Wednesday, 20 November 2019

Tanzania Ina Utoshelevu Wa Chakula Cha Ziada Takriban Tani Mil.2.5 Sawa Na Asilimia 109%

...
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
SERIKALI imesema kwa sasa nchi ina utoshelevu wa chakula cha  ziada takriban tani milioni 2.5 sawa na asilimia 109%   ambapo katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Julai hadi Septemba imeuza tani za mahindi elfu 84.5 nje ya nchi.
 
Akifungua mkutano wa kupokea tafiti kuhusu kuimarisha usalama wa chakula ndani na nje ya Nchi  Nov,19,2019  jijini Dodoma,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Profesa  SIZA TUMBO amesema pia katika kipindi cha miezii mitatu Mihogo tani elfu tano ilipelekwa nchini Burundi na tani elfu 2000 za Mtama zilipelekwa nje ya nchi.
 
Aidha Profesa TUMBO amesema kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Benki ya Dunia tayari Tanzania imeshafikia kwenye uchumi wa kati.

Kwa Upande wake,Mkuu wa Idara ya Ushauri Elekezi kutoka Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) VIVIAN KAZI Kazi amesema  utafiti huo una malengo sita ikiwemo kuboresha uzalishaji wa taarifa ili kuhamasisha mauzo ya mazao ndani na nje ya nchi.

ESRF ilianzishwa mwaka 1994 kama taasisi ya utafiti ikiwa imejikita kufanya kazi zake katika kutoa ushauri elekezi  wa kisera katika nyanja za uchumi na jamii ndani na nje ya nchi na imefanya utafiti huo kwa kushirikiana na ofisi ya Rais TAMISEMI,Uvuvi na Mifugo,Viwanda na Biashara,Kilimo na Ofisi ya Taifa ya Takwimu.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger