Tuesday, 2 July 2019

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne 2 July





















Share:

Monday, 1 July 2019

Tanzania na Nchi ya Falme za Kiarabu Zakubaliana kuimarisha hali ya usalama katika nchi za Somalia na Sudan.

Tanzania na Nchi ya Falme za Kiarabu zimekubaliana kuendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika masuala ya usalama wa eneo la Ghuba na bahari ya Hindi pia kusaidia kuimarisha hali ya usalama katika nchi za Somalia na Sudan.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi alipomtembelea na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Umoja wa Falme za kiarabu Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan.

Katika Mazungumzo hayo wawili hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha udugu wa muda mrefu baina ya mataifa hayo mawili ikiwa ni pamoja na kufufua mazungumzo ya Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) ambayo kwa mara ya mwisho yalifanyika katika Mji wa Abu Dhabikatika Umoja wa Falme za Kiarabu ili kufufua na kutekeleza makubaliano ikiwa ni pamoja na kuangalia fursa za kiuchumi kwa faida ya pande zote mbili.

Akizungumza mara baada ya mazungumzo hayo Waziri Palamgamba John Kabudi amesema pamoja na masuala mbalimbali waliyokubaliana pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Umoja wa Falme za kiarabu Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan ameahidi kufanya mazungumzo na Ubalozi wa Falme za Kiarabu uliopo Nchini Tanzania ili kuharakisha matayarisho ya Ubalozi huo kuhamia Dodoma baada ya serikali ya Tanzania kuupatia ubalozi huo eneo la kujenga ubalozi wa Nchi hiyo mjini Dodoma bure.

Waziri Kabudi ameongeza kuwa mazungumzo hayo yamekuwa ya manufaa kwa pande zote mbili na kwamba yataendelea kuimarisha mahusiano baina ya Nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na kufungua fursa za kibiashara kwa ajili ya maendeleo ya mataifa hayo.

Katika hatua nyingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba John Kabudi akizungumza wakati akihitimisha ziara yake Nchini China,amesema ziara hiyo imekuwa ya manufaa kiuchumi kwa Tanzania ambapo tayari wawekezaji takribani 150 wanatarajiwa kuwasili nchini Tanzania kwa nia ya kuangalia maeneo mbalimbali ya uwekezaji mapema mwezi septemba wakitanguliwa na ujumbe wa watu 10 mwezi Julai 2019,hii ikiwa ni kipindi kifupi sana mara baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuhudhuria mkutano wa kwanza wa maonesho ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika uliofanyika katika mji wa Chanshang katika jimbo la Hunan,Nchini China.

Aidha ametanabaisha kuwa tayari wamepatikana wawekezaji wanaotaka kujenga nyumba ya kulala wageni yenye vyumba mia tatu katika mji wa Karatu ulioko mkoani Manyara kwa nia ya kuhamasisha watalii hususani kutoka China ambao wanatarajiwa kuongezeka maradufu kufuatia hatua ya Tanzania kuweka msisitizo katika kutangaza vivutio vyake vya Utalii.

Pia Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Beijing kimekubali ombi la Waziri Kabudi la kutaka kuongeza idadi ya wanafunzi watakaokwenda kusoma chuoni hapo kutoka 20 hadi kufikia idadi 40 nafasi zitakazotolewa kwa ufadhili wa chuo hicho kila mwaka ili kuandaa nguvu kazi ya kutosha wakati Tanzania ikijiandaa kuingia katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.


Share:

Katibu Mkuu CCM Atoa ONYO Kwa Viongozi Wadokozi wa Mali za Chama Hicho

Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, amekemea viongozi wenye uchu na mali za chama, akiagiza waondolewe ili kuepusha migogoro isiyokuwa na tija ndani ya chama hicho.

“Msiwavumilie hawa viongozi wenye uchu na mali za chama. Wafukuzeni wote. CCM haina uhaba wa wanachama na kila mwanachama ana haki ya kuongoza. Hizi tabia za kulindana na kukingiana vifua ndizo zilizotufikisha hapa,” alisema.

Bashiru ameyasema hayo katika mkutano wa wanachama wa Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam jana.

Dk. Bashiru alisema kuna taarifa za kuwepo migogoro ya viongozi kugombania mali za chama kama ilivyo katika Kata ya Sinza, hasa Sinza B, suala ambalo linatakiwa kushughulikiwa.

Aliwataka wanachama na viongozi kuhakikisha wanatunza mali za chama na kuzilinda, pia kufuata utaratibu mpya uliowekwa, ambao unahitaji malipo yote yatumie mfumo rasmi tofauti na ilivyokuwa zamani.

“Kuna baadhi ya viongozi wanavuruga mfumo, hawalipi kwa kutumia ‘control number’, bado wanaendelea kupokea fedha taslimu na kuzipangia matumizi kiholela. Wengine wanasema mabanda hayana watu kumbe yana watu, wanafanya kama mali yao, hawa hawavumiliki,” alisema.

Alieleza kuwa kwa sasa hawatarajii kupokea fedha kutoka kwa matajiri, na kwamba chama kitaendelea kutumia rasilimali na miradi yake kujipatia kipato kujiendesha.


Share:

Zitto Kabwe Apasua Jipu Kutekwa Kwa Msaidizi Wake.

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo), Zitto Kabwe ameitaka Serikali ya Tanzania kuangalia kwa uzito suala la kutekwa kwa raia wa Kenya anayeishi Tanzania, Raphael Ongagi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Julai 1, 2019 jijini Dar es Salaam, Zitto amesema masuala ya utekaji yamekuwa yakileta taswira mbaya kwa nchi ya Tanzania.

Amesema Tanzania haipaswi kuwa na taswira hiyo kwa mataifa mengine hasa nchi jirani ambazo tumekuwa tukishirikiana nazo katika mambo mengi.

Kutokana na hali hiyo, Zitto amewataka watekaji hao kumwachia huru kwani hana taarifa zake wanazozihitaji.

Raia huyo wa Kenya anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam, wakati akitoka shuleni kwa watoto wake kwenye kikao cha wazazi.

“Siku mbili baada ya Raphael kutekwa, akaunti zangu za mitandao ya kijamii zilidukuliwa na Raphael alikuwa na password zangu, hata hivyo hana taarifa zozote juu yangu hivyo ninawaambia watekaji hawawezi kupata taarifa zozote juu yangu kutoka kwa Raphael kwasababu watamtesa bure na hana taatifa ambazo anaweza kuwapa.

‪“Naamini wananisikia, hivyo wamuachie na kama kuna taarifa zozote wanazoona zina makosa waniite mwenyewe kwa taratibu za serikali mimi nitawapa hizo taarifa,” amesema Zitto

Amesema kuna watu wamefikia kusema rasilimali fedha zake zote zinapita kwa Raphael ambapo amesema hahusiki na chochote ni vyema wakamuita mwenyewe kama hilo ndiyo dhumuni lao.

Akielezea namna alivyokutana na Raphael, Zitto amesema ni raia wa Kenya ambaye tangu mwaka 2002 alikuja nchini na alipata marafiki wengi wa Tanzania na hata kufunga ndoa na Mtanzania.

“‪Baada ya kuamua kuingia kwenye biashara aliendelea kuwa mtu wangu wa karibu na mpaka anatekwa tumekuwa bado ni watu wa karibu hakuwa anajihusisha na siasa kwa namna yoyote,” amesema Zitto.

Hata hivyo, Zitto amesema anawasihi watekaji hao wamuache Raphael mahali kisha wao watakwenda kumchukua.


Share:

Fahamu Chanzo Halisi cha Kupungukiwa Nguvu za Kiume

Unafahamu kwa kina tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume na  maumbile ya kiume kusinyaa?

Wanaume wengi kwa sasa wanasumbuliwa na tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume na maumbile  kuwa mafupi na wengi wao huamua kutafuta tiba ili waweze kujilejeshea nguvu zao za asili bila kujua ni nini chazo cha hilo tatizo 

Tambua kuwa hakuna dawa ya kuongeza maumbile ya kiume  kama  ulikuwa mdogo  tangu unazaliwa, labda kama tatizo limeazia ukubwani kwa kujichua ( kupiga punyeto)  au kutokana na magonjwa 

Pia hakuna dawa ya kuongeza nguvu za kiume kama tatizo umezaliwa nalo bali zipo tiba za kutibu na ukapona matatizo hayo kama yameanzia  ukubwani kutokana na sababu zifatazo ;
1,Unene kupita kiasi 
2.Kuvaa nguo za kubana 
3.Magonjwa ya moyo,kisukar,presha,vidonda vya tumbo,ngiri,tumbo kuunguruma na kujaa gesi,kupiga punyeto,Msongo wa mawazo.

Haya ndo mambo makuu yanayosababisha tatizo hilo. kwa ushauri zaidi , piga simu 0683645920


Share:

Waziri wa Nishati: Tumieni Umeme Kuanzisha Miradi Ya Maendeleo

Na Veronica Simba - Chato
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewaasa wananchi wa Kitongoji cha Mwamagili, Wilaya ya Chato, mkoani Geita kutumia umeme aliowawashia rasmi jana, Juni 30, 2019 kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Akizungumza na wananchi hao muda mfupi kabla ya kuwasha umeme katika nyumba ya mkazi wa kitongoji hicho, Kashonele Kagodoro, Dkt. Kalemani aliwaambia endapo watautumia ipasavyo, hali zao za maisha zitaboreka zaidi.

“Umeme huu siyo kwa ajili ya kuwasha taa peke yake. Anzisheni miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo mashine za kukoboa na kusaga nafaka, saluni za kike na kiume na miradi mingine mbalimbali ili kuinua kipato chenu hivyo kuboresha maisha yenu.”

Aidha, Waziri Kalemani ambaye pia ni Mbunge wa eneo hilo (Chato), aligawa vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) kwa nyumba zote 38 za kitongoji hicho, ambazo zilikuwa bado hazijaunganishiwa umeme ikiwa ni sehemu ya kuwahamasisha wananchi husika kulipia gharama ndogo ya shilingi 27,000 tu ili waunganishiwe nishati hiyo.

“Kwa kutumia kifaa hiki cha UMETA, mtaepuka gharama za kutandaza nyaya katika nyumba zenu. Niwaombe na kuwahamasisha muendelee kulipia kwa sababu bei ya kuunganishiwa umeme ni ndogo sana; shilingi 27,000 tu,” asisitiza Waziri.

Katika hatua nyingine, Waziri amelipia gharama za kuunganisha umeme katika Kanisa lililopo eneo hilo, ambayo pia ni sehemu ya kuhamasisha viongozi wa taasisi mbalimbali za umma kulipia gharama za umeme ili ziunganishwe.

Wananchi kadhaa waliopata fursa ya kueleza maoni yao mbele ya Waziri Kalemani, walipongeza jitihada za Serikali katika kuwapelekea nishati ya umeme.

“Hii ni ndoto kwangu. Sikutegemea. Tangu nizaliwe nilikuwa nikiona umeme maeneo ya mijini nilikowahi kutembelea. Sikuwahi kuwaza kuwa iko siku umeme utawashwa kijijini kwetu, tena katika nyumba yangu,” alisema Kagodolo.

Waziri Kalemani yuko Chato kwa ziara ya kazi.


Share:

Jinsi ya kukabiliana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za kiume tunakuwa katika uwanja mpana zaidi wa tafakari za kibaiolojia na kisaikolojia walizonazo wanaume.

Lakini kwa kufupisha mlolongo wa mambo sehemu kuu tatu zinaweza kabisa kukidhi mchanganuo mzima wa jinsi tatizo hili linavyowasumbua wanaume wengi duniani.

Sehemu kubwa ya malalamiko ya wanaume katika sakata hili yanagusa zaidi maeneo matatu ambayo ni kukosa msisimko, kushindwa kurudia tendo na kukosa kabisa nguvu, huku kufika kileleni mapema kukihusishwa pia kama pacha wa janga hili ambalo linawasumbua zaidi wanaume.
 
Sababu zinazosababisha tatizo la nguvu za kiume zinawekwa katika makundi mawili.
*Matatizo ya kiafya ya mwili (organic causes).
*Matatizo ya kisaikolojia ( Psychological cause).
 
Matatizo ya kiafya:
  1. Magonjwa ya kisukari, (diabetes mellitus).
  2. Ugonjwa wa presha (blood pressure).
  3. Matatizo ya tezi dume (kama mtu amewahifanyiwa operation) (prostatectomy surgery),
  4. Upungufu au mvurugiko wa uzalishaji Homoni za uzazi (hormonal insufficiencies /hypogonadism).
  5. Athari za matumizi ya dawa kwa muda mrefu (drug side effect).
Matatizo haya kwa pamoja hupelekea mishipa ya damu kuziba na mwishowe misuli inakosa nguvu za kuweza kusimama na hatimae uume husinyaa.
 
Tatizo la Kisaikolojia(Psychological reasons)
Ukweli wa mambo ulioibuliwa na wanasaikolojia umebaini wale wote wanaolalamikia/lalamikiwa kuwa hawana nguvu iwe ya kufika kileleni mapema, kutokuwa na msisimko na kushindwa kurudia tendo wamekosa maarifa tu ya kufahamu na hawaijui miili yao na wanaishi kwa kusikia zaidi ya kujitambua.

Watu hao kiuhalisia wanakabiliwa  na matatizo ya kimawazo, kama vile migogoro katika mahusiano, matatizo ya kimaisha na mambo mengine
 
Dalili za tatizo hili
  1. Kushindwa kusimamisha uume mara kwa mara,
  2.  Uume kulala(kusinyaa) katikati ya tendo la ndoa.
  3.  kushindwa kusimamisha ipasavyo.
  4. Kufika  haraka mara baada ya kuanza
  5. kujamiiana.
  6.  Maumivu ya misuli ya uume wakati wa tendo la ndoa.

Magonjwa yanayosababisha tatizo hili:
*kisukari (diabetes)
*presha (blood pressure)
*matatizo yafigo (kidney disorders)
*matatizo ya kisaikologia(psychological cause).
* upungufu wa homoni za uzazi (hormonal insufficiencies).
* Matumizi ya dawa kwa muda mrefu (drug side effect).
* Uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi.
* matatizo ya tezi dume.

Matatizo haya yote Yanatibika kwa dawa. Wasiliana Nami kwa msaada zaidi: 0620510598 au 0759208637

 


Share:

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) yaanza kupokea maombi ya mikopo

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), leo inafungua dirisha la uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020.

Bodi hiyo imeboresha utoaji elimu kwa waombaji wapya pamoja na kutembelea kambi za jeshi walizopo wanafunzi kuwapa maelekezo ya kujaza fomu kabla ya kurejea majumbani kuomba mikopo.

Aidha, mwaka huu, wamefanya maboresho katika muongozo wa utoaji mikopo kwa umri wa waombaji waliopo vyuoni kwa kuongeza umri mpaka miaka 35 badala ya 33 na wanaruhusiwa waliomaliza miaka mitano iliyopita na si miaka mitatu.

Ofisa Mawasiliano Mwandamizi wa bodi hiyo,Veneranda Malima amesema hayo katika banda la bodi hiyo kwenye viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam maarufu Sabasaba.

Alisema katika maonesho hayo wamesogeza huduma kwa jamii na wadau kwa kutoa taarifa za wanaorejesha mikopo, wanaotaka kujua salio na wanaotaka kulipa huku wanafunzi wanaotaka kufahamu kuhusu fedha zao za mafunzo ya vitendo watahudumiwa.

Malima alisema lengo la uboreshaji huo ni kutoa nafasi kwa wanufaika wengi kupata mikopo hasa kwa waliopata matatizo kama ya kufiwa na wazazi hivyo kuwa na uhitaji.


Share:

Afcon 2019: Taifa Stars Kuvaana na Algeria Leo

Timu  ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, leo inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Algeria katika mchezo wa tatu wa Kundi C wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019), inayoendelea jijini Cairo nchini Misri.

Michuano hiyo ambayo ilianza Juni 21 na kutarajiwa kumalizika Julai 19, mwaka huu, nchini humo, timu ya Tanzania haina matumaini ya kutinga hatua ya 16 bora, hata kama itashinda dhidi ya Algeria, baada ya kuanza vibaya.

Hilo linatokana na Taifa Stars kupoteza michezo miwili dhidi ya Senegal na Kenya, ambayo ilifungwa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Senegal, kisha kupigwa mabao 3-2 na jirani zao Kenya.

Kwa matokeo hayo, mchezo wa leo kwa Taifa Stars utakuwa wa  kukamilisha ratiba ya michuano hiyo  kutokana na kutofanya vizuri michezo yake miwili.

Taifa Stars iliyofanikiwa kufuzu michuano hiyo, baada ya kuifunga Uganda  mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano uliochezwa Machi 24, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, imeonekana kushindwa kuhimili mikikimikiki ya Afcon .

Matokeo hayo yaliifanya Tanzania kumaliza nafasi ya pili Kwa kutoka Kundi L, kutokana na pointi,  nyuma ya Uganda aliongoza kundi hilo kwa pointi 13, Lesotho ilimaliza nafasi ya tatu kutokana na pointi sita na Cape Verde ilishika mkia kwa  pointi tano.   

Historia ya timu ya Tanzania  kufanya vibaya Afcon inajirudia baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria kushika mkia katika Kundi A, lililoundwa na mwenyeji, Misri na Ivory Coast.


Share:

WANAUME WAPEWA BURE DAWA NGUVU ZA KIUME

IMEELEZWA kuwa asilimia 85 ya upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume unatokana na magonjwa ya moyo na kisukari, hivyo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeamua kuleta dawa za kurejesha nguvu hizo wakati wanaume wakiendelea na matibabu ya vishawishi.


Dawa hizo zinatolewa katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo Barabara ya Kilwa katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, ambapo taasisi hiyo katika banda lao wanatoa huduma bure ya upimaji, ushauri na dawa.

Akizungumza katika viwanja hivyo, Daktari bingwa na Mkuu wa Idara ya Utafiti na Mafunzo wa taasisi hiyo, Dk Pedro Pallangyo aliliambia gazeti hili kuwa wanatoa huduma za vipimo bure vya urefu, uzito, mapigo ya moyo, shinikizo la damu, sukari, kipimo cha umeme wa moyo (ECG), na kipimo cha utendaji kazi wa moyo (ECHO).

Alisema pia kuna mtaalamu wa lishe anayetoa ushauri bure wa lishe na ushauri na baada ya vipimo, watakaobainika kuwa na magonjwa ya moyo na magonjwa ambatano ya kifua, ganzi, shinikizo la damu na upungufu wa nguvu za kiume watapatiwa dawa.

“Kwa kiwango kikubwa upun- gufu wa nguvu za kiume unatokana na magonjwa ya moyo na kisukari huku chakula kikisababisha kwa kiwango kidogo cha asilimia tano, hivyo kwa wenye upungufu wa nguvu tuna dawa zitakazowasaidia kwa saa 24 hadi 48 wakati wakiendelea na matibabu ya chanzo cha ugonjwa,”alisema Dk Pedro.
Share:

ESRF YAANDAA WARSHA KUBORESHA MRADI WA PSDS 2006


Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida wakati wa warsha ya kitaifa ya utekelezaji wa mkakati wa maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki unaozingatia mchango wa sekta binafsi (EAC- PSDS) iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. (EAC- PSDS) iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa kitengo cha maendeleo ya sekta binafsi Ofisi ya Waziri Mkuu, Diana Makule akiwasilisha mada ya mtazamo wa jumla wa PSDS 2006 na matokeo ya utekelezaji wake wakati wa warsha iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa masuala ya tabia nchi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Martha Ngalowera akiwasilisha mada kuhusu uchakataji wa mazao ya kilimo katika mradi wa PSDS 2006 kwa kuangalia vifungu vinavyohusiana na tabia nchi kwenye warsha iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa warsha, Meneja Ufuatiliaji na Tathmini , Kituo cha Taasisi ya Maendeleo Endelevu (CSDI), Dk Isaack Nguliki akizungumzia biashara kuchagiza uchakataji wa mazao ya kilimo kwa kuangalia vifungu vinavyohusiana na tabia nchi katika PSDS kwenye warsha iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Bi. Rehema Mbugu kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)akiongoza majadiliano ya mtazamo wa jumla wa PSDS 2006 na matokeo ya utekelezaji wake wakati wa warsha iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Washiriki wakishiriki majadiliano wakati wa warsha ya kitaifa ya utekelezaji wa mkakati wa maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki unaozingatia mchango wa sekta binafsi (EAC- PSDS) iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mshehereshaji ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akisisitiza jambo wakati wa warsha ya kitaifa ya utekelezaji wa mkakati wa maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki unaozingatia mchango wa sekta binafsi (EAC- PSDS) iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akifafanua jambo wakati wa warsha ya kitaifa ya utekelezaji wa mkakati wa maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki unaozingatia mchango wa sekta binafsi (EAC- PSDS) iliyoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
**
Wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imejikita katika kutaka kuendeleza mkakati wa sekta binafsi (PSDS) 2018-2022, wenye lengo la kuweka mazingira mazuri ya biashara yatakayochochea ushindani ndani ya sekta binafsi kwa kuongeza uwekezaji, tija na biashara, Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imekutanisha wadau kuangalia namna ya kuboresha mkakati huo.

Katika warsha hiyo wadau walizungumzia na kuainisha mambo mbalimbali yenye lengo la kuuwezesha Mkakati huo kutoa mchango wenye uelewa wa mabadiliko ya tabia nchi, uzalishaji wenye msukumo wa kibiashara na uchakataji wa bidhaa za kilimo.

Dk. Tausi Kida Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), akifungua warsha hiyo mwishoni mwa wiki alitaka washiriki kuwa makini ili kuweza kuona namna gani wanaweza kuimarisha mkakati huo.

Akishawishi umakini katika warsha hiyo ya kitaifa ya utekelezaji wa mkakati wa maendeleo kwa nchi za Afrika Mashariki unaozingatia mchango wa sekta binafsi (EAC- PSDS), alisema bila umakini mchango wa mkakati huo hautaonekana.

Katika warsha hiyo wadau walizungumzia upenyo wa maendeleo endelevu katika uchakataji wa bidhaa za kilimo.

Warsha hiyo ikiwa ni sehemu ya awamu ya pili ya mradi wa kuendeleza kilimo katika nchi za Afrika mashariki unaoangalia mabadiliko ya tabia nchi na mahusiano ya kibiashara katika nchi hizo- (PACT EAC2). Mradi huo umekuwa ukiendeshwa na ESRF kwa kushirikiana na CUTS International yenye makao makuu yake mjini Geneva Uswisi.

Mkurugenzi huyo wa ESRF alisema kwamba toka mwaka 2015 mradi umekuwa ukifanya majadiliano ya kina kwa sekta mbalimbali ambazo nyingi ni mtambuka ili wadau wengi wawe wanajua kwa pamoja mabadiliko ya tabia nchi, mahusiano yao na uzalishaji, biashara, usalama wa chakula na viwanda vya kuchakata bidhaa za kilimo.

Kwa mujibu wa Dk Tausi warsha hiyo ilikuwa na lengo la kuwapa nafasi wadau wote kuangalia njia bora zaidi ya kuwezesha uchakataji endelevu wa viwanda vya bidhaa za kilimo ili kuvipa thamani kupitia sekta binafsi.

Mkurugenzi huyo aliwataka washiriki kujadili kwa kina mchango wa sekta binafsi katika kuchagiza uelewa wa mabadiliko ya tabia nchi, na uendelezaji wa kilimo biashara na usalama wa chakula katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

“Kutokana na ukweli huo napenda mazungumzo yetu ya leo yajikite zaidi katika kufanikisha mkakati wa sekta binafsi kuhusu maendeleo (PSDS) 2018-2022 kuhusu wajibu wake kuendeleza uchakataji wa bidhaa za kilimo endelevu utakaozingatia mabadiliko ya tabia nchi biashara na usalama wa chakula.” alisema Dk Tausi.

Katika warsha hiyo ambapo mada mbili ziliwasilishwa moja ikizingatia mabadiliko ya siasa na sheria nchini na mazingira ya sasa kuhusiana na mkakati huo wa kuwezesha ukuaji wa sekta binafsi na dhana ya uendelezaji wa kilimo biashara katika uhusiano na mabadiliko ya tabia nchi na nyingine.

Mada hizo zimetolewa na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu,wakiangalia PSDS ilivyowezeshwa kusaidia sekta binafsi kuchochea uelewa wa mabadiliko ya tabia nchi, kilimo biashara na uchakataji wa bidhaa za kilimo na usalama wa chakula.

Mada hizo ziliwasilishwa na Diana Makule wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Martha Ngalowera wa Ofisi ya Makamu wa Rais.
Share:

Heslb Online Application system now open 2019/20

HESLB  Online Application system now open 2019/20, heslb application, olams heslb go tz, maombi ya mkopo heslb 2019

HESLB has officially started to receive electronic Loan applications for Academic year 2019/2020

Welcome to Online Loan Application and Management System (OLAMS). ONLY Tanzanian Nationals are eligible to apply for higher education student loans. Kindly provide TRUE information about yourself and follow all the instructions to fill and submit your application package.
Applications for 2019/2020 Academic Year will be accepted from 01st-July-2019 and the deadline will strictly be 15th-August-2019 at 23:59 Hours.


  1. Kindly read carefully the Guidelines and Criteria for Issuance of Loans for 2019/2020 before applying; Download
  2. Click Apply for Loan for registration using your Form IV Index Number and year of completion;
  3. After Providing and confirming your Form Four Index number, you will receive your Control Number (99111xxxxxxx),
  4. Use the generated Control Number to Pay a Non-Refundable Application Fee of TZS 30,000.00 (Pay in-full, NOT by Instalments) through:

MPesa, Tigo Pesa, HaloPesa, Airtel Money, T-Pesa or EzyPesa

  • through Control Number

“generated by the system”

    • as reference number and thereafter you will receive a confirmation message (receipt);

    You can use your Control Number from OLAMS to pay application fee at any NMB, TPB or CRDB Bank Branch or respective Agents. Should you need any assistance, kindly refer to provided instructions or call HESLB Helpdesk through

+255 550 7910

  • ,

0736 665 533

  • or

0739 665 533

 

Apply Now

The post Heslb Online Application system now open 2019/20 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Katibu Mkuu Wizara Ya Kilimo (SMT) Mhandisi Mtigumwe Na Naibu Katibu Mkuu Wizara Ya Kilimo (SMZ) Bi Mansura Waongoza Kikao Cha Mashirikiano

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo (SMT) Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu (SMZ) Bi Mansura Mosi Kassim wameongoza kikao cha mashirikiano baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania katika sekta ya Kilimo.

Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya ofisi ya Makamu wa Rais Muungano kwa wizara zote za SMT na SMZ kukutana na kuzungumzia Mashirikiano baina yao.

Vikao kama hivyo hutuama kujadili kwa pamoja namna ya kutatua changamoto za Muungano zilizopo katika sekta ya Kilimo.

Katika kikao hicho kumejadiliwa kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali yaliyowekwa katika kikao cha makatibu wakuu wa sekta ya Kilimo kilichofanyika mwezi Machi, 2018.

Kadhalika, maeneo mengine ya mashirikiano yaliyojadiliwa ni pamoja na Maendeleo ya mazao, utafiti na mafunzo, huduma za umwagiliaji na Zana za Kilimo na Sera, na Mipango na uimarishaji wa takwimu.

Kikao kazi hicho kilifanyika tarehe 24 Juni, 2019 katika ofisi za wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar.



Share:

Watoroshaji dhahabu katavi kukiona

Mkuu wa mkoa wa Katavi  Juma Homera ameapa kupambana na wanaotorosha dhahabu huku mpaka sasa watu wawili wakishikiliwa na jeshi la polisi kwa kununua dhahabu kinyume cha sheria mkoani humo

RC Homera akiwa ziarani katika migodi mbalimbali ikiwemo Dilifu ambao ni mgodi wa wachimbaji wadogo na mgodi mkubwa wa Katavi na Kapufi mining  alieleza anachotaka wachimbaji wadogo wakauuze madini yao katika soko la madini la mkoa huo.

Homera alianza majukumu ya ukuu wa mkoa ikiwa soko limeshafanya biashara kwa kununua dhahabu gram 238, May 23/2019 jambo ambalo lilimfanya aanze kufatilia na kubaini dhahabu nyingi inayopatikana Mkoani Katavi inauzwa nje ya mkoa wa  Katavi nakupelekea soko hilo kusua sua.

Kufuatia jambo hilo limemfanya  Homera kuyafanyia kazi mapungufu ya soko hilo, mpaka sasa ununuzi na uuzaji wa madini ni Grams 6317.2 sawa na Kg 6 na Grams 317.2 yenye thamani ya Tshs.Million 519,155,127.56 zimenunuliwa kwa kipindi cha Mei na June 30/2019 na serikali kupata mrahaba (Royality7%) Tsh Milioni 36,340,858.92 na Service levy  0.3% Tsh.milioni 1,401,718.85.

Aidha ameimarisha mifumo ya Benk mbili katika soko hilo na ameendelea kuwa bana mablokers na wanunuzi wenye leseni na wachimbaji mbalimbali  kuhakikisha pia wanauza madini yao kwenye soko la mkoa ili tujenge uchumi wa Tanzania na kumuunga mkono Rais wetu Dkt.John Joseph Pombe Magufuli katika kuinua uchumi na miundombinu ya nchi hii kwa kulipa kodi


Share:

Ujangili Wapunguza Idadi Ya Faru Kutoka Zaidi Ya Elfu 10 Hadi 161 Pekee

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Imeelezwa kuwa  idadi ya wanyamapori aina ya  Faru weusi[Black Rhino]   imepungua kutoka faru   zaidi ya elfu  kumi kwa miaka 1970 mpaka 1980 na  kubaki faru   161 pekee  hadi sasa hapa nchini  kutokana na Ujangili.
 
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii Dokta  Hamis Kigwangalla wakati akizindua mpango kazi  wa kulinda na kutunza Faru weusi uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mipango jijini Dodoma.
 
Dokta Kigwangalla amesema kutokana na tishio kubwa la faru kutoweka hapa nchini kwa sababu ya   ujangili, serikali imeandaa mikakati kabambe ya kudhibiti ujangili hali ambayo imeanza kuzaa matunda na kuanza kusababisha faru kuongezeka  ambapo  serikali imetenga Dola milioni 61 sawa na zaidi ya Tsh.Bilioni 120 za kitanzania  kwa ajili ya utekelezaji wa mipango hiyo.
 
Aidha,Dokta Kigwangalla amesema sekta ya  utalii hapa nchini  huzalisha zaidi ya Dola za Marekani bilioni 2  ambazo huchangia asilimia 25%  ya fedha za kigeni  na kuchangia asilimia 17% ya mapato ya ndani ya nchi [GDP ]  na imetoa ajira rasmi laki sita[600,000]  na zisizo rasmi milioni mbili[2000,000] hivyo ulinzi wa wanyamapori  walio katika hatari ya kutoweka wakiwemo faru utaendelea kuimarishwa  na mpango wa serikali ni kuhakikisha  uzalishaji wa faru unaongezeka kwa kasi kwa miaka mitano ijayo.
 
Katika hatua nyingine ,Dokta Kigwangalla ameitaka jamii kuachana na mila potofu za kutumia pembe za faru kama  dawa za kuongeza nguvu za kiume kwani imani hizo hazina ukweli wowote na zinapaswa kupuuzwa.
 
Mtafiti kutoka   taasisi ya utafiti ya wanyamapori nchini,TAWIRI Dokta Edward Kohi  amesema kunahitaji teknolojia zaidi ili kuhakikisha faru anatunzwa   ambapo miaka ya 1998 waliingia kwenye tatizo la kutoweka hadi sasa kuna faru 161 wanaoweza kuhesabiwa na kuonekana.
 
Pia  ,Dokta Kohi ametaja malengo madhubuti ya  Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania,[TAWIRI ] ni Pamoja   kuongeza idadi ya faru si chini ya 5%  kwa mwaka,kuwa na uwezo wa kuhamisha faru kutoka eneo  moja hadi jingine,kuhakikisha ujangili wa faru uwe chini ya 1%     pamoja na kuwa na mfumo wa mawasiliano na mipaka mingine.
 
Naye mwakilishi kutoka  mfuko wa wanyamapori ulimwenguni[WWF] Dokta  Simon Lugandu amesema mradi wa kuhifadhi na kutunza  faru Tanzania unaendelea   katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya uhifadhi wa mazingira ‘
 
Ikumbukwe kuwa Tanzania ilishaanza   kutumia teknolojia ya kufuatilia faru ambapo mradi wa teknolojia hiyo ya kifaa chenye uwezo  wa kutoa  maelezo mwenendo wa faru  ,unagharimu dola za kimarekani 111,320  na unatekelezwa kwa ushirikiano na maafisa wa TANAPA ,Maafisa wa Shirika  la Wanyama la Frankfurt[FZS]na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania[TAWIRI]


Share:

Spika Mstaafu wa Bunge Pius Msekwa Aunga Mkono Tundu Lissu Kuvuliwa Ubunge

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa amedai uamuzi uliofanywa  na Spika wa Bunge Job Ndugai wa kumvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu uko sawa, kwani yeye alishawahi kuwavua Wabunge zaidi ya 50 katika kipindi chake, kwa kosa la utoro ndani ya Bunge.

"Uzoefu wangu mimi katika hili Spika yuko sawa kabisa, kwa sababu hata mimi mwenyewe nilishawavua Wabunge wengi kipindi cha uongozi wangu nawashangaa sana wanaohoji hatua hiyo, ni jambo la Kikatiba lililofanywa na Spika Ndugai" amesema Msekwa

"Mimi mwenyewe niliwavua wengi tu na wala sio mmoja, Wabunge wa Zanzibar walikiuka kifungu cha Katiba alichokinukuu Spika Ndugai, tena walikuwa kama 50 hivi wote nikawavua Ubunge na uchaguzi ulifanyikla tena." ameongeza Msekwa

"Inawezekana watu wakasema Tundu Lissu nchi nzima inajua kuwa anaumwa, lakini katiba haisemi kuwa lazima usikilize kutoka magazetini au mitandaoni inatakiwa Mbunge aandike barua." amesema Pius Msekwa

June 28 katika vikao vya kujadili miswada mbalimbali ya kisheria kwa ajili ya mwaka mpya wa fedha Spika Job Ndugai alitangaza kuwa jimbo la Singida Mashariki liko wazi kufuatia Mbunge wake kutotoa taarifa kuwa yuko wapi.


Share:

Afisa Mtendaji Mkuu wa Safaricom,Bob Collymore Afariki Dunia

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya simu ya Safaricom, Bob Collymore amefariki dunia. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Safaricom, matuti yamekuta Collymore asubuhi ya leo Jumatatu Juni 1, 2019 akiwa nyumbani kwake jijini Nairobi.

Vyombo vvya habari vya Kenya vimesema mwenyekiti wa kampuni hiyo Nicholas Ng'ang'a amesema afya ya Collymore ilikuwa mbaya kwa majuma ya hivi karibuni.

Collymore, alichukua likizo ya matibabu ya miezi tisa mwishoni mwa mwaka 2017 na kwenda Uingereza kwa ajili ya matibabu ya saratani na alirejea  Kenya Juni mwaka jana.

Collymore alianza kuongoza Safaricom mwaka 2010 kutoka kwa Michael Joseph ambaye kwa sasa ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo.

Mwaka 2017 wanahisa walipiga kura kuongeza mkataba wa Bob Collymore kwa miaka miwili baada ya mkataba wake kuisha. Mkataba aliokuwa akiufanyia kazi ulikuwa unatarajiwa kufikia tamati mwaka 2020 na kumfanya kuwa Mkurugenzi aliyekalia kiti hicho kwa muda mrefu zaidi.

Viongozi kadhaa wakiwemo Rais Uhuru Kenyatta wametuma salamu za rambirambi kwa familia kutokana na kifo hicho.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger