Friday, 21 December 2018

HIZI NDIO SABABU KUAHIRISHA UCHAGUZI WA RAIS DRC

Kinshasa, DRC. Uchaguzi wa Rais ulioahirishwa kwa muda mrefu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hautazamiwi kama utaweza kufanyika Jumapili ijayo kama ilivyokuwa imepangwa, baada ya Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo kuwaambia wagombea wa kiti cha urais kwamba haikuweza kuandaa zoezi la upigaji kura kama ilivyoainishwa. Uchaguzi huo ambao umeahirishwa mara kadhaa tangu mwaka 2016 ulitazamiwa kumchagua mrithi wa Rais Joseph Kabila ambaye anapaswa kuondoka madarakani baada ya kushika hatamu za uongozi kwa miaka 18. Hapo jana Alhamis Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (CENI), iliwaita…

Source

Share:

KUELEKEA MECHI NA NKANA ,SULEMAN MATOLA ATOA NENO HILI

NA KAROLI VINSENT WAKATI Mabingwa wa Ligi kuu Bara ,Timu ya Simba wakihitaji ushindi wa Gori moja kwa wapinzani wao timu ya Nkama ya Zambi ili watingie hatua ya makundi. Mchezaji wa Zamani wa Simba ambaye amecheza kwa mafanikio makubwa ,Suleman Matola ,ameibuka na kutoa neno kwa kikosi hiccho cha simba kuelekea kwenye mechi hiyo inayotarajiwa kufanyika Jumapili ya wiki hii. Matola ambaye ni Kocha wa Timu ya Lipuli amekimbia Chanzo changu , kuwa Simba wana nafasi nzuri ya kupata matokeo mbele ya wapinzani wao Nkana FC katika mchezo wa…

Source

Share:

INTERPOL YATAHADHARISHA DAESH (IS) KUFANYA TENA MASHAMBULIZI ULAYA

Lyon, UFARANSA. Katibu Mkuu wa Polisi ya Kimataifa (Interpol), Jürgen Stock, ametahadharisha kuhusu uwezekano wa kundi la kigaidi la Daesh (IS) kufanya tena mashambulizi katika nchi za Ulaya. Bw Stock amesema kuwa, wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh kawaida wanahukumiwa vifungo vya muda mfupi na wataachiwa huru haraka na kuanza kufanya mashambulizi ya kigaidi. Katibu Mkuu huyo wa Interpol ameongeza kuwa, kwa msingi huo nchi nyingi duniani zitakabiliwa na hatari ya wimbi la pili la mashambulizi na harakati za kundi la kigaidi la Daesh. Maafisa wengi wa nchi za…

Source

Share:

DIAMOND NA RAYVANNY WAKUBALI YAISHE, WAWAOMBA RADHI BASATA.

Na Bakari Chijumba (Beca Love),Mtwara. Baada ya kufungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny wamejitokeza hadharani na kuomba radhi kwa kuimba wimbo wa “Mwanza” uliofungiwa, huku wakiwasihi wasanii wenzao kuwa mabalozi wazuri wa utamaduni wa Tanzania. Kupitia kipande cha video chenye sekunde 54 ambacho kimewekwa kwenye ukurasa wa Instagram wa Diamond pamoja na ule wa RayVany leo 21 Dec 2018, wasanii hao wameonekana wakiongea kwa masikitiko na hisia kali na kujutia walichokifanya. “Kwa unyenyekevu mkubwa tunaomba radhi Serikali, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,…

Source

Share:

ZAIDI YA MAKASISI 680 KANISA KATOLIKI MAREKANI WATUHUMIWA KULAWITI WATOTO

Illinois, MAREKANI. Mwanasheria Mkuu wa jimbo la Illinois nchini Marekani, Lisa Madigan, amewatuhumu makasisi 700 wa Kanisa Katoliki katika jimbo hilo kwamba wamewalawiti watoto, ikiwa ni idadi kubwa mno ikilinganishwa na ile iliyokuwa imetolewa na kanisa hilo huko nyuma. Katika taarifa, bi Madigan amesema Dayosisi ya Kanisa Katoliki katika jimbo hilo ilikiri kuwa makasisi na mapadri wake 185 tu ndio wamewalawiti watoto, huku ikificha kwa makusudi majina 500 ya viongozi wa kanisa hilo walioshiriki vitendo hivyo vya ufuska. Mwanasheria Mkuu huyo wa Illinois amesema uchunguzi wao katika hatua zake za…

Source

Share:

PAPA FRANCIS AKOSOA VIKALI MIENENDO YA MADOLA YA MAGHARIBI KWA WAHAJIRI

Vatican City, ITALIA Tatizo la kiulimwengu la wakimbizi ni ukweli ambao umedhihirika wazi katika miaka ya hivi karibuni tena kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa. Kinyume na mtazamo wa weledi wa mambo ambao walikuwa wakiamini kwamba, baada ya kumalizika Vita Baridi (Cold War) kiwango cha migogoro na mivutano ya kimataifa kingepungua mno duniani, hivi leo tunashuhudia kuongezeka migogoro na mizozo pamoja na mapigano ya ndani na ya kieneo na katika mabara mbalimbali ya duniani. Tukiachilia mbali chanzo na sababu tofauti za machafuko na vita, tunaona kwamba yote hayo yamekuwa na mchango…

Source

Share:

KIKOKOTOO CHA MAFAO CHAPINGWA KILA KONA, TALGWU NAO WAKIPINGA BILA KUOGOPA

Dodoma. Kikokotoo cha mafao ya wastaafu bado kimeendelea kupingwa na wadau ikiwa siku nne tangu Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kutoa msimamo kuwa ni kizuri na kina manufaa, hivyo hakiwezi kubadilishwa. Upinzani huo mkali kwa kipindi hiki umetoka Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU), ambacho kama wadau wengine waliotangulia kupinga, kimesema kanuni hiyo mpya imezua hali ya maumivu na manung’uniko kutoka kwa wahusika wa jambo hilo. Kutokana na hali hiyo, chama hicho kimeiomba serikali kurudi katika meza ya majadiliano na viongozi wa…

Source

Share:

BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA LAPITISHA AZIMIO KALI KWA MAREKANI

New York, MAREKANI. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linaloitaka Marekani kukomesha hatua zilizo kinyume na sheria dhidi ya wawakilishi na maeneo ya kidiplomasia ya Russia nchini humo. Ofisi ya mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, azimio lililopitishwa na Baraza Kuu la umoja huo ambalo limependekezwa na Kamati yake ya Sita limekosoa waziwazi hatua zinazochukuliwa na Marekani dhidi ya wanadiplomasia na maeneo ya kidiplomasia ya Russia. Azimio hilo limeitaka Marekani kukomesha mara moja hatua zisizo za kisheria dhidi ya ofisi ya mwakilishi wa kudumu wa…

Source

Share:

MBWA KICHAA AJIUZULU BAADA YA KUTOFAUTIANA KIMTIZAMO NA RAIS TRUMP

Washington Dc, MAREKANI. Waziri wa Ulinzi wa Marekani, James Mattis, maarufu kwa jina la ‘Mbwa Kichaa’ amejiuzulu wadhifa huo kutokana na hitilafu za kimitazamo kati yake na Rais Donald Trump wa nchi hiyo. Waziri Mattis ambaye ni jenerali mstaafu ataachia ngazi mwishoni mwa mwezi Februari na kumruhusu Rais Trump kuchagua mtu anayekwenda sambamba na mitazamo yake. Jenerali Mattis amesema katika barua yake ya kujiuzulu kwamba, hatua hiyo itampa Trump fursa ya kumteua mtu anayeoana zaidi ya mitazamo na fikra zake. Kujiuzulu kwa Mbwa Kichaa au Mad Dog kama anavyojulikana kulitazamiwa…

Source

Share:

HII NDIO TAARIFA YA MWISHO KIKAO CHA 05 CHA MARAIS WA IRAN NA UTURUKI

Tehran, UTURUKI. Marais wa Iran na Uturuki wamesisitiza katika taarifa ya mwisho ya Kikao cha tano cha Baraza Kuu la Uhusiano wa Kistratijia wa nchi hizo mbili, kuhusu umuhimu wa kuchukuliwa hatua za dharura za kufanikisha biashara yenye thamani ya dola bilioni 30 kwa mwaka kati ya pande hizo mbili. Katika taarifa hiyo Marais Hassan Rouhani wa Iran na Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki wametilia mkazo umuhimu wa kuimarishwa zaidi uhusiano wa pande mbili kupitia njia ya kuendelezwa mazungumzo ya kisiasa na kiuchumi na safari za mara kwa mara za…

Source

Share:

DIAMOND NA RAYVANNY WAIANGUKIA BASATA.. WAKIRI KOSA KUPIGA WIMBO WA NYEGEZI

Wasanii nyota wa muziki nchini Tanzania Diamond Platnumz na Rayvanny wameomba msamaha kwa kupiga kibao chao kilichofungiwa katika tamasha lao hivi karibuni.

Wasanii hao wa Bongo Flava walipiga kibao chao kiitwacho Mwanza katika tamasha lao liitwalo Wasafi Festival. 

Kufuatia kukaidi agizo la Basata, nyota hao wawili walifungiwa kwa muda usiofahamika kufanya onesho lolote ndani na nje ya Tanzania.

Asubuhi ya leo wasanii hao wametoa video katika mtandao wa kijamii wa Instagram ya kuomba radhi kwa 'makosa yao'.

"Kwa unyenyekevu mkubwa tunaomba radhi kwa Jamuhuri yetu tukufu ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Habari Sanaa na Michezo, Basata na kila aliyekwazika kwa kuperform (kupiga) wimbo wa Mwanza katika show (onesho) yetu ya Mwanza. Japo tunajitahidi kuwa vijana wa mfano bora katika taifa letu lakini unavyojua binadamu siku zote hauwezi kupatia. Ni kweli tulikosea kwa kuperform mwimbo ambao umefungiwa. Tunaahidi kutorudia tena kosa lilotokea. Lakini pia kwa kutumia kazi za sanaa kuwasihi wasanii wenzetu na mashabiki kuwa mabalozi bora wa tamaduni za Tanzania," amesema diamond katika video hiyo.

Katika maelezo iliyoamabatana na video hiyo, Diamond ameandika: "Ila Utelezapo, ni vyema kulijua Kosa na Kulirekebisha ili kesho na Kesho kutwa lisijirudie....Inshaallah Mwenyez Mungu Atusimamie na kutuongezea Juhudi na Maarifa katika Kazi zetu ili kwa Pamoja tuzidi kuukuza Muziki wetu na Kuendelea Kuiwakilisha vyema na kulipa sifa Nzuri na Heshima Nchi yetu..."


Wakati wakiufungia wimbo huo, Basata walisema kibao hicho "kimebeba maudhui machafu," ambayo ni "ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania" na kwamba umetumia "maneno yanayohamasisha ngono".

Baraza pia liliwataka "kuuondoa wimbo huo mara moja kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kufika saa kumi kamili" siku hiyo, lakini mpaka saa tatu nanusu ya leo asubuhi bado upo You Tube.

Na Jumanne walisema wanafungia wasanii hao kwa kuonesha dharau kwa mamlaka: "Baraza limefikia maamuzi ya kuwafungia rasmi kutokana na wasanii hawa kuendelea kuonyesha dharau na utovu wa nidhamu kwa mamlaka zinazosimamia masuala ya sanaa nchini na uvunjifu wa maadili uliokithiri unaofanywa na waandaaji wa Tamasha la Wasafi 2018, chini ya uongozi wake Diamond Platnumz," ilisema taarifa ya Basata.

Kibali cha tamasha lao pia kimesitishwa "kutokana na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu katika uendeshaji wa tamasha hilo hapa nchini."
Share:

MAKUNDI YA AFCON U-17 2019 YAMEPANGWA MLIMANI CITY DAR ES SALAAM

Shirikisho la soka Afrika CAF jana Desemba 20 2018 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam limeichezesha droo ya kupanga makundi ya michuano ya mataifa ya Africa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17.

Michuano ya AFCON U-17 ambayo yatafanyika jijini Dar Es Salaam April 14-28 2019 jini Dar es Salaam itashirikisha jumla ya timu nane ambazo ni Nigeria, Angola, Senegal, Guinea, Uganda, Morocco, Cameroon na Tanzania ambaye ni mwenyeji.

Share:

MBUNGE MABULA ACHANGIA MILIONI 22 UJENZI SOKO LA MLANGO MMOJA


Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (katikati), akizungumza na wafanyabiashara wadogo (machinga) katika Soko la Mlango Mmoja Jijini Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM) ametoa shilingi Milioni 22 kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya soko la Mlango Mmoja iliyoteketea kwa moto miezi mitatu iliyopita.

Mabula aliyasema hayo jana baada ya kuwatembelea wafanyabiashara wadogo (machinga) katika soko hilo na kubainisha kwamba fedha hizo kutoka mfuko wa jimbo zitasaidia
ujenzi wa paa lote.

Mwenyekiti wa soko hilo, Jackson Kayoza alisema kulingana na tathmini iliyofanyika, shilingi Milioni 98 zinahitaji kwa ajili ya ujenzi wa sehemu iliyoungua moto hivyo alimshukru mbunge Mabula kwa mchango huo.

Mmoja wa machinga katika Soko la Mlango Mmoja ambaye pia bidhaa zake zilitekeketea kwa moto, Isaack Julius, alisema mchango wa mbunge Mabula uwe chachu kwa Halmashauri
ya Jiji la Mwanza kwa kuhakikisha inakamilisha kiasi cha fedha kinachohitajika ili ujenzi huo uanze mara moja.

Septemba 28, 2018 majira ya alfajiri, ajali ya moto ilizuka katika Soko la Mlango Mmoja na kusababisha meza 83 za wajasiriamali, maduka 23 na vyoo vitatu kuteketea ambapo hasara yake haikujulikana mara moja.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Share:

RADI YAUA WATU WATATU WA FAMILIA MOJA RUVUMA

Watu watatu wa familia moja wamefariki dunia kwa kupigwa na radi katika kijiji cha Majimaji, wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma.

Taarifa za tukio hilo zilizothibitishwa na Mtendaji wa Kata ya Majimaji, Neema Mahujilo, zinaeleza kuwa, radi hiyo iliambatana na mvua kubwa ya upepo iliyonyesha Desemba 14, saa 12. 30 hadi saa 1.40 jioni.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Jemini Mushy, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba Polisi inaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha vifo hivyo.


Kamanda Mushy aliwataja watu waliopoteza maisha kuwa ni Zenna Hamadi Ismail (50), Yusuph Abdalah Alli (25) na Zamila Abdalah Abbilahi (3).


Mganga Msaidizi wa Hospitali ya Wilaya ya Tunduru, Edger Ngauje, aliyeifanyia uchunguzi miili ya marehemu, alisema kuwa chanzo cha vifo hivyo ni kuunguzwa na shoti ya umeme uliosababishwa na radi hiyo.
Share:

CHINA YATANGAZA NEEMA KWA WAKULIMA WA KARANGA,UFUTA NA MAHARAGE

Ubalozi wa Tanzania Beijing, China umebainisha kuwa kampuni moja nchini China imewasilisha ombi la kununua ufuta, karanga na maharage ya soya kutoka Tanzania.

Taarifa iliyotolewa jana Alhamisi Desemba 20, 2018 na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) na kusainiwa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa mamlaka hiyo, Theresa Chilambo inaeleza kuwa kampuni hiyo inalenga kununua bidhaa hizo kwa vigezo.

Kampuni hiyo inahitaji ufuta tani 3,000 kwa mwezi, karanga tani 2,000 kwa mwezi na maharage ya soya tani 5,000 kwa mwezi

Theresa amesema ufuta unaotakiwa ni wa ubora wa Taifa daraja la pili.Amebainisha kuwa hata karanga na maharage ya soya yanayohitaji nayo ni katika kiwango hicho cha ubora.

Share:

NANE WAUAWA KATIKA MAANDAMANO YA KUPINGA HALI MBAYA YA UCHUMI

Khartoum, SUDAN. Nchini Sudan watu wasiopungua nane (08) raia wa nchi hiyo, wameuawa katika ghasia na maandamano ya wananchi ya kupinga hali mbaya ya kiuchumi, ughali wa bidhaa na maisha magumu nchini humo. Maafisa wa serikali ya Sudan wametangaza usiku wa kuamkia leo kwamba, idadi ya watu waliouawa katika maandamano ya kupinga hali mbaya ya kiuchumi katika mikoa ya al Qadharif na Nahru Nil imefikia 8. Tangu Jumatano ya juzi miji mbalimbali ya Sudan ilishuhudia ghasia na maandamano makubwa ya wananchi anaopinga hali mbaya ya kiuchumi na ughali wa bidhaa.…

Source

Share:

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA DEC 21,2018


Manchester City itawalazimu kupambana na vilabu vya Barcelona na Paris St-Germain ili kupata saini ya mchezaji kiungo nyota anayechipukia Frenkie de Jong, 21. Dejong raia wa Uholanzi anayechezea Ajax anakisiwa kuwa na thamani ya pauni milioni 60. (Mirror)

Real Madrid hawana mpango wa muda mfupi au mrefu wa kumwajiri tena Jose Mourinho, 55, aliyefutwa kazi na Manchester United jumanne wiki hii. (Marca)

Crystal Palace wana imanikuwa watafanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Nigeria na Chelsea Victor Moses, 28, katika dirisha la usajili la mwezi ujao. (London Evening Standard)

Rais wa klabu ya Napoli Aurelio De Laurentiis amesema klabu hiyo haitamuuza mlinzi wake kisiki raia wa Senegal Kalidou Koulibaly, 27, kwenda Manchester United mwezi ujao, lakini wanaweza kukubali dau kwa wakati ujao. (Corriere del Mezzogiorno, via Star)

Arsenal wanataka kumuuza mchezaji wao anayepokea mshahara mkubwa Zaidi Mesut Ozil, 30, ambaye bado ana mkataba wa kuchezea Washika Bunduki hao wa London mpaka mwaka 2021. Hata hivyo inaweza kuwawia ugumu Arsenal kupata mnunuzi. (Mirror)
West Ham watafanya maamuzi wiki ijayo iwapo wanampatia Samir Nasri, 31, mkataba wa muda mfupi amesema kocha Manuel Manuel Pellegrini has revealed. (London Evening Standard)

Mchezaji wa zamani wa West Ham James Collins, 35, amepoteza mkataba wa pauni 50,000 na klabu ya Aston Villa baada ya kuumia saa moja baada ya kusaini mktataba. (Mirror)Fred hajakuwa na kiwango bora toka alipojiunga na Mashetani Wekundu

Kiungo raia wa Brazil Fred, 25, atapambania mustakabali wake ndani ya Manchester United baada ya kusalia benchi wakati wa uongozi wa kocha aliyefukuzwa Jose Mourinho. (Telegraph)

Evertonkupitia mkurugenzi wao wa mpira Marcel Brands wamesema hawapo tayari kumnunua mchezaji wa PSV raia wa Mexico Hirving Lozano, 23, kwa pauni milioni 30. (Voetbal International)
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger