Friday, 8 November 2019

Jafo akemea viongozi wanaotoa matamko ya kuhatarisha Amani kipindi hiki cha chaguzi wa Serikali za Mitaa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amekemea wadau wa siasa wanaotoa matamko ya kuhatarisha amani katika kipindi hiki ambacho chaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utahitimishwa Tarehe 24/11/2019.

Mhe. Jafo ameyasema hayo Mkoani Njombe alipokua akizungumza na kamati ya Ulinzi na usalama, kamati ya rufaa na wasimamizi wa uchaguzi pamoja na baadhi ya watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Njombe.                     

Alisema baadhi ya wadau wa siasa wanatoa matamko ya kuhatarisha amani ya Nchi sidhani kama ni busara kutamkia Nchi yako maneno mabaya ya kukatisha tamaa, kuvunja mioyo na kutishia amani ingependeza zaidi kama kila mmoja wetu angetekeleza jukumu lake la kisiasa na wakati huo huo kulinda amani ya Nchi.

“Kama mtu anaona ameonewa katika mchakato wowote wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kamati za Rufaa zipo apeleke malalamiko yake huko akiona hayajashughulikiwa ndipo anaweza kutoa lawama:

Cha ajabu ni kuwa watu hawajapeleka malalamiko yao kwenye Kamati ya Rufaa wanalalamika maeneo ambayo si stahiki hivi hawajitendei hako maana Kanuni imeelekeza wapi pa kwenda endapo umeona umedhulumiwa haki yako” alisema Jafo.

Kama watu wameenguliwa kwenye kinyang’anyiro wanastahili waende kwenye Kamati ya Rufaa waone kama malalamiko yao yatashughulikia au lah; nashauri wadau wote wa siasa kufuata Kanuni za Uchaguzi ili zoezi likamilike kwa amani.

Halkadhalika Mhe. Jafo alizitaka Kamati za Rufaa kuhakikisha wanawatendea haki wale wote watakaowasilisha malalamiko yao kwenye Kamati hizo.

“Huu Ndio muda  pekee  wa Kamati ya Rufaa   kuonyesha umahiri wenu katika zoezi hili na kuweka sawa mambo yote ambayo hayakwenda sawa na kusababisha malalamiko”

Aliongeza kuwa Kamati za Rufaa msibanwe na chama chochote wala maelekezo ya aina yeyote fanyeni kazi hii kwa misingi ya sheria iliyowekwa tendeni haki stahiki kwa kila mlalamikaji hatimaye mpate ufumbuzi wa malalamiko yote yatakayowasilishwa aliongeza Jafo.


Share:

Waziri Wa Kilimo: Tunakaribisha Wawekezaji Kwenye Zao La Korosho

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza katika Tasnia ya Korosho nchini Tanzania ili kutumia vyema fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo kuwekeana katika viwanda vya korosho.

Katika kipindi kirefu serikali imekuwa ikiuza korosho ghafi jambo ambalo nitapunguza kipato cha wananchi na pato la serikali hivyo kuagiza wafanyabiashara kuwekeza kwenye viwanda vya korosho.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 7 Novemba 2019 wakati akifungua mkutano wa 13 wa shirikisho la wadau wa korosho Afrika (ACA) unaofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam.

Waziri Hasunga amesema kuwa kwa sasa uwezo wa ubanguaji wa korosho ghafi nchini ni tani 50,000 ambayo ni sawa na takribani asilimia 20 ya uzalishaji wa korosho ghafi msimu wa 2018/2019.

Amesema uwezo huo ni mdogo ikilinganishwa na uzalishaji uliopo sasa na hivyo nchi inapoteza fursa ya ajira viwandani hususani kwa wanawake na vijana, kukosa mapato yanayotokana na bidhaa zilizoongezwa thamani kama vile mafuta ya ganda la korosho (Cashewnut Shell Liquid), vyakula vya mifugo na kupanua wigo wa soko la korosho.

Amesema kwa sasa kuna jumla ya viwanda 25 vya ubanguaji korosho nchini vyenye uwezo wa kubangua tani 78,000 kwa mwaka. Kati ya hivyo, ni viwanda 12 vyenye uwezo wa kubangua tani 24,660 ndivyo vinavyofanya kazi hivyo kuna fursa kubwa ya uwekezaji kwenye viwanda vya ubanguaji korosho.

Aidha, Waziri Hasunga amesema kuwa kwa upande wa wabanguaji wadogo wa korosho nchini kupitia umoja wao (UWWKT) wameendelea kuimarisha Umoja wao kwa lengo la kuongeza kiasi cha korosho kinachobanguliwa nchini.

Mpaka sasa kuna jumla ya vikundi 209 vidogo vya kubangua korosho nchini kutoka Wilaya 14. Katika msimu wa 2018/2019 vikundi hivi vimefanikiwa kubangua korosho tani 78 tu. Ukosefu wa mitaji, mashine za kubangua korosho, na masoko ya uhakika ni baadhi ya changamoto zinazokabiliwa na wabanguaji katika kundi hili.

Kwa ujumla Serikali kupitia Taasisi zake inaendelea kusimamia mikakati iliyopo ya kuongeza uzalishaji wa korosho ghafi kufikia wastani wa tani 1,000,000 ifikapo mwaka 2023/2024.

Mikakati hiyo ni pamoja na kupanda mikorosho mipya 15,000,000 kila mwaka kuanzia mwaka 2019/2020 hadi 2023/2024, kuanzisha mashamba mapya ya kuzalisha mbegu bora za korosho hususani katika maeneo mapya ya kilimo cha korosho, Kutoa elimu ya ugani kwa wakulima juu ya kilimo bora cha korosho ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi na salama ya viuatilifu vya zao la korosho na kuhakikisha upatikanaji wa uhakiki na wa bei nafuu wa viuatilifu vya zao la korosho kwa wakulima.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyataja maeneo ambayo yapo wazi kwa ajili ya uwekezaji katika Tasnia ya Korosho hapa nchini ni pamoja na; Ubanguaji wa korosho ikiwa ni pamoja na usindikaji wa bidhaa zitokanazo na korosho; Ufunguaji wa mashamba makubwa ya korosho (Cashewnut plantations/Block farming); Usambazaji na uuzaji wa mashine za kubangua korosho; Uwepo wa ardhi ya kutosha iliyotengwa katika mikoa inayozalisha korosho kwa wingi kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya kubangua korosho; Uwepo wa sera ya viwanda katika ngazi ya Taifa.

Mhe Hasunga amesema kuwa Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazozalisha korosho ghafi yenye ubora wa hali ya juu. Korosho ya Tanzania inapendwa katika masoko mbalimbali ya Kimataifa kutokana na kuwa na ladha nzuri na ya kuvutia, rangi nyeupe ya asilia ya korosho karanga na ukubwa unaofanana (Uniform size); sifa inayopunguza gharama ya kudarajisha kabla ya kubanguliwa. Pia, faida ya kijiografia (Geographical Advantage) ya kuwahi kwa msimu wa korosho nchini miezi 6 kabla ya nchi nyingine duniani zinazozalisha korosho kwa wingi hazijaingia sokoni.

Sifa hizo pamoja na usimamizi mzuri wa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani ndio kimsingi imepelekea kuimarika kwa bei ya korosho ghafi za wakulima kutoka mwaka 2007/2008 hadi mwaka 2017/2018, ambapo bei ya korosho ghafi imekuwa ikiongezeka  na kufikia ya juu kuwahi kupatikana ya Shilingi 4,128/= kwa kilo katika msimu wa 2017/2018.

Zao hili huzalishwa kwa wingi hapa nchini kutoka mikoa mitano ambayo ni mikoa ya Kusini ya Mtwara, Lindi na Ruvuma na mikoa ya Mashariki ambayo ni Pwani na Tanga. Kutokana na faida za kiuchumi zitokanazo na zao la hili, uwepo wa eneo la kutosha kwa kilimo na hali ya hewa maridhawa kwa kilimo cha korosho hapa nchini zao hili kwa sasa linalimwa na zaidi ya mikoa 17 ikiwemo Singida, Mbeya, Dodoma, Morogoro, Songwe, Njombe, Iringa, Katavi, Tabora, Kigoma, Shinyanga na Kilimanjaro.

MWISHO



Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa November 8





















Share:

Thursday, 7 November 2019

MCHEKESHAJI MAARUFU NJENGA MSWAHILI AFARIKI DUNIA


Mchekeshaji aliyekuwa akishiriki shoo ya Churchill Njenga Mswahili amefariki dunia. 

Mwili wa Njenga umepatikana Alhamisi, Novemba 7,2019 eneo la Daforeti South, katika Soko la Ndonyo nchini Kenya na inadaiwa aligongwa na treni. 
Share:

Serikali Inatambua Mchango Wa Wazee Waliotumika Katika Ukombozi Wa Nchi Na Ujenzi Wa Taifa

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Sima   amesema kuwa Serikali inatambua michango ya watu mbalimbali walioshiriki katika ukombozi na Nchi yetu na ujenzi wa Taifa ikiwa ni pamoja wazee wetu walioshiriki katika tukio la kuchanganya udongo tarehe 26 Aprili, 1964.
 
Ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mheshimiwa Fakharia Shomar Khamis (Mb.) lililouliza Je, Serikali inawaangalia vipi wazee wetu  wane walioshiriki katika kuchanganya udongo siku ya Muungano mwaka 1964, kwa kuwapa asante baada ya utu uzima kuwafikia.
 
Naibu Waziri aliongeza kuwa  Kundi hili ni moja kati ya makundi mengi yaliyotoa mchango wa hali na mali katika kulijenga Taifa hili ikiwemo wastaafu na walioshiriki katika Vita vya Kagera. Hata hivyo, kwa sasa hakuna sheria mahsusi ya asante au malipo kwa watu waliofanya mambo makubwa yanayojenga historia ya Nchi. 
 
“Kuwashirikisha Wazee hawa katika maadhimisho ya sherehe za Muungano ni sehemu ya kutambua mchango wao na kukumbuka tukio muhimu la uchanganyaji wa udongo wa Tanganyika na Zanzibar. Ushiriki wao huwezeshwa na Ofisi ya Makamu wa Rais. Aidha, pamoja na wazee hawa, yapo makundi mengine ya wazee ambao kwa namna moja au nyingine walitoa mchango wao katika ujenzi wa Taifa ambao pia hualikwa kushiriki katika maadhimisho hayo mfano Viongozi Wastaafu na Wanasiasa Wakongwe” alisema Waziri Sima.

Aidha Naibu Waziri Sima akijibu swali la Mh Jaku Hashim Ayoub (B.L.W) lililouliza Kwa mujibu taarifa rasmi ya Serikali Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) iliyotolewa mwaka 2014, Kisiwa cha Latham (Fungu Mbaraka) ni mali ya Zanzibar tangu kilipotangazwa rasmi mwaka 1898. Hata hivyo zipo taarifa zilizothibitishwa kuwa Serikali ya Muungano kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu iliiandikia SMZ kuwataarifu kwamba Kisiwa hicho ni cha Tanzania Bara:- 
 
 Je, Serikali hizi mbili ambazo ni ndugu wa damu watakaa kutatua kero hii ya muda mrefu; na Je, Serikali haioni kuwa umefika muda muafaka kulifanyia kazi suala hilo.

Waziri Sima alisema kuwa Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na sheria ya mabadiliko ya Katiba sura ya 83 Ibara ya 2 (1) inatamka wazi kuwa eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni eneo lote la Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar pamoja na sehemu ya bahari ambayo imepakana na nchi za Kenya, Shelisheli, Comoro na Msumbiji. Hivyo basi, kwa mujibu wa tafsiri ya mipaka hiyo, Kisiwa cha Latham (Fungu Baraka) kiko ndani ya eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na pia hakuna mgogoro wa umiliki wa eneo la kisiwa hicho kwa vile kimo ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Share:

Tanzania Yapunguza Uingizaji Wa Dawa Za Kulevya Aina Ya Heroin Kwa Asilimia 90%.

Na,Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kwa  mujibu wa Shirika la Kimataifa  la kupambana na dawa za kulevya na Uhalifu[UNODC],Tanzania ilipunguza uingizaji wa dawa za kulevya aina ya Heroin  kwa asilimia 90% .
 
Hayo yamesemwa  Nov.6,2019  na Waziri wan chi,Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera,Bunge ,kazi,vijana ,Ajira  na watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama wakati akizungumza na Waandishi wa Habari bungeni jijini Dodoma mara baada ya kuwasilisha  bungeni Taarifa ya Hali za Dawa za Kulevya  ya mwaka 2018.
 
Mhe.Mhagama amesema pamoja na jitihada zilizofanywa na serikali katika kupambana na dawa za kulevya ,bangi imeendelea kuwa tatizo hapa nchini ambapo ametaja mikoa ambayo imeonekana  kuathirika zaidi na kilimo cha bangi ni pamoja na Mara,Tanga,Morogoro,Arusha,Kagera na Ruvuma huku pia Mirungi ikiendelea kutumiwa na watu wa rika hapa nchini.
 
Aidha,Mhe.Mhagama amesema kwa kipindi cha mwaka 2018 juhudi ya vyombo vya dola kwa kushirikiana na wananchi zilifanikiwa ukamataji wa tani 24.3 za bangi zikiwahusisha watuhumiwa 10,061 na tani 8.97 za mirungi  zikiwahusisha watuhumiwa  1,186.
 
Katika kipindi cha Mwaka 2018 jumla ya kesi 7,593 zikiwa  na jumla ya watuhumiwa 10,979  zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini huku jumla ya kesi 7,174 zilizowahusisha watuhumiwa 11,045 ziliendelea   kusikilizwa.
 
Pia,Mhe.Mhagama amesema serikali imeendelea kutoa huduma  za tiba  kwa watumiaji wa dawa za kulevya  ambapo jumla ya vituo 6 vilivyopo katika mikoa ya  Dar Es Salaam,Mwanza,Mbeya,na Dodoma viliendelea kutoa huduma   na hadi kufikia mwaka 2018 ,zaidi ya watumiaji elfu nane[8000] waliendelea kupatiwa huduma za Methadone  katika vituo husika.
 
Hivyo,Waziri Mhagama ameendelea kufafanua serikali itaendelea kuimarisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya huku akivipongeza vyombo vya habari pamoja na wadau mbalimbali kwa kuendelea kusisitiza madhara ya dawa za kulevya kwa Taifa la Tanzania.

Kwa upande wake kamishna wa Kinga na tiba kutoka Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya  nchini Dokta Peter Mfisi amesema bei ya dawa ya kutibu waathirika wa dawa za kulevya [methadone] inanunuliwa kwa Soko la India kati ya dola 650 hadi dola 700 na kilo moja ya Methadone inawezakuhudumia watu 650 mpaka 700.


Share:

Serikali Yawahakikishia Ushirikiano Wanunuzi Wakubwa Wa Tanzanite

Na Asteria Muhozya, Kilimanjaro
Serikali imewahakikishia Ushirikiano Wanunuzi Wakubwa wa Madini ya Tanzanite kutoka nchi za Marekani na Canada ambao Novemba 6, 2019, walihitimisha ziara ya siku tano nchini.
 
Ziara ya wanunuzi hao wakubwa ililenga kuona eneo ambalo madini hayo adhimu yanapozalishwa, kuona namna shughuli za uchimbaji zinavyofanyika, uzalishaji, uthamini, shughuli za uongezaji thamani madini hayo zinavyofanyika pamoja na masuala mengine yanayohusu madini ya tanzanite.
 
Akizungumza katika halfa fupi ya kuuaga ujumbe huo iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa KIA, Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kuwa, ujumbe huo ndiyo wanunuzi wakubwa wa mwisho wa tanzanite yote duniani ambapo wananunua asilimia 75 hadi 80.
 
Ameongeza kwamba, wizara kwa upande wake imefurahishwa na ujio wa ujumbe huo kwa kuwa ni fursa ambayo itasaidia kutangaza madini ya tanzanite na mahali inapotoka na hivyo kuliwezesha taifa kupata wanunuzi zaidi wa tanzanite.
 
“Tumepata watu wakubwa na wameahidi kuendelea kuja, hii itatusaidia kupata wanunuzi wazuri wa tanzanite, watatusaidia kutangaza madini yetu”.
 
Aidha, Waziri Biteko amesema Tanzania ndiyo mahali salama pa kuwekeza katika sekta ya madini na hivyo wizara kwa upande wake, inaendelea kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza nchini ikiwemo wanunuzi wa tanzanite.
 
Pia, amekipongeza Chama Cha Wafanyabishara wa Madini ya Vito (TAMIDA) kwa hatua hiyo ya kuwezesha wanunuzi hao kuja nchini na kueleza “TAMIDA mmethibitisha bila shaka mnaweza kufanya kazi na serikali’’.
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAMIDA Sam Mollel amesema kuwa ziara ya wanunuzi hao ililenga katika kuitangaza Tanzania kama nchi pekee inayozalisha madini ya tanzanite duniani, kuona eneo ambalo madini hayo yanapozalishwa, ikiwemo kuona namna shughuli za uchimbaji wa madini hayo unavyofanywa , uthamini unavyofanywa katika eneo la mirerani pamoja na udhibiti wa Tanzanite unaofanywa na serikali.
 
‘’ Tumepata watu watakao simama na sisi kutangaza madini ya tanzanite, suala ambalo litawezesha pia bei ya tanzanite kupanda. Hata wao wanataka yasipite kwingine yakishaongezwa thamani hapa yaende moja kwa moja kwao.’’amesema Mollel.
 
Akizungumza kwa niaba ya ujumbe huo, Ken Oschipok kutoka kampuni ya  Diamond International amesema ni mara yake ya kwanza kufika Afrika na amevutiwa na mazingira yote kuhusu tanzanite, ukarimu wa watanzania na mazingira ya kibiashara na hivyo kuahidi kutumia fursa  hiyo kutoa elimu kuhusu Madini hayo na uhalisia wake kwa watu wengine. 
 
Mbali ya kutembelea migodi ya tanzanite Mirerani na kujionea shughuli za uzalishaji wa madini hayo, pia, ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko nchini.
 
Aidha, hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mhugwila, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Issa Nchasi na viongozi waandamizi wa Uwanja wa KIA.


Share:

Tanzania Na Malawi Wasaini Makubaliano Ya Kibiashara

Serikali ya Tanzania na Malawi zimesaini makubaliano ya ushirikiano wa kuimarisha na kuongeza biashara, mahusiano ya kijamii na miundombinu hususani ya bandari, barabara na ndege.

Makubaliano hayo yamelenga pia kuingiza sheria mpya ili kufanya mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara baina ya mataifa hayo na kuyaingizia pato la Taifa.

Amesema hayo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe, mara baada ya kupitia makabalinao ya awali baina ya nchi hizo mbili yaliofanyika toka mwaka 1987 na kufafanua namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kufungua nchi yetu na nchi jirani kwa miundombinu bora.

“Nchi ya Tanzania na Malawi imekuwa ikishirikiana kwa muda mrefu katika masuala ya kijamii, na kiuchukuzi na hivyo makubaliano mapya yaliyosainiwa ni kuona namna bora zaidi ambavyo tutashirikiana hasa katika masuala ya kibiashara kwa kuzingatia miundombinu yetu” amefafanua Waziri Kamwelwe.

Akielezea uboreshaji wa miundombinu yetu nchini, Waziri Mhandisi Kamwelwe
ameeleza kuwa Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ya Mpemba – Isongole yenye urefu wa (km 50.3) inayounganisha nchi yetu na mpaka wa Malawi kupitia Wilaya ya Chitipa hivyo ikikamilika itasaidia sana katika masuala ya usafirishaji wa bidhaa na mizigo.

Aidha, ameongeza kuwa katika mpaka wa Kasumulu ambao pia unaunganisha nchi hizo mbili, Serikali imeshaanza ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha (One Stop Border Post – OSBP) ambayo itasaidia katika kurahisisha biashara za Malawi na Tanzania.

Mhandisi Kamwelwe ameeleza uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam ikiwemo kuongeza kina cha maji na gati zake kuanzia Namba 1 hadi 7 ambazo zitaiwezesha bandari hiyo kuhudumia meli kubwa zenye uwezo wa kubeba makasha 5,000 kwa wakati mmoja.

Waziri Kamwelwe asema kuwa katika kujenga mahusiano mazuri kati ya nchi hizo, Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA), ilichukua hatua ya kutembelea nchi ya Malawi na kukutana na kuzungumza na wafanyabishara kwa lengo la kuainisha maeneo ya ushirikiano na kuboresha maisha ya Tanzania na Malawi.

Amefafanua kuwa sasa TPA ipo katika hatua za usimikaji wa(Flow Meter) za kisasa katika Bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ili kurahisisha upakuaji wa mafuta kutoka kwenye meli.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Malawi Mhe. Ralph Jooma,
amesema kuwa mkataba wa makubaliano waliosaini utatekelezwa kwa ufanisi na tija.

Pia Malawi itashirikiana vyema na Bandari ya Dar es Salaam kuwa bandari ya wafanyabishara na hivyo kusaidia kuongeza uchumi wa mataifa yote mawili.
 
Makubaliano ya kibishara kati ya nchi hizo yamefanywa kati ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Malawi Mhe. Ralph Jooma.


Share:

UDOM-Internal University Transfer Forms 2019/2020

UDOM-APPLICATION FORM FOR INTERNAL TRANSFER OF STUDENTS FOR THE 2019-2020 ACADEMIC YEAR, UDOM-ANNOUNCEMENT OF APPLICATION FOR INTERNAL TRANSFER OF STUDENTS FOR THE 2019-2020 ACADEMIC YEAR The University of Dodoma provides a unique environment for teaching, learning, research, and public services to ensure a memorable and lifetime experience. Additionally, since the quality of student experience is as well a… Read More »

The post UDOM-Internal University Transfer Forms 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

ALAF: Swahili scholarship Opportunities at University of Dar es salaam 2019/2020

ALAF: Swahili scholarship Opportunities at University of Dar es salaam 2019/2020 The University of Dar es Salaam University’s Swahili Studies Institute in collaboration with ALAF Limited is pleased to announce the funding of three (3) students studying for the MA Kiswahil program at the University of Dar es Salaam for the 2019 / 2020.   See the appendix for more details.  Attachment : 20191107_092959_UDSM_STALLED CONFIDENTIAL 2019-2020 -RUDIO.doc

The post ALAF: Swahili scholarship Opportunities at University of Dar es salaam 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

SUA-Inter University Transfer Window 2019/2020 Academic Year

SUA-Inter University Transfer Window 2019/2020 Academic Year   SUA-PROCEDURES FOR INTER-UNIVERSITY TRANSFER FOR 2019/2020 ACADEMIC YEAR The Directorate of Undergraduate Studies wishes to inform all prospective students who were admitted to pursue different degree programs in other Universities in the academic year 2019/2020 but would like to transfer to SUA that online application for transfers will be open from… Read More »

The post SUA-Inter University Transfer Window 2019/2020 Academic Year appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Contract Basis Jobs at Mbeya University of Science and Technology (MUST) – 6 posts

Welcome to Mbeya University of Science and Technology (MUST). As a higher learning institution, Mbeya University of Science and Technology endeavors to be a leading University of Science and Technology and ensuring that it becomes a centre of excellence for academics, research and consultancy. MUST further strives to be a centre where modern and indigenous technologies meet for… Read More »

The post Contract Basis Jobs at Mbeya University of Science and Technology (MUST) – 6 posts appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Software Developer – Volunteer required at at Prefix

Job Title : Software Developer – Volunteer Department : Development & Engineering Department Reports To : Development director Date : 7th November 2019 Summary The software developer shall be responsible for the analysis, development, testing and supporting highly complex application software. Requirements The task at hand requires someone who knows the following Laravel Framework for the Back-End, creating… Read More »

The post Software Developer – Volunteer required at at Prefix appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job Opportunities at Kazini Kwetu, Depot Accountants

Place: KAHAMA Deadline: 20th November, 2019 DEPOT ACCOUNTANTs – KAHAMA On behalf of client Kazini Kwetu Limited is looking for Depot Accountants with exceptional abilities and who are ambitious to climb the ladder in their professions. They will work in a well established manufacturing company based in Kahama. Interested candidates should apply online. Responsibilities Post and process journal… Read More »

The post Job Opportunities at Kazini Kwetu, Depot Accountants appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Waste Management Plant Officer at Tindwa Medical and Health Services

Job Title: Waste Management Plant Officer Medical Services, Waste and Environmental Management, Occupation Health and safety both local and international and Medical Supplies Services. Currently, it is looking for a Waste Management Plant Officer, person who is self-motivated, committed, result driven and self-motivated to work with the company. Job Description Reports To : Waste & Environmental Manager Deadline… Read More »

The post Waste Management Plant Officer at Tindwa Medical and Health Services appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

3 Jobs Opportunities at Sokowatch East Africa

Position: Dar es Salaam Warehouse Manager About Us: Sokowatch is transforming communities across Africa by revolutionizing access to essential goods and services. By connecting small shops to the digital economy, we fix inefficient supply chains and provide services that were previously unavailable. Sokowatch aims to provide everything a retailer needs, no wholesalers or banks necessary. Our Vision Dominate… Read More »

The post 3 Jobs Opportunities at Sokowatch East Africa appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Program and Operations Manager, Tanzania Job Opportunity

Position Title: Program and Operations Manager, Tanzania Reports to: Chief of Party, Tanzania Department: International Programs Division, Africa Team Location: Dar es Salaam, Tanzania Freedom House promotes the spread of freedom and democracy around the world through research, advocacy, and programs that support frontline activists. We are a leader in identifying threats to freedom through our highly regarded… Read More »

The post Program and Operations Manager, Tanzania Job Opportunity appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger