Tuesday, 18 February 2020

FULL TIME : YANGA SC 1, POLISI TANZANIA 1

FT:-Polisi Tanzania 1-1 Yanga
Uwanja wa Ushirika,Moshi
Goal: Tariq dk 41
Goal ;Sabilo dk 71

Zinaongezwa dakika nne
Dakika ya 90 mlinda mlango wa Polisi Tanzania anapewa huduma ya kwanza Dakika ya 71 Sabilo anafunga bao la kusawazisha kwa pasi ya Kaheza aliyepiga kona
Dakika ya 67 Sabilo anatengeneza pasi kwa Pato Ngonyani anafunga bao safi kwa kichwa linakataliwalinakataliwa
Dakika ya 66 Morrison anafanya jaribio linaokolewa na mlinda mlango
Morisson anapiga faulo inaokolewa
Dakika ya 66 Yikpe anaingia anatoka Tariq
Dakika ya 62 Morisson anapiga kona ya tano
Dakika ya 60 Morisson anapiga kona ya nne
Dakika ya 58 Tariq anapewa huduma ya kwanza
Dakika ya 56 Juma Abdul anapeleka majalo yanaokolewa na mlinda mlango wa Polisi
Dakika ya 55 Kaheza anapewa huduma ya kwanza
Dakika ya 54 Tariq anafanya jaribio halizai matunda
Dakika ya 53 Majogoro anacheza faulo
Dakika ya 51 Yanga wanafanya mashambulizi Kwa Polisi linaokolewa
Dakika ya 50 Polisi Tanzania wanafanya shambulizi linaokolewa
 Dakika ya 47 Yanga wanapeleka mashambulizi Polisi

ziliongezwa dakika 2 Dakika ya 41 Tariq anafunga goal kwa pasi ya Morisson
Seif anafunga bao la kuongoza Kwa Yanga
Dakika ya 39 Majogoro anafanya jaribio halileti matunda
Dakika ya 38 Polisi Tanzania wanapiga faulo
Dakika ya 37 Juma Abdul anapiga faulo kwa guu lake la kulia inaokolewa
Dakika ya 32 Kaheza anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 31 Niyonzima anamwaga majalo
Dakika ya 30 Morisson anachezewa faulo
Dakika ya 27 Shikalo anaanizisha mashambulizi
Dakika ya 25 Yanga inapiga Kona ya tatu Morrison ndiye anapiga inaokolewa
Dakika ya 24 Polisi wanaanzisha kwenda Kwa Yanga mashambulizi
Dakika ya 23 Niyonzima kwake Tshishimbi
 
Dakika ya 18 Nchimbi anakosa nafasi ya wazi ndani ya 18.Ndani ya dakika 15 timu zote zimecheza Kwa kujiamini na kushambuliana kwa zamu
Dakika ya 15 Kaheza anapeleka mashambulizi Yanga
Dakika ya 13 Juma Abdul alimimina majalo yakakutana na Kichwa cha Morrison kikapaa.
Dakika ya 11 mlinda mlango wa Polisi TanAnia anapewa huduma ya Kwanza baada ya kuokoa Kona iliyopigwa na Morrison


Dakika ya 05 faulo wanapiga Polisi Tanzania
Dakika ya 03 Yanga walipiga kona haikuzaa matunda.

Dakika ya 02 Tariq alifanya jaribio liliokolewa na mlinda mlango wa Polisi Tanzania
Share:

WANAWAKE KUONEANA WIVU, UWEZO MDOGO WA KUFANYA KAMPENI WAKWAMISHA WANAWAKE


Afisa Maendeleo halmashauri ya wilaya ya Kishapu Rehema Edson akizungumza kwenye warsha ya Jinsia,Uongozi na Demokrasia kwa lengo la kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika uongozi iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) iliyofanyika katika Ukumbi wa Bm Maganzo wilayani Kishapu leo Jumanne Februari 18,2020 na kukutanisha maafisa watendaji,viongozi wa serikali za mitaa wilayani Kishapu.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Maendeleo halmashauri ya wilaya ya Kishapu Rehema Edson akizungumza kwenye warsha ya Jinsia,Uongozi na Demokrasia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).
Afisa Mtendaji wa kata ya Maweja, Samsom Masele akichangia hoja kwenye warsha hiyo ambapo alisema baadhi ya wanawake wana uwezo mdogo wa kufanya kampeni za uchaguzi lakini pia wanawake wamekuwa wakioneana wivu wao kwa wao wenzao wanapoomba nafasi za uongozi.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nshishinulu kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge,Esther Lugondeka akizungumza katika warsha hiyo ambapo alisema wanawake ni jeshi kubwa hivyo wanatakiwa kupendana,kushirikiana na kuwaunga mkono wanawake wenzao wanapojitokeza kugombea nafasi za uongozi ili wapate ushindi wa kishindo. 
Diwani wa Viti Maalumu kaya ya Ukenyenge, Josephine Malima akiwashauri wanawake kujihusisha na shughuli za ujasiriamali na kujiunga kwenye vikundi mbalimbali ili kujiimarisha kiuchumi wawe na fedha zitakazowasaidia kununua vitu vidogo vidogo huku akibainisha kuwa sasa jamii imeanza kubadilika na wanawake wameanza kushirikiana badala ya kubezana wao kwa wao.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mayanji kata ya Ukenyenge, Sheikh Othman Ndamo ambaye ni Sheikh wa kata ya Kishapu akiwasilisha kazi ya kundi lake.
Afisa Mtendaji kijiji cha Mwaweja  Charles Makwaya akiwasilisha kazi yake.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Washiriki wa warsha hiyo wakifanya kazi ya kikundi.
Washiriki wa warsha hiyo wakifanya kazi ya kikundi.
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.

**
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Imeelezwa kuwa kitendo cha wanawake kuoneana wivu wao kwao pamoja na uwezo mdogo wa wanawake kufanya kampeni katika uchaguzi pamoja na unachangia wanawake kushindwa kupata nafasi za uongozi katika jamii. 

Hayo yamesemwa na wadau wa haki za wanawake leo Jumanne Februari 18,2020 kwenye warsha ya Jinsia,Uongozi na Demokrasia kwa lengo la kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika uongozi iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) iliyokutanisha pamoja maafisa watendaji,viongozi wa serikali za mitaa na Afisa Maendeleo halmashauri ya wilaya ya Kishapu iliyofanyika katika Ukumbi wa Bm Maganzo wilayani Kishapu.

Afisa Mtendaji wa kata ya Maweja, Samsom Masele alisema baadhi ya wanawake wana uwezo mdogo wa kufanya kampeni za uchaguzi lakini pia wanawake wamekuwa wakioneana wivu wao kwa wao, mmoja akijitokeza kugombea nafasi ya uongozi wanawake wenzake wanaanza kumdhoofisha na kumkatisha tamaa na kusababisha nafasi zao katika uongozi ziwe chache. 

“Wivu baina ya wanawake kwa wanawake ni mkubwa sana,wanaowakatisha tamaa ni wanawake wenzao,wabezana wao kwa wao wanasema ndiyo tuongozwe na huyu? Wanachekaa na kugongeana,hii inarudisha sana nyuma”, alisema Masele.

Aidha alisema ili wanawake waweze kushika nafasi za uongozi,wanawake wanatakiwa wapewe elimu ya upigaji kampeni na wajengewe uwezo wa kujiamini kwa kuwapa elimu na uzoefu mbalimbali pamoja na kuwashirikisha kwenye ngazi za maamuzi 

Aliitaka jamii kuachana na mtazamo hasi juu ya kauli zinazomgandamiza mwanamke ikiwemo ile ya‘Mwanamke akiwa kiongozi atakuwa malaya’ akibainisha kuwa mtu yeyote anaposhika madaraka kiongozi lazima kuna mabadiliko yanajitokeza ikiwemo mavazi. 

“Ukiwa kiongozi lazima utabadilisha hata aina ya mavazi kutokana na hali hiyo wengi wanakuona umebadilika. Kama kioo wa jamii utahitajika kuwa na mabadiliko. Ukiwa kiongozi utakutana na watu mbalimbali kutokana na kwa hali hiyo wanawake wakimuona mwanamke anakutana na wanaume wanakuwa na fikra potofu kuwawanaume zao wanachukuliwa na huyo mwanamke kiongozi”,alisema Masele. 

Naye Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nshishinulu kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge,Esther Lugondeka alisema wanawake ni jeshi kubwa hivyo wanatakiwa kupendana,kushirikiana na kuwaunga mkono wanawake wenzao wanapojitokeza kugombea nafasi za uongozi ili wapate ushindi wa kishindo. 

“Baadhi ya wanawake wamekuwa wakiwabeza wanawake wenzao wanaojitokeza kugombea nafasi za uongozi kwa sababu ya kutojua wajibu wa wanawake endapo watakuwa viongozi.Kubezwa kunasababisha baadhi ya wanawake kukata tama na kuachana na nia ya kuwa viongozi”,alisema Lugondeka. 

Mwenyekiti wa kijiji cha Mayanji kata ya Ukenyenge, Sheikh Othman Ndamo ambaye ni Sheikh wa kata ya Kishapu alisema miongoni mwa sababu zinamkwamisha mwanamke kushika nafasi za uongozi ni kutokuwa na ujuzi wa kufanya kampeni na kushawishi wapate wapiga kura. 

“Wanawake wengi hawana ujuzi wa kupiga kampeni, Wanatakiwa wapewe elimu ya upigaji kampeni ili waweze kufikia malengo yao. Lakini pia Jamii ielimishwe kuondokana na mfumo dume ili kufikia hamsini kwa hamsini na kuongeza nafasi za uongozi”,alisema Sheikh Ndamo. 

Naye Diwani wa Viti Maalumu kaya ya Ukenyenge, Josephine Malima aliwashauri wanawake kujihusisha na shughuli za ujasiriamali na kujiunga kwenye vikundi mbalimbali ili kujiimarisha kiuchumi wawe na fedha zitakazowasaidia kununua vitu vidogo vidogo huku akibainisha kuwa sasa jamii imeanza kubadilika na wanawake wameanza kuwaunga mkono wanawake wenzao.
Share:

ARTISAN-ELECTRICAL – 70 POST AT TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY LIMITED (TANESCO)

POST ARTISAN-ELECTRICAL – 70 POST POST CATEGORY(S) ENGINEERING AND CONSTRUCTION EMPLOYER TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY LIMITED (TANESCO) APPLICATION TIMELINE: 2020-02-17 2020-03-01 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.    Construct and maintain distribution lines network in accordance with the company procedures and standards; ii.    Excavate holes for poles erection to ensure they excavated according to the company standards and… Read More »

The post ARTISAN-ELECTRICAL – 70 POST AT TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY LIMITED (TANESCO) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job Vacancies at Newala District

Share:

KATIBU WA UVCCM AUAWA KWA KUNYONGWA


Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi

Jeshi la polisi mkoani Kagera limeanza uchunguzi wa kifo cha aliyekuwa katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM katika Kata ya Katoke wilayani Muleba.

Mwili wa Jaspar Jasson mwenye umri wa miaka 41, umekutwa kando kando ya barabara Asubuhi ya jana, Februari 17,2020 huku ukiwa na michubuko ya kamba shingoni.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa mwili huo umekutwa na dalili zote za kunyongwa au kujinyonga lakini kinacholeta utata ni eneo ulipokutwa, kwakuwa hakuna mti wala alama zinazoonyesha kuwa tukio limetokea katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa kamanda Malimi, baba huyo alionekana hadharani kwa mara ya mwisho Februari 16, Saa kumi na moja jioni katika kijiji cha Bisore alikohamia baada ya kutelekeza familia yake na kwenda kuishi na mwanamke mwingine na kwamba upelelezi kuhusiana na tukio hilo umeanza, huku akiwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.
Chanzo - EATV
Share:

Jobs Vacancies at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO)

On behalf of Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO); Public Service Recruitment Secretariat invites dynamic and suitably qualified Tanzanians to fill (92) vacant posts.

The post Jobs Vacancies at Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Zitto Kabwe Achukua Fomu Kutetea Tena Nafasi Yake Ndani ya Chama cha ACT Wazalendo

Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe leo Februari 18, jijini Dar es Salaam amechukua fomu ya kuomba kugombea tena nafasi hiyo kwa muhula mwingine. 

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Zitto amesema ameamua kutetea nafasi hiyo kwa awamu ya pili baada ya kushauriana na watu mbalimbali ikiwemo familia yake.

 “Nimechukua tena fomu ya kugombea uongozi wa chama katika uchaguzi utakaofanyika katika mkutano wa chama utakaoanza Machi 14 hadi 16, 2020.”

“Mimi nimeshatumikia muhula mmoja na kwa mujibu wa Katiba yetu mihula ni miwili, kwa hiyo naomba muhula huu wa pili na wa mwisho kwa mujibu wa katiba ya ACT-Wazalendo,” amesema Zitto.


Share:

Serikali Yakanusha Kuporwa Ardhi Ya Wananchi Na Viongozi Wa Umma

Na Munir Shemweta, WANMM DAR ES SALAAM
Serikali imekanusha taarifa ya kuporwa ardhi ya wananchi na viongozi wa umma kilichokuwa kiwanja NA 11 Eneo la Ununio katika Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam kama ilivyosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Akikanusha kuporwa kwa eneo hilo leo jijini Dar es Salaam mbele wa waandishi wa Habari, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo alisema taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kuporwa kwa eneo hilo siyo za kweli kwa kuwa eneo hilo lilishabatilishwa kwa mujibu wa fungu la 48 (3) la sheria ya ardhi Na 4 (1999).

Makondo aliwaasa wananchi kuipuuza taarifa hiyo kwa kuwa ina lengo la kuwachafua viongozi na kubainisha kuwa, kwa mujibu wa sheria ya ardhi namba 4 (1999) Kamishna wa Ardhi anayo mamlaka kisheria kumilikisha ardhi kwa Mtanzania yoyote aliyetimiza masharti kisheria.

Akifafanua kuhusiana na suala hilo Kamishna wa Ardhi Nchini Mathew Nhonge alisema eneo linalodaiwa kuporwa lilipimwa kwa mara ya kwanza mwaka 1988 na kuitwa kiwanja namba 11 eneo la Ununio.

Nhonge alisema, mwaka 1988 Manispaa ya Kinondoni ilimilikisha kiwanja hicho kwa Ndg Goodfreid  Kajana Makaya na kupewa Hati NA 43711 ambapo baadaye kulijitokeza malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wakidai kuwa ni wenyeji wa eneo hilo akiwemo Ramadhani Mwinyihamisi, Waziri Kibosha na Bi Kijakazi Maulid.

Kamishana huyo wa Ardhi nchini alibainisha kuwa, malalmiko hayo yalisababisha mgogoro uliofikishwa Makahakama kuu Kitengo cha Ardhi  kupitia Shauri la Ardhi NA  93/2004 baina ya Bi Kijakazi Maulid dhidi ya mmiliki halali Ndg Goodfreid Kajana Makaya ambapo hata hivyo shauri hilo lilitupiliwa mbali na Mahakama hiyo baada ya Bi. Kijakazi kushindwa kuthibitisha madai yake.

Nhonge aliongeza kwa kusema, mwaka 2007 Ndg Goodfreid Kajana Makaya alihamisha umiliki wake kisheria kwa kuiuzia Kampuni ya Shamiana Builders Limited aliyoieleza kuwa nayo ilishindwa kutekeleza masharti ya uendelezaji kama ilivyoelelekezwa kwenye hati miliki na hivyo kusababisha haki ya umiliki kufutwa mwaka 2017 na serikali kwa mujibu wa fungu la 48 (3) la sheria ya ardhi Na 4 (1999).

Kufuatia hali hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ililipanga na hatimaye kulipima upya eneo hilo na takribana viwanja 22 vilipatikana na kumilikishwa kwa wananchi mbalimbali wakiwemo wakazi wa Uninio ambao maombi yao ya kumilikishwa yaliwasilishwa serikalini.


Share:

Breaking : ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA CHADEMA DK. VICENT MASHINJI AHAMIA CCM


Aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amejiunga na CCM leo Jumanne Februari 18, 2020 na kupokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM nchini Tanzania, Humphrey Polepole katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es salaam.
Share:

Taifa Stars Yatupwa Kundi D Fainali Za Chan 2020

Droo ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN 2020 imepangwa usiku wa jana, Februari 17, 2020 mjini Yaounde nchini Cameroon.
 
Katika droo hiyo, imeshuhudiwa timu 16 zikipangwa katika makundi manne yenye timu nne, ambapo Cameroon ambao ni wenyeji wa michuano hiyo, wakipangwa katika kundi A pamoja na timu za Mali, Burkina Faso na Zimbabwe.

Kundi B likiwa na timu za Libya, DR Congo, Congo Brazzaville, Niger na kundi C likihusisha timu za Morocco, Rwanda, Uganda, Togo.

Taifa Stars ambayo inayoshiriki michuano hiyo kwa mara nyingine ya pili tangu ilipofanya hivyo mwaka 2009 nchini Ivory Coast, imepangwa kundi D pamoja na timu za Zambia, Guinea na Namibia.

Kundi la awamu hii la Taifa Stars linaonekana kuwa ni jepesi kulinganisha na kundi ambalo alipangwa katika CHAN 2009, akipangwa na timu za Senegal, Zambia na wenyeji Ivory Coast. 

Taifa Stars iliondolewa katika hatua ya makundi baada ya kushinda mechi moja dhidi ya Ivory Coast na kufungwa mechi moja dhidi ya Senegal pamoja na sare moja na Zambia.

Zambia na Tanzania zinakutana tena katika michuano hiyo, hivi sasa timu zote zikiwa na kizazi kingine cha soka. 

Michuano hiyo itafanyika kuanzia Aprili 4-25, 2020.


Share:

NG'OMBE 1,400 WALIOAMRIWA NA MAHAKAMA KURUDISHIWA WAFUGAJI SIMIYU WAFA NDANI YA PORI LA AKIBA LA MASWA

WANANCHI wa Kijiji cha Mwangudo wilayani Meatu mkoani kinachopakana na Hifadhi ya Jamii ya Makao pamoja na Pori la Akiba la Maswa wakisalimiana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina aliyefika kijijini hapo kutangaza maamuzi yaliyotolewa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kuhusiana na matumizi ya mita 500 kando mwa hifadhi hiyo kutumika kwa shughuli za malisho ya mifugo. Picha na Mpiga Picha

 NA MWANDISHI WETU, SIMIYU

ZAIDI  ya ng’ombe 1, 400 wa wafugaji wa Wilaya za Itilima na Meatu mkoani Simiyu wamekufa mikononi mwa Maafisa wa Pori la Akiba la Maswa baada ya kushikiliwa  hifadhini  kwa kipindi cha miaka mitatu bila kupatiwa  huduma muhimu za chanjo, dawa, maji na malisho licha ya Mahakama kutoa hukumu kwa wamiliki kurejeshewa mifugo yao.

Wafugaji hao wamesema tangu mwaka 2017 ng’ombe 1, 484 walikamatwa kwa madai kuwa walikuwa ndani ya pori hilo na kwamba licha Mahakama kuamuru warudishiwe ng’ombe wao bado waliendelea kushikiliwa na kuendelea kufa na kubaki 72 na kuwasababishia umasikini mkubwa.

Wafugaji hao walifikisha kilio hicho kwenye mikutano wa hadhara ilioitishwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina aliyefika katika vijiji vya Laini A na Laini B wilayani Itilima, Mwangudo na Malwilo Wilayani Meatu mkoani Simiyu ambapo walisema licha ya Mahakama kutoa uamuzi wafugaji hao warejeshewe mifugo bado hawajarudishiwa mifugo yao hadi sasa na kwamba inadaiwa kuwa mifugo hiyo imekufa.

Baadhi ya Wamiliki  wa mifugo hiyo ni walioshinda kesi kwa upande wa Itilima  ni Malimi Sendama, Ngasa Mbeho, Kongwa Tulutu na Maduhu Mbuli ambapo walimkabidhi Waziri Mpina risiti mbalimbali zinazoonesha mifugo hiyo kuuzwa kwa bei ya kutupa huku ngombe anayetakiwa kuuzwa laki 4 hadi 5 akiuzwa sh laki 1.

Wafugaji wengine kwa upande wa Meatu waliodhulumiwa ng’ombe 345 ni Subi Maduhu, Masunga Muhamali, Zengo Kusekelwa, Kija Badila ambapo mifugo yao inadaiwa kufa huku mfugaji mwingine akidai ngombe wake 55 ambao Mahakama iliamuru alipe faini ya shilingi milioni 1.4 ili arudishiwe mifugo yake na alilipa faini hiyo lakini mifugo yake haijarudishwa hadi sasa.

Akiwasilisha kilio kwa niaba ya wafugaji hao, Katibu wa Mbunge wa Itilima, Alex Ngulukulu alisema wahifadhi hao walitoa maelezo kuwa ng’ombe 289 wamekufa jambo ambalo sio la kweli kwani askari wa hifadhi walikuwa wanaendesha minada ya kuuza mifugo hiyo.


“Ng’ombe walikuwa wanauzwa kwenye minada wakati kesi ikiendelea mahakamani na tuna ushahidi wa kutosha wa risiti zote walizokuwa wanatoa kwa wanunuzi wa mifugo hiyo” alisema Alex.

Diwani wa Kata ya Tindabuligi, Tabu Maghembe alisema maelezo yaliyotolewa kwamba mifugo hiyo imekufa hawakubaliani nayo kwani hakuna mlipuko wowote wa magonjwa ulioripotiwa katika kipindi hicho na hivyo kumuomba  Waziri Mpina kufikisha kilio hicho cha wafugaji wa Itilima na Meatu kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli ili aingile kati waweze kupata haki yao kwani kwa muda mrefu amekuwa akipigania haki za wanyonge.

Mbali na malalamiko hayo pia wafugaji hao walilalamikia kitendo Maofisa wa Pori la Akiba Maswa kutanua mpaka bila kuwashirikisha wananchi na hivyo kuendelea kupunguza eneo la malisho na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wafugaji. Pia wananchi wa Wilaya za Wilaya za Maswa na Meatu wamelalamikia mgogoro wa mpaka katika Ziwa Kitangiri na kwamba wamekuwa wakizuiliwa kuvua na kukamatwa kwamba wameingia wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Juma Mpina amshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kuruhusu matumizi ya mita 500 kutoka kwenye Pori la Akiba la Maswa yatumike kwa shughuli za kulishia mifugo sambamba na kuruhusu matumizi ya mita 60 kutoka kwenye mto kutumika kwa shughuli za akunyesha maji mifugo yao jambo ambalo hapo kabla wananchi walikuwa wakizuiliwa na kusababisha mifugo mingi kufa kwa kukosa maji na malisho.

Akizungumza baada ya malalamiko hayo Waziri Mpina aliwaagiza Wakuu wa Wilaya za Itilima na Meatu kuitisha kikao cha pamoja kitakacho mhusisha Mhifadhi Mkuu wa Pori la Maswa, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Tanzania na Mwanasheria wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wafugaji wanaolalamikia kudhulumiwa mifugo yao na kupitia vielelezo vyote vilivyotumika kukamata, kutunza na kuuza mifugo pamoja na kupitia hukumu ya Mahakama ili haki iweze kutendeka .

Pia ameagiza Kamishna wa Ardhi, Mkurugenzi wa Uvuvi Tanzania, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meatu na Mkurugenzi wa Iramba ili kupitia upya mipaka hiyo na kumaliza kabisa mgogoro huo kuhusu uvuvi katika Ziwa Kitangiri

Kuhusu suala la kutanua mpaka kiholela, Waziri Mpina ameagiza timu ya Wataalamu kutoka Wizara nane kupita kwenye maeneo yanayolalamikiwa na kupima upya mipaka hiyo kwa uwazi na kwamba wananchi watashiriki katika zoezi hilo. Aidha kuhusu upungufu wa maeneo ya malisho vijiji saba vinavyounda WMA ya Makao, Waziri Mpina aliagiza wafanye tathmini ya mahitaji ya ardhi ya wananchi kwa sasa na kuandaa GMP itakayoruhusu baadhi ya maeneo kutumika kwa ajili ya kulishia mifugo.

Hivyo Waziri Mpina ameagiza wafugaji wote mkoani Simiyu walioshinda kesi mahakamani na kutakiwa kurejeshewa mifugo yao kuwasilisha vielelezo vya hukumu za kesi hizo kwenye ofisi za Wakuu wa Wilaya za Itilima na Meatu ili haki iweze kutendeka. Mbali na hayo Serikali imetenga zaidi ya shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuangamiza wadudu aina ya mbung’o katika vijiji vyote vinavyopakana na WMA Makao na maeneo mengine nchini ili kutokomeza kabisa mdudu huyo hatari kwa mifugo.
Share:

BREAKING : Zitto Kabwe Akutwa Na Kesi Ya Kujibu

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT – Wazalendo) Zitto Kabwe amekutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka matatu ya uchochezi yanayomkabili katika Mahakama ya Kisutu.

Zitto amepewa siku nne kuanzia tarehe 17 Machi-20 Machi 2020 kuwasilisha ushahidi wake wa utetezi. 

Hivyo, Kesi hiyo itaanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Machi 17, 18, 19 na 20, 2020


Share:

Watoto wafariki kwa kula vitafunwa vilivyopikwa kwa dawa ya kuulia wadudu

Watoto wawili nchini Uganda wameaga dunia huku wengine 11 wakipelekwa hospitali baada kula kitafunwa aina ya chapati kilichotengenezwa kwa sumu ya kuuwa wadudu badala ya mafuta, gazeti la Daily Monitor linaripoti.

Watoto wote 13 wanatoka familia moja Budumba, magharibi mwa Uganda na  kwamba wana umri wa 5 na 6.

Gazeti hilo limeripoti kwamba watoto hao walijipikia wenyewe vitafunwa hivyo ambavyo vinafahamika kama Kabalagala.

Watoto hao inasemekana kwamba miongoni mwa viambato walivyotumia wakati wanapika ilikuwa dawa ya kuua wadudu inayonyunyizwa kwenye matikiti maji na mbogamboga zinazokuzwa wakidhani kwamba ni mafuta.

Kulingana na gazeti hilo, watoto hao walianza kutapika na kupelekwa hospitali ya Busolwe ambapo wawili wao waliaga dunia huku wengine 11 wakiendelea kupata matibabu.

Mkuu wa polisi wa eneo hilo, Ceasar Tusingwire alithibitisha tukio hilo.

"Watoto 13 kutoka familia moja wanashukiwa kwamba wamekula chapati zenye sumu. Walichanganya dawa ya kuua wadudu na mafuta ya kupikia kwa bahati mbaya," ameeleza bw Tusingwire.

"Walionusurika wanaendelea vizuri lakini bado hawajapa nguvu. Tunajitahidi kuhakiksha watoto wamerejea katika hali yao ya kawaida, mhudumu mmoja wa afya amesema hivyo.

Polisi imesema miili ya waliokufa inafanyiwa uchunguzi na kuongeza kwamba  upelelzi wa tukio hilo unaendelea.

Credit:BBC


Share:

Wawili Kortini Kwa Kujilawiti na Kusambaza Picha za Ngono

Watu wawili jana February 17, 2020 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo kulawiti na kusambaza picha za ngono mtandaoni.

Washatakiwa hao wakazi wa DSM ni Aisha Juma (Video Vixen) na Mfanyabiashara Samwel Philemon 

 Aisha anadaiwa kusambaza video za ngono December 12,2019 katika maeneo tofauti Dar na Samwel katika siku isiyojulikana na mahali pasipo julikana anadaiwa kumuingilia Aisha kinyume na maumbile huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Hakimu Chaungu ametoa masharti ya dhamana ya Tsh. Million 10 ambapo washtakiwa hao wameshindwa kutimizia, kesi imeahirishwa hadi February 26,2020 na washtakiwa wote wamerudishwa mahabusu.


Share:

Serikali Yatoa Elimu Kwa Wachimbaji Wa Dhahabu Juu Ya Madhara Ya Matumizi Ya Zebaki Ili Kulinda Afya Zao

Na Robert Hokororo, Singida
Wakati Serikali inaendelea kuweka utaratibu wa kupata mbadala wa matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu imeshauri watumie vifaa vinavyowakinga wakati wakifanya shughuli hizo.
 
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima wakati akizungumza na wachimbaji wadogo kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Sambaru wilayani Ikungi na Londoni wilayani Manyoni mkoani Singida.
 
Sima alisema kuwa Serikali inaendelea na kuwapa elimu wachimbaji hao katika maeneo mbalimbali nchini ili waweze kuepuka madhara ya kiafya yanayotokana na kemikali hiyo.
 
“Tanzania tuliridhia Mkataba wa Minamata mwaka jana unaotaka kupunguza ama kuondoa kabisa matumizi ya zebaki kwa ninyi wachimbaji ili kuwaepusha madhara ya kiafya na kimazingira katika maeneo yenu,” alisema naibu waziri.
 
Akiwa katika ziara hiyo ambapo alitembela kuona shughuli za uchimbaji na kukagua namna wanavyotunza mazingira, Sima alisema kuwa jukumu la Serikali ni kutoa elimu juu ya madhara ya zebaki ili kulinda afya za wachimbaji wadogo.
 
 “Niwaahidi tu tutashirikiana na Ofisi ya Madini ili muweze kupata vifaa maalumu vya kujikinga wakati wa kuchenjua badala ya mikono, tutawaletea gloves mvae mikononi na musk wakati tunachoma ili kufunika pua kwani kemikali hii ina madhara kiafya,” alisema.
 
Aidha, Naibu waziri aliwataka wachimbaji hao kuacha kukata miti wakati wa shughuli za uchimbaji wa dhahabu na badala yake wawe na utamaduni wa kutumia njia mbadala kama ambavyo wanavyoelekezwa na mamlaka zinazohusika.
 
Aliongeza kuwa jukumu la Ofisi ya Makamu wa Rais na Serikali kwa ujumla ni kuhakikisha nchi inakabiliana na changamoto ya mabadilkko ya tabianchi na hivyo kuleta athari.
 
Alisema tunapoendelea kuchoma na kukata miti ovyo, kulima kholela na kuchimba mashimo ovyo kwa ajili ya madini ni mambo yanayosababisha mvua isije kwa wakati pamoja na jua kuwa kali kuliko kawaida.


Share:

Mwanajeshi Kortini Kwa Kumuua Mwanajeshi Mwenzake Kwa Risasi 19

Askari wa JWTZ Wilayani Nachingwea, Lindi Pascal Lipita(28), amefikishwa Mahakamani akituhumiwa kumuua kwa kumpiga risasi Askari mwenzake ambaye ni Mpenzi wake Baserisa Ulaya.

Mtuhumiwa huyo alifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa huo, Maria Batulaine, na kusomewa shtaka linalomkabili.

Mwanasheria wa Serikali, Abdulrahman Mohamed, alidai kuwa askari hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kwamba wivu ndio unaodaiwa kusababisha mauaji hayo.

Mwanasheria huyo wa serikali alidai kuwa mshtakiwa alifanya mauaji hayo Februari 10, mwaka huu, majira ya Saa 12;00 jioni wakiwa kambi ya Nang’ondo.

Alidai kuwa siku hiyo ya tukio, wakiwa kambini hapo, mshitakiwa akiwa na silaha, alimmiminia askari mwenzake risasi 19 kisha kuchakaza mwili wake na kumkatisha uhai.

Mshtakiwa amerejeshwa rumande na atarudi tena Makamani March 02, 2020 kesi itakapotajwa.


Share:

Zitto Kabwe Arejea Nchini

Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo Zitto Kabwe amewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jana Jumatatu February 17, 2020 akitokea ziarani katika mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani na Uingereza ambapo amesema ziara yake imekuwa ya mafaniko makubwa.

Akizungumza baada ya kuwasili  amedai kuwa bado hana hofu ndio maana amerudi nchini

“Sina hofu na ndio maana nimerudi bila shida yoyote kwa sababu hamna kosa lolote nimefanyana ,nitaendeea kufanya shughuli zangu kama kawaida,.” alisema 

Aidha, Zitto alisema kwa sasa chama chake kiko kwenye mchakato wa uchaguzi na anatafakatri kuwa anachukua fomu ya kugombea nafasi gani ndani ya chama hicho

Hivi karibuni  Zitto Kabwe alitupiwa lawama nyingi na wabunge mbalimbali katika mkutano wa 18 wa Bunge uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma kwa kitendo chake cha kuiandikia barua Benki ya Dunia (WB) akitaka isiidhinishe mkopo wa Sh1.2 trilioni kwa Tanzania kwa ajili ya sekta ya elimu.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger