Saturday, 9 May 2020

MBUNGE AZZA HILAL ACHANGIA NDOO SITA ZA RANGI UJENZI OFISI YA CCM TAWI LA BUGANZO JIMBO LA MSALALA


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ametekeleza ahadi ya kuchangia ndoo sita za rangi kwa ajili ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi tawi Buganzo kata ya Ntobo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala (Jimbo la Msalala).

Akikabidhi ndoo hizo kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama,Thomas Myonga leo Jumamosi Mei 9,2020, Mhe. Azza amesema mchango huo ni kuunga juhudi za wanachama wa CCM ambao wamejenga ofisi ya chama.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama,Thomas Myonga amemshukuru Mbunge Azza Hilal kwa kutimiza ahadi yake ya kusaidia ujenzi wa ofisi hiyo ya chama.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akimkabidhi ndoo sita za rangi Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama,Thomas Myonga (wa pili kulia) kwa ajili ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi tawi Buganzo kata ya Ntobo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala leo Jumamosi Mei 9,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Ndoo sita za rangi Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama,Thomas Myonga zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) kwa ajili ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi tawi Buganzo kata ya Ntobo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala
Share:

Nafasi Za Kazi Zaidi ya 150 Zilizotangazwa Serikalini......Mwisho Wa Kutuma Maombi ni Mwezi Huu wa Tano























Share:

Wagonjwa Wa Corona Uganda Wafika 114 Baada Ya Wengine 13 Kuongezeka

Nchi ya Uganda imepata maambukizi mapya 13 ya Corona na kufikisha idadi ya wagonjwa kuwa 114.

Miongoni mwa wagonjwa hao wapya, 7 ni madereva kutoka Kenya, 4 madereva wa Uganda huku 2 ni kutoka Tanzania.


Share:

Bunge Laishauri Serikali Itumie Vyema mdororo wa bei ya mafuta duniani Kujiwekea Akiba Ya Kutosha Ya Mafuta

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati, imeishauri serikali kutumia vyema mdororo wa bei ya mafuta duniani, ili kupata mafuta kwa masharti nafuu na kuanzisha hifadhi ya mafuta kimkakati kwa ajili ya siku zijazo.

Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo bungeni jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dunstun Kitandula, alisema ni vyema kwa wakati huu serikali ikazungumza na nchi rafiki zinazozalisha mafuta ili kupata mafuta hayo.

Alisema katika kutekeleza hilo ni vyema Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) liwezeshwe ili kupokea akiba hiyo ya mafuta.

Alisema tayari ulimwengu umeanza kushuhudia Sekta za Usafiri wa Anga na Utalii zikisimama, biashara na uzalishaji viwandani kushuka na hivyo kushuka kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mafuta na bei yake kuporomoka.

"Kufuatia mkanganyiko huu na mwenendo usiotabirika wa soko la mafuta ulimwenguni, ipo haja kwa nchi yetu kuweka mikakati thabiti ya kuhakikisha nchi inakuwa na akiba ya mafuta ya kutosha wakati wote,” alisema.

Kitandula alisema kamati pia ilichambua taarifa kuhusu hali ya upatikanaji wa mafuta nchini na kubaini kuwa, kwa kipindi chote cha Julai 2019 hadi Februari 2020, hali ya upatikanaji wa nishati hiyo ilikuwa nzuri na nchi ilikuwa na akiba ya mafuta ya kutosha kwa wastani wa zaidi ya siku 40 kwa kila aina ya mafuta.

“Hii ni ongezeko la asilimia 55 kulinganishwa na siku 15 za akiba ya mafuta zinazotakiwa kwa mujibu wa kanuni,” alibainisha.

Alisema mfumo wa BPS (Bulk procurement System) umewezesha kupungua kwa gharama za meli kusubiri kupakua mafuta kutokana na upangaji na usimamizi mzuri wa uletaji meli za mafuta (laycan) ambao umepelekea muda wa meli kusubiri kupungua kutoka wastani wa siku 45 kwa siku za nyuma hadi wastani wa siku tano kwa sasa.

“Kamati ilibaini kuwa, kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Februari 2020, gharama za meli kusubiri imepungua kwa asilimia 18.4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka 2018/2019,”alifafanua.

Alisema jumla ya lita 4,161,067,814.92 za mafuta ya dizeli, petroli, ndege na taa ziliingizwa kwa matumizi ya ndani ya nchi (local) na nchi za jirani (transit) kwa kipindi cha Julai 2019 hadi Februari 2020.

Kitandula ambaye ni Mbunge wa Mkinga, alisema katika kiasi hicho cha mafuta, jumla ya lita 2,398,969,342.12 sawa na asilimia 58 kilikuwa kwa ajili ya matumizi ya ndani, na lita 1,762,098,472.80 sawa na asilimia 42 kwa ajili ya nchi za jirani.

Vilevile, alisema kamati imeridhishwa na hali ya upatikanaji wa mafuta nchini pamoja na usimamizi mzuri wa uagizaji wa mafuta unaofanywa na wakala wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja (PBPA) kwa kushirikiana na mamlaka nyingine.



Share:

Mchango Wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam Katika Mapambano Dhidi Ya Virusi Vya Corona

Chuo  Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimeanza usanifu wa kuunda mashine za kupumulia ya kiotomatiki inayowasaidia wagonjwa waliozidiwa kupumua na kufanya utafiti wa tiba mbadala zinazoonyesha uwezekano wa kuzuia au kupunguza makali ya ugonjwa wa corona.

Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa  na Ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Utafii), ikielezea mipango mbalimbali ambayo chuo kimejiwekea kusaidia jitihada za serikali kupambana na ugonjwa huo.

Ilisema UDSM pia imejiandaa kutoa fedha za utafiti kuhusu ugonjwa wa corona na imewahimiza watafiti wake kuendelea kufanya utafiti kwa kasi zaidi ili kupata tiba, kinga au njia nyingine ya kudhibiti maambukizo ya ugonjwa wa corona.

“Kupitia Ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo-Utafiti, Chuo kimetenga fedha za utafiti na uvumbuzi kiasi cha Sh. 1,500,000,000 katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 kwa ajili ya mapendekezo yanayohusu athari za maradhi ya Covid-19 na mada nyingine za utafiti,” ilisema.

Ilisema UDSM, kupitia Kituo cha Maendeleo na Uhawilishaji wa Teknolojia (TDTC), kimebuni aina mbili za mashine za kunawia mikono za kiotomatiki na zinazotumia miguu.

Taarifa hiyo ilisema mashine hizo zina tangi la lita 250 na zimeandaliwa maalumu kwa ajili ya taasisi zinazohudumia idadi kubwa ya watu kama vile maeneo ya hospitali, viwanda na masoko.

Ilisema mashine hizo zinatoa sabuni ya maji na maji baada ya mtu kusogeza mikono karibu na sensa kwa upande wa mashine za kiotomatiki na kukanyaga pedeli kwa upande wa mashine zinazoendeshwa kwa kutumia miguu.

“Mashine hizi ni nzuri na hazihitaji kufunguliwa kwa mikono hivyo kupunguza uwezekano wa kuambukizana kwa kushika mabomba ya maji, aidha, Chuo tayari kimeshauza mashine hizi katika taasisi kadhaa zikiwamo, Amref, BoT, NHIF, TAA, WFP, TOL, Tamisemi, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Tanesco,” ilisema taarifa hiyo.

Ilisema kama mchango wake kwa jamii, UDSM, kupitia TDTC, kinatengeneza mashine 20 za kunawia mikono zitakazotolewa kama msaada kwa hospitali za serikali zilizoandaliwa kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa Covid-19 jijini Dar es Salaam na mashine zingine zitapelekwa katika vituo vikuu vya mabasi na daladala.

Ilisema kitengo cha vitambaa na nguo cha Idara ya Uhandisi Mitambo na Viwanda kikishirikiana na Kituo cha (TDTC) cha UDSM kimeanza uzalishaji wa barakoa za kiwango cha hali ya juu zenye matabaka matatu.

Kuhusu uzalishaji wa vitakasa mikono, ilisema UDSM imeanzisha mradi wa kuzalisha bidhaa hiyo kwa ajili ya matumizi yake ya ndani na ya umma kwa ujumla.

Ilisema taratibu za uzalishaji wa vipukusi hivyo vya mikono zimezingatia mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani, pamoja na viambata vingine, kunahitajika alkoholi isiyopungua asilimia 60.

Kuhusu upimaji wa ubora wa barakoa ilisema UDSM kupitia vitengo vyake mbalimbali kimekamilisha utafiti wa ubora wa barakoa za vitambaa zinazozalishwa na taasisi na watu mbalimbali.

“Matokeo ya utafiti huo utakaotolewa hivi karibuni yameainisha aina mbalimbali za vitambaa vinavyotumika na ubora wake na utafiti huo umekuja na mapendekezo ya namna ya kutengeneza barakoa za vitambaa zenye ubora,” ilisema.

Ilitaja hatua zingine inazochukua kuwa ni kubaini, kupima na kuchanganua sumu katika bidhaa asilia zilizoteuliwa kama vile matunda, mboga, mimea-tiba kwa ajili ya kuongeza virutubisho na kuandaa bidhaa za tibalishe.



Share:

Jela Miaka 15 Kwa Kumuua Ndugu Yake Bila Kukusudia

Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Kigoma imemhukumu mkazi wa Kijiji cha Kajana, Wilaya ya Buhigwe, Doto Simoni (21), kifungo cha miaka 15 jela baada ya kukiri kumuua bila kukusudia ndugu yake Manase Ezekieli kwa kumpiga na mti usoni na kufariki dunia papo hapo.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, Athumani Matuma baada ya mshitakiwa huyo kukiri kosa.

Matuma alisema mahakama hiyo inatoa adhabu kali kwa mshitakiwa huyo ili iwe fundisho kwake na kwa vijana wengine wenye tabia za kikatili kama yake.

Alisema mshitakiwa alimuita Manase ambaye kwa sasa ni marehemu aliyekuwa akiishi Wilaya ya Kasulu amfuate kwa ajili ya kumpa dawa ili asilogwe na wachawi.

Jaji Matuma alisema alipofika, mshitakiwa alimchukua ndugu yake huyo na kumpeleka kando ya mto Chai na kumwambia akae chini na kufumba macho na kisha anyanyue uso juu, ndipo alipochukua mti na kumpiga usoni kitendo kilichomfanya aanguke chini na kufariki dunia papo hapo.

Vile vile, alisema mshitakiwa alirudi nyumbani kwake na kunyamaza kimya na kudai kuwa hajui ndugu yake alipo.

Alisema ndugu wengine wa marehemu walienda kutoa taarifa polisi za kupotea kwa ndugu yao na walianza kumtafuta sehemu mbali mbali.

Alisema ndugu wengine wa marehemu pamoja na polisi walimshuku mshitakiwa na kumkamata na kumbana ndipo alipokiri kumuua.

Jaji Matuma alisema baada ya kufika eneo la tukio, walikuta mifupa ya binadamu na nguo za marehemu ambazo ni shati, suruali, bukta na mti, ambazo ndugu wa marehemu walizitambua kuwa ni za marehemu Ezekiel.

Jaji Matuma alisema kitendo alichokifanya mshitakiwa huyu ni cha kikatili pamoja na kukiri kosa lake mahakama inamtia hatiani kwa kosa la kuua ndugu yake bila kukusudia.

Alisema upande wa mashitaka ulikuwa ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Benedict Kivuma.

Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili wa kujitegemea Diana Damson, uliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kuwa bado mdogo na amekaa mahabusu kwa miaka miwili.

Hata hivyo, Jaji Matuma alitupilia mbali utetezi huo.


Share:

Serikali Yasema Dawa Ya Corona Iliyopokelewa Toka Madagascar Haitagawiwa Kwa Wananchi Hadi Ifanyiwe Utafiti Kwanza

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema kuwa dawa za kukabiliana na virusi vya corona ambazo Tanzania imepokea kutoka nchini Madagascar hazitogawiwa kwa wananchi kwa sasa.

Akizungumza katika hafla ya upokeaji wa dawa hizo hapa nchini, Prof. Palamagamba kabudi amebainisha kuwa dawa hizo zitafanyiwa utafiti kwanza, na zitakapothibitika kuwa zina faa, ndipo wananchi wataanza kutumia.

“Dawa hii tumepewa na Madagascar ili tuje tuifanyie utafiti kabla ya kuitumia. Tungekuwa tumeenda kuchukua dawa kwa ajili ya Watanzania wote tungeenda na Bombardier au Airbus, lakini tulienda na ndege ya Rais. Na ieleweka hatukwenda kuchukua kikombe cha babu,” amesema Kabudi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Prof. Abel Makubi amebainisha kuwa katika uchunguzi utakaofanyika, wataaangalia kama dawa hiyo ni salama kutumiwa, na pia ubora wake katika kupambana na corona.

Ameongeza kuwa nchini Madagascar tayari wamefanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa dawa hiyo inafaa ndio maana wameanza kutumia.

Pia amesisitiza kwa mara nyingine kwamba ieleweke kwamba dawa hiyo haikuletwa kwa ajili ya kugawiwa kwa watu.


Share:

Watiwa Mbaroni Kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kutumia akaunti Feki Facebook Yenye Jina la Mama Janeth Magufuli

KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA YA UDANGANYIFU [MTANDAO WA KIJAMII].

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili 1. SOPHIA ELIA MWALUANDA [22] Mfanyabiashara na Mkazi wa Sistila Jijini Mbeya na 2. MPAJI SELEMAN MWINYIMVUA [38] Mkazi wa Manzese Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kutumia akaunti feki ya “facebook” yenye jina la Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli Mke wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.

Watuhumiwa wamekamatwa mnamo tarehe 28.04.2020 majira ya saa 15:00 Alasiri katika operesheni na msako uliofanywa huko eneo la Ikuti Sokoni, Kata ya Ikuti, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya.

Mbinu wanayoitumia watuhumiwa ni kufungua akaunti “facebook” yenye jina la JANETH MAGUFULI SACCOS na kuuaminisha umma kwa kuweka picha ya mama Janeth Magufuli na kisha kutangaza kutoa mikopo nafuu kwa sharti la muombaji kutuma kwanza fedha kiasi cha Shilingi 76,500/= kwenye namba ya simu waliyoiweka kama ada ya mkopo ili aweze kupata mkopo wa Shilingi Milioni 3,000,000/=.

Watuhumiwa wamekutwa na simu mbili aina ya Infinix Smartphone ambayo imetumika kufungulia akaunti hiyo ya “facebook” na simu aina ya Siccoo Mobile [Analogue] inayotumika kupokea fedha zinazotumwa na watu mbalimbali. Aidha watuhumiwa wamekutwa na fedha taslimu shilingi 470,000/= ambazo wamekiri kuzipata kwa njia ya udanganyifu kupitia akaunti hiyo feki.

Mtakumbuka Februari 21, 2020 huko katika Mji Mdogo wa Mbalizi Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliwakamata vijana kumi na moja [11] kwa tuhuma za kujihusisha na wizi kwa njia ya mtandao kwa kutumia akaunti feki za mitandao ya kijamii ikiwemo “facebook” wenye majina ya viongozi wa Serikali na Wasanii maarufu wa hapa nchini. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

WITO WA KAMANDA.

Natoa rai kwa watanzania kuheshimu ikulu kwani ni mahali patakatifu na hapachezewi kabisa, Chombo cha dola hakitavumilia kuona mtu wa aina yeyote kwa vyovyote vile akitumia jina la ikulu kuibia au kutapeli watu wengine.

Ninatoa wito kwa wananchi kuwa makini na taarifa mbalimbali zinazotolewa kwenye mitandao ya kijamii ambazo zinaelekezea fursa mbalimbali kama vile ya mikopo, masomo na biashara ambazo zinawataka kutuma kiasi kadhaa cha fedha ikiwa ni moja ya masharti ya kupata fursa hiyo, ni vyema kujiridhisha kwenda mamlaka za serikali zilizo karibu kwa ajili ya kupata uhakika kabla ya kufikia uamuzi wa kutuma fedha.

Aidha ninawataka vijana kujenga utamaduni wa kufanya kazi ili kujipatia kipato halali badala ya kujiingiza kwenye vitendo vya kihalifu ambavyo vitawasababisha kupata adhabu kali kwa mujibu wa sheria.

Mwisho, ninatoa rai kwa mtu/watu waliotuma fedha kupitia namba ya watuhumiwa kwa lengo la kupata mkopo kufika kituo cha Polisi kilichopo jirani kwa ajili ya kutoa taarifa ili taratibu za kisheria zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA MAUAJI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wanne 1. RIZIKI ANTHONY MUHEMA [20] Mkazi wa Mtakuja Mbalizi, 2. REHEMA KASELA [36] Mama Mzazi wa marehemu na Mkazi wa Iwindi 3. ESTA MSONGOLE [52] Mganga wa Kienyeji na Mkazi wa Sumbawanga na 4. MTUMWA HAONGA [65] Mganga wa Kienyeji na Mkazi wa Mtakuja Mbalizi kwa tuhuma za mauaji ya mtoto TAMALI SIMON, miaka miwili na miezi mitatu.

Watuhumiwa walikamatwa katika operesheni maalum iliyofanywa na kikosi kazi cha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya tarehe 06.05.2020 majira ya saa 04:00 usiku huko Iwindi, Kata ya Utengule Usongwe katika Mji Mdogo wa Mbalizi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao ambao wamekiri kufanya tukio hilo kwa kushirikiana na mama mzazi wa marehemu.

Chanzo cha tukio ni tamaa ya kupata utajiri kwa njia za kishirikina baada ya mtuhumiwa ambaye ni mganga wa kienyeji kuwapa masharti yaliyopelekea kifo cha mtoto huyo.

Awali mnamo tarehe 04.05.2020 majira ya saa 20:00 usiku huko Kijiji na Kata ya Iwindi, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya, Mtoto TAMALI SIMON, miaka miwili na miezi mitatu, Mkazi wa Iwindi alikutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na mtu asiyejulikana na mwili wake kutelekezwa.

Kutokana na tukio hilo, Kikosi kazi cha Polisi Mkoa wa Mbeya kilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa katika maeneo tofauti na katika mahojiano watuhumiwa wamekiri kuhusika kwenye tukio hilo baada ya kupewa masharti na mganga wa kienyeji. Aidha upekuzi umefanyika nyumbani kwa Mganga wa kienyeji na kukamata vifaa mbalimbali vya uganga na dawa za kienyeji za aina mbalimbali. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA TUKIO LA MAUAJI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wanne 1. VIOLETH SIMELUTA [26] Mwalimu na Mkazi wa Isanga, 2. CHARLES SIMELUTA [39] Mkazi wa Isanga, 3. EMMANUEL KIWALE [30] Mkazi wa Mafiati na 4. SOPHIA SAMSON [42] Mkazi wa Airport ya Zamani kwa tuhuma za mauaji ya JUNIOR CHARLES MACHIBYA [30] Mkazi wa Airport ya Zamani.

Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 07.05.2020 baada ya kikosi kazi cha Polisi Mbeya kufanya msako na upelelezi wa kina na kubaini kuwa marehemu aliuawa kwa kupigwa vitu butu usoni na kunyeshwa sumu huku chanzo cha tukio hilo kikiwa ni ugomvi wa kifamilia.

Awali mnamo tarehe 30.04.2020 majira ya saa 20:00 usiku huko Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya JUNIOR CHARLES MACHIBYA [30] Mkazi wa Airport ya Zamani alifikishwa Hospitalini hapo na wasamalia wema wakidai kuwa amekutwa maeneo ya nyumbani kwake akiomba msaada na akilalamika maumivu makali ya tumbo akidai kuwa amenyweshwa sumu bila kutoa ufafanuzi zaidi.

Tarehe 01.05.2020 majira ya saa 18:00 jioni alifariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibabu na ndipo upelelezi ulianza pamoja na msako na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo. Upelelezi unaendelea.


Share:

WATAALAMU WA SEKTA YA RASILIMALI WATU NA WADAU WA SEKTA YA UCHUMI KUKUTANA MTANDAONI

Wakati janga la Corona limeathiri njia za ufanyaji kazi duniani kote, kampuni nyingi duniani zimelazimika kutafuta namna mpya ya ufanyaji kazi.


 Nchini Tanzania, kampuni ya BrighterMonday Tanzania imeandaa semina ya mtandaoni itakayowakutanisha wataalamu katika sekta ya Rasilimali Watu pamoja na wadau katika sekta ya biashara kujadili mchango wa Rasilimali Watu katika kuhakikisha Uendelevu wa Biashara wakati wa mlipuko wa virusi Corona.  

Semina hiyo itafanyika Jumanne, Mei 12, 2020 kwa njia ya mtandao na kuwakutanisha waajiri na wadau mbalimbali wa uchumi na biashara kutoka nchini na nje ya Tanzania. Semina hiyo itaendeshwa na wabobevu katika sekta ya Rasilimali Watu, Bw. Mosses Raymond pamoja na Heather O'shea. Kwa mujibu wa mtandao wa BrighterMonday Tanzania, Maafisa Rasilimali Watu kote nchini wanakaribishwa kushiriki kwa kujisajili kupitia tovuti (https://bit.ly/2SLiDKb)   

Kupitia semina hiyo, wadau wa sekta ya uchumi hasa waajiri watanufaika na uzoefu kutoka kwa makampuni makubwa ambayo yatatoa uzoefu na mbinu za kuendelea na utendaji hasa wakati huu ambapo biashara zimekuwa katika mkwamo, washiriki watanufaika na mbinu za namna ya kuendelea kupata wataalamu, mbinu za namna kukabiliana na mabadiliko ya usaili na kupata wasaa wa kubadilishana mitazamo ya kitaalamu na manguli katika sekta ya rasilimali watu.  

BrighterMonday Tanzania wameandaa mfululizo wa semina kwa njia ya mtandao kama sehemu ya utekelezaji wa  programu yao inayokwenda kwa jina la 'Umoja Wakati wa Shida' yenye lengo la kuhakikisha uendelevu wa biashara wakati huu wa mlipuko wa virusi vya Corona. 

Je, ungependa kuwa sehemu ya semina hiyo ya mtadaoni? Tembelea tovuti hii https://bit.ly/2SLiDKb BOFYA HAPA
Share:

FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO

Zati 50
Full Power
Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:


⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 



⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.



FULL POWER



⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.


⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50

⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.

Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama

Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:

WAJUMBE WA BODI YA SHUWASA WAKAGUA UJENZI WA MRADI WA MAJI WA NGOGWA - KITWANA..WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI


Na Suleiman Abeid - Kahama
WAKAZI wa Kata za Ngogwa na Busoka wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameipongeza Serikali ya Awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa jinsi inavyotekeleza Ilani yake ya Uchaguzi kwa vitendo.

Pongezi hizo zimetolewa na wananchi hao mbele ya wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Shinyanga (SHUWASA) waliotembelea na kukagua utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa maji wa Ngogwa – Kitwana unaotekelezwa kwa mpango wa Force Account Mei 8,2020.

Wananchi hao wamesema mradi huo utakapokamilika wataondoka na kero ya ukosefu wa maji safi na salama ambayo wamedumu nayo kwa kipindi kirefu ambapo mpaka hivi sasa wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku.

Mmoja wa wakazi hao anayejitambulisha kwa jina la Paschal Maganga mkazi wa kitongoji cha Nyandolwa kata ya Ngogwa wilayani Kahama anasema yeye binafsi anaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwaondolea kero ya muda mrefu ya ukosefu wa maji katika kata yao.

“Tunashukuru sana kwa serikali yetu kwa kutuletea mradi wa maji katika kata yetu ya Ngogwa, maana tulikuwa na ukame mkubwa wa maji katika maeneo yetu, lakini baada ya awamu hii ya tano kuanza kutekeleza mradi huu, ni wazi kero hii sasa inamalizika,”

“Tulikuwa tunapata shida kubwa ya maji, maana tulikuwa tunayafuata kule eneo la Manzese, mpaka mtu akayapate ilibidi ajidamke mapema ukifika pale saa mbili asubuhi unarudi saa nane ndiyo nyumbani wapate maji, kwa kweli tunashukuru sana,” alieleza Maganga.

Naye mkazi mwingine mkazi wa kijiji na Kata ya Ngogwa, Martha Mayila Kisandu alisema ujio wa maji kutoka Ziwa Victoria umeonesha wazi utekelezwaji wa ahadi ya Rais Dkt. Magufuli ya kuwatua ndoo vichwani akina mama ambapo anasema kabla ya maji hayo kutoka Ziwa Victoria walikuwa wanahangaika sana kutafuta maji ya matumizi yao ya kila siku.

“Tunashukuru mno, mno kwa kweli kwa mradi huu, serikali hii ya awamu ya tano imetukomboa wanawake, tunashukuru na tunasema ahsante, tulikuwa tunahangaika sana juu ya suala la maji, tulilazimika kuamka usiku kwenda kusaka maji, lakini sasa kero hii ipo mbioni kutuondokea, tunamshukuru Rais Magufuli,” alieleza Mayila.

Awali katika taarifa yake kwa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Shinyanga (SHUWASA), Meneja wa mradi wa Maji Ngogwa – Kitwana, Mhandisi Yusufu Katokola alisema mradi huo kwa sasa unatarajiwa kutumia kiasi cha shilingi milioni 350 kwa ujenzi wa matanki mawili.

Katokola alisema mradi huo unahusisha ujenzi matanki mawili katika maeneo ya Ngogwa na Kitwana na kwamba umelenga kunufaisha watu wapatao 44,618 hadi kufikia mwaka 2033 miaka 15 tangu sasa ambapo tanki la Ngogwa litakuwa na ujazo wa lita za ujazo 600,080 na lile la Kitwana lita 100,035 ikiwemo kujenga mabirika ya kunyweshea mifugo.

“Mradi huu awali ulikadiriwa kutumia kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 650 iwapo ungetekelezwa na wakandarasi wa ujenzi, lakini kwa hivi sasa kwa vile tumeamua kutumia wataalamu wetu wa ndani, tunakadiria ujenzi huu utatumia siyo zaidi ya shilingi milioni 350 kwa matenki yote mawili,” alieleza Katokola.

Meneja huyo alifafanua kuwa Serikali iliiteua SHUWASA kusimamia ujenzi wa mradi huo kwa vile ndiyo Mamlaka ya Maji ya Mkoa ambapo baada ya kukamilika kwa mradi, Mamlaka ya Maji ya Mji wa Kahama (KUWASA) ndiyo itakayoendelea kusimamia mradi huo.

Katika taarifa yake Mhandisi Magige Marwa, ambaye ni Mhandisi wa Mipango na Ujenzi katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Kahama (KUWASA) alisema mradi huo umegawanyika katika sehemu tatu, ambazo ni ujenzi wa matanki mawili ya Ngogwa na Kitwana.

“Sehemu ya pili na ya tatu ni kuunganisha bomba kutoka katika matenki na ya tatu kujenga maeneo ya kusambaza maji pamoja na vituo vya kuchotea maji katika vijiji vyote vilivyopo katika kata za Ngogwa na Busoka na kazi kwa sasa inakwenda vizuri baada ya mvua kusimama ambazo zilitukwamisha kidogo,” alieleza Marwa.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi huo, Mkurugenzi wa SHUWASA, Flaviana Kifizi alisema mamlaka yake ilikabidhiwa na wizara jukumu la kusimamia mradi huo wa ujenzi wa matanki mawili ya Ngogwa na Kitwana na kwamba hakuna changamoto kubwa zilizojitokeza katika utekelezaji wa mradi huo.

“Nichukue fursa hii kuwapongeza wananchi wa maeneo haya kwa jinsi walivyoupokea mradi, hatukupata matatizo yoyote kama inavyotokea katika maeneo mengine, tunawashukuru sana wananchi wa maeneo haya, mbali ya kupokea mradi lakini pia wameshiriki katika kufanya kazi ya ujenzi wa matanki haya,”

“Niendelee kuwaomba tu wananchi wa maeneo haya kwamba kwa vile bomba zimeisha wasili, tunawaomba wakati kazi ya kuzilaza itakapoanza wajitokeze kwa wingi kushiriki katika kazi hiyo ili mradi uweze kukamilika na kuanza kutoa huduma kwa wakati,” alieleza Kifizi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA, Mwamvua Jilumbi alisema utekelezaji wa mradi huo upo katika hatua nzuri ukiachilia mbali changamoto za awali za mvua zilizosabisha kazi kusimama kwa muda na kwamba kwa kasi aliyoiona anaamini mradi utakamilika katika muda uliopangwa.
Wajumbe wa Bodi ya SHUWASA, kutoka kushoto, John Kisandu, Albert Msovela na Mhandisi Luhanyula Christopher wakiangalia kazi ya ujenzi wa tenki la maji katika eneo la Kitwana ambalo ni moja ya matenki mawili yanayojengwa chini ya Mradi wa Maji wa Ngogwa - Kitwana unaosimamiwa na SHUWASA.
Mjumbe wa Bodi ya SHUWASA, ambaye pia ni Katibu Tawala mkoani Shinyanga, Albert Msovela akikagua maendeleo ya ujenzi wa tenki la maji katika eneo la kata ya Ngogwa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, John Kisandu ambao ni wajumbe wa Bodi ya SHUWASA wakiteremka kutoka katika kukagua ujenzi wa tenki la Maji linalojengwa eneo la Kitwana wilayani Kahama.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya SHUWASA wakikagua ujenzi wa tenki lililopo eneo la kijiji na kata ya Ngogwa, tenki hilo linatarajiwa kuwa na ujazo wa maji lita 600,080.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya SHUWASA wakikagua ujenzi wa tenki lililopo eneo la kijiji na kata ya Ngogwa, tenki hilo linatarajiwa kuwa na ujazo wa maji lita 600,080.
Wajumbe wa Bodi ya SHUWASA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukagua kazi za ujenzi wa tenki la maji katika kata ya Ngogwa, wa kwanza kutoka kulia ni Mkurugenzi wa SHUWASA, Flaviana Kifizi, mjumbe, Albert Msovela, Mwenyekiti wa Bodi Mwamvua Jilumbi na John Kisandu.
Mkurugenzi wa SHUWASA, Flaviana Kifizi (wa pili kutoka kulia) akisikiliza maelekezo kutoka kwa mmoja wa wajumbe wa Bodi ya SHUWASA, Albert Msovela (wa kwanza kulia).
Afisa Mahusiano wa SHUWASA, Nsianel Gelard (kulia) na mmoja wa watumishi wa SHUWASA wakitoka eneo la mradi wa ujenzi wa Maji wa Ngogwa - Kitwana wilayani Kahama, hapa ni katika eneo la tenki la Ngogwa.
Sehemu ya mabomba yatakayotumika katika kupeleka maji kwenye matenki ya Ngongwa na Kitwana yakiwa yanateremshwa kutoka jijini Dar es Salaam, mabomba hayo yametengenezwa kwa chuma kizito na kila moja lina uzito wa kilo 160.
Wajumbe wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa KUWASA (hayupo pichani) juu ya njia itakayolazwa mabomba ya maji kutoka kwenye bomba kuu linalotoka Solwa wilayani Shinyanga kwenda kwenye tenki la Ngongwa ambalo litateremsha maji yake kwenda kwenye tenki dogo la Kitwana.
 Wajumbe wa Bodi ya SHUWASA wakisikiliza maelezo juu ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Ngogwa - Kitwana unaotarajiwa kutoa huduma ya maji kwa wakazi wa kata za Ngogwa na Busoka kutoka kwa Meneja wa Mradi, Yusufu Katokola (aliyesimama katikati). Mwenye gauni la bluu na mtandio mweupe ni Mwenyekiti wa Bodi, Mwamvua Jilumbi.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi May 09



















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger