Rais Magufuli ameagiza wakazi wa kijiji cha Nanyala wilayani Mbozi mkoani Songwe, kuendelea kulitumia eneo lenye ukubwa wa ekari 2,115 linalogombewa na wakazi hao na kiwanda cha Saruji Mbeya.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo aliposimama katika kijiji hicho cha Nanyala na kuelezwa kero hiyo na mwenyekiti wa kijiji hicho, Philemon Namwema.

Mwenyekiti huyo amesema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu na wamezuiwa kufanya shughuli yoyote, wananchi 23 wakikabiliwa na kesi mahakamani.
Akitoa uamuzi huo, Magufuli amewaagiza mawaziri kukaa pamoja na kufuta kesi iliyopo mahakamani na baada ya hapo wamjulishe ili aweze kubadili matumizi ya eneo hilo.

0 comments:
Post a Comment