Watu 11 wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa baada ya lori lililokuwa limebeba saruji kufeli breki na kugonga watu mashuhuda wa ajali ya gari dogo aina ya Coaster Tata katika kijiji cha Changombe, kata ya Segera, wilayani Handeni, mkoa wa Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha kwa sababu waliofariki walikuwa wakijaribu kuwasaidia majeruhi wa ajali ya awali.
Kwa mujibu wa taarifa, lori hilo lenye namba za usajili T 680 BQW, likiwa linatokea Tanga, lilishindwa breki na kuwakumba watu waliokuwa pembezoni mwa barabara, kusababisha vifo vya watu 11 papo hapo na kujeruhi wengine 13.
Mkuu wa Mkoa ametoa pole kwa familia za marehemu na kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi wote. Aidha, ametoa wito kwa madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kuhakikisha magari yao yanakuwa katika hali nzuri ya kiufundi ili kuepusha ajali za namna hii.
0 comments:
Post a Comment