MGANGA wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Kashinje Kashinje (55),
mkazi wa kijiji cha Singita kilichopo Kata ya Usanda wilayani hapa
ameuawa kwa kupigwa na wananchi ikielezwa alijaribu kutaka kumbaka mteja
wake.
Mteja huyo ambaye ni mwanamke mwenye umri wa miaka 20 (jina linahifadhiwa) aliyekwenda kutibiwa kwa lengo la kupata mtoto.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne, tukio
hilo ni la Novemba 29 mwaka huu, akisema lilitokea majira ya saa tano
asubuhi.
Alisema Kashinje alifariki dunia alipokuwa anakimbizwa hospitali baada
ya kujeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali katika jicho la kulia na kupigwa
kwa fimbo mgongoni na watu waliojichukulia sheria mkononi.
“Watu hao walijichukulia sheria mkononi baada ya mganga huyo kujaribu
kumbaka mwanamke (jina linahifadhiwa), mkazi wa kijiji cha Ishinabulandi
wilaya ya Shinyanga ambaye alikuwa akimtibu kwa tiba za asili ili aweze
kupata mtoto”, alieleza kamanda Muliro.
Alisema tatizo lililompeleka mwanamke huyo kwa mganga ni kupata tiba ili aweze kupata mtoto.
Kamanda Muliro alibainisha kuwa chanzo cha tukio hilo ni tamaa za
kimwili na uongo wa kimatibabu wa kutaka kumuingilia kimwili mgonjwa
wake baada ya kumlewesha kwa dawa za kienyeji, lakini alifanikiwa kupiga
kelele na ndipo wananchi walipomvamia mganga huyo
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji La Arusha, Athumani Kihamia ametangaza
kusitisha mikataba ya wafanyakazi 66 kati ya 132 wasio na kazi za
lazima katika halmashauri hiyo.
Amewasimamisha kazi kwa lengo la kubana matumizi ili fedha
zitakazookolewa zitaelekezwa kwenye matumizi ya miradi ya maendeleo na
ulipaji wa madeni.
MSHITAKIWA katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, Salum Njwete
(34) ‘Scorpion’, amekiri kupata mafunzo ya kareti kutoka chuo cha
mafunzo cha Ifakara aliyoyafanya mwaka 1989 hadi 1995.
Aidha, upande wa mashitaka katika kesi hiyo umemuongezea mashitaka ya
shambulio kupitia kifungu namba 234 cha Sheria ya Makosa ya Jinai
ambacho kinaruhusu kuongeza au kubadilisha mashitaka.
Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi,
Flora Haule kwamba kesi hiyo imekuja kwa ajili ya mshitakiwa kusomewa
maelezo ya awali ambapo katika maelezo ya zaidi ya saa nane, alikiri
kuhusu jina lake, sehemu anayoishi ya Machimbo Yombo na mafunzo hayo.
Hata hivyo, alikana kuhusu jina la Scorpion, mashitaka yake na kwamba hakukamatwa wala kuhojiwa na Polisi kuhusu mashitaka hayo.
Katuga alidai kuwa Septemba 6, mwaka huu, mshitakiwa alikuwa maeneo ya
Buguruni Sheli na kwamba Septemba 12, alihojiwa na kukamatwa na polisi
maelezo ambayo aliyakana.
“Mashahidi watakaotoa ushahidi katika kesi hii wapo sita ambapo upande
wetu wa mashitaka utawasilisha vielelezo viwili ikiwemo Fomu namba tatu
ya Polisi (PF3) na ripoti ya daktari kwa ajili ya kuthibitisha mashitaka
hayo,’’ alidai Katuga.
Hakimu Haule aliahirisha shauri hilo hadi Desemba 14 mwaka huu, kesi
hiyo itakapokuja kwa ajili ya kusikilizwa. Katika mashitaka yake,
mtuhumiwa inadaiwa alitenda kosa hilo Septemba 6, mwaka huu katika
maeneo ya Buguruni Sheli, wilaya ya Ilala.
Inadaiwa, Njwete aliiba mkufu rangi ya fedha wenye uzito wa gramu 34
wenye thamani ya Sh 60,000, bangili ya mkononi na fedha taslimu Sh
331,000, vyote vikiwa na thamani ya Sh 476,000 mali ya Said Mrisho.
Inadaiwa kabla na baada ya wizi huo, alimchoma kisu machoni, tumboni na mabegani mlalamikaji ili ajipatie mali hizo.
Rais wa Tanzania Dkt. John
Magufuli tayari amekwishasaini mabadiliko ya sheria yanayomtaka mwajiri
kukata asilimia 15 ya mshahara wa mwajiriwa ambaye ni mnufaika wa mkopo
wa elimu ya juu kwa ajili ya kulipa deni lake analodaiwa na Bodi ya
Mikopo
Visanduku vya mawasiliano ajali ya ndege ya Brazil vyapatikana
Ndege
iliyokuwa imewabeba wachezaji wa timu ya mpira kutoka nchini Brazil
ambayo ilipata ajali nchini Colombia inasemekana kwa muujibu wa taarifa
zilizovuja ndege hiyo iliishiwa mafuta kutoka katika kifaa cha kurekodia
mawasiliano.
Katika
mnara wa mawasiliano ya ndege , rubani alisikika akirudia mara kadhaa
akiomba ruhusa ya kutua kwa dharura kutokana na hitilafu ya umeme
iliyokuwamo ndegeni pamoja na kuishiwa mafuta ya ndege.
Kabla
hata mawasiliano hayo yaliyorekodiwa kufikia mwisho ,rubani alisikika
akisema yuko angani umbali wa futi elfu tisa sawa na mita elfu mbili mia
saba na arobaini na tatu.Taarifa za mawasiliano hayo zimekuwa gumzo
katika mitandao kadhaa nchini Colombia na hata katika vyombo vya habari
nchini humo, na hivyo kumekuwepo fununu za taarifa hizo kuwa huenda
zikawa na chembe ya ukweli kwamba kuishiwa kwa mafuta ndiyo chanzo zha
ajali ya ndege hiyo.
Wanajeshi
wa Colombia waliliambia shirika la habari la AFP, kwamba pamoja na
ndege hiyo kuanguka kuna shaka juu ya ajali hiyo kwani pamoja na ndege
hiyo kuanguka hakukuwa na mlipuko wowote na kwamba huenda kulitumika
nguvu ingine tofauti na nadharia ya kwisha kwa mafuta ndegeni.
Wadadisi
wa mambo na wachunguzi bado hawako tayari kufungua mdomo na kuzungumzia
juu ya chanzo chochote cha ajali hiyo na kwamba taarifa kamili ya
uchunguzi itatolewa baada ya miezi kadhaa.
Wachezaji
wa timu ya Chapecoense walikuwa safarini kuelekea nchini Colombian
kwenye mji wa Medellin mahali kulikotarajiwa mechi kubwa ya mpira wa
miguu ya kihistoria na badala yake wachezaji hao wameacha historia
.Kufuatia vifo vya wachezaji wa timu hiyo, ulimwengu mzima umeungana
kuomboleza vifo vyao.
Kwa
muujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka katika shirika la ndege la
Lamia watu wanne waliokuwa wasafiri na ndege hiyo wameponea chupuchupu
kuwa miongoni mwa waliokufa baada ya kukosa tiketi.
Mmoja wa
manusura wa ajali hiyo ambaye ni fundi wa ndege Erwin Tumiri, ameeleza
namna alivyokwepa kifo, kwamba yeye alifuata maelekezo yote ya namna ya
kujiokoa ,anasema abiria wenzie , walio wengi walisimama na kuanza
kupiga kelele nay eye aliamua kuweka sanduku lake la kusafiria kati kati
ya miguu yake na kuamua kubaki hivyo.
Visanduku
viwili vya mawasiliano vya ndege hiyo vyote vilipatikana na tayari
vimeanza kufanyiwa uchunguzi na wataalamu wa masuala ya anga.
Wachunguzi
wataalamu kutoka nchini Uingereza wanasaidiana na mamlaka za Amerika
Kusini kwasababu ndege iliyopata ajali ilitengenezwa na wana anga wa
Uingereza BAE nchini Uingereza.Brazil imeanza siku tatu za maombolezo
wakati maelfu ya watu na washabiki wa timu ya Chapecoense wako katika
mji yaliko makao makuu ya timu hiyo Chapeco wanaendelea mkesha wa
maombolezo wakati maandalizi ya kuchukua mabaki ya wachezaji hao
inafanywa na jeshi kurejeshwa Brazil ili kuzikwa kwa pamoja katika
uwanja wa Chapeco.
Nchi ya Bolivia tayari imekwisha tuma ndege ya kuchukua mabaki ya raia wake waliokufa katika ajali hiyo nchini Colombia.
Timu hiyo
iliandika historia ya mafanikio katika soka kwa kuwa kileleni mwa ligi
ya Brazil kwamara ya kwanza mwaka 2014.Kati ya watu 77 waliokuwa
wameabiri ndege hiyo miongoni mwao ni watu sita tu ndiyo walionusurika
.Abiria walio wengi walikuwa ni wachezaji wa timu ya Chapecoense na
waandishi habari wapatao ishirini walikuwa miongoni mwa walipoteza
maisha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP Peter Kakamba, amefariki dunia
usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua maradhi ya tumbo, Jeshi la Polisi
limethibitisha.
Akizungumza na Mwananchi Digital, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Singida, Mayala Towo amesema Kamanda Kakamba amefia hospitali ya Taifa
Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Mwananchi Digital iliwasiliana na Kaimu Kamanda Towo kupata uthibitisho
wa taarifa zilizosambazwa kupitia mitandao ya kijamii mapema leo kuwa
SACP Kakamba ameaga dunia, baada ya kukosa ushirikiano kutoka kitengo
cha mawasiliano cha Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es
Salaam.
Taarifa iliyokuwa inasambazwa kupitia mtandao wa WhatsApp mapema
asubuhi, ilimnukuu Inspekta wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu
akisema: “IGP anasikitika kutangaza kifo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Singida SACP Peter Kakamba kilichotokea usiku wa saa nne katika
Hospitali ya Muhimbili DSM.
Kamanda Kakamba alikuwa amelazwa hospitalini hapo kwa maradhi ya tumbo alikuwa amefanyiwa operesheni hivi karibuni.”
Kwa mujibu wa Towo, mwili wa marehemu Kakamba utawasili Singida kwa
ajili ya kuagwa kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao mkoani Rukwa
kwa ajili ya maziko.