Monday, 5 August 2019

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu 05 August























Share:

Sunday, 4 August 2019

Ndege Yaanguka Na Kuua Watu Wawili Wilayani Sikonge

NA EVELINA ODEMBA-OFISI YA DED SIKONGE
WATU wawili raia wa Afrika Kusini wamefariki katika ajali ya ndege iliyotokea mapema asubuhi ya leo majira ya saa moja na nusu katika kata ya Igigwa Wilayani Sikonge.

Watu hao waliotambulika kwa majina ya D. Werner mwenye umri wa miaka hamsini na nane 58 pamoja na Werner Fredrick Fronaman mwenye umri wa miaka 36 wote wanamme na raia wa Durbun Afrika ya kusini walikuwa kwenye ndege yenye namba za usajili 19-ZU-TAF mali ya Afrika Kusini.

Akilezea tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri alisema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa tukio hilo na kusema kuwa watu hao  walikuwa katika ziara ya kuhamasisha wanafunzi barani Afrika kusomea maswala ya Anga.

Kabla ya ajali kutokea Ijumaa walitua kwa dharula katika uwanja wa ndege wa Tabora wakitokea Entebe Uganda kuelekea Lilongwe Malawi ili kufika Afrika ya kusini. 

Jana asubuhi walipoanza safari, baada ya muda mchache walifanya mawasiliano na wataalamu wa uwanja wa ndege wa Tabora na kutoa taarifa kuwa injini ya ndege imezimika ghafla wakiwa angani hivyo wanafanya utaratibu wa kurudi Tabora.

Baada ya taarifa hizo hawakuweza kupatikana mpaka walipopata taarifa ya ajali hiyo na kufika wakakuta raia hao wameshafariki.


Share:

Waziri Kalemani: Bado Tunahitaji gesi zaidi itakayosaidia kuimarisha uchumi wa viwanda.

Na Veronica Simba – Dar es Salaam
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, amesema pamoja na kwamba Tanzania imeshagundua gesi futi za ujazo trilioni 57.54 hadi sasa, bado inahitaji gesi zaidi itakayosaidia kuimarisha uchumi wa viwanda.

Aliyasema hayo jana Agosti 3, 2019 jijini Dar es Salaam, alipokutana na kuzungumza na wajumbe wa Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Alisema, kazi ya utafutaji wa gesi inaendelea vizuri lakini akaisisitiza Menejimenti hiyo kuongeza kasi zaidi katika utafutaji wake pamoja na wa mafuta.

“Mahitaji ya gesi ni makubwa. Tunahitaji gesi kuzalisha umeme, tunahitaji gesi ya kutosha kwa matumizi ya majumbani na pia viwandani,” alieleza.

Aidha, Waziri aliitaka Menejimenti husika kutafuta mbinu mbalimbali na kuongeza ubunifu ili shirika hilo liweze kufanya biashara kiushindani, lipate mapato na baadaye lianze kutoa gawio serikalini.

Akifafanua, alisema, mwaka 2015 ilipitishwa sheria mpya ya mafuta ambayo ilibadili majukumu ya shirika kutoka kutegemea ruzuku ya serikali na kuwa shirika lenye kujiendesha kibiashara.

“Sasa, TPDC ikiwa ni kampuni ya serikali yenye kufanya biashara, ni lazima ifanye biashara kiushindani.”
 
Waziri alilitaka shirika hilo kupanua wigo wa usambazaji gesi majumbani hususan mkoa wa Dar es Salaam ambao una watumiaji wengi wa nishati ya mkaa, inayosababisha ukatwaji wa miti kwa kiwango kikubwa.

Vilevile, alitaka viwanda vingi zaidi viunganishiwe mfumo wa gesi kutoka 40 vilivyopelekewa huduma hiyo, ili kuvipunguzia gharama ya uzalishaji inayotokana na matumizi ya nishati nyingine.

Kwa upande wa matumizi ya gesi kwenye magari, Dkt Kalemani aliiagiza TPDC ifungue vituo zaidi vya kujazia gesi katika mikoa mbalimbali ili wateja walioko mikoani wapate huduma ya kubadili mfumo wa magari yao kutoka ule unaotumia mafuta na kuweka unaotumia gesi, ili kuwaepushia usumbufu wa kufuata huduma hiyo Dar es Salaam ambako ndiko kuna kituo pekee kwa sasa.

Aidha, alilitaka shirika hilo kuvifufua vituo vyake sita vya mafuta na kuongeza vingine zaidi ili iendeleze biashara hiyo kama wanavyofanya PUMA na wengine kwa ajili ya kuongeza mapato yake.

Maagizo mengine aliyotoa Waziri kwa Menejimenti hiyo ni kuandaa utaratibu wa kuachana na uagizaji nje ya nchi vifaa mbalimbali vya kusambazia gesi zikiwemo mita na mabomba, badala yake itumie vile vitakavyozalishwa nchini.

“Hii itawezesha viwanda vya aina hiyo kujengwa hapa nchini, watanzania watapata ajira na pia itarahisisha zoezi la kusambaza gesi maana vifaa vitakuwa vikipatikana nchini.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio, alimhakikishia Waziri kuwa shirika lake litatekeleza kikamilifu maagizo yote aliyowapatia.

“Tayari tumeshaanza kujipanga katika maeneo yetu ya kazi yanayojumuisha utafiti, uzalishaji  na biashara ya gesi. Nimerudi nikiwa na nguvu mpya kuwatumikia watanzania,” alisema Dkt Mataragio ambaye amerudishwa katika nafasi hiyo na Rais John Magufuli hivi karibuni, baada ya kusimamishwa kwa muda.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara akiwemo Katibu Mkuu, Dkt Hamisi Mwinyimvua, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Raphael Nombo pamoja na Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi Adam Zuberi.


Share:

Waziri Wa Kilimo Autaka Uongozi Wa Mkoa Wa Simiyu Kuanza Haraka Utekelezaji Wa Bima Ya Mazao

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu
Uongozi wa Mkoa wa Simiyu umetakiwa kuanza haraka utekelezaji wa mkakati kabambe uliozinduliwa leo tarehe 3 Agosti 2019 na Waziri wa Kilimo kuhusu Bima ya Mazao kwa wakulima.

Waziri Hasunga ameyasema hayo wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Simiyu na kuhudhuriwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo kupokea maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa kuhusu mustakali wa zao la Pamba.

Mhe Hasunga alisema kuwa kuanza haraka kwa utekelezaji wa uandikishaji wa wakulima kutaimarisha uwezekano wa kuboresha maisha ya wakulima ambao katika kipindi kirefu wameumia kupitia majanga mbalimbali wanayokumbana nayo ikiwemo mazao yao kuungua moto ama ukame.

Alisema kuwa uzinduzi wa Bima ya Mazao umefanyika katika mkoa wa Simiyu hivyo mkoa huo unapaswa kuanzisha haraka utekelezaji wake.

Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka amempongeza Waziri wa Kilimo kwa kipindi cha muda mfupi ameweza kuonyesha dira na muelekeo chanya katika ukombozi wa sekta ya kilimo nchini.

Alisema kuwa maamuzi ya wizara ya kilimo inayosimamiwa na Mhe Hasunga ya kuanzisha Bima ya Afya, na Usajili wa wakulima ni miongoni mwa mambo muhimu yatakayoinua sekta ya kilimo nchini.


Share:

Rais Magufuli Na Mkewe Mama Janeth Magufuli Washiriki Misa Takatifu Ya Dominika Ya 18 Ya Mwaka "C"

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Paul Haule, Agosti 04,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Paul Haule, Agosti 04,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakitoa sadaka pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakati wa Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam katika Ibada iliyoongozwa na Paroko Msaidizi Padre Paul Haule leo Jumapili Agosti 04,2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam leo Jumapili Agosti 04, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Janeth Magufuli wakipeana mkono wa Amani na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki walioshiriki Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoka nje na kusalimiana na waumini wenzao baada ya Misa Takatifu ya Dominika ya 18 ya Mwaka "C" katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Agosti4, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Simon Sirro nje ya kanisa Katoliki mara baada ya Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaamleo Jumapili Agosti 04, 2019.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimnunulia  IGP Simon Sirro na kijana fulana maalumu za sherehe ya kutimiza miaka 75 Muadhama Polycarp Kadinali Pengo  baada ya Misa Takatifu ya Dominika ya 18 ya Mwaka "C" katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Agosti4, 2019
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimnunulia muumini Rosari baada ya Misa Takatifu ya Dominika ya 18 ya Mwaka "C" katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Agosti4, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaliana na muumini na mtoto wake mara baada ya Misa Takatifu Dominika ya 18 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam leo Jumapili Agosti 04, 2019.


Share:

Waziri Mkuu Kuwa Mgeni Rasmi Katika Kongamano La Uwekezaji Kagera

NA AVITUS BENEDICTO KYARUZI,KAGERA
Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa anatarajia kufungua kongamano la wadau wa uwekezaji Kagera huku mabalo=ozi wanne toka mataifa mbalimbali pamoja na  wafanyabiashara toka nje  wakihudhuria  kongamano hilo lenye lengo la kuonyesha fulsa mbali mbali za kiuchumi zilizopo mkoani Kagera.
 
Kauli hiyo imetolewa Agost 3 mwaka huu na Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Elisha Marco Gaguti mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa rasmi ya maandalizi ya wiki ya Kagera  kikao kilichofanyika katika ofisi za mkoa   zilizopo manisapaa ya Bukoba.
 
Mkuu wa mkoa wa Kagera Marco Gaguti amesema maandalizi ya awali ya uwekezaji  Kagera yamefikia  asilimia 90 kwenda wiki hiyo ya Kagera ambapo yatafunguliwa rasmi Agost 14 mwaka huu na Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Kassimu Majaliwa hivyo amewataka  wadau mbali mbali pamoja na wananchi wa ndani ya mkoa wa Kagera na nje ya nchi  kushiriki kwa wingi katika wiki hiyo.
 
Mkuu huyo amesema  wiki hiyo ya Kagera inayotarajia kuanza Agost 12 hadi 17 mwaka huu ambapo kutakuwa na shughuli mbali mbali ikiwemo maonyesho ya Taasisi mbali mbali watu binafsi wanaofanya shughuli mbalimbali za kiuchumi yatakayofanyika katika viwanja vya Gymkhana manispaa ya Bukoba .
 
Amesema  kuwa  agost 15 mwaka huu Kongamano la wadau wa uwekezaji litaendelea ambapo tarehe 16 mwaka huu wiki hii ya Kagera inatarajia kufungwa rasmi na Waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji Mhe. Angela Kairuki na mara baada ya wiki hiyo kufungwa rasmi wadau mbali mbali wa uwekezaji watapata nafasi ya kwenda kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii pamoja na fulsa mbalimbali za uwekezaji zilizomo mkoani kagera hadi Agost 17 mwaka huu.

Wiki ya Uwekezaji Kagera imebeba kauli mbiu isemayo ‘’Kagera: Eneo la Kimkakati kwa uchumi wetu na Afrika Mashariki” kauli mbiu inayolenga kuonesha mkoa wa Kagera ulivyo kitovu cha uchumi wa nchi za afrika mashariki na kati katika kuyafanya  masoko ya nchi hizo za Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya sudani kusini, na jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambapo soko hilo lina wingi wa watu wasiopungua milioni 190.


Share:

Dereva mlevi asababisha kifo cha abiria na kujeruhi mwendesha pikipiki Shinyanga

NA SALVATORY NTANDU
Mtu mmoja ambaye hajafahamikia jina wala makazi mwenye umri kati ya miaka (35-40) amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya pikipiki aliyokuwa amepanda kugongwa na gari aina ya SUZUKI VITALA  lenye namba za usajili T 432 ALT likiendeshwa na Salum Saidi (30) mkazi wa Mwanza.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa ajali hiyo imetokea jana katika eneo la Ushirika,   barabara ya Shinyanga kuelekea Mwanza, Manispaa na Mkoa wa Shinyanga.

Amesema dereva wa gari hilo  Salum ameumia kifua, aliigonga pikipiki yenye namba za usajili T 295 BSG aina ya kiboko iliyokuwa ikiendeshwa na  Kishimba Sanzago (28) mkazi wa Ibadakuli ambaye ameumia kichwani huku abiria wake akifariki dunia ambaye bado hajafahamika jina wala makazi.

Kamanda Abwao amesema Majeruhi anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga na mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini hapo na  chanzo cha ajali hiyo ni ulevi kwa dereva wa gari hilo  na  amekamatwa huku vyombo husika vipo kituoni.


Share:

Katibu Mkuu CCM Ammwagia Sifa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  Dk Bashiru Ally amesema mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  John Mongella hataondolewa  mkoani humo hadi wakamilishe kazi ya kuufanya kuwa Mkoa ambao wananchi wake watajitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Ametoa kauli hiyo jana Jumamosi Agosti 3, 2019 mkoani Mwanza wakati akizungumza na seneti ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.

“Nichukue fursa hii kumpongeza Mongella anafanya kazi nzuri na ni moja ya viongozi wanaochapa kazi, mfano halisi ni pale ilipotokea ajali ya Mv Nyerere (iliyozama), alionyesha dhahiri utendaji wake, " alisema Bashiru.

Alisema maneno yanayozungumzwa kuwa mkuu huyo wa Mkoa atagombea ubunge Wilaya ya Ilemela si ya kweli, amemhakikishia kufanya naye kazi pamoja.

"Waliokuwa wanamsingizia kuwa ataenda kugombea ubunge haendi huko na akiwa king'ang'anizi atakosa vyote ubunge na ukuu wa Mkoa," alisema Bashiru.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili 04 August

















Share:

Saturday, 3 August 2019

Video Mpya: Joel Lwaga - WADUMU MILELE

Video Mpya: Joel Lwaga - WADUMU MILELE


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger