Watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha huku mmoja akijeruhiwa kufuatia mvua kumbwa zilizonyesha usiku wa kuamkila leo Manispaa ya Morogoro, baada ya Daraja lililopo Mtaa wa Kihimbwa Kata ya Boma kuziba na kusababisha maji kupita juu ya Daraja
Kwa mujibu wa Mtendaji wa Kata ya Kihimbiwa Antipasi Kinange ambapo amesema mvua hiyo imeanza kunyesha usiku wa kuamkia leo na watu hao walienda dukani kwa ajili ya kununua bidhaa ndipo maji yalipozidi na kusombwa na maji.
Waliofariki katika mvua hiyo ni mwanamke aliyefahamika kwa jina la Habia Sanga huku mwanaume akifahamika kwa jina moja la Salum
0 comments:
Post a Comment