Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji la Dodoma limekubali kupitisha pendekezo la kupunguza Bajeti ya jiji kwa mwaka 2019/2020 kutoka Sh Billioni sabini na mbili, milioni mia tisa sabini, laki nne tisini na sita na mia nne ishirini na saba (72,970,496,427) hadi sh Bilioni sitini na mbili, mlioni mia tisa sabini laki nne tisini na sita na mia nne ishirini na saba (62,970,496,427).
Akizungumza katika kikao Maalum cha Baraza hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin kunambi amesema Halmashauri ya jiji ilikadiria kukusanya jumla ya sh bil 72,970,496,427 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya ndani.
Aidha, kunambi amesema katika makadirio hayo, Halmashauri ilitegemea kiasi kikubwa kukusanywa toka katika chanzo cha uuzaji viwanja vitakavyokuwa vimepimwa.
Wakati huohuo, Kunambi amesema hadi kufikia mwezi Disemba mwaka 2019 chanzo hicho, wamefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi Bilioni kumi na tisa, milioni mia moja kumi n ambili elfu ishirini na nne na mia sita tisini na tatu 19,112,024,693 kati ya shilingi Bilioni 27,000,000,000 zilizotakiwa ziwe zimekusanywa kwa kipindi cha miezi sita sawa na asilimia 35.4% kwa tathmini iliyofanyika .
Akizungumzia chanzo cha ushuru wa masoko Kunambi amesema walitarajia kukusanya jumla ta shilingi milioni 362,314,000 katika bajeti yao ya mwaka 2019/2020 kimeshindikana kukusanywa na haitakusanywa kutokana na wafanyabiashara waliokuwa wanalipa kutakiwa kuwa na kitambulisho cha mjasiriamali ambapo hulipa sh elfu 20,000 na fedha hiyo hupelekwa serikali kuu.
0 comments:
Post a Comment