Wednesday, 3 July 2019

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano 3 July



















Share:

Tuesday, 2 July 2019

NUNDU APIGA HESABU ZA UBUNGE JIMBO LA TANGA 2020


Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano katika serikali ya awamu ya nne Mhandisi Omari Nundu ametangaza nia ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Tanga mwaka 2020 mara baada ya kipenga kutangazwa rasmi.

Mhandisi Nundu alitangaza nia hiyo wakati wa halfa ya kukabidhiwa vifaa vya Hospitali ya wilaya ya Tanga vilivyotolewa na wadau wa maendeleo mkoani Tanga kupitia magroup ya mitandao ya kijamii ya Whatsup.

Alisema kwamba wakati ukifika wa kuchukua fomu atafanya hivyo kwa kuchukua na kujaza ikiwemo kuirudisha ili kuwa tayari kwa ajili ya kinyang’anyiro hicho ili kuomba ridhaa ya wananchi wamchague ili awatumikie.

Mhandisi Nundu ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) kwa kipindi cha miaka mitano kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 kubwagwa na mgombea kutoka Chama cha Wananchi (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku.

“Labda niwaambie kwamba ikifika mwaka 2020 wakati wa kugombea nitachukua fomu nitazijaza na kugombea lakini kwa sasa hamtoniona nikigawa fedha kwa watu elfu ishirikiniishirini wala futari “Alisema Waziri huyo wa zamani

“Nimesikia maneno mtaani yanapita kwamba Nundu anataka kugombea ubunge niwaambie kwamba ikifika mwaka 2020 wakati wa kugombea nitachukua fomu nitaijaza na kurudisha”Alisema

Aidha alieleza kwamba hatawapa fedha watu lakini kwenye suala la maendeleo atashirikiana na wananchi kuhakikisha yanapatikana kwa kutatua baadhi ya changamoto.

“Nitasimamia suala la maendeleo mpaka hatua ya mwisho sasa tuna Rais ambaye anasaidia na kusukuma maendeleo kwa kasi kubwa kwani matunda yake yameonekana kwenye sekta mbalimbali”Alisema

Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema kwamba niwashukuru wote waliochangia vifaa hivyo vya matumizi ya hispiotali nikiri hivi sasa tutakuwa tunapokea vifaa kwa utaratibu wa kiserikali.

Mayeji alisema kwamba wao serikali wanapokea misaada yoyote ile hasa isiyo na masharti watapokea na wanaingiza kwenye matumizi hawana sababu yoyote ya kukataa kitu ambacho kimekuwa kikitolewa na wadau.

Watawakabidhi wataalamu waugavi kwa ajili ya kuvipokea huku akieleza kwamba wao kama serikali hawana masharti ya kutokupokea msaada wowote ambao umekuwa ukitolewa.

“Kama kuna mtu anahitaji kutoa msaada kwenye Jiji la Tanga tupo tayari kupokea lakini kikubwa tufuate utaratibu ambao unatakiwa kwa kupeleka kunakohusika na watapokea na kupeleka kwenye matumizi yanayokusudiwa “Alisema Mkurugenzi huyo.

Alisema wamevipokea na vitatumika kwenye matumizi yalyokusudiwa ili viendelee kutumika kwa kuwekewa uangalizi mzuri wa matumizi.
Share:

Picha : MDAU WA BLOG ZA KIJAMII MABULA KUTOKA NHIF TANGA AACHANA NA UKAPERA



Mdau wa Blog za Kijamii Peter Mabula kutoka ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) kushoto akiwa na Mkewe Jenipher Peter wakiingia kwenye Ukumbi wa Regail Naivera mara baada ya kufunga ndoa kwenye Kanisa Katoliki la St.Anthony Chumbageni Jijini Tanga
Mdau wa Blog za Kijamii Peter Mabula kutoka ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) wa pili kutoka kushoto akiwa na Mkewa Janipher Peter wakiwa na wasimamizi wao.
Mdau wa Blog za Kijamii Peter Mabula kutoka ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) wa pili kutoka kushoto akiwa na Mkewa Janipher Peter wakiwa na wazazi na ndugu.
Mdau wa Blog za Kijamii Peter Mabula kutoka ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) wa pili kutoka kushoto akiwa na Mkewa Janipher Peter wakiwa na wanafamilia.
Sehemu ya wageni waliokuwepo kwenye Sherehe hiyo ya harusi hiyo kulia ni Mhandisi Geofrey Hilly ambaye ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa).
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu katika aliyevaa suti akiwa na watumishi wa Mfuko huo wakati wa sherehe ya Harusi ya mtumishi mwenzao Peter Mabula.
Alawi Kupaza wa NHIF Tanga akitoka kumpongeza Bwana Harusi.
Wafanyakazi wanzake na Peter Mabula wakimpongeza.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akitoa nasaha kwa Bwana Harusi Peter Mabula kushoto ni Mhasibu wa NHIF Mkoa wa Tanga Hellena Manyanda.
Msimamizi wa NHIF Ofisi ya Tanga Dinna Mlwilo akizungumza wakati wa sherehe hiyo kulia ni Maneja wa NHIF Mkoa wa Tanga Ally Mwakababu 
Mhasibu wa NHIF Hellena Manyanga akiwa na watumishi wenzake
Share:

MAONESHO YA 43 YA BIASHARA YA KIMATAIFA KUFUNGULIWA

 Afisa Mwandamizi wa Malipo, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma,(PSSSF), Bi.Nyangi Masalu (kulia), akimuhudumia aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Kuendeleza Biashahara Nchini (Tan Trade), ambaye sasa ni Mstaafu na Mwanachama wa PSSSF, Bi.Jacqueline Mneney Maleko (kushoto), alipofika kwenye banda namba 13 la PSSSF/NSSSF viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi hii leo Julai 2, 2019.
Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Donald Peter Maeda (kulia), akimsikiliza Mwanachama huyu aliyefika banda la Mfuko kupatiwa huduma.
 Mkurugenzi wa banda la PSSSF Bi.Eunice Chiume (kushoto), akimsikiliza Mwanachama wa Mfuko huo, aliyetembelea banda hilo kupatiwa huduma.
Muonekano wa banda namba 13 la PSSSF.
 Afisa Matekelezo PSSSF, Bi. Getrude Athanas (kulia), akimuhudumia Mwanachama wa Mfuko aliyefka yeye na familia yake kwenye banda la PSSSF ambalo linatumika kwa ushirikiano na NSSSF.
 Afisa Matekelezo PSSSF, Bi. Getrude Athanas (kulia), akimuhudumia Mwanachama wa Mfuko aliyefka yeye na familia yake kwenye banda la PSSSF ambalo linatumika kwa ushirikiano na NSSSF.
Afisa Uhusiano Mwandamizi PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (aliyekaa), kwa kushirikiana na Afisa Mafao, wa Mfuko Bw. Salvatory Matemu kutafuta taarifa za michango ya Mwanachama (hayupo pichani).
Afisa Uhusiano Mwandamizi PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (kushoto) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Sebera Fulgence wakibadilishana mawazo wakati Bw. Sebera ambaye ni Mwanachama wa PSSSF alipotembelea banda la Mfuko kupata taarifa za michango yake.
Share:

MKUTANO WA 23 WA TAASISI ZA MAWASILIANO AFRIKA MASHARIKI (EACO) WAANZA JIJINI MWANZA


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wapili kushoto), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasilkiano Tanzania (TCRA), Mhandisi James M. Kilaba (watatu kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya (TCRA), Dkt. Jones Killimbe (wanne kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa EACO Dtk. Ally Yahya Simba(wakwanza kulia) na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Mawasiliano Bw.Mulembwa Munaku. (wakzwanza kushoto), baada ya kufungua mkutano wa 23 wa Taasisi zinazosimamia Mawasiliano Afrika Mashariki (EACO), utakaofuatiwa na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 26 wa EACO jijini Mwanza Julai 1, 2019
Muwakilishi wa Umoja wa Shirika la Posta Duniani (upu), Kusini mwa Afrika na Asia, Bi. Gladys Mutyavaviri ambaye
alimwakilisha Katibu Mkuu wa upu, akizungumza kwenye mkutano huo wakati wa ufunguzi.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James M. Kilaba, akizungumza na waandishi wa habari kufafanua baadhi ya mambo kuhusu mkutano huo.
Wajumbe kutoka Burundi, wakisikiliza hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Wajumbe kutoka Kenya, wakisikilza hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Wajumbe kutoka Rwanda, wakisikiliza hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Wajumbe wenyeji Tanzania, wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri Mhandisi Nditiye wakati akifungua mkutano huo.
Wajumbe kutoka Uganda, wakisikilzia hotuba ya Mhe. Naibu Waziri.
Mhe. Naibu Waziri Mhandisi Nditiye na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka mataifa wanachama wa EACO. 
***
MKUTANO wa 23 wa Taasisi zinazosimamia Mawasiliano kwa Nchi za Afrika Mashariki, (EACO) umeanza leo Julai 1, 2019 jijini Mwanza.

Sambamba na mkutamno huo pia wajumbe watashiriki  Mkutano Mkuu wa 26 wa EACO ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kuiweka Afrika Mashariki katika eneo la Uchumi wa Kidijitali".Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi, Atashasta Nditiye, ndiye aliyefungua mkutano huo utakaodumu hadi Julai 5, wenyeji ni Tanzania, pamoja na mataifa mengine ya WAC, ambayo ni Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. 

Share:

KAMPUNI YA TIGO TANZANIA NA TECNO WAZINDUA SIMU MPYA



Meneja wa Bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga, (kushoto) akionyesha kwa waandishi wa habari simu mpya za Smartphone aina ya TECNO S3 na TECNO R7, wakati wa uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Saba Saba jijini Dar es Salaam. (kulia) ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya.
Meneja wa Bidhaa za intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga, (kushoto) akimsikiliza Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya (kulia) wakati akionyesha kwa waandishi wa habari simu mpya za Smartphone aina ya TECNO S3 na TECNO R7, wakati wa uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Saba Saba jijini Dar es Salaam leo
Meneja wa Bidhaa za intaneti wa Tigo,Mkumbo Myonga, (kushoto) akimkabidhi zawadi ya simu aina ya TECNO S3 mmoja wa waandishi wa habari waliojishindia zawadi ya simu wakati wa uzinduzi simu hizo uliofanyika katika viwanja vya Saba Saba.jijini Dar es Salaam (kulia) ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya.
Meneja wa Bidhaa za interneti wa Tigo, Mkumbo Myonga, (kushoto) akiwa na waandishi wa habari waliojishindia zawadi ya simu za TECNO s3 na TECNO S7 wakati wa uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Saba Saba. (kulia) ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya.


*Kuwezesha mteja kupata Intaneti bure kwa mwaka mmoja

Kampuni inayoongoza kwa ubunifu wa kidigitali ya Tigo kwa kushirikiana na kampuni ya kimataifa ya kutengeneza simu za kisasa ya TECNO Mobile ,zimezindua aina mbili mpya ya simu janja za kisasa (smartphones) aina ya TECNO S3 na TECNO R7, katika soko la Tanzania,ambazo zitapatikana kwa bei nafuu na kuwawezesha wateja kufurahia matumizi ya Intaneti kupitia aina za vifurushi watavyochagua kujiunga nayo.

Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika leo katika uwanja wa maonyesho ya Saba Saba,Meneja wa Bidhaa za Intaneti wa Tigo Tanzania,Mkumbo Myonga,alisema kuzinduliwa kwa simu mpya kwa ushirikiano na kampuni ya TECNO Mobile, kwa mara nyingine kunadhihirisha mkakati wa kampuni ya Tigo katika ubunifu wa kidigitali nchini na kufanikisha kuongeza watumiaji wa simu janja,watumiaji wa huduma za data na interneti ya kisasa ya 4G.

“Tunayo furaha kushirikiana na TECNO Mobile leo kuzingua aina mbili za simu janja za kisasa kwa mwaka huu wa 2019.Simu aina ya TECNO S3 na TECNO R7 ni simu zinazatikana katika mtandao wa Tigo pekee katika soko na zinapatikana kwa gharama nafuu ambazo wateja wengi wanamudu kuzinunua”,alisema Myonga.

Myonga alieleza kuwa Tigo inatoa MWAKA MMOJA WA BURE wa kutumia internet kwa wateja watakaozinunua ambapo watakaonunua simu aina ya TECNO R7 watapata (GB54) ambazo zinawezesha matumizi ya internet ya 4G na inauzwa kwa bei ya shilingi 124,900/-.

Kwa wateja watakaonunua simu aina ya TECNO S3,ambayo inawezesha matumizi ya internet ya 3G,watakuwa na uhuru wa kuchagua ofa wanayotaka, ya kwanza MWAKA MMOJA WA BURE wa kutumia internet kutokana na kupatiwa GB 48 na gharama ya kununua simu iyo ni shilingi 95,000/-.Ofa ya pili kwa kunua simu inayouzwa shilingi shilingi 74,900/- na kujipatia internet yenye GB3 ambayo inawezesha mteja kuitumia miezi mitatu bure.Simu hizi mpya katika soko la Tanzania zinapatikana katika maduka yote ya Tigo nchini na zitapatikana katika banda la maonyesho la Tigo lililopo katika uwanja wa maonyesho ya Saba Saba.

Kwa upande wake,Meneja Uhusiano wa kampuni ya TECNO Mobile, Eric Mkomoya, alisema kuzinduliwa kwa simu aina ya TECNO S3 na TECNO R7 kupitia mtandao wa Tigo umelenga kuwezesha wananchi wengi kutumia simu janja na kuweza kufurahia mapinduzi ya ubunifu wa kidigitali ya matumizi ya simu hizi.

“Simu aina ya TECNO R7 imetangenezwa ikiwa na kioo cha ukubwa wa inchi 5,ina scanner ya kisasa,kamera yenye uwezo wa mega 5 upande wa mbele na nyuma na flashi inayowezesha kuchua picha kwa kiwango cha ubora wa juu,imetengenezwa kwa ubunifu wa tekbolojia mbalimbali za kisasa zinazowezesha matmizi ya internet na kupiga picha.Simu ya aina ya TECNO S3 imetengenezwa kwa teknolojia za kisasa zinazowezesha matumizi ya teknolojia ya Android Go OS ,inao ukubwa wa kioo cha mbele cha inchi 4,inawezesha matumizi ya teknolojia za GPS na dual SIM,ambazo zimeongezwa katika simu za Tecno tolea la sasa hivi,”alisema Mkomoya.

Simu zote za TECNO S3 na TECNO R7 zina waranti ya miezi 13.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger