Friday, 21 December 2018

NANE WAUAWA KATIKA MAANDAMANO YA KUPINGA HALI MBAYA YA UCHUMI

Khartoum, SUDAN. Nchini Sudan watu wasiopungua nane (08) raia wa nchi hiyo, wameuawa katika ghasia na maandamano ya wananchi ya kupinga hali mbaya ya kiuchumi, ughali wa bidhaa na maisha magumu nchini humo. Maafisa wa serikali ya Sudan wametangaza usiku wa kuamkia leo kwamba, idadi ya watu waliouawa katika maandamano ya kupinga hali mbaya ya kiuchumi katika mikoa ya al Qadharif na Nahru Nil imefikia 8. Tangu Jumatano ya juzi miji mbalimbali ya Sudan ilishuhudia ghasia na maandamano makubwa ya wananchi anaopinga hali mbaya ya kiuchumi na ughali wa bidhaa.…

Source

Share:

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA DEC 21,2018


Manchester City itawalazimu kupambana na vilabu vya Barcelona na Paris St-Germain ili kupata saini ya mchezaji kiungo nyota anayechipukia Frenkie de Jong, 21. Dejong raia wa Uholanzi anayechezea Ajax anakisiwa kuwa na thamani ya pauni milioni 60. (Mirror)

Real Madrid hawana mpango wa muda mfupi au mrefu wa kumwajiri tena Jose Mourinho, 55, aliyefutwa kazi na Manchester United jumanne wiki hii. (Marca)

Crystal Palace wana imanikuwa watafanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Nigeria na Chelsea Victor Moses, 28, katika dirisha la usajili la mwezi ujao. (London Evening Standard)

Rais wa klabu ya Napoli Aurelio De Laurentiis amesema klabu hiyo haitamuuza mlinzi wake kisiki raia wa Senegal Kalidou Koulibaly, 27, kwenda Manchester United mwezi ujao, lakini wanaweza kukubali dau kwa wakati ujao. (Corriere del Mezzogiorno, via Star)

Arsenal wanataka kumuuza mchezaji wao anayepokea mshahara mkubwa Zaidi Mesut Ozil, 30, ambaye bado ana mkataba wa kuchezea Washika Bunduki hao wa London mpaka mwaka 2021. Hata hivyo inaweza kuwawia ugumu Arsenal kupata mnunuzi. (Mirror)
West Ham watafanya maamuzi wiki ijayo iwapo wanampatia Samir Nasri, 31, mkataba wa muda mfupi amesema kocha Manuel Manuel Pellegrini has revealed. (London Evening Standard)

Mchezaji wa zamani wa West Ham James Collins, 35, amepoteza mkataba wa pauni 50,000 na klabu ya Aston Villa baada ya kuumia saa moja baada ya kusaini mktataba. (Mirror)Fred hajakuwa na kiwango bora toka alipojiunga na Mashetani Wekundu

Kiungo raia wa Brazil Fred, 25, atapambania mustakabali wake ndani ya Manchester United baada ya kusalia benchi wakati wa uongozi wa kocha aliyefukuzwa Jose Mourinho. (Telegraph)

Evertonkupitia mkurugenzi wao wa mpira Marcel Brands wamesema hawapo tayari kumnunua mchezaji wa PSV raia wa Mexico Hirving Lozano, 23, kwa pauni milioni 30. (Voetbal International)
Share:

MARAIS WAWILI WAJITANGAZA WASHINDI WA DURU YA PILI YA UCHAGUZI MADAGASCAR

Antananarivo, MADAGASCAR. Wagombea wawili wa duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Madagascar, ambao wamewahi kuwa marais wa kisiwa hicho, Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina, wamejitangaza washindi wa uchaguzi huo uliofanyika jana, licha ya Tume ya Uchaguzi kusema kuwa imehesabu asilimia tano tu ya kura kufikia sasa. Kwa mujibu wa tume hiyo, matokeo kutoka asilimia tano ya vituo vya kupigia kura yanaonesha kuwa Rajoelina anaongoza kwa asilimia 57 huku mpinzani wake, Ravalomanana akipata asilimia 43. “Tumeona matokeo, sio rasmi lakini ni sehemu ya matokeo hayo na yanaonesha kuwa Papa…

Source

Share:

KWA MARA NYINGINE MKUTANO WA MARAIS WA EAC WAFUTWA TENA

Arusha. Mkutano wa wakuu wa nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambao ulikuwa umepangwa kufanyika jijini Arusha hapa nchini umefutwa kwa mara ya pili ndani ya wiki tatu. Mkutano huo wa marais wa nchi wanachama wa EAC ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi Sudan Kusini ulitazamiwa kufanyika Desemba 27. Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Christophe Bazivamo, amesema, “Ni rasmi sasa, mkutano huo hautafanyika Desemba 27 kama ilivyokuwa imepangwa. Tarehe na mahala pa kufanyika mkutano huo wa 20 wa wakuu wa EAC itatangazwa baadaye.” Kikao cha mawaziri…

Source

Share:

Thursday, 20 December 2018

MAMILIONI YA MFUKO WA JIMBO NYAMAGANA YAMWAGWA SOKO LA MLANGO MMOJA.

  Kiasi cha shilingi milioni ishirini na mbili(22,000.000), kutoka mfuko wa jimbo la Nyamagana Mwanza, kitatumika kukarabati miundombinu ya soko la wajasirimali wadogo wa mlango mmoja uliteketea kwa ajali ya moto miezi miwili iliyopita. Mbunge wa jimbo la Nyamagana, Mhe.Stanislaus Mabula, amesema hayo katika ziara yake maalum ya ukaguzi wa miradi yote inayofadhiliwa na mfuko wa jimbo. Mhe.Mabula, amesema katika awamu hii ofisi yake imetoa shilingi milioni 22 kupitia mfuko wa jimbo ili kukarabati miundombinu ya soko katika paa baada ya kuharibika vibaya na janga la moto miezi miwili iliyopita.…

Source

Share:

WAZIRI UMMY APELEKA GARI YA WAGONJWA RUANGWA.

  Na Bakari Chijumba, Lindi Serikali imeahidi kukipatia kituo cha afya cha Luchelengwa wilayani Ruangwa, gari la kubebea wagonjwa pamoja na mashine ya kisasa ya Xray kabla ya Aprili 2019, lengo likiwa ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi. Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu, ametoa ahadi hiyo alipofika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa na kupokea taarifa ya Afya ya Wilaya hiyo hii leo 20 Desemba 2018. Waziri Ummy amefikia uamuzi huo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim…

Source

Share:

YANGA HII IMESHINDIKANA KABISA,SIMBA WAJIPANGE SANA

NA KAROLI VINSENT WAMESHINDIKANA ndio kauli fupi utaisema kwa Mabingwa wa Historia Timu ya Yanga baada ya kuendeleza rekodi ya kutofungwa kwenye michezo ya Ligi kuu bara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Lyon mchezo uliochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Katika mchezo huo wenye ushindani Bao pekee la Yanga lililofungwa na beki Abdalah Shaibu ‘Ninja’ dakika ya 64 limewafanya waweze kuibuka na pointi tatu muhimu wakiwa ugenini. Matokeo hayo yanaifanya Yanga waendelee kujikita kileleni wakiwa na pointi 47 na kuwaacha wapinzani wao Simba wenye…

Source

Share:

WAWILI WASHITAKIWA KWA KUKAMATWA NA MIGUU 30 YA NYUMBU.

Na,Naomi Milton Serengeti Washitakiwa wawili katika kesi ya uhujumu namba 151/2018 wamefikishwa mbele ya mahakama ya wilaya ya Serengeti kujibu mashtaka yanayowakabili baada ya kupatikana na makosa matatu ikiwemo kukutwa na nyara za Serikali. Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile mwendesha mashtaka wa Jamhuri Renatus Zakeo aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Selemani Mazera(35) na Abasi Waryoba(38) wakazi wa Kijiji cha Ikizu wilayani hapa. Mwendesha mashtaka alisema washitakiwa walikamatwa Disemba 18 mwaka huu katika eneo la Rubana lililoko ndani ya pori la Akiba Ikorongo ndani ya…

Source

Share:

POSHO ZA MADIWANI ZAMTOA JASHO MKURUGENZI MPWAPWA.

  Na, Stephen Noel. Baraza la madiwani Katika Halmashauri ya Mpwapwa mkoani Dodoma wamemtaka MKurugenzi mtendaji wa Halmashauri Hiyo kuweza kuwalipa posho zao za mwezi kutokana na kuto kulipwa posho hizo kwa muda wa miezi 35 mfululizo. Hoja hiyo iliyo chukua muda mrefu wa Kikao mala baada ya Diwani wa Kata Mlunduzi Mhe, Oligenes John alisema tangu mwaka 2015 madiwani hao hawajalipwa posho zao za kikanuni kitu alicho sema kinawapelekea kuona wao wakiwa wasimamiz wa kanuni za vikao vya baraza la madiwani kanuni zinakanyagwa mbele yao. Aidha hoja Hiyo ambayo…

Source

Share:

SAED KUBENEA : SINA MPANGO WA KUHAMIA CCM..MAKONDA ATAONDOKA KWA AIBU

Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Saed Kubenea amesema kuwa kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kusema kuwa yeye na Mbunge wa Kibamba John Mnyika walitaka kujiunga na CCM, si kweli.

Kubenea amesema kuwa hawakuongea vile na Rais bali walikuwa wakizungumza mambo mengine, na Makonda amesema yale ili kuwafurahisha wanachama wa chama cha mapinduzi waliokuwepo kwenye hafla ile.

Kubenea amesema kuwa uchaguzi ujao watahakikisha kuwa wanashinda kwa kishindo hadi serikali inayoongozwa na CCM ishangae.

"Nataka nimwambie tu RC Makonda kwamba katika uchaguzi unaokuja upinzani tutashinda zaidi kuliko ilivyo kawaida, na ataondoka kwa aibu", amesema Kubenea.

Kubenea ameongeza, "Nchi yetu inajenga matabaka, mtu akionekana anaikosoa serikali wanasema huyu mpinzani na siku hizi wametupatia jina jipya wanatuita mawakala wa mabeberu".

Kubenea amesema kuwa, wale wanaomuunga mkono Rais Magufuli wengi wao ndio wanaompinga kimya kimya wakishirikiana na wanachama wengine ndani ya chama ambao wanajiandaa kumpinga katika uchaguzi ujao.

Hayo yamejiri baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, kudai kuwa, amepokea maombi ya wanachama mbalimbali wanaotaka kujiunga na CCM, wakiwemo wabunge wawili wa CHADEMA, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na wa Kibamba, John Mnyika, wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kisasa la Selander na barabara unganishi jijini Dar es salaam.
Share:

RAIS MAGUFULI ATAKA DARAJA LA SELANDER LIBADILISHWE JINA NA KUITWA TANZANITE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 20 Desemba, 2018 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja jipya la Selander linalounganisha eneo la Aga Khan na Coco Beach Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

Daraja hilo lenye urefu wa meta 1,030 na upana wa meta 20.5 litakuwa na njia 4 za magari na njia 2 za watembea kwa miguu, na litajengwa pamoja na barabara unganishi zenye jumla ya kilometa 5.2.

Sherehe za uwekaji jiwe la msingi katika mradi huo zimefanyika katika eneo la Aga Khan na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai, Mawaziri, Wabunge, Mabalozi wa nchi mbalimbali, viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa Dini, viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Paul Makonda.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale amesema ujenzi wa daraja hilo utakaochukua muda wa miezi 30 kuanzia tarehe 23 Julai, 2018 utagharimu shilingi Bilioni 256 zilizotolewa kwa mkopo nafuu kutoka Jamhuri ya Korea kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi (EDCF) na Serikali ya Tanzania.

Mhandisi Mfugale ameongeza kuwa daraja hilo litadumu kwa muda wa miaka 100 na litajengwa bila kuathiri nyumba zilizopo kando ya barabara za Kenyatta na Toure ambazo miongoni mwake wanaishi Mabalozi.

Mhe. Rais Magufuli ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kufadhili ujenzi wa daraja hilo na amemuomba Balozi Mteule wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mhe. Cho Tae-ick kufikisha ujumbe wake kwa Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Moon Jae-in kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na nchi hiyo hususani wakati huu ambapo inaendelea kufanya mapinduzi makubwa ya kiuchumi.

“Jamhuri ya Korea ni marafiki wetu wa kweli, wametusaidia kujenga daraja la Kikwete katika mto Malagarasi na wametusaidia kujenga Hospitali ya Taaluma na Sayansi ya Tiba Mloganzila na miradi mingine, tunawashukuru sana, naomba na sisi Watanzania tubadilike, tuchape kazi, tuwe wazalendo, tuwahimize vijana wetu waje wafanye kazi kwenye mradi huu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli ameitaka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutafuta jina la daraja jipya la Selander na amependekeza lipewe jina la Tanzanite linaloakisi Utanzania.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania wote kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa huku wakitanguliza uzalendo, kudumisha amani na upendo na kutokukatishana tamaa ili Tanzania ifanikiwe kupiga hatua za kimaendeleo kama ilivyofanya Jamhuri ya Korea ambayo uchumi wake ulikuwa sawa na Tanzania miaka ya 60 wakati Tanzania ikipata uhuru.

Mhe. Rais Magufuli amempongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe kwa juhudi zake za kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali ikiwemo kuhakikisha mabasi yote 49,000 yaliyopo nchini yanaanza kutoa tiketi za kielekroniki, kuongeza tija katika ukusanyaji wa mapato ya usafirishaji kwa njia ya reli na kufuatilia meli moja kubwa iliyonunuliwa kwa ushirikiano wa Tanzania na China ili ianze kuja nchini na kuinufaisha Tanzania.

Mapema katika salamu zake Balozi Mteule wa Jamhuri ya Korea Mhe. Cho Tae-ick ameishukuru Tanzania kwa uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati yake na Jamhuri ya Korea ambapo katika kipindi cha miaka 26 ya uhusiano huo, Jamhuri ya Korea imetoa ufadhili wenye thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni 1 na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi inayoongoza kwa ufadhili wa nchi hiyo Barani Afrika.

Nae mwakilishi wa EDCF Mhe. Hyon-jong Lee amesema kwa umuhimu wa kipekee wa uhusiano ya Tanzania na Jamhuri ya Korea, Serikali za nchi hizo zinaendelea na majadiliano ya ufadhili wa miradi yenye thamani ya shilingi Bilioni 687.6 itakayotekelezwa nchini Tanzania katika kipindi cha kuanzia mwaka 2018 hadi 2020.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
20 Desemba, 2018
Share:

KINDOKI AONDOA MKOSI...ASAIDIA YANGA KUICHAPA AFRICAN LYON


Klaus Kindoki (wa pili kulia) akiwa benchi na wachezaji wengine wa Yanga

Mlinda mlango namba mbili wa Yanga kwa sasa, Klaus Kindoki hatimaye ameondoa mkosi kwa kusimama golini hadi mpira unamalizika na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya African Lyon.

Kindoki ambaye amekalia benchi kwa kipindi kirefu tangu alipoharibu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya mwadui FC mjini Shinyanga mwezi uliopita, ameingia leo katika kipindi cha pili baada ya Ramadhani Kabwili kuumia na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Bao la Yanga limefungwa na Abdallah Haji Shaibu katika dakika ya 64 ya mchezo huo baada ya dakika 45 za kwanza kumalizika kwa sare tasa.

Kwa matokeo hayo sasa Yanga inafikisha pointi 47 katika michezo yake 17 iliyocheza mpaka sasa, huku ikiwa haijapoteza mchezo wowote na kuzidi kuwakimbia wapinzani wake katika msimamo wa ligi, Azam FC iliyopo nafasi ya pili na Simba iliyopo nafasi ya tatu.
Chanzo - EATV
Share:

KAMERA ZAMUUMBUA SHABIKI UWANJANI ALIYEMPIGA CHUPA YA KICHWA MCHEZAJI

Share:

JIJI LA DAR KUTIKISIKA KESHO,NI KWENYE KESI YA MBOWE,VIGOGO HAWA WAZITO KUTINGA MAHAKAMA

NA KAROLI VINSENT KESHO Makakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajiwa kutikisika kwa muda wa saa kadhaa wakati wa kesi ya “Kisiasa”inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ndivyo naweza kusema baada Vigogo watatu wa kisiasa nchini,Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),Maalim Seif Sharif Hamad , Pamoja Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye,Pamoja na Kiongozi Mkuu wa Chama cha Act-Wazalendo,Zitto Kabwe pamoja na Viongozi wandamizi wa vyama mbali mbali vya siasa nchini ambao wanapinga kile wanachokiita ukandamizaji wa demokrasai nchini. . Mbowe yuko kwenye…

Source

Share:

MBUNGE KUBENEA AMUUMBUA RC MAKONDA ,

Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Saed Kubenea amesema kuwa kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kusema kuwa yeye na Mbunge wa Kibamba John Mnyika walitaka kujiunga na CCM, si kweli. Kubenea amesema kuwa hawakuongea vile na Rais bali walikuwa wakizungumza mambo mengine, na Makonda amesema yale ili kuwafurahisha wanachama wa chama cha mapinduzi waliokuwepo kwenye hafla ile. Kubenea amesema kuwa uchaguzi ujao watahakikisha kuwa wanashinda kwa kishindo hadi serikali inayoongozwa na CCM ishangae. “Nataka nimwambie tu RC Makonda kwamba katika uchaguzi unaokuja upinzani tutashinda zaidi kuliko…

Source

Share:

SERIKALI YA AWAMU YATANO IMEKUSUDIA KUIMARISHA SEKTA YA NISHATI NCHINI.

Na Mwandishi wetu Songea. Naibu waziri wa nishati ,Mheshimiwa Subira Mgalu amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kuimarisha sekta ya Nishati Nchini kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya kuhakikisha Nchi inakua na Umeme wa Uhakika , na hilo limethibitika kwa kuanza mchakato wa ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya mto Rufuji mkoani Njombe utakaozalisha megawats 358 kwa lengo la kuwa na umeme wa kutosha na wa gharama nafuu. Akizungumza na wananchi wakati akiwasha umeme…

Source

Share:

RAIS MUSEVENI AMSUTA MISS UGANDA BAADA YA KWENDA IKULU...AMTAKA AACHANE NA MAWIGI

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger