Saturday, 5 October 2019

JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA LAADHIMISHWA WILAYANI MISUNGWI

Afisa Tawala Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, Zubeda Kimaro akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima Duniani 2019 yaliyofanyika kiwilaya katika Kata ya Ukiriguru, Oktoba 03, 2019.



Na George Binagi-GB Pazzo
Afisa Elimu Msingi Wilaya Misungwi, Mwl. Frank Magabiko akizungumza kwenye maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi, Kisena Mabuba.
Afisa Elimu Watu Wazima Wilaya Misungwi, Mwl. Lusian Malungo akifafanua jambo kwenye maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi, Zubeda Kimaro akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya elimu ya watu wazima wilayani Misungwi.
Mmoja wa wahitimu elimu ya watu wazima wilayani Misungwi aakipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi.
Mgeni rasmi, Zubeda Kimaro akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya elimu ya watu wazima wilayani Misungwi.
Wahitimu mbalimbali wa mafunzo na elimu ya watu wazima wilayani Misungwi walipokea vyeti kwenye maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi, Zubeda Kimaro akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali kukagua bidhaa zinazotengenezwa na wanufaika wa elimu ya watu wazima wilayani Misungwi.
Mgeni rasmi, Zubeda Kimaro akikagua bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wanufaika wa elimu ya watu wazima wilayani Misungwi.
Mgeni rasmi, Zubeda Kimaro akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali kukagua bidhaa zinazotengenezwa na wanufaika wa elimu ya watu wazima wilayani Misungwi.
Burudani ya ngoma za asili kutoka kwa wanafunzi.
Tazama Video hapa chini


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi October 5



















Share:

Friday, 4 October 2019

Mtalaam Na Bingwa Wa Magonjwa Yote Sugu Nayaliyoshindikana Kama Vile Pumu, Vidonda Vya Tumbo, Busha, Nguvu Za Kiume, Kisukari

Tatizo la upungufu ukosefu wa nguvu za kiume, maumbile madogo  limekuwa kubwa kwa rika zote hapa duniani

Matatizo hayo sio mageni kigeni ni ile tiba sahihi yakutibu na kuponya haya.chanzo cha hayo matatizo ni:KISUKARI, NGIRI,CHANGO, TUMBO KUUNGURUMA NA KUJAA GESI, KIUNO KUUMA, MAUMIVU YA MGONGO,MAGONJWA YA ZINAA, KORODANI KUVIMBANAKUUMA,VIDONDA VYA TUMBO, NK.

Tiba sahihi nabora ya tatizo la nguvu zakiume ni 3Power,Nidawa ya vidonge asilia vilivyotengenezwa kwa kiwango bora na salama kwa ajili yakutibu mojakwamoja tatizo la nguvu za kiume maradufu

1,hutibu nguvu za kiume mda mfupi sana kati ya umri wa miaka 18-85 naitakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20 hadi 40 tendo lakwanza bila kuchoka naitakufanya uwe nahamu yakuendelea na tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila hamu kuisha.

FINA Power Nidawa yakuboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi uipendayo inchi 6,7 hadi 8 kwa mda mfupi sana.dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk 67

Pia tunatibu,KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU,MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE, BP, BUSHA BILA UPASUAJI NK.

ISHOSHA,Nidawa ya mvuto wa biashara,humvuta mme,mke,hawara,mchumba,unaemhitaji

SHEPU EXRA,Nidawa ya yakupunguza matiti,unene tumbo,kitambi kwa akina baba,hutoa mafuta mabaya mwilini,makovu sehemu mbalimbali mwilini,chunusi sugu,minyama uzembe,michirizi mwilini

HUDUMA HIZI NANYINGINE NYINGI MTALAAM BINGWA DR SHEIKH OMARY
Anapatikana dar magomeni moroco
SIMU NO 0767 14 53 57/0629 03 45 50.

NAKAMA NAFASI YAKUFIKA OFISINI HAIPO UTALETEWA HAPO ULIPO.


Share:

[HESLB]TAARIFA MUHIMU: MASAHIHISHO YA MAOMBI YA MIKOPO 2019/2020

Higher Education Students’ Loans Board (HESLB): The focus is on both issuance and recovery of loans from higher education loan beneficiaries. Over the past years, since its establishment in July 2005, the Board has managed to issue loans to needy students and the trend shows a steady growth. [HESLB]TAARIFA MUHIMU: MASAHIHISHO YA MAOMBI YA MIKOPO 2019/2020 You May… Read More »

The post [HESLB]TAARIFA MUHIMU: MASAHIHISHO YA MAOMBI YA MIKOPO 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Dawa Komesha Ya Maumbile Madogo , Nguvu Za Kiume Na Magonjwa Mengineyo

*NGETWA MIX*/
√Hii ndio dawa bora ya mitishamba kiboko ya maumbile Madogo(KIBAMIA) Hurefusha na kunenepesha maumbile  mafupi pia  yaliyoingia ndani kutokana na kitambi ama kuathirika na punyeto

*📌SUPER MORINGA MIX*/
Ni dawabora ya nguvu za kiume yenye mchanganyiko wa miti shamba 10 yenye maajabu yafuatayo:/
🔖(1)Inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimarisha misuri   ilio legea na kusinyaa wakati wa tendo la ndoa/
🔖(2)Kuongeza hamu ya tendo kukufanya uweze kurudia tendo hadi mara tatu bila kuchoka
🔖(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-30 kwa tendo la Kwanza na utakuwa na uwezo wa Kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3-4 bila hamu kuisha na inatibu kabisa/
.
*MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA*/
🔖(1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
🔖(2) Choo kuwa kama Cha mbuzi/
🔖(3)Ngiri/
🔖(4)Kama umejichua sana punyeto/
🔖(5)Kisukari/
🔖(6)Presha ya kupanda na kushuka/
🔖(7)Vidonda vya tumbo,/
.
Na haya yote husababisha/
📍Kuishiwa kwa nguvu za kiume 📌/
. _______________________
Bado hujachelewa dawa hizi ni mpya kabisa  ni tofaut na ulizo wahi kutumia pia zimeonesha mafanikio kwa watu wengi sana/

Pia tuna tibu  KISUKARI,PRESHA,VIDONDA VYA TUMBO N.K/
._______________________
DR .SELEMANI OMARY ANAPATIKANA  DAR ES SALAAM , PIA UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO  NDANI NA NJE YA NCHI .SIMU NO:/
*📞+255788468114*


Share:

RAIS MAGUFULI AMPONGEZA MKUU WA MKOA WA MBEYA KWA KUWACHAPA VIBOKO WANAFUNZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kwa kuwachapa viboko wanafunzi wa shule ya sekondari Kiwanja wilayani Chunya baada ya kuchoma mabweni ya shule.
Share:

BAADA YA KUWACHARAZA VIBOKO WANAFUNZI...MKUU WA MKOA WA MBEYA AFUKUZA WANAFUNZI WOTE

Na Esther Macha - Malunde1 blog  Chunya
SIKU moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kuchapa viboko wanafunzi 14 wa shule ya sekondari Kiwanja wilayani Chunya kwa kosa la kumiliki simu za mkononi, Mkuu huyo wa mkoa amerejea tena shuleni hapo na kuwatimua wanafunzi wote 392 wa kidato cha tano na sita na kuwarejesha majumbani mwao.

Pamoja na adhabu hiyo, wanafunzi hao pia wanatakiwa kulipa shilingi 200,000 kila mmoja kwa wanafunzi 366 ambao hawakuhusishwa na tukio la uchomaji moto wa mabweni ya shule hiyo, huku wenzao 26 ambao ndio waliokamatwa na simu za mkononi wakitakiwa kulipa shilingi 500,000 kila mmoja, fedha ambazo zinahitajika kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya shule hiyo ambayo yalichomwa moto.
Akizungumza na wanafunzi hao jana, Chalamila alitoa muda wa saa nne kuanzia saa 1:00 hadi saa 4:00 asubuhi kwa wanafunzi hao kufungasha kila kilicho chao na kuondoka shuleni hapo.
Chalamila aliiwataka kurejea Oktoba 18, mwaka huu wakiwa tayari wamelipa fedha hizo kupitia akaunti ya shule wakiwa pia na barua ya kukiri makosa yao na kuahidi kutorudia.
Alisema wanafunzi 26 ambao walikamatwa wakiwa na simu za mkononi, licha ya kulipa shilingi 500,000 kila mmoja siku ya kurejea shuleni wanatakiwa kufika na wazazi wao.
 “Tumeamua kunafunga kidato cha tano na Sita kwa sababu hakuna sehemu ya kulala, mabweni mliyokuwa mkilala ndiyo mmeyachoma moto,” Alisema Chalamila.
Chalamila alisisitiza kuwa wanafunzi wote wanatakiwa kurejea shuleni Oktoba 18, mwaka huu akiwa amelipa kiasi hicho cha fedha huku akionya kuwa yeyote atakayekaidi Serikali itamfuata huko aliko na kumkamata.
Alisema hata kama mwanafunzi ambaye hatalipa fedha hizo akihamia shule za binafsi, atafuatwa huko na kuzuiwa kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha sita akiwa popote ndani ya mipaka ya Tanzania.
 Alisema kuwa walimu waliokuwa wakifundisha kidato cha Sita pia wanapewa mapumziko kwa kipindi hicho ambacho wanafunzi watakuwa nyumbani.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhandisi Maryprisca Mahundi aliwaasa wanafunzi hao kutekeleza maagizo yote waliyopewa ili waendelee kupata haki yao ya elimu.
Alisema kukaidi kutekeleza maagizo hayo kutasababisha wafukuzwe shule na kuzuiwa kufanya mtihani wa Taifa wa Kidato cha Sita mahali popote nchini.
“Maelekezo hayo hakikisheni mnayafanyia kazi kadri mnavyopewa, nje ya hapo mtajipotezea haki ya kusoma katika maisha yenu,” alisema Mahundi.
Baadhi ya wanafunzi walisema uamuzi huo unazidi kuwaongezea machungu kwa vile baadhi yao waliunguliwa na vitu vyao ndani ya mabweni na hawana namna ya kupata nauli za kurejea majumbani mwao.
Share:

Waziri Mkuu Ampa Siku Tatu Mhazini Itigi Arejeshe Posho Aliyojilipa Kinyume Cha Taratibu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempa siku tatu Kaimu Mweka Hazina wa wilaya ya Itigi, Bw. Optatus Likiliwike ahakikishe anarejesha sh. milioni 1.6 ambazo alijilipa posho kinyume cha utaratibu.

“Kabla sijamaliza ziara tarehe 7, nataka nione pay in slip kuthibitisha kuwa fedha hiyo imerudishwa. Adhabu yako kaweke fedha benki, niione hiyo pay in slip kabla sijaondoka," amesema Waziri Mkuu.

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Oktoba 4, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Manyoni ambao wanajumuisha Halmashauri za Wilaya za Itigi na Manyoni.

"Wewe si ndiye Otto au Optatus? Mwezi Julai ulilipwa posho ya safari ili uende Dodoma kukamilisha mahesabu ya bajeti lakini hukwenda. Taratibu za fedha zinasema ukitumia fedha, urejeshe, wewe ulifanyaje?," alihoji  Waziri Mkuu.

“Nilichukua fedha lakini kutokana na majukumu mengi niliyo nayo, sikwenda nikawa naenda wikiendi na kuna kazi nyingine haikuwa ni lazima niwepo Dodoma," alijibu Bw. Likiliwike.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemtaka afisa huyo arejeshe sh. milioni 196 za ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ambazo zimetumika kinyume na zilivyopangwa.

"Hizi fedha zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi. Hizi ni fedha za retention, ni nani alikiuka maelekezo na kuamua kuzitumia kwa kazi nyingine?" Waziri Mkuu alijibiwa kwamba ni Mkurugenzi na Mweka hazina waliokuwepo kabla yake.

Waziri Mkuu amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Bw. John Mgalula ambaye aliteuliwa wiki iliyopita asimamie marejesho ya posho za Bw. Likiliwike pamoja na marejesho ya sh. milioni 196 ambazo mweka hazina huyo ameahidi kuwa Halmashauri yake imetenga sh. milioni 70 ili zirejeshwe kila mwaka.

Waziri Mkuu amesema wanapaswa kutenga fedha zaidi ili fedha hiyo iweze kurejeshwa haraka kwa Wakala wa Majengo nchini (TBA) ambaye ni mkandarasi wa jengo la ofisi za Halmashauri hiyo.

Naye Bw. Optatus Otto Likiliwike alisema kwamba fedha zinazodaiwa kutumika zilikuwa zimetumwa na HAZINA kwa ajili ya ujenzi wa ofisi lakini zililazimika kuchotwa na uongozi uliopita ili zitumike kuweka miundombinu ya kuanzisha Halmashauri mpya ya Itigi.

Alisema waliohusika ukiukwaji huo ni Mkurugenzi aliyepita, Bw. Pius Luhende na Mweka Hazina aliyepita Bw. Charles Mnamba. Hata hivyo, alikiri kwamba fedha hizo hazikuombewa kibali cha matumizi hayo.

Akiweka jiwe la msingi kwenye jengo hilo, Waziri Mkuu alisema anaweka jiwe hilo kwa sababu ameridhishwa na maelezo ya Meneja wa TBA kuhusu ujenzi wa jengo hilo.

Amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo wahoji matumizi ya fedha hizo na wawaorodheshe wote waliohusika na matumizi mabaya ya fedha hizo. “Kaeni na mkaguzi wenu wa ndani, awape taarifa juu ya matumizi hayo,” alisema.

Pia amewataka watumishi wa umma waheshimiane na watambue Mamlaka nyingine kama za madiwani. Pia aliwataka wafuate taratibu na kanuni za utumishi na siyo wajifanyie mambo kwa holela.

Awali, Waziri Mkuu alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Bw. Charles Fussi ahakikishe anarejesha mkopo wa sh. milioni 100 kutoka benki ya CRDB ambazo walikopeshwa madiwani, wakarejesha kiasi lakini Halmashuri haijazipeleka benki.

Mkurugenzi huyo alikiri kuwepo kwa deni hilo kutokana na malimbikizo ya muda mrefu na riba zinazotozwa na benki.

“Hakikisha unamaliza hilo deni la sivyo hawa Waheshimiwa hawatapata stahili zao hadi deni liishe. Pia unataka kusababisha mgogoro baina ya benki na Halmashauri.”

Aliwataka wadiwani hao waisimamie kwa karibu Halmashauri yao. “Madiwani muiangalie Halmashauri yenu kwa kina. Hatuwezi kuendesha Halmashauri kwa utaratibu huu wa kila mmoja kufanya kazi anavyotaka.”

Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake wilayani Itigi.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Rais Magufuli Atatua mgogoro wa ardhi kati ya Wananchi na kiwanda cha Saruji Mbeya

Rais Magufuli ameagiza wakazi wa kijiji cha Nanyala wilayani Mbozi mkoani Songwe, kuendelea kulitumia eneo lenye ukubwa wa ekari 2,115 linalogombewa na wakazi hao na kiwanda cha Saruji Mbeya.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo aliposimama katika kijiji hicho cha Nanyala na kuelezwa kero hiyo na mwenyekiti wa kijiji hicho, Philemon Namwema.

Mwenyekiti huyo amesema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu na wamezuiwa kufanya shughuli yoyote, wananchi  23 wakikabiliwa na kesi mahakamani.

Akitoa uamuzi huo, Magufuli amewaagiza mawaziri kukaa pamoja na kufuta kesi iliyopo mahakamani na baada ya hapo wamjulishe ili aweze kubadili matumizi ya eneo hilo.


Share:

MUHAS: A Call For Second Round Applications Diploma 2019/2020

MUHAS: A Call For Second Round Applications Diploma 2019/2020 The Institute of Allied Health Sciences (IAHS) Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) invites Applications for admission into various Diploma Programs for the Academic Year 2019/2020. CALL FOR SECOND ROUND APPLICATIONS Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) invites Applications for admission into various Diploma Programs… Read More »

The post MUHAS: A Call For Second Round Applications Diploma 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MUHAS: Late Applications for Postgraduate Degree Studies for Academic Year 2019/2020

MUHAS: Late Applications for Postgraduate Degree Studies for Academic Year 2019/2020 Late applications are invited from the public for postgraduate degree studies at the Muhimbili University of Health and Allied Sciences for 3 Master of Science Superspecialization programmes indicated below; 1. MSc Interventional Radiology MSc Neuroradiology MSc Plastic and Reconstructive Surgery Eligibility for MSc Interventional Radiology and MSc… Read More »

The post MUHAS: Late Applications for Postgraduate Degree Studies for Academic Year 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

HESLB Orodha ya waombaji mikopo-Postgraduate Loan applicants 2019/2020

HESLB Orodha ya waombaji mikopo-Postgraduate Loan applicants 2019/2020 A list of Loan applicants joining postgraduate programmes Higher Education Students’ Loans Board (HESLB): The focus is on both issuance and recovery of loans from higher education loan beneficiaries. Over the past years, since its establishment in July 2005, the Board has managed to issue loans to needy students and… Read More »

The post HESLB Orodha ya waombaji mikopo-Postgraduate Loan applicants 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

HESLB Orodha ya waombaji mikopo-Law School of Tanzania (Shule ya Sheria) 2019/2020

HESLB Orodha ya waombaji mikopo-Law School of Tanzania (Shule ya Sheria) 2019/2020 A list of Loan applicants joining the Law School of Tanzania. Higher Education Students’ Loans Board (HESLB): The focus is on both issuance and recovery of loans from higher education loan beneficiaries. Over the past years, since its establishment in July 2005, the Board has managed… Read More »

The post HESLB Orodha ya waombaji mikopo-Law School of Tanzania (Shule ya Sheria) 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Serikali Yapiga Marufuku Utoaji Vibali Vya Ujenzi Wa Viwanda Ndani Ya Makazi Ya Watu Mkuranga

Na Munir Shemweta, WANMM MKURANGA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amepiga marufuku utoaji vibali vya ujenzi wa viwanda katika maeneo ya makazi ya watu katika wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana tarehe 03 Oktoba 2019 alipokutana na uongozi pamoja na watumishi wa sekta ya ardhi wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani Mkuranga mkoani Pwani kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi pamoja na kutatua migogoro ya ardhi.

Alisema, halmashauri ya wilaya ya Mkuranga lazima iandae Mpango Kabambe alioueleza kuwa utakuwa dira ya halmashauri hiyo kuonesha matumizi ya ardhi yake kwa kuwa maeneo kama viwanda, makazi na matumizi mengine yatakuwa yameoneshwa na kuondoa ujenzi wa makazi holela.

 ‘’Mkuranga lazima iwe na mpango wa matumizi ya ardhi unaoonesha viwanda vikae wapi, siyo viwanda kujengwa kila kona na katika mipango yenu halmashauri muandae maeneo yatakayowekwa viwanda’’ alisema Dkt Mabula.

Kuhusu zoezi la Urasimishaji, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  ameitaka Mkuranga kuharakisha zoezi hilo ili kuepuka makazi holela na kubainisha ucheleweshaji wowote utasababisha mji kutopangika na kusisitiza zoezi hilo lazima lisimamiwe kwa umakini.

Akigeukia suala la upimaji maeneo katika wilaya ya Mkuranga, Dkt Mabula alisema wilaya ya Mkuranga bado hajafanikiwa katika zoezi la upimaji pamoja na kuwa na viwanda vingi na kushauri wakati wa zoezi la upimaji lazima halmashauri iainishe pia maeneo ya uwekezaji,

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega alisema, wilaya ya Mkuranga ina viwanda vingi kutokana kuwa na eneo linalovutia na kuongeza kuwa atafurahi kama Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi itafanya jitihada za kuharakisha zoezi la urasimishaji.

‘’Kama serikali itaongeza kasi kidogo ya kupanga na kurasimisha maeneo ya wilaya hii basi itakusanya kiasi kikubwa cha fedha maana Mkuranga imekuwa lango la ni kimbilio la wananchi kutoka Dar es Salaam kutokana na mkoa huo kujaa na mahali pekee pa kupumulia ni Mkuranga’’ alisema Ulega.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi kuwa halmashauri yake ina migogoro mingi ya adhi ya kurithi na katika kukabiliana changamoto za ardhi ikiwemo makazi holela, tayari kuna Kampuni saba zinazofanya kazi ya urasimishaji na kusisitiza kuwa mkakati wa halmashauri yake ni kuzuia uanzishwaji makazi holela,

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Philberto Sanga amemtaka mtumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Welbert Mduma kujisalimisha mara moja wilayani humo kujibu tuhuma zinazomkabili za kuhujumu mradi wa upimaji viwanja vya halmashauri ya wilaya ya Mkuranga katika maeneo ya Kikoo na Miale.

Mtumishi huyo ambaye ni Afisa Ardhi hajaonekana ofisi za halmashauri ya wilaya ya Mkuranga kwa muda mrefu tangu arejeshwe akitokea Morogoro alipohamishiwa baada ya kufanya ‘madudu’ katika mradi wa fidia ya ardhi katika maeneo yaliyopimwa viwanja na halmashauri ya Mkuranga.


Share:

Wenye Ulemavu Watakiwa Kuchangamkia Fursa Za Mikopo


NA.MWANDISHI WETU
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masualaya ya Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa amewaasa watu wenye ulemavu  kuchangamkia fursa za mikopo zitolewazo na Serikali pamoja na wadau mbalimbali ili ziwasaidie kuboresha maisha yao.

Ametoa wito huo hii jana (oktoba 3, 2019) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kipindi maalum kinachorushwa na radio Pangani alipotembelea kituoni hapo Mkoani Tanga ili kujionea jitihada zinazofanya na radio hiyo katika kuhabarisha umma juu ya masuala mtambuka ikiwemo vipindi maalum vya elimu ya jamii kuhusu masuala ya watu wenye ulemavu nchini.

Mhe.Ikupa alieleza kuwa Serikali imeendelea kuhakikisha inatekeleza sheria namba 9 ya mwaka 2010 inayohusu haki na ulinzi kwa watu wenye ulemavu na kuhakikisha wanapatiwa haki hizo ikiwemo masuala ya ajira, elimu, afya na utengamao wa maisha yao ili kuondokana na dhana potofu ya utegemezi kwa kundi hilo.

“Kwa muda mrefu sasa watu wenye ulemavu nchini wamekuwa wakinyanyaswa na kunyimwa haki zao za ajira, elimu, afya na kufikia wakati jamii kuwaficha badala ya kuwapa nafasi ya kuonesha uwezo wao na kuweza kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali ili waweze kujikwamua kiuchumi kuondokana na hali ya utegemezi.”alisema Mhe. Ikupa.

Aliongezea kuwa tayari Serikali imeendelea na jitihada za kuwawezesha watu wenye ulemavu kwa kuwatengea asilimia 2 katika kila Halmashauri nchini ambazo zinatumika katika kuwapatia mikopo kwa kupitia uundwaji wa vikundi na kujisajili ili kupewa mikopi hiyo isiyokuwa na riba na kujikwamua kiuchumi.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Zainab Abdallah alieleza kuwa Wilaya yake inatekeleza hilo na kuwataka vijana wenye ulemavu kutumia fursa za mikopo ili kuwezeshwa na kujiendeleza weneywe.

 Akiongezea kuwa, jitihada za Wilaya yake ni kuhakikisha wanawafikia wenye ulemaviu katika kuwapatia mahitaji yao ikiwemo, elimu na kuwapa nafasi katika fursa mbalimbali zinazojitokeaza katika Wilaya yake.

“Niwaombe muendelee kujiunga kwenye vikundi kwani kasi iliyopo hairidhishi kwa kuwa hadi sasa kuna vikundi vitatu tu ambavyo vimesajiliwa Halmashauri na ili uweze kupata mikopo hiyo ni lazima vikundi vitambulike,”alieleza Zainab.

Aliongezea kuwa, ipo haja ya kila mwenye ulemavu kujitahidi kujishughulisha katika shughuli ya kumuongezea kipato kwa kuzingatia uwezo aina ya ulemavu wake kwa kuwa serikali imeendelea kuweka mkazo katika kuliangalia kundi hili.

“Hadi sasa Wilaya yetu ina watu wenye ulemavu zaidi ya 700 hivyo ni wakati sahihi kuona namna kundi hili linaangaliwa na kupatiwa elimu ya ujasiriamali ili waweze kujikimu katika mahitaji yao na familia zao kwa ujumla’”alifafanua Mhe. Zainab

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Hassani Nyange alimpongeza Naibu waziri huyo kwa jitihada anazozifanya katika kuhakikisha kundi la wenye ulemavu linapatiwa huduma kwa usawa na haki ili kuendelea kuboresha mazingira ya kundi hilo.

“Binafsi ninafuraha kwa ujio wako Pangani tunaahidi kuendelea kuunga jitihada za serikali vya vitendo kwa kuzingatia awamu hii ya tano imejikita kuinua uchumi kuanzia mtu mmoja mmoja hadi Taifa kwa ujumla hivyo tutaendela kuhakikisha kila mwananchi anashiriki katika shughuli za uzalishaji mali na kufikia Taifa la uchumi wa kati,”aliongezea Nyange.

=MWISHO=


Share:

Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Kijaji Aiagiza TRA Kuweka Mifumo Imara Ya Ukusanyaji Mapato.

Na Ramadhani Kissimba, WFM, Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuweka mifumo imara ambayo itamtambua kila mfanyabiashara na bidhaa anayouza ili kuweza kukusanya kodi stahiki na kupunguza mianya ya ukwepaji kodi.

Mhe. Kijaji aliyasema hayo kwa viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa Mikoa ya Kodi ya Ilala na Kariakoo, wakati wa ziara yake ya kutembelea Ofisi za Mamlaka hiyo inayoendelea  Jijini Dar es Salaam.  

Dkt. Kijaji alisisitiza kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ina jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba inavuka lengo la makusanyo iliyojiwekea ili kuweza kumsaidia Mhe. Rais DKt. John Pombe Magufuli, atekeleze majukumu yake kwa ufanisi na kulifikisha Taifa pale alipodhamiria.

“Naiagiza Mamlaka kuanza zoezi la kukagua watumiaji wote wa mashine za utoaji risiti za kieletroniki  (EFD) hasa kwa wafanyabiashara wa Kariakoo ili kuhakikisha kila anayeuza anatoa risiti na anayenunua anadai risiti na kwa kufanya hivyo itasaidia  kuongeza makusanyo na kupelekea Taifa letu kujiendesha kupitia  fedha zetu wenyewe kwa kuwa hakuna Taifa huru bila mapato’’ alisisitiza Dkt. Kijaji

Aliwataka Maafisa wa TRA kutokaa ofisini badala yake wawatembelea wafanyabiashara ili kuhakiki matumizi ya mashine za utoaji wa risiti za kieletroniki (EFD).

Awali Meneja wa Ofisi ya Mkoa wa Kodi wa Kariakoo, Bw. Alex Katundu alimueleza Mhe. Kijaji kuwa Mkoa wake wa kikodi una jumla ya wafanyabiashara waliosajiliwa na Mamlaka hiyo 22,279 na kati ya hao wafanyabiashara 16,068 wanatumia mashine za EFD.

Alisema Mkoa wa kodi wa Kariakoo kwa mwaka 2018/19 walidhamiria kukusanya shilingi bilioni 138.66 lakini walifanikiwa kukusanya shilingi bilioni 109 ambayo ni sawa na asilimia 79 ya malengo waliyojiwekea.

Katika Mkoa wa kikodi wa Ilala, Kaimu Meneja Bw. Steven Kuzeni amesema katika kuhakikisha Mkoa wake unakusanya ipasavyo kodi ya Majengo, wamedhamiria kusajili majengo yote yanayozunguka Mkoa huo wa kikodi na hadi sasa wameshasajili majengo katika kata 26 kati ya kata 32 zilizopo katika eneo lake.

“Ofisi yangu kwa mwaka 2019/20 ina mkakati kabambe wa kuhakikisha inaongeza idadi ya walipa kodi ya mapato na wale wa ongezeko la thamani (VAT)” Aliongeza Bw. Kuzeni.

Katika hatua nyingine Kijaji amewapongeza watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania  kwa kuvuka lengo la makusanyo kwa mwezi Septemba ambapo imekusanya sh. trilioni 1.76, kiasi ambacho hakijawahi kukusanywa tangu nchi ipate uhuru na kuwahimiza kukaa pamoja na Taasisi zote zinazofanya kazi kwa karibu na Mamlaka hiyo  ili kuona ni kipi kinaweza kuboreshwa zaidi ili kuwapa fursa Watanzania kulipa kodi bila Serikali kuwalazimisha.

Mwisho


Share:

Watumishi 42 wakiwemo watendaji wa Kata na Vijiji Wafikishwa TAKUKURU Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amekabidhi watumishi 42 wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Rukwa kwa uchunguzi wa upotevu wa fedha wa zaidi ya shilingi milioni 916 baada ya kuonekana utetezi wao juu ya upotevu wa fedha hizo kutokuwa na vielelezo vya kutosha.

Mh. Wangabo ametoa maelekezo hayo baada ya kuitisha kikao cha Wakurugenzi, Wawekahazina, wahasibu na watendaji wa vijiji na kata wa halmashauri zote nne mkoani hapa ambao mfumo wa ukusanyaji mapato ngazi ya halmashauri (Local Government Revenue Collection Information System – LGRCIS) kuonesha kuwa fedha za makusanyo yao kubaki mifukoni mwao.

Aidha, Ametoa siku saba kwa wale wote ambao hawajawasilisha fedha za makusanyo yao benki kuhakikisha wanawasilisha fedha hizo ikiwemo wale waliokabidhiwa kwa TAKUKURU na kuonya kuwa endapo fedha hizo hazitawasilishwa kesi hiyo itatoka TAKUKURU na Kuhamia Jeshi la Polisi ili kuwafikisha mahakamani.

“Mimi natafuta fedha ukishindikana tutakufunga, na ndio maana nimesema jambo hili kwanza lishughulikiwe kwanza na TAKUKURU mpaka uturudishie hizo fedha kwa muda maalum ambao nimeutoa, nimeshatoa siku sita zimeisha leo hii natoa siku saba nyingine, wacha hawa ambao watakuwa wamerudisha, wale ambao watakuwa hawajakabidhisha fedha zao, nitatoa siku saba baada ya hapo kesi hii itatoka TAKUKURU na kuhamia polisi ili iende mahakamani,” Alisema

Katika kujadili sababu mbalimbali zinazopelekea fedha za makusanyo kutumiwa bila ya utaratibu maalum mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Joseph Sengerema amesema kuwa matatizo ya upotevu wa fedha hizo yanasababishwa kutokana na kukiuka sheria ya fedha za Serikali za Mitaa ambayo hairuhusu Mtendaji kufanya matumizi yoyote bila ya ridhaa ya mkurugenzi wa Halmashuri na kabla ya kuwasilisha fedha hizo benki.

“ Ukiangalia katika Halmashuri ya Wilya ya Nkasi mimi nishatahadharisha kwamba, kuna hatari kubwa mtendaji wa kijiji anapokusanya fedha halafu anapeleka fedha hiyo kwa mtendaji wa kata bila ya kuwa na nyaraka maalum inayokiri upokezi wa fedha hizo, kwa hali hiyo unawezaje kusimamia ili fedha hizi zisipotee? Na pia mtendaji wa kata anapozifikisha idara ya fedha anahakikishaje zinfishwa benki kwa wakati?” Alihoji.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda limshukuru Mh. Wangabo kwa kuwasaidia kupambana na upotevu wa mapato katika halmashauri jambo ambalo wamekuwa wakilitolea maelekezo akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya bila ya matunda.

“Usikivu wa watendaji wetu ni mdogo sana lakini nikuahidi kwamba maelekezo uliyoyatoa ya siku saba nitayafanyia kazi na kesho Defaulters (wadaiwa) wote tukutane pale ukumbi mdogo wa halmashauri ili niweze kuwakabidhini kwa Halmashauri ili Mkaanze utaratibu wa uchunguzi,” Alisisitiza.

Mmoja wa Watendaji hao Lusilus Bruno wa Kata ya Kirando, Wilayani Nkasi alikiri kuwepo kwa makosa ya kufanya matumizi kabla ya fedha hizo kufikishwa kwenye halmashauri jambo linalokwamisha kupokelewa kwa fedha pungufu wakati wa kuzipeleka benki na kusema kuwa upungufu huo unatokana na matumizi wanayoyafanya katika shughuli za kila siku za vijiji na kata.

“ Mtendaji wangu wa kijiji Tarehe 15 alinikabidhi shilingi 439,500/= ambazo tulitoa matumizi ya shilingi 150,000/= ambayo tuliandika dokezo kama kawaida na kumpa Mkurugenzi akakataa na kusema kuwa matumizi hayo ni makubwa, hilo deni likafika shilingi 540,100 kwa maana kwamba ile bili ilikuwa bado inasubiri ile 150,000 ili iende benki lakini mpaka jana ilikuwa bado makusanyo ni shilingi 100,800/= ambazo alinikabidhi kwahiyo tulishindwa kusafisha bili kwasababu ya upungufu wa shilingi 150,000,” Alisema.

Kati ya hao waliokabidhiwa TAKUKURU watumishi 22 ni watendaji wa kata na vijiji kutoka Halmashauri ya wilaya ya Nkasi, na watumishi 18 ni watendaji wa kata na vijiji kutoka Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga na mmoja ni mweka hazina na mhasibu wote wa Wilaya ya Nkasi na wengine 16 kutoka halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga walitakiwa kuandika maelezo pamoja na kuambatanisha vielelezo vya kuwasilisha fedha zao kwa mweka hazina wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. 

IMETOLEWA NA
OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger