Monday, 4 May 2020
Taarifa Kwa Umma Kutoka Jeshi La Polisi Jijini Mwanza
Jeshi la polisi (m) Mwanza linawashikilia watuhumiwa 13 kwa tuhuma za kujihusisha na makosa mbalimbali baada ya kufanya operation kali ya kuzuia vitendo vya uhalifu na kuwakamata baadhi ya watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Tukio la kwanza-; kukamatwa kwa watuhumiwa wa mauaji yaliyohusisha ramli chonganishi.
Tarehe 02.05.2020 majira ya 02:00hrs usiku katika kitongoji cha Imalange, kijiji cha Mwanangwa, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza, alikamatwa mtuhumiwa wa kosa la mauaji aitwaye rodha shabani, miaka 27, msukuma na mkazi wa kijiji cha Mwankali, ambaye baada ya kuhojiwa kwa kina alikiri kuhusika na mauaji ya bibi kizee Ndebeto Tabitha Kakula, miaka 78, msukuma, mkulima na mkazi wa kijiji cha Mwankali, aliyeuawa tarehe 29.04.2020 majira ya 08:20hrs, kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali ambacho baadae ilibainika kuwa ni panga sehemu ya shingoni upande wa kulia wakati akitoka kisimani kuchota maji. Tukio hilo lilitokea baada ya mganga wa kienyeji aitwaye Muhangwa Paul kumpigia ramli chonganishi mtuhumiwa aliyemuua bibi kizee huyo kwa madai aliwaroga watoto wake wawili na kusababisha vifo vyao.
Upelezi umewezesha kukamatwa kwa mganga huyo wa kienyeji na panga lililotu–mika kwenye uhalifu huo limepatikana. Upelelezi wa shauri hili umekamilika kwa asilimia 90 na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.
Upelezi umewezesha kukamatwa kwa mganga huyo wa kienyeji na panga lililotu–mika kwenye uhalifu huo limepatikana. Upelelezi wa shauri hili umekamilika kwa asilimia 90 na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.
Tukio la pili; – kukamatwa kwa mama aliye telekeza watoto kwenye mazingira hatarishi ya majaluba ya mpunga.
Tarehe 29.4.2020 majira ya 06:00hrs asubuhi huko Nyakato, wilaya ya Ilemela, mwanamke aitwaye Happines Mafuru, miaka 23, mjita, mkulima na mkazi wa Nyamhongolo, alikamatwa kuhusiana na tukio la kutelekeza watoto wawili lililotokea tarehe 27.04.2020 majira ya 05:00hrs katika mashamba ya mpunga (majaruba), tukio hilo lilitokea mtaa wa mtakuja, nyamhongolo, wilaya ya ilemela, ambapo watoto hao walitelekezwa. Majina ya watoto ni 1. Kelvin mathias, umri mwaka mmoja na miezi 7 na 2. Anastazia mathia, umri miezi 4. Watoto wanaendelea vizuri, hospitali ya rufaa ya bugando.
Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa kina ili kujua mazingira ya tukio husika yakoje ikiwa ni pamoja na kuendelea kumsaka mzazi mwenzake aliyetoroka.Baada ya tukio hili.
Tukio la tatu:-
Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza katika kipindi cha kuanzia mwezi march, 2020 hadi mwezi april 2020, katika maeneo ya jiji la mwanza, liliendesha operesheni kali dhidi ya wahalifu wa matukio ya uvunjaji wa nyumba usiku na wizi wa vifaa vya nyumbani vya ki elektronik, ambapo katika operesheni hiyo watuhumiwa 7, pamoja na flat tv 30, mota za machine 2, deki 2, subwoofer 2 na vifaa vya kuvunjia kama vile nyundo, shoka, nondo, simu 30,tindo, spana, plaizi, baruti na vifaa vya kulipulia vimekamatwa.
Watuhumiwa wanaoshikiliwa ni;-
- Juma said miaka 35, muha, mkazi wa kirumba.
- Saitoti makokoyo, miaka 28, masai, mkazi wa bwiru.
- Kelvin irizikiwa, miaka 32, muha, mkazi wa bwiru.
- Hussein masoud, miaka 42, mnyamwezi, mkazi wa isevya –tabora.
- Kiroba heka, miaka 38, msukuma, mkazi wa nakatunguru.
- Kudra melikiadi, miaka 23, mjita, mkazi wa nakatunguru.
- Busumbilo charles, miaka 25, mjita, mkazi wa kamkoko.
- Simon deonatus @ killer, namagubo.
- Ally bakari, miaka 24, mjita, mkazi wa mdoe.
Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa mashauri hayo, mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani. Aidha linawataka wananchi wote waliowahi kuibiwa tv na vifaa vingine vilivyotajwa wafike kituo cha polisi kati ilemela na nyakato kwa utambuzi.
Jeshi la polisi mkoa wa mwanza linaendelea kuwashukuru wananchi wote wanaoendelea kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Pia linawataka wanachi kuacha kujihusisha na vitendo vya imani potofu za kishirikina kwani hazina ustawi kwa jamii.
Imetolewa na:
Muliro Jumanne Muliro -; ACP
Kamanda wa polisi (m) Mwanza
04 may, 2020
Kamanda Wa Polisi Afanya Ukaguzi Wa Kushtukiza Stendi Kuu Ya Mabasi Mbeya
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ULRICH MATEI leo tarehe 04.05.2020 majira ya saa 05:00 Alfajiri amefanya ukaguzi wa kushtukiza wa Mabasi ya Abiria yanayofanya safari kwenda mikoa mbalimbali kabla ya kuanza safari kwa lengo la kuangalia usalama wa vyombo hivyo vya usafiri pamoja na kujiridhisha na usimamizi na utekelezaji wa maelekezo yake kwa wakaguzi wa magari waliopo Stendi Kuu.
Katika ukaguzi huo alikuta Mabasi matatu ya abiria yenye namba za usajili T.619 CQV aina ya Scania Mali ya Kampuni ya Isamilo Express linalofanya safari kati Mbeya – Mwanza ambalo tairi zake zilikuwa zimeisha na lilikuwa na tatizo kwenye mfumo wa breki, Basi namba T.420 DNM aina ya Toyota Coaster Mali ya Kampuni ya Amazon Tour Express linalofanya safari kati ya Mbeya – Sumbawanga tairi zake zilikuwa zimeisha na Basi namba T.606 DLQ aina ya Euchre Mali ya Kampuni ya Gitu Express pia tairi zake zilikuwa zimeisha.
Kutokana na matatizo hayo, Kamanda MATEI alizuia mabasi hayo kuendelea na safari hadi yatakapofanyiwa marekebisho ikiwa ni pamoja na kuwekewa tairi mpya. Uongozi wa Kampuni ya Isamilo Express ulileta basi jingine la kampuni hiyo na abiria kuhamia kwenye basi hilo na kuanza safari, pia basi la kampuni ya Amazon Tour Express lilibadilishwa tairi na kuruhusiwa kuendelea na safari.
Aidha Kamanda MATEI amekagua usalama wa abiria kabla ya kuanza safari hasa kipindi hiki cha uwepo wa ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu [COVID 19] na kuwataka Madereva, Abiria na Uongozi wa Stendi Kuu ya Mabasi Mbeya kuhakikisha kila mmoja anafuata maelekezo yanayotolewa na Viongozi Wakuu wa Nchi pamoja na Wizara ya Afya hususani kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka yenye sabuni au vitakasa mikono [Sanitizer] ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu.
Aidha Kamanda MATEI ametoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri kuhakikisha wanafanya matengenezo mara kwa mara ya vyombo hivyo kabla na baada ya safari ili kujiridhisha juu ya usalama wake. Pia amewataka abiria kutoa taarifa za mienendo ya mabasi hayo kwa Jeshi la Polisi kupitia namba za simu ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya madereva wanaokiuka sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani.
Corona Yafuta tofauti ya Daimond na Clouds Media ......Kusaga Aagiza nyimbo yake Ipigwe Redioni
CEO wa Clouds Media Group Joseph Kusaga amezindua kampeni ya BONGE LA MPAMBANAJI ambayo ni maalum kwa ajili ya kuwawezesha Wahudumu wa Afya Tanzania kwa vifaa tiba na mahitaji mengine kwenye vita hii dhidi ya kirusi cha corona.
Wakati akihojiwa na Power Breakfast ya Clouds FM Kusaga akasema anao Wapambanaji wenzake ambao wako tayari kuungana na yeye na miongoni mwao ni Vodacom, Tigo na Diamond Platnumz ambaye alimpigia simu LIVE na kuzungumza kwenye Power Breakfast.
Akiongea kwenye PB Diamond amesema “Kwanza nimpongeze CEO Kusaga kwa kuweka nguvu zake kwenye hilo sio kila Mtu mwenye moyo huo, mimi pia nitaweka mchango wangu hapo na kama unavyofahamu tayari pia upande wangu nimeanza kulipia kodi familia zilizokwama kutokana na hii corona”
Baada ya kuzungumzia Bonge la Mpambanaji, CEO Kusaga alimtaka Diamond achague wimbo wake ili uchezwe kwenye PB kuwaamsha Wapambanaji wote ambapo mara ya kwanza alipendekeza apigwe Msanii wake mpya @officialzuchu lakini baada ya Jo kusisitiza kuwa ngoma ya Diamond ndiyo inatakiwa, Platnumz alichagua yope remix na ikapigwa.
Wenye Virusi Vya Corona Uganda Wafika 89 Baada ya Mmoja Kuongezeka
Wizara ya Afya Uganda imesema kuna ongezeko la mgonjwa mmoja wa corona na kufanya jumla ya maambukizi kufikia 89
Waliopona corona Uganda ni Watu 52 na hakuna kifo
Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni leo jioni atalihutubia Taifa hilo kuhusu hatua zaidi baada ya siku 21 za lock down kukamilika kesho.
Waliopona corona Uganda ni Watu 52 na hakuna kifo
Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni leo jioni atalihutubia Taifa hilo kuhusu hatua zaidi baada ya siku 21 za lock down kukamilika kesho.
♦️Today,3 May,2020,1 new COVID-19 case confirmed out of 2,729 samples of truck drivers:39 year old Kenyan male truck driver who arrived via Malaba.Efforts to track him are underway.— Ministry of Health- Uganda (@MinofHealthUG) May 3, 2020
🔸201 samples from community all tested Negative for COVID-19
🔹Total COVID-19 confirmed cases:89
🔸 Total samples tested today: 2,930— Ministry of Health- Uganda (@MinofHealthUG) May 3, 2020
🔹 Total discharges: 52 #STAYSAFEUG
I will address the country tonight at 8pm, guiding on the way forward as the 21-day lockdown extension comes to a close tomorrow. I urge you all to continue observing the guidelines from our health experts as the battle against the Covid-19 pandemic continues.— Yoweri K Museveni (@KagutaMuseveni) May 4, 2020
Maambukizi Ya Virusi Vya Corona Yapindukia milioni 3.5 Duniani Kote
Maambukizi ya virusi vya Corona duniani yamepindukia milioni 3.5 leo Jumatatu, wakati idadi ya vifo vinavyosababishwa na janga hilo imeongezeka hadi zaidi ya 245,000, ingawa viwango vya maambukizi mapya na vifo vimepungua ikilinganishwa na mwezi uliopita, kulingana na ripoti ya shirika la habari la Reuters.
Visa vingi vilivyothibitishwa katika siku za hivi karibuni viliripotiwa katika ukanda wa Amerika ya Kaskazini na nchi za Ulaya, ingawa idadi ya kila siku ya maambukizi mapya inaongezeka katika ukanda wa Amerika ya Kusini, Afrika na Urusi.
Duniani kote, visa vipya 84,004 viligunduliwa ndani ya masaa 24 yaliyopita, shirika la habari la Reuters limebaini, huku likijikita katika takwimu rasmi zilizotolewa na kila, idadi ambayo inafanya jumla ya visa duniani kote kufikia zaidi ya milioni 3.5.
Vifo vinavyotokana na mlipuko wa Covid-19, ugonjwa unaosababisha matatizo ya kupumua vimefikia jumla ya 245,992.
-RFI
-RFI
Teknolojia inavyotuwezesha kuendesha maisha na biashara
Hali inaonesha kwamba, nchi nyingi duniani zimeathirika na homa ya kirusi cha korona na athari hizi huenda zikabaki katika maisha ya watu kwa muda mrefu.
Mbali na njia mbalimbali za kupambana na maambukizi kama kufunga shule na kuzuia mikusanyiko, Watanzania wengi pia sasa wanatumia njia za kidijitali zaidi kuwasiliana na kuendesha maisha na shughuli zao za kila siku kwa sababu maisha lazima yaendelee. Ama kweli sasa kuungana kidijitali limekuwa jambo muhimu sana.
Mawasiliano ya kidijitali yameleta ahueni sana. Mfano wapo watu ambao hawataweza kuwatembelea ndugu, jamaa na marafiki kama walivyozoea lakini sasa wanaweza kuwasiliana kwa simu na kubaki wamoja na wapendwa wao. Jambo hili linaelezwa kuwa ni muhimu kwa afya ya akili.
Teknolojia ya kidijitali imekuwa si tu ya faida kwa mawasialiano ya mtu mmoja mmoja na familia bali pia kwa biashara. Imesaidia biashara hizi kuendelea kutoa huduma kupitia mtandao wa intaneti ikiwemo kuwasiliana na wateja, huduma za masoko na malipo kidijitali.
Kwa bahati nzuri kampuni za mawasiliano ya simu ziko mstari wa mbele kuwezesha sisi kubaki tumeungana kidijitali. Kampuni ya Tigo kwa mfano ina huduma ya Mfano mmojawapo ni kampuni ya Tigo ambayo ina router ya intaneti nyumbani (Home Internet Router) ambayo inasaidia familia kuwasiliana kwa kuipa mtandao bora wa intaneti. Kwa upande wa maofisi nao wana huduma ya intaneti kwa ofisi (Office Internet) ambayo husaidia ofisi kuendelea kubaki pamoja na kufanya kazi kidijitali.
Katika nyakati hizi za changamoto, kubaki tumeungana kidijitali na kuendelea na maisha na shughuli zetu ni jambo muhimu kuliko wakati wowote ule.
Colombia yakanusha kuhusika na majaribio ya mapinduzi ya kisiasa nchini Venezuela
Wizara ya mambo ya nje ya Colombia imetoa taarifa ikikanusha Colombia kuhusika na majaribio ya mapinduzi ya kisiasa nchini Venezuela.
Waziri wa mambo ya nje wa Venezuela Bw. Nestor Reverol amesema mamluki wa Colombia walijaribu kutekeleza shughuli za kimabavu na kufanya mapinduzi kutoka pwani ya jimbo la La Guaira, kaskazini mwa nchi hiyo.
Kikosi cha usalama cha Venezuela kimepambana na magaidi hao, na kuwaua na kuwakamata baadhi yao.
-CRI
Waziri wa mambo ya nje wa Venezuela Bw. Nestor Reverol amesema mamluki wa Colombia walijaribu kutekeleza shughuli za kimabavu na kufanya mapinduzi kutoka pwani ya jimbo la La Guaira, kaskazini mwa nchi hiyo.
Kikosi cha usalama cha Venezuela kimepambana na magaidi hao, na kuwaua na kuwakamata baadhi yao.
-CRI
JITIBU TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME KWA KUTUMIA FULL POWER.. UUME MDOGO ZAT 50 NDIYO SULUHISHO
Zati 50
Full Power
⇒Ngiri,
⇒Henia
⇒Kisukari
⇒Tumbo kujaa gesi
⇒Kutopata choo vizuri
⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu
⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi
⇒Msongo wa mawazo
⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko na kufanya kuwa na muda mrefu na nguvu za kutosha.
ZAT 50
⇨ Inarutubisha maumbile ya uume na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4
⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.
FULL POWER
⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.
⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.
Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama
Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa
Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.
Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Bodi Ya Tumbaku Tanzania Kusimamia Zoezi Laulipaji Madeni Ya Wakulima Ushetu
Bodi ya Tumbaku Tanzania imesema itahakikisha inasimamia zoezi la ulipaji wa Madeni ya wakulima wa zao hilo ya msimu wa mwaka 2018/19 ambayo walikuwa wanaidai kampuni ya Magefa katika kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa kabla ya kufunguliwa kwa masoko mapya ya Mwaka 2020/21.
Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja wa Bodi ya Tumbaku katika mkoa wa Kitumbaku Kahama, Albert Charles wakati akizungumza na Mpekuzi blog kuhusiana na namna zoezi hilo litakavyofanyika na kuwatoa hofu wakulima kuwa watapatiwa stahiki zao.
“Kampuni ya Magefa imetuhakikishia kuwa watalipa fedha hizo kwa vyama vya Msingi, Ilomelo, kangeme na Tumaini Amcos ambazo walinunua tumbaku katika masoko yaliyofanyika mwezi Marchi 2019 zinazokadiriwa kufikia milioni 80,” alisema Charles.
Alifafanua kuwa malipo hayo yalichelewa kutokana na Kampuni hiyo kutolipwa baada ya kuuza tumbaku hiyo nje ya nchi sambamba na uwepo wa Ugonjwa wa Covid 19 ambao umesababisha nchi nyingi kufunga mipaka na kukwamisha kufanyika kwa masoko hayo.
“Katika msimu wa 2018/19 wakulima wote waliofunga mikataba na kampuni za ununuzi wa Tumbaku katika mkoa huu za TLTC, Allience One na JTI walilipwa fedha zao kwa asilimia 100 lakini baadhi yao walibainika kulima tumbaku nje ya mkataba ambazo serikali ilitafuta mnunuzi(Magefa)ambaye hivi karibuni ataanza kuwalipa,”alisema Charles.
Sambamba na hilo Charles amewatahadharisha wakulima kuwa katika msimu ujao wa masoko ya tumbaku hakuna mkulima atakayeruhusiwa kuuza kwa zaidi ya asilimia 110 na wameandaa daftari maalumu ambalo litatumika kwa wakulima wote ili kudhibiti biashara ya Kangomba na ulanguzi wa Tumbaku ili kuepuka usumbufu usiokuwa wa lazima .
“Msimu uliopita kunavyama vya Msingi viliuza tumbaku kwa asilimia 110 hadi 146 kinyume na sheria namba 24 ya mwaka 2001 ya Tumbaku na kanuni zake inayomtaka mkulima kulima zao hilo bila mkataba ama mnunuzi,”alisema Charles.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Emmanuel Charahani amewataka wakulima kuwaepuka walanguzi wa zao hilo katika msimu mpya wa mwaka huu ili kuondokana na tatizo la kukosa masoko na kusababisha serikali kuanza kutafuta wanunuzi kwa tumbaku iliyozalishwa nje ya Mkataba .
“Tunzeni tumbaku zenu vizuri, zingatieni Usafi na pangeni Madaraja kama inavyotakiwa haipendezi kila mwaka tunakamata tumbaku chafu na safi ikiwa imechanganywa sokoni ”alisema Charahani.
Sambamba na hilo pia, Charahani amezitaja kampuni zilizofunga Mkataba wa kununua zao hilo katika mkoa huo kwa mwaka 2020/21, kuwa ni Petrobena east africa L.t.d, Jespany Company L.t.d, Magefa, Grand Tobbaco, Allience one, JTI na kufafanua kuwa kampuni ya JESPANY COMPANY L.T.D haihusiki na deni hilo kwani ndio mara yake ya kwanza kufunga mkataba wa ununuzi wa na wakulima katika mkoa wa kitumbaku Kahama.
Mwisho.
Mkuu wa wilaya ya Babati kuwawajibisha Wanaouza Sukari Bei ya Juu.
Na John Walter-Babati, Manyara
Mkuu wa wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu amewaagiza maafisa biashara,maafisa tarafa na watendaji wa kata kufanya ukaguzi kwenye maduka ya jumla na reja reja na kuwawajibisha wanaouza sukari tofauti na maelekezo ya serikali.
Akizungumza katika baraza la madiwani la halmashauri ya mji wa Babati, Kitundu amesema bei ya sukari katika mkoa wa Manyara kama ilivyoelekezwa ni shilingi laki moja na ishirini na nane (128,000) kwa kilo hamsini ambayo ni sawa na shilingi 2,860 kwa kilo moja kwa bei ya jumla na shilingi 2,700 reja reja.
Mkuu wa wilaya amesema barua alioipokea kutoka kwa katibu tawala mkoa wa Manyara Missaile Musa inaelekeza kuwa mfanyabiashara yeyote asiuze sukari bei ya reja reja zaidi ya shilingi 2700 .
Amesema jambo la kusikitisha ni kwamba hata baada ya tangazo la serikali kutaka bei ishuke na matangazo kubandikwa katika maduka,baadhi ya wafanyabiashara mjini Babati bado wameendelea kukaidi na kuuza bei ya juu ya shilingi 3000 hadi 3500.
Amesema hawezi kukubaliana unyanyasaji huo kwa wananchi wakati serikali kupitia waziri mwenye dhamana na waziri mkuu walishatangaza kuwa hakuna uhaba wa Sukari nchini.
Ameeleza kuwa kukaidi maagizo ya serikali ni kosa kisheria hivyo watendaji wa kata,vijiji na mitaa kuwachukulia hatua wote wanaokiuka.
Bodi ya sukari kupitia tangazo namba 284 lililotolewa Aprili 24,2020 chini ya sheria ya Sukari sura ya 251 ilitoa maekelezo ya bei ya sukari kwa jumla na reja reja kwa mikoa yote hapa nchini.
TANZIA: Mchungaji Dkt. Peter Mitimingi afariki dunia
Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Warehouse Christian Center(WHC), Dkt. Peter Mitimingi amefafiki usiku wa kuamkia leo. Mchungaji Msaidizi wa kanisa hilo Samwel, amethibitisha.
Mpaka anafariki alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma ya the Voice of Hope Ministry, Mshauri wa Saikolojia wa BLCCC.
Alifahamika zaidi kwa mahubiri na mafundisho yake kuhusu mahusiano na maisha ya ndoa yaliyoenea zaidi kupitia Mitandao ya Kijamii.
Sunday, 3 May 2020
Tanzia : MCHUNGAJI PETER MITI MINGI AFARIKI DUNIA
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema Mchungaji Peter Mingi amefariki dunia usiku huu Jumapili Mei 2,2020.
Tutawaletea taarifa kamili hivi punde
Wagonjwa Wa Corona Nchini Kenya Wafika 465....Ni Baada ya Wengine 30 Kuongezeka
Wizara ya afya nchini Kenya imethibitisha maambukizi mapya 30 ya virusi vya corona hii ni baada ya sampuli 883 kufanyiwa vipimo katika muda wa saa 24 na kufanya idadi ya walioambukizwa kufikia 465 .
Naibu waziri wa afya Dk Rashid Aman anasema kuwa 19 ni wagonjwa kutoka Mombasa, 8 jijini Nairobi wawili kaunti ya Bungoma na kimoja kaunti ya Kitui.
Watu wawili zaidi aidha wamefariki kaunti ya Mombasa kutokana na virusi hivyo na kufikisha waliofariki nchini Kenya kuwa 24 na idha waliopona ni 167 baada ya watu 15 zaidi kuruhusiwa kuondoka hospitalini.
Naibu waziri wa afya Dk Rashid Aman anasema kuwa 19 ni wagonjwa kutoka Mombasa, 8 jijini Nairobi wawili kaunti ya Bungoma na kimoja kaunti ya Kitui.
Watu wawili zaidi aidha wamefariki kaunti ya Mombasa kutokana na virusi hivyo na kufikisha waliofariki nchini Kenya kuwa 24 na idha waliopona ni 167 baada ya watu 15 zaidi kuruhusiwa kuondoka hospitalini.
Korea Kaskazini Na Korea Kusini Zashambuliana Kwa Risasi
Serikali ya Korea Kusini imesema leo wanajeshi wake wamefyatuliana risasi na wanajeshi wa Korea Kaskazini katika eneo lisilo na shughuli za kijeshi linalozitenganisha Korea mbili.
Taarifa ya mkuu wa majeshi wa Korea Kusini imesema kituo kimoja cha walinzi kilishambuliwa kwa risasi kadhaa kutoka upande wa kaskazini, lakini hakuna aliyejeruhiwa.
Afisa huyo wa jeshi amesema jeshi la Korea Kusini lilifyatua risasi kujibu shambulizi hilo na kutoa onyo kwa wanajeshi wa upande wa kaskazini.
Makabiliano hayo ya nadra yametokea siku moja tangu vyombo vya habari vya Korea Kaskazini kuripoti kuwa kiongozi wake Kim Jong Un ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu wiki tatu.
Kutoonekana kwa Kim kulizusha uvumi kuhusu hali yake ya afya na wasiwasi juu ya hatma ya taifa hilo
Taarifa ya mkuu wa majeshi wa Korea Kusini imesema kituo kimoja cha walinzi kilishambuliwa kwa risasi kadhaa kutoka upande wa kaskazini, lakini hakuna aliyejeruhiwa.
Afisa huyo wa jeshi amesema jeshi la Korea Kusini lilifyatua risasi kujibu shambulizi hilo na kutoa onyo kwa wanajeshi wa upande wa kaskazini.
Makabiliano hayo ya nadra yametokea siku moja tangu vyombo vya habari vya Korea Kaskazini kuripoti kuwa kiongozi wake Kim Jong Un ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu wiki tatu.
Kutoonekana kwa Kim kulizusha uvumi kuhusu hali yake ya afya na wasiwasi juu ya hatma ya taifa hilo