Saturday, 29 December 2018

Kikosi cha Yanga dhidi ya Mbeya City leo

Kikosi cha Yanga dhidi ya Mbeya City leo

Kikosi cha Yanga dhidi ya Mbeya City mechi ya ligi kuu Tanzania Bara TPL ikichezwa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

1.Ramadhan Kabwili
2.Paul Godfrey 
3.Gadiel Michael
4.Abdallah Haji
5.Kelvin Yondan
6.Feisal Salim
7.Ibrahim Ajibu
8.Haruna Moshi ‘Boban’
9.Heritier Makambo
10.Amis Tambwe
11.Mrisho Ngassa

#AKIBA – Klaus Kindoki
– Juma Abdul
– Cleofas Sospeter
– Maka Edward
– Deus Kaseke
– Pius Buswita
– Jaffar Mohammed.

The post Kikosi cha Yanga dhidi ya Mbeya City leo appeared first on KWATA UNIT Sports News.



from KWATA UNIT Sports News http://bit.ly/2Qauspl
via IFTTT
Share:

Kikosi cha Yanga dhidi ya Mbeya City leo

Kikosi cha Yanga dhidi ya Mbeya City leo

Kikosi cha Yanga dhidi ya Mbeya City mechi ya ligi kuu Tanzania Bara TPL ikichezwa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

1.Ramadhan Kabwili
2.Paul Godfrey 
3.Gadiel Michael
4.Abdallah Haji
5.Kelvin Yondan
6.Feisal Salim
7.Ibrahim Ajibu
8.Haruna Moshi ‘Boban’
9.Heritier Makambo
10.Amis Tambwe
11.Mrisho Ngassa

#AKIBA – Klaus Kindoki
– Juma Abdul
– Cleofas Sospeter
– Maka Edward
– Deus Kaseke
– Pius Buswita
– Jaffar Mohammed.

The post Kikosi cha Yanga dhidi ya Mbeya City leo appeared first on KWATA UNIT Sports News.



from KWATA UNIT Sports News http://bit.ly/2Qauspl
Share:

DED,WATUMISHI 12 MATATANI KWA KUTAFUNA BILIONI 2.9


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ulanga mkoani Morogoro, Yusufu Semguruka na watumishi 12 wanadaiwa kutafuna zaidi ya Sh bilioni 2.9 za Serikali.

Kutokana na hali hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, ameelekeza watumishi hao wavuliwe madaraka na mamlaka za nidhamu na vyombo vya dola vifanye uchunguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Jafo, alisema ofisi yake ilifanya uchunguzi maalumu kwa halmashauri 12 ikiwamo Ulanga.

Alisema malalamiko yalikuwa mengi kwa Ulanga kutoka kwa wananchi na Mbunge wa jimbo hilo, Goodluck Mlinga.

Alisema matokeo ya uchunguzi huo kwa halmashauri hiyo yamebaini matumizi mabaya ya fedha za Serikali zinazofikia Sh 2,980,172,763.60 na watumishi hao wasio waadilifu walikiuka taratibu za fedha, walihujumu na kufanya ununuzi hewa.

“Halmashauri imekuwa ikifanya udanganyifu katika taarifa za miradi ya maendeleo, kufanya manunuzi hewa, kutumia fedha tofauti na makusudio yaliyokusudiwa na udhibiti mbovu wa mapato ya Serikali,” alisema.

Aliwataja watumishi hao kuwa ni Semguruka, Mweka Hazina, Rajabu Siriwa, aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi katika halmashauri hiyo, David Kaijage, wahasibu Stanley Nyange, Isaack Salum, Johnson Mwanyombole na Saleh Mbogoso.

Aliwataja wengine kuwa ni wataalamu wa mifumo ya tehama katika halmashauri hiyo, Yasin Galahenga na Mohamed Said, Ofisa Mnunuzi, Willy Ndabila, Mhasibu wa Hospitali ya Wilaya ya Ulanga, Goodluck Mbata, Mganga wa Wilaya, Dk. Abdallah Risasi na Mfamasia wa Wilaya, Jackson Nyabusani.

JINSI WALIVYOTAFUNA FEDHA

Jafo alisema Semguruka alishindwa kusimamia sheria ya fedha za Serikali za Mitaa katika kudhibiti na kuweka mifumo ya kuhakikisha ziko salama kuanzia makusanyo hadi manunuzi.

“Hii ni pamoja na kushindwa kumsimamia mweka hazina wa halmashauri katika kuyatekeleza majukumu yake na hivyo kuisababishia hasara Serikali ya shilingi 2,980,172,763.60,” alisema.

Kwa upande wa Siriwa, alisema alichangia kuhujumu mapato ya halmashauri kwa kuweka utaratibu uliosababishia hasara.

“Kuidhinisha malipo ya shilingi 225,586,400 nje ya bajeti bila idhini ya ofisi ya Tamisemi, marekebisho ya bajeti hii yalihusisha posho za safari ya mkurugenzi shilingi 192,000,000. Kukusanya na kutopeleka benki shilingi 760,686,732.43.

“Kuandaa taarifa zenye udanganyifu kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotumia fedha za makusanyo ya ndani. Halmashauri inaripoti kupeleka shilingi 301,442,686 wakati uhalisia wamepeleka shilingi 113,406,106,34,” alisema.

Pia alisema amefanya udanganyifu katika fedha za mfuko wa vijana na akina mama baada ya halmashauri kuripoti kupeleka Sh 120,000,000 wakati uhalisia wakiwa wamepeleka Sh 31,500,000 kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018.

“Kukusanya fedha na kuzihujumu, mweka hazina ndiye aliyemjulisha Kaijage mapokezi ya shilingi 470,000,000 lakini mara tu walipozipokea walifanya hujuma ya kuzilipa fedha hizo kwa kampuni iliyowalipa,” alisema.

Kuhusu Kaijage, alisema wakati akikaimu nafasi hiyo Februari mosi hadi Februari 8, mwaka huu alihusika kuihujumu halmashauri kwa mapato ya Sh 470,000,000 yaliyopokelewa kutoka Kiwanda cha Kilombero Valley Teak na kuzirejesha kwa mlipaji siku hiyo hiyo waliyopokea.

“Pia alisaini hati ya malipo kumlipa Bahari Pharmacy kwa siku ambayo hakuwa Kaimu Mkurugenzi na Mkurugenzi alikuwepo,” alisema.

Kwa upande wa wahasibu, Nyange na Salum wao wameihujumu halmashauri kwa kutumia akaunti binafsi kupokea fedha za makusanyo pamoja na kuchukua fedha kutoka vituo vya makusanyo na kutozipeleka benki.

Alisema kwa upande wa Galahenga na Said, wao walishirikiana na wahasibu kurekebisha ankara na kufuta madeni bila idhini ya mkurugenzi.

“Hawa wameihujumu mapato ya halmashauri kwa kufanya marekebisho ya ankara za wateja bila idhini ya mkurugenzi wala maombi ya wateja shilingi 79,926,747, yaani wao ndio wanaomba na wao ndio wanaidhinisha marekebisho,” alisema.

Jafo alisema Ndabila alihusika katika ununuzi hewa wa dawa zenye thamani ya Sh 73,212,909.40 pamoja na kulipa fedha zaidi ya Sh 146,425,818.

Kuhusu Mbata, alisema aliandaa malipo na kusainisha mara mbili kwa watu tofauti huku akijua kufanya hivyo ni kuandaa malipo mara mbili kwa hitaji moja.

Pia alisema Dk. Risasi na Nyabusani walifanya njama ya kununua dawa ambazo halmashauri hawakuzipokea lakini ililipa fedha zaidi ya zile za mkataba wa ununuzi.

“Halmashauri ililipa shilingi 146,425,818 badala ya Sh 73,212,909.40,” alisema.

AAGIZA WAVULIWE VYEO

Jafo alitoa maelekezo wakuu wa vitengo waliohusika Galahanga, Kaijage na Ndabila ambaye amehamishiwa Itilima, Siriwa aliyehamishiwa Gairo wavuliwe madaraka.

Pia watumishi waliohamishwa wakiwa na makosa warejeshwe Ulanga ili kuiwezesha halmashauri na vyombo vya dola kufanya kazi yake.

“Wahasibu waliohusika kuhujumu mapato waondolewe majukumu yao ili kupisha halmashauri na vyombo vya dola kufanya kazi yake. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ieleze ni kwanini hawakuchukua stahiki zenye tija,” alisema.

MLINGA APONGEZA

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili, Mlinga, alifurahia uamuzi huo akidai watumishi hao walikuwa wakitafuna fedha za Serikali bila woga wowote.

Na Ramadhan Hassan-Dodoma
Share:

WABUNGE VITI MAALUMU CCM  WAVIINUA VIKUNDI VYA AKINAMAMA JIMBO LA UKONGA.

  Wabunge viti maalumu CCM Mkoa wa Dar es salaam wameviinua vikundi vya kinamama wa jimbo la Ukonga kwa kuwapa vifaa kazi na fedha. Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Wilaya ya Ilala Amina Dodi ameyasema hayo wakati wa ziara ya wabunge wa wa viti Maalumu katika kata za Kitunda ,Mzinga ,na Majohe,ambapo wabunge hao wametoa msaa wa fedha , pembejeo za kilimo na cherehani kwa vikundi vya akina mama. “Katika kipindi cha uongozi wangu nimejitahidi sana kuwahamasisha wabunge wetu kuwa karibu na wananchi na wabunge hawa wamekubali kushuka chini kabisa…

Source

Share:

SERIKALI YAFUNGA AKAUNTI ZA BENKI ZINAZOMILIKIWA NA WAKULIMA WA KOROSHO

Serikali imefunga kwa muda akaunti 191 za benki zinazomilikiwa na wakulima wa korosho kupisha uhakiki wa kina wa umiliki wa korosho walizouza.

Uamuzi huo unakuja wakati ikiwa imeshaingiza Sh3.8 bilioni kwenye akaunti hizo katika mfululizo wa uhakiki na ulipaji wakulima wa zao hilo unaoendelea nchini.

Akizungunza na gazeti la The Citizen, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema wakulima wenye akaunti hizo wameuza zaidi ya kilo 1,500 kwenye vyama tofauti vya msingi, hivyo ni lazima umiliki wa korosho walizouza uhakikiwe.

“Hatua hii ni muhimu (ya kufunga akaunti hizi kwa muda) ili kupisha uhakiki kwa sababu utaratibu unataka mkulima aliyeuza zaidi ya kilo 1,500 za korosho aonyeshe shamba lake lilipo kwa timu yetu ya uhakiki,” alisema Hasunga.

“Lakini uchunguzi wa awali umeonyesha kuna baadhi ya wakulima wameuza kiasi kinachofikia kilo 3,000 za korosho kwenye vyama vya msingi tofauti.”

Hata hivyo, waziri huyo alisema Serikali bado haijapata kiasi halisi cha korosho ambacho wamiliki wake wameshindwa kuonyesha mashamba yao, lakini alisisitiza kuwa tatizo hilo bado ni kubwa. 

Akizungumzia uhakiki na malipo kwa wakulima, alisema tayari Sh206.092 bilioni zimeshalipwa kufikia Disemba 27 kati ya hizo, Sh188.378 bilioni zilikuwa zimewafikia wakulima kabla ya sikukuu ya Krismasi.

“Wakulima 100,534 wameshalipwa bila kujali ni mara ngapi walipeleka korosho kwenye chama cha ushirika cha msingi. Wakulima hawa wanatoka katika vyama vya msingi 398 kati ya vyama 617 vilivyosajiliwa nchini na vyama 504 vinavyopatikana katika mikoa mitatu ya Mtwara, Lindi na Ruvuma,” alisema.

Alisema tani 188,799. 4 za zao hilo zimeshakusanywa katika maghala mbalimbali na kwamba tani 30,226.25 zimehamishiwa kwenye maghala mengine ili kutengeneza nafasi korosho zilizo mikononi mwa wakulima kupokewa. 

Takwimu za Serikali zinamaanisha kuwa Sh206.092 bilioni zilizotolewa ni malipo kwa tani 62,452.333 kati ya tani 188,799 zilizokusanywa na tani 126, 347.07 zinasubiri mchakato wa malipo. 

“Mchakato hautakamilika mwisho wa mwezi huu kama tulivyotarajia kutokana na changamoto zilizojitokeza, matumaini yetu ni kwamba uhakiki na malipo yatakamilika mwishoni mwa mwezi Januari mwakani.”

Chanzo :Mwananchi
Share:

MWANAJESHI WA JWTZ AUA WATU WAWILI KWA RISASI AKIWEMO MTALAKA WAKE

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma, linamshikilia askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wa kikosi cha Chandarua cha mjini hapa, Sajenti Batisin Samda, kwa tuhuma za kuwaua kwa kuwapiga risasi watu wawili akiwamo mtalaka wake.

Askari huyo alitekeleza mauaji hayo akiwa kazini kwa kumuua askari mwenzake, Sajenti Juma Mkele na mtalaka wake, Veronica Kayombo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Gemini Mushy, jana alisema tukio lilitokea juzi majira ya saa 10 alasiri kwenye eneo la kambi hiyo.

Kwa mujibu wa Kamanda Mushy, inadaiwa kuwa Kayombo alikuwa amekwenda kwenye kambi hiyo kumpelekea hati ya wito kutoka idara ya ustawi wa jamii aliyekuwa mume wake, jambo ambalo linaonyesha lilisababisha askari huyo kupandwa na hasira.

Alisema siku hiyo ya tukio, Kayombo alipofika kwenye kambi hiyo, kabla ya kukutana na Samda, alionana na mkuu wake wa kazi na baadaye mkuu huyo alimpa maagizo Sajenti Mkele ili ampeleke kwake (Samda) akamkabidhi barua hiyo ya wito.

Kamanda Mushy alisema walipofika kwenye eneo alilokuwa anafanyia kazi mtuhumiwa huyo, ghafla wakiwa wanaendelea na mazungumzo kabla ya kumpa barua alipandwa hasira na kumfyatulia risasi Kayombo kisha kummalizia askari aliyekuwa ameongozana naye ambao walifariki dunia papo hapo.

Kamanda Mushy alisema polisi wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yake.
Share:

POLISI ATUPWA JELA MIAKA 20 BAADA YA KUDAKWA NA MENO YA TEMBO


Polisi G.30 PC Reuben Mgamba (36) mkazi wa Forest jijini Mbeya amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka ishirini jela au kulipa faini ya Sh.Milioni 300 baada ya kukiri kukutwa na nyara za serikali meno ya tembo.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Mbeya, Rashid Chaungu baada ya mshtakiwa huyo kufikishwa mahakamani na wenzake watatu wakidaiwa kuhujumu uchumi.

Akiwa mahakamani, askari huyo alikiri kukutwa na vipande vinne vya meno ya tembo jijini Mbeya kitendo ambacho ni kinyume na kifungu namba 86 (1) (2) (iii) cha sheria ya uhujumu uchumi Namba 5.

Awali akisoma shtaka hilo mahakamani hapo wakili wa serikali, Ofmedy Mtenga alidai, kwamba mshtakiwa huyo pamoja na wenzake watatu walikutwa na vipande hivyo katika eneo la Mafiati jijini hapa vyenye thamani ya Sh. Milioni 34,185,750.

Aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Askari Ex.G.30 Pc Reuben Mgamba James (36) mkazi wa forest jijini hapa, Safari Maneno (37) mfanyabiashara na mkazi wa Mabatini Mbeya, James Jeston Mnyamwezi (38) mkazi wa Namkukwe Mkoani Songwe na Adam Shaban maarufu kwa jina la Ilemu (40) mkulima na mkazi wa Mazimbwe wilayani Chunya.

Hata hivyo washtakiwa watatu wamekana kutenda kosa hilo licha ya mshtakiwa wa kwanza kukubali kukutwa na nyara hizo.

Wakili huyo wa serikali alieleza, upande wa mashtaka utawasilisha mahakamani ushahidi wake pamoja na vielelezo vya kuthibitisha shtaka hilo.

Aliiomba mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ambaye alikuwa mtumishi wa jeshi la polisi jijini hapa.

Hata hivyo baada ya polisi huyo kukiri kosa hakimu Chaungu
alimuamuru kulipa faini ya Shilingi milioni mia tatu au kwenda jela miaka 20 ikiwa atashindwa kulipa faini hiyo. 

Washtakiwa wengine watatu waliokana kutenda kosa hilo wamerudishwa mahabusu baada ya kukosa wadhamini hadi Januari 10, mwaka 2019 kwa ajili ya kuanza usikilizwaji wa kesi hiyo.
Share:

DKT MWANJELWA:MADEREVA BAJAJI FUATENI SHERIA NA MSIKUBALI KUTUMIKA KISIASA

Mbeya. Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora, Dakta Merry Mwanjelwa, amewataka madereva wa babaji jijini Mbeya kuendelea kufuata taratibu na sheria za usalama barabarani ili kulinda maisha yao na ya watu wengine. Dkt. Mwanjelwa amezungumza hayo leo alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa ofisi ya chama cha kuweka na kukopa cha Bajaji Saccos jijini Mbeya, ambapo amesema vijana hao wameonesha kitu cha mfano hivyo ni vema wakaungwa mkono na kuelekezwa pale wanapohitaji msaada waweze kuwasaidia ili wajikwamue kiuchumi. Aidha, amewataka askari wa usalama…

Source

Share:

Friday, 28 December 2018

POLISI MBARONI KWA KUMUUNGUZA PASI KIJANA ALIYEKUWA ANAMVIZIA BINTI YAKE

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikikia askari E.9301 Koplo Almas kwa tuhuma za kumuunguza kwa pasi mwanafunzi shule ya sekondari Cheyo, Jumanne Hussein (17).

Akizungumza leo Ijumaa Desemba 28, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ,Emmanuel Nley amesema tukio hilo limetokea Desemba 25, 2018.

Amesema mwanafunzi huyo alituhumiwa na Almas kuwa anataka kufanya mapenzi na binti yake.

Amebainisha kuwa baada ya askari huyo kumhisi mwanafunzi huyo alianza kumpiga na kumuunguza na pasi sehemu mbalimbali mwilini.

Kamanda Nley amesema tayari polisi imechukua hatua za kinidhamu kwa askari huyo ikiwa ni pamoja na kushtakiwa kijeshi na atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.
Share:

Breaking ; RAIS MAGUFULI AMTUMBUA MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Dkt. Irene Isaka.

Taarifa kutoka Ikulu iliyotolewa leo Disemba 28,2018 inasema
Uteuzi wa Mkurugenzi mwingine utafanyika baadae na Dkt. Irene Isaka atapangiwa kazi nyingine.
Share:

YANGA KUTUMIA DAKIKA HIZI 180 NGUMU KUWAZIBA SIMBA MDOMO

MABINGWA wa Kihistoria timu ya soka ya Yanga,wamepania kuhakikisha wamlalua kila anayekuja mbele yake baada ya kuhaidi kuzitumia dakika ngumu 180 kuthibi­tisha kwamba hawakuwa wakibahati­sha kwenye mzunguko wa kwanza. Watoto hao wa Jangwani ambao Kikosi chao hicho kinanolewa na kocha mwenye maajabu yake , Mwinyi Zahera hadi sasa kimecheza mechi 17 na kati ya hizo imeshinda 15 ikiwa imepata alama 47. Lakini kibarua kizito kinakuja kukamilisha mzunguko wa kwanza. ambapo ni ni dhidi ya Mbeya City na Azam FC. Endapo Yanga itafanikiwa kushinda mechi hizo mbili, itakuwa imefikisha alama 53…

Source

Share:

NAIBU WAZIRI NISHATI : LENGO LA SERIKALI KUWAFIKISHIA UMEME, NI MUUTUMIE KAMA FURSA NA KWA SHUGHULI ZA UZALISHAJI

Naibu waziri wa nishati Subira Mgalu amewataka wananchi wanaounganishiwa umeme kupitia miradi ya serikali wautumie kama fursa ya kuongeza shughuli za uzalishaji.    Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Kimarang’ombe wakati alipofanya ziara ya kuwasha umeme vijijini katika wilaya ya Bagamoyo. Amesema hayo wakati alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya usambazaji umeme vijijini iliyoambatana na kuwasha umeme vijijini wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani ambapo amewataka wananchi hao kutumia umeme kama fursa yao katika masuala ya uzalishaji badala ya kutumia kama mwanga tu. “Tusifikirie matumizi…

Source

Share:

ASKARI MAGEREZA AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI


Askari Magereza katika Gereza la Kilimo Kitai wilayani Mbinga, Ruvuma, Adamu Kulwa Mgaga (24), amejiua kwa kujipiga risasi.

Askari hiyo mwenye namba B:8400 WDR, amejiua akiwa lindo la mifigo kwa kujipiga risasi eneo la kidevu na kusababisha kichwa kupasuka

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Ruvuma, Arekizanda Nyifwa, alithibitisha kutokea kwa tuko hilo Desemba 25, mwaka huu, saa 2:30 usiku katika gereza la Kitai-Mbinga.

Alisema askari huyo alipokuwa lindo ilipofika saa 2:30 usiku alichukua bunduki aliyokuwanayo aina ya SAR na kuelekeza bomba kwenye kidevu chake kisha kuhesabu moja hadi tatu na kufyatu risasi ambazo zilifumua kichwa chake na kufariki dunia papo hapo. 


Alisema askari huyo alifanya hivyo akiwa katika sare za jeshi hilo na kwamba chanzo cha kujiua bado hakijafahamika kwa kuwa hakuacha ujumbe wowote.Alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Share:

MTUMISHI WA BENKI YA NMB AJERUHIWA

Watu tisa wamekamatwa Mkoani Mbeya kwa tuhuma za uhalifu wa kuvunja, kuiba na kujeruhi likiwemo tukio la mtumishi wa benki ya NMB Kasumulu Kyela na mkazi wa Iwambi Jijini Mbeya Habib Juma.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ulrich Matei amewataja watuhumiwa wawili waliomjeruhi mtumishi wa NMB ni Richard Jackson fundi ujenzi mkazi wa DDC Mbalizi na David Labi (32) ambao walikamatwa Disemba 9 mwaka huu majira ya saa nane mchana wakiwa na nguo za majeruhi, TV, Simu aina ya Tecno na vifaa vilivyotumika kumshambulia majeruhi.

Matei alisema watuhumiwa wamekiri kutenda uhalifu huo na kuonesha vitu vilivyoibiwa pamoja na bomba lililotumika kumpigia kichwani ambapo hivi sasa majeruhi anapatiwa matibabu Jijini Dar es Salaam.

Aidha Kamanda Matei alisema Disemba 13 mwaka huu Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watu sita kwa tuhuma za kuwavamia watu usiku wakijifanya sungusungu hususani maeneo ya TEKU, Ilomba,Ituha na VETA.

Matei alisema kinara wa tukio hilo ni Pascally Aron (18)dereva wa Bajaj na mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya. Wengine ni Justin Laurence(18) fundi ujenzi mkazi wa Ilemi, Allen Daud(19)mkulima mkazi wa Ilemi, Yassin Naso(19) mkazi wa Ilemi, Hamza Charle (22)mkazi wa Ilemi na Anthony Elias (32)mkazi wa Ilemi. 

Pascally alikiri kujihusisha na uhalifu kwa kujifanya sungusungu ambapo hutishia kwa kutumia mapanga na kuwapora watu vitu vya thamani.

Hata hivyo alisema baada ya uchunguzi kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Alitoa wito kwa yeyote mwenye kufahamu makundi yanayojihusisha na uhalifu kuwasiliana na jeshi la pilisi kupitia ulinzi shirikishi.
Share:

KAULI YA SUMAYE,ZITTO KABWE BAADA YA TUNDU LISSU KUSEMA ATAGOMBEA URAIS 2020

Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamesema wanamsubiri kwa hamu Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu apitishwe na chama chake kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Lissu anayetibiwa nchini Ubelgiji baada ya shambulio la risasi zaidi ya 30 lililotokea Septemba 7, mwaka jana akiwa Dodoma, juzi aliliambia gazeti la Mwananchi kwamba hatakuwa na kipingamizi ikiwa chama chake kitampitisha kuwania nafasi hiyo.


Kauli ya Lissu ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya CCM, imepokewa kwa furaha na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wakiamini anaweza kutoa ushindani mkubwa kwa mgombea wa chama tawala.


Mwenyekiti wa Chaumma, Hashim Rungwe alisema Lissu atavifaa vyama hivyo katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Maoni ya Rungwe yaliungwa mkono na Kiongozi wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye alisema hana shida na kauli ya Lissu.


“Jambo la muhimu kuliko yote ni kuwa mwaka 2019, kwetu ni mwaka wa kudai demokrasia. Azimio la Zanzibar limeweka mpango maalumu wa kukabiliana na ukandamizaji wa demokrasia. Tundu Lissu ni kiongozi muhimu katika harakati hizo,” alisema Zitto.

Pia, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye alisema Lissu hajafanya kosa kutoa kauli hiyo kwa sababu mwanachama yeyote anaweza kueleza nia yake.


“Sijamsikia, lakini kama atapitishwa na chama sioni tatizo, kwa sababu kila chama kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea na ni lazima ufuatwe,” alisema Sumaye.


Sumaye ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chadema mwenyekiti wa Kanda ya Pwani wa chama hicho alisema Lissu si wa kwanza, “Nimemsikia hata mheshimiwa (Edward) Lowassa, mimi sioni tatizo kama mtu anafuata utaratibu wa chama.”


Chanzo - Mwananchi
Share:

WAZIRI MKUU AWAAGIZA MAWAZIRI KUFIKA KWENYE MAENEO YA UJENZI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la tenki la maji la kutolea huduma katika ujenzi wa mji wa Serikali Mtumba badala ya ukumbi wa Hazina kama alivyokuwa amepanga awali.

Akiwa Ihumwa, Waziri Mkuu amewaagiza Mawaziri wafike kwenye maeneo ya ujenzi wa ofisi zao, watathmini uwezo wa wakandarasi wanaojenga majengo ya wizara na pale watakapojiridhisha kuwa uwezo wao ni mdogo, wawabadilishe mara moja.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Ijumaa, Desemba 28, 2018) akiwa kwenye kikao cha kazi (site meeting) na mawaziri 15 na manaibu mawaziri katika eneo la Ihumwa lililoko km. 17 kutoka jijini Dodoma.

“Mawaziri mliopo na makatibu wakuu wote kaeni na wakandarasi wenu hapa site ili waeleze kazi hii itakamilishwa lini. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kazi hii inakamilishwa kwa wakati,” amesisitiza.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa mrejesho Mawaziri juu ya changamoto alizokutana nazo jana alipofanya ukaguzi wa ujenzi kwa kila wizara. “Nataka Mawaziri ambao ofisi zao zinajengwa wa watu wa Mzinga, wakae nao na kutathmini uwezo wao na kama mtaona hawawezi, mkabidhi kwa mkandarasi mwingine,” amesema Waziri Mkuu.

Amewataka wakandarasi wahakikishe wanaongeza idadi ya vibarua ili kazi hiyo iweze kwenda haraka. “Wizara iliyofanya vizuri kuliko zote ni ya Utumishi, wao wako hatua nzuri. Kwa maana ya uchapaji kazi, eneo nililokuta lina wafanyakazi wengi ni magereza,” amesema.

Wakati huohuo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi alimweleza Waziri Mkuu kwamba kuna wagongaji wa kokoto ambao wamepokea fedha lakini wakaamua kufunga machimbo yao kwa sababu ya sikukuu.

“Waziri wa Madini aongee nao hawa watu ili warejee na kufanya kazi kwa sababu baadhi yao wameshapokea fedha na mahitaji ya kokoto hapa ni makubwa na aliyebakia akifanya kazi ni Nyanza Road Works peke yake,” alisema.

Naye Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani alimweleza Waziri Mkuu kwamba wizara yake imetoa transforma tisa za kusaidia kupoza umeme lakini ni wizara nne ambazo zimejitokeza na kulipia line za transforma hizo.

“Wizara yetu tumetoa transforma tisa za kusaidia umeme upatikane eneo la ujenzi. Niwaombe mawaziri waliopo, walipie service line tu ambazo gharama yake ni sh. 921,000 ili wafungiwe transforma na kazi iweze kufanyika mchana na usiku. Hadi sasa, tumeshapokea maombi kutoka wizara nne tu za Maji, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), Elimu na Nishati ili kazi imalizike ndani ya muda mfupi,” alisema.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
Share:

BEN POL AKUTANA NA MEMPHIS DEPAY


Ben Pol akiwa na Memphis Depay

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amekutana uso kwa uso na mchezaji wa zamani wa Manchester United ambaye hivi sasa anachezea klabu ya Olympique Lyon, Memphis Depay.

Ben Pol ambaye yupo Dubai, amekutana na mchezaji huyo katika moja ya maeneo tulivu ya mji huo na kuiweka picha yao wakiwa pamoja katika mtandao wa Instagram.

Katika picha hiyo, Ben Pol ameambatanisha maneno yanayosema, "nimekutana na Memphis Depay tukiwa tunaelekea kupata chakula cha mchana".

Memphis Depay alichezea klabu ya PSV Eindhoven kabla ya kujiunga na Manchester United mwaka 2015 ambako alicheza mechi 33 na kufunga mabao 2. Mwaka 2017 alijiunga na Lyon ya nchini Ufaransa, ambapo mpaka sasa amecheza mechi 69 na kufunga mabao 29.

Ben Pol amekuwa katika ziara mbalimbali barani Ulaya na Asia tangu mwanzoni mwa mwezi Desemba ambapo pamoja na mambo mengine, amekuwa akifanya matamasha mbalimbali.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger