu Wanachama wa Ushirika waweze kupata thamani ya kujivunia vyama vyao kupitia huduma za Vyama zitakazowatofautisha wanachama na wasio wanachama wa Ushirika.
“Tuhakikishe kuwa ndani ya Vyama vya Ushirika wakulima wanapata huduma bora kama vile upatikanaji wa pembejeo kwa bei nafuu na kwa wakati, elimu ya ushirika, bima ya afya, masoko na bei nzuri za mazao,” alisisitiza Mrajis
Mrajis ameeleza kuwa dhana ya Ushirika ndio njia ya kuinua Uchumi wa watu wengi kwa pamoja hivyo ni muhimu kuzingatia utendaji wenye kuzingatia maadili na taratibu za Ushirika ili kulinda uendelevu wa Vyama na kujenga uchumi imara wa wananchi wanyonge.
Dkt. Ndiege amevitaka Vyama vyote vya Ushirika ambavyo vimepata hati chafu kwa mujibu wa Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) kufanya jitihada mahususi za kuondokana na dosari zilizosababisha hati hizo chafu. Alibainisha baadhi ya sababu za hati hizo ni kukosa elimu ya uandishi wa vitabu, utunzaji mbovu wa kumbukumbu na mengine.
Friday, 7 May 2021
RAIS SAMIA ATAJA SABABU ZA KUKUTANA NA WAZEE WA DAR
"Mimi nimekuja hapa sina jambo bali nimekuja niwasikilize, mnielekeze nikayafanyie kazi",amesema Rais Samia.
Rais Samia leo Ijumaa Mei 7,2021 amekutana na kuzungumza na wazee wa Dar es salaam
WAFANYAKAZI WA HOSPITALI WAKAMATWA KWA WIZI WA NETI ZA MBU HOSPITALI
Theresa Anyango Otieno, kaimu afisa katika hospitali eneo la Rabuor; Cynthia Akinyi, kaimu afisa anayeshughulikia usambazaji wa neti katika eneo la Nyang’ande; na David Ouma, afisa anayesimamia hospitali ya Nyang'ande wote walikamatwa Ijumaa, Mei 7,2021.
Kulingana na kamanda wa polisi wa kaunti ya Kisumu, Samuel Anampiu, watatu hao walihusishwa na kutoweka kwa mabunda 181 yaliyokuwa katika hospitali ya Nyang'ande na mabunda mengine 160 kutoka hospitali ya Rabuor, kila bunda likiwa na neti 50.
"Tumewakamata wafanyakazi watatu wa hospitali ambao tunaamini walihusika na wizi wa neti tangu walipoanza kusimamia usambazaji, " Anampiu alisema.
Kamanda wa polisi aliongeza kuwa bado wanawatafuta washukiwa wengine wawili, ambao ni Dickson Malit, aliyekuwa akihudumu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Rabuor na vile vila Samuel Omino.
Kukamatwa kwao kulijiri kufuatia malalamiko kutoka kwa wenyeji ambao walikuwa wamejitokeza kwa ajili ya kupokea neti za bure lakini wakarudishwa nyumbani baada ya kuarifiwa kuwa zimeisha.
Kwa kawaida neti husambazwa na serikali bila malipo kwa familia ambazo zinaishi katika maeneo ambayo huvamiwa na mbu.
Chanzo - Tuko News
MLINZI MBARONI KWA KUMUUA MKEWE BAADA YA KUMBAINI AKITUMIA ARV KWA KUJIFICHA
PROF.MKENDA : SERIKALI KUWEKA KIPAUMBELE CHA KWANZA KUFANYA UTAFITI WA MBEGU ZAO LA MUHOGO ILI KUONGEZA UZALISHAJI
Waziri wa kilimo Prof.Adolf Nkenda
Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Serikali imesema itaweka kipaumbele cha kwanza kufanya utafiti wa mbegu zao la muhogo ili kuongeza uzalishaji kutoka tani 8 hadi tani 50 kwa hekta.
Hayo yamebainishwa Leo Mei 7,2021 jijini Dodoma na Waziri wa kilimo Prof.Adolf Nkenda katika ufunguzi wa mkutano wa wadau wa kilimo Tanzania wenye lengo la kuongeza tija na kutumia fursa za masoko kwa zao hilo.
Prof. Mkenda ameainisha mikakati kabambe katika kuongeza tija zao la muhogo kuwa ni pamoja na uzalishaji kwa wingi na kuongeza bajeti.
Aidha Prof.Mkenda ameagiza kila afisa ugani anakuwa na shamba darasa kuanzia ekari moja na kuendelea .
Katika hatua nyingine Prof. Mkenda amesema maafisa ugani wote watanunuliwa simu za mkononi na kuunganisha na mfumo wa Mobile kilimo hali itakayorahisisha kujua kanzi data wanafanya nini kwa siku.
Pia Waziri huyo wa kilimo amesema serikali itahakikisha inaimarisha masoko ya zao la muhogo huku akitumia fursa hiyo kuipongeza Wilaya ya Kahama kwa kuendelea kufanya vizuri kwa vyama vya ushirika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Maendeleo ya mazao kutoka wizara ya kilimo Nyasebwa Chimago amebainisha malengo mengine ya Mkutano huo ni kutambua changamoto za zao la muhogo na kuzindua mikakati wa miaka 10 wa zao hilo kutokana na kutokuwa na uratibu.
Kauli mbiu ya mkutano wa wadau wa zao la muhogo Tanzania ni"Ongeza Tija,Tumia Fursa za Masoko,Muhogo Unalipa".