Sunday, 4 August 2019

Waziri Mkuu Kuwa Mgeni Rasmi Katika Kongamano La Uwekezaji Kagera

...
NA AVITUS BENEDICTO KYARUZI,KAGERA
Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa anatarajia kufungua kongamano la wadau wa uwekezaji Kagera huku mabalo=ozi wanne toka mataifa mbalimbali pamoja na  wafanyabiashara toka nje  wakihudhuria  kongamano hilo lenye lengo la kuonyesha fulsa mbali mbali za kiuchumi zilizopo mkoani Kagera.
 
Kauli hiyo imetolewa Agost 3 mwaka huu na Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Elisha Marco Gaguti mbele ya waandishi wa habari wakati akitoa taarifa rasmi ya maandalizi ya wiki ya Kagera  kikao kilichofanyika katika ofisi za mkoa   zilizopo manisapaa ya Bukoba.
 
Mkuu wa mkoa wa Kagera Marco Gaguti amesema maandalizi ya awali ya uwekezaji  Kagera yamefikia  asilimia 90 kwenda wiki hiyo ya Kagera ambapo yatafunguliwa rasmi Agost 14 mwaka huu na Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Kassimu Majaliwa hivyo amewataka  wadau mbali mbali pamoja na wananchi wa ndani ya mkoa wa Kagera na nje ya nchi  kushiriki kwa wingi katika wiki hiyo.
 
Mkuu huyo amesema  wiki hiyo ya Kagera inayotarajia kuanza Agost 12 hadi 17 mwaka huu ambapo kutakuwa na shughuli mbali mbali ikiwemo maonyesho ya Taasisi mbali mbali watu binafsi wanaofanya shughuli mbalimbali za kiuchumi yatakayofanyika katika viwanja vya Gymkhana manispaa ya Bukoba .
 
Amesema  kuwa  agost 15 mwaka huu Kongamano la wadau wa uwekezaji litaendelea ambapo tarehe 16 mwaka huu wiki hii ya Kagera inatarajia kufungwa rasmi na Waziri wa Nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji Mhe. Angela Kairuki na mara baada ya wiki hiyo kufungwa rasmi wadau mbali mbali wa uwekezaji watapata nafasi ya kwenda kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii pamoja na fulsa mbalimbali za uwekezaji zilizomo mkoani kagera hadi Agost 17 mwaka huu.

Wiki ya Uwekezaji Kagera imebeba kauli mbiu isemayo ‘’Kagera: Eneo la Kimkakati kwa uchumi wetu na Afrika Mashariki” kauli mbiu inayolenga kuonesha mkoa wa Kagera ulivyo kitovu cha uchumi wa nchi za afrika mashariki na kati katika kuyafanya  masoko ya nchi hizo za Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya sudani kusini, na jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambapo soko hilo lina wingi wa watu wasiopungua milioni 190.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger