Saturday, 7 March 2020

Picha : DC MBONEKO AONGOZA MAMIA YA WANAWAKE KUADHIMISHA KONGAMANO LA WANAWAKE 'SHINYANGA WOMEN'S DAY OUT'

Kongamano la wanawake Shinyanga mjini (Women's Day Out), lililoandaliwa na Kikundi cha Wanawake na mabadiliko (Women for Change - WFC ), limehudhuriwa na mamia ya wanawake kutoka Shinyanga mjini, kwa ajili ya kupewa elimu mbalimbali ikiwamo ya malezi, afya, sheria, pamoja na jinsi ya kujikwamua kiuchumi.

Kongamano hilo limefanyika leo Machi 7, 2020 kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Shinyanga, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo, Mboneko aliwataka wanawake Shinyanga mjini washirikiane na kuungana mkono, ikiwamo kwenye masuala ya kuinuana kiuchumi na kuacha tabia ya kutopendana.

Alisema huu ni wakati wa wanawake kushirikiana, kupendana na kuungana mkono kwenye masuala ya kibiashara kwa kununuliana bidhaa, na kuacha tabia kutopendana ili wapate kusonga mbele kiuchumi.

Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wanawake kutumia vyombo vya habari na mitandao ya jamii kutangaza shughuli wanazofanya.

“Napongeza sana kikundi hiki cha wanawake na mabadiliko cha Women for Change kwa kufanya Kongamano hili la wanawake Shinyanga mjini, na hasa kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ni Machi 8,2020  kwa kukutanisha wanawake kupewa elimu mbalimbali kwa mstakabali wa maisha yao,”alisema Mboneko.

“Kupitia Kongamano hili naomba wanawake, mpendane, mshirikiane, pamoja na kuungana mkono kwenye biashara mbalimbali ili mjikwamue kiuchumi, ambapo dhana za kuchukiana zilishapitwa na wakati, kipindi hiki ni cha mabadiliko wanawake tuungane na kuwa kitu kimoja,”aliongeza.

"Pia nakipongeza kikundi hiki cha wanawake na mabadiliko kwa kufanya ukarabati wa bweni la wavulana kwenye kituo cha kulea watoto wenye ualbino Buhangija, ili kuwaweka katika mazingira mazuri, mfano ambao unapaswa kuingwa na wadau wengine wa maendeleo",alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti Msaidizi wa Kikundi cha wanawake na mabadiliko 'Women for Change, kutoka Shinyanga mjini Getrude Munuo, alisema kikundi hicho kilianzishwa mwaka 2013 na 2014 walipata usajili, na lengo lao kubwa ni kusaidiana kuinuana kiuchumi pamoja na kufanya shughuli za kijamii.

Alisema wameendesha kongamano hilo kwa lengo la kutoa elimu mbalimbali kwa wanawake wa Shinyanga mjini, ikiwamo ya malezi, afya pamoja na namna ya kushirikiana kibiashara ili kuinuka kiuchumi.

TAZAMA VIDEO WANAWAKE WAKICHEZA MUZIKI

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye Kongamano la wanawake "Shinyanga Women's Day Out" lililoandaliwa na kikundi cha wanawake na mabadiliko Women for Change kutoka Shinyanga mjini leo Jumamosi Machi 7,2020. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye Kongamano la wanawake Shinyanga mjini "Shinyanga Women's Day Out" lililoandaliwa na kikundi cha wanawake na mabadiliko Women for Change kutoka Shinyanga.
Waandaaji wa Kongamano la Shinyanga Women's Day Out wakiwa ukumbini.
Waandaaji wa Kongamano la Shinyanga Women's Day Out wakiwa ukumbini.

Wanawake wakiwa kwenye Kongamano la Shinyanga Women's Day Out.
Meza Kuu 'VIP' wakiwa kwenye Kongamano la Shinyanga Women's Day Out.
Meza Kuu 'VIP' wakiwa kwenye Kongamano la Shinyanga Women's Day Out.

Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiingia kwenye Kongamano la wanawake Shinyanga, " Shinyanga Women's Day Out."

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, wapili kulia, akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wanawake na mabadiliko (WCF) wakati alipowasili kwenye Kongamano la wanawake, "Shinyanga Women's Day Out."

Baadhi ya wana kikundi na mabadiliko (WFC) wakipiga picha ya pamoja na wawezeshaji wa mada kwenye Kongamano la wanawake kutoka Jijini Dar es salaam, akiwamo Sadaka Candi ambaye ni mwanasaikolojia (wanne kutoka kulia), akifuatiwa na Mchumi Hilda Kisoka mwenye nguo nyeusi.

Wajumbe wa Kikundi cha wanawake na mabadiliko (WFC), wakifuatilia Kongamano la wanawake ambalo ndiyo waandaaji.

Mwenyekiti Msaidizi wa kikundi cha wanawake na mabadiliko Women for Change Getrude Munuo, akitambulisha wajumbe wa kikundi hicho pamoja na kufungua rasmi Kongamano hilo.

Mwenyekiti wa maandalizi wa Kongamano hilo Fausta Kivambe, akitoa shukrani kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kwenye Kongamano hilo la wanawake.

Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa na mwenyekiti msaidizi wa kikundi cha wanawake na mabadiliko (WFC) Getrude Munuo, wakikata Keki kwa ajili ya kufungua Rasmi Kungamano hilo la wanawake.

Wanawake wa kikundi cha mabadiliko (WFC), Wakifungua Shampeni tayari kwa kuanza kwa Kongamano hilo la Wanawake Shinyanga mjini, "Shinyanga Women's Day Out."

Watoa mada wakiwa wameketi kwenye meza tayari kwa kutoa elimu mbalimbali kwenye Kongamano hilo la wanawake Shinyanga "Women's Day Out."

Mama Edna Shoo akitoa mada kwenye Kongamano hilo la wanawake juu ya Malezi na Mahusiano katika familia.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya akina mama kutoka hospitali ya rufani ya mkoa wa Shinyanga Dk. Rose Malisa, akitoa mada ya Saratani ya Mlango wa kizazi na matiti kwenye Kongamano hilo la wanawake.

Mwanasheria Salome Mbuguni akitoa mada ya Sheria juu ya mirathi pamoja na mwanamke kumiliki mali.

Kongamano linaendelea

Sadaka Candi (Maarufu Ant Sadaka) mshauri wa Saikolojia akitoa mada kwenye Kongamano la  wanawake namna ya kuishi na wanaume pamoja na malezi bora ya watoto katika familia.

Sadaka Candi( Maarufu Anti Sadaka), mshauri wa Saikolojia akitoa mada kwenye Kongamano la wanawake namna ya kuishi na wanaume pamoja na malezi bora ya watoto katika familia.
Mtoa Mada Hilda Kisoka akitoa mada kwenye Kongamano hilo la wanawake namna ya kukua kiuchumi. 
Mbunge wa viti Maalum mkoani Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga akizungumza kwenye Kongamano hilo la wanawake na kuwataka wanawake wapendane.

Wanawake wakiwa kwenye Kongamano la "Shinyanga Women's Day Out" Shinyanga mjini, lililoandaliwa na kikundi cha wanawake na mabadiliko (WFC), wa pili kushoto ni mbunge wa viti maalumu mkoani Shinyanga Mhe. Lucy Mayenga, na wa kwanza kushoto ni Diwani wa viti maalum manispaa ya Shinyanga Mariamu Nyangaka.

Wanawake wakiendelea na Kongamano la Shinyanga Women's Day Out.

Kongamano la wanawake likiendelea.

Kongamano la wanawake likiendelea.

Kongamano la wanawake likiendelea.

Wanawake wakicheza mziki kwenye Kongamano lao, "Shinyanga Women's Day Out".

Wanawake wakicheza muziki
Wanawake wakiwa kwenye kongamano la Shinyanga Women's Day Out

Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwasili kwenye Kongamano la wanawake "Shinyanga Women's Day Out" kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa Shinyanga, akipokewa na wanawake na mabadiliko (WFC) ambao ndiyo waandaji wa Kongamano hilo.
Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Share:

CCM MBOGWE YAITAKA SERIKALI KUDHIBITI WANAUME WANAOWAPA MIMBA WANAFUNZI

Na Salvatory Ntandu - Geita
Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kimeishauri serikali kuchukua hatua za haraka kuwadhibiti wanaume wanaowapa mimba wanafunzi kutokana na kukithiri kwa matukio mimba katika shule za msingi na sekondari.

Ushauri huo umetolewa Machi 5 mwaka huu na Katibu wa (CCM) wilaya ya Mbogwe, Grace Shindika, kwenye kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho, baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo Martha Mkupas.

Alisema serikali inapaswa kuhakikisha inawakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria wanaume wanaowapa mimba wanafunzi kwani vitendo hivyo vimekuwa vikikatisha ndoto zao za kuendelea na masomo.

“Wakamateni wanaojihusisha na mapenzi na wanafunzi ili kutokomeza vitendo hivi,serikali ya awamu ya tano chini Rais Dk. John Pombe Magufuli imetoa fursa ya elimu bure kuanzia darasa la awali hadi kidato cha nne,haiwezekani tukavifumbia macho vitendo hivyo”,alisema Shindika.

Alifafanua kuwa kwa kipindi cha Julai hadi Disemba mwaka 2019 wanafunzi wanne kutoka katika shule za sekondari walipata mimba katika wilaya hiyo na kusababisha kushindwa kuendelea na masomo lakini bado suala hilo halijapewa kipaumbele ili kulidhibiti.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 kwa kipindi cha Julai hadi Disemba,Mkuu wa wilaya ya Mbogwe Matha Mkupas alisema kwa kipindi hicho matukio ya wanafunzi kupata mimba yalikuwa manne katika shule za sekondari ambapo mashauri matatu tayari yameshafunguliwa.

Alifafanua kuwa kwa kipindi hicho shule zilizoripotiwa wanafunzi wake kupata mimba ni pamoja na ya sekondari Masumbwe (1) Iponya (1) Kanegere (1) na Ikunguigazi (1) ambapo tayari jeshi la polisi wilayani humo linaendelea na mashauria matatu katika mahakama za wilaya.

“Ili kutokomeza mimba katika shule zetu ni lazima tuwaelimishe wazazi kuacha vitendo vya kuharibu ushahidi kwa kufanya makukubaliano pindi kunapotokea kwa tukio la mimba kwa wanafunzi na kusababisha watuhumiwa kutoroka au kuwatorosha wanafunzi wenye mimba”,alisema Mkupas.

Kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho, kimepokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM ya mwaka 2015 kwa kipindi cha Julai hadi Disemba 2019.

Share:

KHERI JAMES AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA KATIBU WA UVCCM SHINYANGA..ATAHADHARISHA KUHUSU CORONA

Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi taifa (UVCCM) Kheri James akiweka jiwe la msingi katika jengo la nyumba ya katibu wa UVCCM mkoa wa Shinyanga.

Na Mwandishi wa Malunde 1 blog
Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM) Kheri James amewataka vijana wa kitanzania hususani wanachama wa CCM) kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa corona uliogundulika katika nchi ya China unaoendelea kusambaa kwa kasi kubwa katika mataifa mbalimbali ambao umesababisha vifo vya watu wengi.

Akizungumza katika hafla ya kuweka jiwe la msingi katika nyumba ya Katibu wa Jumuia ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga (UVCCM) uliofanyika Machi 7,2020  katika eneo la Ushirika Manispaa ya Shinyanga.

Alisema  ugonjwa wa Corona umekuwa tishio kwa mataifa mbalimbali hususani nchini China ambako uliripotiwa kwa mara ya kwanza mwaka huu kutokana na virusi vyake kusambaa kwa kasi katika mataifa mbalimbali barani Ulaya na kusababisha vifo kwa watu wengi.

“Tundelee kuchukua tahadhari kuhusiana na ugonjwa huu, serikali yetu kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na watoto, imekwishatoa maelekezo kuhusiana na namna bora ya kujikinga na ugonjwa huu, tuendelee kumuomba Mungu maambukizi yake yasiweze kuingia nchini kwetu”,alisema James.

James alifafanua kuwa bila ya kuwa na jamii yenye afya bora maendeleo hayawezi kupatikana hivyo ni budi elimu kwa vijana itolewe kuhusina na kujikinga na ungonjwa huo pamoja na magonjwa mengine ambayo ni hatari na yanasababisha kupunguza nguvu kazi ya kwa taifa.

Sambamba na hilo James aliwataka Wenyeviti wa UVCCM mikoa yote nchini kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa nyumba za makatibu kwa ngazi za mikoa na wilaya kabla ya mwezi Mei 2020 ili kutoa fursa ya kujiandaa na uchaguzi mkuu.

Katika hatua nyingine James aliwataka Viongozi wa UVCCM katika mikoa yote wasikubali kuwa madalali kwa watu wanaojipitisha katika majimbo na kata mbalimbali wanaotafuta kwa kuwa wao hawana mamlaka ya kuwachagua ama kupitisha majina yao.

“Wanaotaka nyadhifa ndani ya CCM wasubirie chama chetu kitakapotangaza muda wa kuanza kuchukua fomu ndipo watakaporuhusiwa kufanya kampeni kwa sasa ni mwiko kwa mwanachama yeyote kufanya kampeni za chini chini kutafuata uongozi kabla muda haujafika”alisema James.

Naye mwenyekiti wa Jumuia ya Umoja wa vijana mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge amesema nyumba hiyo itatumia shilingi milioni 35 hadi kukamilika kwake na kumshukuru Mwenyekiti wa UVCCM taifa,James kwa kuwachangia mifuko 80 ya saruji huku mbunge wa mkoa wa shinyanga Lucy mayenga akitoa mifuko 20 na kufikia jumla 100.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa aliwataka makatibu wa chama hicho kuhakikisha wanazilea jumuia zote za CCM ili kuzijengea uwezo katika utekelezaji wa majumu yake ya kila siku katika kujijenga chama.

“Toeni ushirikiano kwa jumuia hizi ili ziweze kufanya kazi vizuri kwani kuwepo kwao sisi cha chama tunapata fursa ya kuwaandaa viongozi wa baadae kwa kuwapa maelekezo mazuri kuhusiana na namna bora ya kujiendesha”,alisema Mlolwa.
Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi taifa (UVCCM) Kheri James akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la nyumba ya katibu wa UVCCM mkoa wa Shinyanga iliyopo katika eneo la Ushirika Mjini Shinyanga.
Baadhi ya wanachama wa CCM wakimpokea Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi taifa (UVCCM) Kheri James wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa.
Baadhi ya wanachama wa CCM wakimpokea Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi taifa (UVCCM) Kheri James wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Umoja wa vijana mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akimwongoza Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi taifa (UVCCM) Kheri James kuelekea eneo la uwekaji wa jiwe la msingi la nyumba ya katibu wa UVCCM mkoa wa shinyanga.
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa shinyanga wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti Jumuia ya Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi taifa (UVCCM) Kheri James.

Share:

MWALIMU AUAWA KWA KUPIGWA TOFALI BAADA YA KUGOMA KUNUNUA POMBE

Mwalimu wa Shule ya Msingi Mbugani kata ya Kakese mkoani Katavi Shauri Kiani (35) amefariki dunia baada ya kupigwa na tofali kichwani baada ya kukataa kumnunulia pombe anayetuhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea Machi 3, 2020 saa 5 usiku eneo la Mbugani. 

Mtuhumiwa ni Omary Juma (30) mkazi wa Kakese. Kiani alikimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Katavi lakini alifariki wakati anapatiwa matibabu.”

Amesema polisi walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa anayeendelea kuhojiwa, kwamba muda wowote atafikishwa mahakamani.

Share:

Watu wawili wafariki kwa kusombwa na mafuriko ya Maji Morogoro

Watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha huku mmoja akijeruhiwa kufuatia mvua kumbwa zilizonyesha usiku wa kuamkila leo Manispaa ya Morogoro, baada ya Daraja lililopo Mtaa wa Kihimbwa Kata ya Boma  kuziba na kusababisha maji kupita juu ya Daraja
 
Kwa mujibu wa Mtendaji wa Kata ya Kihimbiwa Antipasi Kinange ambapo amesema mvua hiyo imeanza kunyesha usiku wa kuamkia leo na watu hao  walienda dukani kwa ajili ya kununua bidhaa ndipo maji yalipozidi na kusombwa na maji.

Waliofariki katika mvua hiyo ni mwanamke aliyefahamika kwa jina la Habia Sanga huku mwanaume akifahamika kwa jina moja la Salum

Share:

Mawaziri wa Kazi na Ajira SADC Waipongeza Tanzania kutekeleza Programu ya Ukuzaji wa Ujuzi kwa Vijana.

Na: Mwandishi Wetu
Mawaziri na Wadau wa Utatu wa Nchi Wananchama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) sekta ya kazi na ajira waipongeza Serikali ya Tanzania kwa mikakati iliyojiwekea katika kuwajengea uwezo vijana kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi. 
 
Pongezi hizo zimetolewa na Mawaziri na Wadau wa utatu wa Jumuiya hiyo ikiwemo Jukwaa la Vyama vya Waajiri Kusini mwa Afrika (SPSF), Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Kusini mwa Afrika (SATUCC), Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya Uhamiaji kanda ya Kusini mwa Afrika (IOM). 
 
Akizungumza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) na waandishi wa habari wakati wa ziara yake aliyoambatana na Mawaziri na Wadau wa Utatu wa SADC sekta ya Kazi na Ajira walipotembelea Chuo cha Don Bosco Network kilichopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam na Maeneo ya Vivutio vya Utalii Bagamoyo alieleza kuwa Serikali iliamua kuanzisha programu hiyo lengo ikiwa ni kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kuwajengea mazingira wezeshi na yanayowahamasisha kuajiriwa au kujiajiri. 
 
“Mawaziri na Wadu wa Utatu wa SADC sekta ya Kazi na Ajira wamefurahia kuona namna Serikali inavyotekeleza Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuza kwa Vijana ambayo kwa kiasi kikubwa itawawezesha vijana kupata uwezo na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira kwa nchi hizo wanachama,” alisema Waziri Mhagama. 
 
“Zipo nchi wananachama wameomba kukutana na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo inatekeleza programu hiyo kwa lengo la kuweza kupata uelewa wa taratibu na namna ya kutekeleza programu hiyo, nchi ya Eswatini tayari imeonyesha nia ya kukutana na ofisi yangu ili nao waweze kuanzisha programu hiyo nchini kwao,” alieleza Mhagama 
 
Alieleza kuwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Mkutano huo wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa SADC sekta ya Kazi na Ajira uliozinduliwa Machi 5, 2020 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Serikali iliona umuhimu wa kuzindua Programu mmoja wapo ambayo ni Programu ya Mafunzo ya Vitendo Mahala pa Kazi (Internship) ili kuelezea nchi wanachama mikakati ambayo Serikali imejiwekea katika kutatua changamoto ya ajira inayowakabili vijana kwa kuwawezesha vijana kuwa na uzoefu katika utendaji kazi.   
 
Aidha aliongeza kuwa katika mkutano huo uliowakutanisha waliweza kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya Kazi na Ajira ambazo ni masuala ya Hifadhi ya Jamii, Uhamishaji wa nguvu kazi, mapitio ya sera na miongozo iliyotungwa na nchi wanachama kuhusu masuala ya kazi na ajira, haki na wajibu wa wafanyakazi, mapitio ya mikataba ya kimataifa na mikataba ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) inayoongoza masuala ya ajira pamoja na kuwajengea uwezo vijana. 
 
Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde wakati akielezea kuhusu programu ya ukuzaji ujuzi kwa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa SADC sekta ya Kazi na Ajira alieleza kuwa Programu hiyo ya Taifa ya Kukuza Ujuzi inafadhiliwa na Serikali kwa lengo la kuwawezesha vijana ambao kwa asilimia kubwa ndio nguvukazi ya taifa wanapata ujuzi na uzoefu ambao utawafanya waweze kujitegemea.   
 
“Hii ni habari njema kwa sisi Watanzania kutembelewa na Mawaziri na Wadau wa Utatu ambao wamekuja kujionea namna serikali yetu inavyowajali vijana na jinsi inavyowatumikia katika kuwawezesha kupata ujuzi ambao utawasaidia pindi vijana hao wanapomaliza mafunzo waweze kujiajiri ama kuajiriwa,” alisema Mavunde 
 
Alifafanua kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu inaratibu Programu ya Ukuzaji Ujuzi ikiwemo Mafunzo kwa Njia ya Uanagenzi, Mafunzo ya Urasimishaji Ujuzi uliopatikana Nje ya Mfumo Rasmi, Mafunzo ya Vitendo Mahala pa Kazi kwa Wahitimu na Mafunzo ya Ukuzaji Ujuzi kwa walio Makazini na Mpango huo wa Urasimishaji Ujuzi Uliopatikana Nje ya Mfumo Rasmi (Recognition of Prior Learning).  
 
Katika ziara hiyo Mawaziri na Wadau wa Utatu wa SADC sekta ya Kazi na Ajira walipata fursa ya kutembelea maeneo ya kihistoria yaliyopo Bagamoyo ikwemo Ngome Kongwe, Soko la zamani la Watumwa, Bandari iliyokuwa inatumika kuwasafirisha watumwa, eneo la Msalabani ambapo Ukristo ulianzia kuenezwa hapo na wakoloni, Magofu ya Kaole lengo la ziara hiyo ilikuwa kutangaza maeneo ya vivutio vya kihistoria vilivyopo hapa nchini. 
 
Waziri wa Kazi na Ajira Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Mhe. Ilunga Nkulu Nene alieleza kuwa wamevutiwa sana na maeneo ya kihistoria yaliyopo Tanzania kama vile mji wa kihistoria wa Bagamoyo Pwani, ambayo unaifanya Tanzania iwe nchi ya kuigwa kwa historia ya Nchi za Kusini mwa Afrika. 
 
“Nchi ya Kongo ina maeneo mengi ya kitalii lakini hatuyatangazi kama Tanzania inavyofanya, kama kiongozi nimejifunza jambo katika ziara ya leo na hivyo nitakaporudi Kongo nitahamasisha utangazaji wa maeneo ya kihistoria yaliyopo kwa lengo la kuvutia watalii,” alisema Nene
Mwisho.

Share:

Mawaziri Na Wadau Wa Utatu Wa Sadc Sekta Ya Kazi Na Ajira Wapongeza Serikali Ya Tanzania Kwa Utekelezaji Wa Programu Ya Taifa Ya Ukuzaji Ujuzi Kwa Vijana

Na: Mwandishi Wetu
Mawaziri na Wadau wa Utatu wa Nchi Wananchama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) sekta ya kazi na ajira waipongeza Serikali ya Tanzania kwa mikakati iliyojiwekea katika kuwajengea uwezo vijana kupitia Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi.

Pongezi hizo zimetolewa na Mawaziri na Wadau wa utatu wa Jumuiya hiyo ikiwemo Jukwaa la Vyama vya Waajiri Kusini mwa Afrika (SPSF), Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Kusini mwa Afrika (SATUCC), Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya Uhamiaji kanda ya Kusini mwa Afrika (IOM).

Akizungumza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) na waandishi wa habari wakati wa ziara yake aliyoambatana na Mawaziri na Wadau wa Utatu wa SADC sekta ya Kazi na Ajira walipotembelea Chuo cha Don Bosco Network kilichopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam na Maeneo ya Vivutio vya Utalii Bagamoyo alieleza kuwa Serikali iliamua kuanzisha programu hiyo lengo ikiwa ni kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kuwajengea mazingira wezeshi na yanayowahamasisha kuajiriwa au kujiajiri.

“Mawaziri na Wadu wa Utatu wa SADC sekta ya Kazi na Ajira wamefurahia kuona namna Serikali inavyotekeleza Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuza kwa Vijana ambayo kwa kiasi kikubwa itawawezesha vijana kupata uwezo na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira kwa nchi hizo wanachama,” alisema Waziri Mhagama.

“Zipo nchi wananachama wameomba kukutana na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo inatekeleza programu hiyo kwa lengo la kuweza kupata uelewa wa taratibu na namna ya kutekeleza programu hiyo, nchi ya Eswatini tayari imeonyesha nia ya kukutana na ofisi yangu ili nao waweze kuanzisha programu hiyo nchini kwao,” alieleza Mhagama

Alieleza kuwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Mkutano huo wa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa SADC sekta ya Kazi na Ajira uliozinduliwa Machi 5, 2020 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Serikali iliona umuhimu wa kuzindua Programu mmoja wapo ambayo ni Programu ya Mafunzo ya Vitendo Mahala pa Kazi (Internship) ili kuelezea nchi wanachama mikakati ambayo Serikali imejiwekea katika kutatua changamoto ya ajira inayowakabili vijana kwa kuwawezesha vijana kuwa na uzoefu katika utendaji kazi. 

Aidha aliongeza kuwa katika mkutano huo uliowakutanisha waliweza kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya Kazi na Ajira ambazo ni masuala ya Hifadhi ya Jamii, Uhamishaji wa nguvu kazi, mapitio ya sera na miongozo iliyotungwa na nchi wanachama kuhusu masuala ya kazi na ajira, haki na wajibu wa wafanyakazi, mapitio ya mikataba ya kimataifa na mikataba ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) inayoongoza masuala ya ajira pamoja na kuwajengea uwezo vijana.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde wakati akielezea kuhusu programu ya ukuzaji ujuzi kwa Mawaziri na Wadau wa Utatu wa SADC sekta ya Kazi na Ajira alieleza kuwa Programu hiyo ya Taifa ya Kukuza Ujuzi inafadhiliwa na Serikali kwa lengo la kuwawezesha vijana ambao kwa asilimia kubwa ndio nguvukazi ya taifa wanapata ujuzi na uzoefu ambao utawafanya waweze kujitegemea. 

“Hii ni habari njema kwa sisi Watanzania kutembelewa na Mawaziri na Wadau wa Utatu ambao wamekuja kujionea namna serikali yetu inavyowajali vijana na jinsi inavyowatumikia katika kuwawezesha kupata ujuzi ambao utawasaidia pindi vijana hao wanapomaliza mafunzo waweze kujiajiri ama kuajiriwa,” alisema Mavunde

Alifafanua kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu inaratibu Programu ya Ukuzaji Ujuzi ikiwemo Mafunzo kwa Njia ya Uanagenzi, Mafunzo ya Urasimishaji Ujuzi uliopatikana Nje ya Mfumo Rasmi, Mafunzo ya Vitendo Mahala pa Kazi kwa Wahitimu na Mafunzo ya Ukuzaji Ujuzi kwa walio Makazini na Mpango huo wa Urasimishaji Ujuzi Uliopatikana Nje ya Mfumo Rasmi (Recognition of Prior Learning).

Katika ziara hiyo Mawaziri na Wadau wa Utatu wa SADC sekta ya Kazi na Ajira walipata fursa ya kutembelea maeneo ya kihistoria yaliyopo Bagamoyo ikwemo Ngome Kongwe, Soko la zamani la Watumwa, Bandari iliyokuwa inatumika kuwasafirisha watumwa, eneo la Msalabani ambapo Ukristo ulianzia kuenezwa hapo na wakoloni, Magofu ya Kaole lengo la ziara hiyo ilikuwa kutangaza maeneo ya vivutio vya kihistoria vilivyopo hapa nchini.

Waziri wa Kazi na Ajira Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Mhe. Ilunga Nkulu Nene alieleza kuwa wamevutiwa sana na maeneo ya kihistoria yaliyopo Tanzania na ni nchi ya kuigwa.

“Nchi ya Kongo ina maeneo mengi ya kitalii lakini hatuyatangazi kama Tanzania inavyofanya, kama kiongozi nimejifunza jambo katika ziara ya leo na hivyo nitakaporudi Kongo nitahamasisha utangazaji wa maeneo ya kihistoria yaliyopo kwa lengo la kuvutia watalii,” alisema Nene

MWISHO

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger