Vyombo vya Usalama nchini vimeonywa kutowaonea Wananchi kwa kuwashitaki kama Wazururaji, wakati wana shughuli zao kufanya.
Onyo hilo limetolewa na Rais John Magufuli ambaye amesisitiza kuwa, yeye hawatetei Wazururaji, na kama kweli kuna Mzururaji sheria ziko wazi kwa ajili ya kumshitaki na wala sio kumnyanyasa.
Rais Magufuli ametoa onyo hilo akiwa njiani kuelekea jijini Dodoma, baada ya baadhi ya Wakazi wa mkoa wa Morogoro kudai kuwa, wamekua wakikamatwa na vyombo vya Usalama kama Wazururaji wakati wana shughuli zao za kuwaingizia kipato.
"Vyombo vya usalama ambavyo vinadili na hawa wazururaji, wasiwaonee watu, Umemkuta anauza mahindi ndio yake, unamshika unamuambia mzururaji, haya ya uonevu yasiwepo" -Rais Magufuli.
"Vyombo vya usalama ambavyo vinadili na hawa wazururaji, wasiwaonee watu, Umemkuta anauza mahindi ndio yake, unamshika unamuambia mzururaji, haya ya uonevu yasiwepo" -Rais Magufuli.
Amerejea kauli yake ya kutaka kutobughudhiwa kwa Wafanyabiashara wadogo ambao wamekua wakihangaika kufanya shughuli mbalimbali ili kujiingizia kipato.
Pia Rais Magufuli amesisitiza kuwa, wakati akiomba ridhaa ya kuongoza nchi, aliahidi kulinda haki za Watanzania wote na kuhakikisha sheria zinafuatwa, hivyo hatoruhusu mtu ama chombo chochote kuvunja sheria na kumuonea mwingine.