KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiambatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Ndugu John Mongella, amemtembelea kwa ajili ya kumsabahi na kumjulia hali Mzee Philip Japhet Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu (Bara), nyumbani kwake Msalato, Dodoma, leo Jumapili tarehe 12 Januari 2025.
Baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye maktaba ya Mzee Mangula, Balozi Nchimbi pia alipata wasaa wa kuchukua picha yeye mwenyewe kwa njia ya 'selfie', kama inavyoonekana pichani.
0 comments:
Post a Comment