Na Regina Ndumbaro, Ruvuma
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Jeshi la Wananchi, Chandamali, na kuhudhuriwa na Hakimu Japhet Bwire Manyama, ambaye alitoa viapo kwa maafisa watendaji hao.
Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mkurugenzi wa Daftari la Wapiga Kura na TEHAMA Taifa, Stanslaus Mwita, kwa niaba ya Mheshimiwa Jaji Mstaafu Jacob Mwambegele, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Akizungumzia mafunzo hayo,yaliyoanza rasmi leo, Tarehe 1 Januari 2025M kurugenzi wa Daftari la Wapiga Kura na TEHAMA Taifa, Stanslaus Mwita, amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwafundisha watendaji jinsi ya kujaza fomu za uandikishaji na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (Voter Registration System - VRS) kwa ufanisi.
"Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora. Mafanikio ya zoezi hili yanategemea ushirikiano wa karibu kati ya watendaji wa uboreshaji, serikali, vyama vya siasa, na wadau wengine wa uchaguzi",amesema.
Pia, maafisa wa TEHAMA watapata mafunzo maalumu ya kushughulikia changamoto za kiufundi (troubleshooting) zitakazojitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji wapiga kura katika vituo vya kujiandikisha.
Mwita ameongeza kuwa mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya uandikishaji wapiga kura, hatua itakayosaidia kuhakikisha uwazi na kupunguza vurugu zisizohitajika.
Aidha, maafisa wa uandikishaji wamehimizwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa watendaji wa maeneo yao na kubainisha kuwa vitambulisho walivyopewa na Tume ni utambulisho wa kutosha katika maeneo waliopangiwa.
0 comments:
Post a Comment