Sunday, 31 January 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 31,2021













Share:

TADB YAWEZESHA WAFUGAJI KUPATA NG'OMBE WA KISASA WA MAZIWA


Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada wa kwanza kulia akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 396 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kwa ajili ya wafugaji mkoani Tanga kupata mbegu ya ng’ombe bora wa kisasa wa maziwa wakiwemo wafugaji 114 kupitia vyama vya msingi 5 kupata mikopo ya ng’ombe wa kisasa wa kwanza kushoto anayshuhudia ni Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamungu
Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada wa kwanza kulia akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 396 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kwa ajili ya wafugaji mkoani Tanga kupata mbegu ya ng’ombe bora wa kisasa wa maziwa wakiwemo wafugaji 114 kupitia vyama vya msingi 5 kupata mikopo ya ng’ombe wa kisasa wa kwanza kushoto anayshuhudia ni Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamungu
Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada wa kwanza kulia akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 396 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kwa ajili ya wafugaji mkoani Tanga kupata mbegu ya ng’ombe bora wa kisasa wa maziwa wakiwemo wafugaji 114 kupitia vyama vya msingi 5 kupata mikopo ya ng’ombe wa kisasa wa pili kushoto anayeshuhudia ni Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamungu
 
Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada akizungumza wakati wa halfa hiyo
Sehemu ya wafugaji wakimsikiliza Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada akizungumza wakati wa halfa hiyo

BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imekwisha toa mikopo yenye thamani ya Shilingi billioni 11.80 ili  kuwezesha mnyororo wa thamani wa sekta ya maziwa kote nchini.

Pia imewezesha wafugaji Mkoani Tanga kupata mbegu ya ng’ombe bora wa kisasa wa maziwa wakiwemo wafugaji 114 kupitia vyama vya msingi 5 kupata mikopo ya ng’ombe wa kisasa wenye thamani ya Zaidi ya Tsh 396m.

Akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na shirika la kimataifa la Heifer,Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Benki ya Kilimo (TADB) Jeremiah Mhada alieleza umuhimu wa ushirikiano wa wadau muhimu katika sekta ya mifugo ili kuongeza tija nakuleta mapinduzi ya kweli katika sekta ya maziwa nchini.

Alisema  kupitia mkopo huu, TADB imeweza kuwajengea wafugaji hao mabanda ya kutunzia ng’ombe 25 na kupata mitamba ya kisasa ili wanufaike na ufugajiwa ng’ombe wa maziwa ikiwemo kupatiwa mikopo naafuaa itakayowawezesha kupata mbegu bora za ng'ombe wa maziwa.

 “TADB ili kuhakikisha wafugaji wananufaika na sekta hii ya maziwa tuliingia katika ushirikiano na shirika la kimataifa la Heifer International kuhakikisha wafugaji wetu wanajengewa uwezo wa namna bora ya ufugaji wa ng’ombe wa maziwa lakini pia kujiunga katika vikundi ili kuweza kupata mikopo kwa urahisi.”Alisema

TADB imewezesha vyama vya msingivya UWAMWA, CHAWAMU, UWAKO, UWAMKI na UWADAKI kuweza kupata jumla ya ng’ombe wa kisasa 156 kwa wafugaji 121 ikiwemo wanawake 39 pamoja na kuwawezesha kupata mkopo huo wafugaji hao tayari wana soko la kuuza maziwa yao.

"Kwa hapa Tanga wataweza kuuza kwa kampuni ya Tanga Fresh ambayo nayo TADB imekwisha iwezesha katika kumudu kuweza kununua maziwa kutoka kwa wafugaji hawa wadogowadogo.” Alisisitiza Mhada.

Kabla ya kufanya makabidhiano hayo,TADB kwakushirikiananaShirika la kimataifa la Heifer International waliendesha mafunzo kwa viongozi wa vyama vya ushirika 26 ambao walijengewa uwezo kwenye namna ya usimamizi bora wa biashara, usimamizi wa fedha, utunzaji wa kumbukumbu, utunzajiwa kumbukumbu na uongozi bora.


“Ufugaji ili uwe na tija nilazima wafugaji wajengewe uwezo na ni muhimu kufahamu namna ya kusimamia fedha, utunzaji wa kumbukumbu,uongozi bora na masuala mengine ya usimamizi wa biashara kwa kuwa na uwezo huu, mfugaji anaweza kuona namna anavyonufaika na mkopo na hata kuweza kufahamu kipato chake.”Aliongezea Mhada.

Alisema Wafugaji wadogo kupitia TADB wanaendelea kunufaika na fursa zilizopo kupitia benki ya kilimo na pia kupitia ushirikiano huo wa TADB nashirika la kimataifa la Heifer.
 
Serikali imeainisha sekta ya maziwa kama moja ya sekta muhimu katika kuchochea uwekezaji katika viwanda jambo ambalo TADB inawawezesha wawekezaji kama kampuni za Tanga Fresh, Kahama Fresh, Njombe Milk na viwanda vingine katika maeneo mbalimbali nchini.

Aliongeza kwamba kupitia uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo, pia kama Taifa wanaweza kujihakikishia upatikanaji na usalama wachakula,lishe bora na kipato kwa wafugajina pia kuongezapato la Taifa.

Mhada alisema sekta  ya maziwa nchini inachangia asilimia 1.2% yapato la Taifa huku akieleza ili kuhakikisha wanaongeza kipato kwa wafugaji wadogo wadogo ambao kupitia shughuli hizi za ufugaji huchangia pato la Taifa.

Alisema wamewezesha kupata mitamba ya kisasa na kuwaunganisha na masoko ili kuongeza thamani na kuchochea ongezauzalishaji wa mazi wa nchini.

Share:

Saturday, 30 January 2021

WAZIRI MWAMBE AKUTANA NA WAZALISHAJI WA SUKARI NCHINI JIJINI DODOMA

 

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akizungumza na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba aliyemtembelea ofisini kwake leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akimsikiliza Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba wakati wa mazungumzo ofisini kwake leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba mara baada ya mazungumzo ofisini kwake leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akizungumza na wazalishaji wa Sukari nchini na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

Baadhi ya wazalisha wa Sukari Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,wakati wa kikao cha wazalishaji wa Sukari nchini ambapo amesikiliza changamoto zao na kuahidi kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,akisisitiza jambo zaidi wakati wa kikao na wazalishaji wa Sukari nchini pamoja na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

Afisa Mtendaji Mkuu Utawala TPC Bw.Jaffari Ally akielezea jambo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe(hayupo pichani) wakati wa kikao cha wazalishaji wa Sukari nchini ambapo amesikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma

Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Sukari Tanzania Prof.Kenneth Bengesi,akizungumza kwenye kikao cha wazalishaji wa Sukari nchini ambapo Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Geoffrey Mwambe ameahidi kuzitatua changamoto hizo ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji wa Sukari leo Januari 29,2021 jijini Dodoma


Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,amekutana na wazalishaji wa Sukari nchini na kusikiliza changamoto zao ili kuzitatua na kuongeza uzalishaji na kuhakikisha Sukari inapatikana kwa urahisi wakati wote nchini.

Akizungumza na na wazalishaji hao leo Janauari 29,2021 jijini Dodoma Mhe.Mwambe amesema kuwa Serikali inalenga kuongeza uzalishaji wenye tija kwa kutumia teknlojia na miundombinu ya kisasa ya umwangiliaji.

”Leo nimekutana na nyie kwa leongo la kujifunza na kujua changamoto mlizonazo katika uzalishaji wa sukari nchini na waahidi tutazifanyia kazi”amesema Mhe.Mwambe.

Hata hivyo Mhe.Mwambe amewatoa wasiwasi wazalishaji hao kuwa Serikali itashughulikia changamoto hizo ili kuleta maendeleo na kuongeza uzalishaji zaidi nchini .

Awali Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Geoffrey Mwambe,amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu na Meneja wa kiwanda cha Dangote nchini Tanzania Bw.Abdullahi Baba.

Share:

WAFUGAJI NCHINI WATAKIWA KUFUGA KISASA

Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akizungumza wakati
wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga kushoto aliyekaa ni Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah Mhada
Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxoakizungumza wakati wa halfa hiyo
Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah Mhada akieleza jambo wakati wa halfa hiyo
Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamunguakizungumza wakati wa halfa hiyo
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga kulia ni Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo

Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akimshukuru Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo mara baada ya makabidhiano hayo kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga katika halfa hiyo
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akiwasha moja ya magari hayo

WAFUGAJI  nchini wametakiwa kubadilika na kuachana na ufugaji wa mazoea bali wafuge kisasa kwa ajili ya kupata mazao mengi lakini yenye ubora ambayo yataweza kuuzika kwa faida na hivyo kuongeza mchango wa pato la Taifa.

Ushauri huo umetolewa na Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga.

Alisema kuwa licha ya Tanzania kuwa na mifugo mingi lakini sekta hiyo mchango wake kwenye pato la taifa ni asilimia 7.9% pekee  kutokana na ufugaji wa kimazoea  ambao hautoi matokeo bora.

Akizungumzia uzalishaji wa maziwa nchini Waziri Ndaki alisema ni lita Bil 3.01 huku kati ya hizo lita Mil 2.1 zinatokana na ng'ombe wa asili Mil 31 huku ng'ombe wa kisasa Mil 2 wanatoa lita bil 0.9. 

"Kutokana na uzalishaji mdogo wa maziwa hata kiwango cha unywaji wa maziwa kwa mwananchi mmoja mmoja kimekuwa kidogo kwani kwa mujibu wa takwimu ni lita 54 kwa mwaka sawa na kijiko kimoja kwa siku" alisema Waziri Ndaki.

Nae Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamungu alisema kuwa uwepo wa mradi umesaidia kuongeza kasi ys uanzishwaji wa viwanda vya maziwa hadi kufikia vitano ambavyo vinazalisha maziwa kwa kutumia teknolojia ya UHT.

Alisema kuwa bado kumekuwepo na changamoto katika eneo la ukusanyaji wa maziwa kwani kuna kiasi kikubwa yanakuwa hana kosa ubora kabla ya kufika soko hivyo kuwa hasara kwa mfugaji.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji na masoko kutoka wizara ya mifugo na uvuvi Steven  Maiko alisema kuwa kutokana na tathimini waliyoifanya 2016/17 inaonyesha kuwa ifikapo mwala 2030/31 sekts hiyo itakabiliwa na upungufu mkubwa raslimali zake za nyama na maziwa kutokana na ongezeko la idadi ya watu.

Hivyo kutokana na changamoto hiyo serikali kwa kushirikiana na wahisani waliamua kuja na mradi huo ili  kuongezs uzalishaji, kudhibiti magonjwa ya mifugo lakini.na kuongeza mnyororo wa thamani wa maziwa ikiwemo kuweka mazingira safi ya kufanyabiashara.

Nae  Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo alisema kuwa lengo la mradi wa TMPP kuongeza kipato kwa wafugaji wapatao 50, 000 nchi nzima na kwa kipindi cha miezi mitatu pekee tayari wameweza kuwafikia wafugaji 45, 000 kwa kuwapa mafunzo ya ufugaji wa kisasa ili waweze kupata mazao bora na ambayo yataweza kuuza kwa urahisi.

Alisema kwa upande wa wasindikaji waweze kuwawezesha vifaa ili kuhakikisha wanaboresha ukusanyaji wa maziwa na kudhibiti ubotevu wake ili kumuhakikishia mfugaji  soko lenye uhakika.

Nae Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah Mhada alisema kuwa benki hiyo imewawezesha wafugaji mkopo wa zaidi ya sh Mil 396 pamoja na mitamba bora.

"Ili kuongeza kipato kwa wafugaji wadogo tumewawezesha kupata mitamba ya kisasa na kiwaunganisha ns masoko ili kuongeza thamani na kuchoches kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini" alisema Mhada.


Share:

RAIS MAGUFULI AZINDUA MRADI WA MAJI TABORA NA UJENZI WA JENGO LA WAGONJWA WA HUDUMA YA DHARURA HOSPITALI YA KITETE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wakati akizindua mradi mkubwa wa Maji ya Ziwa Victoria utakohudumia miji ya Tabora, Igunga na Nzega. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuzindua mradi mkubwa wa Maji ya Ziwa Victoria utakaohudumia miji ya Tabora, Igunga na Nzega.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati akikagua ujenzi wa Matanki makubwa ya kuhifadhia maji katika mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria katika miji ya Tabora, Igunga na Nzega.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati akikagua ujenzi wa Matanki makubwa ya kuhifadhia maji katika mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria katika miji ya Tabora, Igunga na Nzega
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati akikagua ujenzi wa Matanki makubwa ya kuhifadhia maji katika mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria katika miji ya Tabora, Igunga na Nzega


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakati akitoka kukagua ujenzi wa Matanki makubwa ya kuhifadhia maji katika mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria katika miji ya Tabora, Igunga na Nzega
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima, Mawaziri pamoja na viongozi wengine wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Idara ya Wagonjwa wa Huduma ya Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora leo tarehe 30 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Idara ya Wagonjwa wa Hudumaya Dharurakatika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora leo tarehe 30 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na WatotoDkt. Dorothy Gwajima wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo la Idara ya Wagonjwa wa Huduma ya Dharurakatika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora leo tarehe 30 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Mabula Mchembe mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Idara ya Wagonjwa wa Huduma ya Dharurakatika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora leo tarehe 30 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kukagua ujenzi wa jengo la Huduma ya Wagonjwa wa Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora leo tarehe 30 Januari 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa mkoa wa Tabora katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora leo tarehe 30 Januari 2021 mara baada ya kuzindua mradi wa maji ya kutoka ziwa Victoria pamoja na jengo la huduma kwa wagonjwa wa dharura.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi wa Tabora mara baada ya kuwahutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora leo tarehe 30 Januari 2021 mara baada ya kuzindua mradi wa maji pamoja na jengo la huduma kwa wagonjwa wa dharura.
Wanafunzi wa Chuo cha Utumishi Tabora wakifurahia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufulialipopita kuwaaga mara baada ya kuhutubia wananchikatika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora leo tarehe 30 Januari 2021
Kwaya ya Chuo cha Utumishi Tabora wakiimba Wimbo maalumu mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora leo tarehe 30 Januari 2021 mara baada ya kuzindua mradi wa maji pamoja na jengo la huduma kwa wagonjwa wa dharura.
Kwaya ya Chuo cha Utumishi Tabora wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora leo tarehe 30 Januari 2021 mara baada ya kuzindua mradi wa maji pamoja na jengo la huduma kwa wagonjwa wa dharura.

PICHA NA IKULU

Soma pia : 

RAIS MAGUFULI AZINDUA MRADI WA MAJI ISAKA- KAGONGWA ...AMPONGEZA AWESO KUFUKUZA WAKANDARASI FEKI



Share:

AGIZO LA WAZIRI NDAKI LATEKELEZWA... WATATU MBARONI

Na. Edward Kondela

Jeshi la polisi Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tarehe 27.01.2021 limewakamata watuhumiwa watatu kwa tuhuma za wizi na utoroshaji wa mifugo maeneo ya mipakani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mwishoni mwa wiki na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Salum Hamduni amesema jeshi hilo limewakamata watuhumiwa hao katika tarafa ya Loliondo, Wilaya ya Ngorongoro mkoani humo kufuatia agizo alilolitoa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki Jumatano iliyopita la kukamatwa kwa watuhumiwa 67 wa utoroshaji wa mifugo na mazao yake.

Kamanda Hamduni amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao watatu kunatokana na baada ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutangaza operesheni ya kudhibiti wizi na utororshaji wa mifugo maeneo ya mipakani ambapo zilipatikana taarifa za uwepo wa watu wanaojihusisha na wizi na utoroshaji wa mifugo katika Wilaya ya Ngorongoro.

Ameongeza kuwa upelelezi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo, mara utakapokamilika jalada litapelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Ametoa wito kwa wananchi kuepuka usumbufu kwa kuhakikisha wanafuata sheria za biashara ya usafirishaji wa mifugo kwani wasipofanya hivyo watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Jumatano ya wiki iliyopita Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki akiwa katika ofisi za wizara hiyo zilizopo katika mji wa serikali Mtumba jijini Dodoma wakati akiwasilishiwa ripoti ya uchunguzi, kuhusu utoroshaji wa mifugo mipakani aliliagiza Jeshi la Polisi nchini Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo kuwakamata mara moja watuhumiwa 67 wa utoroshaji wa mifugo na mazao yake kwenda nchi za jirani.

Katika ripoti ya uchunguzi, kuhusu utoroshaji wa mifugo mipakani, iliyowasilishwa na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Julius Mjengi kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki imeeleza kuwa kabla ya tarehe 7 Novemba, 2020, mifugo iliyokuwa inatoka kwenye minada ya awali ya Handeni na Kilindi kuelekea nchini Kenya kupitia mpaka wa Horohoro haikuwa inafuata taratibu za forodha kama shehena nyingine.

Aliongeza kuwa takwimu za daftari la mifugo katika mpaka wa Horohoro zinaonyesha idadi ya mifugo iliyopitishwa kuelekea nchini Kenya kwa kipindi cha miaka 17 kutoka mwaka 2003 hadi Novemba, 2020 ilikuwa ni ng’ombe 24,980 na Mbuzi na Kondoo 9,368 (sawa na wastani wa Ng’ombe 122 na Mbuzi/Kondoo 46 kwa mwezi).

Taarifa hiyo ilibainisha pia baada ya uchunguzi, ilionekana kuwa kati ya tarehe 7 Novemba, 2020 hadi tarehe 9 Desemba, 2020 (kipindi cha mwezi mmoja tu) jumla ya Ng’ombe 1,096 na Mbuzi na Kondoo 1,044 walipitishwa katika kituo cha Forodha kuelekea nchini Kenya, ambapo huo ni wastani wa idadi ya mifugo iliyopita mpakani ndani ya mwezi mmoja ukilinganisha na siku za nyuma.

Taarifa imebaini pia viashiria vya udanganyifu wa kurekodi idadi sahihi ya mifugo inayokaguliwa kwenda Kenya hususan katika mpaka wa Hororohoro – Tanga.

Mwisho.

Imetolewa: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

30.01.2021

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger