Wednesday, 4 March 2020

Watatu Watiwa Mbaroni Kwa tuhuma za wizi kwenye nyumba za kulala wageni Jijini Mbeya

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
 
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA WIZI KWENYE NYUMBA ZA KULALA WAGENI.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watuhumiwa watatu kwa tuhuma za wizi kwenye nyumba za kulala wageni [Guest House] ambao ni:-

1. WAMBURA DANIEL [47] Mkazi wa Kyabakari Mkoani Mara.

2. SELVANUS MATIKO [53] Mkazi wa Manyamanyama – Bunda.

3. JEREMIA KAKURU [45] Mkazi wa Ukerewe Nansio

Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29.02.2020 majira ya saa 13:00 mchana huko Stendi ya Ilomba, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya.

Ni kwamba mnamo tarehe 29.02.2020 majira ya saa 06:00 asubuhi watuhumiwa wakiwa wamepanga katika moja ya nyumba za kulala wageni walimvizia mpangaji mmoja aitwaye RIZIKI MGWAMA [31] Mkazi wa Mafinga alipokwenda kuoga na kufunga chumba chake lakini watuhumiwa walifungua kufuli la chumba hicho kwa kutumia waya maalum na kisha kuingia ndani na kuiba begi ambalo ndani yake lilikuwa na vitu vifuatavyo:-

1. Laptop moja aina ya hp.
2. Simu ndogo aina ya Samsung
3. Power bank mbili
4. Nyaraka mbalimbali na vitambulisho vya kazi.

Watuhumiwa wamefikishwa Mahakama ya Mwanzo Mbeya Mjini CC.NO.140/2020 – Wizi kwenye Magesti.

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA UVUNJAJI.
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia kijana mmoja aitwaye GIFT BRITHON [20] Mkazi wa Mapelele kwa tuhuma za kuhusika kwenye matukio ya uvunjaji na wizi wa mali mbalimbali.

Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 03.03.2020 majira ya 21:00 usiku huko eneo la Mapelele, Kata ya Ilemi, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi kufanya msako na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa na vifaa mbalimbali vya kuvunjia ambao ni Nondo, Bisibisi, Patasi na Tindo.

Aidha mtuhumiwa baada ya kupekuliwa alikutwa na mali za wizi ambazo ni:-

1. Pikipiki moja MC 233 CEJ aina ya T-Better
2. TV Flat Screen mbili aina ya Samsung
3. Redio Sub Woofer moja [01].
4. Spika mbili [02]
5. Remote Control moja [01]
6. Vitenge doti kumi na tatu [13]
7. Sandals jozi mbili [02]

Mtuhumiwa amekiri kuhusika kwenye matukio ya uvunjaji na wizi katika maeneo mbalimbali hapa Mbeya na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa shauri hili kukamilika.

RAI YA JESHI LA POLISI KWA WAZAZI/WALEZI KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa rai kwa wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao wadogo ikiwa ni pamoja na kuwawekea uangalizi mzuri kwa muda wote ili kuepuka madhara yanayoweza kuwapa watoto hao pindi wanapokuwa wenyewe.

Kwa kipindi cha hivi karibuni, kumekuwa na matukio ya watoto wadogo kufariki kutokana na kutumbukia katika visima vya maji, katika mabwawa ya maji, madimbwi yenye maji au katika mito pindi wanapovuka kuelekea Shuleni au wanapocheza.

Katika msimu huu wa mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali tayari zimeanza kuleta madhara kwa binadamu hasa watoto wadogo. Yapo mambo ya kuepuka hasa matumizi ya vifaa vya umeme kama vile redio, tv na simu za mkononi wakati mvua kubwa zinazoambatana na radi zikinyesha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa tahadhari kufuatia matukio ya kufa maji yanayosababishwa na uzembe wa kutovaa maboya wakati wanapoingia majini, mtoni au ziwani.

Aidha kufuatia mvua zinazonyesha nawasihi wazazi kuwapeleka watoto wadogo shuleni na kuwapokea ili kuwalinda dhidi ya madhara ya kutumbukia katika maji.
 
Pia tunatoa angalizo kwa watu wanaofanya shughuli za uchimbaji madini katika migodi, kuchukua tahadhari za kiusalama ili kuepuka ajali katika maeneo hayo hasa za kuangukiwa vifusi vya udongo hususani msimu wa huu wa mvua.

Tunapaswa kuchukua tahadhari kwa kufukia mashimo yasiyokuwa na dhahabu kwani ni hatari kwa watoto na watu wazima pindi yanapojaa maji.

Ni wito wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuzingatia ulinzi wa mtoto, malezi bora kwa mtoto na pia kuwasaidia watoto hasa kuwavusha katika maeneo yenye mito au maji mengi ili kuepuka madhara yanayoweza kuwapata. Pia ni kipindi cha kufukia mashimo, madimbwi yenye maji kwani ni hatari hasa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali.


Share:

CHADEMA Wajutia Makosa ya 2015.....Baraza la Wazee Lamkataa Benard Membe

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kinajutia uamuzi kiliochukua wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kuchukua wale waliokatwa kutoka CCM ambao sasa wamerejea katika chama chao cha zamani.

Akizungumza ofisi za Makao Makuu ya Chadema jana, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema (Bazecha), Hashim Juma alisema pamoja na heshima aliyonayo kwa aliyekuwa mgombea wa Ukawa mwaka 2015, Edward Lowassa, lakini tathmini ya baraza hilo imeonyesha hakuwa na msaada mkubwa kwenye chama.

“Kwa kweli katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 tuliweka mgombea dhaifu ambaye kwanza alishindwa kulinda kura zetu kwa sababu ya u-CCM wake ambao hakuuvua wakati huo.

“Lakini pia ndani ya Ukawa tulisimamisha mgombea mwenza ambaye pia hakuwa mwana Chadema, hivyo hakuwa na uchungu na chama chetu.

“Kwa hiyo, hatutaki kuona makosa tuliyoyafanya mwaka 2015 yakijirudia mwaka huu, hasa baada ya kukijenga chama nchi nzima kuanzia ngazi ya chini kabisa, kazi tuliyoifanya kwa miaka miwili.

“Ni wazi kwamba tayari kuna mmoja wa viongozi wakuu wa chama, ambaye ana uchungu na chama, aliyeko nje ya nchi kwa sasa, ambaye ameshaeleza utayari wake wa kuwania urais iwapo atateuliwa na chama kwa hiyo huyo ndiye tunayemuunga mkono,” alisema Juma.

Mwenyekiti huyo wa Bazecha alisisitiza kuwa kwa sasa hawako tayari kutumika kama njia ya baadhi ya wanasiasa kutaka kutimiza mahitaji yao binafsi kwa kuingia katika chama hicho na wakikosa wanachokihitaji wanarejea kule walikotoka, kama walivyofanya baadhi ya wanasiasa walioingia Chadema kisha kurejea CCM baada ya kushindwa kutimiza malengo yao binafsi.

Alisema japokuwa baraza hilo halina mamlaka ya Kamati Kuu ya chama, wala ya mkutano mkuu, baraza hilo linatamka wazi kwamba haliko tayari kuona uongozi wa chama hicho ukizungumza suala la kumpokea Bernard Membe, aliyekuwa mwanachama wa CCM ambaye Kamati Kuu ya chama chake imeridhia kwa kauli moja kumvua uanachama.

“Sisi kama wazee tumemridhia na tunampa baraka zetu zote Lissu, kwa hivyo Mheshimiwa Membe tunamtakia kila la kheri na kama atakwenda chama kingine, tutashukuru na tutafurahi kwa sababu kwa vyovyote vile anakwenda kuzigawa kura za CCM.

“Ni kwa sababu, Membe hawezi kuchukua kura hata moja ya Chadema, ataondoka na kundi kubwa la CCM kama Lowasa hivyo atapata kura za chama atachoenda pamoja na za CCM.” amesema Mzee Hashimu. 


Wakati huo huo Mzee Hashimu ameeleza, msimamo wa baraza hilo ni kupigania Tume Huru ya Uchaguzi ili uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2020 uwe wa huru na haki.


Share:

Baraza La Madiwani Halmashauri Ya Jiji La Dodoma Lakubali Kupunguza Bajeti Kutoka Bilioni 72 Hadi Bilioni 62

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji la Dodoma limekubali kupitisha pendekezo la kupunguza Bajeti ya jiji kwa mwaka 2019/2020 kutoka Sh Billioni sabini na mbili, milioni mia tisa sabini, laki nne tisini na sita na mia nne ishirini na saba (72,970,496,427) hadi sh Bilioni sitini na mbili, mlioni mia tisa sabini laki nne tisini na sita na mia nne ishirini na saba (62,970,496,427).

Akizungumza katika kikao Maalum cha Baraza hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin kunambi amesema Halmashauri ya jiji ilikadiria kukusanya jumla ya sh bil 72,970,496,427 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya ndani.

Aidha, kunambi amesema katika makadirio hayo, Halmashauri ilitegemea kiasi kikubwa kukusanywa toka katika chanzo cha uuzaji viwanja vitakavyokuwa vimepimwa.

Wakati huohuo, Kunambi amesema hadi kufikia mwezi Disemba mwaka 2019 chanzo hicho, wamefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi Bilioni kumi na tisa, milioni mia moja kumi n ambili elfu ishirini na nne na mia sita tisini na tatu 19,112,024,693 kati ya shilingi Bilioni 27,000,000,000 zilizotakiwa ziwe zimekusanywa kwa kipindi cha miezi sita sawa na asilimia 35.4% kwa tathmini iliyofanyika .

Akizungumzia chanzo cha ushuru wa masoko Kunambi amesema walitarajia kukusanya jumla ta shilingi milioni  362,314,000 katika bajeti yao ya mwaka 2019/2020 kimeshindikana kukusanywa na haitakusanywa kutokana na wafanyabiashara waliokuwa wanalipa kutakiwa kuwa na kitambulisho cha mjasiriamali ambapo hulipa sh elfu 20,000 na fedha hiyo hupelekwa serikali kuu.



Share:

Wanaotumia Maji Nje Ya Mfumo Kahama Kuchukuliwa Hatua Za Kisheria

NA SALVATORY NTANDU
Mkazi wa mtaa wa Lugela Kata ya Nyahanga wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Ismail Kitinga anashikiliwa na jeshi la Polisi wilayani humo kwa mahojiano baada ya kutuhumiwa kujiunganishia maji kwa njia isiyo halali kutoka Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira Mjini Kahama (KUWASA).

Akizungumza na waandishi wa katika eneo la Tukio  Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini kahama(KUWASA) Misana Shija alisema kuwa Ismail alijiunganishia huduma ya Maji kinyume na utaratibu na Mamlaka hiyo kuisababisha hasara serikali.

“Ismail ni mteja wa KUWASA  tumebaini kuwepo uchepushaji wa maji kabla ya kufika kwenye mita yetu ambayo tumemwekea huku akijua wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria na kuikosesha mamlaka ya mapato,”alisema Shija.

Misana alifafanua kuwa baada ya matumizi ya maji kushuka ya Ismail kutoka uniti 20 kwa mwezi hadi Uniti moja ndipo mafundi wa mamlaka walipofika  nyumbani kwake kufuatilia mfumo wa maji na kubaini kuwepo kwa maunganisho yasiyo halali.

“KUWASA inaendelea na zoezi la kubaini wateja wake ambao wanatumia maji nje ya mfumo na kuwataka wateja wote wanaojiuhisha na vitendo  hivyo kuacha mara moja kwani watakao bainika watachukuliwa hatua kali za kisheria ”alisema Misana.

Kwa upande wake Ismail Kitinga ambaye anatuhumiwa kuhujumu miundombinu ya maji amekiri kutokea kwa wizi wa maji katika nyumba yake na kusema  kuwa yeye hakuwa na taarifa za kuwepo kwa wizi huo kwani hapo awali alishatoa taarifa za kuibiwa mita katika Idara ya Maji, na kuomba kuwekewa mita nyingine ambayo iliwekwa ndani ya uzio wa nyumba yake.

“Mimi binafsi sijui aliyefanya maunganisho haya ila mimi ninachojua ni kwamba walikuja mafundi kutoka KUWASA na kuniwekea mita mpya hapa kwangu baada ya zamani kuibiwa na watu wasiojulikana,siwezi kuiba maji kwani ninauwezo wa kulipa maji”alisema Kitima.

KUWASA inaendelea na zoezi la kukagua miundombinu ya maji kwa wateja wake ili kubaini wanaotumia maji nje ya mfumo ambao unaisababishia hasara Mamlaka na serikali.

Mwisho.


Share:

Ahukumiwa Kunyongwa Hadi Kufa Kwa Kuua na Kisha Kupora Milioni 1, Chupa ya Chai na Simu

Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, imemuhukumu kunyongwa hadi kufa mkazi wa Kijiji cha Kibubwa, Wilaya ya Butiama mkoani Mara, Waryoba Elias baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki kumuua Chacha Ibuga usiku wa kuamkia Novemba mosi, 2017.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, John Kayohoza, alimkumbushia mshtakiwa shtaka lililokuwa linamkabili katika kesi hiyo namba 33/2019.

Jaji Kayohoza akisoma mazingira ya kesi na ushahidi wa mashahidi watano, ilielezwa Novemba mosi, 2017 saa 6.00 usiku, mshtakiwa akiwa na wenzake watano ambao hawajafahamika, wakiwa na tochi mbili na mapanga, walivamia nyumbani kwa Chacha Isoye Ibuga.

Ilielezwa wakati Ibuga akiwa ndani, kabla ya kuvamiwa alisikia mbwa wake anabweka na kuamua kutoka nje kuona kuna nini na ghafla watu hao walimshambulia kwa kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili, hasa kichwani na kupiga kelele kuomba msaada, ndipo mke wake, Lucy Lukondo alilazimika kutoka kwa lengo la kumsaidia.

Wakati Lucy anatoka ndani, alikutana na watu watatu na kumzuia na kumlazimisha kuingia ndani kumtaka awape fedha.

Kwamba mshtakiwa huyo kwa kushirikana na wenzake walifanya upekuzi ndani ya chumba alichokuwa analala marehemu na mke wake na kufanikiwa kupora fedha taslimu Sh milioni moja, chupa moja ya chai na simu moja ya mkononi.

Imeelezwa miongoni mwa watu walioingia ndani, aliyekuwa mmoja wa washtakiwa alikuwa ni jirani yao ambaye anamwita marehemu mjomba.

Watu hao baada ya kutekeleza ukatili huo, walitoweka na kwenda kusikojulikana huku majeruhi Ibuga akipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Butiama ambako baadaye alifariki dunia na baada ya siku kadhaa mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani.

-Mtanzania


Share:

Zaidi ya Vijana 150 waibuka na Kufanya Vurugu Katika Mkutano wa Freeman Mbowe

Mkutano wa Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe uliokuwa ukifanyika jana katika kijiji cha Kikafu Chini, ulivurugwa baada ya kuibuka kikundi cha vijana zaidi ya 50 wa kike na kiume kwenye mkutano huo na kuanzisha vurugu huku wakipiga kelele wakiimba "Sema ulichofanya, tunamtaka Magufuli"

Mbowe  alipanda jukwaani jana  saa 11:12 jioni ambapo alizungumza hadi saa 11:47 jioni ndipo kundi la vijana lilipoibuka na kuanza kupiga kelele, jambo lililomfanya mbunge huyo kunyamaza.

Hata hivyo kabla ya kunyamaza, Mbowe alisema polisi hili ndilo kundi ambalo tuliwaambia na baada ya kauli hiyo alinyamaza akiangalia vurugu hizo.

Vijana hao wanaodaiwa kutoka maeneo mbalimbali walianza kupiga kelele wakisema "sema ulichofanya, tunataka Magufuli” hali ambayo iliwafanya polisi kuingilia kati kuanza kutuliza vurugu hizo.

Baada vurugu kuendelea, polisi ambao walikuwa na gari moja waliongeza nguvu kwa kuja polisi waliokuwa wamevalia sare na kudhibiti kikundi hicho kusogelea jukwaa alilokuwa amesimama Mbowe.

Alivyonyamaza zaidi ya dakika 20 akiwatizama bila kuongea chochote polisi nao walisimama ili wasiende kwenye jukwaa alilokuwa Mbowe.Baadaye waliondoka


Share:

Tanzania Kuuza Makontena 200 ya Maharage nchini Ubelgiji...Changamkia Hiyo Fursa!!

Ubalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji umepata soko kubwa la maharage machanga ya kijani yanayojulikana kama haricots vertz(green thin beans) nchini Ubelgiji. 

Soko hilo limepatikana baada ya Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Jestas Abuok Nyamanga kufanya mazungumzo  na uongozi wa juu wa kampuni ya CBG-Charlier-Brabo Group inayonunua maharage hayo kutoka sehemu mbalimbali duniani na kuyauza katika supermarkets kubwa za Carrefour, Delhaize na Aldi za nchini Ubelgiji, Luxembourg na nchi nyingine za Ulaya.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika tarehe 3 Machi 2020, kampuni hiyo ipo tayari kununua containers kati ya 180-200 za maharage hayo kila mwaka kutoka Tanzania.

Kupatikana kwa soko la maharage hayo nchini Ubelgiji ni habari njema kwa wakulima wa Tanzania na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo hususan wa aina hiyo ya maharage ambayo tayari Tanzania inayauza nchini Uholanzi.

Kampuni hiyo pia imeonesha utayari wa kununua aina nyingine ya maharage ijulikanayo kama red kidney beans na chickpea kwa kiwango cha containers 8 kila mwaka katika hatua za mwanzo.

Ubalozi wa Tanzania unatoa wito kwa Watanzania kuchangamkia upatikanaji wa soko hilo jipya nchini Ubelgiji kwa kuwasiliana na kampuni hiyo kupitia tovuti yao ya www.cbg.be au kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa maelekezo zaidi.


Share:

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje Dkt. Damas Ndumbaro Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Balozi Wa Cuba Nchini

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amekutana na kufanya mazugumzo na Balozi wa Cuba nchini Mhe. Prof. Lucas Domingo Hernandez Polledo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumo hayo viongozi hao wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika sekta ya afya nchini na Cuba imeiomba Tanzania kuiunga mkono katika mpango wake wa kugombea kiti katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Pamoja na mambo mengine walizungumzia kuhusu jinsi ya kuboresha mahusiano yaliyopo katika kati ya Tanzania na Cuba, ambapo Cuba imekuwa mdau muhimu wa maendeleo ya sekta ya afya nchini.


Share:

Prof. Kabudi Apokea Hati Za Utambulisho Kutoka UN,UNHCR

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa (UN) Bw. Zlatan Milišić Pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw. Antonio Canhandula Jijini Dar es Salaam.

Waziri Kabudi amewaeleza Bw. Milišić na Bw. Canhandula kuwa UN pamoja na UNHCR zimekuwa na mchango mkubwa kwa kuiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukuza maendeleo pamoja na zile za kushughulikia masuala ya wakimbizi.

“Kwa ujumla UN imekuwa ikisaidia Tanzania kufanikisha agenda zake za maendeleo endelevu ya kijamii, na kiuchumi hivyo Serikali itaendelea kuhakikisha inaendeleza uhusiano huu," Amesema Prof. Kabudi.

Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Shughuli za Umoja wa Mataifa nchini (UN) Bw. Milisic amesema kuwa uhusiano wa UN na Serikali ya Tanzania ni wa muda mrefu na hivyo ni jukumu la UN kuhakikisha inaimarisha uhusiano huo na kuuboresha.

 “Ni matumaini yangu kuwa uhusiano huu tutauboresha vizuri na kuimarisha kwa maslahi mapana na maendeleo endelevu ya taifa la Tanzania," Amesema Bw. MiliÅ¡ić

Nae Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw. Canhandula amesema wanatambua mchango mkubwa ambao Tanzania imekuwa ikiutoa kuhakikisha inaimarisha ulinzi wa maeneo ya wakimbizi ili wananchi wa maeneo hayo waendelee kuishi kwa amani na utulivu pamoja na kupatiwa mahitaji muhimu kama vile malazi na mavazi.

"Kwa kweli UNHCR tunafurahishwa na jinsi Serikali ya Tanzania ambavyo imekuwa ikipokea wakimbizi na kuwapatia baadhi ya mahitaji muhimu……tunaomba tuendeleze ushirikiano huu kwa maendeleo yetu," Amesema Bw. Canhandula.


Share:

Watuhumiwa Kesi Ya Uhujumu Uchumi Waomba Kurejeshewa Kadi Zao Za Benki

Mkurugenzi wa Uthamini wa madini ya almasi na vito wa serikali, Archad Kalugendo na Edward Rweyemamu, wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wamewasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiomba kurejeshewa kadi zao za benki.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, jana amekiri mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kupokea nakala ya maombi hayo.

Wankyo alidai upande wa Jamhuri unaomba siku 14 kwa ajili ya kujibu maombi ya utetezi.

Upande wa utetezi haukuwa na pingamizi kuhusu ombi la Jamhuri kupewa siku 14.

Awali upande wa Jamhuri ulidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika, lakini wamewaelekeza wapelelezi wafanikishe maeneo machahe yaliyobaki.

Hakimu Shaidi alisema, maombi hayo yatatajwa Machi 6, na kesi ya msingi itatajwa Machi 20, mwaka huu, washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanakabiliwa na kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Sh. 2,486,397,982.54 kati ya Agosti 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga.


Share:

Kenya yasimamisha safari za ndege kutoka Kaskazini mwa Italia

Serikali ya Kenya imesimamisha safari za ndege kutoka Kaskazini mwa Italia kutokana na mlipuko wa nimonia ya COVID-19 nchini humo.

Mwenyekiti wa Kamati ya kitaifa ya mwitikio wa dharura dhidi ya COVID-19 Bw. Mutahi Kagwe, amesema safari za ndege kutoka Kaskazini mwa Italia, hasa miji ya Verona na Milan, kwenda mkoa wa pwani nchini Kenya zimesimamishwa kuanzia tarehe 3 mwezi Machi.

Bw. Kagwe ambaye pia ni waziri wa afya wa Kenya amesema, Kenya itaendelea kufuatilia hali ya nchini Italia na kurekebisha sera yake kulingana na maendeleo ya hali.


Share:

Waziri Mkuu: Maeneo ya Shule Yatumike kwa Shughuli za Kitaaluma

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepiga marufuku shughuli zisizohusiana na taaluma kama ujenzi wa viwanda katika maeneo ya shule ili kutoa fursa kwa wanafunzi kuwa kwenye mazingira mazuri ya kujifunzia.

“Sheria inakataza kuweka matumizi yoyote yasiyokuwa ya kitaaluma katika maeneo ya shule kwani yanasababisha kelele hivyo wanafunzi kushindwa kusoma vizuri.”

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni(Jumanne, Machi 3, 2020) baada ya kupokea malalamiko ya wazazi kuhusu eneo la shule ya msingi Mshikamano iliyoko Halmashauri ya Mji Handeni kuuzwa kwa mfanyabiashara ambaye amefungua karakana ya kutengeneza magari.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu aliuangiza uongozi wa halmashauri hiyo ukazungumze na mfanyabiashara huyo  ili  aondoe karakana katika eneo hilo na kumtafutia eneo mbadala kwa ajili ya kuendesha shughuli zake na eneo hilo libaki kwa ajili ya masuala ya kitaaluma.

Pia, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni upange matumizi bora ya ardhi kwa kuainisha maeneo ya makazi, biashara, viwanda na huduma za kijamii ili kuepuka mji huo kujengwa bila ya mpangilio.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwataka wananchi kuwafikisha kwenye vyombo vya dola walimu watakaobainika kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi. “Serikali imeweka sheria kali ya kumlinda mtoto wa kike, ukimpa mimba, ukimchumbia au kumuoa adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela.”

Akizungumzia kuhusu uwepo wa mabango mengi kwenye mikutano ya hadhara ya viongozi wa Kitaifa, Waziri Mkuu alisema kunadhihirisha wazi kwamba watendaji wa Halmashauri hawawatembelei wananchi katika maeneo yao na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

“Watendaji hamuendi kuwatembelea wananchi na kusikiliza matatizo yao, haiwezekani wawe wanawasubiri viongozi wa juu na kuwasilisha kero zao, sasa jipangeni haya mabango yote mtakuja kuyajibu kwa sababu hoja zote ni za ngazi ya halmashauri,” alisema.

Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeelekeza nguvu kubwa katika kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao, hivyo itasimamia kuhakikisha kila mtumishi anawajibika kwa kiwango kinachostahili.

“Serikali hii haimlindi mfanyakazi ambaye ni mbadhilifu, mwizi na asiyefanya kazi kwa weledi au anayebagua wananchi eti kwa uwezo wake wa kifedha au rangi au dini yake au chama chake. Hivi vitu havipo katika Serikali kila mwananchi aliyeko Nzega anatakiwa kuhudumiwa,”alisisitiza

 (mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU AJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI CHUONI


Picha ya mahali ambapo mwanafunzi huyo amejirusha

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mount Kenya,amefariki dunia kwa kujirusha kutoka ghorofa ya saba katika jengo la Chancellors Tower linalomilikiwa na chuo hicho.

Naibu wa Jeshi la Polisi wa Mji wa Nakuru Daniel Kitavi, amesema mwanafunzi huyo amefariki dunia wakati anapatiwa matibabu katika hospitali ya Thika Level V, ambapo alikimbizwa baada ya kujirusha kutoka ghorofani na kwamba aliumia zaidi maeneo ya kichwani.

Aidha wanafunzi wenzake walidai kwamba, mwenzao huyo alikuwa anajitishia kujitoa uhai kwa sababu ya matatizo yake binafsi.

Chanzo : Citizen Digital
Share:

TARURA KUBORESHA BARABARA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUCHOSA


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ,Josephati Kandege wa Pili kushoto akifanya Ukaguzi wa miradi ya katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, Mkoani Mwanza

Na Geofrey A. Kazaula – BUCHOSA
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI Mhe, Josephat Kandege ameuelekeza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA kuboresha Barabara katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Mkoani Mwanza ikiwa ni pamoja na kukarabati barabara zilizoharibiwa na mvua.

Hayo yamejiri wakati wa kukamilisha ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Mwanza ikiwa ni pamoja na kukagua hali ya barabara zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA.

“Kuna maelekezo kwa TARURA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI kuwa kwa fedha za matengenezo ya barabara katika mipango yao, wahakikishe kuwa matengenezo hayo yafanyike kwa kuaza na maeneo yaliyoharibika sana ili kurudisha huduma kwa wananchi,’’ Amesema kiongozi huyo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mhe, Charles Tizeba ameeleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa ni mpya na hivyo haina Barabara za lami na kuomba Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA kujenga walau kilomita chache kwa kiwango cha lami ili Halmashauri hiyo iweze kupendeza.

‘‘Halmashauri yetu ni mpya na haina barabara za lami hivyo kwakweli naomba TARURA waone namna ya kutusaidia ili Buchosa nayo ifanane na Halmashauri nyingine,’’ Amesema Mbunge huyo.

Naye Mkurugenzi anaye simamia Barabara za Vijijini kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA Mhandisi Abdul Digaga amefafanua kuwa tayari bajeti imetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara za lami kwa Halmashauri ya Buchosa lakini pia matengenezo ya Barabara tayari maelekezo yametolewa kwa nchi nzima kuhakikisha kipaumbele kina kuwa kwa maeneo yaliyo haribiwa zaidi ili kurejesha huduma kwa wananchi.

“Tayari maelekezo yametolewa kwa nchi nzima kuhakikisha matengenezo ya barabara yanazingatia kipaumbele kwa kuanza na maeneo yaliyoharibika sana na tunafanya hivi ili kurejesha huduma kwa wananchi wetu kwani yapo maeneo yaliyoathiriwa na mvua kwa kiasi kikubwa,’’ Amesema Mhandisi Digaga.

Naibu Waziri Kandege pia amesisitiza kuwa atafanya ufuatiliaji wa karibu na kuhakikisha Hospitali ya Wilaya ya Buchosa inafunguliwa na kuanza kutoa huduma kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya miradi aliyoitembelea.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano March 4




















Share:

Tuesday, 3 March 2020

Material Technician at TANROADS

MATERIAL TECHNICIAN  TANZANIA NATIONAL ROADS AGENCY (TANROADS) is a Semi – Autonomous Agency under the Ministry of Work, Communication and Transport established on July 1st 2000 and is responsible for the day-to-day management of the Tanzania Mainland’s Trunk and Regional roads Network. Its primary functions include the Management of Maintenance and Development Works, Operation of the Network and… Read More »

The post Material Technician at TANROADS appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

CAD Technician at TANROADS

CAD TECHNICIAN   TANZANIA NATIONAL ROADS AGENCY (TANROADS) is a Semi – Autonomous Agency under the Ministry of Work, Communication and Transport established on July 1st 2000 and is responsible for the day-to-day management of the Tanzania Mainland’s Trunk and Regional roads Network. Its primary functions include the Management of Maintenance and Development Works, Operation of the Network and… Read More »

The post CAD Technician at TANROADS appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger