Saturday, 9 May 2020

Picha : MBUNGE WA USHETU ELIAS KWANDIKA AKABIDHI GARI LA WAGONJWA KITUO CHA AFYA MBIKA NA VIFAA KUKABILIANA NA CORONA....DC MACHA AWACHANA WANAOWAZA KAMPENI

Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akiwa ndani ya gari la Wagonjwa ‘Ambulance’ iliyotolewa na Serikali kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi amekabidhi gari la Wagonjwa ‘Ambulance’lililotolewa na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu.

Mhe. Kwandikwa amekabidhi gari hilo leo Jumamosi Mei 9,2020 katika hafla fupi ya makabidhiano ambayo imehudhuriwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Ushetu pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha.

Mhe. Kwandikwa amesema gari hilo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli katika kuboresha sekta ya afya ili wananchi waweze kupata huduma bora za afya.

“Naishukuru serikali kwa kusikia kilio cha wana Ushetu kuhusu changamoto ya gari la wagonjwa lakini pia nimshukuru pacha wangu Mhe. Azza kwa ushirikiano anaoendelea kuutoa katika jimbo hili na leo tumefanikiwa kupata gari kwa ajili ya wananchi”,alisema Mhe. Kwandikwa.

“Gari hili linaweza pia kutumika kuhudumia pia maeneo yanayozunguka kituo cha Mbika kama vile Ulowa na Uyogo ingawa kituo chake kikubwa kitakuwa ni hapa Mbika.Naomba gari hili litunzwe na litumike kwa malengo yaliyokusudiwa”,alisema Kwandikwa.

Katika hatua nyingine Mhe. Kwandikwa amekabidhi ndoo 28 za kunawia mikono zitakazogawiwa katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Ushetu, vitakasa mikono ‘ Sanitizers’,sabuni za maji, Barakoa ’Surgical Masks’ kwa ajili ya watumishi wa afya kituo cha afya Mbika.

Mhe. Kwandikwa pia amechangia shilingi Milioni 1 kwa ajili ya SACCOS ya akina Mama Uyogo huku Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga, Mhe, Azza Hilal Hamad akichangia shilingi 300,000/= kwa ajili ya SACCOS hiyo.

Awali akizungumza, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga, Mhe, Azza Hilal Hamad aliishukuru serikali kwa kutekeleza ahadi ya kuleta gari kwa ajili ya wagonjwa aliloliomba kwa ajili ya Kituo cha Afya Mbika akieleza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli inatekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.

“Mwaka 2018 Wakati Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifanya ziara katika Jimbo la Ushetu nilimuomba atusaidie kupata gari la wagonjwa,alikubali na leo hii gari limefika katika kituo cha afya cha Mbika ili wananchi wapate huduma. Namshukuru sana kaka yangu Elias Kwandikwa kwa ushirikiano anaotoa kwa wabunge wa mkoa wa Shinyanga katika kuwahudumia wananchi”,alisema Mhe. Azza.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha aliwapongeza wabunge hao (Azza Hilal na Elias Kwandikwa) kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiuonesha kusaidia wananchi huku akibainisha kuwa wabunge hao wamekuwa mstari wa mbele kuchangia shughuli za maendeleo.

“Mhe. Kwandikwa na Azza ni wabunge ambao wapo mstari wa mbele kuchangia shughuli za maendeleo,wao badala ya kujifungia wao wanatoka kuja kwa wananchi. Wabunge hawa siyo mara yao ya kwanza kushirikiana na wananchi kutekeleza ilani ya uchaguzi",alisema Macha.

“Tunaamini hata kama ni kesho yake tarehe 25 ni siku ya kupiga kura wao wakileta msaada tarehe 24 nikiwaona siku hiyo nitaona ni mwendelezo wala mimi siwezi kuona ni maajabu lakini tukipata watu wanakuja siku za mwisho mwisho hatukuwahi kuwaona tutauliza nyie mlikuwa wapi. 

Niseme kwa hakika mnachofanya ni mwendelezo wa yale mmekuwa mkifanya msije mkaacha kuleta mlivyobakiza mkasema mkija watasema mnafanya kampeni,tunaendelea pale tulipoachia…Wanaoanza ndiyo tutakuwa na mashaka nao”,alisema Macha.

“Kwa kweli naomba nitumie nafasi hii kuwashukuru sana na tunawaona nyinyi ni askari mlio mstari wa mbele na tunaendelea kuwakaribisha na nyinyi kwetu siyo wageni,mmezoea kuja kila siku. Na wale wengine ambao wanajaribu jaribu kupiga jalamba au kutaka kupiga jalamba waangalie umbali kutoka hawa walipo na walivyovifanya. Tuwape nafasi watekeleze majukumu kwa jinsi ambavyo sisi tunaona ni watu wanaotusaidia”,aliongeza Mkuu huyo wa wilaya.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la Wagonjwa ‘Ambulance’lililotolewa na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu leo Jumamosi Mei 9,2020. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga, Mhe, Azza Hilal Hamad, kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akiishukuru serikali kwa kuleta gari la Wagonjwa ‘Ambulance’ kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga, Mhe, Azza Hilal Hamad aliishukuru serikali kwa kutekeleza ahadi ya kuleta gari kwa ajili ya wagonjwa aliloliomba kwa ajili ya Kituo cha Afya Mbika akieleza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli inatekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akiishukuru serikali kuleta gari la wagonjwa Ushetu na kuwapongeza wabunge hao (Azza Hilal na Elias Kwandikwa) kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiuonesha kusaidia wananchi huku akibainisha kuwa wabunge hao wamekuwa mstari wa mbele kuchangia shughuli za maendeleo.
Gari la Wagonjwa ‘Ambulance’lililotolewa na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi (katikati) akikata utepe wakati akiwakabidhi viongozi wa halmashauri ya Ushetu gari la Wagonjwa ‘Ambulance’lililotolewa na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akiwasha gari la Wagonjwa ‘Ambulance’lililotolewa na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akiwa ndani ya gari la Wagonjwa ‘Ambulance’lililotolewa na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akiwa akiwasha king'ora ndani ya gari la Wagonjwa ‘Ambulance’lililotolewa na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa  akiwa ameshikilia sehemu ya Sanitizers na sabuni, barakoa alizotoa kwa ajili ya watoa huduma za afya katika kituo cha afya cha Mbika na vituo vingine vya afya katika Jimbo la Ushetu ili kujikinga na maambukizi ya COVID - 19.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa  akimkabidhi Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu, Mhe. Michael Matomora Sanitizers kwa ajili ya watoa huduma za afya katika kituo cha afya cha Mbika na vituo vingine vya afya kujikinga na maambukizi ya COVID - 19.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa akimkabidhi Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu, Mhe. Michael Matomora  ndoo moja kati ya ndoo 28 alizotoa kwa ajili ya kuwekwa katika maeneo mbalimbali katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu wananchi wanawe mikono kwa maji na sabuni ili kujikinga na maambukizi ya COVID - 19.
Ndoo 28 zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa kwa ajili ya kuwekwa katika maeneo mbalimbali katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu wananchi wanawe mikono kwa maji na sabuni ili kujikinga na maambukizi ya COVID - 19.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa akikabidhi  shilingi Milioni 1 kwa ajili ya SACCOS ya akina Mama Uyogo ambapo pia Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga, Mhe, Azza Hilal Hamad akichangia shilingi 300,000/= kwa ajili ya SACCOS hiyo.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

MBUNGE AZZA HILAL AMNUNULIA BAISKELI KIJANA ALIYEPATA ULEMAVU BAADA YA KUANGUKA KWENYE MTI MSALALA

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametoa msaada wa Baiskeli Maalumu kwa kijana Fikiri Francis (17),mkazi wa kata ya Lunguya halmashauri ya wilaya ya Msalala wilayni Kahama aliyepata ulemavu baada ya kuanguka kwenye mti wa mwembe.

Mhe. Azza amemkabidhi baiskeli hiyo kijana Fikiri Francis leo Jumamosi Mei 9,2020 mbele ya Mkuu wa wilaya ya Kahama,Mhe. Anamringi Macha.

“Nilipewa taarifa na Diwani wa kata ya Lunguya mhe. Benedicto Manwali kuhusu kijana huyu ambaye alipata ajali na kuvunjika mgongo mwaka 2018 akapata ulemavu na hawezi kutembea.Nimetafuta baiskeli kwa ajili ya kijana huyu na leo namkabidhi ili imsaidie kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine”,amesema Azza.

Naye Kijana Fikiri Francis na Diwani wa kata ya Lunguya mhe. Benedicto Manwali wamemshukuru Mbunge huyo kwa msaada huo ambapo sasa hatatumia magongo ya mti kutembea.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amemshukuru Mhe. Azza kwa kumsaidia baiskeli kijana huyo huku akimuomba kuendelea kusaidia watu wenye uhitaji katika jamii.
Wa pili kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati akitoa msaada wa Baiskeli Maalumu kwa kijana Fikiri Francis (17),mkazi wa kata ya Lunguya halmashauri ya wilaya ya Msalala wilayani Kahama aliyepata ulemavu baada ya kuanguka kwenye mti wa mwembe. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha ( wa pili kushoto) akimshukuru Mbunge Azza kwa kumsaidia baiskeli kijana Fikiri Francis (aliyekaa kwenye kiti kilichotolewa na Mbunge Azza Hilal). 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akimpa pole kijana Fikiri Francis kwa ajali iliyompata na kumsababishia ulemavu.
Share:

MBUNGE AZZA HILAL ACHANGIA MIFUKO YA SARUJI KWA AJILI YA UJENZI WA UZIO SHULE YA SEKONDARI MWENDAKULIMA KAHAMA MJI


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) amechangia Mifuko 50 ya saruji yenye thamani ya shilingi 900,000/= kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo katika halmashauri ya Mji Kahama.

Mhe. Azza amekabidhi mchango huo leo Jumamosi Mei 9,2020 kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha.

Mhe. Azza amesema mifuko hiyo ya saruji itasaidia katika ujenzi wa uzio unaoendelea katika shule ya Sekondari Mwendakulima ambayo wasichana wanakaa bweni ili kusaidia kuimarisha ulinzi katika shule hiyo.

“Tukiwa kwenye ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye shule hiyo mwaka 2018 katika risala yao walieleza changamoto ya kutokuwa na uzio nikaahidi kuwa na mimi nitachangia ili watoto wetu wasome katika mazingira bora na salama zaidi”,ameeleza Mhe. Azza.

“Mhe. Mkuu wa wilaya nimenunua mifuko 50 ya saruji yenye thamani ya shilingi 900,000/=, naomba kukukabidhi risti ya manunuzi ya mifuko hiyo ya saruji ambayo itapelekwa shuleni”,ameongeza.

Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha alimpongeza Mhe. Azza kuendelea kutekeleza ahadi alizoziahidi kwa wananchi na kueleza kuwa mifuko hiyo ya saruji itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa kuboresha miundombinu ya shule ya Sekondari Mwendakulima.

“Mhe. Azza ni Mbunge anayetekeleza kwa vitendo ahadi alizoahidi na wakati wa uchaguzi aliomba ushirikiano na ameouonesha katika kuwaletea maendeleo wananchi,tunamshukuru sana kwa mchango wake na siyo mara yake ya kwanza kufika Kahama kuchangia shughuli za maendeleo…huu ni mwendelezo wa shughuli ambazo amekuwa akizifanya”,ameongeza Macha.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku huku wakichukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha risti ya manunuzi ya Mifuko 50 ya saruji yenye thamani ya shilingi 900,000/= kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo katika halmashauri ya Mji Kahama. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akimshukuru Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) kwa mchango wa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika shule ya sekondari Mwendakulima.

Share:

MBUNGE AZZA HILAL ATOA MSAADA WA KOMPYUTA KATIKA SHULE YA SEKONDARI BULIGE NA NGAYA JIMBO LA MSALALA

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametoa msaada wa Kompyuta mbili zenye thamani ya shilingi milioni 4 kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya walimu wa Shule ya Sekondari Bulige na Ngaya zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala.

Akikabidhi Kompyuta hizo kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha leo Jumamosi Mei 9, Mhe. Azza amesema Kompyuta hizo zitawasaidia walimu wa shule hizo katika shughuli zao.

“Nilitembelea shule ya Ngaya walimu wakaniomba niwachangie Computer. Leo nakabidhi Computer mbili zenye thamani ya shilingi 2,000,000 kila moja kwa ajili ya shule ya sekondari Bulige na Ngaya”,amesema Azza.

Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha amemshukuru Mbunge Azza kwa kuchangia katika sekta ya elimu na kuongeza kuwa Kompyuta hizo zitasaidia kurahisha kazi za walimu na mawasiliano kwa njia ya mtandao wa Intaneti.
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha  Kompyuta mbili zenye thamani ya shilingi milioni 4 kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya walimu wa Shule ya Sekondari Bulige na Ngaya zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha  Kompyuta mbili zenye thamani ya shilingi milioni 4 kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya walimu wa Shule ya Sekondari Bulige na Ngaya zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala.

Share:

Wagonjwa Wa Corona Nchini Kenya Wafika 649

Visa vya maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Kenya vimeongezeka na kufikia 649, baada ya hii leo kutangaza visa vipya 28. 

Aidha idadi ya vifo navyo imeongezeka na kufikia 30, huku waliopona wakifikia 207.


Share:

MBUNGE AZZA HILAL ACHANGIA NDOO SITA ZA RANGI UJENZI OFISI YA CCM TAWI LA BUGANZO JIMBO LA MSALALA


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametekeleza ahadi ya kuchangia ndoo sita za rangi kwa ajili ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi tawi Buganzo kata ya Ntobo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala (Jimbo la Msalala).

Akikabidhi ndoo hizo kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama,Thomas Myonga leo Jumamosi Mei 9,2020, Mhe. Azza amesema mchango huo ni kuunga juhudi za wanachama wa CCM ambao wamejenga ofisi ya chama.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama,Thomas Myonga amemshukuru Mbunge Azza Hilal kwa kutimiza ahadi yake ya kusaidia ujenzi wa ofisi hiyo ya chama.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi ndoo sita za rangi Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama,Thomas Myonga (wa pili kulia) kwa ajili ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi tawi Buganzo kata ya Ntobo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala leo Jumamosi Mei 9,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Ndoo sita za rangi Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama,Thomas Myonga zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) kwa ajili ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi tawi Buganzo kata ya Ntobo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala
Share:

Nafasi Za Kazi Zaidi ya 150 Zilizotangazwa Serikalini......Mwisho Wa Kutuma Maombi ni Mwezi Huu wa Tano























Share:

Wagonjwa Wa Corona Uganda Wafika 114 Baada Ya Wengine 13 Kuongezeka

Nchi ya Uganda imepata maambukizi mapya 13 ya Corona na kufikisha idadi ya wagonjwa kuwa 114.

Miongoni mwa wagonjwa hao wapya, 7 ni madereva kutoka Kenya, 4 madereva wa Uganda huku 2 ni kutoka Tanzania.


Share:

Bunge Laishauri Serikali Itumie Vyema mdororo wa bei ya mafuta duniani Kujiwekea Akiba Ya Kutosha Ya Mafuta

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati, imeishauri serikali kutumia vyema mdororo wa bei ya mafuta duniani, ili kupata mafuta kwa masharti nafuu na kuanzisha hifadhi ya mafuta kimkakati kwa ajili ya siku zijazo.

Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo bungeni jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dunstun Kitandula, alisema ni vyema kwa wakati huu serikali ikazungumza na nchi rafiki zinazozalisha mafuta ili kupata mafuta hayo.

Alisema katika kutekeleza hilo ni vyema Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) liwezeshwe ili kupokea akiba hiyo ya mafuta.

Alisema tayari ulimwengu umeanza kushuhudia Sekta za Usafiri wa Anga na Utalii zikisimama, biashara na uzalishaji viwandani kushuka na hivyo kushuka kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mafuta na bei yake kuporomoka.

"Kufuatia mkanganyiko huu na mwenendo usiotabirika wa soko la mafuta ulimwenguni, ipo haja kwa nchi yetu kuweka mikakati thabiti ya kuhakikisha nchi inakuwa na akiba ya mafuta ya kutosha wakati wote,” alisema.

Kitandula alisema kamati pia ilichambua taarifa kuhusu hali ya upatikanaji wa mafuta nchini na kubaini kuwa, kwa kipindi chote cha Julai 2019 hadi Februari 2020, hali ya upatikanaji wa nishati hiyo ilikuwa nzuri na nchi ilikuwa na akiba ya mafuta ya kutosha kwa wastani wa zaidi ya siku 40 kwa kila aina ya mafuta.

“Hii ni ongezeko la asilimia 55 kulinganishwa na siku 15 za akiba ya mafuta zinazotakiwa kwa mujibu wa kanuni,” alibainisha.

Alisema mfumo wa BPS (Bulk procurement System) umewezesha kupungua kwa gharama za meli kusubiri kupakua mafuta kutokana na upangaji na usimamizi mzuri wa uletaji meli za mafuta (laycan) ambao umepelekea muda wa meli kusubiri kupungua kutoka wastani wa siku 45 kwa siku za nyuma hadi wastani wa siku tano kwa sasa.

“Kamati ilibaini kuwa, kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Februari 2020, gharama za meli kusubiri imepungua kwa asilimia 18.4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka 2018/2019,”alifafanua.

Alisema jumla ya lita 4,161,067,814.92 za mafuta ya dizeli, petroli, ndege na taa ziliingizwa kwa matumizi ya ndani ya nchi (local) na nchi za jirani (transit) kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Februari 2020.

Kitandula ambaye ni Mbunge wa Mkinga, alisema katika kiasi hicho cha mafuta, jumla ya lita 2,398,969,342.12 sawa na asilimia 58 kilikuwa kwa ajili ya matumizi ya ndani, na lita 1,762,098,472.80 sawa na asilimia 42 kwa ajili ya nchi za jirani.

Vilevile, alisema kamati imeridhishwa na hali ya upatikanaji wa mafuta nchini pamoja na usimamizi mzuri wa uagizaji wa mafuta unaofanywa na wakala wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja (PBPA) kwa kushirikiana na mamlaka nyingine.



Share:

Mchango Wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam Katika Mapambano Dhidi Ya Virusi Vya Corona

Chuo  Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimeanza usanifu wa kuunda mashine za kupumulia ya kiotomatiki inayowasaidia wagonjwa waliozidiwa kupumua na kufanya utafiti wa tiba mbadala zinazoonyesha uwezekano wa kuzuia au kupunguza makali ya ugonjwa wa corona.

Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa  na Ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Utafii), ikielezea mipango mbalimbali ambayo chuo kimejiwekea kusaidia jitihada za serikali kupambana na ugonjwa huo.

Ilisema UDSM pia imejiandaa kutoa fedha za utafiti kuhusu ugonjwa wa corona na imewahimiza watafiti wake kuendelea kufanya utafiti kwa kasi zaidi ili kupata tiba, kinga au njia nyingine ya kudhibiti maambukizo ya ugonjwa wa corona.

“Kupitia Ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo-Utafiti, Chuo kimetenga fedha za utafiti na uvumbuzi kiasi cha Sh. 1,500,000,000 katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 kwa ajili ya mapendekezo yanayohusu athari za maradhi ya Covid-19 na mada nyingine za utafiti,” ilisema.

Ilisema UDSM, kupitia Kituo cha Maendeleo na Uhawilishaji wa Teknolojia (TDTC), kimebuni aina mbili za mashine za kunawia mikono za kiotomatiki na zinazotumia miguu.

Taarifa hiyo ilisema mashine hizo zina tangi la lita 250 na zimeandaliwa maalumu kwa ajili ya taasisi zinazohudumia idadi kubwa ya watu kama vile maeneo ya hospitali, viwanda na masoko.

Ilisema mashine hizo zinatoa sabuni ya maji na maji baada ya mtu kusogeza mikono karibu na sensa kwa upande wa mashine za kiotomatiki na kukanyaga pedeli kwa upande wa mashine zinazoendeshwa kwa kutumia miguu.

“Mashine hizi ni nzuri na hazihitaji kufunguliwa kwa mikono hivyo kupunguza uwezekano wa kuambukizana kwa kushika mabomba ya maji, aidha, Chuo tayari kimeshauza mashine hizi katika taasisi kadhaa zikiwamo, Amref, BoT, NHIF, TAA, WFP, TOL, Tamisemi, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Tanesco,” ilisema taarifa hiyo.

Ilisema kama mchango wake kwa jamii, UDSM, kupitia TDTC, kinatengeneza mashine 20 za kunawia mikono zitakazotolewa kama msaada kwa hospitali za serikali zilizoandaliwa kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa Covid-19 jijini Dar es Salaam na mashine zingine zitapelekwa katika vituo vikuu vya mabasi na daladala.

Ilisema kitengo cha vitambaa na nguo cha Idara ya Uhandisi Mitambo na Viwanda kikishirikiana na Kituo cha (TDTC) cha UDSM kimeanza uzalishaji wa barakoa za kiwango cha hali ya juu zenye matabaka matatu.

Kuhusu uzalishaji wa vitakasa mikono, ilisema UDSM imeanzisha mradi wa kuzalisha bidhaa hiyo kwa ajili ya matumizi yake ya ndani na ya umma kwa ujumla.

Ilisema taratibu za uzalishaji wa vipukusi hivyo vya mikono zimezingatia mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani, pamoja na viambata vingine, kunahitajika alkoholi isiyopungua asilimia 60.

Kuhusu upimaji wa ubora wa barakoa ilisema UDSM kupitia vitengo vyake mbalimbali kimekamilisha utafiti wa ubora wa barakoa za vitambaa zinazozalishwa na taasisi na watu mbalimbali.

“Matokeo ya utafiti huo utakaotolewa hivi karibuni yameainisha aina mbalimbali za vitambaa vinavyotumika na ubora wake na utafiti huo umekuja na mapendekezo ya namna ya kutengeneza barakoa za vitambaa zenye ubora,” ilisema.

Ilitaja hatua zingine inazochukua kuwa ni kubaini, kupima na kuchanganua sumu katika bidhaa asilia zilizoteuliwa kama vile matunda, mboga, mimea-tiba kwa ajili ya kuongeza virutubisho na kuandaa bidhaa za tibalishe.



Share:

Jela Miaka 15 Kwa Kumuua Ndugu Yake Bila Kukusudia

Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Kigoma imemhukumu mkazi wa Kijiji cha Kajana, Wilaya ya Buhigwe, Doto Simoni (21), kifungo cha miaka 15 jela baada ya kukiri kumuua bila kukusudia ndugu yake Manase Ezekieli kwa kumpiga na mti usoni na kufariki dunia papo hapo.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, Athumani Matuma baada ya mshitakiwa huyo kukiri kosa.

Matuma alisema mahakama hiyo inatoa adhabu kali kwa mshitakiwa huyo ili iwe fundisho kwake na kwa vijana wengine wenye tabia za kikatili kama yake.

Alisema mshitakiwa alimuita Manase ambaye kwa sasa ni marehemu aliyekuwa akiishi Wilaya ya Kasulu amfuate kwa ajili ya kumpa dawa ili asilogwe na wachawi.

Jaji Matuma alisema alipofika, mshitakiwa alimchukua ndugu yake huyo na kumpeleka kando ya mto Chai na kumwambia akae chini na kufumba macho na kisha anyanyue uso juu, ndipo alipochukua mti na kumpiga usoni kitendo kilichomfanya aanguke chini na kufariki dunia papo hapo.

Vile vile, alisema mshitakiwa alirudi nyumbani kwake na kunyamaza kimya na kudai kuwa hajui ndugu yake alipo.

Alisema ndugu wengine wa marehemu walienda kutoa taarifa polisi za kupotea kwa ndugu yao na walianza kumtafuta sehemu mbali mbali.

Alisema ndugu wengine wa marehemu pamoja na polisi walimshuku mshitakiwa na kumkamata na kumbana ndipo alipokiri kumuua.

Jaji Matuma alisema baada ya kufika eneo la tukio, walikuta mifupa ya binadamu na nguo za marehemu ambazo ni shati, suruali, bukta na mti, ambazo ndugu wa marehemu walizitambua kuwa ni za marehemu Ezekiel.

Jaji Matuma alisema kitendo alichokifanya mshitakiwa huyu ni cha kikatili pamoja na kukiri kosa lake mahakama inamtia hatiani kwa kosa la kuua ndugu yake bila kukusudia.

Alisema upande wa mashitaka ulikuwa ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Benedict Kivuma.

Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili wa kujitegemea Diana Damson, uliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kuwa bado mdogo na amekaa mahabusu kwa miaka miwili.

Hata hivyo, Jaji Matuma alitupilia mbali utetezi huo.


Share:

Serikali Yasema Dawa Ya Corona Iliyopokelewa Toka Madagascar Haitagawiwa Kwa Wananchi Hadi Ifanyiwe Utafiti Kwanza

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema kuwa dawa za kukabiliana na virusi vya corona ambazo Tanzania imepokea kutoka nchini Madagascar hazitogawiwa kwa wananchi kwa sasa.

Akizungumza katika hafla ya upokeaji wa dawa hizo hapa nchini, Prof. Palamagamba kabudi amebainisha kuwa dawa hizo zitafanyiwa utafiti kwanza, na zitakapothibitika kuwa zina faa, ndipo wananchi wataanza kutumia.

“Dawa hii tumepewa na Madagascar ili tuje tuifanyie utafiti kabla ya kuitumia. Tungekuwa tumeenda kuchukua dawa kwa ajili ya Watanzania wote tungeenda na Bombardier au Airbus, lakini tulienda na ndege ya Rais. Na ieleweka hatukwenda kuchukua kikombe cha babu,” amesema Kabudi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Prof. Abel Makubi amebainisha kuwa katika uchunguzi utakaofanyika, wataaangalia kama dawa hiyo ni salama kutumiwa, na pia ubora wake katika kupambana na corona.

Ameongeza kuwa nchini Madagascar tayari wamefanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa dawa hiyo inafaa ndio maana wameanza kutumia.

Pia amesisitiza kwa mara nyingine kwamba ieleweke kwamba dawa hiyo haikuletwa kwa ajili ya kugawiwa kwa watu.


Share:

Watiwa Mbaroni Kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kutumia akaunti Feki Facebook Yenye Jina la Mama Janeth Magufuli

KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA YA UDANGANYIFU [MTANDAO WA KIJAMII].

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili 1. SOPHIA ELIA MWALUANDA [22] Mfanyabiashara na Mkazi wa Sistila Jijini Mbeya na 2. MPAJI SELEMAN MWINYIMVUA [38] Mkazi wa Manzese Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kutumia akaunti feki ya “facebook” yenye jina la Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli Mke wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.

Watuhumiwa wamekamatwa mnamo tarehe 28.04.2020 majira ya saa 15:00 Alasiri katika operesheni na msako uliofanywa huko eneo la Ikuti Sokoni, Kata ya Ikuti, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya.

Mbinu wanayoitumia watuhumiwa ni kufungua akaunti “facebook” yenye jina la JANETH MAGUFULI SACCOS na kuuaminisha umma kwa kuweka picha ya mama Janeth Magufuli na kisha kutangaza kutoa mikopo nafuu kwa sharti la muombaji kutuma kwanza fedha kiasi cha Shilingi 76,500/= kwenye namba ya simu waliyoiweka kama ada ya mkopo ili aweze kupata mkopo wa Shilingi Milioni 3,000,000/=.

Watuhumiwa wamekutwa na simu mbili aina ya Infinix Smartphone ambayo imetumika kufungulia akaunti hiyo ya “facebook” na simu aina ya Siccoo Mobile [Analogue] inayotumika kupokea fedha zinazotumwa na watu mbalimbali. Aidha watuhumiwa wamekutwa na fedha taslimu shilingi 470,000/= ambazo wamekiri kuzipata kwa njia ya udanganyifu kupitia akaunti hiyo feki.

Mtakumbuka Februari 21, 2020 huko katika Mji Mdogo wa Mbalizi Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliwakamata vijana kumi na moja [11] kwa tuhuma za kujihusisha na wizi kwa njia ya mtandao kwa kutumia akaunti feki za mitandao ya kijamii ikiwemo “facebook” wenye majina ya viongozi wa Serikali na Wasanii maarufu wa hapa nchini. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

WITO WA KAMANDA.

Natoa rai kwa watanzania kuheshimu ikulu kwani ni mahali patakatifu na hapachezewi kabisa, Chombo cha dola hakitavumilia kuona mtu wa aina yeyote kwa vyovyote vile akitumia jina la ikulu kuibia au kutapeli watu wengine.

Ninatoa wito kwa wananchi kuwa makini na taarifa mbalimbali zinazotolewa kwenye mitandao ya kijamii ambazo zinaelekezea fursa mbalimbali kama vile ya mikopo, masomo na biashara ambazo zinawataka kutuma kiasi kadhaa cha fedha ikiwa ni moja ya masharti ya kupata fursa hiyo, ni vyema kujiridhisha kwenda mamlaka za serikali zilizo karibu kwa ajili ya kupata uhakika kabla ya kufikia uamuzi wa kutuma fedha.

Aidha ninawataka vijana kujenga utamaduni wa kufanya kazi ili kujipatia kipato halali badala ya kujiingiza kwenye vitendo vya kihalifu ambavyo vitawasababisha kupata adhabu kali kwa mujibu wa sheria.

Mwisho, ninatoa rai kwa mtu/watu waliotuma fedha kupitia namba ya watuhumiwa kwa lengo la kupata mkopo kufika kituo cha Polisi kilichopo jirani kwa ajili ya kutoa taarifa ili taratibu za kisheria zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA MAUAJI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wanne 1. RIZIKI ANTHONY MUHEMA [20] Mkazi wa Mtakuja Mbalizi, 2. REHEMA KASELA [36] Mama Mzazi wa marehemu na Mkazi wa Iwindi 3. ESTA MSONGOLE [52] Mganga wa Kienyeji na Mkazi wa Sumbawanga na 4. MTUMWA HAONGA [65] Mganga wa Kienyeji na Mkazi wa Mtakuja Mbalizi kwa tuhuma za mauaji ya mtoto TAMALI SIMON, miaka miwili na miezi mitatu.

Watuhumiwa walikamatwa katika operesheni maalum iliyofanywa na kikosi kazi cha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya tarehe 06.05.2020 majira ya saa 04:00 usiku huko Iwindi, Kata ya Utengule Usongwe katika Mji Mdogo wa Mbalizi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao ambao wamekiri kufanya tukio hilo kwa kushirikiana na mama mzazi wa marehemu.

Chanzo cha tukio ni tamaa ya kupata utajiri kwa njia za kishirikina baada ya mtuhumiwa ambaye ni mganga wa kienyeji kuwapa masharti yaliyopelekea kifo cha mtoto huyo.

Awali mnamo tarehe 04.05.2020 majira ya saa 20:00 usiku huko Kijiji na Kata ya Iwindi, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya, Mtoto TAMALI SIMON, miaka miwili na miezi mitatu, Mkazi wa Iwindi alikutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na mtu asiyejulikana na mwili wake kutelekezwa.

Kutokana na tukio hilo, Kikosi kazi cha Polisi Mkoa wa Mbeya kilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa katika maeneo tofauti na katika mahojiano watuhumiwa wamekiri kuhusika kwenye tukio hilo baada ya kupewa masharti na mganga wa kienyeji. Aidha upekuzi umefanyika nyumbani kwa Mganga wa kienyeji na kukamata vifaa mbalimbali vya uganga na dawa za kienyeji za aina mbalimbali. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA TUKIO LA MAUAJI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wanne 1. VIOLETH SIMELUTA [26] Mwalimu na Mkazi wa Isanga, 2. CHARLES SIMELUTA [39] Mkazi wa Isanga, 3. EMMANUEL KIWALE [30] Mkazi wa Mafiati na 4. SOPHIA SAMSON [42] Mkazi wa Airport ya Zamani kwa tuhuma za mauaji ya JUNIOR CHARLES MACHIBYA [30] Mkazi wa Airport ya Zamani.

Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 07.05.2020 baada ya kikosi kazi cha Polisi Mbeya kufanya msako na upelelezi wa kina na kubaini kuwa marehemu aliuawa kwa kupigwa vitu butu usoni na kunyeshwa sumu huku chanzo cha tukio hilo kikiwa ni ugomvi wa kifamilia.

Awali mnamo tarehe 30.04.2020 majira ya saa 20:00 usiku huko Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya JUNIOR CHARLES MACHIBYA [30] Mkazi wa Airport ya Zamani alifikishwa Hospitalini hapo na wasamalia wema wakidai kuwa amekutwa maeneo ya nyumbani kwake akiomba msaada na akilalamika maumivu makali ya tumbo akidai kuwa amenyweshwa sumu bila kutoa ufafanuzi zaidi.

Tarehe 01.05.2020 majira ya saa 18:00 jioni alifariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibabu na ndipo upelelezi ulianza pamoja na msako na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo. Upelelezi unaendelea.


Share:

WATAALAMU WA SEKTA YA RASILIMALI WATU NA WADAU WA SEKTA YA UCHUMI KUKUTANA MTANDAONI

Wakati janga la Corona limeathiri njia za ufanyaji kazi duniani kote, kampuni nyingi duniani zimelazimika kutafuta namna mpya ya ufanyaji kazi.


 Nchini Tanzania, kampuni ya BrighterMonday Tanzania imeandaa semina ya mtandaoni itakayowakutanisha wataalamu katika sekta ya Rasilimali Watu pamoja na wadau katika sekta ya biashara kujadili mchango wa Rasilimali Watu katika kuhakikisha Uendelevu wa Biashara wakati wa mlipuko wa virusi Corona.  

Semina hiyo itafanyika Jumanne, Mei 12, 2020 kwa njia ya mtandao na kuwakutanisha waajiri na wadau mbalimbali wa uchumi na biashara kutoka nchini na nje ya Tanzania. Semina hiyo itaendeshwa na wabobevu katika sekta ya Rasilimali Watu, Bw. Mosses Raymond pamoja na Heather O'shea. Kwa mujibu wa mtandao wa BrighterMonday Tanzania, Maafisa Rasilimali Watu kote nchini wanakaribishwa kushiriki kwa kujisajili kupitia tovuti (https://bit.ly/2SLiDKb)   

Kupitia semina hiyo, wadau wa sekta ya uchumi hasa waajiri watanufaika na uzoefu kutoka kwa makampuni makubwa ambayo yatatoa uzoefu na mbinu za kuendelea na utendaji hasa wakati huu ambapo biashara zimekuwa katika mkwamo, washiriki watanufaika na mbinu za namna ya kuendelea kupata wataalamu, mbinu za namna kukabiliana na mabadiliko ya usaili na kupata wasaa wa kubadilishana mitazamo ya kitaalamu na manguli katika sekta ya rasilimali watu.  

BrighterMonday Tanzania wameandaa mfululizo wa semina kwa njia ya mtandao kama sehemu ya utekelezaji wa  programu yao inayokwenda kwa jina la 'Umoja Wakati wa Shida' yenye lengo la kuhakikisha uendelevu wa biashara wakati huu wa mlipuko wa virusi vya Corona. 

Je, ungependa kuwa sehemu ya semina hiyo ya mtadaoni? Tembelea tovuti hii https://bit.ly/2SLiDKb BOFYA HAPA
Share:

FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO

Zati 50
Full Power
Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:


⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 



⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.



FULL POWER



⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.


⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50

⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.

Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama

Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger