Na,Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la kupambana na dawa za kulevya na Uhalifu[UNODC],Tanzania ilipunguza uingizaji wa dawa za kulevya aina ya Heroin kwa asilimia 90% .
Hayo yamesemwa Nov.6,2019 na Waziri wan chi,Ofisi ya Waziri Mkuu ,Sera,Bunge ,kazi,vijana ,Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama wakati akizungumza na Waandishi wa Habari bungeni jijini Dodoma mara baada ya kuwasilisha bungeni Taarifa ya Hali za Dawa za Kulevya ya mwaka 2018.
Mhe.Mhagama amesema pamoja na jitihada zilizofanywa na serikali katika kupambana na dawa za kulevya ,bangi imeendelea kuwa tatizo hapa nchini ambapo ametaja mikoa ambayo imeonekana kuathirika zaidi na kilimo cha bangi ni pamoja na Mara,Tanga,Morogoro,Arusha,Kagera na Ruvuma huku pia Mirungi ikiendelea kutumiwa na watu wa rika hapa nchini.
Aidha,Mhe.Mhagama amesema kwa kipindi cha mwaka 2018 juhudi ya vyombo vya dola kwa kushirikiana na wananchi zilifanikiwa ukamataji wa tani 24.3 za bangi zikiwahusisha watuhumiwa 10,061 na tani 8.97 za mirungi zikiwahusisha watuhumiwa 1,186.
Katika kipindi cha Mwaka 2018 jumla ya kesi 7,593 zikiwa na jumla ya watuhumiwa 10,979 zilifunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini huku jumla ya kesi 7,174 zilizowahusisha watuhumiwa 11,045 ziliendelea kusikilizwa.
Pia,Mhe.Mhagama amesema serikali imeendelea kutoa huduma za tiba kwa watumiaji wa dawa za kulevya ambapo jumla ya vituo 6 vilivyopo katika mikoa ya Dar Es Salaam,Mwanza,Mbeya,na Dodoma viliendelea kutoa huduma na hadi kufikia mwaka 2018 ,zaidi ya watumiaji elfu nane[8000] waliendelea kupatiwa huduma za Methadone katika vituo husika.
Hivyo,Waziri Mhagama ameendelea kufafanua serikali itaendelea kuimarisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya huku akivipongeza vyombo vya habari pamoja na wadau mbalimbali kwa kuendelea kusisitiza madhara ya dawa za kulevya kwa Taifa la Tanzania.
Kwa upande wake kamishna wa Kinga na tiba kutoka Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini Dokta Peter Mfisi amesema bei ya dawa ya kutibu waathirika wa dawa za kulevya [methadone] inanunuliwa kwa Soko la India kati ya dola 650 hadi dola 700 na kilo moja ya Methadone inawezakuhudumia watu 650 mpaka 700.
0 comments:
Post a Comment