Friday, 3 April 2020

Watu 1,169 Wafariki Kwa Corona Nchini Marekani Ndani Ya Masaa 24.....Maambukizi Duniani Sasa Yafika Milioni 1

 Ugonjwa wa Covid-19 unaendelea kuathiri nchi mbalimbali duniani, huku maambukizi ya ugonjwa huo duniani yakifikia milioni moja, huku watu wakiendelea kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Wakati huo huo Marekani inaendelea kuripoti visa vingi vya maambukizi ya virusi vya Corona, ambapo vifo vya watu 1,169 vimeripotiwa ndani ya masaa 24.

Uchumi umeangamizwa na janga hilo, kama inavyoonyesha takwimu nyingine ambayo inatisha: katika wiki moja, Wamarekani milioni 6.6 wamepoteza kazi. Nusu ya watu duniani wamekwama kutokana na hatua ya kukaa nyumbani ambayo kwa baadhi ya nchi imekuwa kali.

Idadi ya visa vya maambukizi vilivyothibitishwa ulimwenguni inazidi milioni moja leo Ijumaa, huku watu 52,000 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa Covid-19, kulingana na takwimu zilizotolewa na shirika la habari la AFP.

Ulaya ndio bara lililoathiriwa zaidi, lakini Marekani inaelekea kuwa kitovu kipya cha janga hilo, ikiripoti robo ya visa vya maambukizi. Idadi hii labda ni ndogo, kwa sababu ya ukosefu wa uchunguzi wa kutosha.

Nchini Marekani, idadi ya vifo katika masaa 24 imeiweka nchi hiyo kuwa na rekodi kubwa zaidi: vifo 1,169, kulingana na ripoti ya Chuo Kikuu cha Marekani cha Johns Hopkins.

-RFI


Share:

Serikali Yatakiwa Kutowaonea Aibu Wanaoleta Mzaha Juu Ya Ugonjwa Wa Corona

NA TIGANYA VINCENT
VIONGOZI  wa Dini  Mkoani Tabora wameiomba Serikali kutowaone aibu wale wote wanaoleta mzaha na wanaotafuta umaarufu kupitia janga la ugonjwa wa homa  kali ya mapafu unaoeneza na kirusi kipya aina ya Corona Covid-19.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa maombi na dua maalumu Viongozi wa Dini na Serikali ya Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kuuweka Mkoa wa Tabora ,Taifa na Dunia nzima mikononi mwa Mungu ili awakinge na janga la ugonjwa wa Corona.

Mchungaji wa Kanisa la Agape Miracle Centre Elias Mbagata alisema bado kuna kuna mizaa inaendelea juu ya janga hili hivyo ameiomba serikali isiwaonee haya wanoendekeza hayo hata kama ni viongozi wakubwa wakiwemo wa Dini.

Alisema kinachotakiwa kufanywa kwa sasa ni kuwajengea matumaini wananchi badala ya kuwajaza hofu ambayo itawasababisha wachanganyikiwe.

Askofu wa wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tabora, Dk Elias Chakupewa alisema wameshachukua hatua mbalimbali za kuwaelimisha waumini wao kufuata taratibu zote zinazotakiwa ikiwemo maelekezo ya wataalamu na viongozi wa Serikali namna sahihi ya kujikinga na janga la Covid -19.

Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Tabora Mhashamu Paul Ruzoka aliwaomba waumini kuungana na serikali katika kupigana vita hii iliyo mbele yao kwa kuhakikisha wanatekeleza maelekezo yanayotolewa na viongozi pamoja na wataalam wa afya.

Alisema Kanisa hilo limesitisha kwa muda baadhi ya taratibu za uendesha wa Ibada ikiwa ni seehemu ya mikakati ya kuungana na Serikali katika mapambano dhidi ya Covid -19.

Kwa upande wa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ibrahim Mavumbi aliwashauri viongozi wa Dini kuendelea kushirikiana na serikali na kufuata maelekezo ya wataalamu katika kuhakikisha wananchi na waumini wao wanapata maelekezo sahihi kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa huo hatari.

Askofu wa Kanisa la Morovian Tanzania Magharibi Ezekiel Yona alisema wao kwa kutambua ukubwa wa tatizo wametoa jingo katika Hospitali yao ya Sikonge kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa wa Covid -19 kama kwa bahati mbaya wataonekana.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Magharibi Kati, Askofu Isaac Laizer alimpongeza Rais Dokta John Pombe Magufuli kwa  kwa kuthubutu kuitangazia dunia kwamba janga la ugonjwa wa Corona litamalizika kwa wananchi watakapokubali kumuomba Mungu.

Alisema wao wanaungana na Serikali kwa kusimamisha baadhi ya huduma ikiwemo ya mafunzo kwa watoto wadogo (Sunday school) na kualika wataalamu kutoa elimu ya kujikinga na Corona.

Viongozi hao wamadhehebu ya dini wamesema kwamba pamoja na serikali kuchukua taadhali inabidi wananchi kumlilia Mungu ili awasamehe dhambi na kuwaepusha na janga hilo.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwashukuru viongozi hao wa kiroho kwa ushirikiano wanaotoa kwa Serikali na kuwaomba wasaidie kufikisha elimu kwa waumini wao ili isaidie kuuepusha Mkoa huo na janga la Covid 19.


Share:

Waratibu Wa Tarura Wa Mikoa Watakiwa Kufanya Ukaguzi Wa Mara Kwa Mara Katika Madaraja Na Barabara

Na. Erick Mwanakulya
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff amewataka Waratibu wote wa TARURA nchini kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika barabara na madaraja ili kubaini maeneo yanayohitaji ukarabati na kuyafanyia kazi kabla ya kuleta madhara.

Mhandisi Seff ameyasema hayo, alipokutana na Waratibu wa TARURA wa Mikoa jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za TARURA Makao Makuu zilizopo Mtumba, ikiwa ni sehemu ya kikao kazi kilicholenga kutoa maelekezo na miongozo mbalimbali ya ufanyaji kazi ili kuwapatia wananchi huduma ya usafiri na usafirishaji.

Aidha, Mtendaji Mkuu amesisitiza kuwa, ukaguzi wa mara kwa mara wa miundombinu unasaidia kupunguza gharama kwani uharibifu au uchakavu wa miundombinu ukibainika mapema ukarabati wake unaweza kufanyika katika hatua za awali kwa gharama nafuu na kwamba miundombinu inapoharibika moja kwa moja gharama inakuwa kubwa sana pale inapobidi kujengwa upya.

Pia, Mhandisi Seff amesisitiza juu ya uwekwaji wa alama za barabarani hasa katika maeneo maalumu kama madaraja na maeneo yaliyoharibika ili watumiaji wa barabara watambue vizuri maeneo hayo wakati wa kupita.

‘‘Natoa maelekezo juu ya uwekwaji wa alama za barabarani kwamba, hakikisheni mnaweka alama za kudumu maana sitamsikiliza yeyote atakayekuja na sababu kuwa kibao kimeibiwa wakati angeweza kuweka kibao cha kudumu hata kwa kutumia zege maana bila kuwa na alama hizo inaweza kuwa chanzo cha ajali”, amesisitiza Mhandisi Seff.

Ili kurahisisha usimamizi wa kazi kwa mikoa yote kiongozi huyo ameeleza kuwa, anaendelea kutoa magari kwa Waratibu wote wa TARURA na kisha atatoa magari kwa Mameneja wa TARURA wa Halmashauri ili kuhakikisha wanasimamia kazi na wananchi wanasafiri kwa urahisi.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) unaendelea kutekeleza majukumu yake katika Mji wa Serikali Mtumba baada ya kukamilisha ujenzi wa ofisi yake na kuhamia rasmi.

Mwisho.


Share:

ANZA KUFURAHIA WEEKEND YAKO KWA BIRIANI TAMU ...NI BIRIAN KILA MTAA IJUMAA HII SHINYANGA MJINI



Share:

WABUNGE WAITAKA SERIKALI KUWEKA KIPAUMBELE ZAIDI KATIKA KUTOA ELIMU YA CORONA KWA WALEMAVU

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Wabunge  Wameendelea kutoa michango ya Maoni yao kuhusu  hotuba ya mapitio na Mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi za Ofisi ya Waziri Mkuu na ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021 iliyowasilishwa hapo  April 1,2020  na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa huku wakiitaka serikaka kuweka kipaumbele zaidi katika kutoa elimu ya kujikinga na Corona kwa makundi ya watu wenye ulemavu wakiwemo wasioona.

Wakichangia maoni mbalimbali bungeni jijini Dodoma  akiwemo Mbunge wa viti Maalum ,Amina Mollel amesema katika mapambano dhidi ya Virusi vinavyosababisha na homa kali ya mapafu ,Corona[COVID-19]elimu inahitajika kwa kina zaidi kwa watu wenye ulemavu hususan vipofu.

“Watu wasiokuwa na ulemavu elimu ni rahisi kutolewa ,mfano kumwonesha namna ya kunawa mikono,kwa kutumia sanitizer ,Kwa hawa wenzetu wenye ulemavu wanapata changamoto kubwa sana hivyo ninaomba serikali iweke kipaumbele zaidi katika kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu ,mfano mlemavu wa macho [kipofu]haoni chochote kinachoendelea bila elimu kwa kina ni changamoto kwake”amesema.

Kwa upande wake mbunge wa Korogwe Mjini Mhe.Mary Chatanda  ambaye pia ni Kamishna wa Huduma za Bunge amesema maelekezo yanahitajika zaidi kwa wananchi juu ya tahadhari ya Corona huku mbunge wa viti maalum Mhe.Hadija Nasiri Ali anayewakilisha kundi la vijana Bungeni akitoa ushauri kwa serikali kupunguza masharti kwa taasisi za kifedha ili vijana wengi zaidi waweze kujiajiri.

Mbunge wa Njombe Mjini  Mhe.Edward Franz  Mwalongo amesema serikali inatakiwa kuwaandaa zaidi wananchi kuhusiana hali ya corona ilivyo duniani na hali ikiendelea kuwa mbaya watu wajifungie ndani.

Kuhusu idara inayohusika na ujuzi Mhe.Mwalongo ameomba idara hiyo ipanue zaidi katika maeneo ya vijijini kwenye sekta za kilimo na ufugaji kwani imekuwa ikijikita katika sehemu za mjini pekee.

Bunge linatarajia kuhitimisha kujadili hoja ya hotuba ya mapitio na Mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi za Ofisi ya Waziri Mkuu na ofisi ya Bunge kwa mwaka 2020/2021 kuanzia wiki ijayo ambapo Ofisi ya Waziri mkuu na taasisi zilizo chini yake imeliomba Bunge kuidhinisha Jumla ya Tsh.Bilioni 312,Milioni 802,laki 5 na 20 elfu[312,802,520,000].


Share:

TAKUKURU MANYARA YAMFIKISHA MAHAKAMANI MTENDAJI WA KIJIJI KWA KUOMBA RUSHWA SH. 50,000

Na John Walter- BABATI

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) mkoa wa Manyara imemfikisha mahakamani afisa mtendaji wa Kijiji cha Gichameda  John Bura kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya shilingi elfu hamsini (50,000).

Mwendesha mashtaka wa Takukuru Eveline Onditi alisema shauri hilo namba 94 limetajwa kwa mara ya kwanza mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa Manyara Jumaa Mwambago.

Onditi alisema kuwa Machi 31,2020 katika stendi ya Matufa afisa mtendaji wa Gichameda akiwa mwajiriwa wa Halmashauri ya wilaya ya Babati alimuomba rushwa ya shilingi 50,000 Husein Darabu  ili aweze kumpatia utambulisho wa kwenda kupata dhamana ya mdogo wake ambaye alikuwa kituo kidogo cha polisi Magugu.

Onditi ameeleza kuwa mshtakiwa huyo anadaiwa kugoma kumuandikia barua ya utambulisho Husein Darabu ambaye alikuwa anaenda kumdhamini mdogo wake aliyekuwa anashikiliwa na polisi kituoni hapo.

Amesema Darabu baada ya kuombwa rushwa alifika ofisi za Takukuru na kutoa taarifa ndipo mtuhumiwa aliwekewa mtego na kukamatwa.

Ameyataja makosa ya mtuhumiwa kuwa ni kuomba na kupokea rushwa kinyume na matakwa ya mwajiri wake na kosa jingine ni kuomba na kupokea rushwa.

Onditi amesema mshtakiwa alifanya kosa hilo kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 2007 kifungu cha 15.

Aidha mshtakiwa alisomewa mashtaka Aprili 2, 2020 na amekana makosa yote na amepewa sharti la dhamana kuwa ni lazima awe na mdhamini na kutoa shilingi laki tano (500,000) ambayo ameitoa yote na kuachiwa huru.

Hata Hivyo shauri hilo limeahirishwa mpaka litakapotajwa tena Aprili 30,2020 kwa ajili ya kusikilizwa.


Share:

WATUMISHI MADINI WAPATA ELIMU YA CORONA

 Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Issa Nchasi akiwakaribisha wataalamu wa Afya kutoa mafunzo juu ya ugonjwa wa corona kwa watumishi wa Wizara ya Madini Makao Makuu jijini Dodoma, leo asubuhi.
 Mtaalamu wa afya Dkt. Shamza Said akitoa elimu ya ugonjwa wa corona kwa watumishi wa Wizara ya Madini ili kuwapa uelewa wa ugonjwa huo na namna ya kujikinga
Mtaalamu wa afya Dkt. Shamza Said akitoa elimu ya ugonjwa wa corona kwa watumishi wa Wizara ya Madini ili kuwapa uelewa wa ugonjwa huo na namna ya kujikinga

  Watumishi wa Wizara wakifuatilia mafunzo juu ya ugonjwa wa corona kutoka kwa wataalamu wa afya (hawapo pichani)
 Mtaalamu wa mazingira katika masula ya Afya, Koyi Veronika akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyotolewa kwa watumishi ofisi za Wizara ya Madini Makao Makuu, jijini Dodoma
 Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi, Veneranda Charles akiuliza swali kwa wataalamu wa afya juu ya vitakasa mikono vinavyoshauriwa kutumika ili kujikinga na ugonjwa wa corona.

 Kamishna msaidizi wa Madini anayeshughulikia masuala ya Ushiriki wa wananchi na ncchi katika uchumi wa madini, Ngole akiuliza swali kwa wataalamu wa afya mafunzo hayo yakiendelea.
 Dkt. Shamza Said akijibu maswali juu ya ugonjwa wa Corona aliyoulizwa na watumishi.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala, Issa Nchasi, akiwashukuru na kuwaaga wataalamu wa Afya mara baada ya zoezi la kutoa mafunzo juu ya ugonjwa wa corona kwa watumishi wa Wizara ya Madini Makao Makuu, kukamilika.
 
Asteria Muhozya na Nuru Mwasampeta - Dodoma

Watumishi wa Wizara ya Madini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Issa Nchasi leo Aprili 2, wametembelewa na wataalamu wa afya kwa lengo la kutoa elimu juu ya ugonjwa wa corona unaosababishwa na virusi vya covid-19 na namna ya kujikinga na ugonjwa huo.

Wataalamu hao ni pamoja na Dkt. Shamza Said ambaye ni miongoni mwa wataalamu wa afya wanaojishughulisha na magonjwa yanayoambukiza kwa kasi aliyeambatana na Toyi Veronica mtaalamu wa mazingira katika masuala ya afya.

Akizungumzia virusi vinavyosababisha ugonjwa huo Dkt. Shamza alisema virusi vya covid-19 ni virusi vipya kuwepo duniani vya aina hiyo vinavyotoka kwa wanyama na kusababisha madhara kwa binadamu.

Amesema virusi hivi pindi vinapoingia mwilini mwa binadamu vinasababisha madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushambulia mfumo wa upumuaji, figo, ini na madhara mengine na kuwasihi watumishi na jamii pindi wanapohisi kuwa na dalili za ugonjwa huo, kuhakikisha wanawahi katika vituo vya afya ili kupatiwa huduma stahiki kabla ya ugonjwa kusababisha madhara makubwa mwilini.

Amesema, unapowahi kupata huduma za kitabibu kuna uwezekano mkubwa wa kupona tofauti na mtu anayekwenda kutibiwa awapo katika hali mbaya.

Aidha, Dkt Shamza amewashauri watumishi kupunguza mikusanyiko isiyokuwa ya lazima, kunawa kwa sabuni na vitakasa mikono kila wakati, kuacha kukusanyika katika masherehe, matumizi ya vifaa vya vyakula yasiwe shirikishi, kuzingatia uvaaji sahihi wa mask pamoja na kuwa wawazi wanapojihisi kuwa na maambukizi ya ugonjwa ili kuepusha kuambukiza watu wengine.

Kwa kuhitimisha, Dkt. Shamza amewataka watumishi kutoa elimu ya corona kwa watu wengine katika familia ndugu jamaa na marafiki ili elimu hii iwafikie wengi na waweze kujikinga na hivyo kupunguza maambukizi nchini. “Unapopata elimu, elimisha na wengine” amisisitiza Dkt. Shamza.

Kwa kuhitimisha, Dkt. Shamza amewataka watumishi kutoa elimu ya corona kwa watu wengine katika familia ndugu jamaa na marafiki ili elimu hii iwafikie wengi na waweze kujikinga na hivyo kupunguza maambukizi nchini. “Unapopata elimu, elimisha na wengine” alisisitiza.

Kwa upande wake, Mtaalamu wa mazingira katika masula ya Afya, Koyi Veronika ameushauri uongozi wa wizara kupunguza vikao kazi vya ana kwa ana na badala yake uongozi kwa kushirikiana na wataalamu wa TEHAMA kuratibu mfumo wa kutumia mtandao katika vikao vyao ili kuepusha maambukizo miongoni watumishi.

Kwa kuhitimisha, Dkt. Shamza amewataka watumishi kutoa elimu ya corona kwa watu wengine katika familia ndugu jamaa na marafiki ili elimu hii iwafikie wengi na waweze kujikinga na hivyo kupunguza maambukizi nchini. “Unapopata elimu, elimisha na wengine” alisisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala, Issa Nchasi amewashukuru Wizara ya Afya kwa mpango mzuri walioanzisha wa kupita na kutoa elimu kwa watumishi na kuahidi kuyasimamia yote waliyoelekeza ili kupambambana na gojwa hatarishi la corona.

Baada ya kutoa elimu hiyo zilipo ofisi zaWizara Makao Makuu, wataalamu hao wameelekea zilipo ofisi za Taasisi ya Jiolojia na Utafiti na Ofisi ndogo za Wizara ya Madini, Chuo cha Madini na kumalizia mafunzo hayo ofisi za Tume ya Madini.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa April 3





















Share:

Thursday, 2 April 2020

Wimbo Mpya : MAN NKELEBE - LUCY

Msanii Man Nkelebe ameachia wimbo mpya unaitwa Lucy..Huu hapa chini
Share:

Wimbo Mpya : MAN NKELEBE - UKIMWI

Huu hapa wimbo mpya wa Man Nkelebe unaitwa Ukimwi...Usikilize hapa chini mtu wangu

Share:

Picha : MWILI WA MTANGAZAJI WA TBC MARIN HASSAN MARIN WAZIKWA ZANZIBAR

WANANCHI wakibeba Jeneza lililokuwa na Mwili wa Marehemu Marin Hassan Marin, wakitoka nyumbani kwa marehemu na kuelekea katika Msikiti wa Kibweni KMKM kwa ajili ya kuombea dua kwa ajili ya maziko yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar leo Aprili 2,2020.(Picha na Othman Maulid )
WAUMINI wa Dini ya Kiislam wakiuombea dua mwili wa Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Shirika la Habari Tanzania (TBC) baada ya kumalizika Sala ya Maiti iliofanyika katika Msikiti wa KMKM Kibweni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WAZIRI wa Habaro Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.Mhe. Mahmoud Thabot Kombo akizungumza na kutowa shukrani kwa niaba ya Wizara yake wakati wa hafla ya maziko ya Mwandishi wa Habari Muandamizi Tanzania Marehemu Marin Hassan Marin, yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar.(Picha na Othman Maulid)
MAWAZIRI wa Habari wa SMT na SMZ. Kushoto Waziri Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, wakiwasili katika viwanja vya Msikiti wa Kibweni KMKM kuhudhuria maziko ya Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Marin Hassan Marin, yaliofanyika leo 2/4/2020 na kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.(Picha na Othman Maulid)
WANAICHI na Waumini wa Kiislam wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa maziko ya Marehemu Marin Hassan Marin Mwandishi wa Habari Muandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) yaliofanytika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 2/4/2020.(Picha na Othman Maulid)
Share:

MFANYAKAZI WA MAHAKAMA MBARONI KWA TUHUMA YA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 10 MAHAKAMANI SHINYANGA



Na Salvatory Ntandu - Shinyanga
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia Joseph Masanja (58) mlinzi wa Mahakama ya Hakimu mkazi Wilaya ya Shinyanga kwa tuhuma ya kumbaka Mwanafunzi mwenye umri wa Miaka 10 wakati akiwa kwenye eneo lake la kazi.

Tukio hilo lilitokea tarehe 21 Machi mwaka huu ambapo inaelezwa kuwa mtuhumiwa alimdanganya binti huyo aliyekuwa na mwanzake mwenye umri wa miaka saba kwenda katika eneo lake la kazi kwa madai ya kuwapatia fedha za kununua ndala.

 Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi leo Alhamis Aprili 2,2020 Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema mtuhumiwa alikamatwa baada ya binti hiyo kutoka katika eneo la kazi majira ya saa kumi na moja jioni.

“Ilikuwa saa nane mchana siku ya Jumamosi,mabinti hao walifika mahakamani, Joseph aliagiza binti wa miaka saba kubakia getini na kisha yeye kuingia ndani binti huyu na kumbaka katika moja ya chumba cha ofisi katika eneo la Mahakama”,alisema Magiligimba.

Magiligimba alifafanua  kuwa baada ya  Joseph kutekeleza tukio hilo alimwamuru binti huyo kuondoka eneo la tukio kwa kupitia geti jingine ambapo mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi aliyefahamika kwa jina moja la Leticia alipomkamata binti huyo na alimhoji kuwa ametokea wapi ndipo alipokiri alikuwa akifanya mapenzi na mlinzi huyo.

“Pia kuna Afisa wa polisi alimwona binti wa miaka saba aliyekaa getini muda mrefu,alipomhoji kwanini amekaa kwa muda mrefu katika eneo hilo alijibiwa kuwa anamsubiri mwenzake tangu majira ya saa 8 mchana alipoingia ndani na Mlinzi huyo hajatoka”,aliongeza Magiligimba.

"Askari huyo alimchukua binti huyo na kuingia naye ndani ya eneo la mahakama na kukutana na mwalimu aliyemkamata binti wa miaka 10 wakati akipitishwa geti la pili na Joseph,ndipo walipoamua kutoa taarifa kwa wazazi wa mabinti hao",alieleza Magiligimba.

Aidha alisema kuwa baada ya mabinti hao kufikishwa polisi wazazi wao walifika na kupewa kibali cha kwenda hospitali kwa ajili ya vipimo na vipimo vilibaini kuwa binti wa miaka 10 ameingiliwa (amebakwa)

Hata hivyo Magiligimba alisema,baada ya Joseph kutekeleza tukio ,alikimbia kusikojulikana hadi alipokuja kukamatwa na jeshi la polisi na Alipohojiwa alikiri kumbaka mwanafunzi huyo,na upepelezi wa tukio utakapokamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
Share:

Wimbo Mpya : MAN NKELEBE - AGNESS

Msanii Man Nkelebe anakualika kusikiliza wimbo wake mpya uniatwa Agness ..Usikilize hapa chini
Share:

Habari Mpya Kuhusu Virusi Vya Corona Tanzania Leo Alhamisi April 2, 2020




Share:

Wizara ya afya yatoa ufafanuzi maswali ya Wananchi kuhusu Virusi Vya Corona

Na WAMJW-Dar es Salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema amekuwa akipokea maoni, maswali na ushauri kutoka kwa wananchi wakitaka kujua jitihada mbalimbali za Serikali za kukabiliana na homa kali ya mapafu na amewaagiza wataalamu wake kuanza kujibu maswali.

Waziri Ummy amesema maswali, maoni na ushauri huo unatoka kwa wananchi kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na kituo cha wizara cha kupokea simu kuhusu ugonjwa wa homa ya Corona.

“Moja ya swali linaloulizwa kutoka kwa wananchi ni suala la kupima ugonjwa wa Corona (covid-19), hivyo katika kutoa ufafanuzi ni vema Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Dkt. Nyambura Muremi, aeleze Watanzania nani anakidhi vigezo vya kupima ugonjwa wa Covid-19 na taratibu za kupima ugonjwa huu zikoje,” amesema Ummy Mwalimu.

Katika hatua nyingine, Waziri Ummy Mwalimu amesisitiza wananchi kwamba wanapaswa kukaa umbali wa mita mbili kati ya mtu mmoja na mtu mwingine ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Akizungumzia kuhusu maswali ya wananchi, Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Dkt. Nyambura Muremi amesema kuwa anayepaswa kupimwa ugonjwa wa corona ni yule alitimiza vigezo kama vile mtu kuwa na dalili ya ugonjwa wa covid-19.

“Kama mtu amepata kirusi, ataanza kuonyesha dalili kama vile kupata homa, hapa ndio tutanza kuchukua kipimo na huu ndio uthibitisho wa kisayansi,” amesema Dkt. Muremi.

Akizungumzia taratibu za kupima ugonjwa wa corona, Dkt. Muremi amesema katika ngazi ya mkoa wapo wataalamu wanashughulika kupima sampuli na kwamba wao ndio wamekuwa wakiratibu shughuli zote za kimaabara kila mkoa.

“Baada ya kupima huko mikoani wanaleta Maabara Taifa ya Afya ya Jamii ambayo ina vigezo vitatu vinavyotambulika kimataifa,” amefafanua Dkt. Muremi.

Dkt. Muremi ametaja vigezo vya Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii ni kwamba ina usalama wa kibailojia ngazi ya tatu (BSL-3), wataalamu waliothibitishwa kupima magonjwa hatarishi na mashine stahiki ambayo imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Kutokana na maswali mengi ya Wananchi kuanzia sasa Wizara ya Afya itaendelea kujibu maswali yao.


Share:

KAMPUNI YA TIGO WAUNGA JUHUDI KUPAMBANA NA CORONA WATOA WITO KWA JAMII

Kampuni ya Tigo Waunga juhudi kupambana na Corona watoa wito kwa jamii, tazama video hapo chini


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger