Saturday, 14 November 2020
NI MARUFUKU KULISHA MIFUGO VYAKULA VIBOVU-SERIKALI
Friday, 13 November 2020
SERIKALI KUNUNUA NDEGE YA MIZIGO..... KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA (TIC) CHAHAMISHIWA OFISI YA RAIS
Rais Magufuli amesema kipindi cha miaka mitano ijayo serikali yake imepanga kuendeleza miundo mbinu kwa kununua ndege moja ya mizigo ili kurahisisha usafirishaji wa mazao ya bustani, minofu ya samaki na nyama lengo ni kuwafanya wakulima watajirike kutokana na kazi wanayofanya.
Rais Dk Magufuli ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akizindua rasmi Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 12 huku akilihutubia bunge hilo na Taifa kwa ujumla na kusema kuwa lengo lake ni kuona kila mtanzania ananufaika na maendeleo ya ukuaji uchumi nchini.
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa serikali yake imepanga kuongeza tija kwenye kilimo kwa kukifanya kuwa cha kibiashara lengo likiwa kuwa na hifadhi kubwa ya chakula, malighafi za viwandani na kuuza pia nje ya nchi hivyo upatikanaji wa mbegu na zana za kilimo zitaboreshwa.
Pia Dkt.Magufuli amekihamisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda Ofisi ya Rais.Amesema kuwa anataka kupambana na wale wanaokwamisha uwekezaji, kwani anataka muwekezaji apewe kibali ndani ya siku 14.
“Nataka muwekezaji mwenye fedha zake akija apate kibali ndani ya siku 14, na kwa sababu hiyo nimeamua suala la uwekezaji ikiwa ni pamoja na Kituo Cha Uwekezaji (TIC) kulihamishia kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda ofisi ya Rais, ili wanaokwamisha nikapambane nao mwenyewe”.amesema Rais Magufuli
RAIS MAGUFULI AITAKIA KILA LA HERI TIMU YA TAIFA STARS DHIDI YA TUNISIA NA BONDIA MWAKINYO
Dr Magufuli ameyasema hayo leo tarehe 13 Novemba, 2020, wakati wa hotuba ya ufunguzi wa Bunge la 12 jijini Dodoma ambayo ilitoa dira ya uongozi wake katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
“Tutaanza kutenga fedha kidogo kidogo kwa ajili ya kuzianda timu zetu za Taifa na katika hilo napenda kutumia fursa hii, kuitakia heri timu yetu ya Taifa kwenye mechi yao dhidi ya Tunisia hapo baadaye,” alisema Magufuli.
Aidha Rais Magufuli aliongezea kwa kumtakia heri bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo ambaye anashuka ulingoni hapo baadaye, kupambana na bondia kutoka nchini Argentina kwenye pambano la raundi 12 la ubingwa wa mabara wa IBF.
“Na pia nataka kumtakia heri mwanamasumbwi wetu, Hassan Mwakinyo anayepambana leo, watanzania tunataka ushindi tumechoka kushindwa,” aliongezea Magufuli.
RAIS MAGUFULI : LENGO LA DEMOKRASIA NI KULETA MAENDELEO NA SIYO FUJO
RAIS MAGUFULI : UTUMBUAJI UTAENDELEA 2020 - 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amesema utumbuaji kwa watumishi wa umma wazembe, wala rushwa, wezi na wabadhirifu, utaendelea katika miaka mitano ijayo.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo kwenye Uzinduzi wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo amesema, watumishi wezi, wabadhirifu bado wapo hivyo ataendelea kuwang’oa.
“Watumishi wazembe, wala rushwa, wezi, wala mali bado wapo. Miaka mitano ijayo tutawashughulikia, kwa kifupi niseme utumbuaji utaendelea,” amesema Rais Magufuli.
Head Teacher Primary and Nursery School at Aga Khan Education Service, Tanzania (AKES, T)
The position Aga Khan Education Service, Tanzania (AKES, T), is a private, not for profit, service company registered under the Companies Act and operates three schools in Tanzania. The vision of AKES,T is to provide accessible, world-class education, which prepares students to become self-confident, open-minded articulate and ethical young people with academic qualifications to enable […]
The post Head Teacher Primary and Nursery School at Aga Khan Education Service, Tanzania (AKES, T) appeared first on Udahiliportal.com.
Head of Customer Service at DHL Tanzania
IT’S NOT JUST AN OPPORTUNITY TO GET ON THE CAREER LADDER. IT’S AN OPPORTUNITY TO HELP THE WORLD GET ON TOGETHER Why do people call us the world’s most international company? Is it because we operate in more countries than any other logistics provider? Is it because we invented cross border shipping over 45 years […]
The post Head of Customer Service at DHL Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.
IT Applications Developer at KCB Bank
Key Responsibilities Contribute application development objectives to the overall IT strategy. Work with business units to formulate banking products and contribute technical guidance to the procurement process. Analyze product requirements and design best-fit architecture and solutions guided by KCBT policies and industry best practice. Manage the project resources, schedule, costs, stakeholders, and the application development […]
The post IT Applications Developer at KCB Bank appeared first on Udahiliportal.com.
IT Manager Infrastructure at KCB Bank
Key Responsibilities Manage all data centers environmental parameters in Disaster Recovery and Production to ensure data center equipment’s are working at required environmental parameters. Report and remediate for any deviation Ensure optimal performance against baseline of infrastrsacture in both primary and secondary sites. Ensure any deviation is reported and remediated. Ensuring that systems configurations and […]
The post IT Manager Infrastructure at KCB Bank appeared first on Udahiliportal.com.
Rais Magufuli: Nchi Yetu Iko Salama
Rais Magufuli amesema katika awamu yake ya kwanza madarakani alihakikisha nchi inakuwa na amani huku akivipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kulinda mipaka ya nchi.
Ameeleza hayo leo Ijumaa Novemba 13, 2020 bungeni mjini Dodoma katika hotuba yake ya kulizindua Bunge.
Amesema Watanzania wameendelea kuwa wamoja licha ya kutofautiana katika dini, kabila na itikadi ya vyama vya siasa.
“Wakati naingia madarakani kulikuwa na wimbi kubwa la mauaji ya kutumia silaha mfano matukio ya Kibiti lakini kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na vyombo vya dola yalikomeshwa na kwa sasa nchi yetu ipo salama.
“Nchi yetu imeendelea kuwa kisiwa cha amani na mipaka yake imebaki kuwa salama. Navipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa waliyofanya ya kusimamia amani na niwashukuru pia Watanzania kwa kutoa ushirikiano kwa vyombo hivi.” Amesema
Rais Dr Magufuli Aahidi Kumpa Ushirikiano Mkubwa Rais wa Zanzibar Dr Hussein Mwinyi
Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo leo Novemba 13, 2020, wakati akihutubia na kufungua bunge la 12, kwenye ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
“Nitashirikiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kulinda amani, hatutakuwa na utani hata kidogo na mtu atakayetaka kuvuruga amani na kuingilia uhuru wetu, na namuahidi Rais Dkt. Mwinyi nitampa ushirikiano wa kutosha katika kukamilisha aliyoyaahidi”, amesema.
Aidha Rais Magufuli amesisitiza kuwa serikali yake itaendelea kuboresha mazingira kwa wananchi kuongeza kipato chao ikiwemo mazingira wezeshi ya biashara.
''Katika miaka mitano hii serikali ninayoiongoza itafungua milango ya majadiliano na sekta binafsi na wafanyabishara wote ili kujadili namna ya kuondoa migogoro ya biashara ili tutengeneza mabilionea wengi wakiwemo wabunge'', ameongeza.
IT Digital Channel Manager at KCB Bank
Key Responsibilities Provide technical support for digital channels applications by performing administrative role on the applications. Provide technical support during implementation of tasks related to digital channel projects. Provide monitoring for channels system to increase system availability Provides review of the existing channel services and provide strategic initiative that will improve customer experience and business […]
The post IT Digital Channel Manager at KCB Bank appeared first on Udahiliportal.com.
IT Security And Bcm Specialist at KCB Bank
Key Responsibilities Establish strategy that will provide data and information systems protection against unauthorized access, modification and/or destruction Establishing and managing intrusion detection mechanism, as well as assessment of system patterns to detect unusual patterns of behavior and quickly to determine the cause and deal with any threat. Analyse reports generated by the monitoring system […]
The post IT Security And Bcm Specialist at KCB Bank appeared first on Udahiliportal.com.
Serikali Itahakikisha Wakulima Wa Miwa Wanapata Soko La Uhakika-Kusaya.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amekitaka kiwanda cha sukari Kilombero kuongeza wigo wa ununuzi wa miwa ya wakulima ili uzalishaji wa sukari nchini uongezeke na kuondoa utegemezi wa sukari toka nje ya nchi.
Katibu Mkuu huyo ametoa agizo hilo leo (12.11.2020) wilayani Kilombero wakati akifungua Maonesho ya Siku ya Wakulima wa Miwa yaliyoandaliwa na wadau wa sekta ya sukari nchini.
“Kiwanda cha Sukari Kilombero hakikisheni mkakati wenu wa kuongeza uwezo wa kiwanda kuzalisha sukari toka tani 120,000 za sasa hadi tani 160,000 kwa mwaka unakamilika mapema ili miwa ya wakulima isikose soko kuchakatwa ” aliagiza Kusaya.
Kusaya alisema hayo kufuatia risala ya wakulima wa miwa wa Kilombero kuonesha kuwa uwezo wa kiwanda cha Kilombero kwa sasa ni kuchakata miwa tani 600,000 wakati uzalishaji toka kwa wakulima wadogo kwenye vyama vya msingi 20 vilivyopo Bonde la Kilombero umefikia tani 900,000 kwa mwaka hali inayopelekea malalamiko ya miwa kutonunuliwa.
Katibu Mkuu huyo wa wizara ya Kilimo alisema hali ya uzalishaji sukari nchini bado ni mdogo kukidhi mahitaji ya soko la ndani ambalo ni tani 450,000 kwa mwaka wakati uzalishaji wa viwanda vyote umefikia tani 350,000 hivyo kufanya nchi kutokuwa na utoshelevu wa sukari.
Kiwanda cha Sukari Kilombero kinaongoza nchini kwa kuzalisha sukari asilimia 65 inayochangiwa na wakulima wadogo kwa asilimia 30 toka wilaya za Kilombero na Kilosa hivyo serikali kwa kushirikiana na kiwanda hicho wataendelea kuweka mazingira wezeshi ya kupanua kiwanda.
Ili kukabiliana na upungufu wa sukari nchini Kusaya alisema serikali imeanzisha shamba la miwa Mkulazi ambapo itajenga kiwanda kikubwa cha sukari chenye uwezo wa kuzalisha tani 200,000 kwa mwaka na kuwa inaendelea pia kuhamasisha wawekezaji wengi zaidi kuanzisha viwanda vya sukari nchini
Katika hatua nyingine, Kusaya ametoa rai kwa taasisi za fedha ikiwemo mabenki ya biashara nchini kutoa mikopo yenye masharti nafuu ili wakulima wengi zaidi waweze kuanzisha mashamba ya miwa na viwanda vidogo vidogo vya sukari kukabiliana na changamoto ya mara kwa mara ya nchi kukosa sukari.
Kusaya alizitaka taasisi za fedha ikiwemo benki za NMB na CRDB kuangalia namna ya kupunguza riba kwa mikopo ya wakulima ili wasione ni mizigo na kushindwa kuwekeza kwenye sekta ya kilimo.
“ Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John John Pombe Magufuli tunataka kutimiza malengo ya msingi ya kuhakikisha tunatengeneza mabilionea wengi zaidi kutokana na uwekezaji kwenye kilimo“ alisisitiza Kusaya
Akizungumza na wakulima wa miwa na wadau wa sukari waliokusanyika Kilombero ,Kusaya amesema lengo la maonesho hayo ni kuhamasisha uzalishaji miwa unaotumia teknolojia ya kisasa na matumizi ya mbegu bora ili kuwezesha nchi kuwa na utoshelevu wa sukari.
Akizungumza kwenye maonesho hayo Afisa Ushirika na Msimamizi wa wakulima wa Bonde la Kilombero Jackson Mushumba alisema changamoto iliyopo sasa ni kiwanda cha sukari kuchukua miwa kigodo tofauti ya inayozalishwa na wakulima hali inayopelekea malalamiko na hasara.
"Wakulima wadogo wanazalisha miwa tani 900,000 kwa mwaka wakati uwezo kiwanda ni kuchakata miwa tani 600,000 tu kwa mwaka hivyo kuhitaji viwanda zaidi" alisema Mushumba.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Kiwanda cha Sukari Kilombero Guy Williams alisema wapo kwenye mkakati wa kupanua uwezo wa kiwanda ili changamoto ya miwa ya wakulima imalizike .
Williams aliongeza kusema kuwa kiwanda hicho kinaishi kwenye mwanga na maelekezo ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuhakikisha kinapanuka na kuwa ifikapo mwakani wamiliki na wenye hisa wawili wakubwa watakamilisha makubaliano ili kiwanda cha kisasa kianzishwe na kuchukua miwa yote ya wakulima.
"COVID- 19 ilituweka chini lakini sasa tumejipanga kurudia mazungumzo na makubaliano ili ifikapo Aprili 2021 tutaweza kupanua uwezo wa kiwanda kuchukua miwa yote ya wakulima takribani tani 800,000" alisema Williams.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Klobero akitoa salamu za mkoa kwenye maonesho hayo aliwapongeza wakulima wa miwa wa Kilombero na Kilosa kwa kazi nzuri ya uzalishaji hai inayoufanya mkoa wa huo kuongoza nchini kwa uzalishaji wa sukari.
Mhandisi Kalobero aliongeza kusema wanatambua changamoto za wakulima wa miwa ikiwemo tatizo la uchomaji moto mashamba na uwepo wa wadudu wasumbufu waitwao vidung’ata wa njano wanoshambulia miwa shambani hali inayowapunguzia kipato wakulima na kuwa serikali kupitia Kituo cha utafiti wa Kilimo (TARI) unashugulikia changamoto hizo haraka.
Maonesho hayo yameshirikisha wadau ikiwemo kiwanda cha sukari Kilombero, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI),Bodi ya Sukari, Taasisi za fedha, Chuo cha Taifa cha Sukari na wakulima toka Wilaya za Kilombero na Kilosa.
Mwisho
Imeandaliwa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo
KILOMBERO
12.11.2020
IT Applications And Software Development Manager at KCB Bank
Key Responsibilities Contribute application development initiatives to the overall IT strategy. Work with business units to formulate banking products and contribute technical guidance to the procurement process. Analyze product requirements and design best-fit architecture and solutions guided by KCBT policies and industry best practice. Manage the project resources, schedule, costs, stakeholders, and the application development […]
The post IT Applications And Software Development Manager at KCB Bank appeared first on Udahiliportal.com.
Bso Support Officer at KCB Bank
Key Responsibilities Ensure timely management of Close of Business processes and Ensure smooth T24 updates and reports for use within the KCB Bank Tanzania Work with T24 provider to ensure all Issues that has been escalated are resolved in time. Documentation of procedures and manuals use in systems operation activities Check system performance and report […]
The post Bso Support Officer at KCB Bank appeared first on Udahiliportal.com.